Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 58 | 59 | (Page 60) | 61 | 62 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Na Dixon Busagaga waglobu ya jamii,Moshi.

  WADHAMINI wakuu wa mbio za Kilimanjaro Marathon, kampuni ya Bia ya TBL, imekabidhi msaada wa magodoro na vyandarua kwa uongozi wa hosptali ya Huruma na kituo cha Afya cha Uru Kiaseni kama sehemu ya maandalizi ya mbio za Kilimanjaro marathon zinatarajia kufanyika machi 3.

  Misaada ya aina hiyo hufanywa kila mwaka na TBL wakati wa maandalizi a Mbio za Kilimanjaro Marathon ambazo hufanyika kila mwaka ikiwa ni utaratibu wa kampuni hiyo kurudisha faida iliyopatikana kwa wananchi kutokana na utumiaji wa bidhaa zake.

  Akizungumza katika hafla ya makabidhiano, Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindi, alisema kuwa TBL imeamua kufanya utaratibu huo ambao wamekuwa wakifanya kila mwaka na mwaka huu wameonelea ni vyema wakatoa msaada katika hospitali hizo.

  Kilindi alisema kuwa msaada wa magodoro hayo 210 na vyandarua 200 ni jitihada za kampuni hiyo kuhakikisa jamii ya Tanzania inafurahi na kujivunia kilicho chao na kuongeza kuwa hicho wal;ichokitoa ni sehemu ya shukuruni kwa watanzania ambao wamekuwa wakiwaunga mkono kila mara.

  “Kama wadhamini wakuu wa mbio hizi, tumekuwa tukishiriki katika shughuli nyingi za kijamii na moja yao ni kutoa msaada katika mahospitali, leo tunatoa magodoro 210 na vyandarua 200 kwa hospitali za Kiaseni ya Rau na Huruma ya Rombo, tunaamini katika hili tutakuwa tuimesaidia kwa kiasi fulani,” alisema Kilindi.

  Naye Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Ibrahimu Msengi akipokea msaada huo kwa niaba ya uongozi wa hospitali hizo aliipongeza TBL kwa kuamua kuijali jamii inayonunua na kutumia bidhaa zao na kuongeza kuwa msaada huo anaamini utakuwa wa manufaa makubwa kwa wagonjwa katika hospitali hizo.

  “Moyo wa kutoa sio lazima uwe nacho, TBL wameonesha kuwa kazi yao sio kutengeneza bia tu, bali wanaweza kujali jamii na katika hili nawapongeza sana na ningependa mashirika na makampuni mengine nayo yangekuwa yanafanya hivi,” alisema Msengi.

  Msengi alitoa wito kwa wafanyabiashara wote na wamiliki wa makampuni kuiga mfano mzuri ulioonesha na TBl na kusisitiza umuhimu wa kutoa kwani jukumu la kuhudumia jamii ni la kila mtu na sio serikali pekee.

  Kuhusu mbio za mwaka huu za Kilimanjaro marathon Dkt. Msengi alisema, mbio hizo kufanyika katika ardhi ya Kilimanjaro ni fahari na kuongeza kuwa matarajio ya wote ni kuona kila mtu akinufaika na mbio hizo huku akiwatakia kila kheri wakimbiaji wote hasa wakimbiaji wa Tanzania.

  “Nitumie Fursa hii kuwatakia kila la Kheri wakimbiaji wote wa Kilimanjaro marathon, kila la kheri watanzania wote watakaotuwakilisha keshokutwa naamini tutashinda,” alisema.

  Kwa upande wake Mganga mnku wa mkoa wa Kilimanjaro (RMO), Dk. Mtumwa Mwako, akipokea magodoro na vyandarua hivyo kutoka kwa kaimu mkuu wa mkoa kwa niaba ya uongozi wa Hospitali za Kiaseni na Huruma, alisema kuwa msaada huo utasaidia kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Malaria kwa mama na mtoto.

  Nao madaktari kutoka katika hospitali hizo, Dkt. Godwin Kiwelu wa hospitali ya Huruma ya Rombo na Dk. Delfina Materu wa hospitali ya Kiaseni ya Rau, walisema kwa msaada huo mzigo wa changamoto zinazokabili hospitali hizo zimepungua huku wakisisitiza kuwa bado kuna changamoto nyngi ambazo inatakiwa jamii inatakiwa kujitokeza kusaidia kama walivyofanya TBL.

  0 0

  Balozi Rajabu Gamaha, Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa katika mazungumzo na Balozi Roberto Azevedo, Mwakilishi wa Serikali ya Brazil katika Shirika la Biashara Duniani (WTO) lenye Makao yake Makuu mjini Geneva, Uswisi, alipofika Wizarani tarehe 2 Machi, 2013 kwa ajili ya kuwasilisha ujumbe maalum. Balozi Azevedo pia ni mgombea wa nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo.
  Mhe. Balozi Azevedo akiwa na ujumbe aliufuatana nao  wakimsikiliza Balozi Gamaha (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo yao. Kulia kwa Balozi Azevedo ni Mhe. Fransisco Carlos Luz, Balozi wa Brazil hapa nchini.
  Balozi Gamaha akiendelea na mazungumzo na wageni wake.

  Balozi Azevedo akiendelea na mazungumzo na Balozi Gamaha. Wengine katika picha ni Balozi Celestine Mushy (kushoto kwa Bal. Gamaha), Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Bw. Lucas Mayenga (kulia), Afisa katika Idara hiyo.
  Balozi Gamaha akifafanua jambo kwa Balozi Azevedo wakati wa mazungumzo yao.
  Mhe. Fransisco Carlos Luz (wa kwanza kulia), Balozi wa Brazil hapa nchini pamoja na wajumbe wengine kutoka Brazil wakimsikiliza Balozi Gamaha (hayupo pichani) alipozungumza nao
  Wajumbe wote kwa pamoja wakimsikiliza Balozi Gamaha.
   

  Balozi Gamaha akiagana na Balozi Azevedo mara baada ya mazungumzo yao.
  Picha ya pamoja.

  0 0
 • 03/02/13--01:25: Article 12


 • UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM

  Academic Staff Assembly

   

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 2/3/2013  Utangulizi


  Wapendwa waandishi wa habari. Tunaomba kupitia ninyi tuweze kuongea na watanzania wenzetu kuhusu hali ya amani ilivyo nchini mwetu kufuatia kila aina ya dalili ya watanzania kukosa uvumilivu wa kidini. Tunatambua kuwa serikali yetu imefanya mambo mazuri mengi tu nchini, hilo hatuna mashaka nalo; hata hivyo kama watanzania tunadhani kuna baadhi ya mambo hayaendi sawa. Hivyo basi, tunaomba kuchukua nafasi hii kuelezea wasiwasi wetu kuhusu migogoro hii ya kidini inayozidi kukua nchini.


  Migogoro hii ilianza kuvuka kama moshi lakini sasa inaanza kulipuka na kusambaa zaidi. Tumeshuhudia uchomaji moto wa kanisa kule Mbagala, kumwagiwa tindikali shekhe mmoja kule Zanzibar na Shekhe mwingine kuuawawa, kuchomwa makanisa Zanzibar, kupigwa risasi viongozi wa kikristo kule Zanzibar na pia mgogoro wa kuchinja huko Geita ambako tumeshuhudia mchungaji mmoja akiuawa.  0 0

  Naibu Waziri Jinsia na watoto,Ummy Mwalimu,akifuatiwa na mwenyekiti wa ccm Mkoa wa Tanga,Henry Shekifu akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Chiku Gallawa ambaye ni wa kwanza mkono wa kulia wakiwa katika uzinduzi wa sherehe za kukabidhi cheti cha halmashauri mpya ya bumbuli iliyofanyika wilayani hapo.
  Cheti cha Halmashauri mpya ya bumbuli.
  Wa pili mkono wa kulia ni aliyekuwa katibu mkuu wa ccm,Yusufu Makamba,kushoto kwake ni Mwenyekiti Mstaafu,Mussa Shekimweri na wa tatu ni katibu wa ccm wilaya y korogwe mjini,Ramadhani Mahanyu juzi wakiwa kwenye sherehe za uzinduzi wakifuatilia.
  Baadhi ya wananchi wa halmashauri mpya ya Wilaya ya Bumbuli wakimkadhizi mbunge wao wa jimbo la bumbuli,January Makamba mbuzi na boksi la majani ya chai kwa jitihada zake za kufanikisha kutimiza moja ya ahadi zake za kupatikana cheti cha halmasauri mpya ya bumbuli,juzi katika sherehe za uzinduzi wa kukabidhiwa cheti hicho zilizofanyika bumduli.
  Wananchi wa halmashauri mpya ya Bumbuli wilayani Lushoto wakifuatilia taarifa mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na viongozi juzi katika sherehe za uzinduzi wa kukabiziwa cheti zilizofanyika bumbuli.

  0 0

   Hivi ndivyo uonekanavyo Uwanja wa Ndege wa Buhigwe Mkoani Kigoma.

  0 0

  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mwendesha Mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa(ICC) Bibi Fatou Bensouda wakati alipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa (ICC) Bibi Fatou Bensouda(Wapili kushoto) mara baada ya kufanya mazungumzo ikulu jijini Dar es Salaam leo.Wengine katika picha kushoto ni Mwanasheria Mkuu Jaji Frederick Werema,Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Bibi Angellah Kairuki(Wanne kushoto) na kulia Mwendesha Mashtaka mkuu wa Serikali Bwana Feleshi(picha na Freddy Maro)

  0 0
 • 03/02/13--02:33: kamera inauzwa
 • Habari kaka mchuzi naomba unisaidie kutangaza biashara sina ofis lakin atakayehitaji awasiliane na Mimi kwa email nimuelekeze zilipo tafadhali ipo hivi ni Canon A 2200 > 14,1 MB , 4X zoom, 6.8sm(2,7 inches ) LCDscare. ,28mm wide angels lens , 720p HD film bei ni 250000 kwa anayehitaji anaweza kuwasiliana na Mimi kwa 

  email: joymathew-87@live.se 

  kamera zinatoka Sweden but zinapatikana Tanzania 

  0 0

  Na Mwandishi Wetu

  MWIMBAJI anayekuja juu kwenye muziki wa kiroho nchini, John Lissu ni miongoni mwa wasanii wapya watakaotumbuiza kwenye Tamasha la Pasaka mwaka huu.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama alisema jana kuwa mwimbaji huyo anakuwa msanii wa pili wa hapa nchini kutangazwa baada ya kung’ara katika upigwaji wa kura za maoni kwa mashabiki zilizoendeshwa na kamati hiyo, ambapo wa kwanza alikuwa Rose Muhando.

  “Tulimtangaza Rose Muhando na sasa tuna John Lissu, kadri mambo yatakavyokuwa tutazidi kuwatambulisha. Hawa tayari tumekubaliana nao kuwatangaza washiriki kwenye tamasha letu,” alisema.

  Kwa upande wake, msanii huyo alisema atatumia tamasha hilo kutambulisha nyimbo zake mbalimbali zilizopo kwenye albamu zake mbili ambazo ni Yehova Yu Hai na Upo Hapa alizozieleza kuwa ni moto wa kuotea mbali.

  “Hivi sasa nina albamu yangu inaitwa Uko Hapa ambayo ni moto wa kuotea mbali, nataka mashabiki wote wafurahie na waitambue siku hiyo. Hii ni mara yangu ya kwanza kupata nafasi ya kushiriki kwenye tamasha hilo, hivyo lazima niwape furaha kubwa mashabiki,” alisema msanii huyo.

  Alizitaja baadhi ya nyimbo zake zilizopo katika albamu ya Uko Hapa kuwa ni Wa Kusifiwa, Yu Hai Yehova, Fungua Macho, Uko Hapa, Hakikisha, Uko Juu, Nitakushukuru na Nijaze.

  Kabla ya albamu hiyo aliwahi kutamba na albamu ya Yehova Yu Hai iliyokuwa na nyimbo kama vile Nisimamishe, Wastahili, Tunakuabudu Bwana na Tunakushukuru.

  Tamasha la Pasaka litafanyika Machi 31 mwaka huu jijini Dar es Salaam, kasha Aprili mosi kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

  Tamasha la mwaka jana baadhi ya waimbaji mahiri waliokuwepo ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.

  Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku hiyo.

  0 0

    Mkuu wa Vodacom kanda ya kaskazini Bw. Philemon Chacha akigawa vifaa vya shule  kwa baadhi ya watoto wenye ulemavu wa akili wa kituo cha KKKT usharika wa Longuo Mjini Moshi  ikiwa ni sehemu ya zawadi mbalimbali kutoka kwa wafanyakazi wa Vodacom Kanda ya Kaskazini vyenye thamani ya shilingi Milioni  1.5 ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya Pamoja na Vodacom.

   Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa akili cha KKKT usharika wa Longuo Mjini Moshi  walipotembela kituoni hapo na kukabidhi  msaada  wa vyakula, vifaa vya shule na vitu vingine mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 1.5 katika kituo hicho ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya Pamoja na Vodacom.

  Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini Philemon Chacha akifuatilia kwa karibu mtoto mwenye ulemavu wa akili Arnold Justine anavyoandika jina lake kwa ufasaha huku mtoto mwenzie Gloria Isaack nae akishuhudia. Wafanyakazi wa Vodacom kanda ya Kaskazini walitembelea kituo hicho na kukabidhi vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Shilingi Milioni Moja na Nusu ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya Pamoja na Vodacom inayosaidia makundi yenye mahitaji maalum.

  0 0


           40'HC TO DAR/MOMBASA NOW £1,950
  20' CONTAINER TO DAR/MOMBASA £1,350
  THIS IS MORE THAN £300 DISCOUNT!
  THIS IS FOR MAERSK LINE, CMA-CGM, WEC LINE NA SAFMARINE
  MIZIGO KWA NDEGE TO DAR/NAIROBI
  £1.80 PER KG

  RATIBA YA MELI MPYA FEBRUARY 2013
   
  Vessel: Glorious Leader v015
  Open for deliveries: 4th March 2013
  Ets: 22nd March 2013
  Eta: Mombasa: 17th April 2013
  Eta: Dar Es Salaam: 14th April 2013
  Vessel close: 21.00 / 19th March 2013
  TUNATOA HUDUMA ZA UKAGUZI WA MAGARI MOT/VOSA OFISINI KWETU
  VEHICLE INSPECTION FOR KENYA A NOW CAN BE DONE IN OUR OFFICES
  JUST DROP YOUR  CAR IN OUR OFFICE AND WE WILL INSPECT IT AND DELIVER IT TO THE PORT FOR YOU

  kama unataka kuagiza kitu au kufanya booking yoyote ingia kwenye website yetu au tupigie kwenye namba zifuatazo;
  CHRIS LUKOSI +44 07903828119  & 07404279633 

  0 0


  *Azindua Tume ya watu 15, aipa wiki sita kukamilisha kazi
   WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amezindua Tume maalum aliyoiunda ili ifanye uchunguzi wa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yaliyotangazwa Februari 18, mwaka huu na kuwataka wajumbe wa Tume hiyo watafute kiini cha mserereko wa kushuka kwa ufaulu kuanzia mwaka 2010 hadi 2012.
  Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Jumamosi, Machi 2, 2013) wakati akizungumza na wajumbe wa Tume hiyo kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni, jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa.
  “Nimetafuta takwimu za tangu mwaka 2005, Serikali ya Awamu ya Nne ilipoingia madarakani na kubaini kuwa tangu wakati huo hadi mwaka 2009 tulikuwa tukifanya vizuri, lakini kuanzia mwaka 2010 hadi 2012 matokeo yamekuwa yakishuka sana,” aliwaambia wajumbe wa Tume hiyo na waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo.
  Alisema hali hiyo haikuwa kwenye shule za sekondari za umma (kata) peke yake bali hata kwa shule za Serikali, za watu binafsi na kwenye seminari ambazo kwa miaka mingi zimekuwa na sifa ya kufanya vizuri kuliko shule za kawaida.
  Akitoa mfano, Waziri Mkuu alisema: “Mwaka 2005 kiwango cha ufaulu kilikuwa asilimia 89.3; mwaka 2006 asilimia 89.12; mwaka 2007 asilimia 90.6; mwaka 2008 asilimia 83.6 na mwaka 2009 asimilia 72.5, hapa napo tulikuwa bado tuko vizuri japo si sana ikilinganishwa na miaka mine iliyotangulia.”
  “Lakini mwaka 2010, kiwango cha ufaulu kilishuka na kufikia asilimia 50.4, mwaka 2011 kilipanda kidogo na kufikia asilimia 53.6 na kilishuka zaidi mwaka jana ambapo kilifikia asilimia 34.5. Hapa ni lazima mtu utapata maswali ya msingi na kujiuliza nini kimetokea katika miaka ya hivi karibuni,” alisema.
  Waziri Mkuu alibainisha kwamba idadi ya watahiniwa iliongezeka kutoka 85,292 mwaka 2005 na kufikia 248,336 katika mwaka 2009 wakati idadi ya walimu nayo pia iliongezeka kutoka 20,414 na kufikia 37,218 katika kipindi hichohicho.
  Alisema anatambua changamoto nyingine zinazoikabili sekta ya elimu kama vile uhaba wa vitendea kazi, upungufu wa maabara na walimu wa sayansi, upungufu wa mabweni pamoja na nyumba za walimu.
  Kinachoshangaza, Waziri Mkuu alisema, mbali na kuongezeka kwa walimu kutoka 44,053 mwaka 2010, walimu 55,982 (mwaka 2011) na kufikia walimu 68,784 mwaka 2012 bado kiwango cha ufaulu nacho kilikuwa kikishuka katika kipindi hichohicho.
  Akitoa mfano, Waziri Mkuu alisema: “Kwenye shule za kata, mwaka 2010, walifaulu wanafunzi 114,883; mwaka 2011 wanafunzi 106,286 na mwaka 2012 wanafunzi 74,817 wakati kwenye shule za Serikali, katika kipindi hicho hicho ufaulu ulishuka kutoka wanafunzi 19,412, na kufikia wanafunzi 10,712.”
  Waziri Mkuu alisema katika mchanganuo huo, jambo moja kuu lililo bayana ni kuwepo kwa mzao wa kwanza wa shule za kata katika mwaka 2010 lakini bado athari za kushuka kwa ufaulu zikasambaa kote hadi kwenye shule za serikali, za binafsi na seminari.
  Akianisha kushuka kwa ufaulu wa daraja la kwanza katika makundi hayo, Waziri Mkuu alisema: “Mwaka 2010, kwenye shule za kata, walifaulu wanafunzi 1,225 wakati mwaka 2011 walikuwa wanafunzi 564 na mwaka 2012 walikuwa wanafunzi 162”.
  “Kwenye shule za Serikali, mwaka 2010, walifaulu wanafunzi 952, mwaka 2011 wanafunzi 771 na mwaka 2012 wanafunzi 253. Kwenye shule za binafsi, mwaka 2010, walifaulu wanafunzi 2,476 mwaka 2011 wanafunzi 1,614 na mwaka 2012 wanafunzi 1,032. Kwenye seminari, mwaka 2010, walifaulu wanafunzi 695, mwaka 2011 wanafunzi 428 na mwaka 2012 wanafunzi 197.”
  Akianisha matokeo ya waliofeli kwa kupata daraja ‘0’, Waziri Mkuu alisema: “Mwaka 2010, kwenye shule za kata, walifeli wanafunzi 151,848 wakati mwaka 2011 walifeli wanafunzi 143,552 na mwaka 2012 walifeli wanafunzi 223,774”.
  “Kwenye shule za Serikali, mwaka 2010, walifeli wanafunzi 7,926, mwaka 2011 wanafunzi 9,790 na mwaka 2012 wanafunzi 16,176. Kwenye shule za binafsi, mwaka 2010, walifeli wanafunzi 13,346 mwaka 2011 wanafunzi 16,620 na mwaka 2012 wanafunzi 25,055. Kwenye seminari, mwaka 2010, walifeli wanafunzi 638, mwaka 2011 wanafunzi 972 na mwaka 2012 wanafunzi 1,329.”
  Alisema kwa  mujibu wa hadidu za rejea, wajumbe wa tume hiyo watatakiwa kuangalia ni sababu zipi zimechangia kuwepo kwa matokeo hayo mabaya, mserereko wa kushuka umekuwa ukiongezeka kwa sababu gani, usimamizi katika Halmashauri ukoje, ukaguzi wa elimu na uhamishiwaji wa sekta ya elimu kwenye Wizara ya TAMISEMi umechangiaje kushuka kwa kiwango cha ufaulu.
  Vilevile, watatakiwa kuangalia mitaala na mihutasari ikoje, kuangalia uwiano uliopo kwenye mitihani inayotungwa ikiwa ni pamoja na uhakiki wa mitihani hiyo; kuangalia mazingira ya kufundishia, mfumo wa upimaji, usimamizi na uendeshaji, na kutokuwepo kwa chakula shuleni kunachangiaje kushuka kwa utendaji mbaya wa wanafunzi katika masomo yao.
  Tume hiyo yenye wajumbe 15, imepewa muda wa wiki sita kuanzia Machi mosi iwe imekamilisha kazi hiyo na kuwasilisha taarifa yao kwa Waziri Mkuu. Itaongozwa na Prof. Sifuni Mchome wa Tume ya Vyuo Vikuu, na Makamu wake atakuwa Bi. Bernadetha Mushashu (Mbunge wa Viti Maalum – Kagera).
  Wajumbe wengine ni Bw. James Mbatia (mbunge wa Kuteuliwa), Bw. Abdul J. Marombwa (Mbunge wa Kibiti), Prof. Mwajabu Possi (Chuo Kikuu - UDSM), Bibi Honoratha Chitanda (CWT) na Bibi Daina Matemu (TAHOSSA) na Bw. Mahmoud Mringo (TAMONGSCO).
  Wengine ni Bw. Rakhesh Rajani (TWAWEZA), Bw. Peter Maduki (CSSC), Mwl. Nurdin Mohamed (BAKWATA), Bw. Suleiman Hemed Khamis (Baraza la Wawakilishi), Bw. Abdalla Hemed Mohamed (Chuo Kikuu – SUZA), Bw. Mabrouk Jabu Makame (Baraza la Elimu Z’bar na Bw. Kizito Lawa (Taasisi ya Kukuza Mitaala)
      
  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P 3021,
  DAR ES SALAAM.
  JUMAMOSI, MACHI 2, 2013.

  0 0
 • 03/02/13--12:27: umbea wa nathan mpangala


 • 0 0

  Pambano la masumbwi kutetea makanda wa mabara wa WBF(world boxing forum) wategemea kufanyika katika uwanja wa mkwakwani jijini  Tanga kwa  kuwakutanisha  Alan Kamote, ambae ni bingwa mtetezi wa  mkanda huo aliouchukua  nchini Malawi  kwa  kuzipiga na  Jumanne Mohamed  wa tanga  ambae anavyo vigezo  na sifa zote  za kuugombania ubingwa huo.
  Jumanne Mohamed ambae alipata nafasi  ya kugombania  ubingwa  wa  dunia  nchini Namibia na kuipoteza kwa kupigwa na mnamibia  nafasi hiyo imejirudia tena,safari hii katika ubingwa wa mabara na kuugombania katika ardhi ya nchini mwake.Muandaaji wa pambano hilo Ally Mwanzoa  akizungumza  na viongozi wa ngumi nchini pamoja na katibu mkuu wa ngumi za kulipwa  Ibrahim  kamwe  amesema ameamua kuandaa pambano hilo ili Alan kamote autetee  mkanda wake alioupata  Blantaya nchini Malawi usije ukapoteza kwa kutokuutetea ubingwa wake huo, na kukaa na uongozi wa ngumi  kwa kuangalia bondia gani anafaa  na ikaamuliwa  jumanne Mohamed anafaa kutokana na sifa alizonazo na upinzani walionao  mabondia hao utaleta mshawasha na msisimko mkoani Tanga, kwa hiyo haina haja ya kumleta mtu kutoka nje ya nchi.mwanzoa aliendelea  kwa kusema pia kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi  kati jj ngotiko  na  haji juma wa Tanga katika pambano la raund kumi, na kutakuwepo na mapambno mengine mengi y a utangulizi.

  0 0

  Ahmed Salim Saleh, mshindi wa Tshs, 5,000,000 za DStv Rewards akiwa na uso wa furaha huku ameshikilia mfano wa hundi aliyokabidhiwa.
  Katika muendelezo wa kampeni ya DStv Rewards kampuni ya MultiChoice Tanzania inayo furaha kumtangaza rasmi mshindi wake wa tatu. Mshindi huyo ni Ahmed Salim Saleh, mfanyakazi wa Access Bank ya jijini Dar-es-Salaam.   Kupitia droo ya DStv Rewards, MultiChoice Tanzania inaibua baadhi ya wateja wao kuwa “mamilionea” ambapo katika kila wiki mteja mmoja huibuka mshindi wa kitita cha Shilingi Milioni 5. (Tshs 5,000,000)
  Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu, akiwa na mshindi wa DStv Rewards kwa wiki ya tatu, Ahmed Salim Saleh, baada ya kumkabidhi mfano wa hundi ya kitita cha Tshs. 5,000,000 alichojishindia.
  DStv Rewards ni sehemu ya kampeni maalum ya kampuni ya MultiChoice Tanzania kuwashukuru wateja wao kutokana na ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka kwao.   Kampeni hiyo maalumu ilianza tarehe 5 February, 2013 na inaendelea mpaka tarehe 10 April, 2013. Wateja ambao wanakuwa na nafasi ya kuibuka “mamilionea” ni wale ambao hulipia akaunti zao za DStv kabla hazitajakatwa kwa kulipia kifurushi chochote kati ya DStv Access, DStv Family, DStv Compact, DStv Compact Plus na DStv Premium.
  Mshindi wa DStv Rewards, Ahmed Salim Saleh, akisaidiwa na baadhi ya wafanyakazi wenzake kushangilia kwa kuibuka mshindi wa Tshs, 5,000,000 alizoshinda.

  0 0

  RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga (pichani) amesema Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo na Baraza la Taifa la Michezo (BMT), hazina nguvu ya kusimamia uchaguzi wa shirikisho hilo.

  Tenga aliyasema hayo leo mara baada ya kikao cha kamati ya utendaji na kusema kuwa tangu katiba hiyo ilipofanyiwa marekebisho mwaka 2004 nguvu ya Waziri wala BMT haipo tena na kudai kuwa TFF ina nguvu kamili kama vyama vingine na kina uhuru wake kamili wa kutoa na kusimamia maamuzi yake bila ya kuingiliwa.

  "Nitamtafuta Waziri ili nikutane naye na nimueleze kabisa kuwa agizo alilolitoa alitekelezeki na tutamshauri madhara ya maamuzi yake, serikali kuandika barua ni kutuingilia moja kwa moja na madhara yake ni kufungiwa, na tukishafungiwa hata wadhamini watakaa pembeni, timu zetu pia hazitacheza mpira, kuna watu nasikia wanasema bora tufungiwe, nitahakikisha kwa hali yoyote ile hatufungiwi.

  "Sheria za nchi zipo, lakini ziliridhia toka mwaka 2004 kufanya shughuli zetu wenyewe bila ya kuingiliwa kwa kuzingatia objective (wajibu) zetu ambazo ni kucheza mpira, kama tutafanya kinyume na hapo kama kucheza tenesi au kuvuta bangi hapo ndio tuulizwe inakuwaje objective yenu sio hiyo.

  Kauli ya Tenga imekuja wiki moja baada ya Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Fennela Mukangara kupinga katiba ya TFF kwa madai kuwa imekiuka kanuni ya za sheria ya BMT, namba 11 (1) na kutaka itumike ya mwaka 2006.

  "Natoa agizo kwa wasaidizi wa msajili wa vyama vyote nchi kufuta taratibu za usajjili kwa mujibu wa sheria na kanuni za BMT, sisi hatuitambui katiba iliyotumika katika mchakato wa uchaguzi wa mwaka huu na sasa badala yake tunatambua ile ya mwaka 2006, hii ni batili na imekiuka kanuni na sheria za BMT,"alikaririwa akisema Dk Mukangara wiki iliyopita.

  Pia kufuatia sakata la katiba hiyo kutotambuliwa na serikali Waziri Mukangara alitangaza pia kumsimamisha kazi msajili wa vyama vya michezo nchini Mercy Rwezaura aliyedaiwa kuipitisha katiba hiyo na tayari mchakato wa kumtafuta mwingine umeanza.

  Lakini Tenga alisema: 'Kifungu alichotumia Waziri kuzuia katiba mpya kanuni zake zinaendelea kuzungumzia marekebisho, hatuwezi kuchukua vipande vidogo vidogo kwa jambo kubwa kama hili, katiba tuliipeleka kwa msajili na ikakaa kwa siku 14, baada ya siku hizo kupita akatupatia katiba yetu hatukujaza fomu sasa lilikuwa jukumu la nani kutupa fomu ya kujaza si ni msajili hajatupa sisi tufanyaje?"alihoji "Waziri anaposema hatukufuata taratibu kwa vile hatukujaza fomu sio haki, ametuadhibu kwa kosa ambalo si la kwetu, tunadhani jambo hili lingeangaliwa kwa kina, hata hivyo mwaka 2004 hakukuwa hata na muda wa kuandika muktasari mabadiliko yalifanyika pale pale ukumbini na uchaguzi ukafanyika.

  "Tulishaachana na mambo yetu kuingiliwa na serikali wala BMT maelekezo ya Waziri nadhani amesahau kabisa kuwa tulishatoka huko siku nyingi,ni kweli kabisa uhalali wa marekebisho ya katiba yanatokana na mkutano mkuu peke yake na si mtu mwingine yoyote na BMT wala Waziri nafasi yao haipo tena, na anavyotutuma tuandike barua FIFA tuwambie ametuamuru kufuta katiba yetu, nasema wazi hatutafanya hivyo, sana sana tutawapa maelezo na kuwambia tutakutana naye na kuyamaliza"alisisitiza

  "Marekebisho ya katiba yetu hatukufanya kwa siri tuliwaeleza kabisa hatuna fedha ya kuitisha mkutano mkuu mara mbili, kama mtakumbuka marekebisho haya yalikuwa wakati tumeshaomba wadau wakachangishana fedha kwa ajili ya kuisaidia timu yetu ya Serengeti alafu wiki moja baadae wadau hao wakuone unaitisha mkutano mkuu unaogarimu milioni 135 watakuelewa?

  "Kiongozi mzuri ni yule anayesema kweli hali halisi ndio hiyo tulipeleka waraka zikafanyika kampeni za kuukataa, nikawaangukia na kuwaeleza hali halisi zikapigwa kura 35 walipinga, 70 walikubali sasa kuifuta katiba ina maana watu 70 wote hawana maana? Kiongozi ambaye hawezi kufanya maamuzi magumu inatia shaka.

  "Hata hiyo katiba ya mwaka 2006 anayoitaka Waziri ndio tufanyie uchaguzi haina nafasi ya BMT kusimamia uchaguzi, na kuitumia katiba hiyo ni kuiondoa mikoa mipya kama ya Simiu, Geita,Katavi, Waziri ameshauriwa kwa sababu hakuwa kwenye mpira, na wanaomshauri sidhani kama wanajua masuala ya mpira wala hawaijui katiba ya TFF inasemaje na hawajaisoma ndio maana Waziri akatoa maamuzi kama yale.

  "Mama tafadhali naomba achia huu mchakato uendelee kinyume chake ni kuingiza nchi kwenye moto, kwenye vurugu.

  0 0
 • 03/03/13--00:57: CHEKA UNENEPE

 • 0 0

  · Zavutia zaidi ya wakimbiaji 7,000 · Wakimbiaji wote wapata zawadi ya ushiriki kutoka Vodacom Maelfu ya wakazi wa Mji wa Moshi na vitongoji vyake ikiwemo wageni mbalimbali kutoka nje ya mkoa wa Kilimanjaro na wa nje ya nchi wameshiriki mbio za kujifurahisha za Kilomita Tano za Vodacom zijulikanazo kama”Vodacom 5KM Fun run” zinazofanyika pembezoni mwa mbio za Nyika za Kilimanjaro. 

  Mbio hizo zinazofadhiliwa na kampuni ya mawasiliano Vodacom zimevutia wakimbiaji zaidi ya 7,000 na hivyo kuendelea kuwa za kipekee kwa jinsi inavyotoa nafasi kwa makundi mbalimbali kushiriki kama sehemu ya kusherehekea msimu wa mbio za kila mwaka za Kilimanjaro Marathon. 

  Kupitia mbio hizo za kujifurahisha za Vodacom makundi mbalimbali ya wasio wakimbiaji wa kulipwa yaani Professional Runners hupata fursa ya kushiriki na kuwa sehemu ya shamrashamra za Kilimanjaro Marathon na pia kutumia nafasi hiyo kunyoosha viungo,kuimarisha afya huku wengine wakitumia mbio hizo kama kipimo cha kujipanga kushiriki mbio ndefu katika mashindano mbalimbali. Mbio hizo zilianzia eneo la Nje ya Chuo Kikuu cha Ushirika cha Mjini Moshi zikianzishwa na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Ibrahim Msengi na kumalizikia ndani ya uwanja wa mpira wa miguu wa Chuo hicho ambapo washiriki walipata zawadi mbalimbali za ushiriki kutoka kampuni ya Vodacom. 

  Akizungumzia mbio hizo Afisa Matukio na Udhamini wa Vodacom Ibrahim Kaude amesema Vodacom inajivunia kuwezesha kila mmoja kuwa sehemu ya mbio za Kilimanjaro Marathon zinazofanyika kila mwaka. 

   “Kila mtanzania na hata asie mtanzania hususan wasio wakimbiaji wa kulipwa angependa kuwa sehemu ya tukio hili kubwa lenye mvuto na sura ya kimataifa hivyo kwetu sisi kuwezesha hilo ni jambo tunalolifurahia na kulipa kipaumbele kila mwaka.”Amesema Kaude.

  Amesema katika kuonesha kuwa mbio hizo ni za kipekee na zinafurahiwa na kila mmoja idadi ya washiriki imeongezeka kwa kiasi kikubwa kulinganisha na idadi ya walioshiriki mbio hizo mwaka jana. Pamoja na kubeba jina la mbio za kujifurahisha lakini mbio hizo zimeonekana kuwa na ushindani mkubwa miongoni mwa washiriki miongoni mwao wakiwa wanafunzi wa shule mbalimbali, taasisi, mashirika ya kitaifa na kimataifa pamoja na wakimbiaji mmoja mmoja. 

  Katika kuhakikisha kila mmoja anakuwa sehemu ya mbio hizo baadhi ya watu wameonekana wakikimbia na watoto wao huku wakiwahamasisha kuhakikisha wanamaliza mbio hizo ambao mshindi wa kwanza alitumia kiasi cha dakika 20 Kwa upande wa washindi wanaume Bw.Doto Ikangaa aliyeshika nafasi ya kwanza na Elibariki Buko nafasi ya pili wamesema pamoja na kwamba mbio hizo ni za kujifurahisha bado zimekuwa na ugumu kwa kuwa idadi ya washiriki wenye uwezo wa kukimbia ni kubwa na hivyo kutoa ushindani. 

   Hata hivyo washindi hao wameipongeza Vodacom kwa kutengeneza mazingira ambayo kila mmoja anakuwa na nafasi ya kufurahia msimu wa Kilimanjaro Marathon na hivyo kulifanya tukio hilo kuwa na sura hasli ya kitanzania kwa kuwa kinyume cha hapo ingeshuhudiwa idadi kubwa ya wakimbiaji wa nje wakishiriki katika mbio ndefu. Mbio hizo zimetoa washindi watano ambao wamezawadiwa zawadi mbalimbali ikiwemo simu za mkononi na fedha taslimu zikiwa na jumla ya thamani ya kiasi cha Shilingi Milioni Tisa. Mwisho.
   Mmoja wa washiriki wa mbio za kujifurahisha za”Vodacom 5KM Fun run”Bw.Moses Msaka katikati akimalizia mbio zake mjini Moshi leo. Mmasai huyo alivutia  washiriki wengi wa mbio hizo kwa kukimbia akiwa amevalia nguo zake za kawaida.

   Afisa Matukio na Udhamini wa Vodacom Tanzania,Bw.Ibrahim Kaude akiongea na waandishi wa habari mara baada ya mbio za kujifurahisha za”Vodacom 5KM fun run kuisha.
  Sehemu ya wakimbiaji 7,000 wa Vodacom Run
   .Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi.Rukia Mtingwa pamoja na mfanyakazi mwenzake wakishiriki katika mbio za kujifurahisha za”Vodacom 5KM fun run mjini moshi.
   Baadhi ya washiriki wa mbio kujifurahisha za”Vodacom 5KM fun run wakishiriki katika mbio hizo ambazo ni sehemu yam bio ndefu za Kilimanjaro Marathon.
   Vodacom Fun Run inogile

   Watoto Francis Ngowi kushoto na Moses John wote wenye umri wa miaka 14 wakishiriki katika mbio za kujifurahisha za “Vodacom 5KM fun run ambazo ni sehemu yam bio ndefu za Kilimanjaro Marathon.
   Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakishangilia kwa kumaliza mbio za kujifurahisha za”Vodacom 5KM fun run ambazo ni sehemu yam bio ndefu za Kilimanjaro Marathon.


  0 0


   

  Na Mroki Mroki-Father Kidevu Blog-Moshi
   
   Wanariadha kutoka Nchini Kenya wameendeleza Umwambawao katika mbio za Nyika za Kilimanjaro ‘Kilimanjaro Marathon 2013’ zilizofanyika leo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

  Wakenya walidhihirisha umwamba katika Mbio za Kilometa 42 baada ya Mkimbiaji wao Kipsang Kipkemoi (pichani) kunyakua nafasi ya kwanza  katika mbio hizo za mwaka huu upande wa wanaume na Wanawake ilinyakuliwa na Mwana dada Edna Joseph aliyebeba Medali ya Dhahabu.

  Nafasi ya pili hadi ya tano kwa wanaume ni Julius Kilimo, Dominick Kiagor, Onesmo Maithiya Loshile Moikari ambapo upande wa wanawake ni Eunice Muchiri, Frida Too, Rosaline David na Jane Kenyara.

  Jumla ya wakimbiaji 65000 walishiriki mbio za Kilimanjaro Marathon 2013.

  0 0


  Kama ilivyo ada, baada ya kuhairishwa ka safari ya kwenda Kunduchi wanamichezo toka vilabu vya Namanga na Biafra waliamua kufanya mazoezi pamoja kwa kuanzia Namanga jijini Dar es salaam  na kuishia Biafra. Mbio hizo zilipita katika bara ya Ubalozi (USA), Mwai Kibaki, Migombani, Mission Mikocheni, New Bagamoyo, , Mwinjuma, Hospitali ya Mwananyamala, Dunga, Kawawa na kuishia 90 Degrees Pub ambapo ni Makao makuu ya klabu y Biafra. 
  Jogging barabara ya ubalozi (USA)


  Katibu Mkuu wa Biafra Kaka Poli akiongoza jahazi...ingawa rejeta inaonekana kufuka moshi tehe tehe tehe...
  Kwa mapicha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  MWENYEZI MUNGU AKIKUACHA KATIKA HALI 

  FULANI....MSHUKURU TU!


  Mwenyezi Mungu akikuacha katika hali fulani, basi mshukuru tu wala usilalamike! 
  Kwani yeye ndiye akujuae zaidi. 
  Pia usidhani kama maisha yamekamilika kwa mtu yoyote; kuna mwenye nyumba lakini hana gari.....kuna mwenye gari lakini hana watoto.....kuna mwenye watoto lakini hana pesa.....kuna mwenye pesa lakini hana afya.....kuna mwenye afya lakini hana kazi....kuna mwenye vyote lakini hana Amani wala Furaha... 

older | 1 | .... | 58 | 59 | (Page 60) | 61 | 62 | .... | 3270 | newer