Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 584 | 585 | (Page 586) | 587 | 588 | .... | 3285 | newer

  0 0

   Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inashuka uwanjani Oktoba 12 mwaka huu kuikabili Benin katika mechi ya kirafiki ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

  Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni. Programu ya Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kwa ajili ya mechi hiyo itatangazwa baadaye na Kocha Mkuu Mart Nooij.

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaendelea na taratibu nyingine kwa ajili ya mechi hiyo ikiwemo usafiri wa Benin kuja nchini, ambapo timu hiyo inatarajiwa kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Oktoba 10 mwaka huu ikiwa na msafara wa watu 28.

  Pambano la Stars na Benin litatanguliwa na mechi ya kudumisha upendo kati ya viongozi wa dini ya Kikristo na Kiislamu.

  Wakati huo huo, kutokana na mechi hiyo ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inafanyiwa marekebisho madogo, na marekebisho hayo yatatangazwa kesho (Septemba 26 mwaka huu).

  RAIS MALINZI KUFUNGA KOZI YA WANAWAKE

  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi anatarajia kufunga mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa vyama vya mpira wa miguu wa wanawake vya mikoa ya Tanzania Bara.

  Hafla ya kufunga mafunzo hayo itafanyika kesho (Septemba 26 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za TFF, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

  Mafunzo hayo ya siku tano yalishirikisha viongozi 34 wakiwemo baadhi ya waandishi wa habari na Meneja wa Twiga Stars, na yaliendeshwa na Mkufunzi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Henry Tandau.

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuchanyata kwa Power tiller kwa ajili ya upandaji miche ya mpunga kwenye vijaruba vya kilimo cha zao hilo cha Umwagiliaji vilivyopo katika kijiji cha Mhenge,Kwamndolwa wilayani Korogwe mkoani Tanga leo.

  0 0

   Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platinumz akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza ushirikiano wake na kampuni inayoendesha programu ya Mziiki.Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Spice VAS Africa wanaoendesha programu hiyo ya Mziiki,Arun Nagar na kushoto ni Meneja wa Diamond Platinumz,Babu Talle.

  Mkali wa Bongo Flava Tanzania Diamond Platnumz amepewa nafasi ya kushirikiana na Mziiki kama Brand Partner. Msanii huyu ambaye amefanikiwa kushinda tuzo mbalimbali amekuwa wa kwanza kutia saini kama Brand Partner na tayari ni mmoja wa mamia ya wasanii pekee wa Afrika walio katika program ya muziki unaopendwa zaidi Afrika kupitia simu za kiganjani pamoja na kuwa mwakilishi wa bidhaa hiyo akiwakilisha nchi yake.

  "Tunafurahi kwamba Diamond Platnumz kwa sasa ni Brand Partner wa Mziiki," anasema Arun Nagar, Mkurugenzi Mtendaji wa Spice VAS Africa, watengenezaji wa Mziiki. "Kwa kushirikiana na msanii mwenye kiwango kama Diamond pamoja na mashabiki wake ni hatua nzuri kwa Mziiki.
  Ushirikiano kama huu unaonyesha dhamira yetu ili kuendelea kuhakikisha kwamba watumiaji wetu na muziki bora wa Afrika unawafikia pale walipo na tutaweza kufanya kazi karibu na Diamond na kupanua wigo wa wateja wetu na kuwapatia mashabiki wake zaidi ya kile walichotarajia. Nadhani pia ni ushahidi wa ukweli kwamba sisi tumechukua nafasi kubwa katika ulimwengu wa muziki streaming na wapenzi wa muziki wa Afrika wanapaswa kukumbuka hilo. "


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohamed Shein mwenye tai nyekundu akimsikiliza Mkurugenzi mkuu wa wa Mamlaka ya kusimamiaUvuviwa Bahari kuu Tanzania Zahor Kassim Mohammed akielezea maswali mbalimbali kuhusiana na Usimamizi wa Uvuvi baharini katika Maadhimisho ya siku ya Bahari Duniani huko Bwawani Mjini Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohamed Shein wakwanza kushoto akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Bandari Kapten Ally Machano kuhusiana na uwakaji wa maboya yanayotumia Umeme wa Jua katika Maadhimisho ya siku ya Bahari Duniani huko Bwawani Mjini Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohamed Shein wakwanza kulia akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Bandari Kapten Ally Machano kuhusiana na uwakaji wa Maboya ya Zamani katika Maadhimisho ya siku ya Bahari Duniani huko Bwawani Mjini Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohamed Shein wakwanza kushoto akipata maelezo kutoka kwa Kamanda Mkuu wa Boti KMKM Luten Hassan Ali Makame kuhusiana na namna wanavyokabiliana na matukio mbalimbali ya baharini katika Maadhimisho ya siku ya Bahari Duniani huko Bwawani Mjini Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0

  Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME - SACP amesema tarehe 25/09/2014 alfajiri vimeokotwa vipeperushi maeneo mbalimbali mjini Dodoma vyenye ujumbe ufuatao ONYO – DODOMA SI MAHALI PA KUFUGA WEZI WA FEDHA ZA UMMA. UTAKAYEINGIA BUNGENI KUANZIA KESHO, YATAKAYOKUPATA UTAJUTA.

  Kamanda MISIME amesema tumeendelea kupokea taarifa za watu wanaodaiwa kuandaa vipeperushi hivyo na tunafanyia kazi ili tuweze kuwakamata ili washtakiwe kulingana na kosa walilolitenda hasa la kutoa vitisho na kuhamasisha uvunjifu wa amani.

  Aidha Kamanda MISIME ameongeza ametoa wito kwa wananchi na wageni wanaofika Dodoma watii sheria bila shuruti.  Kila mmoja ajiepushe kujiingiza kwenye kuhamasisha uvunjifu wa amani, kujiingiza katika mikusanyiko isiyo halali na maandamano ambayo yameshapigwa marufuku na Jeshi la Polisi.  

  Atakayekiuka na kujiingiza katika vitendo hivyo vya kiuhalifu atashurutishwa kwa nguvu zote kwa mujibu wa sheria za Nchi na kwa mamlaka iliyopewa Jeshi la Polisi.

  Kamanda MISIME ameongeza kuwa wananchi na wageni wapenda amani waendelee na shughuli zao kama kawaida kwani Jeshi La Polisi limejiimarisha ipasavyo kukabiliana na yeyote yule atakayekiuka sheria na maelekezo yaliyotolewa.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Charles Pallangyo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kabla ya kukabidhi mabasi 6 kwa wakuu wa vyuo vya Afya kutoka katika maeneo mbalimbali .Mabasi hayo yatasaidia kuaondoa upotevu wa muda na adha ya usafiri waliyokuwa wakiipata wanafunzi,watumishi na wakufunzi wa vyuo hivyo kufika kwenye maeneo ya mafunzo kwa vitendo.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Charles Pallangyo akikata utepe kwenye basi moja kati ya sita yaliyonunuliwa kwa ufadhili wa Mradi wa Mfuko wa Dunia mzunguko wa 9 ambayo yamekabidhiwa kwa wakuu wa vyuo vya afya leo jijini Dar es salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Charles Pallangyo akikagua mabasi hayo yaliyonunuliwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Dunia mzunguko wa 9 ambayo yamekabidhiwa kwa wakuu wa vyuo 6 vya afya leo jijini Dar es salaam.
  Sehemu ya ndani ya mabasi hayo yaliyotolewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Mradi wa Mfuko wa Dunia. Picha na Aron Msigwa -MAELEZO.

  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Idd akikanusha taarifa zilizoandikwa na gazeti la Mtanzania la Jumatano 24 Septemba, 2014.
  Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Mohammed Aboud akichangia mada wakati wa mkutano na waandishi wa habari Gazeti hilo.
  Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wakifutailia kwa makini taarifa toka Balozi Seif Ali Idd. (Picha zote na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma)

  Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma. 

  MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Idd amekanusha madai mbalimbali yaliyotolewa na Gazeti la Mtanzania la Jumatano 24 Septemba, 2014 ambalo liliandika kuwa ‘Siri zavuja za AG Zanzibar kujiuzulu’.

  Akikanush taarifa hizo, Mhe. Balozi Idd amesema kuwa Mhe. Othman alitakiwa ashiriki katika kamati kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa upande wa Zanzibar lakini kutokuwepo kwake katika Kamati sio kikwazo cha kupatikana kwa Katiba, kwani waliokuwepo ndani ya kamati kwa upande wa Zanzibar walitosheleza kuiwakilisha Zanzibar kikamilifu.


  0 0

  Jioni hii katika Makutano ya barabara za mitaa ya Aggrey na India,ambapo gari hiyo aina ya Noah iliyokuwa ikitokea katika kituo cha Mafuta imeigonga pikipiki hiyo iliyokuwa katika mtaa wa Aggrey kama ionekanavyo pichani.Dereva wa pikipiki (wa tatu kulia kama anavyoonekana akipatana na mwenye gari) akiweza kuruka na kutoka salama salimini.

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini,John Mongela akisalimiana na Warembo wanaoshiriki shindano la Redd’s Miss Tanzania 2014, walipomtembelea ofisini kwake jijini Arusha leo. Warembo hao Septemba 27 wanataraji kupandaa jukwaani kuwania taji la Miss Top Model litakalofanyika jijini Arusha.
   Warembo wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mAMLAKA ya maji safi na maji taka Jijini Arusha(AUWSA) walipowatembelea leo.
   Wakiwasili AICC.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Bw. Salum Chima akizungumza wakati akifungua semina ya Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa maafisa wa makampuni mbalimbali katika  (Kanda ya Kinondoni) mkoani Tanga leo

  Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF kanda ya Kinondoni (inayojumuisha wilaya za Kibaha,Bagamoyo na mkoa wa Tanga),Bi. Zahra Kayugwa akizungumza na washiriki wa semina ya Mfuko wa PPF kwa maafisa wa makampuni mbalimbali katika (Kanda ya Kinondoni) mkoa wa Tanga leo.
  Maafisa kutoka makampuni mbalimbali katika (kanda ya Kinondoni )mkoa wa Tanga wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa leo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  NA ANDREW CHALE, BAGAMOYO

  KUNDI maalufu la ngoma asili la Utandawazi Theater Group ‘Matwigachallo’ jioni ya kesho wanatarajiwa kuwasha moto wa aina yake kwenye tamasha la Kimataifa la 33 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, lililoanza Septemba 22 mwaka huu kwenye viunga vya chuo hicho.

  Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa tamasha hilo, Abmic am Bafadhil ‘Bura’ alieleza kuwa, kundi hilo ambalo kwa sasa limejizolea umaalufu mkubwa ndani na nje ya Tanzania, linatarajiwa kutoa burudani ya ngoma za asili sambamba na watoto wadoigo wanaotia fola kwa sasa katika sanaa hiyo ya utamaduni, Watoto wadogo Gozibet Bwere (4) na Nyambuli Aginess Muganga (5).
  “Kundi la Utandawazi ‘Matwigachallo’, la Ukerewe, litawasha moto kwa burudani ya aina yake, pamoja na watoto wao wadogo wenye uwezo na kipajimkikubwa cha kuimba, kucheza na kupiga ngoma” alieleza Bura.

  Na kuongeza kuwa, watoto hao wamekuwa maalufu kwa sasa hasa katika sherehe za Kitaifa na Kimataifa kwa kupata kuonyesha uweo wao hivyo kwa uwepo wao kwenye tamasha hilo, itatoa fursa kwa watu mbalimbali kuwaona.

  Mbali na kundi hilo la Utandawazi, pia kutakuwa na Umoja Culture Flying Carpet ambao wataonyesha michezo mbalimbali ya sarakasi, ngoma, muziki na michezo mingine kibao.

  Aidha, Jumamosi kutatanguliwa na mahafali ya 25 ya Chuo hicho huku wahitimu wa 37 wakitarajiwa kutunukiwa vyeti vyao, ambao Wanawake 11 na wanaume 26.

  0 0

  Meneja Kiongozi wa NSSF Mkoa wa Temeke, Yahya Mhamali akizungumza wakati wa semina iliyoandaliwa na Mkoa wa NSSF Temeke kwa Waajiri wake ambayo ilihudhuriwa na Maofisa Rasirimali Watu pamoja na Wahasibu kwa ajili ya uelewa kuhusu moboresho ya formula mpya ya pensheni ambayo imetolewa na SSRA pamoja na huduma zilizoboreshwa kwa kiwango cha Kimatifa kwa NSSF Temeke (ISO). Semina hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam. Wa tatu kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori, wa kwanza ni Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa NSSF, Eunice Chiume.
   Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori, akifafanua jambo wakati wa semina iliyoandaliwa na Mkoa wa NSSF Temeke kwa Waajiri wake ambayo ilihudhuriwa na Maofisa Rasirimali Watu pamoja na Wahasibu kwa ajili ya uelewa kuhusu maboresho ya formula mpya ya pensheni ambayo imetolewa na SSRA pamoja na huduma zilizoboreshwa kwa kiwango cha Kimatifa kwa NSSF Temeke (ISO). Kushoto ni Meneja wa Idara za Serikali na Balozi GDE, Rehema Chuma na Meneja Mafao, James Oigo.
  Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakimsikiliza mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa semina hiyo.


  0 0

  OKTOBA 12 mwaka huu katika kuadhimisha siku ya amani duniani viongozi wa dini wanatarajia kujitupa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kulisakata kabumbu safi kabisa, wakiwa na lengo la kudumisha amani iliyopo nchini.

  Mtanange huo utawajumisha Masheikh,Maimamu,Maaskofu,Wachungaji na Mapadre na mgeni rasmi katika mchezo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye tayari amekubali kuungana na viongozi hao wa dini.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mchezo huo alisema kuwa Mkuu wa Mkoa huo, Said Sadick atakuwa mwamuzi msaidizi akisaidiwa na Kamishna wa Kanda Maalumu, Seleman Kova na Afande IGP Ernest Mangu atakuwa mpuliza kipyenga wa kati.

  Alifafanua kuwa viongozi hao wa dini tayari wameshaanza mazoezi kwa jili ya kujiweka tayari kwa ajili ya kufanya vizuri katika mtangane huo wa kuhamasisha amani na ulivu nchini katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.

  Aliongeza kuwa wanaendelea na mazoezi hayo chini ya kocha mjerumani na Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam, itazipeleka timu mbili mkoani Morogoro kwa ajili ya kujifua zaidi na mtanage huo utakaokuwa wa kukata na shoka kutokana na jinsi timu za viongozi hao wa dini zilivyojipanga kucheza mchezo huo wa amani.

  Ili kujindaa vema na mchezo huo Mwakilishi Mkazi wa Shirilka la KAS,Tanzania, Stefan Reith, alikabidhi kwa Sheikh wa Dar es Salaam, Alhad Salum vifaa mbalimbali vya michezo ikiwemo mipira, jeshi na viatu.
  Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salim (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu maandalizi ya mchezo wa kirafiki wa mpira wa miguu kati ya Masheikh na Mapadre utakaofanyika uwanja wa Taifa Octoba 12-2014. Alhadi Salim ndiye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi wa mchezo huo. Kushoto ni Katibu wa Kamati ya Amani kutoka Kanisa la Anglikana Padri John Solomon na Mwakilishi Mkazi wa Shirilka la KAS,Tanzania Stefan Reith.
  Mwakilishi Mkazi wa Shirilka la KAS,Tanzania Stefan Reith (kushoto), akimkabidhi baadhi ya vifaa vya michezo Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salim kwa ajili ya maandalizi wa mechi hiyo. HABARI/PICHA NA PHILEMON SOLOMON    

  0 0

   Rais wa Shirikisho la Dunia la mchezo wa Karate (UPAM), Profesa  Martina Maurizio (kulia), akiwaelekeza jambo wachezaji wa mchezo huo walioko kambini Dar es Salaam jana. Wachezaji sita wa timu hiyo wanatarajia kuondoka Septemba 28 mwaka huu kwenda nchini Albania kushiriki mashindano ya dunia ya mchezo huo.
   Wachezaji hao sita wakiwa wameshika bendera ya timu hiyo. Kulia ni  Rais wa Shirikisho la Dunia la mchezo wa Karate (UPAM), Profesa  Martina Maurizio.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  DSC_0519
  Shuhuda aliyenusurika kwenye mauaji ya Albino ambaye amekatwa mikono yote miwili, Mariam Stanford akitoa ushuhuda wake na killio chake mbele ya meza na wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani iliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mnazi mmoja.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).

  =======  =======  =======
  Mwanamke albino Mariam Stanford aliyepoteza mikono yake yote miwili wakati iliponyofolewa na majahili asiowajua Oktona7, 2008 ameitaka serikali kuwanyonga wote wanaopatikana na hatia ya kuua albino nchini.

  Alisema hata adhabu ya kifungo cha maisha haiwatoshi kwa jinsi wanavyosababisha maisha ya mashaka na yenye uchungu kwa walemavu wa ngozi. Akiongea kwa uchungu huku hapa na pale akitulia kwa kuzidiwa na machozi kiasi cha kushidwa kuzungumza Stanford ambaye alisema wakati akikatwa mikono yake alikuwa na mimba ya miezi mitano na ambayo ilitoka alisema majahili hao si wa kusamehewa.

  Alisema akiwa mama wa familia kitendo cha kumuondolea mikono yake kimemfanya kuwa tegemezi hali ambayo inaongeza maumivu juu ya maumivu ambayo anayo ya kunyanyapaliwa na jamii.

  Alisema hayo wakati akitoa ushuhuda katika adhimisho la siku ya amani duniani iliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam. Alisema japokuwa Tanzania inaelezwa kuwa nchi ya amani wananchi wake wenye ulemavu wa albino hawana amani kutokana na kuwindwa kama digidigi. Alisema kwa sasa Tanzania ni kisiwa cha matatzio kwa kundi hilo ambalo sasa linajificha na wala kutokujua kesho ikoje au siku hiyo ikoje.
  DSC_0534
  Mke wa Balozi wa Uturuki nchini Yesim Davutoglu, akilia kwa uchungu baada ya kusikia shuhuda kutoka kwa mhanga wa mauaji ya Albino aliyekatwa mikono yote miwili, Mariam Stanford (hayupo pichani) ambaye hadi sasa anapewa matunzo na Shirika la Under The Same Sun.


  0 0

  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Profesa Rwekaza Mukandara akifungua mkutano wa mabadiliko ya tabianchi unaofanyika katika hoteli ya Kunduchi nje kidogo ya jiji la Dar Es salaam ukiwashirikisha watafiti na wanamazingira kutoka nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Tanzania.
  Mkurugenzi wa kituo cha mafunzo ya mabadiliko ya tabianchi cha chuo kikuu cha Dar Es Salaam Profesa Pius Yanda akiwasilisha mada katika mkutano huo.
  Profesa Mukandara akijadiliana na wataalam wanaoshiriki kwenye mkutano huo muda mfupi baada ya ufunguzi wa mkutano huo unaofanyika Kunduchi nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
  Wataalam wa mazingira na watafiti kutoka vyuo vikuu mbalimbali kikiwemo cho kikuu cha Dar es salaam na wadau wengine wa mazingira wanaohudhuria mkutano huo wa mabadiliko ya tabianchi katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Profesa Rwekaza Mukandara muda mfupi baada ya ufunguzi wa mkutano huo.Picha zote na Vedasto Msungu.

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kulima shamba la mpunga kwenye mradi wa kilimo kwanza wa Skimu ya Mahenge.
   Mifereji ya maji kwenye shamba la skimu ya Mahenge.

  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kufyeka majani kwenye eneo la soko la sabasaba mjini Korogwe.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kujenga zahanati Mahenge kwa Mndolwa.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Kaimu mkuu wa mkoa wa Morogoro ambaye ni mkuu wa wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka akikabidhiwa zawadi ya fulana  na Mkurugenzi wa uhusiano na sheria wa TBL, Steven Kilindo yenye ujumbe wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani baada ya mkuu huyo kuzindua rasmi upimaji wa afya kwa madereva wa mabasi na malori ya masafa marefu katika kituo cha mizani cha Mikese mkoa wa Morogoro, zaidi ya madereva 200 wanatarajiwa kupimwa afya katika vituo vya Mikese Morogoro, Mkata mkoani Pwani na Makuyuni mkoani Arusha. katikati ni Mganga mkuu wa macho wa jeshi la polisi Dk Charles Msenga na kulia ni kaimu mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Morogoro, Willie Mwamasika
  Kaimu mkuu wa mkoa wa Morogoro ambaye ni mkuu wa wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka akizungumza jambo mara baada ya kuzindua rasmi upimaji wa afya kwa madereva wa mabasi na malori ya masafa marefu ikiwa sehemu ya kuanza kwa wiki ya nenda kwa usalama barabarani katika kituo cha mizani cha Mikese mkoa wa Morogoro, zaidi ya madereva 200 wanatarajiwa kupimwa afya katika vituo vya Mikese Morogoro, Mkata mkoani Pwani na Makuyuni mkoani Arusha. kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa uhusiano na sheria wa TBL, Steven Kilindo na kulia ni Mganga mkuu wa macho wa jeshi la polisi Dk Charles Msenga na kaimu mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Morogoro, Willie Mwamasika
   Mganga mkuu wa macho wa jeshi la polisi Dk Charles Msenga kulia akimpima uwezo wa kuona macho dereva wa kampuni ya usafirishaji wa abirianya Abood basi Morogoro, Augustino Mpepwa wakati wa uzinduzi wa afya kwa madereva wa mabasi na malori ya masafa marefu ikiwa sehemu ya uzindui wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani katika kituo cha mizani cha Mikese mkoa wa Morogoro, zaidi ya madereva 200 wanatarajiwa kupimwa afya katika vituo vya Mikese Morogoro, Mkata mkoani Pwani na Makuyuni mkoani Arusha.

   DK YOHANA KIBONA KUMPIMA DC ANTHONY MTAKA AFYA KULIA NI DK CHARLES MSENGA MGANGA WA JESHI LA POLISI MAKAO MAKUU PIX NO 5
  DR YOHANA KIBENA akiwaandikisha madereva tayari kupimwa afya zao katika Hospitali ya Polisi ya Morogoro. TBL imefadhili upimaji wa afya hizo. 

  0 0

  Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume Bi. Agnes Mgeyekwa akizungumza na wanamichezo wa TUMESHERIA Sports Club watakaoshiriki mashindano ya SHIMIWI Morogoro.
  Wanamichezo wa TUMESHERIA Sports Club wakimsikiliza Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume Bi. Agnes Mgeyekwa (hayupo pichani) wakati wa kuagwa kwenda kushiriki mashindano ya SHIMIWI mkoani Morogoro.
  Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Tume Bw. Peter Kalonga akizungumza wakati wa kuwaaga watumishi wa Tume watakaoshiriki mashindano ya SHIMIWI mkoani Morogoro.

  0 0
 • 09/26/14--04:00: CAREER OPPORTUNITIES


older | 1 | .... | 584 | 585 | (Page 586) | 587 | 588 | .... | 3285 | newer