Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 598 | 599 | (Page 600) | 601 | 602 | .... | 3272 | newer

  0 0
 • 10/06/14--22:41: OMG!


 • 0 0

  Kali TV was invited to Jakaya Kikwete night in Washington DC two weeks ago. The night which mainly was focusing on honoring President Jakaya Mrisho Kikwete of Tanzania was organized by CCM political party USA branches. Take a look at some of the highlights.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Hussein Mwinyi, kuomboleza kifo cha Meja Jenerali Muhidin Kimario, Waziri Mwandamizi wa Zamani wa Serikali na Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TPDF).

  Aidha, Rais Kikwete amewatumia pole nyingi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Jenerali Davis Mwamunyange na familia ya Meja Jenerali Kimario kufuatia kifo hicho kilichotokea mchana wa leo, Jumatatu, Oktoba 6, 2014, nchini India, ambako alikuwa anapata matibabu.

  Amesema Rais Kikwete katika salamu hizo kwa Waziri Mwinyi: “Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Meja Jenerali Muhidin Kimario, ambaye alilitumikia Jeshi letu kwa heshima kubwa na weledi wa kuigwa na baadaye kulitumikia Taifa letu kwa uaminifu na uadilifu wa kujivunia katika nafasi ya uwaziri.”

  Ameongeza Rais Kikwete katika rambirambi zake: “Uhodari na ujasiri ule ule ambao Meja Jenerali Kimario aliuonyesha akiwa askari na ofisa mkuu ndio ule ule uliomwongoza katika utumishi wa umma na kwa nafasi zote za waziri mwandamizi, ambazo alizishikilia katika maisha yake iwe ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mkuu wa Mkoa ama Mkurugenzi wa Ustawishaji wa Makao Makuu (CDA). Daima tutakosa uongozi na ushauri wake.”

  “Nakutumia wewe Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa salamu za dhati ya moyo wangu kuomboleza kifo hiki. Aidha, kupitia kwako, namtumia pole nyingi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange na Jeshi letu lote kwa kuondokewa na ofisa mwenzao, kiongozi wao na mpiganaji mwenzao,”amesema Rais Kikwete na kuongeza:

  “Aidha, kupitia kwako, natuma salamu zenye huzuni nyingi kwa familia ya Meja Jenerali Muhidin Kimario. Wajulishe kuwa niko nao katika msiba huu mkubwa wa kuondokewa na mhimili wa familia. Vile vile wajulishe kuwa naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke peponi roho ya Marehemu. Amin.”


  Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameelezea huzuni na masikitiko yake kuomboleza kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi za Jumuia ya Madola (CPA), Mheshimiwa Dkt. William Shija.
  Dkt. Shija aliyefariki dunia Jumamosi asubuhi mjini London, Uingereza, ambacho ndicho kilikuwa kituo chake cha kazi, alisomea na kuwa mhadhiri wa uandishi wa habari kabla ya kuwa mbunge wa Sengerema kwa miaka 15 mfululizo na Waziri Mwandamizi wa Serikali katika Wizara mbali mbali.

  Katika salamu zake kwa Sekretarieti ya CPA, Kanda ya Afrika, Rais Kikwete amesema kuwa amestushwa sana na kifo cha Dkt. Shija ambacho kimeinyang’anya Afrika na dunia, na hasa Tanzania na Jumuia ya Madola, mtumishi mwadilifu na mwaminifu, ambaye alitoa maisha yake kwa utumishi wa umma.

  “Alikuwa kiongozi mfano katika nafasi zote za umma alizozishikilia. Aliifanya kazi yake ya uhadhiri wa uandishi wa habari kwa ufanisi mkubwa na aliwapa utumishi uliotukuka wananchi wake wa Sengerema katika nafasi yake ya Ubunge. Dkt. Shija alitumainiwa sana katika nafasi zote nyingi na za uandamizi za Uwaziri wa serikali,” amesema rais Kikwete na kuongeza:

  “Nawatumieni salamu za dhati ya moyo wangu kuomboleza kifo cha Dkt. Shija na naungana nanyi katika kumlilia. Kupitia kwenu, nawatumia wajumbe wote wa CPA na Sekretarieti ya Chama hicho pole nyingi sana kwa kuondokewa na kiongozi na mtendaji wao mkuu. Aidha, naomba pia mniwasilishie pole zangu kwa wana-Sengerema ambao Dkt. Shija aliwatumikia kwa uaminifu na kwa miaka mingi.”

  “Wajulisheni wote kuwa niko nao katika msiba huu mkubwa na naomboleza nao na niko nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweka peponi roho ya Marehemu William Shija. Amin.”


  Imetolewa na;

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu – Dar es Salaam.

  6 Oktoba, 2014.

  0 0


  0 0

   Waziri Mkuu wa Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa amewanyooshea vidole viongozi wa kimila wa kabila la wamasai (malaigwanani),viongozi wa vijiji na wale wa CCM wilayani humo, kuwa wanalaumiwa kwa kushiriki katika uuzaji ardhi kinyume na sheria.

   Akifungua semina ya siku mbili ya juu ya maswala ya ardhi kwenye ukumbi wa hoteli ya Emanyata mjini Monduli,Mh. Lowassa amesema  shutuma hizo zimekuwa nyingi kwa viongozi hao kwa kuuza utajiri (ardhi) na kununua umasikini.

  "Walikuja pale nyumbani kwangu wale watu wa maombezi (walokole), moja ya mambo waliyoyalalamikia ni uuzwaji holela wa ardhi,wakaniambia hivi Mh. Mbunge hamuoni viongozi wa vijiji na wa CCM pamoja na malaigwanan wanavyopokea rushwa na kuuza ardhi?Wanavyowadhulumu wajane?" Alisema Lowassa na kuongeza kuwa kuna umuhimu wa kulijadili kwa kina suala hilo.

   Kutokana na hali hiyo Lowassa amewatahadharisha viongozi wa vijiji kuhakikisha wanaiondoa kero hiyo, kabla ya uchaguzi ujayo wa serikali za mitaa vinginevyo tatizo hilo litawagharimu.

   Aidha Lowassa ambaye ameshirikiana na mbunge wa Viti maalum (CCM),Namelok Sokoine ndiyo walioiandaa semina hiyo, amempongeza mbunge wa zamani wa Monduli hayati Edward Moringe Sokoine, kwa kufanikisha makubaliano kati ya wilaya na jeshi kuhusiana na matumizi ya ardhi.

   "Marehemu Sokoine alifanya jambo kubwa sana kwa kufikia makubaliano yale na faida yake kwetu sisi wana Monduli ni kubwa,kimejengwa hapa Chuo kikubwa cha kijeshi (TMA), na tulikubaliana tusilipwe fidia na jeshi ili tuwe na haki kwa mifugo yetu kuingia eneo lile,lakini kuna watu wameipeleka halmashauri mahakamani kupinga" alisema na kuonya kuwa" tutapambana kuhakikisha tunashinda! tumekuwa na mahusiano mazuri na jeshi na tunataka mahusiano hayo yaendelee".

   Naye mbunge wa viti maalum,Nameloki Sokoine alisema kuwa madhumuni ya kuandaa semina hiyo ni kutoa dira itakayofafanua nini kifanyike kuondoa tatizo hilo la uuzaji holela wa ardhi.

   Amesema mifugo na binadamu wamekuwa wakiongezeka lakini ardhi ni ile ile kwa hivyo bila ya kuwepo kwa dira na mipango thabiti hali itakuwa mbaya.
   Aidha alitoa changamoto kwa mbunge wa Monduli Mh. Lowassa kusaidia kupatikana kwa wawekezaji wa viwanda vya maziwa, ngozi na nyama wilayani Monduli.

   "Ningependa kumuomba Mh. Mbunge najua hili analiweza atusaidie watu wa Monduli tupate wawekezaji wa viwanda vya ngozi, maziwa na nyama,tukiwa na viwanda hivi itasaidia wafugaji kuachana na ufugaji wa kimila wa ng'ombe wengi an badala yake kuwa na ng'ombe wachache wa kisasa wenye tija" alisema Namelok na kushangiliwa.
  Waziri mkuu wa Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akihutubia wakati wa semina ya kwa wakazi wa Monduli juu ya maswala ya ardhi katika hoteli ya Emanyata,Wlayani humo.ambapo alisema kuuza ardhi ni sawa na kuuza utajiri na kununua umasikini.Wilaya ya Monduli ni moja kati ya wilaya zenye matatizo makubwa ya ardhi.
  Mbunge wa Monduli viti maalum,Namelok Sokoine akikabidhi sehemu ya baiskeli 100 alizotoa kwa watendaji wa Kata na kijiji wilayani humo,ili kuimarisha uhai wa Chama.Alikabidhi msaada huo wakati wa semina maalum juu ya ardhi wilayani Monduli.

  0 0

  KAMPUNI ya mawasilianao ya Vodacom Tanzania imezindua huduma mpya itakayowawezesha watumiaji wa mtandao wa kampuni hiyo kupata taarifa muhimu kuhusu afya kwa siku 30 mfululizo bila malipo. 

  Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo inayojulikana kama Simu Dokta, Dk. Meshack Shimwela ambaye ni Bingwa wa magonjwa ya binadamu (Physician), alisema upatikanaji 
  wa taarifa sahihi za kiafya ni moja kati ya hatua muhimu za kupambana na magonjwa mbalimbali.


  Dk. Shimwela alisema huduma hiyo itatoa mchango mkubwa katika kuuhabarisha umma juu ya masuala muhimu ya kiafya na kuongeza kuwa ujumbe wa mara kwa mara utawakumbusha watu na namna 
  ya kujikinga pamoja na kuchukua hatua sahihi juu ya magonjwa.


  Aidha Dk. Shimwela aliipongeza kampuni ya Vodacom kwa kuzindua huduma hiyo kwa ajili ya umma na kusema kuwa ‘’ Inaendana na malengo ya milenia hasa namba sita linalosisitiza kupambana na 
  magonjwa mbalimbali, akiwataka Watanzania kuitumia huduma hiyo ambayo ni muhimu kwa kila mtu’’.


  Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Masoko wa Vodacom Tanzania , Kelvin Twissa alisema taarifa hizo zitakuwa katika mfumo wa ujumbe mfupi wa maneno (sms) na mteja atakuwa 
  akizipata kila siku kupitia simu yake ya mkononi bure kwa mwezi baada ya kujisajili kwa kutuma neno DAKTARI kwenda 15542.


  ‘’Lengo la huduma hii ni kuchochea na kusaidia wananchi kujua mambo mbalimbali ya kiafya ambayo wamekuwa hawayajui au kuwa na taarifa zisizo sahihi, taarifa hizo zitakuwa zikiandaliwa na madaktari 
  bingwa nchini wa magonjwa mbalimbali ambao wamejitolea kuelimisha jamii, pamoja na kusaidia ustawi wa jamii kwa kuwa na jamii yenye uelewa mkubwa wa mambo ya afya na kusaidia kuokoa maisha ya 
  watu wengi,’’ alisema Twissa.


  Hii itakuwa ni huduma ya kwanza ya aina yake kutolewa na Vodacom ikiwahusisha madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali kwa kutoa taarifa kila siku za kuwasaidia kujiepusha na maradhi au kutoa 
  ahueni kwa magonjwa yanayowasumbua.


  Madaktari hao bingwa ni pamoja na Dk. Meshack Shimwela (Bingwa wa magonjwa ya mwili wa binadamu (Physician). Dk. Sulende Kobhoja (Bingwa wa watoto na moyo (Paediatricia & Cardiologist), Dk. 
  Munawara Kaguta (Bingwa magonjwa ya wanawake/wajawazito (OBST/Gynecologist).

  Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Masoko wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa akisisitiza jambo kwa wanahabari (hawapo pichani). Kulia ni Dk. Sulende Kubhoja.
  Bingwa wa magonjwa ya mwili wa binadamu, Dk. Meshack Shimwela akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani).


  0 0

  Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi DAVID MISIME  - SACP ameeleza kuwa kutokana na tukio la kihistoria ambalo litafanyika tarehe 08/10/2014 ambapo Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. JAKAYA MRISHO KIKWETE na Mh. Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dr. ALLY MOHAMED SHEIN watakabidhiwa Rasimu ya Katiba inayopendekezwa, ulinzi umeimarishwa katika maeneo yote ya Mkoa wa Dodoma hususani Dodoma Mjini.

  Kamanda MISIME amesema ufuatiliaji wa taarifa mbalimbali na kuzifanyia kazi umeimarishwa zaidi, doria za miguu, magari, pikipiki na mbwa na farasi nazo zimeimarishwa. Pia vyombo vyote vya dola tumeimarisha zaidi ushirikiano hasa kubadilishana taarifa mbalimbali na wote mitaani kufuatilia tukio hili muhimu kwa kutumia mbinu zote walizo nazo.

  Kamanda MISIME ameendelea kusema niwahakikishie wananchi wa Mkoa wa Dodoma na wageni wote kuwa ulinzi na usalama umeimarishwa tunachowaomba ni ushirikiano wao pale watakapomtilia mashaka mtu yeyote  au jambo lolote wajulishe Polisi haraka nao watalifanyia kazi. Vilevile wenye nyumba za kulala wageni waimarishe ulinzi kwenye maeneo yao ya biashara na kuwapa maelekezo sahihi wafanyakazi wao na wakitilia shaka mgeni yeyote watoe taarifa Polisi.

  Aidaha Kamanda MISIME amewataka wananchi wote pamoja na wageni wote watii sheria bila shuruti na yeyote anayepanga kukiuka sheria ili kuvunja amani na utulivu atashurutishwa kwa nguvu zote kwa mujibu wa sheria za nchi na kwa mamlaka waliyopewa  Jeshi la Polisi.

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzunduzi wa Mbio za Uhuru Marathon,uliofanyika leo kwenye hoteli ya Kebby's,Mwenge jijini Dar es Salaam.Mbio hizo ambazo zinaenda sambamba na Maadhimisho ya Uhuru wa Taifa letu la Tanzania,zitafanyika Desemba 7,2014 katika viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es salaam.Wengine pichani ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania,Bi. Ombeni Zavala (katikati) na kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Dar es salaam,B. Zaibab.
  Mratibu wa Mbio za Uhuru Marathon,Innocent Melleck akizungumzia maandalizi ya mbio hizo na namna ya washiriki waakavyoweza kujiandikisha,ambapo amesema kwa wale wanariadha ambao wako nje ya nchi wanaweza kujiandikisha kupitia tovuti rasmi wa mbio hizo,ambayo ni www.uhurumarathoni.com.Wengine pichani ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania,Bi. Ombeni Zavala.
  Baadhi ya wanahabari wakifatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa.Picha zote na Othman Michuzi.

  Na Daudi Manongi

    Chama cha Riadha Tanzania kimetakiwa  kuwajengea wachezaji fikra chanya na maandalizi bora  ili waweze kupata mafanikio katika mashindano ya Kimataifa na Kitaifa.

  Hayo yamebainishwa leo na Naibu katibu mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni  na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel alipokuwa akifungua Mbio za Riadha za Uhuru  zinazotarajiwa kuanza hivi karibuni jijini  Dar es Salaam.ambazo zitafikia kilele chake 7/12/2014  katika viwanja vya leaders mjini dar es salaam.

  Alisema michezo ya Riadha itumike kama daraja katika jamii kwa ujumla ili iweze kujenga mahusiano mema, kudumisha amani na kuenzi Muungano wetu.

  Alitoa rai kwa viongozi wa riadha Tanzania kusimamia vyema mchezo huo ikiwa ni pamoja na kutafuta vijana wenye vijana  ili kuweza kupata vijana bora ambao watashiriki karika mashindano mbalimbali ya ngazi tofauti yatakayofanyika nchini na nje ya nchi.

  Wakati huohuo  amewaasa  wadau,wafadhali na taasisi mbali mbali kuwa mstari wa mbele katika kuendeleza na kuchangia michezo mbalimbali ikiwemo kusaidia mafunzo na vifaa wakati wa mashindano.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam Zainab Mbilo alisema michezo ni nguzo kuu katika kupunguza magonjwa na kuweka mwili katika hali nzuri pamoja na kusisitiza kwamba michezo inaleta umoja kwani hukutanisha watu wa rika tofauti katika jamii.

  Nae mratibu wa mashindano hayo Bw. Innocent Melleck aliishukuru serikali kwa kuwapa moyo,mwongozo katika maandalizi ya mbio hizo kila yanapofanyika na kuyafanya kuwa bora

  “Riadha ni mchezo ambao umewahi kuiletea nchi medali nyingi kwenye michezo mbalimbali ya kimataifa, ikiwamo Michezo ya Jumuiya ya Madola, Olimpiki na ya Afrika”. Alisema Bw. Melleck

  Uhuru marathon ni tukio ambalo huadhimisha Siku ya Uhuru wa Tanzania huku ikiweka mkazo katika kuimarisha Amani,Upendo na Umoja.


   Mwaka huu zitajumuisha mbio ndefu za kilometa 42,mbio fupi za kilometa 21 pamoja na kilometa 3 zitakazojumuisha viongozi ili kuonyesha uzalendo zikiwa mbio za tatu kufanyika tokea kuanzishwa kwake.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Professa Rogath Kivasi, wakati alipofika kutoa pole nyumbani kwa marehemu Goigi jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 7, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mke wa ,marehemu Prof. Amelia Kivasi, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Goigi jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 7, 2014 kwa ajili ya kutoa pole msiba wa Prof. Rogath KIvasi.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waombolezaji wakati akiondoka baada ya kutoa pole na kusaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa Professa Rogath Kivasi, Goigi jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 7, 2014. Picha na OMR.

  0 0

   Meneja wa tamasha la Karibu Music Festival, Richard Lupia akizungumza katika mkutano na waandishi wa Habari Dar es Salaam hii leo juu ya maandalizi ya tamasha hilo. Kushoto ni Mratibu wa Tamsha, Issam Ramadhan na Kulia ni Afisa Habari wa Karibu Music Festival, Said Hashim.
  Meneja wa tamasha la Karibu Music Festival, Richard Lupia akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa Habari Dar es Salaam hii leo juu ya maandalizi ya tamasha hilo. Kushoto ni Mratibu wa Tamsha, Issam Ramadhan


  0 0

  Serikali imeondoa zuio la mikutano ya Vyama vya Siasa lililokuwa limetangazwa mwezi Mei mwaka juzi kuzuia mikutano hiyo kufanyika katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

  Zuio hilo limeondolewa leo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mathias Chikawe.
  Mikutano hiyo ilizuiliwa kutokana na vurugu za wananchi waliokuwa wakipinga ujenzi wa mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam hali iliyosababisha kuvunjika kwa amani na utulivu katika mikoa hiyo.

  Katika vurugu hizo, watu kadhaa walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa huku magari na nyumba zikichomwa moto.

  Hatua hii ya sasa imechukuliwa baada ya Serikali kuridhika kuwa hali na amani na utulivu imerejea katika mikoa hiyo na kuwa mikutano hiyo sasa inaweza kuendelea kwa kufuata sheria na utaratibu uliowekwa.

  Aidha Jeshi la Polisi litaendelea kutoa ushirikiano katika uendeshaji wa mikutano ya kisiasa inayoendelea katika maeneo mbalimbali nchini na kuwa vibali vya mikutano vitaendelea kutolewa kufuatana na mazingira yatakayokuwepo katika eneo ambapo Chama husika kitakuwa kimeomba kibali.

  Ni matumaini ya Serikali kuwa Vyama vya Siasa vitatumia fursa hii kuendesha mikutano yao kwa amani na utulivu kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kama taratibu za uendeshaji wa mikutano hiyo zinavyoelekeza.

  Imetolewa na:  
  Isaac J. Nantanga
  MSEMAJI
  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
  07/10/2014


  0 0

  Kampuni ya simu za mkononi Airtel inawatangazia wateja wake, wasanii na wanamuziki kuwa yale mashindano yanayotoa fulsa kwa wenye vipaji ya Airtel Trace yanazinduliwa rasmi kesho katika viwanja vya Coco beach jijini Dar es saalam kuanzia saa 12 jioni.

  Uzinduzi huu utawashirikisha wasanii Wakali nchini akiwemo Ommy Dimples pamoja na kundi zima la ya YAMOTO BAND kwa burudani kabambe kwa umati utakao jitokeza hapo kesho katika viwanja hivyo.

  Akitoa maelezo kuhusu uzinduzi huo, Meneja Masoko wa Airtel,Aneth Muga alisema "tunawakaribisha wateja wetu, wapenzi wa muziki na watanzania kwa ujumla katika viwanja vya coco beach kesho jumatano ili kushiriki pamoja nasi katika kusherehekea uzinduzi huu rasmi na kuanza safari ya kumtafuta mshindi wa Airtel Trace Tanzania.

  Airtel kupitia Trace Music Star inatoa nafasi kwa wapenzi wa muziki na waimbaji chipukizi kupata dili poa kabisa kwa kurekodi akapela zao kupitia simu zao za mkononi kwa kipaga na kuimba kaktika namba 0901002233 na hatimae kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo kuingia katika kinyanganyiro cha kuwa super star na mshindi wa Airtel Trace wa Afrika.

  Sambamba na hilo tunapenda kuwatangazia watanzani kuwa namba yetu ya kukuwezesha kuwa mshindi ya 0901002233 sasa iko wazi, hivyo wanaweza kurekodi na kutuma nyimbo zao sasa . kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya www.tracemusicstar.com
  Meneja Masoko wa Airtel Tanzania,Anethy Muga akitangaza namba itakayotumika katika mashindano ya Airtel Trace Music kuwa ni 0901002233 PIGA, IMBA , SHINDA na AIRTEL
  Kikundi cha yamoto Band wakipasha kwaajili ya kutoa burudani kesho katika viwanja vya COCO beach kuanzia saa 12 jioni wakati wa Uzinduzi wa Airtel Trace Music Stars, Kiingilio ni BURE


  0 0

  Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager, Edith Bebwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mashindano ya mbio za Mitumbwi Kanda ya Ziwa, zijulikanazo kama “Balimi Boat Race” iliyofanyiak Dar es Salaam leo.

  0 0

  Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania (TMF), Addo Novembar (katikati) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati akilipongeza Bunge Maalum la Katiba kwa kuingiza katika Katiba vipengele vitatu vinavyolinda maslahi ya wanamuziki. 
  Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Kasimu Mapili (kulia), akiimba na kupiga gitaa lake wakati Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania (TMF), Addo Novembar (katikati), alipozungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu kulipongeza Bunge la Katiba kwa kuingiza katika Katiba vipengele vitatu vinavyolinda maslahi ya wanamuziki. Afya ya Mapili imeimarika baada ya kuugua ugonjwa wa moyo.

  Shirikisho la Muziki Tanzania (TMF), limeunga mkono rasimu ya mabadiliko ya katiba kwa kile walichodai kuwa kimegusa maslahi yao hivyo wataipigania kwa nguvu zote kuhakikisha inapita.

  Akizungumza kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo, Mwenyekiti wa TMF Addo November alisema kuwa kwa miaka mingi wasanii walikuwa wakililia sheria ambayo italinda maslahi yao ambayo kwa mara ya kwanza tangu uhuru upatikane wataanza kula matunda ya kazi zao baada ya katiba mpya kupita.

  "Wasanii wamekuwa wakifanya kazi kubwa lakini hawanufaiki na kazi zao, wasanii wa zamani ukiangalia walifanya makubwa kwenye tasnia hii ya sanaa lakini baadhi yao wamekufa ni maskini wa kutupwa, na wengine mpaka sasa wanaishi maisha ya dhiki hayalingani na thamani ya kazi waliyokuwa wanafanya.

  "Nchi za wenzetu wasanii wamekuwa wakiishi maisha ya mazuri na kuendesha magari ya kifahari, lakini kwa Tanzania ni tofauti magari ya kifahari yanaendeshwa na wanasiasa, wasanii wananyonywa, tunashukuru katiba hii imetambua haki za wasanii kwa kuingiza vipengele vitatu ambavyo vitalinda maslahi ya wasanii na kuwainua kiuchumi.

  Novemba alivitaja vipengele hivyo ni ibara ya 15 (1.e) ambayo inasema kuweka mazingira kwa wasanii kunufaika na kazi zao, ibara ya 38 (iii) inayosema kufanya ugunduzi, ubunifu na utafiti wa sanaa, sayansi na mapokeo ya asili.

  "Ibara ya 56 (1) inasema kila mtu atakuwa na uhuru wa kushiriki kwenye mambo yanayoendeleza na kukuza sanaa, taaluma, ubunifu na ugunduzi. "Kipengele cha (iii) Serikali itakuza na kuendelza utafiti, ubunifu na ugunduzi katika sanaa, sayansi na teknolojia kwa kutunga sheria ambazo zitalinda hakimiliki na haki za wabunifu, watafiti na wasanii.

  Novemba alisema Wasanii kutambuliwa kama kundi maalum, sababu zikiwa ukubwa wa kundi hili, ambalo liko katika kila kijiji nchini, na machango wa pato la Taifa la kundi hili ambao kwa mujibu wa ripoti ya WIPO ya 2010, wasanii walichangia asilimia nne ya GDP, na walichangia asilimia tano ya ajira nchini.

  "Kitendo cha rasimu hii kuweka wazi katika Katiba umuhimu wa ulinzi wa mali itokanayo na ubunifu 'Intellectual property' sheria ambayo italinda maslahi ya wasanii, tutaipigania kwa nguvu zote tupo tayari kufanya kampeni nchini nzima kuipigania ili ipite, tunaiunga mkono kwa asilimia 100 na kesho (leo) viongozi wenzetu watamsindikiza Rais kuipokea rasimu hiyo.

  Aliwataja viongozi wa Shirikisho ambao watamsindikiza Rais Jakaya Kikwete kupokea rasimu hiyo kuwa ni katibu Abdul Salvador, Makamu Mwenyekiti Samweli Mbwana na Mweka Azina Mwinyi Ally.

  0 0

  Na Georgina Misama-MAELEZO 

   Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) imeiwezesha Serikali kukusanya mrabaha wa jumla ya shilingi billioni 5.2 tangu kuanzishwa kwa wakala huo.

  Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi uzalishaji na usafirishaji wa madini Bwn Conrad Mtui wakati wa ziara ya waandishi wa habari walipotembelea migodi ya Lugoba na Msolwa Chalinze, hivi karibuni.

  “Wakala umefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi bilioni 5.2 kutokana na madini hayo yaliyozalishwa na kuuzwa na wamiliki halali wa leseni katika mikoa mbalimbali kwenye kanda za Kaskazini, kati, Kusini, Kusini Maghalibi, Maghalibi, Mashariki na Ziwa Victoria” alisema Mtui.

  Aidha,Wakala kwa kushirikiana na Ofisi za Madini ulibuni matumizi ya “Hati ya Mauzo” kwa lengo la kudhibiti shughuli za uzalishaji na mauzo ya madini, mkakati ambao ulianza kutumika mwezi Juni, 2011 utakaohusisha Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

  Pia, Wakala ulifanya ukaguzi na uhakiki wa madini yaliyozalishwa na kuuzwa na migodi mikubwa ya madini nchini, ikiwa na lengo la kupata mrabaha na takwimu sahihi za madini yaliyozalishwa na migodi hiyo.

  Akitaja migodi iliyofanyiwa ukaguzi alisema ni Mgodi wa dhahabu wa Geita, Golden Pride, Bulyanhulu, Tulawaka, North Mara, Buzwagi na New Luika iliyowezesha kukusanywa kwa jumla ya Dola za Marekani milioni 427.98 Akizungumzia kuhusu hatua wanazochukuliwa baadhi ya wamiliki wa migodi wanaokiuka taratibu za “Hati ya Mauzo” Mkaguzi wa Madini ya Ujenzi na Viwandani Abubakari Jihango alisema kuwa hadi sasa kuna kuna kesi 53 mahakamani, na kama itadhihirika ukiukwaji wa sheria, taratibu za kisheria zitafuatwa.
  Meneja wa Maabara kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) Mhandisi Mvunilwa Mwarabu akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) mashine ya kupimia kiwango cha madini inayoitwa Atomic Absorption Spectroscopy (AAS) walipotembelea Maabara ya Wakala huo jijini Dar es Salaam leo.
  Mkemia Alfred Aloyce kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) sampuli ya jiwe la dhahabu iliyotayarishwa kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kimaabara ili kubaini kiasi cha madini ya dhahabu kwenye jiwe hilo.


  0 0

  Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-ughaibuni inampa salam za heri ya siku ya kuzaliwa Rais Dr. Jakaya Kikwete, bendi hiyo yenye makao kule ujerumani inamtakia kila la heri,afya bora na maisha marefu Mheshimiwa Rais Dr.Jakaya Kikwete ambaye pia Amri jeshi mkuu. Happy Birth day Mhe.Rais J.K.

  0 0


  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Mkutano  wa viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa  siku nne ulioanza jana  unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Mkutano  wa viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislam nchini kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa  siku nne ulioanza jana  unajulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence.


  0 0

   Mwenyekiti wa Mamlaka  ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Dk. Martern Lumbanga (kushoto), akizungumza katika mkutano  na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu matokeo ya ukaguzi wa shughuli za ununuzi katika taasisi za umma uliofanywa na PPRA kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30 mwaka huu. Kulia ni Mjumbe wa Bodi ya PPRA, Jaji mstaafu, Thomas Mihayo.
   Mjumbe wa Bodi ya PPRA, Jaji mstaafu, Thomas Mihayo akizungumza katika mkutano huo. 
   Wajumbe wa Bodi wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mhandisi Leonard Chamuriho, Profesa Silvia Temu na Mhandisi Boniface Muhegi.

  BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

  0 0

  The Permanent Secretary in the Prime Minister's Office, Dr. Florens Turuka(centred) and the President of Assian Injury Prevention Foundation, Creig Craft(third right) during the Official talks held in Prime Minister's Office this afternoon concerns about the support of government to the Helmet factory project expected to take off at Ukonga Central Prison in Dar es Salaam.
  President of Assian Injury Prevention Foundation, Creig Craft(third right) in conversation with his host The Permanent Secretary in the Prime Minister's Office, Dr. Florens Turuka(not in picture). The first right is the Agro Economist, Superitendent of Prisons, Uswege Mwakahesya(centered) is the Chief Executive Officer of the Helmet Vaccine Inniciative Tanzania, Mr. Alpherio Nchimbi.
  The Chief Executive Officer of Tanzania Prisons Cooperation Sole, Senior Assistant Commissioner of Prisons, John Masunga(right) listens a comment from the The Permanent Secretary in the Prime Minister's Office, Dr. Florens Turuka(left) is Mr. Asanterabi Sang'enoi, Assistant Director in the Prime Minister's Office.
  The Permanent Secretary in the Prime Minister's Office, Dr. Florens Turuka(right) shares a light moment with the Chief Executive Officer of Tanzania Prisons Cooperation Sole, Senior Assistant Commissioner of Prisons, John Masunga(left)after an Official talks about the support of government to the Helmet factory project expected to take off at Ukonga Central Prison in Dar es Salaam.
  The Permanent Secretary in the Prime Minister's Office, Dr. Florens Turuka(centred) in a group photo with the President of Assian Injury Prevention Foundation, Creig Craft(third right) during the Official talks held in Prime Minister's Office in Dar es Salaam this afternoon. Others are Senior Prisons Officers' who accompanied the President.
  The Permanent Secretary in the Prime Minister's Office, Dr. Florens Turuka(right) accompany the President of Assian Injury Prevention Foundation, Creig Craft(left) after the Official talks held in Prime Minister's Office this afternoon concerns about the support of government to the Helmet factory project expected to take off at Ukonga Central Prison in Dar es Salaam.

  0 0

  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akizungumza na Uongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati alipotembelea ujenzi wa Daraja la Kigamboni,jijini Dar es Salaam leo.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akipokea kadi maalum ya pongezi ya siku yake ya kuzaliwa leo Oktoba 07,2014 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhan Dau.Rais Kikwete anasherehekea siku yake ya kuzaliwa leo,akiwa ametimiza miaka 64 toka kuzaliwa kwake.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangaliwa maendeleo ya ujenzi wa Daraja Kigamboni jijini Dar es Saalam leo,wakati alipotembelea kuona maendeleo yake.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alieambatana na Waziri wa Ujenzi,Dkt. John Magufuli,Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick wakitembelea eneo la Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam leo.ujenzi huo unafanywa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).


older | 1 | .... | 598 | 599 | (Page 600) | 601 | 602 | .... | 3272 | newer