Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 600 | 601 | (Page 602) | 603 | 604 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Aina hii Malware inayojulikana kama Tyupkin yaleta maafa katika mashine za ATM. Tyupkin imekua ikisambazwa na kundi la wahalifu mtandao kutokea ulaya mashariki na kusababisha pesa nyingi kuweza kutoka kupitia ATM mashine ambapo tayari wataalam wa usalama mitandao kutoka Kaspersky Lab wakishirikiana karibu na polisi wasio na mipaka “Interpol” wameshaanzisha oparesheni ya pamoja kutafuta chanzo na ugunduzi katika mashine 50 umebainika hadi sasa.
  Uchunguzi wa kina umeonyesha Mashine zilizo athirika zimekua zikigundulika kuwa na Window XP yenye 32-bit ambayo tayari Microsoft walisha tahadharisha watumiaji wake. Utafiti unaonyesha Mashine nyingi za ATM bado zimeendelea kutumia Window XP ambapo imekua ikirahisisha sana kuingiliwa na wahalifu. 
   Tahadhari imeendelea kutolewa katika maeneo mengine kwani ingawa kunajitihada za dhati za kukabiliana na Tyupkin bado inaonekana kusambaa katika maeneo mengine mbali mbali duniani na hofu ni kubwa kuwa huenda Afrika ikaonekana kuwa ni eneo jipya litakaloathirika. 
   Ili kupata kujua zaidi juu ya ya angalizo la Window XP  BOFYA HAPA HAPA
  Na  kupata taarifa za kitaalam za  ya Tyupkin 
  na uchunguzi wake BOFYA HAPA

  0 0


  Mama Furaha akipika katika nyumba ya rafiki yyake Cady ambaye aliwakaribisha nyumbani mwake.© UNHCR/A.Nijimbere
  Maisha baada ya kuishi ukimbizini huhitaji msaada mkubwa katika nyanja zote za uchumi, kijamii na hata kisaikolojia! 
  Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini Kenya limejikita kusaidia wakimbizi katika kustawisha maisha yao ambapo huanza kwa makazi.
  Akizungumza wakati wa mahojiano na Joseph Msami wa idhaa hii mwakilishi mkazi wa UNCHCR nchini Burundi Abel Mbilinyi anasema hatua hiyo inakomboa maisha ya wakimbizi takribani laki tano huku pia akizungumzia nafasi ya wakimbizi katika uchaguzi mkuu ujao. Kwanza anaanza kufafanua namna UNHCR inavyopoka na kusidia wakimbizi
  (SAUTI MAHOJIANO)

  0 0
 • 10/08/14--19:22: mchakarikaji


 • 0 0

  East African Legislative Assembly
  East African Legislative Assembly, Brussels, Belgium, October 8, 2014: A delegation of EALA legislators arrived in Brussels yesterday ready for a five day benchmarking visit.

  The benchmarking visit will see the EALA meet and exchange ideas with Parliamentarians and key officials of the European Parliament and the European Commission respectively. The delegation which is headed by the EALA Speaker, Rt. Hon Margaret Nantongo Zziwa, consists of Members of the Commission, Chairpersons of the Committees of EALA and key Parliamentary staff.

  The Speaker of EALA termed the visit fundamental as EALA makes its contribution to strengthening the integration dispensation.

  The objectives of the benchmarking visit are noble.   As you are aware, both the European Parliament and EALA share some unique attributes in terms of similarities and differences.  Only the EU Parliament and EALA have legislative powers that supercede national laws. 

  The visit thus enables us to learn and to be better informed about the EU Parliament as well as sharing of experiences” Rt. Hon Dr Zziwa said.

  Today, the legislators will visit the Parliamentarium (visitors centre of the European Parliament) so as to learn more about the institutions of the EU and to apprise themselves of the journey of European integration and the impact it has on the lives of the people.

  Later on in the afternoon, a session facilitated by a Parliamentary Consultant, Mr. Allistair Doherty on Committee processes shall be held.   Other areas of interest to be covered during the five day tour include budgeting and financing of the European Parliament, relationships between the Parliament and National Parliaments, relationships between the EU Commission and the Parliament and how Parliamentary democracy works.  

  A key meeting with high ranking representatives of the European Commission shall be held on Friday this week. The visit is supported by the Westminster Foundation for Democracy and the Association of European Parliamentarians for Africa (AWEPA).

  The European Parliament has been on the scene longer than the EALA. The European Parliament was established in 1952 with 78 Members and initially had no legislative powers.  Today, the Parliament which works closely with the Council of Ministers and the Commission (Secretariat) to exercise legislative functions has perhaps the largest trans-national democratic electorate in the world.   EALA on its part was inaugurated in 2001.

  It is anticipated that the trip shall enable the sharing of experiences on best practices in legislative procedures, Parliamentary administration and operation of Committees. Further on, the trip creates an opportunity for future interactions and exchanges on current Parliamentary affairs.

  0 0

   JAJI KIONGOZI WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA MHE. SHABAAN A. LILA WA KWANZA KULIA NA MTENDAJI MKUU WA MAHAKAMA BW. HUSSEIN A. KATTANGA WAKIWA NDANI YA STUDIO ZA MAGIC FM JIJINI DAR ES SALAAM KWENYE KIPINDI ASB KINACHOENDESHWA NA WATANGAZAJI OREST KAWAU, MARY EDWARD NA KIBWANA DACHI.

   WATANGAZAJI WA KIPINDI CHA MORNING MAGIC , MARY EDWARD NA OREST KAWAU WAKIWA NDANI YA MAGIC FM WAKATI WA MAHOJIANO NA JAJI KIONGOZI WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA MHE. JAJI SHABAAN A. LILA NA MTENDAJI MKUU WA MAHAKAMA BW. HUSSEIN A. KATTANGA AMBAO HAWAPO PICHANI. 

   WATANGAZAJI WA KIPINDI CHA MORNING MAGIC  NDANI YA REDIO MAGIC FM WA KWANZA KULIA NI KIBWANA DACHI, ANAYEFUATA BW. HUSSEIN  A. KATTANGA –MTENDAJI MKUU MAHAKAMA  TANZANIA, ORESTI KAWAU , JAJI KIONGOZI WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA MHE  JAJI  SHABAAN A. LILA, MARY EDWARD NA MARY GWERA  OFISA HABARI WA MAHAKAMA KUU  TANZANIA,  WAKIWA KATIKAPIHA  YA PAMOJA MARA BAADA YA KUMALIZA MAHOJIANO KUZUNGUMZIA UTARATIBU ULIOANZISHWA WA KUSIKILIZA/KUMALIZA KESI ZA MUDA MREFU NCHINI. 

  Kusikiliza sehemu ya kipindi hicho na mahojiano na Jaji Kiongoze nenda:


  0 0

  Ndani ya mwezi ujao wa Kumi na Moja (November) Tarehe 2 itakuwa ni siku yenye Neema kwani Arusha Kutashushwa Baraka ya Kumthamini na kumuonyesha Upendo Mama Wa Kitanzania na Duniani Kote.

  Hadi sasa Maandalizi ya Tamasha la Upendo kwa Mama Yamekamilika ambapo Tarehe 2 November 2014 Ndani ya Viwanja vya Sheikh Amri Abeid Kutafanyika tamasha hilo lililobarikiwa jina la UPENDO KWA MAMA ambapo Tamasha hilo litaongozwa na waimbaji wa Nyimbo za Injili wakubwa kutoka humu Nchini na Nchi Jirani ya Kenya.
  Wasanii hao wa Injili Watakaoongoza Tamasha la UPENDO KWA MAMA Sara K kutoka Nchini Kenya na Cristina Shusho kutoka Tanzania, huku likipambwa na Ambwene Mwasongwe, Baraka Maasa, Eng calros Mkundi, Ester Bukuku, Matha Mwaipaja, Nesta sanga, Meth Chengula, Matumaini, Eline Patrick bila kuwasahau waimbaji wengine kutoka Mkoani Arusha pamoja na Kwaya Mbalimbali.
  Lengo hasa la tamasha hilo la UPENDO KWA MAMA ni kutoa Mitaji kwa zaidi ya akina mama 50 wajasiriamali ili kuwaongezea uwezo wa kujiajiri, vilevile utakuwa ni wakati mwafaka wa kuwashukuru wakinamama wote kwa upendo walionao ukiambatana na kujitolea katika kusimamia Familia na malezi ya watoto.
  Kama Mtanzania au Usiyekuwa Mtanzania mwenye Mapenzi na mama Basi unaalikwa Kufika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha Tarehe hiyo na utashuhudia Tamsha hilo kwa Kuchangia Kiingilio Kidogo tu ambacho ni Sh. 3,000/= (Elfu Tatu ya Kitanzania)
  Tamasha la UPENDO KWA MAMA limeandaliwa na Mkundi Production ya Jijini Arushana wao kama kamati ya maandalizi ya Tamasha la UPENDO KWA MAMA wanatoa nafasi kwa watanzania, Taasisi na Mashirika yote ambayo yako tayari kuungana na Studio ya Mkundi kwa Ufadhili wa hali na mali ili kufanikisha tamasha hili la UPENDO KWA MAMA.
  SAM_0669
  Engineer Carlos Mkindi ambaye ni mkurugenzi wa mkundi production akiongea na wanahabari kuhusiana na Tamasha la Upendo kwa mama ambalo linalenga kutoa mitaji kwa zaidi ya akina mama 50 wajasiriamali ili kuwawezesha kujiajiri pamoja na kuwaombea na kuwashukuru kwa moyo wa upendo waliyonayo kwa kujitoa katika kusimamia familia na malezi
  SAM_0670
  Mratibu wa Tamasha la Upendo kwa mama Bw. Linus Kilembu akiongelea maandalizi ya Tamasha kuwa limekamilika kwa asilimia 90

  0 0

  Ernest Napoleon ni Mtanzania MUIGIZAJI anaeishi San Francisco, amefanya movie inayoitwa Going Bongo bit.ly/goingbongoitunes.
  Hivi sasa yupo kwenye mchakacho wa kushirikishwa katika filamu ya kampuni ya Forest Whitaker inayoitwa “The Driver”.
  Ernest Napoleon akiwa na  Forest Steven Whitaker actor, producer, na directorwa filamu za kiMarekani
  Ili kufanikiwa kwenye filamu hiyo, alikuwa anahitaji kura za waTanzania na waKenya kwa ujumla ili kumfikisha Shindano hilo.
  Tunaomba msaada wenu wa ku SHARE habari hii pamoja na maelekezo ya jinsi ya kunipigia kura:
  1)Bonyeza link hiyo hapo Bit.ly/castErnest kisha una log in kwa kutumia Facebook account.
  2)Unabonyeza "newest" Unasukuma kidogo.
  3)Unaibeba picha (drag) hadi kwenye kibox kilichopo juu na kuipachika. p.s: tumia computer badala ya simu kuvote itapendeza zaidi
  Tafadhalini fata maagizo ili kumnyanyua Mtanzania mwezetu, kwani kesho ndio mwisho wa kuchukua mahesabu ya upigaji kura yako Bofya hapa and Vote now.. 

  0 0

  Warembo wataoshiriki fainali za Miss Tanzania Jumamosi katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam
  Kutoka maktaba: Hashim Lundenga akiwa na mshirika wake
  Prashant Patel katika moja ya mashindano ya urembo yaliyopita

  Na Mwene Saidi, Kisutu
  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imeamuru mashindano ya urembo Tanzania yaliyopangwa kufanyika Oktoba 11, mwaka huu kuendelea baada ya kutupilia mbali maombi ya dharura yaliyowasilishwa na Prashant Patel dhidi ya Hashimu Lundenga ya kuzuia kuendelea kuendesha kinyang'anyiro hayo kwa madai ya kukiuka mkataba wa makubaliano yao. 
   Kadhalika mahakama hiyo imesema maombi ya hati ya dharura yaliyowasilishwa na Patel hayana mashiko ya kisheria na kwamba kuzuia kufanyika mashindano hayo ambayo madhamini mbalimbali wamewekeza fedha zao itasababisha mgangano wa kimaslahi. 
   Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi Frank Moshi baada ya kusikiliza hoja za mawakili wa pande zote mbili kuhusu maombi hayo ya dharura ya kuzuia mashindano hayo kufanyika Oktoba 11, mwaka huu. Hakimu Moshi alisema mlalamikaji amefungua kesi mahakamani hapo pamoja na maombi ya hati ya dharura akiitaka mahakama yake kuzuia mashindano kufanyika kutokana na mlalamikiwa kuvunja haki dhidi ya mwanzilishi mwenzake Patel. 
   Alisema Patel kupitia hoja za maombi yake, amedai kuwa Lundenga alivunja mkataba huo kwa kufanya mawasiliano moja kwa moja na mawakala bila kumshirikisha. Hata hivyo, mahakama bila kuacha shaka imeona hakuna sababu za msingi katika hati hiyo ya kusababisha mashindano hayo yasifanyike na kwamba hayawezi kuathiri kesi ya msingi iliyofunguliwa na mlalamikaji huyo. 
   “Mahakama imeona hakuna sababu ya kuzuia mashindano hayo kwa sababu wadhamini na washiriki wametumia gharama zao na kwamba kwa kufanya hivyo kutasababisha mgongano wa kimaslahi” alisema Hakimu Moshi wakati akitupilia mbali hati hiyo ya dharula. 
   Akifafanua zaidi alisema hati ya dharura ya mlalamikaji haina mashiko kisheria kwa sababu kesi yake ya msingi ipo mahakamani na kwamba haina uhusiano na mashindano yatakayofanyika Oktoba 11, mwaka huu. Mapema juzi, mahakama hiyo ilitupilia mbali pingamizi la awali la Lundenga lililotaka hati hiyo ya dharura kutupiliwa mbali.

  0 0  0 0

  Mzee Alfredy Raphael Kiswaga 
  Baba leo unatimiza miaka kumi na tano toka ulipotutoka. Mtoto wak Fredy Kiswaga, Kaka na dada pamoja na ndugu, jamaa, marafiki na majirani wanakukumbuka siku ya leo, huku wakiwa na imani kuwa japo kimwili haupo nao, lakini kimawazo na upendo viko pale pale.
  Siku ya Jumapili Oktoba 12, 2014  kutakuwa na misa ya kumbukumbukatika Kanisa Katoliki la Mwenge la Mt. Maximilian saa mbili asubuhi. 
  Nyote mnakaribishwa kumkumbuka na kumuombea 
  Mzee Alfredy Raphael Kiswaga.
  Mbarikiwe sana. 

  0 0
 • 10/09/14--01:23: Bei ya Madafu leo


 • 0 0

   Afisa Mtendaji Mkuu wa TSN group, Bw.  Farough Baghozah (wapili kushoto)akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 13 Mratibu wa Mbio za Rock City Marathon 2014, Bw. Mathew Kasonta (wa kwanza kulia) wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Mbio hizo zitafanyika mkoani Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba tarehe 26 Mwezi huu. Wakishuhudia wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Operesheni wa TSN Group Bi. Pamela Mandari, na Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo Bi. Koiya Kibanga (wa kwanza kushoto). 
   Afisa Mtendaji Mkuu wa TSN group, Bw.  Farough Baghozah  (wapili kulia)akifafanua jambo  kwa waandishi wa habari wakati wa kukabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 13 iliyotolewa na kampuni hiyo kudhamini mbio za Rock City Marathon 2014 zitakazofanyika mkoani Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba tarehe 26 Mwezi huu. Wakishuhudia kulia ni Mkurugenzi wa Operesheni wa TSN Group Bi. Pamela Mandari, Mratibu wa mbio hizo, Bw. Mathew Kasonta (wapili kushoto) na Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo Bi. Koiya Kibanga (wa kwanza kushoto). 
   Mratibu wa mbio za Rock City Marathon, Bw. Mathew Kasonta, (wa pili kushoto) akiongea na waandishi muda mfupi kaba ya kupokea hundi yenye thamani ya shilingi milioni 13 iliyotolewa na kampuni ya TSN Group kuoitia kinywaji chake cha Chili Willy kama udhamini wa mbio hizo kwa mwaka huu zitakazofanyika mkoani Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba tarehe 26 Mwezi huu. Kushoto kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa TSN group, Bw.  Farough Baghozah akifuatiwa na Mkurugenzi wa Operesheni wa TSN Group Bi. Pamela Mandari, na kushoto ni Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo Bi. Koiya Kibanga (wa kwanza kushoto). 

  0 0

   Mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba Mhe.Samuel Sitta akikabidhi  katiba inayopendekezwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho kikwete na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Mohamed Ali Shein katika hafla iliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma Oktoba 08, 2014
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho kikwete na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Mohamed Ali Shein wakiwa wameinua juu  Katiba inayopendekezwa katika hafla iliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma Oktoba 08, 2014 Kulia ni Mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba Mhe.Samuel Sitta akifuatiwa na Makamu wake Mhe samia Suluhu Hassan 

  0 0

  Na. Ally Mataula – Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

  Baraza la Maadili limetoa amri ya kukamatwa mara moja Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Mrisho Gambo kwa kukaidi wito wa kufika mbele ya Baraza hilo kujibu tuhuma zinazomkabili.

  Akizungumza baada ya kuahirisha kikao cha Baraza hilo lililoanza vikao vyake tarehe 9/10/2014, Mwenyekiti wa Baraza la Maadili Mhe Balozi Jaji (Mst.) Hamisi Msumi alisema kuwa amri hiyo imetolewa kwa mujibu wa fungu la 24 (4) la Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya 1995 ambayo imempa mamlaka Mwenyekiti wa Baraza hilo kutoa amri ya kukamatwa Kiongozi yeyote atakaekaidi wito wa kufika mbele ya Baraza na kwa mujibu wa fungu hilo amri hiyo itatekelezwa na Afisa wa Polisi.

  Kiongozi huyo ambaye anatuhumiwa kwa makosa ya matumizi mabaya ya Madaraka aliitwa mbele ya Baraza hilo ili aweze kujibu tuhuma zinazomkabili.

  Baraza la Maadili limeanza vikao vyake ambapo mashauri 19 ya viongozi wa kada mbalimbali wanaotuhumiwa kikiuka Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kutumia vibaya madaraka yao na kushindwa kuwasilisha Tamko la Mali na Madeni yatasikilizwa.

  Vikao hivyo vya Baraza la Maadili vinafuatia kukamilika kwa uchunguzi wa awali uliofanywa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuhusu tuhuma za ukiukwaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma dhidi ya Viongozi husika.

  Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Baraza hilo litaendelea na vikao vyake mpaka tarehe 17/10/2014.
  Mwenyekiti wa Baraza la Maadili Mhe. Balozi Jaji (Mst.) Hamisi Msumi katikati akiwa na Wajumbe wa Baraza hilo Bibi Selina Wambura kushoto na Bibi Hilda Gondwe kulia kabla ya kuanza kusikiliza Mashauri ya ukiukwaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma yaliyowasilishwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
  Mwanasheria wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. Hassan Mayunga akifafanua jambo mbele ya Mwenyekiti wa Baraza la Maadili Mhe. Jaji Hamis Msumi.

  0 0
 • 10/09/14--07:26: POLISI JAMII AKIWAJIBIKA
 • Moja ya kitu ambacho Jeshi la Polisi nchini limecheza heko,ni kuanzisha kitengo cha Ulinzi shirikishi kwa kuwachukua vijana mbali mbali mitaani na kuwafunda vyema baadhi ya kazi za jeshi hilo vijana wa Polisi Jamii,hiki ni kitu kikubwa na safi sana kwa vijana hao kwa wingi wao,kwani wameweza kulipiga tafu Jeshi hilo,hasa katika kusaidia Askari wa Usalama Barabarani kuongoza magari ili kupunguza misongamano isiyokuwa na ulazima.pichani ni mmoja wa Polisi Jamii akiongoza magari barabarani.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Tabota Fatuma Mwasa akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya katika maonesho ya wiki ya vijana yanayofanyika kitaifa mkoani humo, aliyesimama ni Meneja wa Mfuko Mkoa wa Tabora.
  Vijana wakiwa kwenye banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakipima afya zao. Katika maonesho hayo Mfuko unaendesha zoezi la upimaji afya bure.
  Mtaalam wa macho Antony Janken akimpima macho Rehema Majaliwa ambapo huduma ya macho pia inatolewa bandani hapo. 
  Kijana John Masanja akipata vipimo na ushauri wa kuepukana na maradhi yasiyoambukiza bandani hapo.  0 0

  "Mhisani anayekusaidia kujijengea uwezo wa kujitegemea ni muhimu sana kuliko Yule anayekupatia msaada kila siku bila kukujengea uwezo wa kusimama mwenyewe na kujitegemea”anasema Bw.Omar Abdul Kyaruzi Katibu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Mwandaliwa kilichopo eneo la Boko wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam kutokana na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania kusaidia kituo hicho kujenga banda la kisasa kwa ajili ya kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku.

  Mbali na kufadhili ujenzi wa banda la kuku pia wafanyakazi wa Vodacom Tanzania katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja inayoendelea wamejitolea muda wao kushiriki katika ujenzi wa banda hilo la kisasa ambalo lina ukubwa wa kufugiwa kuku wapatao 2,000 kwa pamoja.

  Afisa Mwandamizi wa Vodacom Tanzania kutoka kitengo cha Huduma kwa wateja Benson Megehema, amesema kuwa wiki hii mbalimbali na kuongea na wateja na kuwaelimisha huduma bora zinazotolewa na kampuni pia wameona ni muhimu kutenga muda wao kusaidia shughuli za kijamii hususani kusaidia wahitaji kwenye jamii.

  “Kwetu Vodacom kusaidia jamii ni moja ya sera yetu na siku zote tutakuwa mstari wa mbele kusaidia jamii tunayoishi na kufanyia biashara na tunaamini kuwa kusaidia sio kutoa fedha tu bali ni kujitoa muda wetu pia kujumwika na watoto hawa wapatao themanini na kitu na kuweza kusaidia shughuli za kijamii kwani tunatambua uhitaji wetu ni muhimu sana kwa watoto hawa tukiwa na lengo la mradi huu kuweza kuwasaidia katika mahitaji yao ya hapa na pale”Anasema Magehema.

  Kwa upande wake Katibu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Mwandaliwa,Bw.Omar Kyaruzi,alisema kuwa wanashukuru kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kuona umuhimu wa kuweajengea banda kwa ajili ya uanzishaji wa mradi wa ufugaji wa kuku.

  Pia aliongeza kuwa wamefarijika kuona wafanyakazi wa Vodacom wanaacha kazi zao ofisini na kuungana na mafundi katika kazi ya ujenzi “Suala hili limetutia moyo sana hata watoto tunaowalea wamejifunza kuwa msaada sio kutoa fedha peke yake bali kutumia muda wako kusaidia jamii ni msaada mkubwa kwa kuwa wakati ni pesa”Alisema Kyaruzi.

  Kyaruzi alisema kuwa Kituo cha watoto yatima cha Mwandaliwa kinatoa malezi kwa watoto yatima na kimekuwa kikitegemea kujendesha kupitia misaada mbalimbali inayotolewa na wafadhili.
  Katibu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Mwandaliwa cha Bunju jijini Dar es Salaam, Bw.Omar Abdul Kyaruzi(kushoto)akimpa maezo Meneja wa Vodacom Foundation,Grace Lyon jinsi ujenzi wa banda la kisasa kwa ajili ya kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku unaufadhiliwa na taasisi ya Vodacom foundation unavyoendelea kituoni hapo walipotembelewa na wafanyakazi wa Vodacom katika kushiriki kwenye ujenzi huo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja duniani.
  Wafanyakazi wa Idara ya huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,wakishiriki katika ujenzi wa banda la kisasa kwa ajili ya kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha Mwandaliwa kilichopo Bunju, jijini Dar es salaam,Wafanyakazi hao walishiriki katika ujenzi huo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja duniani.

  0 0

  KAMPUNI ya simu za mkononi ya airtel imezindua rasmi namba itakayowawezesha watanzania kushiriki mashindano ya kusaka vipaji ya muziki ya Airtel Trace Music Stars kwa kurekodi na kutuma nyimbo zao kwa kutumia simu zao za mkononi huku baadhi ya wasanii chipukizi wakipata nafasi yakuonyesha vipaji vyao katika viwanja vya Coco Beach

  Akizungumza katika uzinduzi huo uliopambwa na burudani mbalimbali ikiwemo Yamoto bendi katika viwanja vya Coco beach jijini Dar es salaam meneja uhusiano wa airtel bw. jackson mmbando amesema kila mtanzania anayo nafasi ya kushiriki katika shindano hilo kwa kupiga simu namba 0901002233.

  Aidha Mmbando ameongeza kuwa lengo la kuanzisha shindano hilo ni kuinua vipaji vya watanzania wenye kujua kuimba ili wapate nafasi ya kuwa staa wa kimataifa.

  Nae balozi wa shindano hilo Ommy Dimpoz amewaomba watanzania kujitokeze kwa wingi katika kushiriki mashindano hayo ambapo mshindi atajinyakulia zawadi kabambe ikiwemo kurekodi na kusambaziwa nyimbo zake chini ya studio kubwa ulimwenguni pamoja na safari ya kwenda nchini marekani kwa ajili ya kupata mafunzo ya kimuziki na nguli wa muziki wa amerika Akon.
  Wasanii wa kundi la yamoto band wakiwa na msanii maarufu nchini ambae pia ni balazo wa airtel trace music stars tanzania Ommy Dimpos wakionyesha namba maalum itakayotumika kupiga na kutuma nyimbo kwa wasanii chipukizi kwenye shindano la airtel trace music stars lililozinduliwa rasmi jana.
  Meneja uhusiano wa airtel Jackson Mmbando akizindua na kutangaza rasmi namba itakayowawezesha watanzania kushiriki mashindano ya kusaka vipaji ya muziki ya airtel trace music star kwa kukerekodi na kutuma nyimbo zao kwa kutumia simu zao za mkononi jana coco beach.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0
 • 10/09/14--08:33: UJUMBE MARIDHAWA


 • 0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeo (CHADEMA) - Zanzibar,Bw. Salumu Mwalimu (kulia) akikabidhiwa vifaa vya ofisi kutoka kwa mtangulizi wake,Bw. Hamad Yusuf (kushoto) wakati wa hafla ya kumkaribisha iliyofanyika kwenye ofisi za chama hicho Daraja bovu mjini,Zanzibar jana.Katikati ni Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa.
  Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeo (CHADEMA) - Zanzibar,Bw. Salumu Mwalimu akiongea kwenye mkutano wa ndani baada ya kuwasili kwenye ofisi za chama hicho Daraja bovu mjini Zanzibar jana.
  Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa akiongea na wanachama na viongozi wa Chadema jana
  Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeo (CHADEMA) - Zanzibar,Bw. Salumu Mwalimu akipokewa na viongozi wa chama hicho baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Zanzibar akifuatana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk.Wilbrod Slaa (kulia) na viongozi wengine wa chama hicho jana.
  Sehemu ya Wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeo (CHADEMA) wakiwa kwenye mapokezi ya Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Salumu Mwalimu baada ya kuwasili kwenye ofisi hiyo Darajabovu mjini Zanzibar jana.
  Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa akiteta jambo na Manaibu wake,Mh. John Mnyika - Bara (kushoto) na Salumu Mwalimu - Zanzibar (kulia) kwenye mkutano na wanachama na viongozi wa chama hicho jana.
  Wanachama na wapenzi wa Chadema wakimsikiliza Dk.Slaa alipozungumza nao kwenye ofisi za chama hicho huko Darajabovu mjini Zanzibar jana.

older | 1 | .... | 600 | 601 | (Page 602) | 603 | 604 | .... | 3283 | newer