Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 599 | 600 | (Page 601) | 602 | 603 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Rising Tanzania rap artist G Fullah passed away October 5th 2014, 8 days before the scheduled October 13th release of this track. RIP G Fullah. | Msanii chipukizi wa hip hop G Fulllah alifariki tarehe 5 Octoba 2014, siku 8 kabla ya tarehe iliyopangwa kuachiwa kwa singo Octoba 13. RIP G Fullah.

  0 0
 • 10/07/14--15:35: DR WILLIAM SHIJA R.I.P
 • I am saddened by   the untimely  death  of  Dr  William  Shija  , Baba, a  friend and  above  all  a  diplomat.I  had  known  Dr  William  Shija. 
  Since  his  appointment  as  the  secretary  General in  London, by  then I  was   a sitting  journalist  covering   the  British  houses  of  Parliament and  the  West  Minister  Village,  clicked instantly  and  I had the honour to being   the  first  journalist  to  interview  him  since  he was  the  The  first  ethnic  Minority  person  to  hold  that  post 
  .That caused  a  buzz  around  Westminster  and  in  the  corridors  of  power  in  the  Commonwealth  fraternity.
  We  became  good  friends  and  through  his  esteemed  office  I  was  able  to  learn  more  about  the  inner  working of  the  Commonwealth.
  He  invited  me  to  several  meetings  and  conferences  and  the  most  memorable  part  was  when  he  invited  me  to  accompany  him  to  meet  Her Majesty the  Queen.
  For  us  who  knew him Dr Shija served the Commonwealth Parliamentary Association with commitment, and with an enduring enthusiasm for its potential always to do more for its members and for the citizens of the Commonwealth at the grassroots level whom parliamentarians represent.
   I personally as  a  journalist, had a very fruitful , rewarding and collaborative partnership with Dr William and  his office in strengthening the work of Commonwealth parliaments. I recall our common endeavor in serving the citizens of the Commonwealth with warmth and gratitude through  journalism. And  I  also  remember  that  every  time  he  called  me,  he had  fresh  ground  nuts  from  Tanzania. 
  Rest  in  Peace  Baba, you  have  left  the  commonwealth  fraternity  a  better place  than  you  found  it.

  Tearfully yours,
  Ayoub Mzee

  0 0  Habari Ankal Michuzi,

  Bila shaka wewe ni bukheri wa afya. Nakupongeza kwa kazi adhimu ya kulihabarisha taifa. Basi na mimi bila kusita naomba kupitia kwenye globu hii maarufu ya jamii nipate kuwahabarisha watanzania wote wanaopenda maisha juu ya libeneke jipya la maakuli.

  Nina furaha na shauku kubwa ya kuwaambia watanzania wenzangu kuwa tunawaletea libeneke jipya la Misosi – Ladha ya Maisha. 
  Libeneke la http://www.misosi.co.tz/home ni maalumu kwa kupata habari za mapishi pamoja na kutafuta huduma za kijamii karibu nawe – mfano kujua sehemu za kula au maduka ya bidhaa za nyumbani karibu na ulipo.

  Lengo kubwa la tovuti hii ya Misosi ni kuchangia na kubadilishana ujuzi kuhusu mambo ya maisha ya kila siku, hasa kuhusu afya ya familia. Tunaamini kila kitu kina jibu, na penye wengi hakukosi mafanikio, jumuika nasi kwenye misosi.co.tz ili tupate kupata ufumbuzi wa maisha kwa urahisi.

  Ni wazi kuwa katika pilika zetu za maisha ya kila siku huwa tunakosa muda wa kupanga ratiba nzuri za kujua tunafurahiaje maisha baada ya kazi. Mama akiwa nyumbani au kazini anakuwa na kazi ngumu ya kupanga mipango kuhusu maakuli na afya ya familia. Hii si kazi rahisi hata kidogo.

  Misosi imetambua kilio hicho na kutafuta njia mbadala ya kutatua tatizo na kuokoa muda wa mama kufanya maamuzi magumu ya nyumbani kwa kuweka uwanja mpana wa kuchagua kilicho bora na rahisi karibu yake. Kuzingatia hilo, mtandao wa Misosi unakidhi haja kwa kutoa majibu kwa maswali yote yanayohusu mapishi, afya, pamoja na mahitaji ya kila siku nyumbani kwa urahisi.

  Misosi haishii kwa mama tu nyumbani, bali ni suluhisho kwa kila mmoja wetu – baba na watoto. Kwa kuhakikisha hili, angalia kama utajibu ‘Ndiyo’ kwenye Kipengele chochote kati ya hivi vifuatavyo:

  1. Je unapenda kujifunza mapishi?

  Misosi inatoa nafasi ya kujifunza mapishi au kupata mawazo juu ya nini cha kuandaa kirahisi nyumbani. Misosi.co.tz tunaweka maelekezo rahisi ya kuandaa vyakula vya aina mbali mbali. Kama unapenda kubadilisha ladha ya mapishi, au unapenda kujifunza kuhusu mambo mapya, basi misosi ndio nyumbani kwako. Ukitaka kusoma mapishi au habari za blog ya Misosi ni bure, na hakuna masharti yeyote, tembelea tu http://www.misosi.co.tz/home.

  2. Je unapenda kuchangia ujuzi wako wa mapishi?

  Je wewe una ujuzi wa kuwafunza wengine? Misosi inakukaribisha kuchangia mawazo yako. Kama unaopenda kuchangia ujuzi wa mapishi mbalimbali, misosi inakupa nafasi ya kuweza kutimiza hilo. Unachohitaji ni kujisajili bila gharama yeyote na kuweka mapishi yako. Kujisajili ni rahisi sana na inachukua dakika 2 tu. Kila kitu kimerahisishwa kuhakikisha unafanya vitu kwa ufanisi na haraka. Kujisajili sasa bofya hapa.

  3. Je una biashara ya vyakula au bidhaa za nyumbani ?

  Misosi inakutanisha watu wa kila aina, na hasa wale wanaopenda kujua bidhaa nzuri zinapatikana wapi. Sasa, kama una biashara na unahitaji kuwafikia wateja wako kirahisi, basi misosi ndio mkombozi wako. Misosi inakupa nafasi ya kusajili biashara yako bila gharama yeyote. Lengo likiwa kutoa taarifa sahihi za upatikanaji wa huduma karibu na walaji. Ukitaka kusajili biashara yako bofya hapa.

  Kwanini ujisajili na Misosi.co.tz ?

  Kujiunga na misosi hakuna gharama yeyote. Na hizi ndio faida utakazipata ukijisajili nasi:

  ·         Unakuwa na uhuru wa kuweka mapishi bila kikomo

  ·         Unakuwa na uhuru wa kuweka biashara yako BURE na kuwafikia wateja kwa urahisi!

  ·         Unaweza kuchangia mada tofauti kuhusiana na misosi

  ·         Unaweza kuweka biashara yako na kufuatilia maoni ya wateja wako

  ·         Unaweza kutangaza matukio kama sherehe au mikutano bure kupitia tovuti

  ·         Unaweza kuweka habari kuhusiana na chakula, afya au biashara yako bure.

  ·         Unakuwa mmoja wa jumuiya ya watu wenye fikra chanya kama zako. Unapata kusikia mawazo chanya toka kwa watu wenye mtazamo unaofanana na wako. Vilevile mawazo yako yanapata kuwafikia wale walengwa wako kwa urahisi zaidi na wakati muafaka.


  Karibuni sana kwenye libeneke la misosi. Karibuni sana tujirambe na ladha ya maisha.
  – Misosi Team


  0 0

  Awali ya yote nianze kwa kumshukuru mwenyezi mungu, mwingi wa rehema na mwenye kurehemu, kwa kutujalia afya njema na kutukutanisha hapa siku hii adhimu ya leo, maana ni kwa utashi wake tu tunaweza kuyafanya haya yote.


  Nitumie fursa hii kwa namna ya kipekee kuwashukuru nyote kwa kuacha shughuli zenu kuja kunipokea na kushiriki mkutano huu. Mmenipa heshima kubwa sana na mimi nawajibika tu kusema ‘ahsanteni sana’.


  Mimi hapa ni aidha mtoto wenu, mjukuu wenu ama mdogo wenu, mnapoacha shughuli zenu kuja kunisikiliza mimi, mnakuwa mmenitwisha mzigo mzito sana. Ninajiona nawajibika kwenu kutoa utumishi uliotukuka. Ninajipa deni la kuongeza bidii kubuni miradi itakayotatua shida zetu hapa Nzega, kupigana kuondoa umaskini, ujinga na maradhi.

  Sote tuliopo hapa ni mashahidi, kuwa tumefanya mengi katika miaka hii minne ya uwakilishi wangu, maana kati ya hayo, mengi tumefanya pamoja nanyi. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  DSC_0120
   Mwalikishi wa Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ambaye pia ni mshauri na mkufunzi wa redio jamii, Bi. Rose Haji Mwalimu akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues kwenye sherehe za uzinduzi wa kituo hicho cha redio jamii Uvinza FM uliofanyika wilayani Uvinza mkoani Kigoma.
  Kutoka kushoto ni Meneja wa huduma za kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi, Mkurugenzi Mtendaji wa Uvinza FM Radio Bi. Nuru Kalufya, Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya na Mkuu wa Wilaya  ya Uvinza Mwalimu Hadijah Nyembo. 

  0 0
 • 10/07/14--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Nuhu Mziwanda - Msondo Ngoma

  0 0

  Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF umeanza  hatua ya kutambua kaya maskini katika mikoa ya Mwanza,Shinyanga,Tanga, Morogoro,Pwani na Simiyu ikiwa ni utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya maskini PSSN unaoratibiwa na mfuko huo nchini kote kwa awamu. Akifungua warsha ya kuwajengea uelewa viongozi wa wilaya ya Maswa ,Mkuu wa wilaya hiyo Luteni Mstaafu Abdallah Kihato ametoa wito kwa wananchi kuzingatia miongozo ya TASAF ili waweze kunufaika na mpango huo. 

  Amesema serikali wilayani humo itatoa ushirikiano kwa wataalamu wa TASAF na watendaji wengine ili zoezi la kuzibaini kaya maskini liweze kufanikiwa. Kwa upande wake meneja fedha wa TASAF Bw. Njego Nyamukowa kwa niaba ya mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga amesema utekelezaji wa mpango huo unafanyika kwa mafanikio makubwa .
   Mtaalam kutoka TASAF Bw. Hamis Kikweppe akitoa maelezo juu ya Mpango wa kunusuru kaya maskini wakati wa warsha ya kujenga uelewa kwa timu ya wawezeshajio wa wilaya ya Maswa mkoani Simiyu. (2)
   Meneja wa Fedha wa TASAF Bw.Njego Nyamuko aliyeshika kipaza sauti mbele akitoa maelezo juu ya Mpango wa kunusuru kaya maskini unaoendeshwa na TASAF katika warsha ya kuwajengea uelewa viongozi wa wilaya ya Maswa.

   Mkuu  wa wilaya ya Maswa Luteni Mstaafu Abdallah Kihato akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya kujengewa uwezo juu ya mpango wa kunusuru kaya maskini katika wilaya ya Maswa.

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsifia Mbunge wa Jimbo la Isimani,  William Lukuvi kwa uchapakazi wake mzuri wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Magozi, Kata ya Ilolo Mpya, Iringa Vijini leo. Kinana alimjia juu Waziri wa Maliasili na Utalii, Nyalandu kwa kushindwa kutafutia ufumbuzi migogoro ya wananchi.Pia aliwataka wananchi kuacha kukwepa majukumu yao ya kuwatumikia Wananchi. 
   Katibu wa Itikadi na Uenezi wa  CCM, Nape Nauye akihutubia katika mkutano huo
   Kinana akisalimiana na wananchi alipowasili kushiriki ujenzi wa jengo la CCM tawi la Luganga Kata ya Ilolo Mpya.
   Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Kinana na Mbunge wa Jimbo la Isimani, William Lukuvi wakishiriki kufyatua tofali za ujenzi wa jengo la Ofisi ya CC,
   Kinana na Lukuvi wakisaidia kufyatua tofali za kujengea jengo hilo la CCM.

  0 0

  UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga umesema utakwenda mahakamani kuishtaki Kampuni ya Binsul Tyre kutokana na kitendo cha kutengeneza tisheti za Coastal Union zenye nembo ya kampuni Sound na kuwapa bure mashabiki kuingiza nazo kwenye mechi mbalimbali za ligi kuu Tanzania bara wakiwa wamelipiwa na viingilo vya mchezo husika.

  Hali hiyo ni kinyume na utaratibu kutokana na kuwa tayari kampuni hiyo ilishajitoka kufadhili timu hiyo na tayari klabu ya Coastal Union ilikwishapata mfadhili mwengine ambayo ni kiwanda cha Kutengeneza Unga Ngano mkoani Tanga cha Pembe Flours Mills.

  Kauli hiyo imetolewa kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji Kilichoketi mwishoni mwa wiki ambapo kilikuwa na agenda nne za msingi ambazo ni Suala la mshambuliaji wa Coastal Union Danny Lyanga,Utoaji slipi benki,Jezi za Sound,Tarehe ya Uchaguzi.

  Kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi wa mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union,Steven Mguto,Katibu Mkuu Kassim El Siagi,Mjumbe wa Kamati ya Utendaji,Albert Peter Saimu Amiri na Meneja wa Coastal Union Akida Machai.

  Kama unavyojua kuwa Kampuni ya Binslum Tyres ilikuwa mhisani wetu na sasa hatuko naye na tayari alishapeleka fedha zake kwenye vilabu vingine ikiwemo Mbeya City sasa tunamshangaa kuendelea kufanya biashara ya matangazo kupitia mashabiki wetu kwa kuwapa tisheti za kuvaa bure ikiwemo kuwalipia viingilio kwenye mechi za ligi kuu zinazochezwa Mkwakwani.

  Hivyo kutokana na suala hilo tayari uongozi wa Coastal Union umeshamkamata mshabiki mmoja ambaye ni wakala wa kusambaza tisheti hizo kwa mashabiki na kumpeleka polisi na taratibu za kisheria zinaendelea ili kuweza kukomesha vitendo hivyo ambavyo sio vya kiungwana.

  Tayari Kampuni ya Pembe Flours Mills ilishasaini mkataba na Klabu ya Coastal Union wa kuifadhili timu ya Coastal Union kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo tayari makubaliano hayo yameshaanza kutekelezwa

  Hata hiyo kikao hicho kilipendekeza tarehe ya kufanyika uchaguzi mdogo wa kama ilivyo maagizo ya shirikisho la soka nchini (TFF) kuitaka kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi zilizokuwa wazi kwenye safu ya uongozi wa Klabu hiyo.

  Kamati hiyo imependekeza kuwa uchaguzi huo ufanyika Novemba 23 mwaka huu mkoani Tanga.

  Ambapo kimsingi uchaguzi huo unafanyika ili kuweza kuziba nafasi zilizokuwa wazi ambayo ni Mwenyekiti na wajumbe wawili wa kamati ya utendaji.

  Hata hiyo alisema kuwa wanatarajia kuunda kamati ya uchaguzi ambayo itasimamia uchaguzi huo ili kuweza kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika.

  0 0


  0 0  Na Mwene Said,Globu ya Jamii

  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu,jijini Dar es Salaam, jana iliamuru mashindano ya urembo Tanzania yaliyopangwa kufanyika Oktoba 11, mwaka huu kuendelea baada ya kutupilia mbali maombi ya dharura yaliyowasilishwa na Prashant Patel dhidi ya Hashimu Lundenga ya kuzuia kuendelea kuendesha kinyang'anyiro hicho kwa madai ya kukiuka mkataba wa makubaliano yao.

  Kadhalika mahakama hiyo imesema maombi ya hati ya dharura yaliyowasilishwa na Patel hayana mashiko ya kisheria na kwamba kuzuia kufanyika mashindano hayo ambayo wadhamini mbalimbali wamewekeza fedha zao itasababisha mgangano wa kimaslahi.

  Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi Frank Moshi  baada ya kusikiliza hoja za mawakili wa pande zote mbili kuhusu maombi hayo ya dharura ya kuzuia mashindano hayo kufanyika Oktoba 11, mwaka huu.

  Hakimu Moshi alisema mlalamikaji amefungua kesi mahakamani hapo pamoja na maombi ya hati ya dharura akiitaka mahakama yake kuzuia mashindano kufanyika kutokana na mlalamikiwa kuvunja haki dhidi ya mwanzilishi mwenzake Patel.

  Alisema Patel kupitia hoja za maombi yake, amedai kuwa Lundenga alivunja mkataba huo kwa kufanya mawasiliano moja kwa moja na mawakala bila kumshirikisha.

  Hata hivyo, mahakama bila kuacha shaka imeona hakuna sababu za msingi katika hati hiyo ya kusababisha mashindano hayo yasifanyike na kwamba hayawezi kuathiri kesi ya msingi iliyofunguliwa na mlalamikaji huyo.

  “Mahakama imeona hakuna sababu ya kuzuia mashindano hayo kwa sababu wadhamini na washiriki wametumia gharama zao na kwamba kwa kufanya hivyo kutasababisha mgongano wa kimaslahi” alisema Hakimu Moshi wakati akitupilia mbali hati hiyo ya dharula.

  Akifafanua zaidi alisema hati ya dharura ya mlalamikaji haina mashiko kisheria kwa sababu kesi yake ya msingi ipo mahakamani na kwamba haina uhusiano na mashindano yatakayofanyika Oktoba 11, mwaka huu.

  Mapema juzi, mahakama hiyo ilitupilia mbali pingamizi la awali la Lundenga lililotaka hati hiyo ya dharura kutupilia mbali.

  0 0


  Aga Khan Hospital, Dar es Salaam will offer free clinical breast examination and breast health education on Saturday, October 11th from 9.00 a.m. to 2:00 p.m.

  Early Screening helps detect cancers in people who have no symptoms. This is when it's most treatable.

  This Saturday, to mark the Breast Cancer Awareness month, Aga Khan Hospital, will offer free breast exams, free ultrasound screening and health education. 

  The forum will also provide current information on breast cancer treatment as well as an opportunity to interact with a panel of Aga Khan Hospital’s specialists.

  You are all encouraged to attend.

  0 0

  Jumamosi ya tarehe 4 Mwezi wa Oktoba 2014,wakazi wa ukonga walipata fursa ya kupagaishwa na burudani ya mziki mnene inayoandaliwa na kituo cha redio cha EFM kwenye ukumbi wa Ukonga Reaction Centre.

  Idadi ya watu wasio hesabika walijitokeza kwa wingi ndani ukumbi huo. Tuliongea na mmoja wa waandaji wa tamasha hili Dickson Ponella,ambae alisema kuwa mziki mnene utazunguka Dar Es Salaam nzima na viunga vyake,kama ratiba inavyo elekeza.

  “Haina haja ya watu kugombania kuingia ndani,wakumbuke tamasha hili halina kiingilio,ni kwa watu wote.Tunashukuru kuona baadhi ya watu walio safari kutoka mikoa ya karibu kama vile Morogoro,Tanga na Mtwara kuja kutushika mkono”,alisema.

  Kwa upande mwingine meneja uhusiano wa EFM Kanky Mwaigomole,alisema kuwa wasikilizaji wote waendelee kusikiliza matangazo yao ili wajue watakuwa wapi na lini.
  “Kwakila tamasha hili tuna kipengele kiitwacho kibunda.Huwa tunawaita watu angalau watatu,na tunawauliza maswali kumi ndani ya dakika moja na mshindi hupewa zawadi mbali mbali,ikiwemo pesa taslimu”,alisema Mwaigomole.

  Meneja uhusiano huyo aliendelea na kusema kuwa tamasha hilo la muziki mnene litaendelea tena jumamosi ya tarehe 11 mwezi huu wa Oktoba mwaka 2014,huko Kigamboni Navy Beach,Dar es Salaam.

  0 0

  Na Happiness Shayo,Morogoro

  Timu za kamba za Ikulu, Hazina na Mahakama zimeingia hatua ya nusu fainali kwa kishindo baada ya kuzivuta timu pinzani katika michezo ya SHIMIWI iliyofanyika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro leo.

  Michezo hiyo ya kusisimua iliyovuta mashabiki wengi ilianza majira ya saa moja asubuhi ambapo timu ya kamba ya wanawake ya Ikulu iliivuta timu ya kamba ya wanawake ya Kilimo na kuibuka mshindi kwa kuvuta mivuto yote miwili.

  Mchezo wa pili ulikuwa kati ya timu ya kamba ya wanawake ya Wizara ya Ujenzi na timu ya kamba ya wanawake ya Wizara ya Uchukuzi zilizolazimishana kutoka droo kwa michezo miwili ya kwanza na hatimaye Uchukuzi kuibuka mshindi kwa mvuto mmoja baada ya kuvutana kwa mara ya tatu.

  Katika mchezo mwingine timu ya kamba ya wanawake ya Wizara ya Mambo ya Ndani ililazimishana droo na timu ya wanawake ya RAS Iringa na kulazimu waamuzi kurudia mchezo huo na hatimaye RAS Iringa kuibuka mshindi kwa kuwa na pointi 1-0.

  Mchezo mwingine ulichezwa kati ya timu ya kamba ya wanawake ya TAMISEMI ikiivuta timu ya wanawake ya Mahakama kwa mvuto mmoja.

  Kwa upande wa timu za kamba za wanaume,Ikulu iliibuka mshindi baada ya kuivuta timu ya NFRA huku Uchukuzi ikiibuka mshindi baada ya kuivuta timu ya Afya kwa mivuto yote miwili.

  Timu nyingine zilizoingia dimbani kwa upande wa timu za wanaume ni timu ya kamba ya Mahakama iliyoivuta timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani na kuibuka na pointi 2 huku timu ya kamba ya Hazina ikiivuta timu ya kamba ya Maliasili na kuibuka na pointi 2.

  Timu za kamba kwa wanawake na wanaume leo zimetoana katika hatua ya robo fainali ambapo washindi wataingia nusu fainali itakayochezwa hapo kesho.
  Kamati ya Waamuzi wa mchezo wa kuvuta kamba ikisubiri kumkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (hayupo pichani) aliyetembelea viwanja vya Jamhuri,Morogoro mapema leo kushuhudia michezo ya kuvuta kamba.
  Mwamuzi wa mchezo wa kamba Bw.Ruvu Kiwanga (kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil alipotembelea viwanja vya Jamhuri, Morogoro mapema leo.


  0 0

  Na. Aron Msigwa-MAELEZO.

  Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Septemba 2014 umepungua hadi kufikia asilimia 6.6 kutoka asilimia 6.7 iliyokuwepo mwezi Agosti kutokana na kupungua kwa bei ya bidhaa na huduma katika maeneo mbalimbali nchini.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Ephraim Kwesigabo amesema kuwa bidhaa za vyakula zikiwemo mchele, mahindi, ulezi, matunda, Sukari na vinywaji baridi zimechangia kupungua kwa mfumuko wa bei nchini Bidhaa nyingine zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei nchini ni Sare za shule, Simu za mkononi, runinga na viatu huku akibainisha kuwa Fahirisi za bei kwa maana ya kipimo kinachotumika kupima mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zinazotumiwa na kaya nchini zimeongeka na kufikia 149.93 kwa mwezi Septemba 2014 ikilinganishwa na 140.61 za mwezi Septemba mwaka jana.

  Kwa upande wa mfumuko wa bei unaopimwa kwa kipimo cha mwezi ameeleza kuwa umeongezeka kwa asilimia 0.4 kwa mwezi Septemba 2014 ikilinganishwa na asilimia 0.1 za mwezi Agosti kutokana na kuongezeka kwa Fahirisi ya baadhi ya bidhaa zikiwemo samaki, matunda, mbogamboga, mihogo na vinywaji baridi, mkaa, mazulia na dawa za Binadamu kuwa na mchango mkubwa katika ongezeko la fahirisi.

  Aidha, amesema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula nyumbani na migahawani umepungua hadi asilimia 8.3 mwezi Septemba 2014 kutoka asilimia 8.5 za mwezi Agosti 2014 na kuongeza kuwa uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma za jamii kwa mwezi Septemba, 2014 umefikia shilingi 66 na senti 70.

  Kwa upande wa mfumuko wa bei wa Tanzania na baadhi ya nchi za Afrika Mashariki Bw. Kwesigabo amesema kuwa una mwelekeo unaofanana, Kenya ukipungua na kufikia asilimia 6.6 mwezi Septemba kutoka 8.34 za mwezi Agosti huku Uganda ikiwa na mfumuko wa bei wa asilimia 1.4 mwezi Septemba kutoka asilimia 2.8 za mwezi Agosti.
  Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akitoa taarifa ya mfumuko wa bei nchini kwa mwezi Septemba, 2014 leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Meneja wa Takwimu za Ajira na Bei wa Ofisi hiyo Bi. Ruth Minja.

  0 0
 • 10/08/14--08:51: Ndumbaro kikaangoni TFF
 • NA RIPOTA WA GLOBU YA JAMII

  MWANASHERIA, Damas Ndumbaro ameingia kikaangoni baada ya kuitwa kwenye kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili kujibu tuhuma alizozitoa wiki iliyopita.

  Barua hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa imemtaka Ndumbaro kufika kwenye ofisi TFF zilizopo jengo la PPF Tower leo saa 8:00 mchana kujadili masuala mbalimbali ikiwemo tuhuma alizozitoa kwenye vyombo vya habari hivi karibuni.

  Ndumbalo ambaye ni mwanasheria wa klabu za Ligi Kuu wiki ilitoa tamko kwa niaba ya wateja wake kuhusiana na makato ya asilimia tano ya wadhamini wa Ligi Kuu Tanzania Vodacom na Azam Media.

  Kwa upande wake Ndumbaro alisema TFF ya sasa inamfanya kushuhudia maajabu makubw amabyo hayajawahi kutokea Duniani ya Wakili kushitakiwa kwa kosa la kumtetea mteja wake.
  “Hii ni mara ya kwanza katika historia ya dunia hii Wakili anashitakiwa kwa kuwatetea wateja wake. Kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni,” alisema Ndumbaro.

  Aliendelea kufafanua kuwa uwakili ni kazi yake na ataendelea kutetea vilabu kwa nguvu zote mpaka haki sio tu itendeke bali ionekane kuwa inatendeka.

  Hata hiyo aliitaka TFF kuanisha makosa yake kwa uwazi nasi kumuita tu bila kujua anakwenda kujibu nini na aliwata kusogeza mbele kikao hicho hadi Novemba atakapotejea nchini kwa kuwa hivi sasa anakwenda nchini Marekani kwa safari ya kikazi.

  0 0

   Mbunge wa Kilolo Profesa Msola akieleza alivyosimamia utekelezaji wa ilani ya CCM katika jimbo hilo kwenye mkutano huo
   Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Utengule kwa tiketi ya Chadema, Parcras  Mkakatu akimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati wa mkutano kwenye zahanati ya Kijiji hicho
   Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Utengule (Chadema), Parcras  Mkakatu akieleza utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika kijiji cha Utengule kwa Kinana wakati wa mkutano kwenye zahanati ya Kijiji hicho
   Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Utengule (Chadema), Parcras  Mkakatu akiendelea kueleza kwa Kinana shughuli mbalimbali za maendeleo wakati wa mkutano kwenye zahanati ya Kijiji hicho
   Wazee wa Kihehe wakimpamba Kinana kwa mavazi rasmi ya keshima ya kabila hilo katika kijiji cha  Utengule, baada ya kuhutubia wananchi kwenyeviwanja vya zahanati ya Kijiji hicho.

  0 0

  Kila mwaka Bodi ya Magavana ya Shirika la Fedha la Kimataifa na kundi la Benki ya Dunia hukutana kwa ajili ya kujadili kazi za Taasisi zinazowahusu. Mikutano hii imeanza tarehe 06 Octoba na itafikia kilele chake hapo tarehe 13, mwezi Octoba, 2014.
  Mikutano hii hufanyika mjini Washington DC kwa miaka miwili mfululizo na kwa mwaka wa tatu hufanyika kwa nchi mwanachama. 
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile ndiye kiongozi wa ujumbe kutoka Tanzania na yeye anawakilisha kama Gavana mbadala (Alternate Governor) pamoja na Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu ambaye pia ni Gavana katika mikutano hii. 
   Mikutano hii inatoa nafasi ya kuweza kujadiliana na Benki ya Dunia pamoja na Shirika la Fedha la Kimataifa kuhusiana na hali ya uchumi kwa maana ya sera za fedha na sera za mapato na matumizi. Nia yao kubwa ni kutaka kusikia mawazo yetu kuhusu jinsi ya kuboresha uchumi ili wawe katika nafasi nzuri ya kuangalia ni wapi wanaweza kutusaidia kuboresha na kuona kwamba nchi yetu inaendelea kufanya vizuri zaidi. 
  Maeneo ambayo yameshajadiliwa ni pamoja sera kuhusu kiasi cha ubadilishaji fedha, mapato ya nchi kwa ujumla na mwendo wa matumizi ya fedha. Hali ya utendaji wa kiuchumi na hali ya matumizi na mapato ya fedha ya Tanzania imeonekana ni ya kuridhisha japo pado kunachangamoto ya ajira. 
   Imetolewa na: 
  Ingiahedi Mduma 
  Msemaji -Wizara ya Fedha 
  Washington D.C 
  7/10/2014
   Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa serikali  akiwa pamoja na ujumbe kutoka Tanzania. Kutoka kushoto ni Kamishna wa Bajeti Bw. John Cheyo akifuatiwa na Bi.Mwanaidi  Mtanda ambaye ni mhasibu mkuu wa Serikali na wa mwisho kutoka kulia ni Balozi Liberata Mulamula.
   Bw.Herve’ Joly ambaye ni Mkurugenzi msaidizi na Mkuu wa idara ya Afrika sehemu ya Mashariki akishauriana na mwenzake baada ya kupokea hoja kutoka kwa Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali.
   Balozi wa Tanzania nchini Marekani – Washington Mhe.Liberata Mulamula pamoja na Serikali Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  wakifurahia pongezi walizopewa na ujumbe wa IMF kuhusu muelekeo mzuri wa uchumi wa Tanzania.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile akielezea mikakati ya nchi ya Tanzania katika kuinua uchumi na kuongeza pato la Taifa kwenye Mkutano uliofanyika leo juu yuliohusu  masuala na fedha na sera ya kiwango cha ubalilishaji fedha.

  0 0

  Timu kongwe visiwani Zanzibar Jamhuri ya Wete Pemba iliyoanzishwa mwaka 1954 imepokea vifaa mbali mbali vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 8 kutoka kwa Bw.Suleiman Saleh ambaye alimkabidhi mdaada huo mjini Wete Pemba jioni ya Jumanne Oktoba 7 2014 katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa shule ya Sekondari ya Utaani iliyopo Wete Pemba.
  Bw.Saleh ambaye ni Afisa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Washington DC alikabidhi vifaa mbali mbali vikiwemo viatu, mipira, nyavu za magoli na vifaa mbali mbali vya mazoezi ili kuihamasisha timu hiyo ambayo mwaka 2003 walikuwa mabingwa Zanzibar na miaka ya 2008 na 2011 ilishiriki katika klabu bingwa Afrika ambapo ilitolewa na St.George ya Ethiopia na Hangwe FC ya Zimbabwe.

  Bw. Suleiman Saleh ambaye akikabidhi msaada huo mjini Wete, Pemba,  jioni ya Jumanne Oktoba 7 2014 katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa shule ya Sekondari ya Utaani iliyopo Wete Pemba. 
  Katika kujiwekea malengo ya kucheza tena kimataifa katika miaka mitatu ijayo Jamhuri inayoundwa na vijana wadogo imeandaa mkakati maalum kukamilisha azma yao hiyo.

  0 0

  Courtesy of KTN Kenya

older | 1 | .... | 599 | 600 | (Page 601) | 602 | 603 | .... | 3272 | newer