Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 580 | 581 | (Page 582) | 583 | 584 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba. Mhe. Samuel Sitta akiongoza bunge hilo leo 22 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Amon Mpanju akisoma Azimio la kupitisha marekebisho ya Kanuni za Bunge Maalum leo 22 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Ezekiel Olouch akichangia mada wakati wa usomaji wa Azimio la kupitisha marekebisho ya Kanuni za Bunge Maalum leo 22 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Pindi Chana akichangia mada wakati wa usomaji wa Azimio la kupitisha marekebisho ya Kanuni za Bunge Maalum leo 22 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Selemani Jafo akichangia mada wakati wa usomaji wa Azimio la kupitisha marekebisho ya Kanuni za Bunge Maalum leo 22 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
  Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakifuatilia mjadala bungeni wakati wa usomaji wa Azimio la kupitisha marekebisho ya Kanuni za Bunge Maalum leo 22 Septemba, 2014 mjini Dodoma.

  0 0

  Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
        
  Watu wawili wameuawa Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma katika matukio mawili tofauti.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema tukio la kwanza limetokea mnamo tarehe 20/09/2014 majira ya saa 23:30hrs katika Kijiji cha Mzogole Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma ambapo mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la MWAJUMA D/O CHOMOLA mwenye umri wa miaka 48, Mgogo mkazi wa Mzogole aliuawa kwa kupigwa na Rungu tumboni upande wa kushoto na mumewake aliyefahamika kwa jina la RICHARD S/O KODI mwenye umri wa miaka 55, Mhehe mkulima na mkazi wa kijiji cha Mzogole Wilayani Mpwapwa Mkoani  Dodoma ambaye nae aliuawa tarehe 21/09/2014 majira ya saa 09:00hrs baada ya kushambuliwa na wananchi waliojichukulia sheria mkononi na alifariki dunia akiwa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa baada ya wananchi hao kupata taarifa kuwa mwanamke huyo kafariki kutokana na kipigo cha mume wake.

  Kamanda MISIME amesema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi kwani RICHARD aliuawa na wananchi baada ya kumuua MWAJUMA ambaye alikuwa mkewake aliyekuwa akiishi nae, baada ya kuchelewa kurudi kutoka kwenye sherehe iliyokuwa hapo kijijini akidhani kuwa ameenda kwenye masuala mengine.

  Aidha Kamanda MISIME amesema wananchi waliojichukulia sheria mkononi bado wanatafutwa ili wafikishwe mahakamani.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC Ms Mzimga Melu alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na Ujumbe aliofuatana nao leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Ujumbe wa Benki ya Taifa ya Biashara ya NBC unaoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Ms Mzimga Melu (wa pili kulia) walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC Ms Mzimga Melu baada ya mazungumzo alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na Ujumbe aliofuatana nao leo.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (wapili kulia) wakisalimiana na Askofu Damian Kyaruzi wa Jimbo la Sumbawanga (kulia) katika Ibada ya kumweka wakfu Askofu wa Dayosisi ya Ziwa Tanganyika, Ambele Mwaipopo iliyofanyika kwenye kanisa kuu la kiinjili la Kilutheri la mjini Sumbawanga Septemba 21, 2014. Wapili kushoto ni Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Alex Malasusa.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (wapili kulia) wakimkabidhi zawadi Askofu wa Dayosisi ya Ziwa Tanganyika, Ambele Mwaipopo (wapili kushoto) katika ibada ya kumweka wakfu Askofu huyo iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la Kiinjili la Kilutheri mjini Sumbawanga, Septemba 21, 2014. Kulia ni mke wa Askofu huyo, Tunsume Mwaipopo na kushoto ni Askofu Israel Mwakyolile wa Dayosisi ya Konde.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika ibada ya kumweka wakfu Askofu wa Dayosisi ya Ziwa Tanganyika, Ambele Mwaipopo katika Kanisa kuu la Kiinjili la Kilutheri mjini Sumbawanga Septemba 11, 2014.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (kushoto) wakiwa katika Picha ya pamoja na Askofu wa Dayosisi ya Ziwa Tanganyika, Ambele Mwaipopo na mkewe Tunsume Mwaipopo (kulia) katika katika ibada ya kumsimika Askofu huyo iliyofanyika kwenye Kanisa kuu la Kiinjili la Kilutheri mjini Sumbawanga Septemba 11, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

  The five-day East African conference on inter-religious collaboration to strengthen peace and security concluded successfully in Kigali, Republic of Rwanda, today with a resolution to create first ever East African Community Inter-Religious Council (EAC IR Council) for sustainable dialogue and information sharing among and between religious leaders and communities in the Region.

  The leaders of Inter-Religious Councils of Burundi, Rwanda, Kenya, Tanzania and Uganda signed in full view of over 150 delegates a two-page dubbed “Kigali Declaration” to pursue justice, peace and security also facilitate dialogue and shared vision in the face of the distortion of religious values and principles in the Region, among others.

  Guest of Honour hon. Harelimana hands over to the EAC deputy secretary general a copy of the signed Kigali declaration
  Deputy Secretary General and the guest of honour share a point at the closure of the conference.
  Representatives of the religious leaders and the Deputy Secretary General display the signed Kigali declaration to the delegates as the guest of honour witnesses
  Guest of honour, Deputy Secretary General, heads of religious communities and Miriam of GIZ in a group photo after the conclusion of the conference.

  READ MORE HERE

  0 0

  Mhe. Dr. Titus Mlengeya Kamani (Mb), Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb), Waziri wa Sayansi na Teknolojia na Katibu Mkuu, Wizara ya Sayansi na Teknolojia Prof. Patrick Makungu wakifuatilia kikao cha 58 cha Shirika la nguvu za atomiki Duniani (58th General Conference of the International Atomic Energy Agency) unaofanyika Vienna nchini Austria kuanzia tarehe 22-26 Septemba, 2014.
  Kutoka kushoto Prof. Patrick Makungu, Katibu Mkuu, Wizara ya Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb), Waziri wa Sayansi na Teknolojia ,Mhe. Dr. Titus Mlengeya Kamani (Mb), Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, na Mhe. Modest Mero, Balozi wa kudumu Umoja wa Mataifa, Geneva ambaye pia anaiwakilisha Tanzania IAEA (International Atomic Energy Agency) wakiwa katika picha ya pamoja katika banda la Tanzania kwenye maonesho yanayoenda sambamba na kikao cha 58 cha Shirika la nguvu za atomiki Duniani (58th General Conference of the International Atomic Energy Agency) unaofanyika Vienna nchini Austria kuanzia tarehe 22-26 Septemba, 2014.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal leo amekutana na mabalozi wa Norway na Balozi mteule wa Tanzania nchini Rwanda na kufanya nao mazungumzo ofisini kwake ikulu jijini Dar es Salaam.

  Balozi wa Norway nchini Tanzania mheshimiwa Hanne Marie Kaarstad ndiye alikuwa wa kwanza kufanya mazungumzo na mheshimiwa Makamu wa Rais ambapo licha ya kufika kujitambulisha alimueleza mheshimiwa Makamu wa Rais kuwa atajitahidi kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizi mbili katika kipindi chake kama Balozi na kwamba Tanzania ni nchi rafiki kwa Norway na akasisitiza kuzidi kuimarisha uhusiano hasa katika masuala ya utunzaji wa mazingira.

  Kwa upande wake mheshimiwa Makamu wa Rais alimuelezea Balozi Hanne kuwa, Tanzania inajivunia uhusiano wake na Norway na kwamba uhusiano huo kwa sasa unazidi kuimarika na tena Tanzania inategemea kujifunza mengi toka Norway kutokana na nchi hiyo kuwa miongoni mwa nchi zenye teknolojia ya juu katika masuala ya gesi na mafuta.

  Balozi Hanne ambaye aliwahi kufanya kazi nchini Tanzania pia alionesha kufurahishwa kwake na maendeleo ambayo Tanzania inapiga na akafafanua kuwa mji wa Dar es Salaam ni kiashiria kimojawapo kinachoonesha wazi kuwa Tanzania inakuwa kwa kasi.

  Pia, Mheshimiwa Makamu wa Rais alimpokea Balozi Ali Said Siwa aliyepangiwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda na akamtaka Balozi huyo kuhakikisha anasaidia mahusiano baina ya nchi zetui kuzidi kuimarika huku akimsisitizia kuhusu uhusiano wetu kama majirani na pia wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Balozi Siwa alitumia nafasi hiyo kumshukuru Mheshimiwa Makamu wa Rais kwa uteuzi wake na akaahidi kuiwakilisha vema Tanzania nchini Rwanda.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne Marie Kaarstad, wakati alipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 22, 2014 kwa mazungumzo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne Marie Kaarstad, (wa pili kulia) na ujumbe wake baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 22, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi wa Tanzania, nchini Rwanda, Mhe. Ali Said Siwa, wakati alipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 22, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Tanzania, nchini Rwanda, Mhe. Ali Said Siwa, leo Septemba 22, 2014. Picha na OMR.

  0 0

  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Concilia Niyibitanga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo jijini Dar es Salaam.Kuliani Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana Dkt. Steven Kissui na kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari MAELEZO Bw. Frank Mvungi.
  Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana Dkt. Steven Kissui akionyesha Kitabu cha Sera ya Maendeleo ya Vijana kwa waandishi wa habari wakati alipokuwa akito ufafanuzi kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana (YDF) leo jijini Dar es Salaam. Kuliani ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Concilia Niyibitanga.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa kuhusu Mfuko wa Vijana wakati wa mkutano wa msemaji wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na waandishi hoa uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO leo jijini Dar es Salaam. Picha na Frank Shija

  0 0

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama (lushoto), akimkabidhi sehemu ya msaada wa vyakula Katibu Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Maunga Center cha Kinondoni jijini Dar es Salaam, Rashid Mpinda.  Msaada huo wenye thamani ya sh. milioni 7 unatokana na mapato yaliyopatikana katika  tamasha la Pasaka na Krismasi. (Picha na Francis Dande) 
   Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions Ltd, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kukabidhi misaada kwa vituo vya yatima jijini Dar es Salaam.
  Watoto wa kituo cha Mwandaliwa cha Mbweni wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kituo hicho, Halima Ramadhan wa tatu kulia.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Washiriki wa maonesho, wananchi mbalimbali wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani iliyozinduliwa katika Kiwanja cha Mpira wa Amri Abeid jijini Arusha leo. Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mrongo aliyazindua maonesho hayo huku akiwataka madereva nchini wawe makini kwa kufuatia sheria za barabarani ili kuepuka ajali. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Maamuzi yako Barabarani Hatma Yetu-Fikiri Kwanza”.
  Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mrongo akitoa hotuba ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani alioizindua Kitaifa jijini Arusha leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Maamuzi yako Barabarani Hatma Yetu-Fikiri Kwanza”. Katika hotuba yake, Mrongo aliwataka viongozi wa usalama barabarani kuhakikisha kuwa adhabu dhidi ya madereva wazembe nchini inaongezeka ili wawe na woga wa kufanya makosa barabarani.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (kushoto) akimpa zawadi ya ngao Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mrongo baada ya mgeni rasmi huyo kuyafungua Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambapo kwa mwaka huu maadhimisho hayo kitaifa yanafanya jijini Arusha. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Maamuzi yako Barabarani Hatma Yetu-Fikiri Kwanza”.
  Waendesha pikipiki (bodaboda) pia walishiriki kikamilifu katika uzinduzi wa maonesho hayo yaliyofanyika katika Kiwanja cha Mpira cha Amri Abeid, jijini Arusha leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Maamuzi yako Barabarani Hatma Yetu-Fikiri Kwanza”.
  Trafiki Makao Makuu jijini Dar es salaam, Mkaguzi Msaidizi, Yohana Mjema (kulia), akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mrongo (watatu kushoto), namna ajali barabarani zinavyoweza kuepukika endapo watumiaji barabara watakuwa waangalifu kwa kufuata sheria za barabarani. Mkuu wa Mkoa aliyazindua maonesho hayo ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani katika Kiwanja cha Mpira Amri Abeid jijini Arusha leo. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima, na kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mohamedi Mpinga.
  Sajenti wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Damian Muheya (kulia) akiwaelimisha wananchi wa jijini Arusha jinsi mtungi mdogo wa kuzimia moto unavyotumika wakati moto unapotokea. Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani imezindulia leo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha (Magesa Mrongo katika Kiwanja cha Mpira cha Amri Abeid jijini humo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Maamuzi yako Barabarani Hatma Yetu-Fikiri Kwanza”.
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mrongo (katikati waliokaa), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (wanne kutoka kushoto-waliokaa) wakiwa na wajumbe wa usalama barabarani katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo Kitaifa mwaka huu yanafanyika jiijini Arusha leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Maamuzi yako Barabarani Hatma Yetu-Fikiri Kwanza”. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0
 • 09/22/14--07:08: IN LOVING MEMORY


 • 0 0

  Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Prof. Makame Mbarawa ameongoza zoezi la utiaji Saini Mkataba wa Utendaji baina yake na Wenyeviti wa Bodi za Taasisi zilizo chini ya Wizara kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya Taasisi zao kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015.

  Lengo la Mhe. Waziri kuwekeana saini Mkataba wa Utendaji na Wenyeviti wa Bodi ni kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa majukumu ya Wenyeviti wa Bodi hizo ili kuleta ufanisi na tija kwenye Sekta ya TEHAMA, Sayansi na Teknolojia ili iweze kuendelea kuchangia ukuaji wa uchumi na mchango wa sekta kwenye pato la Taifa.

  Aidha, Mhe. Mbarawa alisema kuwa mapitio ya utekelezaji wa mkataba huo utafanyika kila baada ya miezi mitatu ili kufuatilia namna unavyotekelezwa na kubaini changamoto zinazowakabili wenyeviti wa Bodi za Taasisi zilizo chini ya Wizara kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha wa 2014/2015.

  Taasisi zilizo chini ya Wizara ni pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, Kampuni ya Simu Tanzania, Shirika la Posta Tanzania, Taasisi ya Sayansi na Teknolojia, Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya, Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Tume ya Nguvu za Atomii Tanzania na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote.

  Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Prof. Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa Utiaji Saini Mkataba wa Utendaji baina yake na Wenyeviti wa Bodi za Taasisi zilizo chini ya Wizara kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya Taasisi zao kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015.

  Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote,Prof. John Nkoma akiweka saini mkataba wa utendaji baina yake na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Mhe. Prof. Makame Mbarawa kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya Taasisi kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015
  Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Mhe. Prof. Makame Mbarawa akipeana mkono na Prof. Nkoma baada ya kuwekeana saini mkataba.


  0 0

  The newly expected couple sitting together with their Patron Ansigar Mtandika and Matron Neema Njau.
  The newly expected couple Richard Miller and Kara Lee from America poses in a picture at Shira Cave point shortly before descending to a place where they exchanged vows in Mount Kilimanjaro yesterday.
  Chief Park Warden for Kilimanjaro National Park Erastus Lufungulo (right) and TANAPA’s Corporate Communications Manager Pascal Shelutete (second left) poses in a picture with the newly expected couple at Shira Cave point shortly before they exchanged vows in Mount Kilimanjaro.


  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw.Magessa mulongo, akimkabidhi ngao Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Georgia Mutagahywa kwa kutambua mchango na jitihada za Vodacom kuhakikisha usalama barabarani,ngao hiyo ilikabidhiwa wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani yamefanyika kitaifa mkoani Arusha,kampuni ya Vodacom ni moja wa wadhamini wakubwa wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mwaka huu
  Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Georgia Mutagahywa akiwa na maofisa wa jeshi la polisi wakisilikiza hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Bw.Magessa mlongo,wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani ambayo imefanyika kitaifa mkoani Arusha,ambapo Vodacom Tanzania wamepewa tunzo ya kutambulika kwao katika kutoa mchango na jitihada za kuhakikisha usalama barabarani,Tuzo hiyo wamekabidhiwa katika siku ya ufunguzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mwaka huu.
  Baadhi ya wananchi waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani wakimuangalia mtaalamu wa masuala ya uokoaji Bw. Nelson Gachiru,aliyekuwa kwenye moja ya banda la maonyesho katika uwanja waSheikh Amri mjini Arusha,Vodacom Tanzania ni moja ya wadhamini wakuu wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mwaka huu na kuweza kujinyakulia ngao ya kutambulika kwa mchango wake na jitihada za kuhakikisha usalama barabarani.

  0 0

  Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh. Omar Othman Makungu,akifungua mafunzo ya Majaji na Mahakimu wa Afrika ya Mashariki kuhusiana na mkakati wa kupiga vita masuala ya Ugaidi uhalifu wa Kimataifa ambayo yanahatarisha usalama wa wananchi wake pamoja na wageni,semina hiyo inafanyika Lagema Nungwi.
  Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh. Omar Othman Makungu (katikati),akifuatana na Jaji Mkuu wa Sudan ya Kusini Chaan Reec Madut (kushoto),mara baada ya kuyafungua mafunzo ya siku tano juu ya mikakati ya kuupiga vita ugaidi na uhalifu wa Kimataifa kwa nchi za Afrika ya Mashariki,mkutano huo unafanyika katika hoteli ya kitalii ya Lagema Nungwi,(Picha na Abdallah Masangu).

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa nnne kulia) akiwepo na Rais Mstaafu wa Zanzibar DK.Amani Abeid Karume wakijumuika na waisalmu katika kumswalia Marehemu aliyekua Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Iddi Pandu Hassan katika Msikiti wa Mchekeni Magomeni Mjini Zanzibar leo na Kuzikwa kijijini kwao Makunduchi.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ALhaj Dk. Mohamed Gharib Bilali waliungana na wananchi mbali mbali katika maziko ya aliyekua Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Iddi Pandu Hassan aliyezikwa kijijini kwao Kipunguni Makunduchi jana.
  Marehemu Iddi Pandu Hassan aliyekua Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein alipofika nyumbani kwa Marehemu Iddi Pandu Hassan aliyekua Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwapa pole wafiwa leo kabla ya kufanyika mazishi huko kijijini kwao Makunduchi.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Ndugu wa Marehemu Iddi Pandu Hassan aliyekua Mwanasheria Mkuu wa Serikali alipofika kuwapa pole wafiwa nyumbani kwa marehemu Magomeni Mjini Zanzibar leo kabla ya kufanyika mazishi huko kijijini kwao Makunduchi.
  Baadhi ya akina mama walioshiriki katika mazishi ya aliyekua Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Marehemu Iddi Pandu Hassannyumbani kwake Magomeni Mjini Unguja jana.{Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba akiwaeleza waandishi wa Mikakati inayowekwa na shirika hilo ikiwemo kutekeleza miradi mbalimbali ya kuzalisha, kusafirisha na kusambaza Umeme ili kuhakikisha wanakabiliana na Tatizo la Umeme Nchini,wakati wa Ziara kwenye Mradi wa “Tanzania Energy Development and Access Program (TEDAP)” unaotekelezwa katika maeneo ya Mbagala, Gongo la Mboto na Kinyerezi, Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akiwaeleza waandishi wa habari kufurahishwa kwake na ziara hii iliyoratibiwa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo kwa kushirikiana na Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) yenye lengo la kuona nini Shirika hilo linatekeleza katika jitihada za kukabiliana na Tatizo la Umeme Nchini.Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba.
  Baadhi ya mafundi wakiedelea na kazi ya kusuka Transfoma iliyopo katika eneo la Mradi Mbagala lenye MVA (MEGAVOLT-AMPERE) 50.


  0 0

  Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA) Imeanza rasmi zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu Mkoa wa Morogoro pamoja na uchukuaji alama za vidole, picha na saini ya kielektroniki kwa wananchi wa Wilaya ya Kilombero ambao zoezi la Ujazaji fomu za maombi ya vitambulisho lilishafanyika. Kuanza kwa usajili na Utambuzi wa Watu mkoa wa Morogoro kumefuatia kukamilika kwa zoezi kama hili mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara ambapo sambamba na usajili unaoendelea sasa mkoani Morogoro zoezi la uchukuaji alama za vidole picha na saini ya kielektroniki limekuwa likiendelea katika baadhi ya Wilaya za mkoa wa Pwani.

  Mkoani Morogoro; katika eneo la Mikese kijiji cha Fulwe tumeshuhudia msururu wa watu wakisubiri kusajiliwa huku wengine wakiwa katika harakati za kuingizwa katika Rejesta ya Makazi inayomilikiwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na Vijiji. Kwa utaratibu wa sasa ili uweze kusajiliwa lazima kwanza kuwa unatambulika katika serikali yako ya Mtaa/Kijiji na kuwa umeorodheshwa katika Rejesta ya Makazi ya Mtaa au Kijiji husika.
  Leo ikiwa ni siku ya kwanza ya kuanza kwa zoezi hilo litakalodumu kwa siku saba mpaka Jumapili ya tarehe 29/09/2014 wananchi wengi wameonekana kuhamasika na kujitokeza kwa wingi katika siku ya kwanza tofauti na mazoea ya wengi kujitokeza siku za mwisho za zoezi.

  Changamoto kubwa bado imebaki wananchi wengi kukosa Viambata msingi vya kuwatambulisha kama vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya elimu ya msingi au sekondari n.k jambo ambalo limekuwa likisisitiziwa sana na NIDA katika kurahisisha utambulisho wa mwombaji. (Picha na Rose Mdami- NIDA)


  0 0

  Mradi wa nyumba unaosimamiwa na kampuni ya Hifadhi inayoitwa Dege Eco-Village umeshiriki maonyesho ya nyumba yaliyoanza kufanyika jijini Dar es Salaam jana.

  Wakati Meneja Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege eco-Village akiongea alisema “Kwa sasa ujenzi unaendelea na karibu aina ya nyumba (apartment) 3000 zitakuwa tayari ifikapo Januari 2015. Aliongezea kusema kwamba kupitia mradi huu waTanzania watanufaika kwa kupata ajira na pia kuwa na huduma kama hospitali, shule na maduka katika eneo la Kigamboni.

  Mradi huo unajengwa kwenye eneo takriban heka 300 na kampuni hiyo imewekeza zaidi ya dola milioni 350. Kwa ujumla nyumba aina ya villa ziko 300 na apartment ziko 7400. Mradi huu utakamilika mwaka 2018. Apartment zitakamilika mwaka 2017 na villa mwaka 2018.

  Ndani ya mji huu wa Dege Eco-Village wakazi hawatahitaji kwenda popote kwasababu kila kitu kitakuwepo kama shule za watoto, kituo cha polisi, hospitali, supermarket, na kadhalika.
  Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo,Bw. Azhar Malik akiefafanua juu ya mradi huo wa Dege Eco Village kwa wateja wapitao katika banda lao (hawapo pichani).
   Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo,Bw Azhar Malik akihojiwa na wahandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika maonyesho ya nyumba.
  Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo,Bw Azhar Malik (katikati)  akiongea na mteja kuhusu mradi huo wa Dege Eco-Village na kulia kwake na Mkurugenzi msaidizi wa Masoko na Mauzo Bw. Adam Jusab.
  Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo,Bw Azhar Malik  akiwa na wateja ambao wametembelea banda hilo na kuwaonyesha vifurushi ya mradi huo.

  0 0

  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa na Dkt. Peter Feiler, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kiuchumi katika Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani wakati alipowasili kwenye Ofisi ya Ubalozi wa Ujerumani kwenye Umoja wa Mataifa huko New York alipokwenda kuhudhuria mkutano uliozungumzia masuala ya elimu: kuwawezesha vijana kufanya maamuzi sahihi ya kiafya tarehe 22.9.2014.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano wa masuala ya elimu kwa vijana wa bara la Afrika ili waweze kufanya maamuzi sahihi ya kiafya. Mkutano huo umeandaliwa na serikali ya Ujerumani na ulifanyika huko New York tarehe 22.9.2014.
  Baadhi ya washiriki kwenye mkutano uliojadili masuala ya elimu kwa vijana wa Afrika ili wafanye maamuzi sahihi ya kiafya wakisikiliza hotuba ya Mama Salma Kikwete.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani Mheshimiwa Gerd Mueller (kulia) na Mke wa Rais wa Malawi Mheshimiwa Getrude Mutharika wakati wa ufunguzi wa mkutano ulioandaliwa na serikali ya Ujerumani kuzungumzia masuala ya elimu ili kuwawezesha vijana barani Afrika kufanya maamuzi sahihi ya kiafya.


older | 1 | .... | 580 | 581 | (Page 582) | 583 | 584 | .... | 3272 | newer