Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 4 | 5 | (Page 6) | 7 | 8 | .... | 3272 | newer

  0 0
 • 12/28/12--08:19: INVESTING Vs. SPENDING TIME

 • by monfinance

  Every one of us has two major choices on how to use of time.
  1. Investing time.
  2. Spending time.
  We invest time when:
  we use it today to create a flow of money that will keep expanding as we get into the future. Smart people start by identifying where to invest time and then use every minute of their time to take small steps that lead to creation of their own future income flow.
  We spend time when:
  -We do nothing and just let it go by.
  -We use it to build small unstable businesses.
  -We use it to work for someone for a fixed pay.
  -We do not give enough time to an idea to fully develop it.
  Spending time may involve working to obtain satisfaction or meet our needs in the immediate present. When we stop working, money also stops coming. Once we belong to a group of those who spend time, the time we use now will never pay us back in the future. We may be opened to lots of great ideas but trouble sticking with one long enough to develop it fully so it gives us a continuous flow of income.
  The choices we make today on how to use our time determines whether we will have a serious income flow in the future.
  Income generating sources like employment are excellent alternatives to start with in life but employment may be one of the riskiest income creating choices people make. Employment makes you a time spender not a time investor.
  Smart people keep investing time. Most other people choose to spend time because they do not know the difference between investing and spending time.
  Contributed by Paschal of Creative Minds Associations. (CMA)

  0 0


  Mwezi Novemba 2012, Kampuni ya Addax Energy SA ya Uswisi ilishinda zabuni ya sita ya  kuingiza mafuta kwa pamoja chini ya utaratibu unaosimamiwa na Kampuni ya uagizaji mafuta kwa Pamoja (PICL). Zabuni hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya mafuta ya Mwezi Desemba 2012 na mwanzoni wa Januari 2013.


  Utaratibu wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja huzingatia pamoja na mambo mengine viwango vya ubora wa mafuta kama vinavyoelekezwa na Shirika la Viwango  nchini (TBS). Aidha, TBS hukagua ubora wa mafuta hayo kabla hayajaingia nchini.


  Pamoja na aina nyingine za mafuta, Addax Energy SA ilipaswa kuleta mafuta ya dieseli  yenye ujazo wa MT 100,000 sawa na takriban lita 100,000,000 katika zabuni ya sita. Meli ya AL BURAG iliyobeba mafuta hayo ilitakiwa kufika hapa nchini na kupakua mafuta kati ya tarehe 17 mpaka 20 Desemba 2012. Hata hivyo, meli hiyo ilifika tarehe 24 Desemba 2012 ikiwa imechelewa kwa siku nne kwa mujibu wa ratiba.  Mafuta hayo yalipimwa  na TBS tarehe 26 Desemba 2012 na kugundulika kuwa yako chini ya viwango vinavyotakiwa kwa Tanzania. Aidha, tarehe hiyo hiyo, Kampuni binafsi ya Intertek Testing Services iliyoajiriwa na PICL pamoja na Addax Energy SA ilipimamafutahayo na kujiridhisha kuwa yalikuwa chini ya viwango vinavyotakiwa. 

  Kwa kuzingatia hali hiyo Serikali imechukua hatua zifuatazo:


  1.    Imeiagiza PICL pamoja na EWURA kwamba mafuta YARUDISHWEyalikotoka,


  2.    Imeiagiza EWURA ichukuwe hatua stahiki za KISHERIA dhidi ya Kampuni ya Addax Energy SA,


  3.    PICL ichukuwe hatua zinazotakiwa dhidi ya Kampuni ya Addax Energy SA kulingana na  MKATABA, na


  4.    Imeziagiza PICL pamnoja na EWURA kuhakikisha kuwa hali hii haijirudii tena hapa nchini.


  Aidha, Wizara ya Nishati na Madini inapenda kuwahakikishia wananchi kuwa kutopokelewa kwa mafuta hayo yaliyo chini ya viwango HAKUTAATHIRI upatikanaji wa mafuta ya dieseli nchini kwa kuwa kwa sasa kuna mafuta ya kutosha.  Imetolewa na


  Katibu Mkuu
  Dar es Salaam, Desemba 28, 2012


  0 0

  Leo Jumamosi Dec 29 ni mwaka mmoja tokea mtangazaji wa kwanza wa kike kutangaza mpira katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati Halima Mchuka (pichani) kufariki dunia.

  Halima Mchuka atakumbukwa kwa weledi wake wa hali ya juu katika tasnia ya utangazaji, hasa wa mpira ambapo aliweza kubuni maneno na majina mengi ambayo yanatumika hadi hii leo, mfano mkubwa ni 'mpira umeenda fyongo' akimaanisha mpira umepigwa vibaya na mchezaji.

  Leo saa kumi jioni kutakuwa na kisomo nyumbani kwa dada yake  Mwajuma Mchuka Mbezi Beach, Dar es salaam. Karibuni wote kumuenzi na kumuombea dua  shujaa huyu.

  0 0

  Ndugu Michuzi na kikosi kizima cha Blog yetu ya Jamii,

  Kwa niaba yangu na uongozi mzima wa Kanisa la Umoja hapa Dallas, Texas, Marekani, napenda kuwakaribisha watu wote katika  mji huu na maeneo ya jirani kwenye ibada ya mwisho katika  mwaka huu na kukaribisha mwaka mpya - 2013.

  Kikundi chetu cha Praise and Worship kitatuongoza katika siku hii ya kipekee katika mwaka huu. Shuhuda mbali
   mbali pamoja na maombi vitakuwa sehemu katika  ibada hii.

  Kumbuka ni Jumapili hii!
  Muda ni saa Kumi na mbili kamili jioni..
  Anuani: 6411 LBJ FREEWAY DALLAS TX,75240
  Mawasiliano: 214 554 7381,682 552 6402
  Pastor Absalon Nasuwa

  0 0
 • 12/28/12--18:35: bonanza la hockey zanzibar

 •  Baadhi ya wachezaji wa timu ya Mpira wa magongo (HOCKEY) Zanzibar wakiisubiri timu ya wazee kwa ajili ya mechi iliyoandaliwa na chama cha mpira huo huko katika uwanja wa Mau.
   Mwandishi wa habari kutoka Chuchu FM Redio Yahya Saleh akimuhoji kocha wa timu ya mpira wa magongo (HOCKEY)  Mgeni Haji  juu ya upatikanaji wa vifaa vya mchezo huo ambapo alisema ni ghali mno.
   Timu ya wachezaji wa zamani wa magongo (HOCKEY) wakiwa katika mapumziko mafupi (Halftime)huko katika uwanja wa Mau.
  Mchezaji wa timu ya Kombaini Halifa Abdallah Maabadi mwenye bukta ya njano akisawazisha bao katika mechi hiyo ambayo ilitoka mbili mbli.
   Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar

  Na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar 

  Makamo Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa magongo (HOCKEY) Zanzibar Ramadhan Pandu Makame ameiomba Serekali pamoja na wadau wa Michezo kusaidia upatikanaji wa vifaa vya mchezo huo ili waweze kuuendeleza na kushiriki katika mashindano ya ndani na nje ya nchi.

  Ramadhan ameyasema hayo katika Bonanza la Mchezo huo lililoandaliwa na chama hicho kwa lengo la kujindaa na mashindano ya Mapinduzi Cup yanayotarajiwa kufanyika jijini Dar es laam Januari 09 mwakani.

  Amesema Vifaa vya mchezo wa Mpira wa Magongo ni ghali sana kiasi cha wao kushindwa kumudu kuvinunua na hivyo kulazimika kuomba msaada ili wasaidiwe kupatikana kwake.
  Ameongeza kuwa Zanzibar kuna vipaji lukuki vya mchezo huo lakini kinachokosekana ni vifaa na ushajihishwaji wa vijana kujiunga na mchezo huo.
  Ramadhan amedai kuwa kama kutakuwa na ushirikiano wa kutosha na kuwezeshwa kikamilifu chama hicho anaamini kuwa Zanzibar inaweza kuwa na timu zinazoweza kufanya vizuri katika mashindani ya kitaifa na kimataifa.
  Akizungumzia kuhusu mashindano ya Mapinduzi Cup Ramadhan amesema mashindano hayo yatazishirikisha timu nane ikiwemo timu ya Zanzibar.

  Kwa upande wao Wachezaji wakongwe wa Mpira wa magongo wamekipongeza chama cha mpira huo kwa kuandaa mechi kati yayo na timu ya kombaini ya Zanzibar ikiwa pamoja na kuwashajihisha vijana ili kuupenda mchezo huo.
  Aidha wamekishuri Chama hicho kuandaa mechi za mara kwa mara kati yao ili kuipa ukomavu timu hiyo na pia kuutangaza mchezo kwa Wazanzibari
  Katika Bonanza hilo Timu ya Maveterani wa mchezo huo ilipimana nguvu na Timu ya Kombaini ya JWTZ na KMKM ambapo matokeo ya mchezo huo ni suluhu ya mabao mawili kwa mawili.
  IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

  0 0

  Muziki wa Kongo si Ndombolo ya solo pekee, kama walivyodhihirisha vijana wa TRIO MADJESI & SOSOLISO walipotamba na vibao kibao ikiwamo hiki cha PHOTO YA MADJESI. Asante mdau Mesiaki kwa kutuletea ngoma hii na kutupa ujumbe huu chini: 

   Ankal, 
  Hii kitu ya photo madjesi ya Sosoliso ilikuwa moto wa kuotea mbali yaani mabrazameni wa wakati huo hawawezi kupatikana leo tuwape vitu wadau 
  I am sorry....
   Mdau Mesiaki

  0 0

  Mwanadada Rosemary Mizizia anakualika katika Libeneke lake la Mama na Nyumba upate kujua haya na yale kuhusu nyumba na unyumba na pia kuchangia katika mada zilizomo. Kumtembelea BOFYA HAPA

  Globu ya Jamii inampongeza Dada Rosemary kwa kuwa na blog iliyo tofauti na nyingi, hasa ikizingatiwa kuwapo kwa ile dhana potofu kwamba blogs ni kuhusu habari tu. Kuna mada kibao bado hazijaguswa na  zinahitaji wana libeneke kuzishughulikia. 

  Mfano, ukiwa wewe ni seremala, mvuvi ama mshona viatu, fungua blog inayohusu hayo unayoyajua na kamwe hutokosa wasomaji. Nasema haya kwa kuona wengi wanapenda Libeneke tatizo wanadhani blog ni mambo ya habari tu, wakati sio kweli. Blog ni ya kila jambo ama kitu.

  Mbaya zaidi wengi hawana taaluma, vifaa na hata fursa ya kupata habari lakini wanapenda kuleta habari. Wako huru, sawa, kufanya watajkalo lakini dhambi kubwa ya kwanza ya kuendesha blog ni kuwa bingwa wa copy & paste habari na picha za wengine, tena bila idhini. 

  Ushauri kwa anayetaka kuendesha blog ni kuwa na mada yake, jua wasomaji wako na zaidi ya yote, usikose kuweka kitu kipya kila siku ama hata kila saa, ukiweza, ili usiboe wasomaji. Inapendeza kuwa na blogs nyingi iwezekanavyo, mradi isiwe 'sare sare maua' kama ilivyo sasa, ambapo utakuta habari ile ile katika kila blog unayosoma... 

  Usiogope wala usikate tamaa kwa kudhani usipoandika mambo ya habari utakosa wasomaji.Ondokana na dhambi hiyo kuu nawe utaona matunda yake. Kwa msaada wa promotion  na ushauri, wa bure, usisite kuwasiliana nasi kupitia  issamichuzi@gmail.com
  -Ankal

  0 0

  Kijana mdogo Aslay anayetokea kundi la TMK anatisha na ngoma yake ya 'Nakusemea'.

  0 0

  Kikosi cha timu ya Chama Cha waandishi wa habari za Michezo nchini (TASWA FC) kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa kirafiki kati yake na timu ya Bagamoyo Veteran uliofanyika kwenye uwanja wa Mawanakerenge Mjini Bagamoyo jana jioni, ambapo timu ya TASWA FC ilichezea kichapo cha magoli 4-0 na maveterani hao kutoka mjini Bagamoyo,Timu ya Waandishi wa habari ya TASWA FC imeshiriki katika mchezo huo ikiwa ni moja ya programu ya mkutano wa chama hicho unaofanyika leo kwenye hoteli ya Kiromo View mjini Bagamoyo ambao umefunguliwa na Mdau wa Michezo,Ridhiwani Kikwete na Kufungwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ndugu Assah Mwambene.
  Hiki ndicho kikosi cha timu ya Bagamoyo Veteran kilichotoa kichapo kwa timu ya TASWA FC mjini Bagamoyo.
  Baadhi ya waandishi wa habari ambao ni mashabiki wa timu hiyo wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
  Mjumbe wa kamati ya utendaji wa klabu ya Simba Ibrahim Masoud katikati akizungumza na Mzee Willy Chiwango kutoka gazeti la This Day (kulia) na Beny Kisaka mkurugenzi mwanadamizi gazeti la Jambo Leo.
  Mkuu wa Wilala ya Bagamoyo,Mh. Ahmed Kipozi (wa pili kulia) akizungumza na mwandishi mkongwe kutoka Zanzibar Said Salim huku wanahabari wengine wakifuatilia mazungumzo hayo.
  Mchezaji wa timu ya TASWA FC,Juma Pinto (kushoto) akimiliki mpira mbele ya beki wa timu ya Bagamoyo Veterani katika mchezo huo uliofanyika kwenyeuwanja wa Mwanakerenge mjini Bagamoyo
  Mchezaji wa timu ya TASWA FC Shafii Dauda (kushoto) akimiliki mpira huku beki wa timu ya Bagamoyo Veterani akiuwania katika mchezo huo, katikati ni mchezji wa timu ya TASWA FC Mohamed Akida.
  Mshauri wa timu ya TASWA FC,Masoud Sanani akihimiza wachezaji wa TASWA FC kucheza kwa bidii baada ya kuchapwa magoli 4-0 huku wachezaji wa timu hiyo wakishangaa wasijue la kufanya wakati zikiwa zimesalia dakika za majeruhi.

  0 0

  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (wa tatu kulia) akiangalia jana nyavu za kuvulia samaki za Kikundi cha Msifuni kilichopo katika kijiji cha Kemondo wilayani Bukoba ambacho kilipata mkopo kutoka mfuko wa maendeleo ya vijana na kuanzisha mradi wa bwawa la samaki. Kushoto ni Katibu wa kikundi hicho Johanes Joel.
  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kushoto) akiangalia kahawa katika shamba darasa inayolimwa na Ibrahim Mulokozi (kulia) ambaye ni mkazi wa kijiji cha Ibwera wilayani Bukoba aliyenufaika na mkopo wa shilingi laki nne kutoka mfuko wa maendeleo ya vijana. Waziri Dk. Mukangara alilitembelea shamba hilo la kahawa na migomba jana ili kuona fedha za mkopo walizozipata vijana kutoka SACCOS ya Ibwera zimewanufaishaje kimaisha.
  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kushoto) akimuangalia samaki mwenye umri wa miezi mitatu anayefugwa katika bwawa la Kikundi cha Msifuni kilichopo kijiji cha Kemondo wilayani Bukoba ambacho kilipata mkopo kutoka mfuko wa maendeleo ya vijana. Waziri Dk. Mukangara alilitembelea bwawa hilo jana ili kuona fedha za mkopo walizozipata vijana kupitia mfuko wa Halmashauri nimewasaidiaje vijana kujikwamua kiuchumi.
  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kushoto) akipokea taarifa ya SACCOS ya Ibwera iliyopo wilayani Bukoba kutoka kwa Benedicta Peter ambaye ni katibu msaidizi. SACCOS hiyo ilipata mkopo wa shilingi milioni tano kutoka mfuko wa maendeleo ya vijana na kuvikopesha vikundi mbalimbali vya maendeleo vya vijana.
  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (wanne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa SACCOS ya Ibwera na viongozi wa wilaya ya Bukoba wakati alipowatembelea jana ili kuona fedha walizopata kutoka mfuko wa waendeleo ya vijana zilivyoweza kuwasaidia vijana kujikwamua kimaisha.
  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara akiangalia shamba darasa la kahawa na migomba la mkazi wa kijiji cha Ibwera wilayani Bukoba Ibrahim Mulokozi (hayupo pichani) wakati alipolitembelea jana ili kuona fedha za mkopo wa mfuko wa vijana alizozipata kupitia SACCOS ya Ibwera zimemnufaishaje kimaisha. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi. Picha na Anna Nkinda – Maelezo

  0 0

  Mwanamitindo bora wa mwaka 2012 Catherine Masumbiga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Unique Model Photogenic Elizabeth Pertty (kushoto) na Unique Model Talent Vestina Charles mara baada ya kutangazwa kwa mshindi.
  Mwanamitindo wa mwaka 2012 Catherine Masumbiga (katikati) amepatikana jana usiku kwenye shindano lililofanyika kwenye Klabu ya New Maisha jijini Dar es Salaam akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa pili Cesilia Michael (kushoto) na mshindi watatu Amina Ayubu.
  Washiriki waliongia tano bora.
  Washiriki waliongia tano bora.
  Majaji wa shindano hilo kutoka kushoto ni Gymkhana Hilal kutoka Paka Wear , Asia Idarous na Martine Kadinda.
  Wakitumbuiza mashabiki mapema kabla ya kuingia kuonyesha mavazi ya aina mbalimbali.
  Washiriki 12 wa shindano hilo wakiwa wamejipanga tayari kusubiri kutangazwa mshindi.

  0 0


  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege ya Flightlink,Munawer Dhiren akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha usiki iliyokuwa imeandaliwa maalum kwa ajili ya kukutana kwa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo pamoja na familia zao ikiwa ni sehemu pia ya kuuaga mwaka iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana.
   Sehemu ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Ndege ya Flightlink pamoja na familia zao wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo,Munawer Dhiren (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza nao wakati wa hafla ya chakula cha usiki iliyokuwa imeandaliwa maalum kwa ajili ya kukutana kwa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo pamoja na familia zao ikiwa ni sehemu pia ya kuuaga mwaka iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana.
   Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Flightlink wakipozi kwa picha wakati wa hafla ya chakula cha usiki iliyokuwa imeandaliwa maalum kwa ajili ya kukutana kwa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo pamoja na familia zao ikiwa ni sehemu pia ya kuuaga mwaka iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana.
   Picha ya pamoja kwa wafanyakazi wote wa Kampuni ya Ndege ya Flightlink.
  Wakurugenzi wa Kampuni ya Flightlink wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa.


  0 0

  Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia kushinda timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys,Bw. Ridhiwan Kikwete akifungua mkutano mkuu wa chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA unaofanyika kwenye Hoteli ya Kiromo View Bagamoyo mkoani Pwani ambao unajadili mambo mbalimbali ya Maendeleo na changamoto zinazokabili chama hicho.Waandishi wa habari za michezo ambao ni wanachama kutoka vyombo mbalimbali nchini wanahudhuria mkutano huo ambao ni wa siku moja.
  Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA,Bw. Juma Pinto akimkaribisha mgeni rasmi ili kufungua mkutano huo leo asubuhi unaofanyika kwenye hoteli ya Kiromo View Bagamoyo.
  Katibu wa Chama cha Waandishi wa habari za michezo TASWA Bw. Amir Mhando akizungumza katika mkutano huo, kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa TASWA Maulid Kitenge, Mwenyekiti Juma Pinto, Mgeni rasmi Ridhiwan Kikwete na kushoto ni George John Katibu Msaidizi.
  Mtaalam wa SACCOS kutoka Manispaa ya Ilala Bw. Luambano akitoa mada kuweka na kukopa kwa waandishi wa habari wanachama wa TASWA waliohudhuria katika mkutano huo
  Kutoka kulia ni waandishi wakongwe Mwina Kaduguda, Mzee Wlly Chiwango na Mzee Salim Said Salim kutoka Zanzibar wakiwa katika mkutano huo.
  Kutoka kulia ni Shafii Dauda, Erasto na Ibrahim Masoud wakiwa katika mkutano huo.
  Kutoka kulia ni Elizaberth Mayemba , Timzo Kalugira na Crala Alphonce wakifuatilia mada katika mkutano huo.
  Kutoka kushoto ni Elius Kambili, Alfred Lucas na Salum Jaba wajumbe wa kamati ya utendaji ya TASWA wakiwa katika mkutano huo.
  Kutoka kulia ni Mgaya Kingoba, Salum Jaba, Richard Mwaikenda na Tulo Chambo wakifuatilia mada katika mkutano huo.
  Wajumbe mbalimbali wakihudhuria mkutano wa Chama cha Waandishi wa habari za michezo TASWA kwenye hoteli ya Kiromo View mjini nje kidogo ya mji wa Bagamoyo mkoani Pwani .PICHA NA FULLSHANGWEBLOG

  0 0

  Trela la lori lililokuwa limebeba mafuta likiteketea kwa moto mchana huu eneo la Kibamba Darajani jijini Dar es Salaam.haijafahamika mara moja chanzo kutokea kwa moto huo.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Padri Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae mjini Zanzibar anayeuguza majeraha katika taasisi ya mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) jijijini Dar es salaam leo Jumamosi Dsemba 29, 2012 kufuatia kupigwa risasi sehemu za mdomoni na watu wasiojulikana mapema wiki hii wakati akisubiri kufunguliwa geti la nyumbani kwake maeneo Kitomondo Mjini Zanzibar akiwa ndani ya gari aliyokuwa akiendesha akiwa pekee yake. Rais Kikwete amempa Padri Mkenda pole nyingi na kumuombea apate nafuu haraka.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Padri Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae mjini Zanzibar anayeuguza majeraha katika taasisi ya mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) jijijini Dar es salaam leo Jumamosi Dsemba 29, 2012 kukupigwa risasi sehemu za mdomoni na watu wasiojulikana mapema wiki hii wakati akisubiri kufunguliwa geti la nyumbani kwake maeneo Kitomondo Mjini Zanzibar akiwa ndani ya gari aliyokuwa akiendesha akiwa pekee yake. Rais Kikwete amempa Padri Mkenda pole nyingi na kumuombea apate nafuu haraka. PICHA NA IKULU

  0 0


  Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar  

  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema matangazo ya mfumo wa Analogia yatazimwa rasmi katika Mikoa yote ya Zanzibar ifikapo Februari 28 mwakani ili kupisha mfumo mpya wa matangazo kwa njia ya Dijitali.

  Waziri wa habari, utamaduni, utalii, na Michezo Said Ali Mbarouk ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari katika ukumbi wa Habari maelezo kikwajuni mjini Zanzibar kuhusiana na matayarisho ya kuhamia katika mfumo mpya wa matangazo ya Dijitali.

   Amesema Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Kamisheni ya Utangazaji Zanzibar (ZBC) zimeshauriana na kukubaliana kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iingie katika mfumo mpya wa Dijitali kwa awamu ambapo kwa zoni ya Zanzíbar imekubaliwa kuwa February 28 2013 ndio iwe mwisho rasmi wa matangazo ya Analogi.

  Waziri Mbarouk amesema Wizara yake haitozima mitambo ya matangazo ya Analogi ifikapo Disemba 31 bali itakachofanya ni kutangaza kwa pamoja matangazo ya Analogi na Digitali kwa mfumo unaojulikana kitaalamu kama SIMU L CAST hadi itakapofika muda rasmi wa kuhama mfumo wa Analogy.

  Akizungumzia matayarisho ambayo yamefanywa na Wizara yake katika kuukabili mfumo mpya wa Matangazo ya Dijitali Waziri Mbarouk amesema tayari wamejenga kituo cha usambazaji ishara(signals) katika eneo la Rahaleo kitakachokuwa na kazi ya kupokea na kusambaza ishara na mitambo ya uendeshaji.

  Aidha Wizara imetayarisha maeneo matatu Unguja ambayo ni Kizimkazi,Masingini na Nungwi ambapo kwa upande wa Pemba ni Kichunjuu,Mkanjuni na Konde kwa ajili ya kurushia matangazo ya Dijitali.

  Matayarisho mengine ni pamoja na kuandaa utaratibu mzuri wa upatikanaji wa Ving’amuzi na maudhui kwa bei nafuu ambapo amesema vitaanza kuuzwa mwishoni mwa mwezi wa Januari mwakani.

  Amefahamisha kuwa bei ya Ving’amuzi hivyo itakuwa rahisi kuliko vingamuzi vingine ambapo mwananchi atatakiwa kukinunua kwa Sh l50,000 na kukilipia sh l8,000 kwa mwezi ili kupata huduma ya matangazo hayo.

  Amevielezea Ving’amuzi hivyo ambavyo vitakuwa na huduma mbali mbali ikiwemo Mtandao, Video on demand, programme guide, exclusive service yaani mawasiliano ya makundi maalum ambapo pia jumla ya Chaneli 36 za ndani na nje ya nchi zitapatikana kwa uhakika.

  Waziri Mbarouk amesema uzinduzi wa mitambo na matangazo ya Dijitali unatarajiwa kufanyika wakati wa sherehe za Mapinduzi Januari 8 mwakani katika maeneo ya Rahaleo mjini Zanzibar.

  Mabadiliko ya Mfumo wa matangazo kutoka Analogia kwenda Dijitali yamekuja kufuatia agizo lililotolewa na Shirikisho la Mawasiliano la Afrika Mashariki EACO kuwa Nchi wanachama wa Shirikisho hilo ziwe zimehamia katika mfumo mpya wa Dijitali ifikapo mwaka 2013.
   
   
  IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

  0 0


  Come and enjoy New Year's eve on 31st December 2012 in our Night Club and V.I.P Lounge. Reggae mix with free entrance and cocktail for the ladies + surprise gift for the best dancing couple. For more information please call us on 0714075621.

  MAKHOT RESORT located in the middle of Mbezi Beach few meters off old Bagamoyo Road.
  Phone: +255 22 261 7830

  0 0

  Akaja Colonel Abrams na ngoma ya 'Trapped'na kukamata chati si mchezo....

  0 0

  Sijui kazamia wapi siku hizi, ila alipoibuka MB Dogg na ngoma yake ya 'Latifah' ilikuwa taabu mjini...

older | 1 | .... | 4 | 5 | (Page 6) | 7 | 8 | .... | 3272 | newer