Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 607 | 608 | (Page 609) | 610 | 611 | .... | 3272 | newer

  0 0


  MAONYESHO ya Biashara ya Kimataifa ya Tiba Asili ya Mwafrika yamepangwa kufanyika jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia Novemba 16 hadi 23. 

  Maonyesho hayo ambayo yanafanyika nchini kwa mara ya kwanza yameandaliwa na Jukwaa la Tiba Asili Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Mamlaka ya ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE). 
  Mwenyekiti wa Kamati ya Manndalizi ya Maonyesho hayo, Boniventure Mwalongo alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa wadau mbalimbali wa Tiba Asili na Tiba Mbadala wanatarajia kushiriki katika maonyesho hayo.

   Kwa mujibu wa Mwalongo washiriki hao ni pamoja na Watabibu wa Tiba Asili, Watengenezaji wa Dawa Asili, Wakunga wa Tiba Asili, Kampuni za Dawa Asili na vipodozi vya dawa asili, Wasambazaji wa Tiba Asili na Tiba Mbadala, Watengenezaji wa vyakula asili, kliniki za tiba asili na Tiba Mbadala. 

  Aidha mwalongo alisema kuwa wanaendelea na taratibu za kufanya maongezi na wadhamini mbalimbalia ambapo watatoa taarifa rasmi baada ya kufikia tamati ya maongezi, ikiwa ni pamoja na kutoa ratiba nzima ya maonyesho hayo. 
  “Tunafanya maongezi na wadau mbalimbali ambao wameonyesha nia ya kutusaidia, lakini pia kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Ushirikiano wa Tiba Asili na Tiba za kisasa katika kuhimarisha huduma ya Afya Afrika’, alisema Mwalongo. 
  Aliongezea kuwa hadi sasa wana orodha wadau wasiopungua 280 ambao tayari wameonyesha nia ya kushiriki katika maonyesho hayo, baada ya kuwapelekea taarifa kwa njia mbalimbali za mawasiliano. Kwa mujibu wa Mwalongo, gharama za kushiriki zimegawantika katika makundi tofauti ambapo Watambuzi wa magonjwa, watengenezaji wa dawa asili, wakunga wa tiba asili, Wenye virutubisho vya tiba asili na wauzaji wa dawa asili gharama yao ni 100,000/-. 

  Kampuni za dawa asili na vipodozi asili zitalipa 500,000/-. Wasambazaji wa dawa za asili na dawa mbadala watatakiwa kulipa ada ya 1,000,000/-. Wauza vyakula asili watalipia 150,000/- wakati kliniki ya tiba asili watalipia 1,500,000/- Kliniki ya tiba mbadala gharama yake ni 2,000,000/-. Kampuni za virutubisho kutoka nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki zitalipia dola za Marekani 1,500. Viwango vingine ni dola 500 za Marekani kwa Kampuni za Tiba Asili ndani ya Jumuiya ya Afrika Mshariki. 

  Gharama za ushiriki kwa Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Taasisi za Serikali ni 2,000,000/-. Wajasiliamali wa kazi za uchongaji watalipia 500,000, wakati vyama vya tiba asili vitalipia 1,000,000. Aidha Mwalongo alitoa wito kwa makundi mengine ambayo yangependa kushiriki, kujitokeza mapema ili taratibu ziweze kufuatwa. 
  “Huenda kuna makundi mengine ambayo labda tumeyasahau, lakini milango bado iko wazi kwa yeyote ambaye angependa kushiriki maonyesho haya,” alisisitiza Mwalongo. 
   Alisema kuwa wana imani baada ya maonyesho hayo kutakuwa na mtandao mkubwa wa kibiashara katika huduma ya tiba asili na tiba mbadala kwa nchi za Afrika na hata nje ya Afrika. Aidha alisema kuwa wako mbioni kuyasajili rasmi maonyesho hayo ili yawe yanafanyika kila Agosti 30 pale inapoadhimishwa siku tiba Asili ya Mwafrika.

  0 0

   Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Iddi (wa pili kulia), akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhan Dau, alipotembelea mradi wa nyumba zinazojengwa na shirika hilo, Kijichi, Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi John Msemo. 
  Makamu wa pili Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhan Dau (kulia) na Meneja Miradi wa shirika hilo, Mhandisi John Msemo, wakimwangalia mke wa Makamu wa pili wa Rais, Mama Asha Seif, wakati akionyesha michoro wa nyumba ziliomvutia, walipotembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa, Kijichi Dar es Salaam
  Makamu wa pili Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (wa pili kulia), akiwasikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhan Dau (kulia kwake) na Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi John Msemo, wakati wakimuonyesha baadhi ya nyumba za kisasa zinazojengwa na shirika hilo, Kijichi, Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhan Dau (wa tatu kushoto), akimuonyesha Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Iddi, baadhi ya nyumba zinazojengwa na shirika hilo, Kijichi, Dar es Salaam leo. Wa pili kulia ni Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi John Msemo.
   Mhandisi Msemo akitoa maelezo ya mradi kwa Makamu wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi. Kulia ni Mkewe Mama Asha Iddi na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dkt. Ramadhan Dau
  Baadhi ya nyumba za kisasa zinazojengwa na NSSF Kijichi, Dar es Salaam.

  0 0

  Mgeni rasmi,Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Leornad Thadeo  akifungua bonanza la NGUVU YA KODI lililofanyika katika Viwanja vya chuo cha ustawi wa jamii katika siku ya kumbukumbu ya kuadhimisha miaka kumi na tano (15) tangu hayati  baba wa taifa Mwalimu Julius K Nyerere alipofariki  Dunia  Jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo limemkumbuka Baba wa Taifa kwa kutoa Elimu na maelezo ya kutosha juu ya Kodi na Nguvu yake katika kuchangia maendeleo ya Taifa letu na Kukuza uchumi.
   Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Leornad Thadeo (kushoto) akiwa na Mratibu wa Shirika La Activista Ein Ahimidiwe wakati akimkaribisha kusaini katika ubao wa saini
   Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Leornad Thadeo akisai ubao kuungana na Activista pamoja na Action Aid Tanzania katika upingaji wa watu kuto kulipa kodi
  Mkurugenzi wa Fedha wa TRA Bw.Salehe B Msholo ambaye alikuwa mgeni Rasmi katika bonanza akitia Saini yake katika ubao wa saini katika uwanja wa ustawi wa jamii siku ya kumbukumbu ya kuadhimisha miaka kumi na tano (15) tangu hayati  baba wa taifa Mwalimu Julius K Nyerere alipo fariki Dunia  Jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Na Othman Khamis Ame.OMPR
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali itaendelea na juhudi zake katika kuona mazao ya wakulima vijijini hasa chakula cha nafaka  yananunuliwa ili kuwaongezea uwezo wa kimapato wakulima hao katika kyukabiliana na ukali wa maisha. 
  Balozi Seif alisema hayo wakati akizungumza na Wananc hi wa Kijiji cha Lugagala kwenye mkutano wa hadhara baada ya kushiriki kazi za ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kijiji hicho pamoja na kuweka jiwe la msingi la nyumba za miradi ya vikundi vya uchumi katika Kijiji cha Muungano Zomba akiwa katika ziara ya siku mbili Mkoani Ruvuma kukagua shughuli za kiuchumi, ustawi wa jamii na maendeleo. 
  Alisema Serikali haiwezi kuona nguvu za Wananchi zina potea bure bila ya kuunga mkono hasa ikizingatia kwamba asilimia 90% ya Watanzania wote wanaishi katika maeneo ya uzalishaji vijijini. 
  Alifahamisha utafiti na uchunguzi wa kina utafanywa kupitia Halmashauri za Wilaya zinazohusika na uzalishaji wa mazao hayo ya biashara ili kuwadhibiti walanguzi wenye tabia ya kuwanyhonya wakulima kwa ujanja wa kununua mazao yao kwa bei ya chini. 
  Naye Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi alihimiza kwamba Kiongozi lazima awe mfano wa maendeleo ya jamii badala ya kushabikia vurugu na siasa chafu. 
  Mama Asha alisema siasa ni kwa Viongozi kusimamia juhudi na harakati za kiuchumi na maendeleo za wale wanaowaongoza kwa lengo la kuwakomboa kimaisha. Katika kuunga mkono juhudi za wananchi wa Mkoa wa Ruvuma Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alichangia Shilingi Milioni 1,500,000/- kusaidia Vikundi hivyo pamoja na kuahidi nguvu za uwezekaji kwa majengo ya vikundi hivyo. 
  Balozi Seif pia akachangia shilingi Milioni 1,500,000/- kuendeleza ujenzi wa Kituo cha Afya cha Lugagala pamoja na kuahidi kutoa mifuko mia tano ya saruji ya ujenzi wa kituo hicho.
    Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mh. Jenista Mhagana na wanavikundi vya uchumi wa Kijiji cha Lugagala wakishangiria ujio wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliyefanya ziara ya kukagua miradi ya kiuchumi na maendeleo katika kijiji pao.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiweka jiwe la msingi la uanzishwaji wa majengo ya vikundi vya uchumi katika kijiji cha Muungano Zomba Mkoani Ruvuma.
   Balozi Seif akishiriki kazi za ujenzi wa Taifa katika Kituo cha Afya cha Kijiji cha Lugagala kata ya Kilagano Mkoani Ruvuma.
   Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akiwapongeza wananchi wa Kijiji cha Lugagala kwenye Mkutano wa Hadhara kwa ushiriki wao katika shughuli za kiuchumi.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibarf Balozi Seif akiagana na Makamanda wa vikosi mbali mbali vya ulinzi na usalama kwenye uwanja wa ndege wa Songea mara baada ya kukamilisha ziara yake ya siku mbili Mkoani Ruvuma. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

  0 0

  Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Simba itakayochezwa Jumamosi (Oktoba 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 7,000. Washabiki watakaolipa kiingilio hicho ni wale watakaokaa viti vya rangi ya bluu na kijani ambavyo jumla yake ni 36,693 katika uwanja huo wenye viti 57,558. 
  Viingilio vingine ni sh. 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 20,000 kwa VIP B na C wakati VIP A itakuwa sh. 30,000. Tiketi zitakazotumika kwenye mechi hiyo ni za elektroniki, na zimeanza kuuzwa jana (Oktoba 13 mwaka huu). 
  Tiketi zinapatikana kwa mtandao wa M-PESA, CRDB Simbanking na maduka ya CRDB Fahari Huduma ambayo yapo zaidi ya mia moja sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam. Mechi hiyo namba 27 itakayochezeshwa na mwamuzi Israel Mujuni Nkongo akisaidiwa na John Kanyenye na Ferdinand Chacha itaanza saa 10 kamili jioni. 
  Kamishna wa mechi hiyo ni Salum Kikwamba kutoka mkoani Kilimanjaro. Washabiki wanatakiwa kununua tiketi mapema, kwani hazitauzwa uwanjani siku ya mechi. Milango yote ukiwemo ule wa upande wa Mbagala (Uwanja wa Ndani) itafunguliwa kwa ajili ya washabiki, na itakuwa wazi kuanzia saa 4 asubuhi. 
   Magari maalumu tu yenye stika ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia uwanjani kwa kupitia Barabara ya Mandela. Pia washabiki hawaruhusiwi kuingia uwanjani wakiwa na silaha, vitu vya vyuma na mabegi makubwa. Barabara ya kuingilia upande wa Chang’ombe itafungwa kwa watumiaji wa magari. 
   IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

  0 0
 • 10/14/14--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • P-Square - Personally

  0 0

  DSC01247
  Mkuu wa shule ya msingi Ikungi mchanganyiko wilaya ya Ikungi, Mwl. Olivary Kamilly, akitoa taarifa yake kwenye kilele cha mahafali ya 63 yaliyofanyika kwenye viwanja vya shule hiyo kongwe iliyoanzishwa mwaka 1944.

  Na Nathaniel Limu, Ikungi
  MWENYEKITI wa halmashauri ya wilaya Ikungi mkoani SIngida, Celestine Yunde, amewaagiza maafisa mipango kushirikisha viongozi wa taasisi zenye mahitaji maalumu wakati wa kuandaa bajeti.

  Mwenyekiti Yunde ametoa wito huo wakati akizungumza kwenye mahafali ya 63 ya wahitimu wa darasa la saba shule ya msingi Ikungi mchanganyiko. Alisema hatua hiyo itawajengea mazingira mazuri maafisa kutambua ukubwa wa bajeti katika taasisi husika.

  Akifafanua,Yunde alisema shule ya msingi Ikungi Mchanganyiko, ni taasisi maalum kwa madi kwamba inayo wanafunzi wenye ulemavu mbali mbali na wasio walemavu ambao baadhi wametoka nje ya mkoa.

  “Wanafunzi wenye ulemavu mbali mbali , ni wanafunzi ambao mahitaji yao mengi ni ya gharama kubwa.Ukiachilia mbali gharama za nauli wanakotoka,karibu kila kundi lina mahitaji maalum na ni ghali", alifafanua Yunde.

  Alisema wanafunzi hao walemavu wanaishi kwenye mabweni, mahitaji yao ni ya gharama kubwa na hivyo halmashauri inayo jukumu la kushirikisha viongozi wa shule hiyo,wakati wa kuandaa bajeti itakayokidhi mahitaji.
  DSC01263
  Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi,Celestine Yunde, akizungumza kwenye mahafali ya 63 ya shule ya msingi Ikungi mchanganyiko yaliyofanyika kwenye viwanja vya shule hiyo.


  0 0

  3
  Meneja wa mradi wa CIRDA kutoka UNDP, Bonizella Biagini akizungumza wakati akitambulisha maofisa waliokuwepo katika uzinduzi wa warsha ya siku tatu ya kimataifa ya ukusanyaji na matumizi ya taarifa ya hali ya hewa kwa nchi 12 duniani. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa mataifa la Mipango ya maendeleo duniani (UNDP) Phillippe Poinsot, Mwakilishi wa Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Binilith Mahenge, Bw. Richard Muyungi.

  Na Mwandishi wetu
  MATAIFA 11 ikiwemo Tanzania yanakutana jijini Dar kwa mafunzo ya siku tatu yanayohusu utengenezaji wa mifumo bora ya upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa,uchakataji wake na matumizi ya taarifa hizo kwa wananchi wa kawaida na watunga sera ili kuwa na uhakika na Mipango ya maendeleo.

  Mataifa hayo ni yale yalioyopo katika mradi wa Multi Country Support Programme to Strengthen Climate Information Systems in Africa (CIRDA).
  Nchi zinazohusika katika mpango huu pamoja na wenyeji Tanzania ni Benin, Burkina Faso, Ethiopia, the Gambia Liberia, Malawi, Sierra Leone, Sao Tome and Principe,Uganda na Zambia.

  Mpango wa CIRDA unafadhiliwa na Global Environment Facility (GEF) na Least Developed Country Fund (LDCF) ukilenga kuwezesha utumiaji wa teknolojia mpya miongoni mwa wakulima, watunga sera na sekta binafsi ili kuweza kufanya maamuzi sahihi kwa kuzingatia taarifa sahihi za hali ya hewa.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkazi wa UNDP,Phillippe Poinsot Mpango wa CIRDA, ambao ni mfano wa kuigwa kwa juhudi za mataifa ya Afrika ya kuwa na ubadilishanaji wa maarifa na taarifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, huzingatia uhusishaji wa sekta binafsi, matumizi ya simu na takwimu za kilimo (agricultural index insurance).
  DSC_0083
  Akifungua mafunzo hayo, kwa niaba ya waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa rais, mazingira Binilith Mahenge, Ofisa anayeshughulikia mradi huo nchini Richard Muyungi alisema mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka ambapo dunia nzima iko katika changamoto kubwa ya mabadiliko ya tabianchi.


  0 0


  0 0

  Kiongozi wa mbio za mwenge 2014 Rachel Kassandra akikabidhi mwenge wa Uhuru kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa maadhimisho ya kilele cha mbio za mwenge ulius na kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora leo.Kulia ni Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na michezo Dkt.Fenela Mkangara. 

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mwenge wa Uhuru wakati wa maadhimisho ya kilele cha mbio za mwenge ziizofanyika mkoani Tabora leo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mbio za mwenge mwaka huu wakati wa maadhimisho ya kilele cha mbio hizo zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora leo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa kilele cha mbio za mwenge 2014 ziilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora leo. Picha na Freddy Maro.
  Kupata hotuba ya Rais Kikwete BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

   Pichani (wa tatu kulia),Meneja Matekelezo Mfuko wa Pensheni wa LAPF,Bwa.Victor Kikoti akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani),mapema leo katika ofisi zao zilizopo jengo la Millenium Tower,Kijitonyama jijini Dar,kuhusiana na kufanyika kwa mkutano wao wa 7 wa mwaka wa wadau kuanzia Oktoba 23 mpaka 24, 2014.

  Mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano (AICC),jijini Arusha.Bwa.Victor amesema kuwa kauli mbiu ya mkutano huo ni '' kusherehekea miaka 70 ya ukuaji na huduma bora kwa Wanachama''. '' Kauli mbiu hii imefikiwa baada ya mfuko kutimiza miaka 70 tangu ulipoanzishwa mwaka 1944,ambapo Wadau wa mkutano huo watajadili kwa kina juu ya huduma za LAPF kwa miaka 70iliyopita pamoja na kushiriki mafanikio ya mfuko kwa pamoja.

  Matekelezo Mfuko wa Pensheniwa LAPF,Bwa.Victor Kikoti amesema kuwa,Mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwaWAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh.Hawa Ghasia
   
  Pichani kulia ni Meneja Mkoa Bwa.Ramadhani Mkeyange,Meneja Takwimu,Tathmini na Hadhari Bwa.Abubakar Ndwata pamoja na Meneja wa Kanda ya Dar,Bi.Amina Kassim
   Meneja Takwimu,Tathmini na Hadhari Bwa.Abubakar Ndwata,akifafanua moja ya swali aliloulizwa na Waandishi wa Habari kuwa mfuko wa LAPF unaendelea kujivunia mafanikio ya kuwa mfuko unaokuwa kwa kasi hapa nchini pamoja na kuwa bora kwa miaka mitano mfululi kwenye suala zima la uwajibikaji na utunzaji wa vitabu.

  Amesema kuwa mfuko pia utazindua logo mpya  inayotumika,ambayo  inaashiria ukuaji wa mfuko huo na dhamira yao ya kuendelea  kukua zaidi  na kuboresha huduma kwa wanachama wao,ameongeza kusema kuwa mfuko huo utatoa fursa  mpya ya mkopo wa elimu kwa wanachama wake ilivyozinduliwa mwezi Agosti mwaka huu.
  Pichani ni baadhi ya wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo wa LAPF.

  0 0

  Kampuni ya African Barrick Gold (ABG) imesaini mkataba wa miaka miwili (MoU) na Chuo Kikuu cha Afya cha Muhimbili (MUHAS) idara ya Mazingira na Afya bora kazini(Environmental and Occupational Health Sciences) ili kuboresha taluma za madaktari.

  Ushirikiano huu utawezesha wanafunzi wa idara hiyo kupata nafasi za kwenda kufanya masomo kwa vitendo yani (field practise) kwenye ofisi na migodi ya kampuni ya ABG, pia pesa hizo zitatumika kwenye kukarabati majendo na utoaji wa vifaa mbalimbali vya maabara na utafiti kwenye kitivo hiyo ya Mazingira na Afya bora kazini.

  Mkataba huu unathamani ya zaidi ya shilingi za Kitanzania milioni 300jiwa kuanzisha mfumo maalumu wa kuwasaidia wanafunzi wa kitivo cha Mazingira na Afya Kazini, kwa lengo la kuimarisha maarifa ya wahitimu wenye mafunzo ya vitendo.

  Akizungumza katika tukio hilo, Bw,Deo Mwanyika: Makamu wa Rais Shughuli za Ofisi: amesema "Kwa miaka miwili iliyopita ABG, imekuwa ikushirikiana na MUHAS ili kusaidia na kuboresha ujuzi wa wanafunzi na wafanyakazi kwa lengo la kukuza na kuendeleza wataalamu wenye vipaji.

  Makubaliano haya tunayo saini leo yatawapa nafasi wanafunzi bora 20 kupata misaada ya kifedha kwa miaka miwili ijayo. Zaidi ya hayo wanafunzi watapata fursa za kufanya mafunzo kwa vitendo kwenye migodi yetu kupitia mpango huu".

  Sisi kama ABG,tutaendelea kufanya kazi na taasisi nyingine ili kutafuta ufumbuzi wa uhaba wa wataalamu wenye ujuzi wa madini kwa usimamizi bora wa sekta ya madini Tanzania.

  Na kama sehemu ya Chama cha Madini na Nishati Tanzania (TCME) na Mpango maendeleo ya ujuzi, ABG na wadau wengine ambao ambao wanatoa Mafunzo ya Ufundi (IMTT) ya muda mrefu ili kukidhi mahitaji ya haraka ya sekta ya madini inayokua haraka.
  Kaimu Mkuu wa Chuo cha Sayansi ya Afya cha Muhimbili (MUHAS) Prof. Ephata Kaaya (kushoto) akiwa na Makamu wa Rais wa shughuli za Ofisi wa African Barrick gold,Deo Mwanyika Wakitiliana saini ya makubalino ya miaka miwili ambapo kampuni ya ABG imetoa zaidi ya TSH 300 ili kusaidia wanafunzi na wafanyakazi wa MUHAS kitivo cha Mazingira na Sanyansi ya Afya bora Makazini, makubaliano hayo pia yatasaidia wanafunzi kupata nafasi za kufanya mazoezi ya vitendo kwenye migodi ya ABG, na vilevile kukarabati majengo, ada za wanafunzi bora,kununua vifaa vya maabara na kutenga fungu la kufanya utafiti.
  Kaimu Mkuu wa Chuo cha Sayansi ya Afya cha Muhimbili (MUHAS) Prof. Ephata Kaaya (kushoto) akiwa na Makamu wa Rais wa shughuli za Ofisi wa African Barrick gold,Deo Mwanyika Wakibadilisha mikataba baada ya kutiliana saini makubalino ya miaka miwili ambapo kampuni ya ABG imetoa zaidi ya TSH 300 ili kusaidia wanafunzi na wafanyakazi wa MUHAS kitivo cha Mazingira na Sanyansi ya Afya bora Makazini, makubaliano hayo pia yatasaidia wanafunzi kupata nafasi za kufanya mazoezi ya vitendo kwenye migodi ya ABG, na vilevile kukarabati majengo, ada za wanafunzi bora,kununua vifaa vya maabara na kutenga fungu la kufanya utafiti.


  0 0

  Na Saidi Mkabakuli

  Ugeni kutoka Tume ya Mipango na Maendeleo ya China imevutiwa na kasi ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania hali inayochochewa na mipango thabiti ya kuvutia uwekezaji hasa kwenye Maeneo Maalum ya Kiuchumi (SEZs).

  Akizungumza wakati wa kikao cha pamoja na viongozi wa Tume ya Mipango ya Tanzania, Kiongozi wa Msafara huo, Bw. Wang Jianjun ambaye ni Naibu Mkurugenzi Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, alisema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi chache barani Afrika zenye fursa kubwa ya kufikia maendeleo na kuweza kuondoka kwenye kundi la nchi maskini ndani ya kipindi kifupi kijacho.

  Bw. Jianjun aliongeza “ili kuweza kufikia maendeleo ya haraka zaidi, Tanzania inapaswa kuwekeza katika viwanda ili kuongeza tija katika uzalishaji na kuongeza thamani bidhaa zake ili kuvutia masoko toka nje ya nchi.”

  Akizungumza wakati wa kuwakaribisha wageni hao, Naibu Katibu Mtendaji anayeshughulikia Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Kiuchumi, Bw. Paul Sangawe, amesema kuwa Tanzania imedhamiria kuwa nchi ya viwanda ndani ya muda mfupi ujao.

  “Tumedhamiria kuwekeza nguvu zetu kwenye uwekezaji katika viwanda; katika Mpango wa Pili wa Maendeleo, nguvu kubwa tunaiweka katika maendeleo ya viwanda ili kuweza kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025,” alisema Bw. Sangawe.

  Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 imedhamiria kuifikisha Tanzania kuwa nchi yenye hadhi ya kipato cha kati na kuondokana na umaskini kufikia mwaka 2025.
  Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla), Prof. Longinus Rutasitara (Wapili kushoto) akizungumza na Ugeni kutoka Tume ya Mipango na Maendeleo ya China wakati walipofanya ziara nchini. Kushoto ni Naibu Katibu Mtendaji (Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Kiuchumi), Bw. Paul Sangawe.
  Naibu Katibu Mtendaji (Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Kiuchumi), Bw. Paul Sangawe akizungumza wakati wa ziara hiyo. Kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri.


  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba Taifa la Tanzania hivi sasa linahitaji kuendelea kuwa na hali nzuri ya amani kuliko wakati mwengine wowote kutokana na kwamba linapita katika kipindi cha kuundwa kwa Katiba mpya.

  Balozi Seif alieleza hayo wakati wa hafla fupi ya kuweka jiwe la Msingi la Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Kijiji cha Peramiho uitwao Masjid Jidah akiwa katika ziara ya siku mbili Mkoani Ruvuma kukagua shughuli za maendeleo, kiuchumi pamoja na ustawi wa jamii.

  Alisema zipo dalili za wazi zinazoonyesha baadhi ya watu, viongozi na hata makundi ya kijamii na kidini zinaanza kujikita katika kuichezea amani ya nchi jambo ambalo ni hatari kwa hatma ya wananchi.

  Balozi Seif alisema kwamba Kizazi cha sasa na kile kijacho kinahitaji kutengenezewa mazingira mazuri ya mfumo wa maisha yao ili kiepukane na wimbi la migogoro inayoonekana kuyakumba mataifa mbali mbali duniani.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaasa waumini hao wa Dini ya Kiislamu wa Peramiho kuendelea kushikamana kama dini yao inavyosisitiza suala la kutunza amani, utulivu na kuvumiliana baina yao na wale wa imani nyengine.

  Alisema wapo baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wanaopenda kuleta mtafaruku ndani ya maeneo ya dini vitendo ambavyo havina tija na ni lazima viepukwe kwa hali yoyote ile.

  “ Tumeshuhudia mfano wa ushirikiano ulioonyeshwa hivi karibuni na makundi ya dini na madhehebu mbali mbali yalipoamua kucheza mechi ya kirafiki iliyozikutanisha timu za amani na Mshikamano katika dhana ya kudumisha umoja jambo ambalo sisi tulio nyuma yao tunapaswa kuliiga “. Alisema Balozi Seif. Alisisitiza kwamba waumini na hata wananchi wote nchini wanapaswa kujifunza matokeo ya kutetereka kwa amani yaliyotokea katika nchi tofauti ulimwenguni ambazo hivi sasa hali ya maisha ya wanawake na watoto yamekuwa hatarini.

  Alifahamisha kwamba nchi hizo hivi sasa hazikaliki kutokana na kuichezea amani yao hali inayopelekea hata shughuli za kiuchumi na maendeleo kushindwa kutekelezeka.

  Akitoa taarifa fupi ya ujenzi wa Msikiti huo wa Ijumaa wa Kijiji cha Paremiho mjumbe wa kamati ya Masjid Jidah Sheikh Ali Namawela alisema tathmini ya ujenzi wa msikiti huo inakisiwa kugharimu shilingi za Kitanzania Milioni Sitini { 60,000,000/- } hadi kukamilika kwa msikiti huo. Sheikh Ali alisema kuyumba kwa ujenzi wa msikiti huo kunatokana na wachangiaji wengi wa msikiti huo kuchelewa kupata malipo ya fedha zao kutokana na mauzo ya mazao yao ya kilimo.

  Mjumbe huyo wa Kamati ya Uongozi wa Msiki huo alifahamisha kwamba hadi sasa ujenzi unaoendelea wa hatua ya msingi umeshafikia gharama ya shilingi milioni Kumi. Katika kuunga mkono juhudi za waumini hao wa dini ya Kiislamu Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alichangia shilingi Milioni 1,500,000/- ili kuendeleza harakati za ujenzi huo.

  Balozi Seif pia akaahidi kuchangia matofali elfu 10,000 kuendeleza ujenzi huo pamoja na kuahidi kuchangia mabati itakapofikia hatua ya uwezekaji ili kutoa fursa na nafasi nzuri kwa waumini hao kufanya ibada zao katika mazingira mazuri.
  Kikundi cha dhikri cha Msikiti mkuu wa Ijumaa wa Kijiji cha Peramiho Mkoani Ruvuma kikimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hayupo pichani kukagua ujenzi wa msikiti wao.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akihutubia waumini wa dini ya Kiislamu wa Kijiji cha Peramiho alipofanya ziara fupi na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa msikiti huo.Kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe ambae pia Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kepteni Aseri Msanga na sheikh Mkuu wa Kijiji cha Peramiho Sheikh Said Rasid, wakati kushoto yake balozi ni mkewe Mama Asha Suleiman Iddi.
  Baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu wa Kijiji cha Peramiho wakimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif hayupo pichani wakati alipote mbelea harakati za ujenzi wa msikiti wao wa ijumaa wa Masjid Jidah.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na ujumbe wake akikagua ujenzi wa msikiti wa ijumaa wa kijiji cha Peramiho wakati wa ziara yake ya siku mbili Mkoani Ruvuma.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Kijiji cha Peramiho { Masjid Jidah } mara baada ya kuwahutubia waumini wa msikiti huo. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

  0 0

  Kamishna wa Ustawi wa Jamii,Bw. Dunford Makalla akikata utepe kuashiria ufunguzi wa mtambo wa mpya wa kusafishia maji safi na salama katika Mahabusu ya Watoto iliyopo Upanga,jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni wafanyakazi wa Kampuni ya Davis&Shirtliff.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya DAVIS & SHIRTLIFF, Bw. Benjamin Munyao akimuonyesha Kamishna Wa Ustawi wa Jamii, Bw. Dunford Makalla jinsi mtambo huo unavyofanya kazi ya kusafisha maji na kuwa salama na safi kwaajili ya Kunywa.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya DAVIS & SHIRTLIFF, Bw Benjamin Munyao akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) pamoja na wageni waalikwa juu ya mtambo wa kusafishia maji walioutoa kwa Mahabusu ya Watoto,iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Kamishna Wa Ustawi wa Jamii,Bw. Dunford Makalla na Kaimu Afisa Mfawidhi wa Mahabusu ya Watoto iliyopo Upanga,Bi Zuhura Mfinanga
  Kamishna Wa Ustawi wa Jamii,Bw. Dunford Makalla akiishukuru kampuni ya Davis & Shirtliff kwa kujitolea kuisaidia Mahabusu ya Watoto. Pembeni yake ni Kaimu Afisa Mfawidhi wa Mahabusu ya Watoto,Bi Zuhura Mfinanga.

  0 0

  Na Samwel Mtuwa.

  Wakala wa Jiolojia Tanzania , umefanikiwa kupunguza gharama za upimaji wa sampuli za dhahabu katika maabara yake kwa kufanikiwa kwa asilimia mia moja kuweza kutengeneza vikombe vya kupimia dhahabu (Crusible) ndani ya maabara yake ya Jiolojia mkoani Dodoma.

  Kwa mujibu wa mtaalam wa Jioloji katika Maabara ya GST, Bw. Philipo Momburi alieleza kuwa hapo awali maabara ilikuwa inaagiza vikombe vya kupimia dhahabu maabara kutoka nje ya nchi , jambo ambalo lilikuwa likiingiza taasisi katika gharama kubwa , lakini baada ya utafiti wa kuandaa vikombe vya kupimia sampuli ya dhahabu kukamilika umeweza kupunguza ghara kwa asilimia hamsini (50%).

  Bw. Momburi aliongeza kuwa utafiti ulianza mwaka 1994 ambapo ulidumu kwa miaka ishirini kabla ya kukamilika, ambapo baada ya kukamilika  utekelezaji wake ulianza rasmi mwaka  2013, kutokana na kukamilika kwa utafiti   GST imeweza kuongeza huduma za kibiashara kwa kuongeza idadi ya upimaji wa sampuli kutoka vikombe 20 mpaka 40 kwa siku.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maabara ya Jioloji GST Bi Augustine Rutaihwa, aliongeza kuwa baada ya kuweza kutengeneza vikombe hivyo , taasisi imeweza kupata  ubora mzuri wa upimaji wa sampuli  katika maabara ya  GST , kuongeza ujuzi kwa wataalamu , kutoa huduma kwa wakati , lakini pia kuweza kutumia malighafi za ndani badala ya kuagiza kutoka nje ya nchi.

  Maabara ya upimaji wa sampuli za  madini ilianzishwa mwaka 1929 kwa ajili ya kuboresha shughuli za Idara hasa kwa upande wa uchambuzi wa kimaabara wa sampuli za miamba , madini na maji.
  Mtaalam wa Jiolojia Bw. P.B Momburi akieonesha vikombe vya kupimia dhahabu katika maabara ya Wakala wa Jiolojia Tanzania.

  0 0

   Meneja Biashara wa Bayport Tanzania, Thabit Mndeme kushoto; na Meneja Masoko na Mawasiliano (katikati), Ngula Cheyo waki zinduwa Mkopo wa Bidhaa, Bayport Head office Daressalaam.
  =====  =====  =====
  TAASISI ya kifedha ya Bayport Tanzania, leo imezindua huduma mpya ijulikanayo kama Mikopo ya Bidhaa ikiwa na lengo la kurahisha utendaji kazi wa watumishi wa umma na wafanyakazi wote wa kampuni zilizoidhinishwa na Bayport.

  Uzinduzi huo uliofanyika jana, umeonyesha matumaini mapya ya Watanzania wanaosumbukia usafiri katika vituo vyao vya kazi, hususan maeneo ya mikoani ambako mara kadhaa kumesikika malalamiko ya maisha magumu ya watumishi wa umma.

  Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Meneja Biashara wa Bayport Tanzania, Thabit Mndeme, alisema kwamba  ni wakati wa kukuza uchumi wan chi kwa kuhakikisha kuwa watu wote wanafanya kazi kwa bidii na shauku yote.

  Alisema wapo watumishi ambao wanaishi kwa tabu kutokana na changamoto ya usafiri na mahitaji mengine ya kijamii, hivyo kwa kupatikana hudumaa mpya ya kukopeshwa pikipiki bodaboda ni jambo zuri kwao.

  ‘’Bayport tumekaa na kuangalia namna gani Watanzania wataendelea kufanya kazi kwa moyo na kukuza uchumi wetu, tukaona sambamba na kuwakopesha fedha kama tunavyofanya, pia tuwakopeshe bidhaa kama vile Boxer, Toyo na Lifan.

  ‘’Zote hizi zitakuwa kwenye mpangilio mzuri sambamba na kuzikatia huduma ya bima, kuzifanyia servise mara tatu bure, garantii ya mwaka mmoja, huku mkopaji akitakiwa kulipa kwa miezi 36 sawa na miaka mitatu,’’alisema Mndeme.

  Naye Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Tanzania, Ngula Cheyo, alisema kuwa mikopo hiyo mipya itapatikana kwa masaa 24, huku ikipatikana pia kwa mikoa yote na wilaya zote kwenye ofisi za Bayport Tanzania.

  ‘’Tunawaomba watu waendelee kuiunga mkono Bayport kwa kuhakikisha kuwa wanachangamkia fursa hii ya mikopo ya bidhaa ambayo tumeianzisha ili kuwafanya watumishi wa umma na wafanyakazi wengine warahisishiwe utendaji wao wa kazi,’’ alisema Cheyo.
     

  0 0

  Na: Atley Kuni- Afisa habari Mwanza. 
   Halmashauri za majiji na manispaa zimehimizwa kutunza na kuhifadhi miradi yote ya maendeleo inayo tekelezwa katika maeneo yao na kuhakikisha inadumu kwa manufaa ya kizazi cha leo na kijacho. 
   Kauli hiyo imetolewa mapena hivi leo na Zuberi Samataba, Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) katika hoteli ya Gold Crest Jijini Mwanza wakati wa kikao cha pamoja baina ya TAMISEMI, Benki ya Dunia (World Bank) DANIDA na watendaji kutoka halmashauri zinazo tekeleza miradi ya Tanzania Strategic Cities Project (TSCP). Samataba, amesema, kuna haja kwa kila halmashauri kuhakikisha inatunza miradi yote ambayo inafadhiliwa na wahisani hata baada ya wahisani kumaliza muda wao na kuondoka kasha miradi hiyo mikononi mwa Halmashauri. 
  "Ni vyema mkawa mnatenga fedha kwa ajili yakuhudumia miradi inayo anzishwa na wafadhili kwa ajili ya ukarabati na kuimarisha ili iendelee kudumu kwa muda mrefu hata baada ya miradi hiyo kuisha muda wake na wafadhili kuicha mikononi mwetu". Katika hatua nyingine amewaagiza watendaji hao kutoa taarifa kwa wakati ili kujenga imani kwa wafadhili wanao toa fedha zao kwa ajili ya miradi mbali mbali ya maendeleo wanayo ifadhili, 
  "Wenzetu suala la mrejesho ni muhimu sana lakini zaidi sana mrejesho kwa wakati, kwani ni kama wanasheria wanavyo amini kuwa HAKI ILIYO CHELEWESHWA NI HAKI ILIYO NYIMWA". kwa mantiki hiyo kutoa taarifa kwa wakati ni suala muhimu sana, vinginevyo au kinyume chake nikuwafanya wafadhili kupoteza imani kwa wanao wafadhili kwenye miradi amesema na kuongeza kuwa kwa kuwa serikali inaondoka kwenye utendaji wa kawaida na kuelekea kwenye utendaji wa upimaji ufanisi kwa matokeo (Performance for Result ) hivyo moja ya kigezo muhimu kitakachotumika ni kupima matokeo ni uwasilishaji wa taarifa kwa wakati. 
   Kikao hicho cha siku tatu kina wakutanisha Watendaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Halmashauri Jiji la Mwanza , Manispaa ya Ilemela, Manispaaya Kigoma Ujiji, Manispaa ya Dodoma, (CDA), Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Halmashauri ya mikindani Mtwara, Jiji la Tanga, Jiji la Arusha pamoja na wawakilishi wa DANIDA sambamba na Benki ya Dunia.
  BW. ONOUR OZLY- MWAKILISHI WA BENKI YA DUNIA, ALIPOKUWA AKITOA MALEZO MAFUPI KUHUSU LENGO LA MKUTANO HUO.
  NDG. ZUBERI M. SAMATABA, KAIMU KATIBU MKUU- OWM-TAMISEMI AKIFUNGUA MKUTANO HUO  . .

  BI. JANE JACOB- MWAKILISHI WA DANIDA ALIPOKUWA AKITOA SALAM ZA DANIDA KATIKA KIKAO CHICHO.
   WASHIRIKI WA MKUTANO HUO WAKIFURAHIA JAMBO WAKATI WA MKUTANO HUO.
  MHANDISI EZEKIELI MAGOTI KUNYALANYALA, AKIWASILISHA MADA 

  0 0


older | 1 | .... | 607 | 608 | (Page 609) | 610 | 611 | .... | 3272 | newer