Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 57 | 58 | (Page 59) | 60 | 61 | .... | 3284 | newer

  0 0
 • 02/28/13--19:23: cheka unenepe

 • 0 0

  NMB leo hii imeweka historia kwa kuanzisha huduma mpya itakayowawezesha wateja wake nchini kuweza kuweka amana zao kupitia mawakala zaidi ya 40,000 wa M-Pesa Nchi nzima. Pia wateja wa NMB wataweza kutuma fedha kutoka NMB kwenda MPESA. NMB na Vodacom zimezindua huduma hiyo rasmi jana kwenye makao makuu ya NMB.

  Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Mark Wiessing,( kulia) na Afisa Mkuu wa Biashara- M-Pesa- Jacques Voogt wakitia sahihi katika mkataba kama ishara ya ushikiano na makubaliano ya kumwezesha mteja wa NMB kufanya muamala wowote kwenye akaunti yake kwa kutumia huduma ya M-Pesa wakati maofisa wa NMB na Vodacom wakishuhudia.

  Sasa mtu yeyote au wateja wa NMB hawatahitaji kwenda ndani ya benki ili kuweka fedha kwenye akaunti kwani sasa wataweza kuweka fedha kwenye akaunti ya NMB bila kwenda tawini. Pia sasa wateja zaidi ya 800,000 wa NMB mobile wataweza kutuma fedha kwenda MPESA.

  Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo, Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bw.Mark Wiessing, “alisema “Ni huduma ya aina yake ambayo itawezesha mzunguko wa miamala baina ya wateja na benki kufanyika kwa urahisi na haraka, jambo litakalosaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki sanjari na kuboresha hali ya maisha na uchumi kwa watanzania wote mijini na vijijini”.

  Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Mark Wiessing,( kulia) na Afisa Mkuu wa Biashara- M-Pesa- Jacques Voogt wakibadilishana mkataba kama ishara ya ushikiano na makubaliano ya kumwezesha mteja wa NMB kufanya muamala wowote kwenye akaunti yake kwa kutumia huduma ya M-Pesa wakati maofisa wa NMB wakishuhudia.

  Akizungumza kwa niaba ya Vodacom, Afisa Mkuu wa Biashara- M-Pesa- Jacques Voogt, amesema, "Hii ni hatua nyingine ambayo tunaifikia leo. Kampuni ya Vodacom inaendelea kupanua mtandao wake wa huduma ya M-Pesa kwa kushirikiana na benki ya NMB ambapo kwa kufanya hivyo itaruhusu wateja wa NMB kuweza kuweka amana zao kwenye akaunti zao kwa urahisi zaidi. Wakati huo huo, tunawaleta wateja wa benki ya NMB karibu na akaunti za benki zao kwa kuwezesha pesa kutoka benki kwenda M-Pesa. "

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu Shirika la Taifa Hifadhi ya Jamii ya Jamii (NSSF),Ramadhani Dau akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya Shirika hilo iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 
   Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka akizungumza wakati wakati wa uzinduzi wa bodi mpya Shirika la Taifa Hifadhi ya Jamii (NSSF) 
   Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Abubakar Rajabu akitoa neno la shukrani baada ya Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka (kushoto) alipozindua bodi hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Ramadhani Dau.
   Baadhi ya wajumbe wa bodi.
   Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka akipeana mkono na Mkurugenzi Mkuu Shirika la Taifa Hifadhi ya Jamii ya Jamii (NSSF), Ramadhani Dau mara baada kuzindua bodi mpya ya Shirika hilo.
   Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka (kulia) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa bodi ya NSSF, Abubakar Rajabu na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF,  Crescentius Magori.

  0 0


  MWIMBAJI mahiri wa muziki wa kiroho nchini, Rose Muhando ameongoza kwa kupata kura nyingi kwa mashabiki wanaotaka atumbuize kwenye Tamasha la Pasaka mwaka huu.

  Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo,Alex Msama ilieleza kuwa msanii huyo amepata asilimia kubwa ya mashabiki wanaotaka atumbuize kwa waimbaji wa ndani, hivyo tayari kamati yake imempitisha kushiriki tamasha hilo.

  "Tunaendesha kura ya maoni kwa mashabiki wetu kwa njia ya kutuma ujumbe mfupi wa maandishi au kupiga simu kuelezea ni waimbaji gani wa ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania wanaotaka wawepo kwenye tamasha la mwaka huu.

  "Kwa hiyo mwimbaji Rose Muhando amepata asilimia kubwa ya mashabiki wanaotaka awepo, zaidi ya asilimia 90 wanamtaka Muhando. Hivyo huyo tayari anakuwa tumeshampitisha tunaomba mashabiki waendelee kutuma maoni yao kwa kamati yangu ili kupitisha wasanii wengine.

  "Dhamira ya tamasha letu mwaka huu ni liwe la aina yake na tuwashirikishe mashabiki wetu, ndiyo sababu kuanzia mikoa litakapofanyika mpaka suala la waimbaji tumewapa fursa mashabiki wenyewe wateue," alisema Msama na kuongeza kuwa msanii atakeyekuwa amepigiwa kura kwa wingi ndiye watakayemtangaza.

  Tamasha la Pasaka limepangwa kufanyika Machi 31 mwaka huu jijini Dar es Salaam na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

  Tamasha la mwaka jana baadhi ya waimbaji mahiri waliokuwepo ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.

  Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku hiyo.

  0 0

  Mheshimiwa  Balozi Hamisi Kagasheki (MB)Waziri wa Maliasili na Utalii akisalimiana na wageni toka Lichinga Msumbiji.

  Mhe.Balozi Hamisi Kagasheki (MB)Waziri wa Maliasili na Utalii akiweka Ngao .

   Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akiweka Sime.

  Katika kuwakumbuka Mashujaa waliotangulia mbele za Haki Jeshi la Wananchi limeweka Utaratibu Maalumu ikiwa ni pamoja na kulipua mizinga na Fataki katika kuwakenzi Mashujaa. Picha na Demasho news

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dr. Albina Chuwa ambaye anaongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 44 wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa, Mkutano huo unajadili taarifa mbalimbali zinazohusiana na masuala ya takwimu. Tanzania ni Mjumbe wa Kamisheni hiyo. Akichangia majadiliano kuhusu taarifa ya mpango wa uboreshaji na ukusanyaji wa takwimu za uhalifu, Dr. Chuwa amesema, nchini zinazoendelea Tanzania ikiwa moja wapo zinahitaji uwezeshwaji katika eneo hilo hasa ikizingatiwa kwamba uhalifu baina ya nchi moja na nyingine unatofautiana na kwa sababu hiyo hata ukusanyaji na uandaaji wa taarifa na takwimu zake hauwezi kufanana kutoka na utofauti wa kimazingira na uhalisia wa nchi husika na kusisitiza kwamba mpango wowote kuhusu eneo hilo lazima uzingatie mahitaji ya nchi. Aliyekaa nyuma ya Dr. Chuwa ni Mkurugenzi wa Shughuli za Takwimu, Bi. Redegunda Maro.
  Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi (2012) Hajjat Amina Mrisho Said akifuatilia majadiliano kuhusu masuala mbali mbali yahusuyo Takwimu katika Mkutano wa 44 wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa.

  Na Mwandishi Maalum

  Tanzania imeshauri kwamba nchi zinazoendelea zisaidiwe katika ukusanyaji, uchambuzi na utayarishaji wa takwimu zinazohusu masuala ya uhalifu.

  Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu,(NBS) Dr. Albina Chuwa, wakati alipokuwa akichangia taarifa kuhusu mpango Makati kuhusu wa uimarisha wa ubora na upatikanaji wa takwimu zinazohusu makosa ya jinai katika katika ngazi ya Kitaifa na Kimataifa.

  Taarifa hiyo imeandaliwa na Taasisi ya Takwimu na Geografia ya nchini Mexico kwa kushirikiana na Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Madawa na Uhalifu.

  Dr. Chuwa anaongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa 44 wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa.Mkutano huo unafanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa ukiwakutanisha wataalam wa masuala ya Takwimu kutoka nchi mbalimbali.

  Katika mchango wake, licha ya kuwashukuru waandaji wa taarifa hiyo, Mkuu huyo wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu amesema, ni vigumu kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania kuutekeleza mpango huo kutokana na upana wake na vile vile kutozingatia uhalisia na mahitaji ya kila nchi.

  Dr.. Chuwa, kama ilivyo kuwa kwa wachangiaji wengine akabainisha kuwa hata aina ya makoja ya jinai yanatofautiana kati ya nchi nchi na kwa sababu hiyo hata namna ya ukusanyaji wa taarifa zake unapashwa kuzingatia mahitaji ya kila nchi.

  “ Makosa ya jinai yanayotokea kwa mfano Tanzania hayawezi kulinganishwa au kufanana na yale yanayotokea nchini Marekani, kwa hiyo hata ukusanyaji wa taarifa zake, pia utatofautiana kwa kuzingatia aina ya makoa ya jinai na mapana yake” akasisitiza na kuongeza.

  Lakini “ jambo la msingi zaidi, ni kwamba kwa nchi kama Tanzania tuna hitaji kuwezeshwa ili ukusanyaji wa takwimu zinazohusu jinai, maandalizi yake na uainishaji wake uweze kuwa na ubora na viwango vya kimataifa.

  Baadhi ya wajumbe wengine waliochangia ajenda hiyo, walikwenda mbali zaidi kwa kutaka kuainishwa au kuwepo na tafsiri sahihi kuhusu jinai u, badala ya kuuweka makosa yote ya jinai katika kundi moja.

  Aidha wajumbe wengine walitaka pia kuwapo kwa mafunzo, vipaumbele, uratibu na uwiano katika suala zima la ukusanyaji wa takwimu zinazohusu jinai .

  Mkutano huo wa 44 wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa, licha ya kujadili taarifa ya mpango mkakati wa kuimarisha ubora na upatikanaji wa takwimu za jinai , pia umejadili taarifa za takwimu nyingine nyingi zikiwamo zinazohusu masuala ya elimu, jinsia, mazingira, biashara, ajira, huduma, uchumi, viashiria vya maendeleo , sayansi na teknolojia, kilimo, sekta isiyo rasmi, takwimu zinazohusu bei, na takwimu zinazo husu afya.

  0 0

  SHOSTISTO TABLE  300,000/=
  PIGA NAMBA
  0784 418941 AU 0755  551077 (ULETEWE TIKETI)
  TIKETI ZITAPATIKANA
  SHEAR ILLUSIONS (MLIMANI CITY)
  8020 FASHIONS (SINZA MAPAMBANO)
  SILVER BOUTIQUE (POSTA AZAM)
  VIATUZI (SEA VIEW UPANGA)
  ROZELLA FASHIONS (KINONDONI)
  MAZNAT BRIDAL SALOON ( MIKOCHENI )
  JACKZ COSMETICS ( KINONDONI TX MARKET)UTAPATA NA ZAWADI
  FABAK FASHIONS (MIKOCHENI KWA WARIOBA)AMAYA BEAUTY SALOON & SPA (POSTA)ANGALIZOTIKETI HAZITOUZWA MLANGONI
  WENYE  TICKET ZENU MKONONI
  NGUO ZENU ZA #AFRICANPRINT.... Mmezihang wenyewe lakini ;)
  NAOMBA NIWASISITIZIE PLZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZZ PLZZZZZZZZZZZZZZZZZ TAFADHALIIIIINI SAANA TUZINGATIE MUDA ILI PROGRAM ZETU ZIENDE SAWA TUPATE MUDA WA KUCHEZA KWA RAHA ZETU
  MAMBO YA KIKE KIKENI SHOST!!
                                                              #INSTAGRAM
                           Mama Tunu Pinda. akiwa ndani ya #kente #african print na ndo dresscode         SIKU YETU.....SHUGHULI YETU.....KWA RAHA ZETU

  0 0


  0 0


   Rais wa FIFA Sepp Blatter akiwa na Rais wa TFF Leodegar Chilla Tenga walipokutana hivi karibuni makao makuu ya FIFA jijini Zurich

  Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limetuma mapendekezo 10 ya marekebisho ya Katiba yake kwa wanachama wake kwa njia ya waraka.

  Mapendekezo hayo yametumwa kwa kila nchi mwanachama kupitia waraka namba 1320, ambapo wanachama kwa kupitia kwa mashirikisho yao ya mabara watapiga kura ya ndiyo au hapa. Kwa upande wa Afrika, wanachama wa FIFA wanatakiwa kuwasilisha kura zao kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

  Baadhi ya mapendekezo hayo ni wajumbe wa Kamati ya Utendaji kuthibitishwa na Mkutano Mkuu wa FIFA (FIFA Congress). Makamu wa Rais wa FIFA na wajumbe wa Kamati ya Utendaji wanaochaguliwa katika mabara ambapo itabidi wathibitishwe na FIFA Congress.

  Muundo wa Kamati ya Utendaji; nafasi moja ya vyama vya mpira wa miguu vya Uingereza (British FAs) sasa inahamishiwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA). Pia Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi ya FIFA anatakiwa kushiriki vikao vya Kamati ya Utendaji bila kuwa na haki ya kupiga kura.

  Uchaguzi wa Rais; mgombea anatakiwa kuungwa mkono na idadi ya kutosha ya vyama wanachama kutoka katika mabara mawili tofauti. Ukomo wa uongozi; kuanzisha vipindi vya uongozi. Ukomo wa umri; ukomo wa umri usiozidi miaka 72 wakati wa kugombea utekelezwe.

  Uwakilishi wa kutosha kwa makundi yenye maslahi katika FIFA; makundi yenye maslahi katika mpira wa miguu kama wachezaji wapate uwakilishi katika Kamati ya Mpira wa Miguu. Uteuzi wa mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia; uteuzi sasa ufanywe na Mkutano Mkuu wa TFF.

  0 0


  Ndugu Wanajumuia,
   
  Nina masikitiko makubwa kuwajulisha kwamba kaka mpendwa Mabula Aloys Nyamenda amefariki dunia February 22, 2013 hapo San Diego, California.  Marehemu allikua akisumbuliwa na cancer ya damu (Leukemia); na ameacha mke na mtoto wa miaka 11.
   
  Familia ya marehemu inatarajia kusafirisha mwili kwenda Tanzania mnamo March 8, 2013.  Gharama za usafirishaji mwili inakisiwa kuwa $7,200.  Kwa wale wanaoweza, tafadhali weka mchango wako katika account ya benki ifuatayo: Jina la Benki: Bank of America - California.     Jina la Mwenye Account: Paschal Nyawabila     Account Number: 325013556996    Zip Code:  92129 (kwa ajili ya transfer)
   
  Ndugu, jamaa, na marafiki watakua pamoja kwa kutoa heshima za mwisho siku ya Ijumaa - March 1, 2013; 12:00 - 2:00 pm katika anuani ifuatayo: 
  St. Michael Parish,   15546 Pomerado Rd., Poway, CA 92064
   
  Na baadae kuelekea kwenye chakula kwemye anuani ifuatayo: 4688 Convoy Street, San Diego, CA 92111   Namba ya simu: 858-279-6888
   
  Misaada ya kihali na kimali inahitajika katika kipindi hichi kigumu.  Naomba tuwaombee wafiwa Mwenyezi Mungu awape subira; na tumuombee marehemu Mabula Aloys Nyamenda aende mahala pema peponi, amin.  Kwa maelezo zaidi, naomba wasiliana na:
  Soon Nyamenda (858)-539-9800 (Mke wa Marehemu)    
  Henry Nyamenda (858)740-6865 (Kaka wa Marehemu)
  Paschal Nyawabila (858)231-0849
  Joseph Kisaka (760)212-2000
  Felician Nyamenda 011-255-769-069003 (Familia ya Marehemu - Tanzania)
   
  Wenu katika majonzi,
  Rabia

  0 0

   Rais wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya ISACA Tawi la Tanzania, Boniface Kanemba akifafanua jambo wakati wa semina kuhusu teknolojia ya mawasiliano na Utawala Bora vinavyoweza kuchangia maendeleo ya uchumi na kufanyika jijini Dar es Salaam. Semina hiyo iliandaliwa na ISACA Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Norway Registers Development.
   Baadhi ya washiruiki wa Semina hiyo kutoka katika taasisi za Fedha
   Rais wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya ISACA tawi la Tanzania, Boniface Kanemba  akitoa mada katika semina hiyo.
   Washiriki wa semina.
   Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Norway Registers Development (NRD), Jon Birger F Jalestand amkitoa mada katika semina hiyo.
  Rais wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya ISACA tawi la Tanzania, Boniface Kanemba akizungumza na waandishi wa habari kuhusu teknolojia ya mawasiliano na Utawala Bora vinavyoweza kuchangia maendeleo ya uchumi na kufanyika jijini Dar es Salaam. Semina hiyo iliandaliwa na ISACA Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Norway Registers Development. (NRD). (Picha na Habari Mseto Blog)

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), akizungumza na  aliyekuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri wa Japan, Bw.Osamu Fujimura alipofika na ujumbe wake Ofisini kwa Mhe. Waziri leo ambapo walizungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Japan ikiwemo maandalizi ya Mkutano wa Tano unaohusu Ushirikiano kati ya Japan na Afrika (TICAD V) utakaofanyika nchini humo mwezi Juni 2013.
  Mhe. Membe akiendelea na mazungumzo huku ujumbe kutoka Japan ukimsikiliza.
  Mhe. Membe akimsikiliza Bw. Fujimura wakati wa  mazungumzo yao.
  Mhe. Masaki Okada (kulia), Balozi wa Tanzania hapa nchini akimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati ujumbe kutoka Japan ulipomtembelea Mhe. Membe ofisini kwake. Wengine katika picha ni Balozi Mbelwa Kairuki (katikati), Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Bw. Khatib Makenga, Afisa katika Idara hiyo.
  Mhe. Membe akiwa katika picha ya pamoja na Bw. na Bibi Fujimura (kushoto) na Mhe. Masaki Okada (kulia), Balozi wa Japan hapa nchini mara baada ya mazungumzo.

  0 0

  NA BASHIR NKOROMO, MOROGORO 

  MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Hamis Juma Sadifa amesema baada ya uchaguzi mkuu wa Jumuia hiyo uliomalizika mwishoni mwa mwaka jana, sasa kazi iliyopo mbele ya UVCCM ni kuhakikisha CCM inaimarika zaidi na kushinda chaguzi zote.

  Amesema baada ya uchaguzi huo na uteuzi wa Viongozi wa Baraza Kuu, wajibu walionao viongozi wa Jumuia hiyo sasa ni kujishusha chini na kuacha kabisa tabia ya kujitutumua na kuwaogopa waliowashinda kwenye uchaguzi ikiwa ni njia mojawapo ya kuvunja makundi ndani ya jumuia hiyo.

  Sadifa alisema hayo, Februari 28, mwaka huu, wakati akizungumza na Baraza Kuu la UVCCM mkoa wa Morogoro, alipowasili kwa ajili ya ziara ya siku tatu mkoani humo ambayo ni ya kwanza kufanya nchini tangu kuchaguliwa kwake kuwa Mwenyekiti wa Jumuia hiyo.

  "Baada ya uchaguzi kumalizika na kukamilisha uteuzi wa wajumbe wa Baraza letu kuu, sasa kazi iliyobaki mbele ya ni kuhakikisha CCM inakuwa imara na kushinda chaguzi zote zinazokuja. Wale tuliochaguliwa sasa tujishushe kwa wanachama wetu, na kuacha kabisa tabia tuliyonayo baadhi yetu ya kujitutumua na kuwakoga tuliowashinda, tabia hizo hazina faida na ni sumu kabisa kwa uhai wa Jumuia na Chama chetu", alisema.

  "Tabia hiii tuiache kabisa, ni sumu inayoendeleza makundi yaliyotokana na uchaguzi, kuendelea kwake ndiko kumekuwa kukisababisha CCM kushindwa katika chaguzi mbalimbali hata katika maeneo ambayo wapinzani wala hawajai mkononi, eeh, wakipata kura zao kidogo na za sisi wenyewe tunaovurugana wanashinda!" alisema.

  Alisema, ni wajibu wa viongozi walipata nyadhifa, kuwabembeleza waliowashinda ili kuwaleta karuibu yao, badala ya kuwananga na hivyo kusababisha kujenga mpasuko ndani ya Jumuia hiyo ambao alisema siyo lazima kuwepo kama busara hiyo inatumika.

  "Wewe ukishakuwa kiongozi, jitahishi kutumia kila mbinu kuhakikisha yule uliyemshinda au ambaye hakukuunga mkono wakati unatafuta ushindi unakuwa karibu naye kiasi cha kujenga urafiki wa kumfanya akuamini kwamba wewe ni muungwana, hivyo ndivyo siasa inavyotakiwa kufanywa", alisema Sadifa na kuongeza;

  "Unajaribu kwa mara ya kwanza kumvuta, ukishindwa unajaribu tena hata mara ya pili hadi ya tatu, kama naye ni muungwana lazima ataondoa kinyongo, na kama ukiona haelekei kuwa kuondoa kinyongo mwache, lakini usimchukie kabisa maana kama hakukuunga mkono wakati huu ipo siku atakuunga mkono kwa jambo jingine".

  Katika ziara hiyo, Mwenyekiti huyo wa UVCCM, yupo pamoja na viongozi wengine wa Kitaifa wa Jumuia hiyo wakiwemo Katibu Mkuu, Martine Shigella na Naibu Katibu Mkuu Mfaume Kizigo na makada wawili wa aliohamia CCM hivi karibuni wakitoka Chadema, Mwampamba na

  Katika siku tatu za ziara hiyo viongozi hao watatakwanyika wilaya karibu zote za mkoa wa Morogoro na kushambulia kila kona kuimarisha uhai wa Chama.

  0 0

  H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to H.E. Raúl Castro Ruz, President of the Council of State of Cuba on the occasion of his re-election.

  The message reads as follows;

  “H.E. Raúl Castro Ruz,

  President of the Council of the State of Cuba,

  Havana,

  CUBA.

  Your Excellency,

  On behalf of the Government and people of the United Republic of Tanzania and on my own behalf, I wish to convey sincere congratulations to you for your re-election as the President of the Council of the State of Cuba.

  Your re-election to the High Office is a clear testimony of the confidence and trust bestowed upon you and your leadership qualities, by the people of Cuba.

  Cuba and Tanzania enjoy very long and cordial relations over the years. I am confident that the ties of friendly co-operation and partnership between our two countries will continue to grow for our mutual benefit. I wish to reassure Your Excellency, my personal commitment as well as that of my Government, to work closely with you in the days and years to come.

  Please accept, Your Excellency, my best wishes for Your personal good health and success”.

  ISSUED BY: MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND INTERNATIONAL CO-OPERATION, DAR ES SALAAM

  1ST MARCH, 2013

  0 0

  Suma Lee
  ASANTENI, On behalf of the Sporah Show Team

  0 0

  Picha na Habari na John Nditi, Morogoro. 

   JAMII ya Wafugaji wa Kimasai wanaishi Kijiji cha Kambala, Kata ya Hembeti, wilayani Mvomero, mkoa wa Morogoro wamepongezwa kwa kuitikia wito wa kuwasomesha watoto wao ikiwa ni hatua ya kuwarithisha elimu kuliko mifugo. 

   Pongezi hiyo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa mfuko wa The Foundation For Civil Society (FCS), John Ulanga , katika hotuba yake kwa jamii hiyo wakati wa ziara yake alipokitembelea Kijiji cha Kambala chenye asili ya wafugaji wa kimasai na kuwakuta wakiwa na mwamko wa kuwasomesha shule watoto wao.

   Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko huo ambaye alifuatana na baadhi ya wawakilishi wa nchi za Ulaya zinafadhili mfuko ,aliwasifu wafugaji wa jamii hiyo kwa kuamua kuuza sehemu ya mifugo yao na kupata fedha za kuwasomesha shule watoto wao. 

   “Pamoja na kuona maendeleo ya jamii wa wafugaji wa kimasai wa kijiji hiki, wito wangu kwa wengine ambao wana ng’ombe wengi tumieni kuendeleza watoto wenu kielimu huo ni urithi pekee tofauti na mali ama ng’ombe” alisema Ulanga. 

   Wakizungumza mbele ya wajumbe hao, wafugaji wa jamii hiyo walisema kutokana na kutambua umuhimu wa elimu , wameamua kujenga hosteli ya wanafunzi wakike wa shule ya Msingi Kambala ambao wanatoka maeneo ya vitogoji vya mbali na shule . 

   Mweyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Kambala, Issaya Rijiwa, alisema mbele ya ujumbe huyo, jamii hiyo imeamua kuchanga kila mmoja wao sh: 10,000 kwa ajili ya kupata fedha za ujenzi wa Hoteli hiyo na itakapokamilika utakiwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 200. 

   “ Tumeanza mchakati wa kukusanya fedha na kupima eneo la ujenzi ambapo awamu ya kwanza ni kukamilisha jengo la kuchukua watoto 60 na tumelenga wanafunzi wakike ambao hawamudu kutembea umbali wa kilometa zaidi ya 10” alisema Rijiwa. 

   Naye Mwenyekiti wa Society for Women and Aids in Afrika (SWAA)- Morogoro,Hellen Mbezi, alisema kuwa uamuzi wa kujenga Hosteli ya wanafunzi wa shule ya Msingi Kambala ni hatua ya kuwalinda watoto na vitendo viovu hasa wanapokuwa njiani kwenda Shuleni. Alisema, wananchi wa Kata 12 za Wilaya ya Mvomero wamepatiwa elimu juu ya kuwalinda watoto na katika Kijiji cha Kambala, wananchi waliamua kuibua mradi wa ujenzi wa Hoteli ili watoto wajamii ya wafugaji hasa wakike wanaishi karibu na shule. 

   Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka , liupongeza mfuko wa FCS kwa kuonesha umakini katia utendaji wake wa kazi kusaidia vikundi vya wananchi vinavyoanzishwa kwa malengo ya kutoa huduma kwao. Hata hivyo alisema , kufuatia msaada wa Mfuko huo wa kusaidia kutoa fedha kwa ajili ya mchakato wa ujenzi wa Hosteli ya wanafunzi wa shule ya Msingi Kambala , Serikali ya Wilaya pamoja na Halmashauri itaunga mkono jitihada hizo wakati jengo litapaofikia usawa la kutaka kupauliwa.
   Mkuu wa wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro, Anthony Mtaka ( kati kati) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa The Foundation For Civil Society , John Ulanga , ( wapili  kushoto) wakipata nyama choma ya mbuzi  iliyoandaliwa na Jamii wa wafugaji wa Kimasai wa Kijiji cha Kambala, Kata ya Hembeti, iliyopo wilayani humo  wakati baadhi ya wajumbe wa kutoka nchi mbalimbali za Ulaya zinazofadhili  mfuko huo walipoitembelea jamii hiyo  juzi , kijijini hapo.
   DC ANTHONY MKATA AKIONESHA CD ILIYOREKONDIWA MPANGO KAZI WA UJENZI WA HOSTELI YA WANAFUNZI WA JAMII YA WAFUGAJI WA KIMASA
   Baadhi ya wawakilishi wa nchi wafadhili wa mfuko wa FCS wakisikiliza tafsili ya hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka ( hayupo pichani) kijijiji Kambala
   Elizabeth Anania , mkazi wa kijiji cha Kambala akisoma risala ya wanakijiji ikielezea mpango wa ujenzi wa hosteli ya wanafunzi wa shule ya Msingi karibu na Shule yao
   Mkurugenzi Mtandaji wa FCS, John Ulanga ( mwenye koti jeusi) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka( kati kati) kijijini Kambala
   Katibu wa kwanza wa Ubalozi nchi ya  Netherlands hapa nchini, Orjen Kool akitafakari ulaji wa nyama choma ya mbuzi  iliyoandaliwa na Jamii wa wafugaji wa Kimasai wa Kijiji cha Kambala, Kata ya Hembeti, wilayani Mvomero , eneo la Shule ya Msingi ya Kijiji hicho wakati ujumbe wa wa kutoka nchi mbalimbali za Ulaya zinazotoa ufadhili katika mfuko wa The Foundation For Civil Society walipowatembelea kijijini hapo,juzi  (wenye kuvaa koti) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko huo, John Ulanga.
  Wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili wa jamii ya wafugaji wa kimasai wa kijiji cha Kambala wakiwa nje ya viwanja vya shule ya Kambala

  0 0
 • 03/01/13--19:00: CHEKA UNENEPE
 • Women Take Biden's Shotgun Advice

  0 0
 • 03/01/13--19:00: Ngoma Azipendazo Ankal
 • Mzee mzima  Carlos Santana ana ngoma nyingi kali kama hii ya 'Oye Como Va' ambayo enzi hizo kina Mesiaki walijifunzia kucheza cha cha cha pale YMCA. Watoto wadogo hata jina la wimbo hawaujui

  0 0

   Mabango mbalimbali yameenezwa kila mahali katika mji wa Moshi. Mashindano hayo ya kila mwaka yanafanyika kesho March 3, 2013.
   Misururu ya magari si kawaida katika mji wa Moshi lakini kutokana na heka heka za Kilimanjaro Marathon hali hiyo imeanza kuonekana hasa katika maeneo ya katikati ya mji.
   Maandalizi ya jukwaa la burudani
   Uandikishaji ukiendelea katika hotel ya Keys
  Uandikishaji ukiendelea katika hotel ya Keys. Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi.

  0 0


  Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi Diwani Athuman 
  Akizungumza na waandishi wa habari


  MBEYA   Matukio 2
  -       Watoto walioibwa 2, Me 1,Ke 1
  -       Watuhumiwa      Me 1,Ke 1
  [Wamepatikana]
  MOMBA            -     Tukio 1
  -       Watoto walioibwa       Ke 1
  -       Watuhumiwa  -Nil
  Amepatikana
  KYELA     -     Tukio 1
  - Watoto walioibwa Ke 1
  Amepatikana
   JANUARI – DESEMBA 2012 WIZI WA WATOTO

  MBEYA Matukio 4
   
  -       Watoto walioibwa  Me 3, Ke 1
  -       Wamepatikana wote wazima
  -       Watuhumiwa      Me 3, Ke 1 
   
  RUNGWE   -     Kesi 2
  -       Watoto walioibwa 2, Me 1,Ke 1
  -       Wamepatikana
  -       Watuhumiwa      Me 1,Ke 1
  MBARALI             -     Kesi 1
  -       Mtoto 1
  -1  Amepatikana
   
  Uchunguzi wa mashauri hayo bado unaendelea ili kubaini chanzo cha matukio hayo, yeyote mwenye taarifa kuhusiana na matukio haya azitoe kwenye vyombo vya ulinzi na usalama

older | 1 | .... | 57 | 58 | (Page 59) | 60 | 61 | .... | 3284 | newer