Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 59 | 60 | (Page 61) | 62 | 63 | .... | 3286 | newer

  0 0


  Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Bwana Epraim Mafuru anasikitika kuwatangazia kifo cha Mama yake Mzazi Bi. Anastazia Nyate Mugaya Mafuru. 
  Ibada na mazishi ni leo Jumapili (3/03/2013) kuanzia saa sita mchana hapa nyumbani Boko na baadae makaburini Bahari Beach jijini Dar es salaam. 
  Mungu ampokee mama yetu. Ufunuo 14.13

  0 0  ·       Liewig aahidi kupambana hadi mwisho
  ·       Poppe aahidi mamilioni kwa wachezaji
  ·       Kapombe asema Sunzu atawaua Waangola

  Na Ezekiel Kamwaga, Kwanza Sul, Angola
  KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Jean Elysee Liewig, amesema ana matumaini timu yake itapata matokeo mazuri katika mchezo wa kesho baina ya Wekundu wa Msimbazi na Libolo ya Angola.
  Mechi hiyo imepangwa kuchezwa leo kuanzia saa tisa alasiri katika Uwanja wa Estadio Libolo, uliopo katika mji mdogo wa Calulo jimbo la Kwanza Sul.
  Katika mechi ya kwanza baina ya timu hizo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita, Simba ilifungwa 1-0 na mabingwa hao wa Angola.
  Hata hivyo, Liewig alisema ingawa matokeo ya kufungwa nyumbani hayakuwa mazuri, ana imani Simba nayo inaweza kufanya vizuri ugenini.
  “Kama wao walitufunga kwetu kwanini sisi tusiwafunge kwao. Ukiangalia kwenye ile mechi ya kwanza wao walipata nafsi moja tu ya maana na wakaitumia. Sisi tulipata nafasi kama tatu hivi na hatukutumia vizuri hata moja,” alisema.
  Liewig alisema ameridhishwa na ari na mazoezi mazuri ambayo Simba imefanya kwa wiki nzima kujiandaa na mechi hiyo na kwamba kuna dalili kuwa timu yake inaweza kufanya lisilotarajiwa.
  Akizungumza na wachezaji katika kikao kilichofanyika katika Hoteli ya Anisaan Ritz ambako Simba imefikia, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Zacharia Hans Poppe, alitoa ahadi ya Sh milioni 10 iwapo watafanikiwa kuitoa Libolo.
  Aliwataka wachezaji wa Simba kuwakumbuka mamilioni ya washabiki wao waliopo Tanzania ambão hawalali wala kula vizuri wakati timu yao kipenzi inapokuwa na matokeo mabaya.
  Poppe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba na pia kundi la Friends of Simba, alisema ana imani kubwa na wachezaji wa timu yake kwa vile ndiyo bora Tanzania na kama wataamua kucheza kwa nguvu zao zote, matokeo mazuri yanawezekana.
  “Nyie ni wachezaji wazuri sana. Kama nyote mtacheza kama timu na mkacheza kwa uwezo wenu wote, ni wazi kwamba mnaweza kuibuka na ushindi,” alisema.
  Akizungumzia mechi hiyo, nahodha msaidizi wa Simba, Shomari Kapombe, alisema mechi baina yao na Libolo itakuwa tofauti na ya kwanza kwa sababu ya kuwepo kwa mshambuliaji Mzambia, Felix Sunzu.
  “Tulimkosa sana Sunzu kwenye mechi ya Dar es Salaam. Mipira ilikuwa haikai kule mbele na hilo lilikuwa tatizo kubwa, kubwa sana na hiyo ni kwa sababu Sunzu hakuwepo. Nadhani sasa tuna nafasi zaidi kuliko mara ya kwanza,” alisema.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Ulinzi na Usalama, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Musoma, leo kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili katika mkoa huo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Gabriel Tupa. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Wazee wa Chama cha Mapinduzi, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Musoma, leo kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili katika mkoa huo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakifurahia burudani ya ngoma ya asili, wakati walipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Musoma, leo kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili katika mkoa huo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Gabriel Tupa. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo jumapili Februari 3, 2013 ameanza rasmi ziara ya siku mbili ya kikazi katika mkoa wa Mara.

  Akiwa Mkoani Mara Mhe. Makamu wa Rais, anatarajia kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo, ikiwa ni pamoja na kufungua Barabara inayounganisha Mkoa mpya wa Simiyu na Mkoa wa Mara.

  Aidha Makamu wa Rais, atazindua rasmi Kivuko cha Mv. Musoma, kinachofanya kazi ya kusafirisha wananchi ambao ni wakazi wa Rorya na Musoma, ambapo pia atazindua mradi wa nyumba za Watumishi wa Umma, mkoani Mara na kuzungumza na wananchi kabla ya kuondoka kurejea jijini Dar es Salaam.


  0 0


  Mgeni Rasmi katika Hafla ya Siku ya Wanawake,Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akisoma hotuba fupi mbele ya wageni mbalimbali waliofika kwenye hafla ya wanawake (Women's Celebration 2013) iliondaliwa na kampuni ya 8020 Fashions,iliofayika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee VIP,jijini dar.Hafla hiyo imefanyika ikiwa ni mwelekeo wa kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani itakayoadhimisha Machi 8 Duniani kote.
   Mke wa waziri Mkuu Mstaafu,Mama Regina Lowassa akisalimiana na mgeni rasmi,Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda kwenye hafla ya Women's Celebration 2013 iliofanyika leo jijini Dar.
  Muandaaji wa hafla ya Women's Celebration 2013 kutoka kampuni ya 8020 Fashions, Shamim Mwasha akipongezwa na Mgeni Rasmi Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda kwa kazi nzuri alioifanya ya kufanikiwa kuwakusanya wanawake wenzake na kujadili mambo mbalimbali yakiwemo ya kifamilia na maendeleo kwa ujumla,hafla hiyo imefanyika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee VIP,jijini dar.Hafla hiyo imefanyika ikiwa ni sehemu ya kuelekea kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani itakayoadhimishwa Machi 8 Duniani kote.
   Mwimbaji mahiri wa miondoko ya taarab nchini,Khadija Kopa akitumbuiza mbele ya wageni mbalimbali waliofika kwenye hafla ya  wanawake (Women's Celebration 2013) iliondaliwa na kampuni ya 8020 Fashions,iliofanyika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee VIP,jijini dar.


  KUONA PICHA ZAIDI
  BOFYA HAPA
  AU
  BOFYA HAPA

  0 0

  Meneja wa Bia ya Kiliamanjaro, Geogre Kavishe akimpongeza Edina Joseph mmoja wa washiriki wa Mashindano ya Kilimanjaro Marathon, yaliofanyika jana, Moshi Mkoa wa Kilimanjaro, mashindano hayo yalidhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro, Premium Lager, Gapco, Vodacom , Tanga Cement , CFAO Motors, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, Tanzania one, New ArushaHotel, UNFPA, Fastjet, Cluods FM, na Kilimanjaro Water.
  Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars akimaliza mbio ya Kilimanjaro Premium Lager Marathon za kilomita 21 zilizofanyika jana mjini Moshi.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Terezya Huvisa akiwa hutubia Wananchi wa Wilaya ya Kinondoni Wakati Sherehe za Kuadhimisha Siku ya Mazingira Barani Afrika Sherehe hizo zmefanyika kenye Viwanja vya Tanganyika Packere huko Kawa Jijini Dar es Salaam.
  Mawaziri wa Nchi Katika Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan na Wamazingira Dk Terezya Huvisa,Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Chalrs Kitwanga na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Sar es Salaam Said Meek Sadiki wakifanya Usafi Kandokando Mwabarabara ya kawe Wakati wa Kuadhimisha Siku ya Mazingira Barani Afrika Sherehe hizo zimefanyika kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers Jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meek Sadiki akifanya Ufasi Wajiji katika Barabara ya Kawe kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, Wakati wa Kuadhimisha Siku ya Mazingira Barani Afrika Kulia Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dk Julias Ningu.
  Baadhi ya Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Wakifanya Usafi Kuadhimisha siku ya Mazingira Barani Afrika kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers kawe Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.[Picha na Ali Meja]

  0 0


  TIMU YA SIMBA YA JIJINI DAR ES SALAAM,YASHINDWA KUONYESHA MAKEKE YAKE MBELE YA TIMU YA FC LIBOLO YA NCHINI ANGOLA,BAADA YA KUKUBALI KICHAPO CHA BAO 4-0 KATIKA MCHEZO ULIOMALIZIKA MUDA MFUPI ULIOPITA.

  NA HUKO NCHINI SUDAN KUSINI,TIMU YA AZAM FC LEO WAMEENDELEA KUONYESHA CHECHE ZAO,BAADA YA KUWATANDIKA WAINZANI WAO BAO 5-0.

  HABARI KAMILI ITAKUJA BAADAE.

  0 0
 • 03/03/13--11:12: MKUTANO WA CHADEMA MBEYA
 • Mwenyekiti wa Chadema taifa, Freeman Mbowe  akiongea na viongozi wa Chadema wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini katika ukumbi wa mkapa jijini Mbeya 


  mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa wa pili kushoto akiwa katika mkutano huo 


   Makamanda wa Chadema  wakiwa katika Maandamano  ambayo yaliongozwa na Mbowe yaliyoanzia katika eneo la Uhasibu Mafiat hadi katika Uwanja wa Ruanda Nzovwe,Mbowe aitembea kwa mwendo wa kilomita tano ambapo makundi ya waendesha bodaboda, baiskeli na watembea kwa miguu walijitokeza kwa wingi kuunga mkono maandamano hayo.
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema kuwa kitalazimisha maandamano nchi nzima iwapo Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Naibu wake hawatakubali kujiuzulu kwa kusababisha anguko la elimu nchini.
  Mbunge wa  jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa akitema  cheche zake na  kuwakuna  zaidi  wana Mbeya kwa hotuba nzuri na hili kwa Iringa mjini ni jembe  la ukweli
  Mbunge  wa jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi a.k.a MR SUGU akiunguruma
  Umati  wa  wananchi  waliofika katika mkutano  huo

  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kuwa kimeamua kuanza kutekeleza sera yake ya kuongoza kwa majimbo sasa ili kuongeza nguvu ya mapambano na harakati za kuhakikisha wanafanikisha malengo yao ya kushika dola mwaka 2015, badala ya kuendelea kutumia mfumo wa zamani ambao ilikuwa rahisi kudhibitiwa na serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) .

  Kadhalika, chama hicho kimesema hakitampokea mwanachama yeyote wa Chama Cha Mapinduzi atakayekosa nafasi ya kugombea kwenye chama chake na kutimkia Chadema katika dakika za mwisho kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.

  Mwenyekiti wa Chadema taifa, Freeman Mbowe aliyasema hayo wakati akizungumza na viongozi wa Chadema wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ikiwa ni maandalizi ya kuzindua kanda yake kwenye kanda hiyo.

  Alisema kuwa mfumo wa zamani ambao mambo yote ya harakati za chama hicho yalianzia makao makuu ya chama,  ulikuwa ni rahisi kudhibitiwa na dola ya CCM kwa kuwa walikuwa wakiwavizia viongozi wa kitaifa wanapotoka nje kwenda kuendesha harakati wanawapiga mabomu, kuwakamata na kuwafungulia kesi mahakamani.

  “Tunataka dola ikusubiri viongozi wa kitaifa watoke makao makuu ili wawadhibiti, wasikie mapambano yanatokea kwenye kanda zetu kama hii ya Nyanda za Juu Kusini, kanda ya Magharibi na nyinginezo,” alisema Mbowe.

  Alisema kuwa katika mabadiliko hayo pia Chadema inaachana na siasa za kiuanaharakati na badala yake inaanza kujikita kwenye siasa za maandalizi ya kushika dola.

  Akizungumzia utaratibu wa baadhi ya wanachama wa vyama vingine, kikiwemo chama tawala CCM kukimbilia ndani ya chama hicho baada ya kutoswa kwenye nafasi za uchaguzi, Mbowe amesema kuwa kuanzia sasa Chadema hakitampokea mwanachama yeyote wa aina hiyo.

  Mbowe alisema kuwa Chadema hivi sasa ipo kwenye maandalizi makubwa ya kunyakua dola mwaka 2015 na hivyo inao wajibu wa kuwaandaa wanachama wake ipasavyo ili kiweze kuwa na wagombea wazuri, imara na wenye uwezo wa kuwezesha chama hicho kupata ushindi mkubwa.

  “Kama kuna mtu leo anakula matunda ya ufisadi ndani ya Chama Cha Mapinduzi akidhani kuwa atahamia Chadema kwa kuwa ana fedha za kununua kura za maoni, ameula wa chuya, hatutampokea mtu wa aina hiyo, ” alisema Mbowe.

  Alisema kuwa kuanzia sasa Chadema itawapokea wanachama kutoka vyama vingine baada ya kuwapima uadilifu wao, kuchunguza historia yao na utayari wao wa kutumika ndani ya chama ili waweze kupata wanachama na viongozi wazuri watakaokisaidia chama kushika dola mwaka 2015.

  Alisema kuwa Chama Cha Mapinduzi kimekuwa kikitumia mbinu mbalimbali za kukisambaratisha Chadema, ikiwa ni pamoja na kuwatumia mamluki ndani ya chama, lakini kutokana na uimara wa Chadema mbinu hizo zimekwama na Chadema inasonga mbele.

  Mbowe ambaye pia ni kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni alisema kuwa yeye pamoja na wapambanaji wenzake wametumia zaidi ya miaka 20 kuijenga Chadema na kuipa nguvu kisiasa hadi hapo na hivyo hatakubali kuruhusu chama hicho kihujumiwe au kusambaratishwa kwa namna yoyote ile.

  Alisema kuwa ikiwa wana-Chadema wataruhusu Chadema ife leo, itawachukua tena miaka 20 mingine kuijenga na kuifikisha mahali iilipo hivi leo.

  Mbowe alitolea mfano wa vyama vya siasa vilivyowahi kupata nguvu na umaarufu mkubwa wa kisiasa nchini kama vile Chama cha Wananchi, CUF, NCCR – Mageuzi na TLP ambavyo alidai kuwa CCM illifanikiwa kuvizima na kuwa hata vyenyewe itavichukua muda mrefu usiopungua miaka 20 kurejesha umaarufuvilivyokuwa nao.
      
  Na mbeya yetu

  0 0

   Mfumania nyavu anaeshikila rekodi ya ufungaji bora wa muda wote ndani ya Azam fc John Raphael Bocco ameiongoza timu yake katika utoaji wa maji ya uhai yenye ujazo wa lita 5 kwa askari wa El Nasri Juba katika uwanja wa taifa uliopo mjini Juba, Sudan ya kusini.
  Bocco ameitunga El Nasri goli 2 katika ushindi wa goli 5-0 walioupata Azam fc hii leo katika mchezo wa marejeano wa michuano ya kombe la shirikisho la soka Afrika na kupelekea El Nasri kutolewa kwa jumla ya goli 8-1 katika michuano hiyo ya pili kwa ukubwa barani Afrika katika ngazi ya vilabu.
  Azam fc waliingia katika uwanja huo wa Taifa la Sudan Kusini  wakiwa na akiba ya goli 3-1 na John Bocco ndiye aliyefungua karamu ya magoli kwa Azam hii kabla ya Khamis Mcha kuifungia Azam fc goli la 2.
  Bocco alimpeleka kwa mara nyingine kwenye nyavu kipa wa El Nasri aliyekuwa kizuizi katika mchezo wa awali kwa Azam kutoka na ushindi mnono pale alipoifungia azam fc goli la 3.
  Mcha alifunga goli lake la pili kati michuano hiyo baada ya kuifungia Azam fc goli la 4 ikiwa ni kabla ya Kipre Herman Tchetche kuhitimisha kalamu ya mabao kwa kuifungia Azam goli la 5 likiwa ni goli lake la 3 kuifunga El Nasri baada ya mchezo wa awali kuifunga magoli mawili.
  Kwa matokeo hayo imeisogeza Azam katika mzunguko wa pili ambapo mpinzani wake atafahamika hapo baadae.

  0 0

   At the threshold of elections in Kenya, we hope and pray that elections will be conducted in peace and dignity. The success of this election has far reaching effects on the integration of EAC. As EALA MP, i wish our Partner State all the best!! 
  Hon. Shy-Rose Bhanji

  0 0

  Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Makamu wa Pili wa Rais wa zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwasisitiza Wana CCM kuendeleza amani licha ya cheche za hujuma zinazoonekana kufanywa na baadhi ya watu nchini.
   Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi akifurahia moja ya darasa la Jengo la Skuli Mpya ya Matetema ambayo tayari wanafunzi wa Kijiji hicho wameanza kulisomea kwa karibu wiki moja sasa.
   Mjumbe wa Kamat Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi vifaa vya ujenzi Mwenyekiti wa CCM Tawi la Boma Ndugu Bakuda Edwanr kwa ajili ya uendelezaji ujenzi wa Tawi hilo.

  Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi alikikagua na baadae kukikabidhi Kisima cha maji kwa ajili ya matumizi ya wananchi wa Kijiji cha Boma kiliomo ndani ya Jimbo la Kitope. 
  Picha na Hassan Issa – OMPR - ZNZ

  0 0
 • 03/03/13--19:00: ngoma azipendazo ankal

 • Mambo ya UB40 ya 'Red red wine' balaa

  0 0


  President to the Institution of Engineers Tanzania (IET), Eng Dr Malima Bundara speaks duringengineers’ public meeting held at the weekend in Dar es Salaam. From his immediate right are former IET president Eng Ladislaus Salema, followed by IET Treasure Eng Rizwan Qadri and Secretary to the institute Eng Swaleh Kassera. Photo by correspondent.
  ========  =======  =========
  TANZANIA’S economic growth hangs in balance if Government does not take stern measures to build capacity for local engineers, the Institution of Engineers Tanzania (IET) has warned.

  The warning was made by a cross-section of engineers who attended the engineers’ public meeting on re-engineering IET and role of engineers in Tanzania’s current challenges as far asemployment, education, abuse of engineering profession and natural resources are concern. Speaking during the event, the IET President Eng. Dr. Malima Bundara said the challenges facing the country’s engineering sector will only be solved with engagement of local engineers.

  “The engineering sector is facing many challenges but such challenges will only be solved if local engineers are incorporated in the problem solving equation. “We should not deceive ourselves that foreign engineers will find lasting solutions to our problems. They come to make money and take it back with them. The only thing to do is build capacity of our local engineers,” he said.

  Bundara cautioned the Government against neglecting local engineers in trying to look for solutions to the current and looming development setbacks facing the country. And engineers on the other hand should abstain from complaining without taking pro active direction in the improvement of the national economy.
  “The backbone of every country’s economic growth is pegged on availability of a strong and well elaborate infrastructure. Infrastructural development and industrial growth lie in the hands of engineers. 

  If the Government and its institutions make good use of competent local engineers, a quick transformation on the country’s economic landscape will be felt,” said Eng. Bundara. He mentioned that IET is embarking on building capacity for local  engineers phase 2 so as to be enable them give professional solutions to issues associated to their professional fields, which also have direct effect to the country’s economy.

  Eng. Ladislaus Salema, former IET President, wondered why a country like Tanzania endowed with abundant minerals and natural resources in varying intensities, is still struggling to create jobs and is ranked among the developing countries. He wanted the Government to work closely with local engineers in unlocking unemployment challenges in the country.

  Eng. Shabbir Khataw (IET member) on the other hand warned his fellow engineers against laziness, saying that some of graduated University engineers like to sit in offices instead ofpractising to gain skills, a habit that he said would not give them room to improve on their expertise.   Similarly, IET has expressed concern over this year’s massive form four failures and that these results will have a direct impact on the universities output in general within a few years to come.

  The engineers pointed out that the poor results will greatly affect the number of students going for higher education as the poor exams results will create a vacuum that will greatly affected growth in all sectors. It was also remarked that selfishness among Tanzanians was undermining collaborative initiatives.

  0 0

  MWIMBAJI mahiri wa muziki wa kiroho nchini, Upendo Nkone ni miongoni mwa wasanii wa ndani watakaopamba Tamasha la Pasaka Machi 31 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

  Upendo anakuwa msanii wa tatu wa ndani kutangazwa atashiriki katika tamasha hilo baada ya Rose Muhando na John Lissu ambao walitangazwa Ijumaa na Jumamosi.

  Akizungumza Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema mwaka huu katika tamasha hilo wanawapa mashabiki kile wanachokitaka. “Tunaendesha maoni kwa mashabiki wetu wapendekeze wasanii gani wawepo, hivyo hao watatu ndiyo mpaka sasa wameshika nafasi za juu kwa kupendekezwa sana na mashabiki. Wengine tutawatangaza kadri mambo yatakavyokuwa mazuri na pia tukiwa tumezungumza nao juu ya ushiriki wao, ” alisema Msama.

  Tamasha la Pasaka litafanyika Dar es Salaam Machi 31, kisha siku inayofuata itakuwa Uwanja wa Sokoine Mbeya, Aprili 3 itakuwa Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri Dodoma na Aprili 7 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

  Tamasha la mwaka jana baadhi ya waimbaji mahiri waliokuwepo ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku hiyo.

  0 0


    Millen Magese akikabidhi hundi ya milioni kumi na tano kwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mjini, Mhe. Wilman Ndile; kulia ni Mbunge wa Mtwara Mjini, Mhe. Hasnain Murji
    Millen Magese akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa mkuu wa wilaya Mtwara kabla ya kuanza ziara ya kutembelea mashuleni. 
  Millen Magese akiongea kabla ya kukabidhi mchango wake wa milioni kumi na tano kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa madarasa na madawati.
   Millen magese akiongea na wanafunzi na walimu wakati wa ziara yake mashuleni.

  0 0

  Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mhe. Hab  Mkwizu  akifungua Mkutano wa siku mbili kati ya  Bodi ya  Mishahara na Masilahi  katika Utumishi wa Umma na Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu kutoka utumishi wa umma. Mkutano huo ulikuwa na lengo la kujadili mbinu na mikakati ya kuboresha masilahi na tija kwa watumishi nchini na ulifanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
  Katibu wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bibi. Tamika Mwakahesya akitoa mada juu ya Muundo na Majukumu ya Bodi hiyo  kwenye mkutano  wa siku mbili wa  wajumbe wa Bodi ya  Mishahara na Masilahi  katika Utumishi wa Umma na Wakuu wa Idara, Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu kutoka utumishi wa umma uliofanyika jijini Dares Salaam.
  Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu (kushoto) akijadiliana  jambo na wadau wa Bodi ya  Mishahara na Masilahi  katika Utumishi wa Umma wakati wa Mkutano wa Bodi hiyo wa siku mbili uliowahusisha Wakuu wa Idara, Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu kutoka utumishi wa umma uliofanyika hivi karibuni jijini Dares Salaam. Wa kwanza kulia ni Katibu wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bibi Tamika Mwakahesya, wakifuatiwa  na Mkuu wa Kitengo cha Utawala na Menejimenti ya Rasilimali  watu -Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bibi Lucy Matozi na Mkurungezi wa  Rasimali watu –Bunge, Bibi. Kitolina Kippa 
  Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu wa tatu kutoka kushoto akiwa  kwenye picha ya pamoja na  wadau wa mkutano wa  siku mbili  Bodi ya  Mishahara na Masilahi  katika Utumushi wa Umma na  wakuu wa Idara, Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu kutoka utumishi wa umma uliofanyika jijini Dares Salaam

  0 0

  Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Sadifa Hamis Juma akihutubia aktika mkutano wa UVCCM uliofanyika jioni hii kwenye Uwanja wa shule ya msingi Mkwajuni, Kata ya Kichangani mkoani Morogoro leo Machi 3, 2013, ikiwa ni mwisho wa ziara yake na viongozi wa kitaifa wa Jumuia hiyo mkoani humo, kukagua na kuimarisha uhai wa Chama na UVCCM
  Mbunge wa Morogoro, Abdulazizi Mohammed Abood akieleza utekelezaji wa ilani ya CCM, baada ya kupandishwa jukwaani na Sadifa (wapili kushoto) wakati wa mkutano huo.
   Sadifa akikabidhi kadi ya Umoja wa CCM, kwa mwanachama mpya wakati wa mkutano huo. Jumla ya wanachama 1700 walipewa kadi.
  Sadifa na baadhi ya viongozi wakishirikina na wanachama kula kiapo cha CCM baada ya wanachama wapya wa UVCCM kupewa kadi kwenye mkutano huo
  Katibu Mkuu wa UVCCM, Martine Shigela akihutubia kwenye mkutano huo
   Mmoja wa vijana machachari aliyehama hivi karibuni kutoka Chadema, Mtela Mwampamba akihutubia kwenye mkutano huo.
  "Vijana Chadema wanawazingua tu, wanawahamasisha kufanya maandamano ili wawapige picha za kwenda kuonyesha  nchi za nje kwa marafiki  zao kwa ajili ya kupatiwa mamilioni ya fedha", anasema Mwampamba kwenye mkutano huo. Kulia ni Mkuu wa Utawala Makao Makuu ya UVCCM Kaka Mpokwa.
  VIjana wakiwa wamembeba Mwampamba baada ya kuingiwa na hotuba yake kwenye mkutano huo
  Kama Mwampamba, Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) Taifa, Juliana Shonza, ambaye amehamia CCM hivi karibuni, akibebwa na vijana wa UVCCM, baada ya 'kuimwagia razi' Chadema jukwaani kwenye mkutano huo.
  "Hawa walijaribu kuwapiga mawe ili msifike kwenye mkutano huu, lakini tazama mlivyofurika! Sasa ninasema, Uwezo wa kuwapiga tunao na nia ya kuwapiga tunayo..Tutawapiga, lakini sisi hatutawapiga kwa mawe ila kwa sera zetu makini" akasema Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda wakati akihutubia kwenye mkutano huo.
  Mbunge wa Morogoro, Abdulaziz Mohamed Abood akiongoza msafara wa pikipiki kwenda kwenye mkutano huo
   Vijana wakiserebuka kwa nyimbo za hamasa kwenye mkutano huo
   "Raaaaaaa UVCCM" Vijana hawa wa CCM wakati wa shamrashamra kwenye mkutano huo
  Kujimwaya mwaya hakukukoma hadi mwisho wa mkutano. 
  PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

  0 0
 • 03/03/13--21:41: Article 2


 • 0 0

  Magari Yanauzwa Karibu Ya Mapya Haraka: 
   2 (Mbili) Toyota Landcruisers VX petrol engine 
   1 (moja) Rav 4 J - 2000 model - 
  Bei Mapatano Haraka - Fedha taslimu Au malipo nusu 50% na baki (balance) baada ya miezi mitatu. 
   Contact simu Numbers 
  0755723897 Henry 
   0712022929 Ahmed
  0 0

  The Alliance Life Assurance Ltd Assistant General Manager George Nyakundi (right) hands over a dummy cheque to the outgoing Precision Air Services Group Managing Director and Chief Executive Officer Alfonce Kioko (left) meant for payment of an insurance claim for an employee of Precision Air Services who died while in employment. Alliance Life Assurance Ltd has insured employees of Precision Air Services and a claim is paid in case of death of an employee

older | 1 | .... | 59 | 60 | (Page 61) | 62 | 63 | .... | 3286 | newer