Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110079 articles
Browse latest View live

RAIS KIKWETE ALIPOFUNGUA JENGO LA KITEGA UCHUMI LA HOTELI YA PPF MWANZA

$
0
0
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe ikiwa ni ishara ya ufunguzi rasmi wa jengo la hoteli ya Gold Crest linalomilikiwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF katika hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika hivi karibuni jijini Mwanza.Wengine pichani toka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Evarist Ndikilo,Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa PPF,ndg. Ramadhan Kijjah,Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Adam Malima,Mkurugenzi  Mkuu wa Mfuko wa PPF,William Erio pamoja na Waziri wa Ujenzi,Mh. John Magufuli.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika hafla ya ufunguzi wa jengo la kitega uchumi la hoteli linalomilikiwa na Mfuko wa PPF jijini Mwanza.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifatilia kwa makini maelezo ya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa PPF Ndg. William Erio.
Naibu Waziri wa Fedha,Mhe. Adam Malima (Mb) akihutubia wageni waalikwa katika hafla ya ufunguzi wa jengo la kitega uchumi la hoteli inayomilikiwa na Mfuko wa PPF jijini Mwanza. Ufunguzi huo uliambatana na Rais kutembelea sehemu mbalimbali za jengo hilo la Hoteli.


BREAKING NEWZZZZZ: MAHARUSI WANUSURIKA KIFO BAADA YA MTUMBWI WALIOPANDA KUZAMA ZIWA TANGANYIKA

$
0
0
Waokoaji wakijindaa kwenda katika eneo ilipotokea ajali ya mitumbwi iliyobeba harusi kutoka Kigoma mjini kwenda katika kijiji cha Kigalya kutafuta miili ya marehemu ambayo bado haijapatikana


 Waokoaji toka vikosi mbalimbali wakiwemo wanajeshi wa JWTZ wakijiandaa kwenda kutafuta miili ambayo bado haijapatikana kutokana na jali ya mitumbwi katika kijiji cha kalalangabo
 Bibi harusi Mariamu Mduwa aliyenusurika  katika ajali ya mitumbwi katika kijiji cha kalalangabo akiwa anaendelea na matibabu katika hospitali ya  mkoa wa Kigoma 
Ndugu,  jamaa na wapambe wa bwana na bibi harusi walionusurika katika  ajali ya mtumbwi katika kijiji cha Kalalangabo wakiwa wanaendelea na matibabu katika hospita ya Mkoa wa Kigoma

Na Editha Karlo wa 
Globu ya Jamii, Kigoma
WATU sita wamekufa maji katika ziwa Tanganyika na wengine 11  kunusurika kifo akiwemo bwana harusi Shaaban Idd na bibi harusi
Mariamu Mduwa baada ya mitumbwi miwili  waliyokuwa wakisafiria kutoka kigoma mjini kwenda katika kijiji cha Kigalye kilichopo mwambao mwa ziwa Tanganyika kuzama ziwani.

Tukio hilo limetokea leo saa nane na nusu mchana baada ya mitumbwi hiyo kupigwa wimbi kali na kuzama  katika kijiji cha Kalalangabo wakati bwana harusi huyo akitoka kuoa katika eneo la mwandiga na kurudi nyumbani akiwa na ndugu na jamaa pamoja na wapambe.

Akiongea na Globu ya Jamii  katika wodi namba 5 katika Hospital ya Mkoa wa Kigoma alipolazwa bibi harusi huyo alisema kuwa alishikwa na bumbuwazi sana baada ya tukio hilo kwani mpaka sasa bado hajielewi.

''Sikumbuki kitu kwani baada ya mtumbwi kuzama kila mtu alikuwa anahangaika kujiokoa na kifo.

"kwakweli mimi naona kama mkosi siku ya harusi yangu watu wanakufa ila namshukuru Mungu kwa kutunusuru na kifo na yote mimi nimemwachia Mungu''alisema bibi harusi huyo

Mwathirika  mwingine aliyenusurika katika ajali hiyo Zabibu Issa alisema kuwa mitumbwi waliyokuwa wamepanda ilikuwa imejaza sana watu na mizigo ndiyo maana ilizidiwa uzito na kuzama baada ya kupigwa na wimbi.

''Safari ya kwenda kijijini kwetu lazima tupite njia za majini hakuna barabra kabisa sababu vijiji tunavyoishi vipo mwambao mwa ziwa Tanganyika kungekuwa na barabara tungepita barabrani''alisema Bi Zabibu Issa.

Naye muuguzi wa wodi namba tano walipolazwa majeruhi hao alisema kuwa majeruhi wote waliopo wodini hali zao zinaendelea vizuri na kwamba mpaka sasa wameshapokea jumla ya maiti sita.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kigoma Jafari Mohamed akithibitisha hayo alisema kuwa mpaka sasa jumla ya watu 27 wameshaokolewa, na miili sita kuopolewa pamoja na walionusurika 11.

"Lakini bado inahofiwa kuwa kuna miili mingine zaidi ambao bado haijapatikana kwani mitumbwi hiyo inakadiriwa kuwa ilikuwa na watu zaidi ya sabini", alisema na kuongezea kuwa vikosi vya ukoaji kwa kushirikiana na askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania vinaendelea na kazi ikiwa ni sambamba na kuchunguza chanzo cha  tukio hilo.

Mhariri Gazeti la MTANZANIA akabidhi vyeti Shule ya Salma Kikwete

$
0
0
WAZAZI na walezi nchini wametakiwa kutambua wajibu kwa kuhakikisha wanawekeza kwenye elimu kwa watoto wao.

Wito huo ulitolewa Dar es Salam na Mhariri Msanifu wa gazeti la MTANZANIA, Khamis Mkotya alipokuwa akizungumza katika mahafali ya tano ya Jumuiya ya wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Salma Kikwete.

Mkotya ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo ambapo alisema ni lazima jamii ikubali kuondokana na kulalamika na badala yake iandae mazingira mazuri ya watoto wao kuhakikisha wanasoma kwa bidii.

“Bado siku chache wanafunzi wa kidato cha nne nchini, mtafanya mitihani ya kuhitimu lakini tambueni kumaliza elimu hii kwa ngazi yetu ni chachu ya kutafuta zaidi ya elimu.

“Na mkiwa hamtafanya hivi mtakuwa mmekwenda ninyume na mafundisho ya Mtume wetu Muhammad (S.A.W) ambaye amatutaka tutafute elimu hadi uchina. Na hata leo ukimaliza mtihani wa kidato cha nne na kuona umemaliza tambueni elimu mlionayo sasa ni sawa na elimu ya msingi,” alisema Mkotya.

Alisema ili maendeleo chanya yaweze kupatikana nchini ni lazima jamii ijiandae vema kuyapokea kwa kuwa na mkakati hasa kwa wanafunzi kujifunza kwa bidii kwenye masomo yao.
Mhariri Msanifu wa Gazeti la Mtanzania, Khamis Mkotya, akikabidhi cheti kwa mwanafunzi Ahmed Adamu katika mahafali ya tano ya wahitimu wa Kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Salma Kikwete iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam juzi. Kulia ni Mwenyekiti wa walimu wa maarifa ya Uislamu Dar es Salaam, Suleiman Gombe.

TANZANIA AMONG THE LEADING COUNTRIES WITH TEACHER RECRUITMENT NEEDS

$
0
0
Tanzania is one of the top ten countries globally with the highest projection of the total number of teachers who have to be recruited by 2030.

According to the new paper, jointly released by the UNESCO Institute for Statistics (UIS) and the Education for All Global Monitoring Report on World Teachers' Day, Tanzania needs to recruit at least 406,600 new teachers by 2030.

Closely followed by Tanzania is Uganda, which stands as the tenth most needy country in teacher recruitment. According to the statistics, Uganda needs at least 372,800 new teachers by 2030. Other African countries leading the league of ten most needy countries are Nigeria at number four and Democratic Republic of Congo at number seven.

The new data released by UNESCO show a chronic lack of trained teachers in many countries. Without action, it will be impossible to get all children into school and learning by 2030. In total more than 27 million teachers will be needed to achieve universal primary education by 2030.

The report also shows that in the rush to fill this gap, many countries are recruiting new teachers with little training. In the past decade, countries have made great efforts to steadily increase the supply of teachers.

Since 1999, at least 22 countries have more than doubled their teacher workforces. In particular, Afghanistan, Burundi, Congo and Niger have tripled their teaching staff over the same period. To date, in primary education alone, there are about 29 million teachers working in classrooms around the world.

For more information about the statistical data on teachers, please consult. http://tellmaps.com/uis/teachers/ or contact j.alima-kotta@unesco.org

latest updates: MAITI ZAIDI ZAPATIKANA ZIWA TANGANYIKA BAADA YA AJALI YA MITUMBWI YA MAHARUSI JANA

$
0
0
Na Editha Karlo wa 
Globu ya jamii Kigoma 
Mpaka sasa jumla ya maiti nne zimeopolewa na kufanya kufikia idadi ya maiti kumi zimepatikana katika ajali ya mitumbwi iliyotokea jana mchana katika kijiji cha Kalalangabo baada ya mitumbwi iliyokuwa imebeba maharusi ndugu jamaa na wapambe kupigwa wimbi na kuzama. 
 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Mstaafu Issa Machibya ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya maafa ya Mkoa amesema kuwa bado idadi maiti zilipo kwenye maji ni kubwa ambazo bado hazijapatikana. 
 ''Zoezi hili linakuwa gumu sababu ya uhaba wa waokoaji pamoja na miundombinu duni ambavyo ni kikwazo katika zoezi hili la ukoaji. Lakini bado tunaendelea na kazi ''Mkuu wa Mkoa huyo ameiambia Globu ya Jamii asubuhi hii.
Viongozi wa Mkoa wa Kigoma wakiwa katika eneo la ajali wakiangalia zoezi la upoaji wa miili iliyopatikana katika ziwa Tanganyika kufuatia ajali ya mitumbwi iliyotokea jana. Nao ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Mstaafu Issa Machibya (wa pili kushoto) anayefuata ni Katibu Tawala wa Mkoa John Nduguru na Ramadhani Maneno Mkuu wa Wilaya ya Kigoma. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Kigoma
Waokoaji wakiwa wamebeba mwili uliopatikana katika ziwa Tanganyika baada ya ajali ya mitumbwi katika kijiji cha kalalangabo
Wanajeshi wa Jeshi la Wananch (JWTZ) wakiendelea na zoezi la kuopoa miili ya watu waliopata ajali ya mitumbwi katika kijiji cha Kalalangabo baada ya mitumbwi waliyokuwa wakisafiria kuzama
Zoezi la uopoaji wa miili linaendelea na vikosi mbalimbali vya ukoaji katika ziwa Tanganyika kufuatia ajali ya mitumbwi iliyotokea jana 

Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya mtoto wa kike yaliyo ratibiwa na WiLDAF yafana jijini Dar es salaam

$
0
0
Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike yaliyo ratibiwa na Women in Law and Development in Africa - WiLDAF yafana jijini Dar es salaam.

Octoba 11 ya kila mwaka ni siku iliyopitishwa na Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuwa Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike duniani kote. Maadhimisho haya yalifanyika katika Hoteli ya Double Tree, Dar es Salaam.
Washiriki wa maadhimisho hayo wakiwa katika picha ya pamoja.
Mmoja wa washiriki waliofika kwenye hafla hiyo ya maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Mtoto es Kike yaliyoratibiwa na WiLDAF akichangia mada.
PICHA ZAIDI INGIA HAPA.

KONGAMANO NA MAONESHO YA TATU YA MAFUTA NA GESI ASILIA TANZANIA

Bei ya Madafu leo


Prof. Ali Alamin Mazrui afariki Dunia leo

$
0
0
Msomi maarufu nchini Kenya na Afrika Mashariki,Prof. Ali Alamin Mazrui (pichani) amefariki dunia leo asubuhi Binghamton Jijini New York nchini Marekani. 

 Prof. Mazrui amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 81,taarifa za awali zinaeleza kuwa Prof. Mazrui hakuwa akijisikia vizuri kwa miezi kadhaa kabla ya kifo chake. 

 Mwenyekiti wa Haki za Binadamau za Waislam (MUHURI) Khelef Khalifa amesema mwili wa marehemu Prof. Prof Mazrui utasafirishwa kwa ndege kwenda Kenya kwa mazishi.

Rais Kikwete azindua kijiji cha Mfano cha Vijana Sikonge mkoani Tabora leo

$
0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi wakati wa uzinduzi wa kijiji cha mfano cha vijana Pathfinders Green City katika kata ya Igigwa wilayani Sikonge leo.Rais Kikwete yupo Mkoani Tabora kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo ambapo pia atakuwa mgeni rasmi katika kilele cha mbio za mwenge hapo kesho.watatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bi.Fatma Mwassa na wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Bi.Hanifa Selenga.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya uchakataji asali kutoka kwa mmoja wa vijana waishio katika kijiji cha mfano cha vijana wajasiriamali katika kata ya Igigwa, wilayani Sikonge, Mkoani Tabora leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua baadhi ya madawati yaliyotengenezwa na kikundi cha vijana wajasiriamali katika kijiji cha mfano cha Pathfinders katika kata ya Igigwa, wilayani Sikonge,Mkoani Tabora muda mfupi baada ya kukizindua kijiji hicho.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua viatu vya ngozi vilivyotengenezwa na vijana wajasiriamali katika kijiji hicho cha mfano
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua viatu vya ngozi vilivyotengenezwa na vijana wajasiriamali katika kijiji hicho cha mfano. Picha na Freddy Maro.

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR ZIARANI MKOA WA RUVUMA

$
0
0
 Na Othman Khamis Ame, OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewasili Mkoani Ruvuma kwa ziara ya siku mbili kuangalia miradi mbali mbali ya kiuchumi na maendeleo ya Mkoa huo kwa mualiko wa Uongozi wa Jimbo la Peramiho. 
Kwenye uwanja wa ndege wa Songea Balozi Seif na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi akiambatana pia na Wake wa wabunge na wawakilishi Zanzibar alilakiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambae pia ni Mkuu wa Mkoa Mpya wa Njombe Mh. Aseri Msangi pamoja na viongozi mbali mbali wa Serikali na Siasa. 
Akitoa Taarifa fupi ya Mkoa huo mara baada ya mapokezi hayo hapo Ikulu ya Mkoa wa Ruvuma Kaimu Mkuu wa Mkoa huo Mh. Aseri Msangi alisema Mkoa wa Ruvuma umekuwa na mafanikio makubwa ya sekta ya kilimo kwa kubarikiwa kuwa na mvua za kutosha. 
Mh. Msangi alisema Msimu huu wa kilimo Mkoa wa Ruvuma umezalisha tani Milioni Moja nukta nne za chakula ukiwa na ongezeko la ziada ya Tani Laki Tisa ikiwa ni sawa na Asilimia 10.2%. Alisema mafanikio hayo yamesababisha changamoto kubwa la uhifadhi wa nafaka kutokana na uhaba wa maghala pamoja na uchelewaji wa fedha za ununuzi wa Mahindi kutoka kwa wakulima. Hata hivyo Kaimu Mkuu huyo wa Mkoa wa Ruvuma aliwahakikishia wakulima waliouza mahindi yao ambao bado hawajapata fedha zao kwamba Serikali imeshatenga fedha hizo zinazotarajiwa kuwafikia wakati wowote kuanzia sasa. 
Akigusia huduma za maendeleo na kiuchumi Mh. Msangi alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Ruvuma imekuwa mstari wa mbele katika kusimamia mipango ya kiuchumi ili kutekeleza sera na ilani ya CCM ya mwaka 2010. 
Alisema mipango hiyo iliyojikita zaidi katika miradi ya kiuchumi na ustawi wa jamii imelenga kwenda sambamba na Dira ya Taifa iliyokusudia kuifanya Tanzania kuwa na uchumi wa kati na kati ifikapo mwaka 2025. 
Kuhusu sekta ya afya Mh. Aseri Msangi alifahamisha kwamba Mkoa wa Ruvuma umefikia kuwa na vituo vya afya 271 kukiwa na ongezaeko la zaidi ya asilimia ishirini na sita. Alisema kinachoupa mtihani Mkoa huo hivi sasa ni ongezeko la maambukizi ya virusi vya ukimwi iliyofikia asilimia 7% hali ambayo Uongozi wa Mkoa huo unatafuta mbinu za kupunguza kasi ya kuenea kwa maambukizi hayo. 
Mh. Msangi alisema juhudi za ziada zitachukuliwa katika kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi mapya hasa katika skuli zote za sekondari na msingi ili kupunguza kasi hiyo iteremke hadi kufikia asilimia 3%. 
Akitoa shukrani zake kwa mapokezi hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzinbar Balozi Seif Ali Iddi alizipongeza juhudi zinazochukuliwa na Viongozi na wananchi wa Mkoa wa Ruvuma katika kujiletea maendeleo yao. Balozi Seif alisema takwimu zinaonyesha wazi kwamba Mkoa wa Ruvuma umepata mafanikio makubwa katika sekta ya kilimo, afya pamoja na elimu na kuwa mfano bora kwa mikoa mengine hapa nchini. 
Alisema Wananchi na Jamii kote Nchini wanapaswa kumpongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kutokana na juhudi anazochukuwa za kusimamia na kuhamasisha maendeleo ya umma hasa katika sekta muhimu ya Elimu. 
Balozi Seif alisema muongozo wa Rais Kikwete wa kuzitaka Wilaya zote nchini kumaliza ujenzi wa madarasa ya Maabara katika skuli zote za sekondari Wilaya ifikapo Mwezi Disemba mwaka huu umeonyesha juhudi hizo za kumkomboa Mtoto wa Kitanzania ili aoane na karne hii ya sayansi na Teknolojia Duniani. 
Naye Mbunge wa Jimbo la Peramiho ambaye ndie mwenyeji wa ziara hiyo Mh. Jenista Mhagama alisema ziara ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar imeonyesha mapenzi na mshikamano uliopo kati ya pande mbili zilizounda Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. 

 Kijana wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoani Ruvuma Mustafa Hamad Mlanzi akimfunga skafu Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Songea kuanza ziara ya siku mbili Mkoani humo kukagua miradi ya maendeleo.
 Balozi Seif akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Serikali na Kisiasa mara baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Songea.
 Kikundi cha Utamaduni ya Shaba Sanaa cha Songea kikiimba wimbo maarufu wa Lisombe kumkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Songea kwa ziara ya siku mbili Mkoani Ruvuma.
Mbunge wa Jimbo la Paramelo Mh. JenistaMhagama akimshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwa kukubali kwake kufanya ziara Mkoani Ruvuma. Kushoto ya Mh. Jenista ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi wakati kulia ya Mh. Jenista ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh. Aseri Msangi.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR,  ZNZ.

MAJUMUISHO YA MAJADILIANO YA AWALI KATI YA TANZANIA, BENKI YA DUNIA NA IMF

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile ambaye ni kiongozi wa ujumbe kutoka Tanzania na anawakilisha kama Gavana Mbadala (Alternate Governor) pamoja na Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu ambaye pia ni Gavana katika mikutano hii. Katika picha viongozi hao wakiwa wanafanya majumuisho ya majadiliano ya awali na kukubaliana cha kufanya kwa pamoja na viongozi kutoka IMF na WB kuhusiana na hali ya uchumi kwa maana ya sera za fedha na sera za mapato na matumizi.
Bw.Herve’ Joly ambaye ni Mkurugenzi msaidizi na Mkuu wa idara ya Afrika sehemu ya Mashariki akimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile hayupo katika picha, alipokuwa akitoa msimamo wake kuhusu sera zinazopendekewa na IMF na WB.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile alipokuwa akitoa msimamo wake kuhusu sera zinazopendekewa na IMF na WB.

Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali akiwa pamoja na ujumbe kutoka Tanzania.Wakichukua mapendekezo kutoka kwa viongozi wa IMF na WB hawapo kwenye picha. Kutoka kushoto ni Gavana wa Benki kuu ya Tanzania akiwa amefuatana na Bi. Natujwa Mwamba Naibu Gavana wa Benki kuu ya Tanzania na kutoka kulia ni Bw. Philip Mpango Katibu Mtendaji tume ya Mipango akifuatiwa na Msaidizi wa kamishna sera Bw. Shogholo Msangi na wa mwisho ni Kamishna wa Bajeti Bw. John Cheyo na walioketi nyuma wote ni wajumbe kutoka Tanzania.

WATAKA WESTERN SAHARA IWE HURU KUJIAMULIA HATIMA YAKE

$
0
0
 Na Mwandishi Maalum, New York 
Umoja wa Mataifa unaitambua Western Sahara kuwa ni Koloni ambalo linapashwa kuondokana na minyororo ya ukoloni , liwe huru na lijiamulie mambo yake yenyewe kama taifa huru. 
Hata hivyo tangu mwaka 1963 Western Sahara ilipotambuliwa kuwa koloni, pamoja na michakato mbalimbali inayosimamiwa na Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na wadau wengine wengi, bado safari ya koloni hilo pekee Barani Afrika ya kuikata minyororo ya ukoloni inazidi kuwa ndefu na yenye mabonde mengi. 
Kama hiyo haitoshi, mchakato wa kuisaidia Western Sahara kufikia hatua ya kuwa nchi huru inaelekea sasa kuigawa Jumuiya ya Kimataifa katika pande zinazokinzana. 
Kwa zaidi ya wiki Moja sasa wajumbe wa Kamati Maalum ya Nne ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa inayohusika na Masuala ya Siasa na Umalizaji wa Ukoloni, wamekuwa wakijadiliana na kubadilishana mawazo ya namna, pamoja na mambo mengine, kuchagiza umalizwaji wa ukoloni kwenye makoloni 17 yanayotambuliwa rasmi ndani ya Umoja wa Mataifa ikiwamo Western Sahara. 
Ni katika majadaliano hayo, ambapo pia wajumbe wa Kamati waliwasikiliza petitioners zaidi ya 60 waliojenga hoja mbalimbali zikiwamo zinazoitaka Jumuiya ya Kimataifa kwa maana ya Umoja wa Mataifa kuharakisha mchakato wa kuipatia Western Sahara uhuru wake kamili au iwe sehemu ya Morocco. 
Ni katika majadiliano hayo, ambapo pia, misimamo ya wazi wazi imejitokeza kwa baadhi ya wajumbe kusimamia au kuegemema upande wa Morocco ambaye ndiye mtawala ( Mkoloni)wa sasa wa Western Sahara baada ya mkoloni wa awali Hispania kuliacha mwaka 1963. Wajumbe wengine zikiwamo nchi za Afrika zinazozungumza Kiingereza pamoja na nchi za Amerika ya Kati wao zenyewe zinasimamia katika kutaka Western Sahara iachwe huru na iwe na haki kuajiamulia hatima yake. Kwa wale wanaogemea upande wa Morocco, zikiwamo baadhi ya nchi zinazozungumza Kifaransa nyingi zikiwa za Kiafrika. 
Wao wanapigia chapuo hoja inayopendekezwa na Morocco ya kuipatia Western Sahara uhuru wa kujiamulia baadhi ya mambo yake ( limited autonomy) lakini ibaki kuwa sehemu kamili ya Morocco. 
 Wanaounga mkono hoja hii wanaamini kwamba pengine huu ndiyo mwelekeo sahihi wa kisiasa na wenye kutekelezeka. Lakini wakati huo huo unakosa hoja ya msingi ya uhuru kamili na kujitawala. Hata hivyo kundi la pili na ambalo pengine ni kubwa zaidi lenyewe linapendekeza kuwa wananchi wa Western Sahara na kwa mujibu wa maazimio ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na Baraza Kuu la Usalama wanapashwa kuachiwa wenyewe fursa ya nini wanataka iwe hatima yao kama ni kuwa na uhuru kamili nakujiamulia mambo yao au pendekezo hilo la limited autonomy. 
Lakini wafanya hivyo bila ya kushinikizwa na wala wasiamuliwe. Wanaopendekeza hivyo wanasimamia katika ile misingi inatoainishwa na katiba ya Umoja wa Mataifa inayowapatia watu wa Saharawi haki yao ya msingi inayoainishwa katika maazimio mbalimbali ya Umoja wa yanayowataka wafanye hivyo kupitia kura ya maoni ( referendum), kama ilivyopendekezwa na kupitishwa na Baraza Kuu la Usalama kupitia maazimo 658 ( 1990) na 690 ( 1991). Hata hivyo pamoja na kupitishwa kwa maazimio hayo pamoja na kuundwa kwa chombo cha kusimamia kura hiyo ya maaoni ( MINURSO). 
Kura hiyo haijafanyika kutoka na kile kinachoelezwa ni pingamizi zinayowekwa na Morocco. Jitihada mbalimbali za Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Christopher Ross zimeshindwa kusukuma mbele mchakato wa kuipatia Western Sahara uhuru wa kujiamulia mambo yake. 
Kama hiyo haitoshi, Umoja wa Afrika umemteua Rais mstaafu wa Msumbiji Joachim Chisano kuwa mjumbe wake maalum wa kulishughulikia suala la Western Sahara na afanye kazi kwa karibu na Umoja wa Mataifa. Wajumbe wa Kamati ya Nne wameelezwa kuwa kadri suala la Western Sahara linavyochelewa kupatiwa ufumbuzi ndivyo hali inavyozidi kuwa tete hususani katika makambi ya wakimbizi yanayohudumia wakimbizi wa Western Sahara wanaohifadhi humo. 
Wakati wa majadiliano hayo zilitolewa taarifa zinazoonyesha kuwa katika kambi hizo za wakimbizi hususani ile ya Tinduff imegeuka au imo katika hatari ya kugeuzwa eneo ambalo vijana wa Kisaharawi wanarubuniwa na kuingizwa katika makundi ya ugaidi. Waliozungumza wanasema vijana hao wameamua kuingia katika vitendo vya ugaidi kwa kile kinachodaiwa kukata tamaa na mkwamo wamchakato mzima wa kuamua hatima yao yaani kuwa huru. 
 Ni kwa sababu hiyo na tishio hilo la ugaidi katika kambi hizo na mstakabali mzima wa hali ya Amani na usalama katika eneo la Maghereb, imefikia wakati sasa ambapo Jumuiya ya Kimataifa inashauriwa kuliangalia kwa jicho pana zaidi suala la Western Sahara.
Balozi Ramadhan Mwinyi,  Naibu Muwakilishi wa Kudumu wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akichangia majadiliano  ya jumla kuhusu agenda  ya umalizaji wa ukoloni katika makoloni 17 yanayotambuliwa rasmi na Umoja wa Mataifa likiwamo  la Western Sahara  koloni pekee katika Bara la Afrika. Akizungumza kwa  niaba ya  Tanzania Balozi Mwinyi pamoja na  mambo mengine alirejea  wito  Uliotolewa na  Mhe.  Rais Jakaya  Mrisho Kikwete wakati alipolihutubia Baraza Kuu   la Umoja wa Mataifa mwezi Septemba, ambapo alilitaka Baraza   Kuu la Usalama la Umoja wa  Mataifa   kutumia  uwezo wake kulitafutia ufumbuzi wa kudumu na wa mwisho kuhusu Koloni hilo la Western  Sahara. Tanzania ni kati ya nchi ambazo  zimesisitiza haki na uhuru wa  watu wa Saharawi kujiamulia hatima yake  kwa mujibu wa maazimio na  mapendekezo ya    Umoja wa Mataifa.  Tanzania licha ya kuwa  mjumbe wa Kamati ya Nne inayohusika na masuala ya Siasa na Umalizaji wa Ukoloni  pia ni mjumbe wa  Kamati  ya   nchi 24 ( C24) ambayo imekasimiwa jukumu la kumaliza ukoloni.

ngoma azipendazo ankal

Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Costantine Magavila


NSSF yanogesha mbio za Rock City 2014

$
0
0
 
 Afisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Jumanne Mbepo (kulia) akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 15 ili kudhamini mbio za Rock City Marathon 2014 Mratibu wa mbio hizo Bw. Mathew Kasonta (kushoto) katika hafla ya kukabidhi hundi hiyo na kutangaza rasmi zawadi zitakazotolewa katika mbio hizo iliyofanyika jijini Dar es Salaam Jana. Mbio hizo zitafanyika mkoani Mwanza, katika uwanja wa CCM Kirumba tarehe 26 mwezi Oktoba mwaka huu. NSSF ikiwa kama mdamini mkuu wa mbio hizo.
 Mratibu wa mbio za Rock City Marathon 2014 kutoka Capital Plus International (CPI), Bw. Mathew Kasonta (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 15 iliyotolewa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kudhamini mbio za Rock City Marathon 2014 na kutangaza rasmi zawadi zitakazotolewa katika mbio hizo jijini Dar es Salaam jana. Mbio hizo zitafanyika mkoani Mwanza, katika uwanja wa CCM Kirumba tarehe 26 mwezi Oktoba mwaka huu. NSSF ikiwa kama mdamini mkuu wa mbio hizo. Wakishuhudia katikati ni Afisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Jumanne Mbepo na Afisa Uhusiano wa NSSF, Bi. Anna Nguzo (Kulia).
 Afisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Jumanne Mbepo (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 15 kudhamini mbio za Rock City Marathon 2014 na kutangaza rasmi zawadi zitakazotolewa katika mbio hizo jijini Dar es Salaam jana. Mbio hizo zitafanyika mkoani Mwanza, katika uwanja wa CCM Kirumba tarehe 26 mwezi Oktoba mwaka huu. NSSF ikiwa kama mdamini mkuu wa mbio hizo. Wakishuhudia kushoto ni Mratibu wa mbio kutoka Capital Plus International (CPI), Bw. Mathew Kasonta na Afisa Uhusiano wa NSSF, Bi.. Anna Nguzo (Kushoto).
=========  =======  ========
NSSF yanogesha mbio za Rock City 2014
  • · Zawadi nono zatangatazwa kwa washindi

Zawadi za washindi wa mbio za Rock City zitakazofanyika katika mkoa wa Mwanza tarehe 26 mwezi huu zimetangazwa jana huku mdhamini mkuu wa mbio hizo, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) likitoa shilingi milioni 15 kuboresha mbio hizo.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya hundi ya shilingi milioni 15 kwa waratibu wa mbio hizo, Capital Plus International Limited, Afisa uhusiano wa NSSF, Bw. Jumanne Mbepo amesema kuwa NSSF imeendelea kudhamini mbio hizi kwa mwaka wa sita mfululizo kutokana na kuona maboresho yanayofanyika katika mbio hizo kila mwaka.

“Mbio hizi zitaambatana na kutoa elimu kwa wakulima na wachimbaji wadogowadogo wa madini katika kanda ya ziwa, juu ya umuhimu wa kujiunga na mfuko wa NSSF ili waweze kunufaika na huduma zitolewazo na shirika kama vile mkopo, bima ya afya pamoja na mafao mbalimbali,” Alisema Bw. Mbepo.

Mratibu wa mbio hizo, Bw. Matthew Kasonta amesema kuwa udhamini huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha maandalizi ya mbio hizo na kuleta maboresho makubwa katika mbio za mwaka huu. Amesema kuwa maboresho hayo ni pamoja na kuwepo kwa mbio fupi zitakazo jumuisha vijana kutoka katika shule za sekondari na wale waliopo shule za msingi madarasa ya juu.

“Baada ya kupata udhamini huu, tunafaraja ya kutaja zawadi watakazopatiwa washindi. Kwa mbio za Kilomita 21, jumla ya shilingi milioni saba na laki moja zimetengwa kwa ajili ya washindi. Washindi wa kwanza watazawadiwa Tsh 1.5m/- huku washindi wa pili watapata laki tisa na washindi wa tatu watapata laki saba kila mmoja.

Kwa mbio za kilomita tano, zaidi ya shilingi laki nne zimetengwa kwa ajili ya washindi. Jumla ya shilingi laki tatu na arobaini zimetengwa kwa ajili ya washindi wa mbio za kilomita 3 na shilingi laki mbili imetengwa kama zawadi kwa ajili ya mbio za watoto za kilomita mbili.” 

Bw. Kasonta amesema kuwa kwa mbio fupi ambazo zimeanzishwa mwaka huu (mita 100, mita 400 na mita 1,500) jumla ya shilingi laki nne na themanini pesa taslimu zimetengwa kwa ajili ya washindi huku washindi wote wa kwanza (wa kike na kiume) watapata king’amuzi cha Continental Decoders.

Bw. Kasonta aliwataja wadhamini waliofanyikisha mbio hizo kuwa ni Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), TSN Group kupitia kinywaji chake cha Chilly Willy, pamoja na African Barrick Gold, IPTL, Air Tanzania, New Mwanza Hotel, Nyanza Bottling, Sahara Media Group, Continental decoders, New Africa Hotel, PPF, Tanapa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

 “Nawasihi watu waendelee kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za usajili katika ofisi za kampuni ya Capital Plus International Limited (CPI) jengo la ATC ghorofa ya tatu jijini Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Mwanza, Ofisi zote za wilaya za Michezo na Utamaduni mkoani Mwanza na Uwanja wa Nyamagana,” alisema Bw. Kasonta.

WORD LUNG FOUNDATION NA SERIKALI YA MKOA WA KIGOMA WAZINDUA KAMPENI YA THAMINI UHAI OKOA MAISHA YA MAMA MJAZITO NA MTOTO

$
0
0
Na Editha Karo wa Globu ya Jamii, Kigoma

SERIKALI ya Mkoa wa Kigoma kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Word Lung Foundation chini ya ufadhili wa Swedish Internatinol Agency (SIDA) wamezindua Mkoani hapa kampeni ya''THAMINI UHAI OKOA MAMA MJAMZITO NA MTOTO''

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya alisema kuwa lengo la kampeni hiyo kuongeza na huduma kwa akina mama wajawazito waweze kujifungulia katika vituo vya huduma ya afya.

''Hawa ndugu zetu wa WLF wamekuwa wakitusaidia sana katika masuala ya afya ya mama mjazito na mtoto hapa kigoma,Mambo ya kujifungulia nyumbani yameshapitwa na wakati,nina waomba akina mama wote wanapo pata ujauzito kuanza klinik mapema ili waweze  kuonana na wataalam mapema''alisema machibya 

Naye Mganga Mkuu wa Hospitali  ya Mkoa wa Kigoma Dkt Leonard Subi alisema kuwa shirila la WLF limekuwa mstari wa mbele katika kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto katika Mkoa wa Kigoma.

Alisema wanawake wanaojifungulia katika vituo vya afya Mkoani Kigoma ni wachache hali hiyo ndiyo inayosababisha idadi ya vifo vya akina mama wajawazito kuwa kubwa,wengi hupenda kujifungulia manyumbani sababu ya fikra potofu.

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Word Lung Foundation nchini  Nguke Mwakatundu alisema kuwa shirika kupitia kampeni hiyo limedhamiria kupunguza matatizo ya uzazi wakatiwa kujifungua kwa akina mama.

Alisema kampeni hiyo itakayodumu kwa muda wa miezi mitatu inawalenga wanawake na wanaume wote MkoanI Kigoma itafanyika kwa njia ya radio,mabango,simu za mkononi,katuni na uhamasishaji.

''Nina amini kampeni hii itafanikiwa katika Mkoa wa Kigoma japo kuna changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa watumishi katika vituo vya afya,vitendea kazi pamoja na akina mama kuchelewa kufika katika vituo vya afya kwa wakati kujifungua''alisema Mkurugenzi Mkuu
Wahudumu wa Hospita ya Mkoa wa Kigoma maweni pamoja na wananchi wakitembea kwa maandamano kuelekea katika viwanja vya sekondari ya mwananchi Mkoani Kigoma kwaajili ya uzinduzi wa kampeni ya ''THAMINI UHAI OKOA MAISHA YA MAMA MJAZITO.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya akizindua kampeni ya ''THAMINI UHAI OKOA MAISHA MAMA MJAMZITO''katika viwanja vya sekondari ya mwananchi wa nyuma yake ni Katibu Tawala wa Mkoa Mhandisi John Ndunguru.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma pamoja na viongozi wengine wa serikali ya Mkoa wa Kigoma wakipiga makofi baada ya uzinduzi kufanyika.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali msataafu Issa Machibya akimpongeza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Word Lung Foundation Nchini Dkt Nguke Mwakatundu baada ya uzinduzi wa kampeni na anayefuata ni Mganga Mkuu wa Hospita ya Mkoa wa Kigoma Dkt Leonard Subi.

SALAMU ZA RAMBIRAMBI TOKA NRA KWA WAKAZI WA MKOA WA KIGOMA KWA AJALI YA BOTI

$
0
0

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam NAIBU KATIBU MKUU TAIFA NA KATIBU MKUU WA BODI ya CHAMA CHA UJENZI WA TAIFA, NRA (NATIONAL RECONSTRUCTION ALLIANCE), Mhe HASSAN KISABYA ALMAS, ametoa pole kwa wananchi wa mkoa wa kigoma na Uongozi Mzima wa mkoa kwa msiba mzito uliowapata baada ya watu zaidi ya kumi kupoteza maisha kwa ajali ya boti.
Ndugu Kisabya alisema, ajali ni jambo lisilotarajiwa na kuwataka ndugu jamaa na marafiki waliopoteza jamaa zao kuna na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.
Ndugu kisabya,aliomba uongozi wa mkoa kufuatilia kwa ukaribu sana ajaili hiyo ili kubaini chanzo cha ajali hiyo na kuweka mikakati thabiti ili ajali kama hiyo isitokee tena.
Kwa upande wa wahudumu wa safari hizo aliwaasa kutochukua idadi kubwa wa watu tofauti na uwezo wa chombo husika ili kuepusha majanga kama hayo, Ndugu kisabya alitoa shukurani kwa askari wetu wa Jeshi la wananchi walioshirikiana na wananchi katika kuopoa maiti na Mali za wahanga wa ajali hiyo,pia alitoa shukurani kwa uongozi wa SERIKALI ya mkoa Mzima kwa kuonyesha mshikamano Mkubwa katika ajali hiyo.
Katika salamu zake ,ndugu kisabya alisema, "NIMEGUSWA SANA NA MKASA HUU, NI AJALI MBAYA KUTOKEA ,NAUNGANA NA WAFIWA, WANANCHI WOTE,NA UONGOZI WA MKOA WA KIGOMA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU,HASA UKIZINGATIA NI NYUMBANI KWETU,PIA WALIOPOTEZA MAISHA NI WATANZANIA WAJENZI WA TAIFA NA NI HAZINA YA NGUVU KAZI YA TAIFA"
Mungu awalaze pema marehemu wote,MUNGU IBARIKI AFRIKA MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU IBARIKI KIGOMA!

NEWS ALERT: LORI LA MAFUTA LAWAKA MOTO MBAGALA JIJINI DAR USIKU WA KUAMKIA LEO

$
0
0
Sehemu ya mabaki Lori la mafuta lililoteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo maeneo ya Mbagala jijini Dar es salaam, baada ya kupiga mwereka likiwa katika hatakati ya kulikwepa gari lingine lililokuwa likitokea Kongowe ambalo liliingia ghafla barabarani bila ya tahadhari.
Awali, Lori hilo pamoja na kupiga kwake mwereka halikufanya na madhara yeyote wala dalili ya kusema litawaka moto.  Ila baada ya muda likaja kundi la vijana likiwa na madumu na mifuko ya plastiki na kuanza kuchukua mafuta yaliyokuwemo kwenye lori hilo hali iliyopelekea kutokea mlipuko mkubwa ulioliteketeza kabisa lori hilo.
Haijafahamika mpaka sasa kama kuna mtu yeyote aliyepoteza maisha katika moto huo, ila hasara kubwa imeonekana kutokea kwa nyumba tatu zilikuwepo jirani na eneo la tukio  ambazo zimeteketea kwa moto. Nyumba moja ni ya makazi ya watu, ingine ni duka la juma la Mchele pamoja nyumba ya kulala wageni. Globu ya jamii inaendelea kufatilia kwa ukaribu tukio hilo na tutaendele kujuzana.
Sehemu ya Lori hilo likiwa limeteketea kabisa.
Sehemu ya Wakazi wa Maeneo hayo wakiangalia kilichotokea huku wakiwa hawaamini wanachokiona.
Sehemu ya Nyumba zilizoteketea kwa moto.

JOOMLA! CMS WEBSITE / BLOG DESIGN & MAINTENANCE BOOT CAMP

$
0
0

November 8,9,15 and 16

DUDUMIZI TECHNOLOGIES LTD, Website design and Development Company in Tanzania is organizing 4 days  (2 Saturdays and 2 Sundays) training to equip participants with the skills, knowledge and techniques of designing, developing and maintaining good websites / blog by using Open source Content Management System called Joomla! 
Joomla is an award-winning content management system (CMS), which enables people to build Websites and powerful online applications. Joomla the most popular Websites software in the world. Almost 80% of Websites in Tanzania are designed using Joomla.

 Teaching Methodology
This is practical base boot camp will teach you how to do. Our Instructor will use his 5 years of experience working with Joomla to make sure when you finish, you are no longer a beginner.

However, that is not all. You will have the e-mail and contact numbers of your instructor entitled to Skype and email support for a period of 30 days after attending the Bootcamp. Even though you might not be ready to launch your website after the 5 days of training, you can work on your website at your own pace, with the added benefit of never being alone again when facing a question or uncertainty.

What you will learn:
  • Understanding Joomla World and Web technologies
  • How to design, secure and optimize website using Joomla
  • The art of Web Usability
  • Joomla Maintenance Issues
  • Introduction to Hosting and Server Management

Target Audience

  • Individuals who would like to have their very own website.
  • SMEs and small businesses owners who wish to cut down the costs of web development projects and manage their own website.
  • Individuals who wish to be self-employed in Website design and development
  • Web masters, website administrator, computer systems analysts, public relationship officers, communication officers and entrepreneurs.
  • Corporate IT Managers who wish to evaluate, optimize or secure their Joomla Website.

Training fee and Mode of payment

Participants will be required to pay 350,000/= Tanzania Shs. covering;
  • Tuition fees
  • Training materials. (Includes one copy of Joomla 3 Book)
  • 1 Year Kilimanjaro Hosting package (Worth 100,000) from Dudumizi.net
  • One .co.tz domain (worth 27000) from Dudumizi.net
  • Lunch

Venue:

Dudumizi Home, Mbezi Beach Dar es Salaam

Registration Process:

 In order to control and make this Bootcamp effective, There are limited seats available for this Bootcamp. Please book your seat before November 5, 2014. 

Certificates will be awarded to all participants!


Viewing all 110079 articles
Browse latest View live




Latest Images