Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

Article 13


ajali yaua watu wawili na kujeruhi wawili mkoani lindi

$
0
0
Na Abdulaziz Ahmed, Lindi
Watu wawili wamekufa na wawili kujeruhiwa baada ya gari waliyokuwa wanasafiria kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha Michenga, wilaya ya Ruangwa Ruangwa mkoani Lindi.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Lindi, ACP Renatha Mzinga alisema gari hiyo aina ya Toyota Rava4 yenye namba za usaji T574CWC.Iliyokuwa inaendeshwa na Mohamed Mchalaganya(27) iliacha njia na kupinduka katika barabara ya Ruangwa-Nanganga, ilitokea jana saa 11.30 jioni.

Kamanda Mzinga aliwataja waliokufa kwenye ajali hiyo kuwa ni Binasa Mapua(51) mkazi wa Tabata Dar-eS-salaam na Elizabeth Chipoleka(53),mkazi wa Yombo, Dar es salaam.

Kamanda Mzinga amewataja waliojeruhiwa kuwa ni Mussa Mchalanganya na Rashid Mchalanganya ambaye ni mwanafunzi katika Chuo cha Usafirishaji (NIT), ambapo wote ni wakaazi wa Tabata, Dar es salaam. Dereva wa gari hilo ametiwa mbaroni na upelelezi unaendelea kujua chanzo hasa cha ajali hio.

IPU underway in Geneva, EALA Speaker Zziwa addresses General Assembly

$
0
0
East African Legislative Assembly

The 131st Inter-Parliamentary Union Conference commenced in Geneva, Switzerland yesterday with a clarion call to end violence against women and to strive to tackle growing threats to global peace, security and human rights.

The global conference will also see the election of a new President of the IPU following the expiry of the three year term of incumbent, Hon Abdelwahad Radi of Morrocco.

In his remarks, the out-going President of the IPU, Abdelwahad Radi remarked that the Assembly had committed to enhancing its role in championing for democracy and towards ensuring equity, equality and justice for all.   He said that gender inequality and violence continues to undermine equal opportunities and human rights. 

The UN Secretary General, Ambassador Ban Ki Moon called for more advocacy for women and an increase in numbers of women in Parliament.   In a brief recorded message to the participants, the UN Chief said it was important for the IPU to champion the cause for gender equality as a means to realizing the Millennium Development Goals (MDGs).

The Speaker of EALA, Rt. Hon (dr) Margaret Nantongo Zziwa urged Partner States to embrace affirmative action in decision making to support gender equality.  Rt. Hon Zziwa also called for enhanced sensitization to reverse the trend.

“Sensitization of the men through all forms of education, role modeling “”and constant reminding is important to enable them to realize that women must co-exist in all spheres of life to ensure sustainability and development. Empowering women and the girl child through education like gender equality and role modeling clubs will help reduce their vulnerability and dependency solely on the male gender or spouse.”

The Speaker of the Parliament of Uganda, Rt. Hon Rebecca Kadaga noted that research on domestic violence against women, particularly, on the causes and consequences of violence had shown increase in the vice over time.

“Despite the recommendation, many cases of violence still go unreported. In a survey conducted in the 28 EU States, 42,000 women revealed that only 14% of women reported their most serious incident of intimate partner violence to the police, and among 13% reported most serious non-partner violence to the police - many simply because statistics of dead women, due to the clan or trade land settling that prevents victims from “embarrassing” the family in speaking out”, the Speaker noted.

Rt. Hon Kadaga who is an Executive Committee Member of the IPU, remarked that girls and women continued to be maimed, assaulted and killed as they go on with their daily duties. Speaker Kadaga called for more sensitization to embrace change in the Community.   She called for additional legislation on protection of violence against women.  

The Speaker of New Zealand Parliament Rt. Hon David Carter, noted that his country had made significant progress in empowerment of women and that there was more representation in Parliament by women today as it strives for equal and proportional representation.

An unprecedented 744 MPs from 141 countries, including 104 Speakers and Deputy Speakers of Parliaments are attending the IPU Assembly.  The Assembly expects to adopt some emergency items. The current proposals include fighting terrorism and extremism, protecting the rights of the Palestinian people, addressing sovereign debt crises and combating human trafficking.

The elections of the new President of IPU takes place on October 16, 2014. Indonesian MP Nurhayati Ali Assegaf, Speaker of the Australian Parliament Bronwyn Bishop, Bangladesh MP Saber Chowdhury and former Speaker of the Maldives Parliament Abdulla Shahid have so far declared their candidature for the post.
 
The election, will cement a new leadership structure following the election of the first African IPU Secretary General Martin Chungong (Cameroon) in March this year.


The Inter-Parliamentary Union (IPU) also formally welcomed back the Republics of Guinea and Madagascar as Members of the Organization. Their re-admission of both countries at the opening session of IPU’s 131st Assembly in Geneva increases IPU membership to 166 national parliaments.
 
Guinea had previously been an IPU Member between 1996-2007 and 2008-2009. Both departures from the Organization were due to the political instability in the West African country - the last one in 2009 following the dissolution of the National Assembly by a military coup in December 2008.


In earlier meetings called on the sidelines of the Assembly, young Parliamentarians from 61 countries called for wide-ranging measures to be put in place to ensure the world’s youth are politically engaged and represented at the conclusion of the first global conference of its kind.
 
More than 180 young MPs, youth leaders and experts yesterday, identified youth quotas for parliaments and political parties among several key actions to assure youth political representation and participation. Currently MPs under 30 years of age represent less than two per cent of Parliamentarians.


Faces Of Africa - Mwalimu Julius Nyerere by CCTV News

VIINGILIO MECHI YA SIMBA NA YANGA VYATAJWA

$
0
0
Afisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania,Boniface Wambura akizungumza na wanahabari,wakati akitangaza viingilio na utaratibu wa kuingia uwanjani katika Mechi ya Watani wa Jadi,Simba na Yanga unaotaraji kuchezwa Oktoba 18,2014 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Picha na Othman Michuzi.
Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Simba itakayochezwa Jumamosi (Oktoba 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 7,000.

Washabiki watakaolipa kiingilio hicho ni wale watakaokaa viti vya rangi ya bluu na kijani ambavyo jumla yake ni 36,693 katika uwanja huo wenye viti 57,558. Viingilio vingine ni sh. 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 20,000 kwa VIP B na C wakati VIP A itakuwa sh. 30,000.

Tiketi zitakazotumika kwenye mechi hiyo ni za elektroniki, na zimeanza kuuzwa jana (Oktoba 13 mwaka huu). Tiketi zinapatikana kwa mtandao wa M-PESA, CRDB Simbanking na maduka ya CRDB Fahari Huduma ambayo yapo zaidi ya mia moja sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo namba 27 itakayochezeshwa na mwamuzi Israel Mujuni Nkongo akisaidiwa na John Kanyenye na Ferdinand Chacha itaanza saa 10 kamili jioni. Kamishna wa mechi hiyo ni Salum Kikwamba kutoka mkoani Kilimanjaro.

Washabiki wanatakiwa kununua tiketi mapema, kwani hazitauzwa uwanjani siku ya mechi. Milango yote ukiwemo ule wa upande wa Mbagala (Uwanja wa Ndani) itafunguliwa kwa ajili ya washabiki, na itakuwa wazi kuanzia saa 4 asubuhi.

Magari maalumu tu yenye stika ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia uwanjani kwa kupitia Barabara ya Mandela. Pia washabiki hawaruhusiwi kuingia uwanjani wakiwa na silaha, vitu vya vyuma na mabegi makubwa. Barabara ya kuingilia upande wa Chang’ombe itafungwa kwa watumiaji wa magari.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

ANKAL IRENE ASHEREHEKEA KUHITIMU DARASA LA SABA

$
0
0
Mwanafunzi Irene Philibert Ndaki akiwa amepozi kwa furaha na zawadi zake siku ya sherehe yake ya kumaliza darasa la saba katika shule ya msingi Kigano iliyopo Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma,sherehe iliyofanyika jumamosi katika ukumbi wa chuo cha ualimu Kasulu

Group la Kandanda katika Mtandao wa Facebook kuadhimisha miaka mitano ya uwepo wake

$
0
0
Group  la Kandanda katika Mtandao wa Facebook tarehe 25/10/2014 litakuwa likitimiza miaka 4 tangu kuanzishwa ndani ya facebook.

Kuadhmisha siku hiyo, Members wa Kundi hilo wametengeneza timu ambazo ni #TeamDizomoja na #TeamIsmail, ambazo zitachuana siku hiyo katika viwanja vya TCC Sigara-Chang’ombe.

Timu hizo zote mbili zimekuwa na maandalizi ya Takribani Miezi miwili sasa, na usajili ulishafungwa tarehe 11/10/2014.

Sherehe hizo zinatarajiwa kuanza saa 3 Asubuhi ikifuatiwa na Offline Socializition ya members wa kundi hilo ambao hutumia 24/7 kujadili masuala ya soka katika Facebook.

Kamati ya maandalizi inawakaribisha wanakandanda wote kwa makabila (Timu) tofauti popote mlipo katika viwanja hivyo vya TCC Sigara, usisahau Jezi yako tuu! Ndicho kitambulisho cha Kabila zetu (timu zetu).


BURIANI BURIANI PROFESA ALI MAZRUI

$
0
0
Oktoba  14,  mwaka jana  Uwakilishi wa Kudumu wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa  uliandaa hafla ya kwanza ya aina yake ya kumkumbuka na kumuenzi Baba wa Taifa  Mwalimu Julius   kambarage Nyerere.  
Hafla hiyo ilihudhuriwa na  Wanadiplomasia wanaoziwakilisha nchi zao hapa  Umoja wa  Mataifa na wageni mbalimbali. Ni hafla iliyoambatana na uzinduzi wa kitabu kinachomhusu Baba wa Taifa. Kitabu hicho   kiliandikwa kwa ufundi mkubwa na Profesa Ali Mazrui   kwa kushirikiana na  Profesa Linda Mhando ambaye ni Mtanzania. 
Uwakilishi wa Kudumu wa  Tanzania  katika Umoja wa Mataifa  umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa  za kufariki Profesa Ali Mazrui. Ulitufunza mengi siku ile kumhusu Mwalimu na ambayo pengine hayajapatwa kuandikwa popote. Mwenyezi Mungu aiweke Mahali Pema Peponi Roho ya Marehemu Profesa Ali Mazrui 
Amen.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWAONGOZA WANANCHI WA SENGEREMA KUMZIKA DKT. SHIJA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dkt. William Shija, wakati wa shughuli za maziko yaliyofanyika Kijijini kwake, Nyampande Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza, jana Oktoba 13, 2014.
Spika wa Bunge la Jamhuri, Mhe. Anne Makinda, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dkt. William Shija, wakati wa shughuli za maziko yaliyofanyika Kijijini kwake, Nyampande Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza, jana Oktoba 13, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dkt. William Shija, wakati wa shughuli za maziko yaliyofanyika Kijijini kwake, Nyampande Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza, jana Oktoba 13, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dkt. William Shija, wakati wa shughuli za maziko yaliyofanyika Kijijini kwake, Nyampande Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza, jana Oktoba 13, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika Kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dkt. William Shija, wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika Kijijini kwa marehemu, Nyampande Wialaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza jana, Oktoba 13, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bialal, akiwafariji wanafamilia wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dkt. William Shija, wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika Kijiji ch Nyampande Wilaya ya Sengerema, Mkoa wa Mwanza jana, Oktoba 13, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakijumuika na waombolezaji wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika nyumbani kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dkt. William Shija, Kijiji cha Nyampande Wilaya ya Sengerema, jana Oktoba 13, 2014. Picha na OMR

TAARIFA YA MSIBA KUTOKA TTCL

$
0
0
Menejimenti ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) inasikitika kutangaza kifo cha mfanyakazi mwenzao Bw. Amin Elias Mbaga aliyekuwa Meneja Uhusiano kilichotokea tarehe 13.10.2014 katika Hospitali ya Regency jijini Dar es Salaam. Mipango ya Mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Sinza Kumekucha.

Ibada ya kumuombea marehemu itafanyika tarehe 15/10/2014 katika Kanisa la KKKT Sinza Kumekucha kuanzia saa saba mchana na baada ya ibada safari ya kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Same kwa maziko itaanza.

Maziko yanatarajia kufanyika katika kijiji cha Muhezi Mwembe Mlimali Same siku ya Alhamisi tarehe 16/10/2014.

 Amin tulikupenda lakini Mungu amekupenda zaidi pumzika kwa Amani. 

Amen.

Imetolewa na menejimenti ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL)

shukurano toka libeneke la jimmcarter.com

$
0
0
Napenda kutoa shukrani kwa uongozi wa Michuzi blog {BLOG YA JAMII} kwakile ambacho nimeweza kukipata kutoka kwenu. Mimi ni kijana wa miaka 20 Niko Chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha {AJTC} nachukua diploma ya utangazaji wa radio na Tv 

Ni moja ya watu ambao nilikuwa nikipenda sana kazi za michuzi blog nakutamani siku moja kuwa kama yeye. Nashukuru   Mungu Ndoto zimetimia sasa natambulika Arusha nzima, na  Uongozi wa chuo unanitumia kama mfano wa kuigwa kwa wanafunzi wengine kwani ni moja ya mtu ninayemiliki website ya burudani na  marika yote wanaweza kutembelea.

Sina chakukulipa ila nashukuru kwa kuweza kufikisha malengo yangu ya kumiliki Website. Naomba Mungu akupe uzima  japo nami nije kupata nafasi ya kukushika mkono wamshukrani  kwa hatua hii ya kumiliki www.jimmcarter.com 
natumaini ipo siku nitapata nafasi yakuonana na uongozi wa michuzi blog nitoe shukrani zangu.
-------------------------------------
Kaka shukurani umeshazitoa na kwa kuonesha kwa vitendo kile ulichokuwa unaota ni shukrani tosha kwangu. Najisikia  mwingi wa furaha na fahari kwa hayo uyasemayo, na nimeguswa sana sana nayo. Ni wachache wanaweza kuwa kama wewe. Nami nakukuhakikishia ushirikiano endelevu kwani naona kabisa utakuwa kileleni muda si mrefu ujao. Ushauri wangu kwa sasa ni kuweka mambo ya nyumbani kwa asilimia japo 60% na mambo ya nje fanya asilimia 40%. Hapo utakuwa umewatendea haki Watanzania kwa asilimia 100%. Vinginevyo kaza buti endeleza LIBENEKE!

Muhidin Issa Michuzi

ZOEZI LA UOPOAJI WA MIILI KATIKA AJALI YA MITUMBWI ZIWA TANGANYIKA LASITISHWA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Kanali mstaafu Issa Machibya akiongea na waandishi wa habari(ambao hawapo pichani)ofisini kwake juu ya kusitisha kwa zoezi la uopoaji wa miili ya ajali ya mitumbwi iliyotokea hivi karibuni katika kijiji cha kalalangabo ziwa Tanganyika.
Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma

SEREKALI ya Mkoa wa Kigoma imesitisha zoezi la uopoaji wa miili ya ajali ya mitumbwi miwili ya maharusi iliyotokea tokea hivi karibuni katika Ziwa Tanganyika kwenye  kijiji cha Kalalangabo kilichopo mwambao mwa ziwa Tanganyika .

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kanali mstaafu Issa Machibya alisema kuwa vikosi mbalimbali vya ukoaji kwa kushirikiana  jeshi la wananchi(JWTZ)wakishirikiana na wananchi wamefanya kazi kubwa sana ya kuopoa miili kwa kipindi cha siku tatu mfululizo.

Alisema jumla ya miili kumi ili patikana katika zoezi hilo la ukoaji lakini hivi sasa wameachia uongozi wa kijiji cha serekali ya kalalangabo kuendelea kutoa taarifa kama kuna miili mingine itakayoibuka.

''Ile mitumbwi ilikuwa imejaza sana watu ambayo idadi yake kamili mpaka sasa bado haijajulikana kwani walivyokuwa wanaenda kupanda walikuwa na haice tatu,pikipiki 10 na vyote vilikuwa ndugu jamaa na wapambe wa maharusi.

ili kuwa mitumbwi miwili ya kienyeji tena ile inayotumika kuvulia samaki na dagaa,sasa tunahofia kwamba miili mingine zaidi itakuwa bado ipo majini kwani jana waokoaji walifanikiwa kupata baadhi ya vitu majini kama vile simu,nguo na saa''alisema Machibya.

Mkuu wa Mkoa aliwataka wananchi kuacha tabia ya kutumia vyombo visivyo rasmi katika usafiri na ambavyo havijasajiriwa na  mamlaka ya usafiri wa nchi kavu na majini(SUMATRA)pia aliwataka wavuvi na wale wenye vyombo majini waache tabia ya kusafirisha abiria kwa kutumia mitumbwi ya kuvulia dagaa ili kuepuka ajali.

Pia aliwataka wamiliki wa vyombo vya majini wote wasajili vyombo vyao na wahakikishe vinaanzia safari katika vituo vinavyotambulika.

''Kuna siku mimi na kamati yangu ya ulinzi na usalama tunaingia majini wenyewe kufanya ziara ya ghafla siku nzima na kuwakamata wale wote wanaokiuka sheria za kusafirisha abiria ziwani''alisema Machibya

Machibya alisema kuwa mmiliki wa mitumbwi hiyo bado hajafahamika vyombo vya usalama bado vinaendelea na juhudi kumtafuta mmiliki wa mitumbwi hiyo ili aweze kufikishwa katika sheria
Hii ndo mitumbwi iliyopigwa wimbi na kuzama na kusababisha maafa,ilikuwa imebeba maharusi na ndugu na jamaa pamoja na wapambe, watu wanaokadiliwa zaidi ya 80 wanakadiriwa walikuwa katika mitumbwi hii wakisindikiza harusi

MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA YA DHAMINI KONGAMANO LA MAFUNZO YA MFUMO MPYA WA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA USAFIRI WA ANGA (ICAO)

$
0
0
Afisa wa Kanda ya Afrika wa ICAO Papa Issa Mbengue (kushoto)akisisitiza jambo juu ya mfumo mpya wa shirika la Kimataifa la usafiri wa Anga (ICAO) lenye kulenga ufanisi wa wataalamu wa kuongoza ndege ,vyombo vya usafiri wa anga pamoja na mitambo ya kuongonzea ndege wakati wa Kongamano la mafunzo ya ufanisi wa masuala ya uongozaji wa ndege linalofanyika kwa siku tatu katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam kwa udhamini wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wanaomsikiliza ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chacha(watatu kutoka kulia) Kaimu Mkurugenzi Idara ya Huduma za Uongozaji ndege Said Onga (Kulia) Meneja mratibu wa safari za ndege Afrika Frederic Legrand. (wapilia kutoka kulia) na Makamu wa rais wa airspace and airlines Servises Airbus ya Ufaransa Don Facpues Ould.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chacha(kushoto) akiongea wakati wa uzinduzi wa kongamano la mafunzo ya mfumo mpya wa shirika la Kimataifa la usafiri wa Anga (ICAO) lenye kulenga ufanisi wa wataalamu wa kuongoza ndege ,vyombo vya usafiri wa anga pamoja na mitambo ya kuongonzea ndege katikati ni Meneja mratibu wa safari za ndege Afrika Frederic Legrand, Kongamano hilo linazihusisha nchi za Afrika linafanyika hapa nchini kwa siku tatu kuanzia leo katika hateli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi Idara ya Huduma za Uongozaji ndege Said Onga (Kulia)
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chacha akimsikiliza kwa makini Meneja mratibu wa safari za ndege Afrika Frederic Legrand(African Flight Proceducare Manager) wakati alipokuwa akizungumza kwenye kongamano la mafunzo ya mfumo mpya wa shirika la Kimataifa la usafiri wa Anga (ICAO) lenye ufanisi wa wataalamu wa kuongoza ndege ,vyombo vya usafiri wa anga pamoja na mitambo ya kuongonzea ndege.Kongamano hilo la siku tatu katika hateli ya Serena jijini Dar es Salaam kwa udhamini wa TCAA.
Baadhi ya washiriki wa kongamano la mafunzo ya mfumo mpya wa shirika la Kimataifa la usafiri wa Anga (ICAO) lenye ufanisi wa wataalamu wa kuongoza ndege ,vyombo vya usafiri wa anga pamoja na mitambo ya kuongonzea ndege,wakifuatilia moja ya mada zilizokuwa zikitolewa hapo kongamano hilo limedhaminiwa na TCAA.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chacha (kulia)akisalimiana na Makamu wa rais wa airspace and airlines Servises Airbus ya Ufaransa Don Facpues Ould, baada ya kufungua kongamano la mafunzo ya mfumo mpya wa shirika la Kimataifa la usafiri wa Anga (ICAO) lenye ufanisi wa kulenga wataalamu wa kuongoza ndege ,vyombo vya usafiri wa anga pamoja na mitambo ya kuongonzea ndege.Kongamano hilo linafanyika kwa siku tatu kuanzia leo katika hateli ya Serena jijini Dar es Salaam.Katikati ni Meneja mratibu wa safari za ndege Afrika Frederic Legrand.(African Flight Proceducare Manager)
Washiriki wa kongamano lamafunzo ya mfumo mpya wa shirika la kimataifa la usafiri wa anga (ICAO)kutoka nchi za Nigeria,Mali,Ivort coast,Senager,Rwanda,Cape Verde,Gabon na Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Kongamano hilo la siku tatu linalofabnyika kwenye hoteli ya serena jijini Dar es Salaam.

TUMKUMBUKE MWALIMU NYERERE KATIKA SIKU YAKE LEO NA CONSTANTINE MAGAVILLA

TAARIFA YA MSIBA

$
0
0
Familia ya Bandawe ya Newark Delaware inasikitika kutangaza kifo cha baba mzazi wa Bi.Vicky Bandawe Mzee Jonas Soka kilichotokea asubuhi ya kuamkia leo huko Arusha baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Msiba upo nyumbani kwa wafiwa 719 6th St Newark Delaware 19711.
Kama desturi yetu tunaombwa tuchukue nafasi hii kuwapa pole na faraja wafiwa Bw. na Bibi Bandawe katika kipindi hiki kigumu.. Mazishi yanatarajiwa kufanyika huko Kombo Moshi Jumamosi Oktoba 18,2014.

Kwa taarifa zaidi unaweza kuwasiliana na :
Emmanuel Bandawe 302-803-9487.
Vicky Bandawe 302-256-4516.

Eunice Magonya 301-204-0357.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa na jina lake lihimidiwe. AMEN.

UNDP “yaipiga jeki” Serikali namna ya kuandaa, kujadili na kusimamia miradi mikubwa na mikataba ya gesi asilia Nchini

$
0
0
Picha ya pamoja ya washiriki wa Warsha ya kujenga uwezo kwa maafisa wa Serikali kutoka taasisi mbalimbali. Kutoka kushoto (waliokaa) ni Bw. Styden Rwebangila kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Bi.Anna Shakarova ambaye ni Mkurugenzi wa Program wa Maendeleo ya Kiuchumi, Bw. Yohane Masara –Kaimu Mkurugenzi,Divisheni ya Mikataba kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali(katikati),Bw.Steven Sparling na Bi Clare Power kutoka Kampuni ya Uwakili ya K&L Gates ambao ni wawezeshaji wa Mafunzo hayo.
Bi.Anna Shakarova ambaye ni Mkurugenzi wa program ya Maendeleo ya Kiuchumi ya ISLP akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo.
Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo wakifuatilia mada wakati wa mafunzo hayo.Kutoka kushoto ni Bw.Mikidadi Rashidi kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Bw.Juma Karibona(kati) kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu -Zanzibar na kulia ni Bw.Patric Malogoi kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Tanzania.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

MUHEZA KUPATA MIL 500 KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji, Mh. Amos Makalla ameahidi Sh. Milioni 500 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji kwa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza. 

Mhe. Makalla alitoa kauli hiyo leo,  alipotembelea Wilaya hiyo kukagua utekelezaji wa miradi ya maji na hali ya huduma ya maji wilayani humo.

 “Nawapongeza sana Halmashauri yenu na uongozi wake kwa kununua mashine kwa ajili ya kuchimba visima vya maji, sijawahi kutembelea Wilaya yoyote nchini nikakuta jambo hili. Kitendo cha Halmashauri kukusanya mapato yake na kufanya hivi, mnastahili pongezi na kuwa mfano kwa Halmashauri nyingine nchini,” alisema Makalla. 
“Nimeridhishwa na jitahada zenu na nitahakikisha mnapata mgao wa Sh. Milioni 500 ili kufanikisha lengo la kupatia ufumbuzi tatizo la maji Muheza,” aliongeza Makalla. 
Naibu Waziri alisema kwamba kama kiongozi mwenye dhamana kwenye Serikali Kuu, atahimiza maamuzi yafanyike upesi ili jitihada zinazofanywa na Wilaya ya Muheza zifikie lengo walilojiwekea kuwapatia wananchi maji. Aidha, Naibu Waziri wa Maji, Mh. Amos Makalla leo ameendelea na ziara yake kwa kutembelea Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira jijini Tanga (Tanga UWASA) na kujionea utendaji wa Mamlaka hiyo. 
Mhe. Makalla alisikia taarifa ya utendaji wa Mamlaka hiyo na kufurahishwa nayo, hasa kwa jinsi walivyofanikiwa kupiga hatua kubwa ya kupunguza kiwango cha upotevu wa maji kwa kiasi kikubwa na ukusanyaji mzuri wa mapato kutoka kwa wateja wake. 
“Kwa kweli nimefurahishwa mno na jitihada zenu za kupunguza upotevu wa maji na kwa kufikia kiasi cha asilimia 23 ni kiwango kizuri, ukilinganisha na Mamlaka nyingine nchini. Hasa ikizingatiwa hii ni changamoto kubwa na kama Wizara tunafanya jitahada kupata suluhisho lake,” alisema Makalla. Pia, aliongeza ukusanyaji mzuri wa mapato ni hatua kubwa kwa Mamlaka hii, kwani itarahisisha na kuchangia utendaji mzuri wa kazi na maendeleo ya Mamlaka hiyo katika kuhakikisha inainua Sekta ya Maji jijini Tanga na mkoa mzima kwa ujumla. 
Katika ziara hiyo Mhe. Makalla amefanikiwa kutembelea miradi ya maji ya vijiji vya Misengeni, Mikwamba na Michungwani, wilayani Muheza. Na vilevile, chanzo cha maji cha Mibayani, kituo cha kusukuma na kutibu majisafi cha Mowe na eneo la ujenzi wa mabwawa ya majitaka lililopo Utofu, Tanga Mjini. 
 Mhe. Makalla ameanza ziara yake ya siku 6 jana mkoani Tanga, ikiwa ni hatua ya kuhakikisha utekelezaji wa programu ya wa Big Results Now na miradi yote ya maji inatekelezwa kwa kasi na ufanisi ili kuleta matokeo yenye tija na kwa wakati.

Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Amos Makalla na Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu wakiwa wamesimama kwenye mashine ya kuchimbia visima iliyonunuliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Muheza kwa takribani Sh. Mil 240.

Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Amos Makalla akikagua mradi wa maji wa Michungwani, Muheza.

Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Amos Makalla akiwa na viongozi na wataalamu alioongozana nao katika ziara yake kwenye chanzo cha maji cha Mibayani.

Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Amos Makalla, akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga UWASA, Inj. Joshua Mgeyekwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Tanga UWASA, Salum Shamte na Mkurugenzi Msaidizi wa Maji Vijijini, Ritha Kahwili wakisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Mtambo wa Maji, Mowe (mwisho kushoto).

Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Amos Makalla alipotembelea Mtambo wa Maji, Mowe.

RAIS KIKWETE AWAPA URAIA WAKIMBIZI WA BURUNDI 162,156 MJINI TABORA LEO

$
0
0
 Rais Jakaya Kikwete akimpa cheti cha uraia wa Tanzania, Loveness Ruhaga (kulia) aliyekuwa Mkimbizi kutoka nchini Burundi katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Tabora leo. Rais Kikwete alitoa vyeti vya uraia kwa wakimbizi 162,156 na kuwatangazia kuwa sasa wamekuwa raia halali wa Tanzania hivyo wahakikishe wanafuata sheria zote za nchi na waepuke kufanya vurugu za aina yoyote kwani wakikiuka masharti hayo waweza kunyanganywa uraia huo. Wakimbizi hao walioingia nchini tangu mwaka 1972 walionyesha furaha kwa kuimba na kucheza vyimbo mbalimbali. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.  
 Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (kushoto) akimuonesha Rais Jakaya Kikwete (kulia) mchoro unaoonesha jinsi wakimbizi wa Burundi walivyoingia nchini wakati walipokuwa wanatoka nchini kwao mwaka 1972. Rais Kikwete alitoa vyeti vya uraia kwa wakimbizi 162,156 waliokuwa raia wa Burundi katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkoa wa Tabora leo. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.
 
 Rais Jakaya Kikwete akizungumza baada ya kuwapa vyeti vya uraia wa Tanzania, waliokuwa wakimbizi 162,156 kutoka nchini Burundi walioingia nchini tangu mwaka 1972. Tukio la utoaji wa vyeti hivyo lilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora mjini humo leo. Raia Kikwete katika hotuba yake aliwataka raia hao wapya kuwa waadilifu na kufuata sheria zote za nchi. Wanne kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi nchini, Harrison Mseke.  
 Msoma risala ambaye ni mwakilishi wa raia wapya 162,156 nchini ambao walikuwa wakimbizi kutoka nchini Burundi, Dafroza Baragwimba akiisoma risala yao mbele ya Rais Jakaya Kikwete (watatu kulia) wakati ya hafla ya utoaji wa vyeti kwa raia hao. Rais Kikwete alitoa uraia kwa wakimbizi hao na kuwataka wawe waadilifu na kufuata sheria zote za nchi. Wanne kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. 
Rais Jakaya Kikwete (wasita kushoto waliokaa), mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa nchini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (watano kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke (watatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa (wasita kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya raia wapya 162,156 wa Tanzania (nyuma waliosimama) baada ya kupewa vyeti vya uraia na Rais Kikwete katika hafla iliyofanyika  katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini humo.  Picha zote na Felix Mwagara, wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

KIINGILIO MECHI YA SIMBA NA YANGA BUKU SABA

$
0
0
Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Simba itakayochezwa Jumamosi (Oktoba 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 7,000.

Washabiki watakaolipa kiingilio hicho ni wale watakaokaa viti vya rangi ya bluu na kijani ambavyo jumla yake ni 36,693 katika uwanja huo wenye viti 57,558. Viingilio vingine ni sh. 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 20,000 kwa VIP B na C wakati VIP A itakuwa sh. 30,000.

Tiketi zitakazotumika kwenye mechi hiyo ni za elektroniki, na zimeanza kuuzwa jana (Oktoba 13 mwaka huu). Tiketi zinapatikana kwa mtandao wa M-PESA, CRDB Simbanking na maduka ya CRDB Fahari Huduma ambayo yapo zaidi ya mia moja sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo namba 27 itakayochezeshwa na mwamuzi Israel Mujuni Nkongo akisaidiwa na John Kanyenye na Ferdinand Chacha itaanza saa 10 kamili jioni. Kamishna wa mechi hiyo ni Salum Kikwamba kutoka mkoani Kilimanjaro.

Washabiki wanatakiwa kununua tiketi mapema, kwani hazitauzwa uwanjani siku ya mechi. Milango yote ukiwemo ule wa upande wa Mbagala (Uwanja wa Ndani) itafunguliwa kwa ajili ya washabiki, na itakuwa wazi kuanzia saa 4 asubuhi.

Magari maalumu tu yenye stika ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia uwanjani kwa kupitia Barabara ya Mandela. Pia washabiki hawaruhusiwi kuingia uwanjani wakiwa na silaha, vitu vya vyuma na mabegi makubwa. Barabara ya kuingilia upande wa Chang’ombe itafungwa kwa watumiaji wa magari.


IMETOLEWA NA 
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

introducing Wimbo mpya wa CBH na Dully Sykes.

Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images