Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 586 | 587 | (Page 588) | 589 | 590 | .... | 3286 | newer

  0 0

   Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa kivuko hicho kipya cha MV Tegemeo.

   Kivuko kipya na chakisasa cha MV Tegemeo kama kinavyoonekana, kimetengenezwa kama mfano wa Meli kutokana na huduma zake.

   Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akimuonesha Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal jinsi kivuko kipya cha MV Tegemeo kitakavyofanya kazi.
   Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Mhandisi Marceline Magesa akimuonesha Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal baadhi ya sehemu ndani ya Kivuko hicho kipya.

  0 0

  Dear Friends and Colleagues,
  Greetings from the Eastern Africa Diaspora Business Council, EADBC!
  Once again EADBC is partnering with Homestrings and DMA in presenting an engaging and informative conference on Diaspora Investment Opportunities.
  To RSVP Now for the Investing in East Africa, Diaspora Investment Symposium, London UK - October 10th, 2014.
  You can also keep up on social media via Hashtags in social media using #IEA and #diasporainvests. Download the FREE Homestrings App to follow investments back home.
  Come Make a Difference in Africa!
  Keep up with EADBC activities by visiting us atwww.eadiaspora.org and liking us athttps://www.facebook.com/EasternAfricaDiasporaBusinessCouncil

  0 0

  Wachezaji wa Boda Boda FC na washabiki wao wakishangilia ushindi baada ya kujinyakulia kombe  la virutubishi katika pambano ililofanyika katika uwanja wa Bondeni wilayani Karatu
  Timu zenye upinzani wa jadi wilayani Karatu mkoani Arusha za  Boda Boda FC na Young Generation  jana zilikuwa na mpambano mkali wa mchezo  wa soka ambapo timu ya Boda Boda iliibuka na  ushindi wa mabao 2-1.

  Mechi hiyo ambayo ilichezwa katika uwanja wa Bondeni chini ya udhamini wa  Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kitengo cha kutoa elimu ya virutubishi kwa jamii ilishuhudiwa na wakazi wa wilaya ya Karatu wapatao 8,000 na mgeni wa heshima alikuwa Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Karatu (OCD) Jubileth Nyange.

  Timu zote 2 zilicheza kwa kujituma na kushangiliwa na wapenzi wa soka ambao ni washabiki wa timu hizo ambapo katika kipindi cha pili Boda FC ilifanikiwa kupachika mabao 2 mfululizo na wapinzani wao wakafanikiwa kurejesha bao moja.

  Kwa matokeo hayo timu iliyoshinda iliweza kujipatia kombe na seti ya jezi za kisasa wakati wapinzani wao walijipatia mipira miwili kutoka kwa mdhamini.Mratibu wa  mchezo Allan Rwechungura kutoka taasisi ya Foot Print alisema lengo la  mchezo huo  lilikuwa ni kutoa burudani kwa wananchi wakati huo huo kuwapatia elimu ya lishe na matumizi ya vyakula vilivyowekewa virutubishi,kampeni ambayo inaendelea katika wilaya mbalimbali nchini chini ya usimamizi wa Wizara ya Afyana Ustawi wa Jamii.
  Alisema kwa kuwa michezoni jukwaa la kukusanya watu wengi wataandaa mashindano ya michezo mbalimbali kwenye wilaya za hapa nchini ambapo timu zitakazofanya vizuri zitajipatia vifaa vya michezo wakati huo huo wananchi wataofika viwanjani kupatiwa elimu ya lishe bora na matumizi ya virutubishi lengo likiwa  ni kufikisha ujumbe wa wananchi wa kawaida.

  0 0

  Na John Gagarini, Kibaha
  HUKU ikiwa imepita wiki moja ya tukio ambalo lilisababisha kifo cha mfanyabiashara wa Jijini Dar es Salaam  Mahoro Mlelwa kupigwa risasi na majambazi na kufa eneo la Maili Moja wilayani Kibaha watu wanaodhaniwa kuwa ni wezi wakiwa na silaha za jadi wamevamia maduka na kupora.

  Watu hao walivamia maduka hayo baada ya kupiga baruti kwa lengo la kuwatisha watu ili waweze kufanikisha wizi huo.
  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana mjini Kibaha kaimu kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Athuman Mwambalaswa (pichani) alisema kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 26 mwaka huu majira ya saa 2 usiku.
  Kamanda Mwambalaswa alisema kuwa mawili yaliyopo eneo la Kwa Mathias wilayani Kibaha na kufanikiwa kupora fedha taslimu kiasi cha shilingi 200,000 pamoja na simu 4 pamoja na vocha za simu zenye thamani ya shilingi 200,000.
  “Katika tukio hilo watu hao walivamia kwa Godfrey Lunyelele (32) na kumwibia simu nne na fedha taslimu kiasi cha shilingi 100,000 na kwa Hassan Mkuwili (42) waliiba vocha za simu zenye thamani ya shilingi 200,000 na fedha taslimu shilingi 100,000,” alisema Kamanda Mwambalaswa.
  Aidha alisema Lunyelele alipata ujasiri baada ya kubaini silaha hizo hazina madhara na kumpiga kwa tofali kichwani mwizi mmoja kati ya watatu, na alipoanguka chini walimkamata na anashikiliwa na jeshi hilo kuhusiana na tukio hilo.
  “Mtu tuliyemkamata jina linahifadhiwa ili uchunguzi usiharibike na tunaendelea kumshikilia ili atupe taarifa za wenzake ambao walifanikiwa kukimbia,” alisema Kamanda Mwambalaswa.
  Alibainisha kuwa kutokana na tukio hilo wamefanya kikao na maofisa wa jeshi hilo na kuamua kufanya doria ya nguvu ya miguu pamoja na magari ili kuhakikisha wanafanikiwa kudhibiti matukio hayo na kuwataka wananchi kutoa taarifa ya watu wanaowadhania kuwa ni majambazi.
  Mwisho. 

  0 0

  Dont Miss Diamond Platnumz One On One with Sporah this 
  Tuesday 30th Sep.
  EUROPE: At 8:00pm(GMT) On VOXAFRICA TV SKY CHANNEL 218
  AFRICA: At 8:00pm(GMT) On DSTV CHANNEL 191
  REPEAT: Thursday at 8:00am(GMT)
  Friday at 05:15pm(GMT)
  Sunday at 6:00pm(GMT)

  TANZANIA: ON CLOUDS TV Jumanne Saa Nne Usiku
  MARUDIO :Ijumaa Saa Nane Mchana Na
  Jumapili Saa Sita Na Nusu Mchana.

  DONT MISS OUT THIS TUESDAY 30th SEP 2014.    

  THE SPORAH SHOW TEAM  
  Tel: 0044 (0) 2075360382
  Mob: 0044 (0) 7932911205
  Fax: 02030698368
  St Andrews Way
  Devons Road
  Bow, London
  E3 3PA.
  Facebook/Twitter

  0 0

   Katibu  Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishona nguo kwenye ofisi ya Veronica Simba (kushoto) iliyopo Mombo Sokoni,kulia ni Mbunge wa Korogwe Vijijini Ndugu Stephen Ngonyani ,Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya siku moja katika wilaya ya Korogwe Vijijini ambapo licha ya kukagua miradi mbali mbali ya ujenzi wa maabara na ofisi za CCM alipata nafasi ya kuwahutubia wananchi na kuwasikiliza.
    Katibu  Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimuelekeza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kushona nguo kwenye ofisi ya Veronica Simba (kushoto) iliyopo Mombo Sokoni.
   
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Ueneziwakinunua matunda kabla ya kwenda kwenye mkutano wa hadhara Mombo.
   Wananchi wakiwa wamekaa kwa shauku ya kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCm Ndugu Abdulrahan Kinana.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia) akiwapungia watu wakati wa kuwasili kwenye uwanja wa mikutano mjini Mombo akiwa pamoja  na Katibu wa NEC Itikadi Nape Nnauye.
   Umati wa wakazi wa Mombo uliojitokeza kwenye Mkutano wa Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana.

  0 0

  Na Mwandishi Maalum, New York
   Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeahidi kuongeza kiwango cha ushiriki wake katika Operesheni za Ulinzi wa Amani kupitia Umoja wa Mataifa, ambapo imebainisha kusudio lake thabiti la kuongeza vikosi vitatu ili kusaidia kurejesha Amani palipo na migogoro ndani ya Afrika. 
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe ( Mb) ametoa ahadi hiyo siku ya Ijumaa, hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano wa kilele wa ngazi ya Mawaziri Uimarishaji wa Operesheni za Ulinzi wa Amani ulioandaliwa na Marekani na kuongozwa na Makamu wa Rais wa nchi hiyo Bw.Joe Biden. 
  Mkutano huo uliohudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, Rais wa Rwanda, Mawaziri Wakuu wa Japan, Bangladesh na Pakistan. Ulikuwa na lengo la kukusanya ahadi mpya za kuimarisha operesheni za ulinzi wa Amani ambapo Joe Biden alitangaza kuwa nchi yake imetenga dola 110 milioni zitakazotumika katika kuimarisha uwezo wa nchi za kiafrika kushiriki kwa ufanisi katika ulinzi wa Amani. 
  Fedha hizo zitatolewa kwa kipindi cha kati ya miaka mitatu na mitano. Mhe. Membe yuko hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa akishiriki mikutano mbalimbali inayokwenda sambamba na majadiliano ya Jumla ya Baraza Kuu la 69 ( UNGA) ambalo Mhe. Rais Jakaya Kikwete alilihutubia siku ya Alhamis. 
  Waziri Membe amesisitiza kuwa Tanzania haichukuli wajibu wa operesheni za kulinda Amani kwa kubahatisha au kiurahisi, bali inauchukua wajibu huo kwa uzito na kwa dhamana kubwa. Ameongeza kuwa, ni kwa kutambua uzito na umuhimu wa dhamana hiyo ndiyo maana Tanzania hivi sasa ni nchi ya 12 kati ya 122 zinazoongoza kutoa walinzi wa Amani duniani ikiwa na wanajeshi zaidi 2,300 kati ya 96,535 wanaohudumia Misheni 16 za Umoja wa Mataifa zilizopo sasa. 
  “Tunaamini katika msemo wa Muasisi wa Taifa letu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwamba, nyumba ya jirani yako ikiwaka moto, basi jua kijiji kizima kiko hatarini”. 
  Waziri aliongezea kuwa  ni msingi huo unaoendelea kutoa mwongozo wa ushiriki wa Tanzania katika Operesheni za Ulinzi wa Amani kwa kupeleka wanajeshi wake huko Lebanon,(UNIFIL), Darfur ( UNAMID) na DRC ( MONUSCO). Pamoja na Tanzania nchi nyingine zaidi ya thelathini zimetoa ahadi zao katika mkutano huo.
   Waziri wa  Mambo ya Nje na  Ushirikiwano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe  (kwenye TV shati la njano) akizungumza wakati wa mkutano wa Kilele wa ngazi ya Mawaziri uliozungumzia  Uimarishaji wa Operesheni za Kulinda Amani. Mkutano huo uliandaliwa na  Marekani ambapo Makamu wa Rais wa nchi hiyo Bw. Joe Biden ndiye aliyeongoza mkutano.  Waziri  Membe ametoa ahadi ya ushiriki zaidi wa Tanzania  katika operesheni  za kulinda amani chini ya Umoja wa Maifa
  Sehemu ya washiriki wa mkutano wa  uimarishaji wa  Operesheni za Kulinda Amani uliokuwa umeandaliwa na Marekani na kufanyika hapa Umoja wa  Mataifa sambaba na  majadiliano ya jumla ya   Baraza Kuu la 69 la Umoja wa Mataifa ( UNGA) zaidi ya  nchi therethini zimetoa ahadi zao wakati wa mkutano huo uliohudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban ki  Moon
  Mhe. Waziri akiteta jambo na  Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano huo ambao uliongozwa na  Makamu wa Rais wa Marekani Bw. Joe Biden.


  0 0

  President Jakaya Mrisho Kikwete chats with  Cable News Network (CNN) 's Richard Quest and Maggie Lake when he visited  CNN Studios at the  Time Warner Cente in New York.  
  CNN is an American basic cable and satellite television channel that is owned by the Turner Broadcasting System division of Time Warner. 
  The 24-hour cable news channel was founded in 1980 by American media proprietor Ted Turner.  Upon its launch, CNN was the first television channel to provide 24-hour news coverage, and was the first all-news television channel in the United States.
  While the news channel has numerous affiliates, CNN primarily broadcasts from its headquarters at the CNN Center in Atlanta, theTime Warner Center in New York City, and studios in Washington, D.C. and Los Angeles. CNN is sometimes referred to as CNN/U.S. to distinguish the American channel from its international sister network, CNN International.
  President Jakaya Mrisho Kikwete poses with CNN's Richard Quest and Maggie Lake when he visited CNN Studios at the Time Warner Building in New York
  President Jakaya Mrisho Kikwete presents an elephant doll to  CNN's Richard Quest when he visited CNN Studios at the Time Warner Cenytre  in New York. Right is Ms. JulietRugeiyamu Kairuki, the Executive Director of the Tanzania Investment Centre. The Tour was jointly organized by the TIC and CNN as part of an on going partnership to promote Tanzania  as an attractive destination for investment and tourism. 
  They also discussed  the forthcoming African Journalist of the year Awards Ceremony to be held in Dar es salaam later this year.

  0 0

  DSC_0316

  Chief Executive Officer, MeTL Group, Hon. Mohammed Dewji.


  0 0

  Diwani wa Kata ya Kipawa Mhe. Bona Kaluwa akifafanua jambo kwa wajumbe wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Shina la Pamba jijini Dar es Salaam, mapema jana wakati alipokuwa mgeni rasmi katika kutambulisha jumuiya hiyo.Shina hilo lipo katika Kata ya Kivukoni , Manispaa ya Ilala.
  Diwani wa Kata ya Kipawa Mhe. Bona Kaluwa(katikati) akizungumza na wajumbe wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Shina la Pamba jijini Dar es Salaam, mapema jana wakati alipokuwa mgeni rasmi katika kutambulisha jumuiya hiyo.Tawi hilo lipo katika Kata ya Kivukoni , Manispaa ya Ilala.Kulia ni Mwenyekiti UWT Kata ya Kivukoni Bibi. Rahilu Nyundo na kushoto ni Mwenyekiti wa UWT Shina la Pamba Bibi. Sophia Mbwille.
  Diwani wa Kata ya Kipawa Mhe. Bona Kaluwa akipokea risala ya UWT Shina la Pamba kutoka kwa Mjumbe wa Jumuiya hiyo Bibi. Twihuvila Faith Nyimbo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa mgeni rasmi katika mkutano wa jumuiya hiyo.
  Diwani wa Kata ya Kipawa Mhe. Bona Kaluwa akifurahia jambo na wajumbe wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Shina la Pamba jijini Dar es Salaam, mapema jana wakati alipokuwa mgeni rasmi katika kutambulisha jumuiya hiyo.Shina hilo lipo katika Kata ya Kivukoni , Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wajumbe wa UWT Shina la Pamba lililoko katika manispa ya Ilala jijini Dar es Salaam wakimskiliza mgeni rasmi ambaye ni Diwani wa Kata ya Kipawa Mhe. Bona Kaluwa (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao jana jijini Dar es Salaam. Picha zote na Frank Shija, MAELEZO

  0 0

  Msanii wa Muziki wa Taarabu na mpiga Gitaa maarufu nchini Bw. Thabit Abdul akizungumza na vijana wa jijini la Dar es Salaam wakati wa hafla ya Jamvi la Vijana ambalo uendeshwa maramoja kila mwezi na Kituo cha Vijana UMATI kilichopo wilayani Temeke alipokuwa mgeni rasmi katika jamvi hilo jana jijini Dar es Salaam. Jamvi hilo lilikuwa na ujumbe mahususi kwa vijana uliolenga kuwa hamasisha kufika katika vituo vya afya kwa ajili ya kuchunguza afya zao na kupata matibabu.
  Mratibu wa Kituo cha Vijana cha UMATI kilichopo Temeke jijini Dar es Salaam Bi. Upendo Daud akifafanua jambo kwa vijana waliohudhuria Jamvi la Vijana katika kituo hicho jana jijini Dar es Salaam. Ambapo jamvi hilo lilikuwa na ujumbe mahususi kwa vijana uliolenga kuwahamasisha kufika katika vituo vya afya kwa ajili ya kuchunguza afya zao na kupata matibabu.
  Msanii wa Muziki wa Taarabu na mpiga Gitaa maarufu nchini Bw. Thabit Abdul akipima kwa hiari Virusi vya Ukimwi jana jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuhamasisha vijana kujitokeza kujua afya za na kupata matibabutukio hilo limefanyika jana alipokuwa mgeni rasmi katika ya Jamvi la Vijana ambalo uendeshwa mara moja kila mwezi na Kituo cha Vijana cha UMATI kilichopo wilayani Temeke. Jamvi hilo lilikuwa na ujumbe mahususi kwa vijana uliolenga kuwa hamasisha kufika katika vituo vya afya kwa ajili ya kuchunguza afya zao na kupata matibabu.Kushoto ni Mnasihi wa Kituo hicho Bibi. Neema Orgeness.
  Msanii wa Muziki wa Taarabu na mpiga Gitaa maarufu nchini Bw. Thabit Abdul akipata maelekezo ya matumizi sahihi ya Kondomu kutoka kwa mueleisha Rika wa Kituo cha Vijana cha UMATI kilichopo Temeke jijini Dar es Salaam Bi. Mwanahamis Issa(kushoto) alipo kuwa mgeni rasmi katika Jamvi la Vijana ambalo ufanyika kila mwisho wa mwezi.Mwezi huu jamvi hilo lilikuwa na ujumbe mahususi uliolenga kuwa hamasisha vijana kufika katika vituo vya afya kwa ajili ya kuchunguza afya zao na kupata matibabu.Kushoto ni Mnasihi wa Kituo hicho Bibi. Neema Orgeness.
  Kikundi cha Sanaa cha Malezi kikitoa burudani kwa vijana wakati wa Jamvi la Vijana jana jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya washiriki wa Jamvi la Vijana wakifurahi burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali waliotumbuiza na kutoa burudani katika Jamvi la Vijana lilofanyika jana jijini Da es Salaam. Jamvi la Vijana uendeshwa mara moja kila mwezi na Kituo cha Vijana cha UMATI kilichopo wilayani Temeke kwa mwezi huu Jamvi hilo lilikuwa na ujumbe mahususi kwa uliolenga kuwahamasisha vijana kufika katika vituo vya afya kwa ajili ya kuchunguza afya zao na kupata matibabu. PICHA NA FRANK SHIJA, MAELEZO

  0 0

   Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la kisasa la Kigamboni, kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi Karrim Mataka (kulia), akitoa maelezo ya mradi ujenzi wa daraja hilo kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari, wanaotembelea mradi mbalimbali ya uwekezaji unaofanywa na NSSF. Wa pili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Creasentius Magori.
   Wahariri wa Vyombo vya Habari, wakijaribu kupita kwenye njia ya dharura, kwa ajili ya kuangalia mradi mkubwa wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, unaofanywa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
   Wahariri wa Vyombo vya Habari, wakimsikiliza kwa makini, Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la kisasa la Kigamboni, kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi Karrim Mataka (mwenye koti kulia), wakati akitoa maelezo ya mradi ujenzi wa daraja hilo, wakati wahariri hao, walipotembelea miradi mbalimbali ya uwekezaji inayofanywa na NSSF. Wa tatu kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Cresentius Magori. 
   Wahariri wa Vyombo vya Habari wakimshuhudia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Cresentius Magori, akipita kwenye kwenye kivuko cha muda, wakati wakitoka kuangalia mradi mkubwa wa Ujenzi wa daraja la kisasa la Kigamboni, Dar es Salaam jana.
   Wahariri wa Vyombo vya Habari, wakimsikiliza kwa makini, Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la kisasa la Kigamboni, kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi Karrim Mataka (mwenye koti), wakati akitoa maelezo ya ujenzi wa daraja hilo, wakati wahariri walipotembelea miradi mbalimbali ya uwekezaji inayofanywa na NSSF.
   Wahariri wa Vyombo vya Habari wakipita kwenye daraja la muda, lililojengwa kwa ajili ya kupitisha vifaa vya ujenzi, walipofanya ziara ya kuangalia miradi mikubwa ya uwekezaji inayofanywa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dar es Salaam jana.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Cresentius Magori, akijibu maswali ya Wahariri wa Vyombo vya Habari, walipotembelea mradi mkubwa wa uwekezaji katika Kijiji cha DEGE Eco, Kigamboni, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha, Lodovick Mroso na Meneja Kiongozi wa Mahusiano na Huduma kwa Wateja, Eunice Chiume.

  0 0

  Walimu waliokuwa wakiendesha mafunzo kwa watoto hao wakiwa katika picha ya pamoja. Kutoka kushoto ni Beatha Qambayot, Zilpa Masunga, Mtendaji Mkuu wa Olimpiki Maalumu Tanzania, Frank Macha na Alphonsia Mwairafu.
  Walimu hao wakiwa wameshika mipira ya kufundishia.
  Watoto wenye ulemavu wa akili wakiwa katika picha na  wazazi, pamoja na walimu wao baada ya kumaliza mafunzo  ya mwezi mmoja ya Olimpiki Maalumu Tanzania  yaliyofikia tamati wilayani Temeke Dar es Salaam leo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Na: Geofrey Tengeneza

  Shirika la hifadhi la taifa (TANAPA) kwa kushirikiana na mamlaka ya hifadhi ya eneo la Ngorongoro pamoja na shirika la ndege la Ethiopia wamedhamini onesho la kimataifa ya utalii lijulikanalo kama ‘Swahili International Tourism Expo’ (S! TE).

  Taasisi hizo tatu zinakuwa ndio wadhamini wakuu wa maonesho hayo ya kimataifa ya utalii ya kwanza Tanzania yanayoandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya Pure Grit Project and Exhibition Management Ltd ya Afrika Kusini ambao pia ndio waandaji wa onesho la utalii la INDABA linalofanyika kila mwaka Afrika Kusini.. Onesho hili la kwanza la S!TE litafanyika kuanzia mwezi Oktoba, tarehe 1 – 4, 2014 katika ukumbi wa mikutano Mlimani City. Pamoja na maonesho ya bidhaa na huduma mbalimbali za utalii lakini pia kutakuwa na maonesho ya utalii wa utamaduni wa mtanzania.


  Aidha sambamba na maonesho kutakuwa pia na kongamano kwa muda wa siku zote nne ambapo mada mbalimbali kuhusu utalii zitawasilishwa na wataalamu katika sekta ya utalii na kujadiliwa.


  Onesho hili la utalii la kimataifa ambalo lmelenga watalii wanaokuja Afrika yanatarajia kuvuta maelfu ya wasafirishaji wakubwa wa watalii na wadau wa sekta ya kitalii na usafiri kutoka kila pande za Dunia. Kama sehemu ya udhamini wake, licha ya mashirika mengine, shirika la ndege la Ethiopia ndilo litakuwa wasafirishaji wakubwa wa watalii na wandishi wa habari wa kimataifa kutoka nchi mbalimbali duniani zikiwemo Marekani, Uingerza, Ujerumani n.k wanaokuja kwa ajili ya onesho hili.

  S!TE litakalo kuwa likifanyika kila mwaka mwezi Oktoba, litachukua muundo wa maonesho ya kiusafiri na kibiashara likilenga pia katika kuonyesha utalii endelevu wa kisasa, uhifadhi na mambo mengine yanayohusiana na masoko ya utalii.


  Ni ukweli usiopingika kwamba Tanzania imebeba vivutio mbalimbali vya kitalii kama vile mlima Kilimanjaro, Zanzibar na hifadhi ya Taifa ya Serengeti.


  Kwa ujumla Tanzania inaweza tu kuitwa kitovu cha vivutio vya asili Afrika kwani Tanzania ndio nchi pekee yenye vivutio vitatu kati ya saba vya asili barani afrika ambavyo ni Mlima Kilimanjaro ambao ni mrefu kuliko yote barani afrika; Ngorongoro Crater ambayo ni kubwa duniani isiyomomonyoka, na hifadi ya Taifa ya Serengeti, maarufu kwa nyumbu wanaohama wakiwa katika makundi makubwa na misururu mirefu kutoka kusini kuelekea kaskazini na kurejea.

  0 0

  Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi akishangilia bao aliloifungia timu yake wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara dhidi ya Polisi ya Morogoro uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Ramadhani Singano 'Messi'
  Golikipa wa Polisi Morogoro, Abdul Ibad akijaribu kuokoa bila mafanikio kiki iliyopigwa na mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
  Golikipa wa Polisi Morogoro, Abdul Ibad akijaribu kuokoa bila mafanikio kiki iliyopigwa na mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. 
   Okwi akiipangua ngome ya Polisi Moro.
  Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi akimtoka beki wa Polisi Morogoro, Lulanga Mapunda wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

   Mshambuliaji wa Simba, Amisi Tambwe akiwa katikati ya wachezaji wa Polisi Morogoro,  Lulanga Mapunda (kushoto) na golikipa wa timu hiyo, Abdul Ibad  wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
   Mshambuliaji wa Simba, Amisi Tambwe akiwa katikati ya wachezaji wa Polisi Morogoro,  Lulanga Mapunda (kushoto) na golikipa wa timu hiyo, Abdul Ibad  wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
   Kipa wa Polisi Moro akipata matibabu baada ya kuuimia.Picha na Francis Dande,Globu ya Jamii.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa JET, John Chikomo akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya uendeshaji wa chama cha waandishi wa habari za mazingira kwenye mkutano huo.
  Baadhi ya viongozi wa chama cha waandishi wa habari za mazingira JET katika mkutano wa mwaka wa chama hicho ulioganyika jijini Dar Es Salaam, kutoka kushoto ni Mkurugenxi Mtendaji wa JET John Chikomo, Mwenyekiti wa JET Johnson Mbwambo, Katibu Mtendaji wa JET Chris Rweyemamu na Makamu Mwenyekiti wa JET Aisha Dachi.
  Baadhi ya waandishi wa habari za mazingira ambao pia ni wanachama wa JET na wajumbe wa mkutano huo wakiwa katika majadiliano wakati mkutano ukiendelea jijini Dar Es Salaam.
  Baadhi ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo wakiwemo waandishi wa habari za mazingira kutoka mikoa mbalimbali nchini ambao ni wananchama wa JET wakipitia nyaraka mbalimbali za mkutano huo­ (picha zote na Vedasto Msungu wa JET)

  0 0

   Kamishina Mkuu Msaidizi Programu ya Vijana wa Chama cha Skauti Tanzania (TSA), Mary Anyitike (kushoto), akimvisha  Nishani ya Skauta, Safi Shabani kiongozi wa Skauti kutoka  Shule ya Sekondari Lugoba iliyopo Bagamoyo mkoa wa Pwani wakati wa hafla ya kufunga mashindano hayo jana.
   Kamishina Mkuu Msaidizi wa Utawara Bora wa Chama cha Skauti Tanzania (TSA), Mwalimu mstaafu John Lusunike (kushoto), akikagua skauti kabla ya kuanza mashindano Septemba 23,2014. 
   Vijana wa Skauti wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa tayari kwa ukaguzi.
   Vijana wa Skauti wa Kikosi cha Simba kutoka Mkoa wa Morogoro ambao walikuwa washindi wa Mashindano ya Skauti katika nchi za Afrika Mashariki yaliyofanyika nchini Burundi mwaka 2013 wakiwa tayari kwa ukaguzi huo kabla ya mashindano hayo yenye lengo la kuwapata washiriki katika mashindano ya Afrika Mashariki yatakayofanyika nchini Rwanda Desemba 2014.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samia Suluhu akiongoza kikao cha Bunge hilo Septemba 27, 2014.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd wakiteta Bungeni mjini Dodoma Septemba 27, 2014.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Stephene Wasira akichangia Bungeni mJini Dodoma Septemba 27, 2014.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Kingunge Ngombale Mwiru akichangia bungeni mjini Dodoma Septemba 27, 2014.


  0 0

  Na RAMADHANI ALI /HABARI MAELEZO ZANZIBAR
  Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu (UNFPA) limekabidhi msaada wa magari manne ya Ambulance kwa Wizara ya Afya ya Zanzibar ambayo yatatumika katika Hospitali nne visiwani hapa.

  Mwakilishi wa UNFPA Tanzania Dkt. Natalia Kanem alimkabidhi Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman magari hayo katika sherehe fupi zilizofanyika Wizarani Mnazi mmoja.

  Dkt. Natalia alitaka magari hayo yatumike kwa uangalifu ili kufikia malengo ya millennia ya kupunguza idadi ya vifo vya mama wajawazito na watoto wanaozaliwa hasa katika maeneo ya vijijini.

  Alisema moja ya sababu inayopelekea vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga ni tatizo la usafiri ambalo linachangiwa na uwezo mdogo wa baadhi ya familia hasa katika maeneo ya vijijini.

  Aliongeza kuwa msaada huo ni sehemu ya Mpango maalum wa Shirika la Umoja wa Mataifa ulioanza mwaka 2011 na kumalizika Juni 2015 ambao huenda ukaendelea hadi mwaka 2016 kusadia masuala ya Afya na Lishe.

  Amesema mpango huo wa miaka minne ambao unahusisha maeneo makuu saba unaendeshwa kwa pamoja na Mashirika manne ya Umoja wa Mataifa ambayo ni WHO, UNFPA, UNICEF na WFPA.

  Mwakilishi huyo wa UNFPA amewapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein kwa juhudi kubwa wanazochukua katika kuimarisha huduma za mama wajawazito na watoto wachanga.

  Aliesema UN inathamini juhudi hizo na juhudi za kuimarisha uchumi hivyo aliahidi kuwa wataendelea kuunga mkono kuhakikisha mama wajawazito na watoto wanaozaliwa wanaendelea kuishi katika mazingira yaliyo salama.

  Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman, alilishukuru Shirika la UNFPA kwa misaada mbali mbali inayotoa kwa Wizara hiyo na ameahidi kuwa magari hayo yatatumika katika malengo yaliyokusudiwa.

  Amekiri kuwa tatizo la usafiri kwa mama wajawazito Zanzibar limekuwa likiwasumbua wananchi wengi na inafikia wakati akinamama hujifungua wakiwa kwenye gari wakati wa kupelekwa Hospitali ambazo hazina stara wala hazifai kwa kazi hiyo.

  Alieleza matarajio yake kuwa tatizo hilo kwa sasa litapungua kwa kiasi kikubwa baada ya kupatiwa msaada huo ambao umekuja wakati muwafaka ambapo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaelekeza juhudi zake kuimarisha huduma za afya mijini na vijijini.

  Gari hazo za ambulance ambazo zitapelekwa katika Hospitali ya Kivunge, Mwembeladu, Mkoani na Micheweni zimegharimu shilingi milioni 245,000,000 za kitanzania.
  Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mh. Rashid Seif Suleiman akionyesha moja ya funguo za gari ya Ambulance zilizotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu (UNFPA), alieshikana mkono ni Mwakilishi wa Shirika hilo Dkt. Natalia Kanem.
  Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mh. Rashid Seif wakati akilijaribu moja ya gari hilo zilizotolewa na UNFPA katika hafla ilizofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
  Gari nne za Ambulance zilizotolewa na Shirika la UNFPA zikiwa zimeegeshwa mbele ya Ofisi ya Wizara ya Afya Mnazimmoja.
  Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mh. Rashid Seif akizungumza na watendaji wa Wizara yake na wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za kukabidhiwa msaada wa gari za ambulance uliotolewa na UNFPA.( Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

  0 0


older | 1 | .... | 586 | 587 | (Page 588) | 589 | 590 | .... | 3286 | newer