Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 597 | 598 | (Page 599) | 600 | 601 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Geita Gold Mine (GGM) has signed a five-year contract worth over TZ 680million to support Lake Victoria’s first medical boat, which is an initiative of The Jubilee Hope Medical and Dental Programme - a partnership between the African Inland Church of Tanzania and the Vine Trust.

  As part of the contract, GGM will cover all fuel and maintenance costs for the boat until 2019, thereby ensuring that the 450,000 residents of the Lake Victoria islands have access to the much needed primary health care services. It is anticipated that the Programme will provide medical and dental care to about 100,000 residents per annum.

  “GGM is proud to participate in this noble initiative,” said Managing Director of GGM, Michael Van Anen. “This is in keeping with our core value of leaving our host communities with sustainable futures.”


  Willie McPherson, Vine Trust CEO, speaking of the project, said “I’m delighted with the optimism and good will that Jubilee Hope is being greeted by within the Lake Zone of Tanzania and the wide support amongst those concerned with the provision of primary health care in the island communities” Jubilee Hope is the third medical ship we have launched to benefit remote communities in developing countries. 
  Other similar ships treat their one-millionth patient on the Peruvian Amazon in South America.


  GGM has previously funded a number of health care projects in the Geita region, which include the construction of dispensary facilities for the local health centres, the upgrade of Regional Geita hospital operating theatre and maternity ward and the construction of the Geita HIV/AIDS and Information Centre in Geita Town.

  0 0

   Mafundi wa Taa za Barabarani jijini Dar wakiifanyia marekebisho moja ya taa hizo zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam iliyokuwa na hitilafu.


  0 0

   Rais Jakaya Kikwete (kulia) akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Menejimenti ya Barclays Africa, Bi. Mizinga Melu  (wa tatu kushoto) alipokwenda kumuaga Ikulu, Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Bi Rukia Mtingwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bw. Pius Tibazarwa. Bi Melu aliyekuwa mkurugenzi tendaji wa benki hiyo alichaguliwa kushika wadhifa huo hivi karibuni.

   Rais Jakaya Kikwete (kulia) akimsindikiza  Mtendaji Mkuu wa Menejimenti ya Barclays Africa Bi. Mizinga Melu  alipokwenda kumuaga Ikulu, Dar es Salaam leo.


   Rais Jakaya Kikwete  katika picha ya kumbukumbu na  Mtendaji Mkuu wa Menejiment ya Barclays Africa, Bi Mizinga Melu  (wa pili kushoto) alipokwenda kumuaga Ikulu, Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Bi Rukia Mtingwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa  NBC, Pius Tibazarwa. Bi Melu aliyekuwa mkurugenzi tendaji wa benki hiyo alichaguliwa kushika wadhifa huo hivi karibuni.
   Rais Jakaya Kikwete akiagana na Mtendaji Mkuu wa Menejiment ya Barclays Africa, Bi Mizinga Melu (wa pili kushoto), alipokwenda kumuaga Ikulu, Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Bi. Rukia Mtingwa, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji  wa NBC, Bw. Pius Tibazarwa na Meneja Mahusiano wa benki hiyo, Bw. William Kallaghe. Bi Melu aliyekuwa mkurugenzi mkurugenzi wa benki hiyo alichaguliwa kushika wadhifa huo hivi karibuni. PICHA NA IKULU

  0 0

  Wakurugenzi wote wa Airtel wakiongozwa na mkuu wao Sunil Colaso (kati) wakikata keki leo wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja ambapo inaadhimishwa duniani kote kuanzia tareh 6, Airtel imejipanga kuadhimisha wiki hii kwa kuwashuru wateja wake wote, kuongeza motishaa kwa watoa huduma wake wote nchini kuendelea kuhudumia wateja, pamoja na kuhamasisha kila mtoa huduma nchini kufahamu umhimu wa mteja.
  Mkurugenzi mkuu wa Airtel Tanzania Bw Sunil Colaso akiongea na wafanyakazi wote pamoja na wanahabari leo hii (hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja leo katika makao makuu ya Airtel, Airtel inaadhimisha wiki hii kwa kuwashuru wateja wake wote, kuongeza motishaa kwa watoa huduma wake wote nchini kuendelea kuhudumia wateja, pamoja na kuhamasisha kila mtoa huduma nchini kufahamu umhimu wa mteja.
  Mkurugenzi wa Airtel huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba akiongea na wafanyakazi wote pamoja na wanahabari (hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja leo katika makao makuu ya Airtel, Airtel inaadhimisha wiki hii kwa kuwashuru wateja wake wote, kuongeza motishaa kwa watoa huduma wake wote nchini kuendelea kuhudumia wateja, pamoja na kuhamasisha kila mtoa huduma nchini kufahamu umhimu wa mteja.
  Meneja wa huduma kwa wateja wa Airtel Bw, Deo Hugo akielezea jinsi Airtel ilivyojipanga kutimiza dhamira yake ya huhudumia wateja vyema hata baada ya wiki ya huduma kwa wateja kuisha, moja kati ya huduma zitakazoendele ni pamoja na kuwatembelea wateja kwenye soko, kuwapigia simu na kujadili nao mambo muhimu ya mawasiliano.


  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Dkt. Eng. Binilith Satano Mahenge (wa kwanza kushoto,) akiwa pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais Magdalena Mtenga,(mwenye nguo nyekundu) na Dr. Robert Ntakamalenga, Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji-NEMC katika ziara ya kukagua viwanda jijini Dar Es Salaama leo.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Dkt. Eng. Binilith Satano Mahenge, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kiwanda cha Bin Fijaa Industry Bwana Ahmed Abdallah, jinsi wanavyo tumia mashine na maligafi mbalimbali katika kuzalisha mifuko. Kiwanda hiko kipo barabara ya Nyerer jijini Dar Es Salaam.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Dkt. Eng. Binilith Satano Mahenge, akikagua mifuko inayozalishwa na kiwanda cha Tanplast Ltd anayemuonyesha Waziri mifuko hiyo ni Bwana Kaushal Josh ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Dkt. Eng. Binilith Satano, akizungumza na Waandishi wa habari baada ya kuhitimisha ziara yake ya kukagua viwanda mbalimbali vya jijini Dar Es Salaam.

  0 0

  Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akimkabidhi Mkurugenzi wa Afrika wa kampuni ya TE (TE Connectivity) Bi. Patricia Testa kitabu kinachobainisha fursa za uwekezaji Tanzania. Bi. Patricia amemtembelea Balozi Kamala leo Ofisi kwake Brussels kumweleza mipango ya kampuni yake kuingia katika soko la Tanzania. Pamoja na mambo mengine Balozi Kamala ameishauri kampuni hiyo kushiriki ziara ya Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Ubelgiji itakayofanyika Tanzania mwezi Novemba mwaka huu.

  0 0


  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Leonidas Gama aliyelazwa kwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Paschal Mabiti aliyelazwa kwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba Mhe. Dkt Henry Mwijarubi Nyamubi aliyelazwa kwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo.   0 0

  Dear Family & Friends,
   On the outside chance that you have not yet donated 1 minute of your life to vote for Under The Same Sun (UTSS), PLEASE donate that minute now – SEE BELOW.

  If you have voted but did not ask your family and friends to do the same, PLEASE do it now. If you are part of a business, church or student body, please send this email to them.

  Voting ends October 11th. Thanks to so many voters, UTSS has taken over first place today BUT we must remain in the top 3 to be eligible for the grant.

  Click here to see the voting results so far:


  IF YOU HAVE NOT YET VOTED, KEEP READING:
   UTSS has become eligible for a One Hundred Thousand Euro grant from the Netherlands. Every year, the Dutch Ministry of Foreign Affairs awards the Human Rights Tulip to a human rights defender who promotes and supports human rights in innovative ways.

  UTSS has been shortlisted to 1 of 30 charities from the original 1 of 160. The next phase of shortlisting will bring us to 1 of 3 charities who become eligible for the grant. This next phase of shortlisting will occur through a website voting system.

  Please vote for UTSS.

  FIRST – click here
  THEN – follow these INSTRUCTIONS: 
  -        Click on the pink VOTE icon on the right side of the page to proceed to the voting ballot
   -        Then enter your email address
   -        Then click on the VOTE icon again
   -        Within a few seconds you should receive a confirmation email – MAKE SURE YOU CONFIRM YOUR VOTE.
   -        If the confirmation email does not arrive within a few seconds, check your spam mail
   DONE
   Thanks so much for your vote,

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiangalia fuvu la aliyekuwa Chifu wa Wahehe, Mkwawa alipotembelea Makumbusho ya shujaa huyo aliyepambana na wajerumani na kujiua kwa bunduki baada ya kuona yupo hatarini kukamatwa na wajerumani.
   Picha ya kuchora ya Chifu Mkwawa
   Mrithi wa Chifu Mkwawa, Abdul Adam Mkwawa akimkaribisha Kinana kutembelea makumbusho ya Chifu Mkwawa katika Kijiji cha Kalenga, Iringa Vijijini wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2010. 
   Kinana akivishwa kilemba
   Kinana akiwa katika picha ya pamoja na wazee wa kimila baada ya kukabidhiwa mkuki.

  Kinana akiwa amekaa na Chifu Abdul Mkwawa pamoja na wazee wa kimila wa kabila la Wahehe.

  0 0


    Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt, Rehema Nchimbi akitoa ufafanuzi kuhusu makabidhiano ya Rasimu ya katiba yatakayofanywa kati ya viongozi wa Bunge maalumu la katiba watakao kabidhi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Jakaya Kikwete na wa Zanzibar Dkt Mohamed Sheni kwa waandishi wa habari, makabidhiano hayo yatafanyika Oktoba 08, 2014 katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.(Picha na John Banda wa Pamoja Blog)
    Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt, Rehema Nchimbi kwa makini wakati alipokua akielezea kuhusu makabidhiano ya Rasimu ya katiba yatakayofanywa keshokutwa Oktoba, 08 mwaka huu katika uwanja wa jamhuri ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete na Dkt Mohamed Sheni ndiyo watakabidhiwa.

  WANANCHI wa mkoa wa Dodoma na mikoa jirani wametakiwa kufika katika uwanja wa jamhuri mjini Dodoma Jumatano ya oktoba 8, 2014   kwa ajili ya kushuhudia tukio la kihistoria kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein kukabidhiwa katiba iliyopendekezwa na bunge maalumu la katiba.
  Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema Tukio hilo litafanyika hapa mjini Dodoma kwenye viwanja vya Jamhuri kuanzia saa 6:00 Mchana na Milango ya uwanja wa itafunguliwa kuanzia saa 12:00 asubuhi.
  Mkuu huyo wa Mkoa amesema watu watakaojitokeza ili kushuhudia tukio hilo watakuwa wengi hivyo kwa kuzingatia kuwa milango ya uwanja wa Jamhuri itafunguliwa mapema, wananchi wanashauriwa kuwahi kufika viwanja vya Jamhuri na kuhakikisha kuwa kila mtu atakayehudhuria awe tayari amekaa kwenye nafasi yake ifikapo saa 5:00 asubuhi.

  Dkt Nchimbi amesema tukio hilo litahudhuriwa na Marais wastaafu wa Tanzania, Marais wastaafu Zanzibar, Viongozi wa kitaifa na watendaji wakuu, Viongozi wakuu wastaafu, Maspika wastaafu, Waheshimiwa Mabalozi na wawakilishi wa Taasisi za Kimataifa, Taasisi za Kidini, Taasisi zisizo za kiserikali na wamiliki wakuu wa vyombo vya habari.


  Amesema Vilevile kutakuwepo na Makundi mbalimbali kutoka mikoa ya Tanzania bara na Zanzibar. Makundi hayo ni pamoja na Wafugaji, Wakulima, Wavuvi, Wanawake, Vijana, Wazee, Wachimbaji madini wadogo, Walemavu na Wasanii.


  Aidha Dkt, Nchimbi ameseama Tukio hilo la Kihistoria litatanguliwa na tukio muhimu na maalum  la kuomba Dua na Shukrani kwa kukamilika salama kwa shughuli za “Bunge Maalum la Katiba” hapa Mkoani Dodoma katika viwanja vya Nyerere Squere hapo kesho saa 10 jioni.

  0 0

  Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
  Katibu wa Klabu ya Ikulu Ramadhani Bendera ameipongeza klabu yake kwa kufanya vizuri katika mashindano ya Shirikisho la Michezo ya watumishi wa Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayoendelea mjini morogoro. 
  Bendera alitoa pongezi hizo kwa klabu yake kufuatia ushindi waliopata katika michezo mbalimbali iliyochezwa leo katika uwanja wa Jamhuri. 
  Timu za Ikulu zilizofanikwa kuingia hatua ya robo fainali za mashindano hayo ni timu ya mchezo wa mpira wa pete, mchezo wa kuvuta kamba wanaume na ya wanawake. 
  Katika mchezo wa mpira wa pete, timu ya Ikulu imewabwaga timu ya Ulinzi kwa magoli 52-10 na hivyo kuingia hatua ya robo fanali na kusubiria timu zitakazofuzu hatua hiyo. 
  Kwa upande wa mchezo wa kuvuta kamba, timu ya Ikulu wanaume imeibuka washindi kwa kuwavuta timu ya Wizara Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi 2-0 wakati timu ya wanawake ya Ikulu nao wameivuta timu ya Wizara Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kwa mizunguko yote miwili ambapo hadi mwisho wa mchezo Ikulu wameshinda 2- Mifugo 0. 
  Aidha Bendera amesema kuwa maandalizi mazuri ya klabu yake na wachezaji kujituma ndio msingi wa ushindi wao wa leo kaatika michezo hiyo. 
  Mashindano ya SHIMIWI nchini lengo lake kuwajengea watumishi afya bora na kujenga umoja wa kitaifa kupitia Wizara na mikoa mbalimbali ambapo michezo inawakujenga ari ya ushindani ndani ya watumishi wa umma na hatimaye kuleta ufanisi na tija kwa taifa wakati wakitekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.
   Timu ya Ikulu ya kuvuta kamba wanawake wakiwa kwenye mechi za hatua ya timu 32 wakiwavuta timu ya Wizara Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kwa kuwashinda kwa 2-0 wakati wa mashindano ya SHIMIWI taifa leo uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro
   Timu ya Ikulu ya kuvuta kamba wanaume wakiwa kwenye mechi za hatua ya timu 32 wakiwavuta timu ya Wizara Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kwa kuwashinda kwa 2-0 wakati wa mashindano ya SHIMIWI taifa leo uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

   Mchezaji Monica Kassy (GS) (wa kwanza kushoto) wa timu ya mpira wa pete ya Ikulu akiwa amefanikiwa kufunga goli wakati wa mechi kati ya timu ya Wizara Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi katika mashindano ya SHIMIWI yanayoendelea mjini Morogoro.

   Mchezaji wa timu ya mpira wa pete ya Ikulu Rukia Kibayasa akimiliki mpira wakati wa mchezo dhidi ya Ikulu na Wizara Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi katika mashindano ya SHIMIWI yanayoendelea mjini Morogoro.
  Sehemu ya  ya mashuhuda wa mchezo wa mpira wa pete kati ya Ikulu na Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi. Picha zote na Eleuteri Mangi-MAELEZO

  0 0


  Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Ujerumaninchini Tanzania, Egon Kochanke (katikati) na mkewe Wendy Marshall Kochanke wakimkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tafrija hiyo. 
  Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Ujerumani nchini Tanzania, Egon Kochanke akisoma hotuba yake.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akisoma hotuba yake. 
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Ujerumani nchini Tanzania, Egon Kochanke wakigonganisha glasi kama ishara ya kusherehekea tafrija hiyo. 
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Ujerumani nchini Tanzania, Egon Kochanke na mke wa Balozi wakikata keki maalum  kama ishara ya kusherehekea tafrija hiyo.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA  0 0

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka akisikiliza maelekezo kutoka kwa Meneja wa Mawasiliano wa Shirika la Nyumba la Taifa, Yahya Charahani. 
  Katika ujumbe wake wa siku ya makazi mwaka huu Waziri Tibaijuka ameviagiza vyombo vinavyohusika na upangaji miji kuongeza zaidi kazi ya upimaji wa makazi na kisha kuyaboresha makazi yaliyokwishavurugika kwa hivi sasa kwa mujibu wa takwimu za UN HABITAT, robo ya idadi ya watu wanaoishi mijini kote duniani na Tanzania ikiwamo wanaishi katika mitaa duni ambayo yana mazingira hatarishi, huku hali ya maisha ikiwa yenye uhaba wa huduma muhimu, ujumbe wa mwaka huu ni "Sauti kutoka Makazi Duni"
  Waziri Tibaijuka ameziagiza Halmashauri za Miji, Manispaa na Wilaya kujenga nyumba angalau 100 kwaajili ya wafanyakazi wake ili kwanza kupanga mij, lakini pia kupunguza tatizo la makazi holela yanayoikabili nchi kwa sasa. (Picha kwa hisani ya Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Jamii cha Shirika la Nyumba la Taifa)

  0 0

    Mbunge we jimbo la Kigamboni Dr. Faustine Ndugulile akikata utepe kufungua rasmi kiota kipya Mji Mwema Kigamboni. Kiota hicho kinaitwa  Fursat Dhahabiyya.

   Wadau mbalimbali wakijivinjari ndani ya kiota kipya cha Fursat Dhahabiyya Kilichopo Mji Mwema Kigamboni
   Mwonekano wa Ndani wa Kiota Hicho

  0 0


  Mchakato wa uuzaji na ununuaji wa bidhaa umerahisishwa sana kwa kadri waendashaji wa makampuni ya biashara kwa njia ya intaneti wanavyozidi kuwa wabunifu na wagunduzi zaidi.

  Kaymu Tanzania, kampuni inayoongoza kwa kuuza na kununua vitu kwa njia ya mtandao imejitanua zaidi baada ya kuzindua app (programu ya simu) yake Septemba 2014.

  Kaymu Tanzania imezindua huduma zake za kwanza za programu ya simu nchini, hivyo kuwawezesha watumiaji wa Android kufanya manunuzi ya bidhaa na kuweka oda moja kwa moja kupitia simu zao za viganjani, na kuwawezesha pia wauzaji kusimamia maduka na oda zao kwa uharaka na uwepesi zaidi.

  Akizungumza na wanahabari kwenye makao makuu ya kampuni hiyo hapo Mikocheni- Dar-es-salaam, Mkurugenzi mtendaji wa Kaymu Tanzania Erfaan Mojgani alisema, “Programu hii ina matumizi yote yanayotakikana, kuwawezesha wanunuaji kutimiza muamala wowote ikiwemo: kutembelea maduka na kuangalia aina tofauti za bidhaa mbali mbali, kuweka oda, na hata kuwasiliana moja kwa moja na wauzaji katika mchakato huo"

  Kwa kuongezea, application (programu) hii – inayopatikana kwenye Google Play Store – haina makato yoyote ya pesa kwa watumiaji wa "smartphone" wanaotumia mtandao wa Tigo. Mnunuaji au muuzaji yoyote anaweza akadownload hii application, na akafungua akaunti yake na kuitumia kwa kupitia intaneti.

  “Faida za programu hii ni kubwa pia kwa wauzaji, ikiwarahisisha uwekaji wa picha za bidhaa mpya na ikiwapa wepesi wa kusimamia accounts zao, kuhariri orodha ya bidhaa, na kuona mauzo yao” Erfaan aliongezea.


  Kwa kutambua kuwa asilimia kubwa ya ongezeko la watumiaji wa intaneti nchini Tanzania wanatumia intaneti kupitia simu za mikononi, Kaymu imedhihirisha jinsi ilivyojikita kwenye suala la ubunifu na kuwapa wateja wao uwezo wa kutumia hii app (programu) kwa urahisi zaidi. Zaidi ya hayo, kuonyesha kuwa watumiaji wa iphone hawajasahaulika, Erfaan aliongezea kuwa application hii kwa watumiaji hao tayari iko katika matengenezo.


  0 0

  Kushirikiana katika maswala mbali mbali ili kuweza kufikia malengo ni jambo kubwa lililopata kusikika katika mkutano mkuu wa mwisho wa mwaka unaoendelea nchini Kenya unaojadili changamoto mbali mbali za sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. 

  Swala la usalama katika mitandao limepata kuangaliwa na changamoto mbali mbali katika mijadala Rasmi (Ndani ya Kikao) na isiyo rasmi (tuwapo nje ya ukumbi wa mkutano) zilipata kuangaliwa kwa ukaribu. 

  Swala uhimu nililo jifunza ni jinsi uhalifu mtandao katika mataifa haya mawili Kenya na Tanzania yanavyofanyika na kujua ya kuwa kubadilishana mawazo katika hili litasaidia kujipanga kukabiliana na uhalifu mtandao ambao tayari kwa nchi ya Kenya umeendelea kukua.
  Ikiwa bado kwa Tanzania haujaonekana sana huku Kenya nilijifunza pia ili kuweza kujipanga kabla ya uhalifu usika kuweza kushika kasi. 
   Namna mbalimbali zinazotumika na wenzetu wa Kenya ambao wameathirika sana na uhalifu mtandao (Mfano: Wakati Mkutano unaendelea – Baadhi ya mifumo mtandao ya serikali iliripotiwa kuangushwa na wahalifu mtandao) kwenye kukabiliana na uhalifu mtandao huku tukiangalia kwa karibu namna ambavyo teknolojia zinazotumika kupambana na uhalifu mtandao katika nchi hiyo zinavyoweza kutoa msaada wa kina kwenye makabiliano na uhalifu mtandao Nchini Tanzania.
   Washiriki wa mkutano mkuu wa mwisho wa mwaka uliowahusisha wakuu wa TEHAMA wa sekta mbali mbali mbali nchini Kenya wakiendelea na Mkutano wao jijini Nairobi kujadili mambo mbalimbali na changamoto zake
   Mkutano ukiendelea
   Mshiriki akitoa maoni yake
   Dr. Waudo Siganga akiongea wakati wa kufungua  mkutano huo. 
   Mshiriki akitoa yake machache
  Picha ya pamoja ya washiriki  nje ya ukumbi.

  0 0
 • 10/06/14--17:02: Nathan mpangala live!

 • 0 0

  Imperial Secondary School situated on a 27 acres, located on Plot No. 1, Block “ C “ Msolwa – Chalinze, along Dar es Salaam – Morogoro road.
  Imperial Secondary School is a friendly, co-educational, boarding school that caters for students throughout their secondary education. At Imperial Secondary School we cultivate students’ desires to learn through questions and think critically. Personal excellence is the goal for each student, as they are inspired to achieve at the best level in ways best suited to each individual.
  The school has a committed team of teachers who are at best in their chosen fields. The methodology followed to impart education is a good mix of conventional and sophistications utilizing the latest in teaching gadgets and techniques. We put in our best efforts to help students pursue their goals, achieve their dreams and find their niches in society. Our main goal to equip every student not only with the best education, but create in each student a character of high moral standards, who will become in future a responsible citizen of his country.
  We look forward to seeing you and your family.
  Karibuni
  Iryna Kanyoko
  School Principal

  0 0
 • 10/06/14--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Linah - Ole Themba

older | 1 | .... | 597 | 598 | (Page 599) | 600 | 601 | .... | 3283 | newer