Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

PSPF YADHAMINI MASHINDANO YA SHIMIWI YANAYOENDELEA MKOANI MOROGORO KATIKA UWANJA WA JAMUHURI

$
0
0
Baadhi ya watu wakiwa wanafuatilia mashindano hayo ya SHIMIWI yanayo endelea Mjini Morogoro katika uwanja wa Jamuhuri 
Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Netball wakiwa wanajiandaa na Mchezo wao
 Afisa wa PSPF akimsajili uanachama mmoja wa wanamichezo walikuwepo katika Mashindano hayo ya SHIMIWI
 Aliyevaa Tshirt ya Blue ni Afisa Masoko wa PSS Bwana Delphin Richard akitoa maelezo kwa wanachama wa PSPF wakati Michezo hiyo ikiendelea
 Baadhi ya wachezaji wakiwa katika mapumziko.

BONDIA WA KIKE MWAFRIKA ACHUKUA UBINGWA WA NGUMI ULAYA

$
0
0
Bondia maarufu wa kike mwafrika barani ulaya Bintou Yawa Schmill,mkazi wa Ujerumani siku ya ijumaa 26.September 2014 alifanikiwa kuchukua taji la ubingwa wa ngumi za kulipwa unaotambuliwa na IBF,Bondia Bintou alimpiga na kumshinda mpinzani wake bondia Mirjana Vujic kwa K.O katika raundi ya 3,. Pambano hilo lilionyeshwa Live katika TV channel ya euro sport na kutazamwa na maelfu ya watu wakishuhudia bondia wa kike mwafrika akirusha ngumi kali kuliko radi.

Bintou Schmill (30) aka The Voice ameshapigana mapambao ya kulipwa 9 na ameshinda 8 kwa K.O,Katika pambano la Ijumaa 26.September 2014 liliofanyika kwenye ukumbi wa Stadthalle/ Saalbau Frankfurt-Nied,alifanikiwa kumpa wakati mgumu mpinzani wake kuanzia round ya kwanza hadi ilipofika raund 3 bondia Mirjana Vujickatika alipigwa kwa KO na Bintou Schmill aka "The Voice" kutangazwa ndie bingwa mpya wa uzito wa Welterweight barani ulaya na kuvikwa mkanda huo unatambuliwa na IBF.

Bintou Schmill aka 'The Voice' anaye fananishwa na Simba Jike (Bintou is the Lioness),Simba ambaye ukimuona mpishe njia ulingoni. Bintou "The Voice" Schmill sasa kapania kuweka rekodi ya kuwachapa wapinzania wake kila kona duniani !
Bintou Schmill aka The Voice new IBF europe Championess.
Boxer Bintou Schmill face to face with Mirjana Vujic

Zaidi ya sh. Milioni 100 zapatikana katika harambee ya kuchangia Mfuko wa Bonnah Education Trust Fund jijini dar

$
0
0
 Mgeni Rasmi katika hafla ya Chakula cha jioni cha kuchangia Mfuko wa Bonnah Education Trust Fund,Mwenyekiti wa CCM Mkoawa Dar es Salaam,Ndg. Ramadhan Madabida akitoa hotuba yake kabla ya kuanza kuendesha harambee hiyo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.Zaidi ya sh. Milioni 100 zilipatikana katika harambee hiyo.
 Mwenyekiti Mwanzilishi wa Bonnah Education Trust Fund,Bonnah Kaluwa akitoa hotuba yake kwa wageni wa mbali mbali (hawapo pichani) waliohudhulia hafla ya Chakula cha jioni cha kuchangia Mfuko wa Bonnah Education Trust Fund,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.Zaidi ya sh. Milioni 100 zilipatikana katika harambee hiyo.Picha zote na Othman Michuzi.
 Katibu wa Bonnah Education Trust Fund,Mary Muwasa akizungumza machache ikiwa ni pamoja kuwatambulisha wadhamini mbali mbali waliojitolea ili kufanikisha harambee hiyo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
  Mgeni Rasmi katika hafla ya Chakula cha jioni cha kuchangia Mfuko wa Bonnah Education Trust Fund,Mwenyekiti wa CCM Mkoawa Dar es Salaam,Ndg. Ramadhan Madabida (kushoto) akipokea mfano wa hundi ya Dola za Marekani Elfu 8 kutoka kwa Mwenyekiti wa GCUT Group Tanzania,Lucy Jeremiar Gilya.Katikati ni Mwenyekiti Mwanzilishi wa Bonnah Education Trust Fund,Bonnah Kaluwa.
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo,Ndg. Ramadhan Madabida akipokea mfano wa hundi ya Dola za Marekani Elfu 15 kutoka kwa Meneja wa Miles Networks International nchini Tanzania,Diana Paul (kulia).Katikati ni Mwenyekiti Mwanzilishi wa Bonnah Education Trust Fund,Bonnah Kaluwa.
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo,Ndg. Ramadhan Madabida akipokea mfano wa hundi ya Sh. Mil. 4.4 kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Kampuni ya Resolution Insurance,Angela Tungaraza (kulia).Katikati ni Mwenyekiti Mwanzilishi wa Bonnah Education Trust Fund,Bonnah Kaluwa.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

RAIS WA ZANZIBAR MGENI RASMI KATIKA MAHAFALI CHUO CHA UDAKTARI ZANZIBAR

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa zawadi kwa mwanafunzi bora zaidi ya wote walimaliza masomo ya Udaktari Nadhira Suleiman Said katika Mahfali ya Kwanza ya Chuo cha Madaktari Zanzibar yaliyofanyika leo katika viwanja vya Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Mbweni nje ya Mji wa Unguja (katikati) Dk.Salhia Ali Muhsin Mratibu wa Chuo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake wakati wa Mahfali ya Kwanza ya Chuo cha Madaktari Zanzibar yaliyofanyika leo katika viwanja vya Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Mbweni nje ya Mji wa Unguja, jumla ya wanafunzi 35 wamehitimu mafunzo na kupewa shahada zao leo (kulia) Waziri wa Afya Rashid Serif Suleiman (kushoto) Mkuu wa Kitivo cha Tiba DEAN Ulpiano Perez kutoka Cuba.
Waziri wa Afya Rashid Serif Suleiman akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kuzungumza na wanachuo na wananchi waliohudhuria katika Mahfali ya Kwanza ya Chuo cha Madaktari Zanzibar yaliyofanyika leo katika viwanja vya Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Mbweni nje ya Mji wa Unguja, jumla ya wanafunzi 35 wamehitimu mafunzo na kupewa shahada zao leo.

Tanzania yaendelea kunufaika na uhusiano mwema ulipo baina yake na Taifa la China.

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji na Uwezeshaji Dkk. Mary Nagu akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam.

 : Balozi wa China nchini Tanzania Balozi Lui Youqing akigonga glasi ya mvinyo wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam.

 Picha ya Keki kwa ajili ya hafla ya maadhimisho ya miaka 65 tokea kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China hafla hiyo imefanyika jana jijini Dar es Salaam.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Uwekezaji na Uwezeshaji) Dkt. Mary Nagu  na Balozi wa China nchini Tanzania Balozi Lui Youqing wakikata Keki  wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam.

TANZANIA, KENYA, ZAMBIA WAANZA KUJADILI UTEKELEZAJI MRADI UMEME WA PAMOJA

$
0
0
Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam

Wataalamu kutoka nchi za Zambia, Kenya na Tanzania kutoka Wizara zinazoshughulika na masuala ya nishati wameanza majadiliano ya Utekelezaji wa Mradi wa Kuunganisha Mtandao wa Umeme katika Gridi za nchi hizo. Kikao cha Majadiliano hayo kiliongozwa na Makatibu Wakuu kutoka katika nchi husika na kitafuatiwa na mkutano wa Mawaziri utakaofanyika tarehe 30 Septemba, 2014 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika kikao hicho Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi amezitaka nchi hizo kuunga mkono jitihada za utekelezaji wa mradi huo kutokana na umuhimu wake kiuchumi ikiwemo kuhakikisha nchi hizo zinakuwa na nishati ya umeme ya kutosha.

Aidha, ameongeza kuwa, tayari Tanzania imeanza kufanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha inaanza utekelezaji wa mradi huo ambao umechukua kipindi kirefu kuanza kutekelezwa na kuongeza kuwa, Tanzania iko tayari kushiriki katika utekelezaji wa mradi huo ikiwemo kuhakikisha kwamba mradi huo unafanikiwa.

Kwa upande wake mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Petroli Kenya Mhandisi Richard Mwiru, ameeleza kuwa, kuna matokeo bora yatakayotokana na utekelezaji wa mradi huo, matokeo ambayo yatasaidia biashara ya umeme na upatikanaji wa umeme rahisi kwa nchi hizo. Aidha, ameongeza kuwa, nchi ya Kenya iko tayari kushiriki katika utekelezaji wa mradi huo.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Migodi,Nishati na Maendeleo ya Maji wa Zambia, Charity Mwansa, ameeleza kuwa, anatarajia mkutano huo utatoa fursa zitakazosaidia utekelezaji wa mradi huo kuendelea kutoka mahali ulipofikia ili kuweza kutoa matokeo chanya yatakayokuwa na manufaa kwa nchi hizo ukizingatiwa kuwa, nchi hizo zimebahatika kuwa na rasilimali asilia za kutosha.

Aidha, Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya Soko la pamoja la nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika anayeshughulikia miradi (COMESA), Dkt. Kipyego Cheluges amezitaka nchi hizo kuhakikisha kwamba mradi huo unatekelezwa kutokana na manufaa ambayo nchi hizo zitayapata ikiwemo bara la Afrika na kuongeza kuwa, COMESA itashirikiana kwa karibu na nchi hizo kuhakikisha kwamba, mradi unatekelezwa kama ulivyopangwa.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, akiongea wakati wa kikao cha Wataalamu kutoka nchi za Zambia, Kenya na Tanzania Kujadili Utekelezaji wa Mradi wa Kuunganisha Mtandao wa Umeme katika Gridi za nchi hizo. Wengine kutoka kushoto ni Balozi wa Zambia nchini Judith Kapijimpanga, Katibu Mkuu Wizara ya Migodi, Nishati na Maendeleo ya Maji Zambia, Charity Mwansa, Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Petroli Kenya, Mhandisi Richard Mwiru na Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya Soko la pamoja la nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika anayeshughulikia miradi (COMESA), Dkt. Kipyego Cheluges.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Petroli Kenya, Mhandisi Richard Mwiru (wa pili kulia) akiongea jambo wakati wa kikao hicho, ambapo ameeleza utayari wa nchi ya Kenya katika utekelezaji wa mradi huo.
Sehemu ya Wataalamu kutoka nchi za Zambia, Kenya na Tanzania wakifuatilia kikao cha Kujadili Utekelezaji wa Mradi wa Kuunganisha Mtandao wa Umeme katika Gridi za nchi hizo.
Mtaalamu Mwelekezi kutoka nchi ya Zambia Siyanga Zomba, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji na hatua mbalimbali zilizofikiwa katika utekelezaji wa mradi wa kuunganisha Mtandao wa Umeme katika Gridi kwa nchi za Zambia, Kenya na Tanzania.

Je,Unamfahamu Sensei Magoma Nyamuko Sarya??

$
0
0
Sensei Magoma N. Sarya ndiye aliyekuwa gwiji wa Karate na kiungo muhimu kwa sensei N. C. Bomani katika kuendeleza mwenendo wa Sanaa ya Karate nchini Tanzania. Sensei Magoma (Daud) amefundisha wanafunzi wengi wa Karate nchini Tanzania Zaidi ya mwalimu yeyote hapa nchini. 

Amekuwa mwafunzi kiongozi mwenye mamlaka ya kusimamia Zanaki dojo na matawi yake Tanzania tokea mwaka 1976 hadi 1982.

Sensei Magoma ni mmoja kati ya wanafunzi wa tano nchini kupata shahada ya kwanza “Shodan” mkanda mweusi mwaka 1976 akiwa mwenye umri mdogo kulikoni wenzake wote chini ya sensei Bomani. Wanafunzi hao ni: Sensei Mapfumo Gamanya ( Mzibabwe), sensei Tola Sodoinde Malunga, Sensei Abome Mabruki na kaka yake sensei Adombe Mabruki, na mwisho kwa umri kati ya hao ni Sensei Magoma Nyamuko Sarya.


Wakati sensei Bomani akiwa nje ya nchi huko nchini Marekani kuanzia mwaka 1976 hadi mwaka 1981 sensei Magoma ndiye alikuwa mwanafunzi mkuu kiongozi na mwenye mamlaka yote ya mapendekezo na kutoa test na hata mikanda yote ya mtindo wa Okinawa Goju Ryu Kyokai chini ya mfumo wa kiongozi wao wa Karate duniani Master Eiichi Miyazato, mwalimu wa sensei Bomani. Vigumu mno kuwataja wanafunzi wote waliopitia chini yake, bali tu, kila mwanafunzi aliyekuwa dojo kwa miaka ya 1976 hadi 1982 alikuwa chini ya himaya yake.


Licha ya kuwa mkufunzi mkuu wa Karate nchini Tanzania, mara tu baada yakuondoka kwake mwaka 1982 hapa nchini kuelekea nchi za mashariki ya mbali ikiwemo, India, Nepal, Singapore, Malaysia na Phillipines. Mwalimu Magoma aliacha pengo kubwa ambalo hadi hii leo hamna hata mwenye kuweza liziba katika kuimarisha Sanaa ya Karate Tanzania.

Sensei Magoma pia, ni mkufunzi wa Sanaa ya Yoga na anauzoefu mkubwa katika fani hiyo ambayo ilimpeleka nchi nyingi akiwa kama mwalimu na wakati huohuo kufundisha Karate. Alipata mafunzo ya Sanaa ya Yoga nchini India kutoka katika chuo cha “Neo- Humanist Studies” katika mji wa Varanasi, mwaka 1983.


Mengi aliyoyafanya akiwa bado yupo nchini kwa wakati huo, ni pamoja na kutenganisha darasa la mafunzo ya Karate la watoto na watu wazima na kuliita kwa jina ka heshima ya mwanzilishi wa shule hiyo “ Bomani Brigade” au “BB” kama ilivyokuwa anaitwa.


Kundi hilo la vijana wagodo, lilikuwa halisomi Karate tu, bali pia mwalimu Magoma alijitolea muda wake wote kuwasaidia kimasomo yao kama vile kuwafundisha “Tuition” ya hisabati, Kiingereza, na kuandika isha mbalimbali zinazohusu maisha kiujumla. Leo hii, ni Zaidi ya miaka takriban therasini na wale vijana wamefaidika sana kwa mfano kuna wengi wao kwa hivi sasa ni walimu wa Sanaa ya Karate pia.

Sensei Magoma, ni mwalimu mwenye upeo wa hali ya juu sana katika Sanaa ya Karate ya Okinawa Goju Ryu Karate-do Jundokan Kyokai na kama nilivyoeleza hapo awali, ameacha pengo kubwa mno ambalo sasa ni dhahiri kwamba kurejea kwake katika kufundisha sanaa hii nchini, kunaweza kuwahamasisha walimu wengi na kuiga mfano wake wa kuwa na moyo na nia ya kusaidia vijana na kuwapa nishani katika maisha yao ya baadae.

Kwa mengine Zaidi yanayohusika na Sensei Magoma na jinsi yakuwasiliana nae yatafuatia hao baadae.

BEI YA MADAFU LEO


Article 20

CCM YATOA MASWALI MAGUMU KWA TUME YA UCHAGUZI

Mh. Lowassa amkaribisha Monduli Balozi wa Japan nchini Tanzania

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akimkaribisha wilayani Monduli Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada wakati alipowasili wilayani humo jana Jumapili Septemba 28,2014 kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayofadhiliwa na nchi hiyo.Balozi huyo aliahidi kusaidia vifaa vya kisasa katika hospitali mpya ya kisasa inayojengwa wilayani humo.
Meneja wa Hoteli ya Emanyata mjini Monduli,Bi. Neema (kushoto) akimkaribisha Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada hotelini hapo.Pembeni kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli,Bw. Twalib Mbasha.
Balozi wa Japan nchini,Mh. Masaki Okada (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,Twalib Mbasha (kulia) na Meneja wa Hoteli ya Emanyata mjini Monduli,Bi. Neema alikofikia balozi huyo na ujumbe wake katika ziara yake ya siku mbili wilayani humo.

Dully Sykes ndani ya kipindi cha mawazo huru

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO TAREHE 29.09.2014.

Mke wa Waziri Mkuu achangisha Milioni 128 kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa jijini Dar

$
0
0
Mke wa Waziri Mkuu,MamaTunu Pinda akipokea kiasi cha dola elfu moja kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko utafiti na huduma kwa wateja wa Benki ya CRDB,Tully Esther Mwampamba kama mchango wake wa kuendeleza ujenzi wa Kanisa la kiinjili Moroviani Tanzania (KKMT) Mburahati jijini Dar es salaam.kulia ni Askofu David Martin Mwalyambile wa kanisa hilo Mama Pinda alikuwa mgeni rasimi katika kuendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo ambapo kuliweza kupatikana kiasi cha shilingi milioni mia moja na ishirini na nane.Picha na Chris Mfinanga
Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda akimshukuru mtoto Cecylia Mashaka Mwaisaka mwenye umri wa miaka mitatu kwakuchangia shilingi elfu ishirini kama mchango wake wa kuendeleza ujenzi wa Kanisa la Moroviani mburahati jijini Dar es salaam.Mama Pinda alikuwa mgeni rasimi katika kuendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo ambapo kuliweza kupatikana kiasi cha shilingi milioni mia moja na ishirini na nane.
Kwaya ya kanisa la Moroviani Mburahati ikitumbuiza katika sherehe ya kuchangia ujenzi wa Kanisa lao.
Picha ya pamoja.

Dk.Shein akutana na Ujumbe Kutoka CUBA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Naibu Waziri wa Ufundishaji na Utafiti katika Wizara ya Afya ya Jamii Cuba Dr.Marieta Cutino Redriguez akiongoza Ujumbe wa Viongozi wa Afya Kutoka Cuba walipokutana na Rais Ikulu Mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Ujumbe wa Viongozi wa Afya kutoka Cuba unaoongozwa Naibu Waziri wa Ufundishaji na Utafiti katika Wizara ya Afya ya Jamii Cuba Dr.Marieta Cutino Redriguez akiwemo na Balozi wa Cuba Nchini Tanzania Jorge Luis Lopez Tormo walipokutana na Rais Ikulu Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

KUNDI LA WAMAREKANI WAJA NCHINI KUTIZAMA FURSA ZA UWEKEZAJI

$
0
0
Baadhi ya Marais,Wenyeviti na Wakurugenzi wa Makampuni mbalimbali ya nchini Marekani waliokuja nchini kwa lengo la kutizama fursa za uwekezaji.
Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Washington DC,Suleiman Saleh (katikati) akibadilishana mawazo na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya kufua Umeme ya TANASI ,William Crawford.Ziara hiyo inayo ratibiwa na Ubalozi wa Tanzania,Washington DC ni ya siku ambapo wageni hao wataembelea sehemu mbalimbali kujionea fursa za uwekezaji.
Afisa Ubalozi wa Tanzaini ,washington DC ,Suleiman Saleh akizungumza juu ya ujio wa wageni hao 11 kutoka Marekani ambao wako nchini kwa ajili ya kutizama fursa ya uwekezaji.Hii ni mara ya tatu sasa Viongozi wa Makampuni mbalimbali ya  Marekani wanafika nchini ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa Rais Kikwete kutekeleza Dipromasia ya Uchumi.
Rais wa Kampuni ya Ahmed's Moving Express,Inc  ,Ahmed Issa,ambaye pia ni Balozi wa heshima akizungumza na waandishi wa habari katika hotel ya Mount Meru, jijini Arusha kuhusu ujio wa Marais,Wenyeviti na Wakurugenzi wa makampuni mbalimbali ya Marekani walioko Tanzania .Issa tayari ambaye ni ziara yake ya tatu sasa kuja Tanzania tayari ameanza uwekezaji katika sekta ya Utalii ikiwemo kufungua ofisi ya Utalii Carfonia Marekani iliyozindiliwa hivi karibuni na Rais JAkaya Kikiwete.

ASKARI POLISI WATAKIWA KUTOA HUDUMA BORA KWA JAMII

$
0
0
Na Frank Geofray – Jeshi la Polisi, Moshi.

Askari Polisi kote nchini wametakiwa kuendelea kutoa huduma bora kwa jamii, kwa kuwa kufanya hivyo kutasaidia kuimarisha na kuboresha uhusiano mwema na jamii ambao utasaidia kukabiliana na vitendo vya uhalifu na wahalifu vinavyojitokeza hapa nchini.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Nchini, Abdulrahman Kaniki wakati alipokuwa akifungua mkutano wa Maafisa wanadhimu, wahasibu na watunza stoo kutoka mikoa na vikosi vya Jeshi la Polisi kote nchi ni unaoendelea mkoani Kilimanjaro katika chuo cha Polisi Moshi (CCP) ukiwa na kauli mbiu isemayo usimamizi wa raslimali ni tunu ya Jeshi la Polisi kwa maendeleo yake.

Kaniki alisema askari wote wanapaswa kutoa huduma bora kwakuwa wananchi ndio wanaotoa tathmini ya huduma zinazotolewa na jeshi hilo hivyo wananchi watakapopata huduma bora wataendelea kutoa taarifa ambazo zitasaidia kuwabaini wahalifu wanaoishi nao katika jamii inayowazunguka.

Pia amewataka washiriki wa mkutano kutumia fursa waliyoipata katika kuweka mipango ya pamoja itakayosaidia kupunguza uhalifu na kuhimarisha amani na utulivu unaoendelea hapa nchini ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa bajeti ya jeshi la Polisi.

Aidha amewapongeza askari kwa utendaji wao wa kazi ambao umesaidia nchi kuwa katika hali ya amani na utulivu licha ya kukumbana na changamoto mbalimbali katika utendaji kazi wao wa kila siku.

Kwa upande wake Kamishna wa fedha na logistiki Clodwig Mtweve, alisema lengo la mkutano huo ni kutathmini hali ya utendaji wa Jeshi la polisi na kutafutia ufumbuzi changamoto zinazolikabili hasa katika upande wa rasilimali.

“Kupitia mkutano huu utaboresha mipango yetu katika matumizi ya raslimali tulizonazo na kuhakikisha zinaleta tija kama ilivyokusudiwa jambo ambalo ni muhimu katika maendeleo ya Jeshi letu la Polisi.”Alisema Mtweve.
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki (kushoto) akielekea kufungua mkutano wa Maafisa wanadhimu, Wahasibu na watunza stoo wa Jeshi la Polisi kutoka Mikoa na Vikosi vya Polisi kote Nchini unaofanyika katika Chuo cha Polisi Moshi.Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi Dkt.Ibrahim Msengi na Mkuu wa Chuo cha Polisi Moshi, Matanga Mbushi.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa Maafisa wanadhimu, Wahasibu na watunza stoo wa Jeshi la Polisi wakiwa wanafuatilia hotuba ya Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo unaofanyika katika Chuo cha Polisi Moshi.
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki (katikati) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Dkt.Ibrahim Msengi wakati wa ufunguziwa mkutano wa Maafisa wanadhimu, Wahasibu na watunza stoo wa Jeshi la Polisi kutoka Mikoa na Vikosi vya Polisi kote Nchini unaofanyika katika Chuo cha Polisi Moshi. Kushoto ni Kamishna wa fedha na logistiki Clodwig Mtweve.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)

Msama awapiga jeki KKKT Segerea

$
0
0
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama mbaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASAT) akizungumza katika tamasha la Uimbaji na Uchangiaji wa Ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Segerea jijini Dar es Salaam na kuahidi kutoa sh. milioni 6 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa kanisa hilo. Msama alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo akimwakilisha Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Miochezo, Dk. Fenela Mukangala.
 Mchungaji Emmanuel Masanja 'Masanja Mkandamizaji' aliguswa na kutoa ahadi ya shilingi milioni 1 katika hafla hiyo.
 Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la KKKT Usharika wa Tabata Matumbi, Mchungaji Christosiler Kalata akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama sehemu ya mchango walioahidi katika tamasha la Uimbaji na Uchangiaji wa Ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Segerea jijini Dar es Salaam. Usharika huo ulitoa ahadi ya sh. laki 7.


MJUMBE wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Alex Msama ametoa kitita cha sh. mil 6 katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika Segerea.



Msama ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, alitoa kiasi hicho katika harambee hiyo ya kufanikisha ujenzi huo, iliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubelee jijini Dar es Salaam, huku akitoa na ushuhuda wa maisha yake mpaka kufikia hatua aliyofikia sasa.



Akizungumzia ushuhuda huo, Msama aliwataka waumini kuiga mfano wake kwa kujitolea bila ya kugeuka nyuma, kwani ana imani Mungu yupo na anatenda muujiza kama alioutenda kwake.

"Unajua mimi katika maisha yangu hakuna ninayemwamini zaidi ya Bwana Yesu, kwa kuwa bila ya yeye mie nisingekuwa hapa nilipo, kwa taarifa yenu wapendwa mimi nilishakuwa dereva taxi, nilishakuwa kondakta wa daladala, lakini Mungu ni mwema na anatenda muujiza mpaka mimi kuwa hivi," alisema Msama.

Msama ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, aliongeza kuwa hata hivi karibuni katika ajali aliyoipata akienda Dodoma licha ya kupinduka gari mara nne lakini alitoka akiwa hai.

Harambee hiyo iliyoenda sambamba na mnada, ilihudhuriwa na wasanii mbalimbali wa muziki wa Injili kama Masanja Mkandamizaji, Edson Mwasabwite aliyeimba wimbo wa Ni kwa neema tu.

Mbali ya kiasi hicho alichotoa, Msama pia alichangia katika mnada uliofanyika katika tamasha hilo na kununua mtungi wa gesi kwa sh. laki 5.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YAANDAA WARSHA YA KUPITIA SHERIA JUU YA MATUMIZI YA TUMBAKU.

$
0
0
 Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Mohd Dahoma, akifungua warsha ya kupitia sheria ya kudhibiti matumizi ya tumbaku Zanzibar iliyofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resourt Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
 Mshauri wa Ufundi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika William Onzivu akizungumza na washiriki wa warsha  hiyo (hawapo pichani) katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resourt.
 Afisa kutoka Bodi ya Mapato Tanzania (TRA) akitoa mchango katika warsha ya kupitia sheria ya matumizi ya tumbako iliyofanyika Hotelini hapo. Kulia Mwenyekiti wa warsha hiyo Dkt Mohd Dahoma.
Wajumbe wa warsha  ya kupitia sheria ya kudhibiti matumizi ya tumbaku  wakifuatilia  sheria hiyo ilipowasilishwa  na Mwanasheria wa Wizara ya Afya Amina Jabir (hayupo picha).(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

TAMASHA LA WANAFAMILIA LA AIRTEL LAFANA FUN CITY WEEKEND

$
0
0
 Wafanyakazi wa kampuni ya Airtel Tanzania (kutoka kushoto), Kema Mabango, Abdallah Gunda na Jackson Mmbando wakishiriki katika shindano la kukuna nazi wakati wa Siku ya Wanafamilia ya Airtel, iliyofanyika katika viunga vya Fun City Kigamboni jijini Dar es salaam jana.
Washindi wa shindano la kukuna nazi wakishow love. Kutoka
(kushoto), Mshindi wa Kwanza, Abdallah Gunda, Mshindi wa Pili, Jackson
Mmbando na Mshindi wa Tatu, Kema Mabango
 
 Watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya Airtel Tanzania wakiogelea wakati wa Siku ya Wanafamilia ya Airtel, iliyofanyika katika viunga vya Fun City Kigamboni jijini Dar es salaam jana.
 Watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya Airtel Tanzania wakishiriki katika michezo  wakati wa Siku ya Wanafamilia ya Airtel, iliyofanyika katika viunga vya Fun City Kigamboni jijini Dar es salaam jana.
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images