Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

WANAMICHEZO , WANANCHI WAJITOKEZA KUPIMA AFYA BANDA LA NHIF UWANJA WA JAMHURI MOROGORO

$
0
0
Na John Nditi, Morogoro

MAMIA ya wanamichezo na wananchi wa Mkoa wa Morogoro, wameendelea kujitokeza kwa wingi katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ili kupima afya zao.

NHIF Mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na Makao makuu , wanaendesha zoezi la upimaji wa afya kwa wanamichezo wa Shimiwi sambamba na wananchi wa mkoa huo ikiwa ni sehemu ya majukumu yake ya kutoa huduma kwa wanachama wake na wananchi kwa ujumla.

Zoezi hilo lililoanza Septemba 27, mwaka huu na litaendelea hadi Oktoba 11, mwaka huu siku ya kilele cha mashindano ya 34 ya Shimiwi yanayofanyika mkoani Morogoro ni la bure.

Meneja wa NHIF Mkoa wa Morogoro, Rose Ongara, alisema hayo leo ( Sept 29) wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii, kwenye banda la Mfuko huo lililipo ndani ya uwanja wa Jamhuri wa hapa.

Hata hivyo alisema , NHIF ni wadau katika kusaidia michezo ya Shimiwi kwa kujitolea kupima afya za wachezaji kabla ya mchezaji hawajaanza kushiriki kucheza ama baada ya kucheza michezo yao mbalimbali.

Kwa mujibu wa Meneja wa NHIF Mkoa wa Morogoro, kuwa katika zoezi hili , wanamichezo na wananchi wa mkoa huo watapimwa shinikizo la damu (BP), Kisukari,uzito na urefu kwa wahusika na kuainisha uwiano kati ya uzito na urefu na wanaokutwa na matatizo watapewa ushauri wa kilaalamu na madaktari wa Mfuko huo waliopo kwenye banda hilo.

Hivyo alitumia fursa hiyo kuwaomba wanamichezo wa Shimiwi sambamba na wengine pamoja na wakazi wa Morogoro kuutumia muda huyo kwa kujitokeza katika uwanja wa Jamhuri ili kupima afya zao .
Baadhi ya wafanyakazi wa NHIF wakiwajibika kikamilifu kuwahudumia wateja wao ambao ni wanamichezo wa Shimiwi na wananchi wa kawaida ndani ya Uwanja wa Jamhuri wa Morogoro.
Baadhi ya watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakiwa kazini ndani ya uwanja wa Jamhuri wa Mjini Morogoro, kwenye mashindano ya Shimiwi 2014 wakiwa tayari kwa uwajibikaji.
Daktari wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya , akimpima mmoja wa wanamichezo wa Shimiwi mwenendo wa msukumo wa damu kabla ya kuanza mashindano .
Daktari wa NHIF akichukua sampuli ya damu ya mteja wake ambaye ni mwanamichezo , wakati wa zoezi la upimaji wa afya.
Mshiriki wa michezo ya Shimiwi 2014 akipima uzito na urefu kwenye banda la NHIF lililopo uwanja wa Jamhuri wa Morogoro.
Wananachi wa Morogoro na wanamichezo wakiwa katika upimaji wa afya zao kwenye banda la NHIF katika uwanja wa Jamhuri Morogoro.

MPENDE MWANAO......

MEREMETA NA HASSANALI collection launch in Harare

$
0
0



 
MEREMETA NA HASSANALI collection launch in Harare, Zimbabwe,  on 26th  September during  at the Zimbabwe Fashion week



 P
Mustafa Hassanali comes out for the bow during the  MEREMETA NA HASSANALI collection launch in Harare, Zimbabwe,  on 26th  September during  at the Zimbabwe Fashion week.



TASWIRA TOKA BUNGE MAALUM LA KATIBA MJINI DODOMA LEO

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mjumbe wa Bunge Maalum la katiba, Kapteni John Komba, Bungeni mjini Dodoma Septemba 29, 2014.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Fahmi Dovutwa wakiteta, Bungeni Mjini Dodoma Septemba 29, 2014.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Pandu Ameir kificho (kushoto) na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi wakiteta, Bungeni mjini Dodoma Septemba 29, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza, Bungeni Mjini Dodoma Septembe 29, 2014.

MFUMO DUME NA MAWAZO MGANDO: KIKWAZO USHIRIKI WA MWANAMKE KATIKA UONGOZI

$
0
0
20140924_085545
Mkurugenzi Mtendaji wa Uvinza FM Radio, Nuru Kalufya akisimamia usajili wa washiriki wa mafunzo ya Maadili, Jinsia na Kuandika Habari za Migogoro yaliyoanza katika kijiji cha Uvinza, wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma tarehe 24 Septemba hadi 01 Oktoba 2014.

Na Mwandishi wetu, Uvinza.
Imethibitishwa kwamba mfumo dume ulioota mizizi katika jamii kwa kisingizio cha mila, desturi na dini unachangia kwa kiasi kikubwa katika unyanyasaji wa mtoto wa kike na mwanamke nchini.

Hayo yalithibitishwa na washiriki wa mafunzo ya maadili na jinsia yanayofanyika katika kijiji cha Uvinza mkoani Kigoma wakati wakichangia mada ya Jinsia na Vyombo vya Habari iliyowasilishwa na mkufunzi kutoka Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi Rose Haji Mwalimu.

Mshiriki kutoka Loliondo Joseph Munga ambae alizungumzia jinsi gani mfumo dume mgando unavyonyima haki za mtoto wa kike wa Kimasai, alisema kwamba mtoto wa kike hapaswi kwenda shule, kuna kiwango cha juu cha shinikizo la ndoa za utotoni, ukeketaji na wanawake kutokuwa na mamlaka ya kufanya maamuzi.

“Ubaguzi unaanza katika familia, mtoto wa kike hana haki ya kuchagua mume anayemtaka au lini aolewe. Mtoto huyo huyo ni lazima akeketwe kwa sababu mtoto wa kike asiyekeketwa anaonekana ni laana katika familia na hawezi kupata mume. Kutokana na sababu hizo watoto wa kike huridhia kukeketwa ili waondoe laana hiyo lakini pia kwa kushinikizwa na wazazi wa kike.”

Hadi leo haijathibitishwa ni laana gani huwapata wasichana wasiokeketwa kwa maana kuna baadhi yao ambao hawakukeketwa, wameolewa na wanaendelea na maisha ya kawaida.
20140924_085927
Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Uvinza FM Radio Bi. Nuru Kalufya wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Maadili, Jinsia na Kuandika Habari za Migogoro katika maandalizi ya uchaguzi mkuu 2015.

Rais Kikwete apongeza ushirikiano wa Chuo Kikuu cha Rutgers na Tanzania

introducing uganda's ABBA MARCUS: GAME OVER from LEONE ISLAND MUSIC EMPIRE 2014.

$
0
0
Says producer Jose Chameleone; "It started with some free styles,Went down to paper and finally out! Its amazing to work with young people with Talent!!! Enjoy the works and effort of this 8year old. 

mwaliko wa mnuso wa sherehe za nondozzz kwa mheshimiwa diwani Clement Bocco

$
0
0
Mimi Clement Bocco, napenda kuwakaribisha marafiki zangu wote, madiwani wenzangu, wanakwaya wenzangu wa kkkt Kijitonyama, wanasiasa wenzangu, ndugu na jamaa wote mje kufurahi pamoja na familia yangu kwenye sherehe ya mahafali (graduation) yangu ya Masters kwenye chuo cha IFM jijini Dar es salaam mwezi ujao tarehe 10.10.2014. 
Baada ya ratiba ya chuoni itafuatiwa na tafrija itakayofanyika kwenye ukumbi wa Pine Lodge jirani na Bahari Beach Hotel kuanzia saa 12:30 jioni.
Hakuna kiingilio. KARIBUNI WOOOTE
Kwa maelezo zaidi piga 0754-073014

MARIE STOPES TANZANIA YAJIVUNIA USHIRIKIANO WAKE NA SERIKALI

$
0
0
 Na Mwandishi Maalum, New York 
 Ushirikiano na uhusiano mzuri baina ya Serikali na Shirika lisilo la Kiserikali la Marie Stopes umeliwezesha shirika hilo kuwafikishia wananchi wengi zaidi huduma mbalimbali za afya zikiwamo za uzazi wa mpango 
Hayo yameelezwa  na Mwakilishi Mkazi wa Marie Stopes nchini Tanzania, Bi. Ulla E. Muller wakati alipomtembelea na kufanya mazungumzo na Balozi Tuvako Manongi, Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa. 
“ Tunafanya kazi kwa karibu sana na serikali na kwa kweli tumekuwa na uhusiano nzuri na ambao tunajivunia, uhusiano ambao pia nimekuwa nikiueleza kwa wafadhili wetu mbalimbali wakiwamo niliokutana nao hapa New York.”
Akaeleza Kama sehemu ya kudhihirisha uhusiano huo na serikali amesema Shirika lake kwa nyakati tofauti wamekuwa wakizitumia hotuba mbalimbali za Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete hususani zile zinazohusu masuala ya afya bora na uzazi salama. 
Akabainisha kuwa matokeo hayo ya ushirikiano na maelewano na serikali, siyo tu yamewezesha kuwafikia wananchi wengi wanaohitaji huduma mbalimbali za afya hasa wale walio maeneo yasiyofikika, bali pia kumelifanya Shirika lake kuingia katika utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa. 
Bi. Muller ambaye kwa mara ya kwanza alifika nchini Tanzania mwaka 1994 na kurudi tena miaka miwili iliyopita anasema Tanzania inasonga mbele kimaendeleo jambo analosema ni la kujivunia. Amesema. 
“ Nilifika mara ya kwanza mwaka 1994 na kuondoka lakini miaka 20 ya kuifahamu kwangu Tanzania ninaona mabadiliko makubwa kwa nchi hii mabadiliko ambayo kwa mtu au mgeni wa muda mfupi hawezi kuyaona, lakini mimi nimeona tofauti kubwa ya wakati huo na sasa”. 
 Pamoja na kujikita katika utoaji na usambazaji wa huduma za afya salama ya uzazi, uzazi wa mpango na huduma nyinginezo, Mwakilishi Mkazi, amemwambia Balozi kuwa Shirika lake pia linataka kuwekeza zaidi kwa vijana ambao ndio wengi nchini Tanzania. 
Amesema takwimu za idadi ya watu zinaonyesha kuwa vijana ndiyo wengi zaidi kuliko kundi jingine la jamii. Ni kwa sababu hiyo anasema kuna kila sababu ya kuwekeza katika kuwasaidia vijana ili pamoja na mambo mengine kuongeza kasi ya kuupiga vita umaskini. 
Kwa upande wake Balozi Tuvako Manongi amesifu na kushukuru mchango wa Marie Stopes katika kusambaza huduma zake kwa walengwa mbalimbali na kubwa zaidi kwa kufanya kazi kwa karibu na Serikali. 
Balozi amesisitiza haja na umuhimu wa Mashirika hayo yasiyo ya kiserikali kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia vipaumbele vya Kitaifa kwa kuwa ndivyo vyenye maslahi zaidi kwa watanzania.
Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Tuvako Manongi akiwa na   Mwakilishi Mkazi wa MARIE STOPES TANZANIA Bi. Ulla E. Muller aliyefika  Uwakilishi wa Kudumu  na kisha kuwa na mazungumzo na Balozi.  Bi. Muller pamoja na kuelezea shughuli za  Shirika lake amesema   anajivunia na kuridhishwa  na ushirikiano  uliopo baina ya  Serikali na Shirika lake, ushirikiano ambao anasema amekuwa akiuelezea kila  alipokutana na wafadhili wanaosaidia miradi mbalimbali  nchini Tanzania.

beauty creation salon and spa @ mbezi beach, dar es salaam

RAIS KIKWETE KUFUNGUA BARABARA YA MWENGE-TEGETA KESHO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Mwenge- Tegeta utakaofanyika tarehe 1 Oktoba 2014.

Ufunguzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta wenye urefu wa Kilomita 12.9, utafanyika kuanzia saa nne asubuhi katika eneo la Lugalo njia panda ya Kawe.

Upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.

Taarifa hii imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini(GCU)
Wizara ya Ujenzi

Mahojiano na Dr Patrick Nhigula. Mgombea u-Rais wa DICOTA

$
0
0
Karibu katika mahojiano kati ya Mubelwa Bandio wa Kwanza Production na Dr Patrick Nhighula, mgombea wa nafasi ya uRais wa DICOTA 2014. Mbali na kuielezea DICOTA yenyewe, pia ameeleza nia yake kugombea nafasi hiyo Karibu umsikilize

PROGRAMU MPYA YA KUJIFUNZA SOMO LA HISABATI KWA KUTUMIA SIMU ZA MIKONONI YAZINDULIWA JIJINI DAR LEO

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia,Mh.Jonh Mgodo akizungumza mapema leo mbele ya Wanahabari kuhusiana na uzinduzi wa Programu mpya ya kujifunza somo la hisabati kwa kutumia simu za mikononi.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia,Mh.Jonh Mgodo akizungumza mapema leo mbele ya Wanahabari katika ukumbi wa COSTECH,Sayansi Kijitonyama,jijini Dar kuhusiana na uzinduzi wa Programu mpya ya kujifunza somo la hisabati kwa kutumia simu ya mikononi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia,Mh.Jonh Mgodo (wa tatu shoto) akioneshwa na mmoja wa wataalamuwa programu hiyo mpya ya kujifunza somo la hisabati kwa kutumia simu ya mikononi,iliyozinduliwa leo inavyoweza kufanya kazi katika simu za mikononi.
 Mmoja wa Wataalamu wa mradi huo wa Programu mpya ya kujifunza somo la hisabati kwa kutumia simu za mikononi,kutoka Nokia Mobile Mathematics,Bi.Riita Vanska akifafanua jambo kwa wanahabari na wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo iliyofanyika leo katika ukumbi wa COSTECH,Sayansi Kijitonyama,jijini Dar.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia  COSTECH,Dkt.Hassan Mshinda ambao pia ni sehemu ya mafanikio ya programu hiyo,akizungumza jambo mbele ya wanahabari (hawapo pichani) kuhusiana na uzinduzi wa programu mpya ya kujifunza somo la hisabati kwa kutumia simu za mikononi. 
  Baadhi ya wageni waalikwa na wadau mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo.

ONESHO LA S!TE KUFUNGULIWA KESHO JUMATANO MLIMANI CITY,JIJINI DAR

$
0
0
ONESHO la kimataifa la utalii ‘Swahili International Tourism Expo’ (SITE) linaloandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) linafunguliwa rasmi leo (kesho Jumatano) katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City na litamalizika Jumamosi.

Tayari maandalizi yote kuelekea ufunguzi wa onesho hilo yamekamilika na kwamba watanzania wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuja kujionea vivutio adhimu wa taifa hili.

Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) pamoja na Shirika la Ndege la Ethiopia ndio wadhamini wa onesho hilo linalotarajiwa kushirikisha mataifa mbalimnali ulimwenguni.

Wadhamini wengine ni pamoja na Zanzibar collection, Hoteli za Sea Cliff, Serena hotel, Southern Sun,NewAfrica, Hyatt Regency,Protea, Serena hotel, Bouganvillea Safari lodge, Acacia Farm lodge na Soroi Tented Camp zimedhamini huduma ya malazi kwa wageni maalumu.

Pamoja na washiriki wengine onesho hilo linatarajiwa kushirikisha wafanya biashara wakubwa na watalii kutoka Marekani, Uingereza, Ujerumani pamoja na wandishi wa habari wa kimataifa wanaokuja kwa ajili ya onesho hilo.

Wakati Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa ikitoa udhamini wa mabasi ya kubebea washiriki wakati wa onesho hilo, benki ya CRDB imetoa udhamini wa fedha taslimu na inatarajiwa kuwa na banda ndani ya maonesho hayo ya aina yake.

Usafiri wa ardhini utadhaminiwa na makapuni Zara Tours, Naeda Safaris Ltd, Wildlife Expedition Safari, huku Azam Marine wakijitokeza kudhamini usafiri wa baharini kutoka Zanzibar. Mashirika ya ndege ya Rwandair, Precision Air na Uturuki (Turkish airline) yatatoa tiketi za ndege kwa ajili ya kuwasafirisha baadhi ya wageni wakati wa onesho hilo.

Makampuni mengine yaliyojitokeza ni yale yanayomiliki majarida. Haya ni Event, Dar Life na 7th Floor Media kutoka hapa nchini na Go Places kutoka Kenya, ambavyo wanatangaza onesho hili kupitia majarida yao.

Aidha kampuni ya Montage imetoa udhamini wa kuwa mpambaji katika kumbi za mikutano. Boogie woogie pia wametoa udhamini na watakuwa na mgahawa wao wa chakula katika banda la utalii wa utamaduni ilhali wadhamini wengine Black Tomato wao watakuwa na banda la kuuza kahawa ya Tanzania. ‘Swahili International Tourism Expo’ litakuwa likifanyika kila mwaka mnamo mwezi wa Oktoba na kuhudhuriwa na washiriki kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Saddick akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uwepo wa onyesho la kimataifa la utalii ‘Swahili International Tourism Expo’ (SITE) linaloandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB),litakalofunguliwa rasmi kesho Jumatano katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB),Devota Mdachi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu onyesho hilo la kimataifa la utalii ‘Swahili International Tourism Expo’ (SITE) litakalofunguliwa rasmi kesho Jumatano katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam.

Mkutano wa Kimataifa wa Tekinolojia ya Mawasiliano waanza jijini dar

$
0
0
Mkurugenzi wa Kampuni ya Tekinologia ya Huawei Tanzania, Vincent Wen(kushoto) akizungumza na washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Tekinolojia ya Mawasiliano ulioanza jana katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam kwa udhamini wa HUAWEI.
Sehemu ya washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Tekinolojia ya Mawasiliano wakifatilia kwa makini mkutano huo ulioanza jana katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam kwa udhamini wa HUAWEI.

26 WAITWA TAIFA STARS ITAKAYOIVAA BENIN

$
0
0
Wachezaji 26 wameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) kwa ajili mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya Benin itakayochezwa Oktoba 12 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Kocha Mart Nooij ambaye yuko Cairo, Misri kwenye kongamano la makocha la Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), amesema kikosi cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kitaingia kambini Oktoba 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Wachezaji walioitwa ni makipa Deogratias Munishi (Yanga), Aishi Manula (Azam), na Mwadini Ali (Azam).

Mabeki ni Said Moradi (Azam), Shomari Kapombe (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Miraji Adam (Simba), Charles Edward (Yanga) na Emmanuel Simwanda (African Lyon).

Viungo ni Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Amri Kiemba (Simba), Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Ndemla (Simba) na Haruna Chanongo (Simba).

Washambuliaji ni Khamis Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwegane Yeya (Mbeya City), na Juma Liuzio (Zesco, Zambia).

Article 17

Timu ya Habari yatoa kipigo kwa RAS Simiyu katika mashindano ya SHIMIWI

$
0
0
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO

Timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele katika mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Watumishi wa Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayoendelea mjini Morogoro.

Wakicheza kwa kuonana timu hiyo ikiongozwa na Nahodha wao Carlos Mlinda walilisakama lango la wapinzani wao RAS Simiyu ambapo katika kipindi cha kwanza mcheza aliyevalia jezi yenye namba 11 Erick Mfugale aliwapatia goli la kuongoza kwa kipindi cha kwanza hadi mapumziko. Kipindi cha pili kilinza kwa timu zote kusaka ushindi ili kujihakikishia hatua inayofuata.

Dakika ya saba ya kipindi cha pili mchezaji aliyevalia jezi namba 8 Maurus Ndenda ndiye aliwanyanyua mashabiki wa timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kufunga goli la pili kwa shuti kali na kuingia wavuni.

Hadi kipenga cha mwisho cha mwamuzi wa mchezo huo Ramadhani Omari, timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imeshinda 2 na RAS Simiyu hawajapata kitu ambapo ubao wa matokeo ulisomeka (Habari 2-Simiyu 0).

Aidha kwa upande wa mpira wa pete timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo leo bahati haikuwa yao wamefungwa goli 39 kwa 10 na wapinzani wao Wizara ya Ardhi, Nyumba Na Maendeleo ya Makazi.
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo waki wa katika picha ya pamoja kabla ya mtanange dhidi ya RAS Simiyu leo katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) mjini Morogoro.
Waamuzi wa mchezo mpira wa miguu kati ya timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na RAS Simiyu wakiongozwa na mwamuzi wa kati Ramadhani Omari (wa pili kulia) wote kutoka kituo cha michezo ya vijana chini ya miaka 20 kijulikaanacho kama Twalipo cha mjini Morogoro.
Mchezaji wa timu ya mpira wa pete Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Agnes Mbambo akimiliki mpira wakati wa mechi yao na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwenye mashindano ya SHIMIWI leo mjini Morogoro.
Wachezaji Johari Kachwamba (kulia) na Hadija Omari Jaa (kushoto) wakiwa kwenye harakati za kuwania mpira wakati wa mechi kati ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. (Picha zote na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

TANZANIA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA GIZ

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Michael John akitoa tamko kuhusu Siku ya Soko la Afya iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na Shirika la GIZ , itakayofanyika Oktoba 2 katika ukumbi wa Diammond Jubelee jijini Dar es salaam.
Naibu Meneja wa Miradi ya Afya wa GIZ Bw. Christian Ptleiderer akizungumza na waandishi wa habari kutoa wito kwa mashirika mengine yanayotoa huduma za afya nchini kuendelea kusaidia na kusambaza huduma zao katika maeneo yenye changamoto ya miundombinu na uhaba wa watumishi wa afya.Kulia ni Mtaalam na Mawasiliano wa shirika la GIZ nchini Bi. Vida Mwasalla. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Na. Aron Msigwa – MAELEZO.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Shirika la Ujerumani la GIZ katika uanzishaji na uendelezaji wa programu mbalimbali za utoaji wa huduma za afya zinazolenga kupunguza vifo vya watoto walio chini ya umri wa miaka 5.

kwa habari kamini BOFYA HAPA

Azam yadhamini maonesho makubwa ya Keki Dar

$
0
0
Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan wazamini wa maonesho hayo. Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan wadhamini wa maonesho hayo.Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias. Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias.Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan wazamini wa maonesho hayo na kulia ni Meneja Bidhaa za Azam, Abubakar Suleiman. Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan wazamini wa maonesho hayo na kulia ni Meneja Bidhaa za Azam, Abubakar Suleiman.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images