Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 587 | 588 | (Page 589) | 590 | 591 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Kool & the Gang - Get Down On It

  0 0

    Baadhi  ya viongozi wa CCM wilaya ya Ilala wakiwa na mgeni rasmi  Alhaji Ramadhan Madabida.
  Baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala ambao ni  wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi ya chama hicho Wilaya ya Ilala wakifuatilia baadhi ya hotuba zilizokuwa zikiwasilishwa katika mkutano huo.
    Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa jumuiya ya wazazi ya ccm wilaya ya ilala.

   Mwenyekiti  wa ccm mkoa wa Dar Es Salaam  Ramadhan Madabida akiingia Ukumbini kufungua mkutano wa jumuiya ya wazazi ya ccm wilaya ya ilala.

  0 0

  Meza kuu ikipokea maandamano kabla ya ufunguzi rasmi wa michezo ya SHIMIWI mjini Morogoro.
  Watumishi wa Serikali kutoka Wizara na Idara za Serikali wakiwa kwenye maandamano kabla ya ufunguzi wa mashindano ya michezo ya SHIMIWI mjini Morogoro leo.
  Watumishi wa Serikali kutoka Wizara na Idara za Serikali wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina O. Kombani (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mashindano ya michezo ya SHIMIWI mjini Morogoro leo.


  0 0

  President Jakaya Mrisho Kikwete meets and hold talks with South Sudan President Salva Kiir during the UN General Assembly in New York yesterday(Photo by Freddy Maro)


  0 0

  The Dodoma University Vice Chancellor Professor Idris Kikula and Rutgers University Chancellor Richard Edwards sign Memorandum of Understanding between the two universities on academic partnership during a brief and colorful ceremony held at New Jersey Rutgers University campus yesterday.
  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete delivers his public lecture on “The role of Academic Partnerships in Finding Solutions to Global Challenges and Advancing Tanzania’s Priorities,” at Rutgers University in New Jersey United States yesterday. The public lecture was preceded by the signing of the Memorandum of Understanding between Dodoma and Rutgers university on academic partnerships.
  President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete receives a standing ovation shortly after he delivered a public lecture on “The Role of Academic Partnerships in Finding Solutions to Global Challenges and Advancing Tanzania’s Priorities,” at Rutgers University New Jersey Campus yesterday(photos by Freddy Maro).

  0 0

  Meneja wa huduma na bidhaa wa Vodacom Tanzania,Liginiku Milinga(kushoto)akielezea kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)uwezo wa simu mpya aina ya Vodafone Smart Kicka katika matumizi ya mitandao ya kijamii ya Youtube,Twitter,Facebook na whatsup. Simu hizo huuzwa kwenye maduka ya Vodacom kwa bei ya Sh 79,999 zikiwa na ofa ya 3G na SMS 1,200 kwa muda wa miezi sita.Kulia ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.
  Meneja wa huduma na bidhaa wa Vodacom Tanzania,Liginiku Milinga na Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu(kulia)wakiwaonesha waandishi wa habari(hawapo pichani) simu mpya aina ya Vodafone Smart Kicka yenye ufanisi katika matumizi ya mitandao ya kijamii ya Youtube,Twitter,Facebook na whatsup. Simu hizo huuzwa kwenye maduka ya Vodacom kwa bei ya Sh 79,999 zikiwa na ofa ya 3G na SMS 1,200 kwa muda wa miezi sita.

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Lwandai kata ya Mlola ambapo aliwasisitiza wananchi hao kushiriki kazi za maendeleo na kujiunga kwa wingi kwenye mfuko wa Afya ya jamii.
  Umati wa wakazi wa kata ya Mlola wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihutubia wananchi hao.
   Wazee Maarufu wa kijiji cha Lwandai wakifuatilia kwa makini mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye anafanya ziara za kujenga na kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi,Pia katika mikutano yake ya sasa Katibu Mkuu amekuwa akitoa nafasi kwa wananchi kuhoji maswali ,kutoa maoni au ushauri kuhusu maendeleo yao katika maeneo yao.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Lwandai ambapo aliwaambia wawe makini na maneno ya wanasiaa ambao wanahusisha hoja ya katiba mpya na uchaguzi wa mwaka 2015, alisema kuwa kuna watu wana sahau kuwa hiyo siyo ajenda ya wananchi na si makubaliano ya vyama vya siasa .
   Kila kona ya uwanja ilijaza watu.

  0 0  Gari dogo aina ya Suzuki Carry likiteketea moto katikati ya barabara maarufu kama Double Road jirani na makao makuu ya jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro.
  Askari wa Kikosi cha zimamoto akijaribu kuzima moto uliokuwa ukiteketeza gari hilo.


  0 0

  Mshindi wa taji la Redd’s Miss Tanzania Top Model 2014, Jihan Dimachk (katikati) akipozi kwa picha na mshindi wa pili Doreen Robert (wapili kulia), mshindi wa tatu Evelyn Baasa ambaye pia ni Miss Tanzania Photogenic 2014 (wapili kushoto), mshindi wa nne, Lilian Timothy (kulia) na Mshindo wa tano Nasreen Abdul, mara baada ya kushinda taji hilo jana ambapo Jihan amekuwa mrembo wa pili kuingia katika nusu fainali za Miss Tanania 2014 baada ya Miss Photogenic. Shindano la Miss Tanzania Top Mode lilifanyika katika ukumbi wa Triple A jijini Arusha na kuwashirikisha warembo 30..Picha na Father Kidevu Blog

  0 0
 • 09/28/14--03:46: KIBONZO CHA NATHAN MPANGALA
 • 0 0

   Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasiliamali Watu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. D. Mndeme (kushoto) akizungumza na wanamichezo wa Ofisi yake wakati akiwaaga na kukabidhiwa vifaa vya michezo leo asubuhi kwa ajili ya kuelekea Mjini Morogoro kushiriki katika michuano ya Shimiwi iliyofunguliwa leo. Katikati ni Afisa Utawala wa TTCL Tanzania, Ulrick Swai (kulia) ni Katibu wa timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Mandia.
    Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasiliamali Watu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. D. Mndeme (kushoto) akipokea sehemu ya vifaa vya michezo (jezi) kutoka kwa Afisa Utawala wa TTCL Tanzania, Ulrick Swai, wakati wa hafla fupi ya kuagwa timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais na kukabidhiwa vifaa vya michezo leo asubuhi kwa ajili ya kuelekea Mjini Morogoro kushiriki katika michuano ya Shimiwi iliyofunguliwa leo. Kulia ni Katibu wa timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Mandia.
   Picha ya pamoja baada ya makabidhiano hayo....
  Baadhi ya wanamichezo wa Ofisi ya Makamu wa Rais, wakipanda katika basi tayari kwa safari kuelekea Morogoro.

  0 0

  Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) Prof. Emanuel Mjema akizungumza wakati wa hafla ya kuwakaribisha waliokuwa wanafunzi wa chuo hicho waliohitimu miaka iliyopita wakati wa mwendelezo wa shughuli mbalimbali za chuo hicho kutimiza miaka 50.
  Bw. Alexander Msofe akizungumza na wahitimu wa miaka ya nyuma wa chuo cha CBE kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya kuchangia maendeleo ya CBE iliyowahusisha wahitimu hao jijini Dar es salaam.
  Bw. Isdori Kwayi, mmoja wa wahitimu wa chuo cha CBE mwaka 1972 akitoa mchango wake kuhusu namna chuo hicho kinavyoweza kukusanya fedha kutoka katika vyanzo mbalimbali ili kuboresha miundombinu yake wakati wa hafla fupi iliyowahusisha wahitimu wa chuo hicho jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya wahitimu wa CBE wa miaka iliyopita wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa hafla ya kuchangia maendeleo ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam ambacho kimetimiza miaka 50. Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.


  0 0

  Na: Geofrey Tengeneza

  Taasisi na makampuni kadhaa yameendelea kujitokea kudhamini onesho la kimataifa la utalii la Swahili ‘Swahili International Tourism Expo’ (SITE) linaloandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na ambalo linatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City kuanzia Oktoba 1 – 4, 2014.

  Aidha Bodi ya Utalii Tanzania imesema milango bado ipo wazi kwa makampuni na taasisi mbalimbali za serikali na binafsi kuwaunga mkono kwa kujitokeza kudhamini onesho hili linalofanyika kwa mara ya kwanza.

  Licha ya wadhamini wakuu wa onesho hilo ambao wako kiwango cha platinum shirika la hifadhi ya taifa (TANAPA), mamlaka ya hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) pamoja na shirika la ndege la Ethiopia, wadhamini wengine katika viwango vya dhahabu (Gold) na Silva (sliver) ni pamoja Zanzibar collection, Hoteli za Sea Cliff, Serena hotel, Southern Sun, New Africa, Hyatt Regency, Protea, Serena Bouganvillea Safari lodge, Acacia Farm lodge na Soroi Tented Camp zimedhamini huduma ya malazi kwa wageni maalumu ambao ni wafanya biashara wakubwa wa kusafirisha watalii kutoka Marekani, Uingereza, Ujerumani n.k pamoja na wandishi wa habari wa kimataifa wanaokuja kwa ajili ya onesho hilo.

  Wakati Wizara ya mambo ya nje na Uhusiano wa kimataifa ikitoa udhamini wa mabasi ya kubebea washiriki wakati wa onesho hilo, benki ya CRDB imetoa udhamini wa fedha taslimu na inatarajiwa kuwa na banda ndani ya maonesho hayo ya aina yake.

  Kwa upande wa usafiri wa ardhini utadhaminiwa na makapuni Zara Tours, Naeda Safaris Ltd, Wildlife Expedition Safari, huku Azam Marine wakijitokeza kudhamini usafiri wa baharini kutoka Zanzibar. Mashirika ya ndege ya Rwandair, Precision Air na Uturuki (Turkish airline) yatatoa tiketi za ndege kwa ajili ya kuwasafirisha baadhi ya wageni wakati wa onesho hilo.

  Makampuni mengine yaliyojitokeza ni yale yanayomiliki majarida. Haya ni Event, Dar Life na 7th Kenya,ambavyo vinatangaza onesho hili kupitia majarida yao. Aidha kampuni ya Montage imetoa udhamini wa kuwa mpambaji katika kumbi za mikutano. Boogie woogie pia wametoa udhamini na watakuwa na mgahawa wao wa chakula katika banda la utalii wa utamaduni ilhali wadhamini wengine Black Tomato wao watakuwa na banda la kuuza kahawa ya Tanzania.

  ‘Swahili International Tourism Expo’ litakuwa likifanyika kila mwaka mnamo mwezi wa Oktoba na kuhudhuriwa na washiriki kutoka ndani na nje ya Tanzania. Floor Media kutoka hapa nchini na Go Places kutoka

  0 0

  Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wakianza matembezi ya hisani ya takribani Kilomita 10 jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni moja ya matukio ya benki hiyo kudhimisha Siku ya Moyo Duniani ambapo kiasi cha pesa watakachochangisha kitapelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kusaidia watoto na vijana wanaosumbuliwa na matatizo ya ugonjwa wa moyo. Siku ya Moyo Duniani huadhimishwa kimataifa Septemba 29 kila mwaka.
  Hapa baadhi ya wafanyakazi hao wakipita katika barabara ya Ocean Road kulekea maeoneo ya Coco Beach wakitokea makao makuu ya beni hiyo katika Tawi la Corporate, Posta Mpya.
  Hapa ni daraja la Salender, kwa moyo wa kujitolea wafanyakazi hawa wa NBC wakiendelea na matembezi hayo ili kupata fedha kusaidia watoto na vijana wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo.
  Safari inaendelea, hapa baadhi ya wafanyakazi hao wakikaribia kufika mwisho wa matembezi yao hapa ikiwa ni Barabara ya Kenyatta wakielekea Coco Beach.
  Baada ya kumaliza matembezi hayo wafanyakazi hao wakipiga picha ya pamoja kuonyesha ushindi na mshikamano wao katika kusaidia watoto na vijana wanaosumbuliwa na matatizo ya magonjwa ya moyo.

  0 0

  Padri Evod Shao (kulia) akiongoza  misa ya shukurani ya Edgar Mutta  (hayupo pichani) iliyofanyika Silver Spring, Maryland nchini Marekani ya kumtolea Mungu shukurani ya kuwezesha kupoma maradhi yaliyokua yakimsumbua kushoto ni Padri Leandry Kimario 
  Edgar Mutta (kati) katika picha ya pamoja na wazazi wake wakti misa ya shukurani ikiendelea.
  Kulia ni Adrian Mutta na mama yake wakiendelea na misa ya shukurani iliyofanyika siku ya Jumamosi Sept 27, 2014.
  Judith na Liberata (kulia) wakifuatilia misa.
  McDonald akisoma somo.
  Padri Leandry Kimario akiombea familia ya Colonel Adolph Mutta ambaye ni mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada
  Mtoto Brian akiongoza kwaya kwa kupiga kinanda.
  Watanzania na marafiki zao waliohudhuria misa ya shukurani ya Edgar Mutta.
  Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula akiongea jambo na Balozi Karume na mkewe kushoto ni Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV bwn. Iddi Sandaly.
  Colonel Mutta akiotoa neno la shukurani.
  Kwa picha zaidi bofya HAPA

  0 0

  Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)Gasto Leseiyo akiwa ame ‘pose’ kwa picha na Bibi harusi Federica Sikale baada ya kufunga pingu za maisha katika Kanisa Katoliki Parokia ya Roho Mtakatifu Ngarenaro Arusha jana na kufatiwa na sherehe iliyofanyika ukumbi wa Leons Garden Sakina.
  Gasto Leseiyo na Mke wake Federica Sikale baada ya kufunga pingu za maisha katika Kanisa Katoliki Parokia ya Roho Mtakatifu Ngarenaro Arusha wakiwa katika picha ya pamoja na Mama wazazi .
  Bwana harusi Gasto Leseiyo akisalimia wageni kwenye ukumbi wa Leons Garden,Sakina jijini Arusha akiwa na Mke wake Federica Sikale baada ya kufunga pingu za maisha.
  Bwana harusi Gasto Leseiyo na Mke wake Federica Sikale wakiwa na wapambe wao Endrick Fredick(shoto) na Lucy Fransis(kulia) kwenye ukumbi wa Leons Garden Sakina.
  Bwana harusi Gasto Leseiyo na Mke wake Federica Sikale wakijumuika kusakata muziki na ndugu zao waliohudhuria sherehe hiyo.

  0 0


  0 0

  Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiwa kwenye maandamano siku ya ufunguzi wa mashindano ya SHIMIWI taifa yanayoendelea mjini Morogoro.
  Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Ikulu wakimsikiliza Mgeni Rasmi (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mashindano ya SHIMIWI taifa yanayoendelea mjini Morogoro.
  Yameanza vema mashindano ya Shirikisho la Michezo ya watumishi Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) kwa kuendeleza ushindi na kung’ara katika mashindano hayo yanayoendelea mjini Morogoro.
  Mfungaji mahiri wa magoli wa timu ya mpira wa pete Ikulu aliyecheza nafasi ya (G.S) Monica Kassy akiwania mpira dhidi ya wapinzani wao RAS Morogoro wakati wa mechi ya ufunguzi ambapo Ikulu walishinda kwa magoli 62 kwa11 dhidi ya wapinzani wao.
  Baadhi ya wachezaji wa timu ya Ikulu wakifuatilia mchezo wa mpira wa pete wanawake kati ya timu yao na wa wapinzani wao RAS Morogoro. (Picha zote na Eleuteri Mangi MAELEZO)

  0 0

  SAM_0646Engineer Carlos Mkindi ambaye ni mkurugenzi wa mkundi production akiongea na vyombo vya habari kuhusiana na Tamasha kubwa la upendo kwa mama linalotarajiwa kufanyika jijini Arusha katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid tarehe 02-11-2014
  SAM_0669
  Engineer Carlos Mkindi ambaye ni mkurugenzi wa mkundi production akiongea na wanahabari kuhusiana na Tamasha la Upendo kwa mama ambalo linalenga kutoa mitaji kwa zaidi ya akina mama 50 wajasiriamali ili kuwawezesha kujiajiri pamoja na kuwaombea na kuwashukuru kwa moyo wa upendo waliyonayo kwa kujitoa katika kusimamia familia na malezi
  SAM_0670
  Mratibu wa Tamasha la Upendo kwa mama Bw. Linus Kilembu akiongelea maandalizi ya Tamasha kuwa limekamilika kwa asilimia 90
  SAM_0675
  Engineer Carlos Mkindi mwenyekiti wa Tamasha la upendo  ambaye ni mkurugenzi wa mkundi production akifanyiwa mahojiano na wanahabari katika studio za mkundi production zilizopo njiro mkoani Arusha
  SAM_0676
  Kampuni ya Makundi Production ya jijini Arusha iko katika maandalizi ya kufanya tamasha kubwa la aina yake litakalo julikana kwa jina la UPENDO WA MAMA ambalo linatarajiwa kufanyika tarehe 02 Novemba 2014 katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid.
   
  Tamasha hilo litaongozwa na waimbaji wa Nyimbo za Injili wakubwa kutoka Kenya, Sara K, na Cristina Shusho kutoka Tanzania, huku likipambwa na Ambwene Mwasongwe, Baraka Maasa, Eng calros Mkundi, Ester Bukuku, Matha Mwaipaja, Nesta sanga, Meth Chengula, Matumaini, Eline Patrick bila kuwasahau waimbaji wengine kutoka Mkoani Arusha pamoja na Kwaya Mbalimbali.
   
  Lengo la tamasha hilo la UPENDO KWA MAMA linalengo la kutoa Mitaji kwa zaidi ya akina mama 50 wajasiriamali ili kuwaongezea uwezo wa kujiajiri, vilevile utakuwa ni wakati mwafaka wa kuwashukuru wakinamama wote kwa upendo waliyonao ukiambatana na kujitolea katika kusimamia Familia na malezi ya watoto.
   
  Studio ya Mkundi nakamati ya maandalizi ya Tamasha la UPENDO KWA MAMA wanatoa nafasi kwa watanzania, Taasisi na Mashirika yote ambayo yako tayari kuungana na Studio ya Mkundi kwa Ufadhili wa hali na mali ili kufanikisha tamasha hili la UPENDO KWA MAMA.(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog Arusha)

  0 0

  Mshambuliaji wa Yanga, Andrey Coutinho akitafuta mbinu za kuwatoka wachezaji wa Tanzania Prisons, Lauvian Mpalile (kushoto) na Jeremia Juma wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga imeshinda 2-1. (Picha na Francis Dande)
  Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngasa akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Tanzania Prisons, Lauvian Mpalile.
  Jaja akimtoka beki wa Prisons, Nurdin.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 587 | 588 | (Page 589) | 590 | 591 | .... | 3270 | newer