Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 601 | 602 | (Page 603) | 604 | 605 | .... | 3285 | newer

  0 0


  WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya St Mary's ya Mazinde Juu iliyopo mkoani Tanga wameibuka vinara wa shindano la uandishi wa barua lililoshirikisha wanafunzi wa shule mbalimbali nchini katika kuadhimisha siku ya posta duniani.

  Shindano hilo la uandishi wa barua  limeratibiwa na Shirika la Posta Tanzania kwa kushirikiana na umoja wa posta duniani.
  Akizungumza  Dar es saalam leo katika hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya posta duniani, Mkurugenzi Mkuu wa Posta nchini,  Deus Mdeme  alitoa pongezi kwa washindi hao na walimu wao kwa kufanikiwa kuibuka videdea ambapo mshindi wa kwanza ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya barua ya kimataifa yatakayofanyika baadaye mwaka huu nchini Uswisi.

  "Madhumuni ya shindano hili ni kuwajengea uwezo vijana ambao hawajazidi miaka 15'' alisema Mdeme.


   Katika Shindano hilo la uandishi wa barua jumla ya washindi kumi walipatikana, huku St Mary Mazinde juu wakiibuka videdea kwa kutoa washindi wawili huku mshindi wa pili akitoka Shule ya Sekondari ya Lufingilo mkoani humo ambapo walikabidhiwa vyeti na zawadi mbalimbali.


  Aidha katika kuadhimisha siku hiyo ya posta duniani, yenye kauli mbiu isemayo posta inachukua nafasi yake katika mageuzi ya sekta ya mawasiliano imeadhimishwa kwa kuelezea malengo na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Posta Tanzania.


  Wakati huo huo Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Patrick Makungu kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, Profesa Makame Mbarawa, alielezea mafanikio na changamoto mbalimbali zinazoikabili Sekta ya Posta Tanzania katika kufanikisha malengo yake.

  Vilevile alitumia nafasi hiyo kuhamasisha wanafunzi wengi zaidi kushiriki katika shindano hilo linaloandaliwa na umoja wa posta duniani na kuwataka wadau wa posta nchini kushirikiana na shirika hilo ili likue na kutoa huduma kwa jamii baada ya kubadilisha ufumo wa utoaji huduza zake kwa kutumia zaida Tehama.

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Mkoma, akizungumza katika mkutano huo.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,  Sayansi na Teknolojia, Profesa Patrick Makungu akihutubia katika uzinduzi huo. 
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,  Sayansi na Teknolojia, Profesa Patrick Makungu (kushoto), akimkabidhi zawadi Mwalimu  Lucy Mshomi wa Shule ya Wasichana ya Kifungiro kutokana na mchango mkubwa kwa wanafunzi wao. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Posta, Deus Mndeme.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0
 • 10/09/14--09:22: WAPI HAPA??


 • 0 0
 • 10/09/14--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Ali Kiba - Mwana Dar es salama

  0 0

  Today is the World Day against Death Penalty. It is also the European Day against Death Penalty.

  The European Union and the Council of Europe have together reaffirmed their strong and absolute opposition to capital punishment in all cases and under all circumstances, and their commitment to its worldwide abolition.

  Death Penalty is against all the European Union stands for: our principles and values are about the promotion and protection of Human Rights which are universal and indivisible. The abolition of death penalty globally is one of the core objectives of EU's external policy and a personal objective of EU's High Representative / Vice-President Ashton.

  No Member State of the European Union applies death penalty. This is a core requirement to become a member of the European Union. Death Penalty inflicts capital punishment that becomes irreversible even in the case of victims of judicial error. Moreover, data show that the believed Death Penalty's deterrent effect has not resulted in the decrease of the targeted crimes. The EU as a whole works relentlessly towards the abolition of death penalty, focusing as a first step on setting and keeping a moratorium in the countries that still retain death penalty.

  While the overall trend towards the abolition of death penalty is positive, this year we note that the number of executions has increased worldwide, with breaches of moratoria, so we cannot be complacent in our efforts. Where death penalty still exists, we need to make sure that it is applied only for the most serious crimes, with guarantees of fair trial and sparing at least the youth and the mentally disabled.

  We welcome Tanzania's continued de facto moratorium since 1995 and we continue calling for the abolition of death penalty in Tanzania. We also welcome recent steps taken by the African Union towards the adoption of an Additional Protocol to the African Charter on Human and Peoples’ Rights on the Abolition of Death Penalty.

  We regret that Tanzania has not used the opportunity of the constitutional review process to move towards the abolition of death penalty and encourage her to consider this issue further in the next steps. We call on Tanzania to support the Resolution on a moratorium on the use of death penalty which will be put to vote at the 69th session of the UN General Assembly in December 2014.

  Finally, we congratulate the Tanzanian civil society organizations working towards the abolition of death penalty in Tanzania for their relentless efforts of awareness raising and campaigning.

  0 0

  photo 1photo 2photo 3photo 4photo 5f

  0 0
 • 10/09/14--22:31: KUMBUKUMBU
 • MAREHEMU MAMA JULIANA JOHN MBUYA
     11/10/2008 - 11/10/2014

  SIKU,WIKI,MIEZI  HATIMAYE  LEO IMEFIKA MIAKA SITA TANGU UTUTOKE DUNIANI.KAMWE HATUTAWEZA KUISAHAU SIKU HII.TUNAKUKUMBUKA  KWA  UPENDO ,USHAURI, NA UKARIMU WAKO NA KUTUREKEBISHA PALE TULIPOKOSEA NA KUTUONYESHA NJIA ILIYO SAHIHI YA KUFUATA.

  PUMZIKA KWA AMANI MAMA HUKO ULIPO. NA SIKU ZOTE ZA MAISHA YETU TUTAKUKUMBUKA SANA. TUKIAMINI  SIKU MOJA TUTAWEZA KUONANA.

   DAIMA UNAKUMBUKWA NA  MUME WAKO (MZEE JOHN MBUYA), WATOTO WAKO, WAJUKUU ZAKO, NDUGU JAMAA NA MARAFIKI  WOTE.

  RAHA  YA MILELE  UMPE EHE BWANA  NA MWANGA WA MILEE UMWANGAZIE
  ASTAREHE  KWA  AMANI. 
  AMEN

  0 0

  Na Hassan Hamad - India. 
  Kiasi cha wagonjwa 65,000 wenye ulemavu wa aina tofauti wanapatiwa visaidizi pamoja na matibabu kila mwaka nchini India, hatua ambayo huwawezesha kuendelea na shughuli zao za kimaisha kama kawaida. 
  Meneja wa kituo kikuu cha viungo bandia vya binadamu katika mji wa Jaipur jimbo la Rajasthan kaskazini mwa India, Om Prakash Sharma ameeleza hayo mbele ya waandishi wa habari kutoka baadhi ya nchi za Afrika, Asia na Latin America waliofika kituoni hapo hivi karibuni kwa ziara maalum ya kimasomo. 
  Sharma amesema kituo hicho kijulikanacho kwa jina la “Bhagwan Mahaveer Viklang Sahayata Samiti (BMVSS), ndio kituo kikubwa zaidi duniani kinachojihusisha na utengenezaji na utoaji wa viungo bandia vya binadamu vikiwemo miguu na mikono. 
  Amesema mara mgonjwa anapofika kituoni hapo au tawi lolote la kituo hicho miongoni mwa matawi 23 yaliyoko nchini India, hufanyiwa vipimo na baada ya siku chache hupatiwa viungo anavyohitaji bila ya malipo, ambavyo humuwezesha kuendelea na shughuli zake kama ilivyokuwa awali baada ya muda mfupi. 
  “Mara baada ya mgonjwa kupatiwa viungo anavyostahiki hufanyishwa mazoezi na baada ya siku chache tu anaweza kufanya shughuli zake za kimaisha ikiwa ni pamoja na kushiriki katika masuala ya kiuchumi pamoja na michezo”, alieleza Sharma na kuongeza; “Viungo vinavyotengenezwa na kituo hiki ni imara na vyenye viwango vya hali ya juu, na vinatengezwa kisayansi. Vinaweza kudumu hadi miaka sita au kumi bila ya kufanyiwa matengenezo ya aina yoyote”. 
   Amefahamisha kuwa mara nyingi wagonjwa wanaofika kwenye kituo hicho ambacho pia hujulikana kwa jina la “Jaipur Foot Knee/Limb” pamoja na matawi yake, ni wale waliopata ulemavu wa viongo kutokana na sababu mbali mbali zikiwemo za kimaumbile, ajali za barabarani, matukio ya vita na maradhi mbali mbali yakiwemo polio. 
  Sharma ameeleza kuwa kituo hicho kilichoanzishwa mwaka 1975 kwa lengo la kuwasaidia wagonjwa wanaopoteza viungo kutokana na sababu mbali mbali hasa watu wa daraja la chini, kilianza kwa kutengeneza na kutoa miguu na mikono bandia 59, ambapo hadi kufikia katikati ya mwaka huu tayari kimewahudumia watu wapatao milioni moja na laki nne (1.4 million), ambao ni wastani wa watu 50,000 hadi 65,000 kwa mwaka. 
  Ameongeza kuwa mbali na wagonjwa kupatiwa viungo hivyo, baadhi yao wamekuwa wakipatiwa visaidizi vyengine vikiwemo vigari na baiskeli ambavyo huwasaidia kuendeleza harakati zao za kimaisha ikiwa ni pamoja na kufanya biashara mbali mbali. 
  Pia baadhi yao wamekuwa wakipatiwa misaada ya fedha na vitendelea kazi kwa masharti nafuu. Katika jitihada za kuwasaidia wananchi hasa wa kiwango cha chini, Sharma amesema baadhi ya watendaji hulazimika kusafiri katika maeneo tofauti yaliyokumbwa na majanga yakiwemo vita ndani na nje ya India, ambako hufungua kambi katika maeneo hayo na kutoa huduma za kimatibabu kwa waathirika. 
  Amesema hadi kufikia mwaka 2014, tayari wametoa huduma katika kambi zipatazo 26 katika nchi mbali mbali zikiwemo Afghanistan, Philippines, Nigeria, Sudan, Rwanda na Kenya. Mohamad Sehebay kutoka mji wa Uttar Pradesh aliyefika kituoni hapo kwa ajili ya marekebisho ya mguu wake wa bandia, aliwaambia waandishi hao kuwa amekuwa akiutumia mguu huo kwa kipindi cha miaka sita mfululizo bila ya matatizo yoyote. 
  “Nilipata ajali ya barabarani mwaka 2008 na baada ya kupata taarifa za kituo hiki nilikuja hapa, na nashkuru nilipatiwa mguu bandia na unanisaidia sana. Tayari nilikuwa nimeshakata tamaa na maisha lakini namshukuru Mwenyezi Mungu kwa msaada wa kituo hiki nimeendelea kuishi kwa matumaini makubwa”, alisema Mohamad huku akionesha uso wa bashasha. 
  Wazo la kuanzishwa kituo hicho kinachofanya kazi kama taasisi binafsi (NGO), lilikuja baada ya bwana D.R.Mehta ambaye ni mwanzilishi wake kupata ajali mbaya ya barabarani, na kuungwa mkono na madaktari wawili waliompatia matibabu, wote kutoka hospitali ya Mahatma Gandhi, Jodhpur nchini India.
  Waandishi wa habari kutoka nchi mbali mbali wakiangalia viungo bandia vya binadamu, walipotembelea kituo kikuu kinachotengeneza viungo hivyo nchini India.
  Waandishi wa habari kutoka nchi mbali mbali wakiangalia viungo bandia vya binadamu, walipotembelea kituo kikuu kinachotengeneza viungo hivyo nchini India.
  Waandishi wa habari kutoka nchi mbali mbali wakiangalia viungo bandia vya binadamu, walipotembelea kituo kikuu kinachotengeneza viungo hivyo nchini India.
  Meneja wa kituo kikuu cha viungo bandia vya binadamu katika mji wa Jaipur nchini India, OM Prakash Sharma akionyesha mguu bandia wakati waandishi wa habari kutoka nchi mbali mbali walipofika kituoni hapo kwa ziara ya kimasomo. Picha kwa hisani ya Hassan Hamad-India


  0 0

  Lorraine akiwasili muda
  Lorraine Clement akipungia watu waliofika kumlaki , alipokuwa akiwasili uwanja wa ndege JNI, alipokuwa akitokea nchini, Thailand, kushiriki mashindano ya Miss Grand International 2014, ambapo Lorraine aliibuka nafasi ya 20 bora.

  Na Andrew Chale
  MWANADADA Lorraine Clement aliyeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo ya kimataifa ya Miss Grand International 2014, na kufanikiwa kushika nafasi ya 20 bora katika shindano lililofanyika mjini, Bangkok, Thailand, ametua nchini jana Oktoba 9 majira ya saa 10 jioni na kuwashukuru watanzania kwa kumuunga mkono.
  Akizungumza na wandishi wa habari muda mfupi alipowasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es Salaam, Lorraine aliwashukuru wadau mbalimbali kwa kufanikisha ushiriki wake kwenye mashindano hayo makubwa duniani, ikiwemo kampuni ya Redline Communication Ltd, Iliyofanikisha mshiriki huyo kushiriki kwa mwaka huu.
  “Pongezi kwa wadau wote mliofanikisha mimi kupeperusha vyema bendera ya Tanzania. Millen Magese kupitia kampuni yake ya MMG, Jacqueline Kibacha, Doreen Mashika, Husna Tandika na wengine wengi.
  Lorraine Clement akishukuru
  Lorraine Clement akishukuru Mungu, alipokuwa akiwasili uwanja wa ndege JNI, alipokuwa akitokea nchini, Thailand, kushiriki mashindano ya Miss Grand International 2014, ambapo Lorraine aliibuka nafasi ya 20 bora.

  0 0


  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Kiongozi wa Kampuni ya ZANCHICK inayojishuhulisha na biashara ya Kuuza  Kuku  (Perdue)kutoka Marekani  Dk.David Elua akiwa na ujumbe wa kampuni hiyo ulipofika Ikulu Mjini Unguja jana kwa mazungumzo
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein akizungumza na Uongozi wa Kampuni ya ZANCHICK inayojishuhulisha na biashara ya Kuuza  Kuku (Perdue) kutoka Marekani unaoongozwa na  Dk.David Elua  katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja jana. [Picha na Ramadhan Othman Ikulu, Zanzibar

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara, Uwanja wa Mashujaa mjini Mafinga, wakati wa ziara yake katika Jimbo la Mufindi Kaskazini, Iringa, ikiwa ni mwendelezo wa kuiamarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
  Kinana aliwataka viongozi kutokuwa na tamaa ya kuwa kiongozi na wakati huo huo kutaka kuwa matajiri pia aliwataka kuacha kujipendelea kujipa tenda badala ya kuwapatia kwanza wananchi.
   Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamoud Mgimwa akihutubia na kuelezea miradi mbalimbali iliyotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010 katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini Mafinga leo.
   Kinana akiangalia mashine za kupasua mbao katika kiwanda cha mtu binafsi cha Emanuel, mjini Mafinga, Mufindi.
   Kinana akiwa na mkurugenzi wa kiwanda binafsi cha mbao cha Emanuel, Charles Akyoo alipotembelea kiwanda hicho leo.
   Kinana akitembelea kiwanda hicho wakati wa ziara yake katika Jimbo la Mufindi Kaskazini. Picha zaidi BOFYA HAPA.

  0 0

  Mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika hufanyika kila mwaka wakati wa mikutani ya Benki ya Dunia na IMF na unahusisha kundi la nchi za Benki ya Dunia ambazo zinapata mikopo nafuu kutoka IDA. IDA ni shirika au mfuko wa maendeleo kwa ajili ya kutoa mikopo nafuu kwa nchi zinazoendelea kwa kundi la Benki ya Dunia.

  Katika mikutano hii wanazungumzia zaidi masuala ya sera za kibenki na mambo ya utawala kama vile ajira , uchaguzi wa wenyeviti wa mikutano hiyo na kamati mbalimbali. Mkutano huo unaudhuriwa na Mawaziri wa Fedha. Kwa mwaka 2014 -16 Mwenyekiti atakuwa Waziri wa Fedha kutoka Ethiopia na Makamu wake anatoka Gambia. Viongozi hawa wataongoza mpaka mwaka 2016. Mwaziri wa Fedha ni Magavana na Matibu wakuu ni MaGavana mbadala, hivi ni vyeo vya uwakilishi kattika Benki ya Dunia.

  Akiongea katika mkutano huo mwenyekiti aliyemaliza muda wake alisema kuwa”tumepata Mkurugenzi Mtendaji mpya wa kundi la kwanza la nchi za Afrika ambaye anatoka visiwa vya Shelisheli na Mbadala wake anatoka Zimbabwe “ alisema.

  Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo aliwaambia wajumbe kuwa anayemaliza muda wake anatoka Zambia na kuwa Viongozi hawa wanachaguliwa kwa kupigiwa kura na kila nchi. “Hawa watakuwa watendaji moja kwa moja kuanzia sasa na nafasi hizi zinapatikana kwa mzunguko.”alisisitiza.

  Vilevile katika kundi hilo kutakuwa na kamati ya maendeleo ambayo itakuwa na mwenyekiti ambaye atatoka Uganda na wajumbe watatoka Tanzania, Namibia pamoja na Sierralion.

  Jambo lingune ambalo limeongelewa kwenye mkutano huo muhimu ni kwamba Benki itaendelea kutoa misaada ya fedha kwa nchi zinazoendelea toka kwenye mfuko wa IDA kwa kuzingatia vipaumbele vya nchi husika.

  Vilevile walisisistiza suala la gonjwa la EBOLA. Walielezea kuwa wataendelea kusaidia kupeleka misaada kwa nchi zinazokabiliwa na hilo tatizo. Pia Benki ya Dunia itaendelea kupeleka wafanyakazi kujifunza jinsi Benki ya Dunia inavyofanya kazi na kusisitiza kuwa ni muhimu kuchagua watu wazuri ambao wana uwezo ili wanaporudi nchini kwao waweze kutumia ujuzi wanao upata.

  Mwisho walimalizia kwa kusema kuwa Benki itaendelea kusaidia jitihada ambazo zinalenga matokeo makubwa sasa kwani hata wao wanafanya kazi kwa kuzingatia matwakwa ya BRN. Hivyo wanatagemea fedha zinazotolewa zitafanikisha kuwa na matokeo makubwa sasa. Hali ya hewa mjini hapa ni baridi kiasi.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile akifuatilia kwa makini mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika- Benki ya Dunia ambao umefanyika leo hapa mjini Washington DC.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile akisoma nyaraka za mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika- Benki ya Dunia ambao umefanyika leo hapa mjini Washington DC.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile akisoma nyaraka za mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika- Benki ya Dunia ambao umefanyika leo hapa mjini Washington DC. Aliye kaa nyuma yake ni Kamishna wa Fedha za Nje Bw. Saidi Ngosha Magonya.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile akisoma nyaraka za mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika- Benki ya Dunia ambao umefanyika leo hapa mjini Washington DC. Picha zote na Ingiahedi Mduma- Wizara ya Fedha.

  0 0

  Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Steven Kissuiakizungumza katika mdahalo wa vijana leo mkoani Tabora ambapo mdahalo huo umefanyika ikiwa ni kuadhimisha Wiki ya Vijana ambayo kitaifa inafanyika mkoani hapa.
  Mchumi Mkuu Sekretariat ya Mkoa wa Tabora Bw.Nicholas Kileka akitoa mada kuhusu ijue Tabora leo mkoani humo wakati wa mdahalo uliohusisha vijana mbalimbali wanaoshiriki maadhimisho ya Wiki ya Vijana ambayo kitaifa yanafanyika mkoani humo.
  Afisa Vijana Mwandamizi kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Florent Karist akitoa mada kuhusu maudhui ya Wiki ya Vijana leo mkoani humo wakati wa mdahalo uliohusisha vijana mbalimbali wanaoshiriki maadhimisho ya Wiki ya Vijana ambayo kitaifa yanafanyika mkoani humo.


  0 0

  Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

  Halmashauri ya Geita  itaanza kupata  wastani wa  Dola za Marekani milioni 1.8 kwa mwaka  kutoka Mgodi wa  Dhahabu wa  Geita (GGM) baada ya kusainiwa rasmi kwa marekebisho ya mkataba  baina ya kampuni hiyo na Serikali.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo  kabla ya kutiliana saini marekebisho ya mkataba huo  ambao uliosainiwa  awali mwaka 1999. Awali, Halmashauri hiyo ilikuwa ikipata  ushuru wa huduma wa  Dola za Marekani  200,000 kila mwaka badala ya kulipwa  asilimia 0.3 ya mapato ghafi ya kila mwaka  kama sheria ya fedha ya serikali za mitaa ya mwaka 1982 inavyotaka.

  Kwa kuzingatia kiwango cha mapato ghafi  ya mgodi wa Geita kwa mwaka yanayopatikana hivi sasa,  Halmashauri ya Geita itakuwa na uhakika wa kupata  kiasi kisichopungua  Dola za Marekani  milioni 1.8 kwa mwaka.

  Kwa mujibu wa makubaliano  yaliyofikiwa  kati ya Serikali  na wamiliki wa mgodi huo, malipo hayo yataanza kulipwa  rasmi kuanzia tarehe 01 Julai, 2014.
  Profesa Muhongo alisema kuwa fedha hizi ni nyingi mno  na kuwataka  wananchi wa Geita kujiandaa kwa ajili ya maendeleo ya miundombinu  pamoja na huduma za jamii  zitakazopelekea uchumi wake kukua kwa kasi.

  Profesa Muhongo alisisitiza kuwa ni vyema makabidhiano ya  fedha hizo kwa njia ya hundi yakafanyika kwa uwazi mbele  ya wananchi ili kupunguza malalamiko, ikiwa ni pamoja na kuongeza imani kati ya wananchi na migodi.

  Aidha, aliwataka Viongozi wa Halmashauri hiyo,   kusimamia vyema fedha hizo kwa kuhakikisha kuwa zinachangia katika shughuli za maendeleo badala ya kutumika katika matumizi yasiyo ya lazima na tija katika jamii, hususani kulipana posho  za vikao na safari.

  “ Kwa mazingira ya sasa, mji wa Geita hauna sababu ya kukosa maji, barabara bora, vituo  vya afya, ni imani yangu kuwa fedha hizi zitachangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi wa Geita iwapo zitasimamiwa ipasavyo,” alisema.

  Maeneo mengine yaliyofanyiwa  marekebisho  kwenye mkataba wa awali  uliosainiwa mwaka 1999 ni kupandisha kiwango  cha malipo ya mrabaha kutoka asilimia  tatu ya mapato baada ya kuondoa gharama za uchakataji madini na kufikia asilimia nne ya mapato ghafi.

  Eneo jingine lililofanyiwa marekebisho ni kufuta kipengele kilichokuwa kinatoa nyongeza ya asilimia 15 kwenye mtaji wa uwekezaji ambao haujarejeshwa. Kuendelea kuwepo kwa kipengele hiki kwenye mkataba, kungeipunguzia serikali  kodi ya mapato.


  0 0

  Marehemu Dkt. William Shija.

  0 0

  Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye tai nyekundu) akiwa katika picha ya pamoja Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Wabunge hao wanashiriki ziara ya mafunzo Brussels ya kutembelea taasisi mbalimbali za Jumuiya ya Ulaya.

  0 0

  Familia ya  Mzee Ndege Inasikitika kutangaza  kifo cha  ndugu yao mpendwa Omar Ndege Mgori  (pichani) kilichotokea India. Mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwa Marehemu Mbezi Juu Njia ya Goba.Habari ziwafikiw ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo.

  Kwa taraarifa zaidi wasiliana na :

  0718066661 - Jaji Mgori
  0787523152 - Tumaini Mgori
  +199869103747 - Mohammed Mgori

  0 0  0 0


  0 0
 • 10/10/14--08:58: KUMBUKUMBU
 • MZEE ASHERI MWASANDUBE

  Umetimiza miaka miwili tangu ulipoitwa na Bwana tarehe 11 Oktoba, 2013. Tunamshukuru Mungu kwa kutupa nguvu ya kuvumilia hadi sasa. Tunakumbuka hekima na busara zako ambapo pengo hilo hakuna wa kuliziba kwani ulikuwa kiongozi, nuru na furaha katika familia yetu.

  Unakumbukwa daima na Mke wako mpendwa Elesia Katapa, watoto wako Hilda, Salome, Stephen, Sekela, Abrahamu, Wakwe zako wajukuu zako pamoja na ndugu jamaa na marafiki.

  Tunaamini siku moja tutaungana nawe katika uzima wa milele.

  Pumzika kwa amani baba yetu mpendwa.
  2 Timotheo 4:7-8

older | 1 | .... | 601 | 602 | (Page 603) | 604 | 605 | .... | 3285 | newer