Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 578 | 579 | (Page 580) | 581 | 582 | .... | 3282 | newer

  0 0

  Na Dotto Mwaibale

  SERIKALI imesema itaainisha ukomo wa tozo kwa kila huduma inayotolewa kwa kila ngazi ya kituo cha huduma ili kudhibiti gharama za huduma za afya nchini.

  Kauli hiyo ilitolewa  na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid Dar es Salaam leo asubuhi wakati akizindua bodi mpya ya ushauri ya Hospitali binafsi nchini.

  Dk. Rashid alisema hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa malalamiko kuhusu huduma zinazotolewa na hospitali hizo hivyo hatua hiyo itasaidia kuboresha mfumo na kuwatendea haki wananchi wanaotumia vituo  vya kutolea huduma za afya.

  "Malalamiko haya ni pamoja na huduma zisizo na ubora unaotakiwa na gharama zinazotolewa kwa huduma hizo .Sheria iliyopo inatutaka kudhibiti bei ya huduma hizi kwa kuzingatia malalamiko haya pamoja na matakwa ya sheria yenyewe," alisema Dk. Rashid.

  Hata hivyo alibainisha kuwa licha ya kuwepo wa changamoto hizo huduma zinazotolewa na hospitali za watu binafsi zimechangia katika mafanikio  yaliyopatikana katika kufikia malengo ya maendeleo ya milenia.

  Kuhusu bodi hiyo Dk .Rashid aliwataka wajumbe wapya wa bodi hiyo kufanya vikao vya mara kwa mara vinavyolenga uboreshwaji wa utoaji wa huduma.Na kuwataka kuendeleza utaratibu wa kusajili vituo vipya na kufupisha usajili kwa kutmia muda mfupi  kwa kutumia mfumo wa kielektroniki.

  Alibainisha kuwa wajumbe wa bodi ya awali iliyosimamiwa na Mwenyekiti Dk. Deo Mtasiwa imesaidia kuboresha uwajibikaji wa wahusika hivyo kuboresha huduma na imeokoa maisha ya wananchi wengi ambayo yangekuwa hatarini endapo bodi isingetekeleza majukumu yake ipasavyo.

  Alitaja wajumbe wa bodi mpya kuwa ni Dk.Donan Mbando ambaye ni Mwenyekiti, Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa mbeya Dk. Mpoki Ulisubisya, Mkurugenzi wa Hospitali ya Bugando Profesa Chalres Majinge, Mkurugenzi wa Tiba na Masuala ya Kiufundi (NHIF), DK. Frank Lekey.


  Wajumbe wengine ni Mkurugenzi Msaidizi- Hospitali za Umma na Binafsi Idara ya Tiba Dk. Sijenunu Aaron, Mkurugenzi wa Association of Private Health Facilities (APHTA), Mwakilishi wa Mkurugenzi, Christian Social Services Comission (CSSC), Dk.Jane Kahabi na Mwanasheria Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Onorious Njole.
   Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid, akizungumza na wajumbe wa bodi hiyo iliyomaliza muda wake na mpya wakati akizindua bodi hiyo Dar es Salaam leo asubuhi.
   Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid (kulia),akimkabidhi cheti cha utumishi wa bodi hiyo,Profesa Bakari Lembariti. Katikati ni Mganga Mkuu wa Serikali, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dk.Donan Mmbando. Vyeti hiyo walitunukiwa wajumbe wote waliomaliza muda wao.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUba), Michael Kadinde (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam, kuhusu Tamasha la 33 la taasisi hiyo litakalofanyika kuanzia Septemba 22 hadi 28 mwaka huu. Kulia ni Mwenyekiti wa Tamasha hilo, Abraham Fadhil na Mkuu wa Mafunzo, Gabriel Kiiza.
  Dotto Mwaibale

  TAASISI ya sanaa na utamaduni Bagamoyo (TaSUba) imeanadaa tamasha la 33  lenye lengo la kukuza mila na desturi za watanzania.

  Katika tamasha hilo kauli mbiu itakuwa sanaa na utamaduni katika kukuza utalii na mgeni rasmi ni Mbunge wa Afrika Mashariki Makongoro Nyerere ambaye atamwakilisha Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, Spika wa Bunge hilo Margareth Zziwa .

  Akizungumza  Dar es Salaam, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUba), Michael Kadinde alisema tamasha hilo pia lina lengo la kuonyesha sanaa zilizoandaliwa kiutalaam na wanafunzi wa Tasuba.

  "Katika tamasha hili pia tuaihamasisha jamii ije ione tofauti ya sanaa iliondaliwa kitaalamu na isiyo kitaalamu kuweka ushindani kati kati ya taasisi yetu na vikundi vingine,"alisema.

  Kadinde alisema katika taasisi yao wanafundisha maigizo,ngoma muziki ufundi wa majukwaa,sanaaza ufundina filamu za televisheni.

  "Vikundi ambvyo vitashiriki katika tamasha hilo vya ndani ni 143 na vikundi vya nje vitakuwa vitano Kenya watakuwa na fani ya ngoma,Newzealand watakuwa na muziki, Norway, watakuwa na muziki,Newzealand muziki,Ujerumani maigizo na ,na Korea Kusini watakuwa na muziki,"alisema.

  0 0

  Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu wa Maafa yatoa Mafunzo ya Dhana ya Maafa kwa wataalamu kutoka Halmashauri na Manispaa ya Mkoa wa Mtwara kwa ajili ya kuandaa Mpango wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa. Miongoni mwa masuala yanaoelezwa ni pamoja na, jinsi ya Kujiandaa na Maafa, Kukabili, Kuzuia na namna ya kurudisha hali baada ya Maafa kutokea.


  0 0

   President Kikwete deliveres a keynote speech at  the USAID Frontiers in Development Forum: Ending Extreme Poverty at the Reagen Building in Washington  DC.
    President Kikwete deliveres a keynote speech at  the USAID Frontiers in Development Forum: Ending Extreme Poverty at the Reagen Building in Washington  DC
    President Kikwete in a souvenir photo with the US Secretary of State Mr John Kerry  and the USAID Administrator Dr Rajiv Shah  before the start of  the USAID Frontiers in Development Forum: Ending Extreme overty at the Reagan Building in Washington  DC.
  STATE HOUSE PHOTOS.


  CLICK HERE FOR MORE PHOTOS

  0 0

  Hivi karibuni kumekuwa na tuhuma mbalimbali ambazo zimekuwa zikiripotiwa na baadhi ya Vyombo vya Habari na Mitandao ya Kijamii kuhusiana na kunyanyaswa, kutendewa vitendo visivyo vya kiungwana na kuteswa gerezani kwa Watuhumiwa wa Makosa ya Ugaidi kinyume na taratibu za Uendeshaji wa Magereza.

  Kufuatia tuhuma hizo, Jeshi la Magereza Tanzania Bara limefanya uchunguzi kwa kufanya mazungumzo na Watuhumiwa wenyewe na wamekanusha tuhuma hizo dhidi ya Jeshi la Magereza. Ukweli ni kuwa taarifa hizo si za kweli na hatuelewi kusudio lao ni nini.

  Jeshi la Magereza Tanzania Bara linatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa kuhusiana na Utunzaji wa Wahalifu na haki zao kwa kuzingatia misingi ya Haki za Binadamu. Vitendo vya kunyanyasa au kudhalilisha Wafungwa vinakemewa vikali magerezani na si Sera ya Jeshi la Magereza au Serikali.

  Napenda kuufahamisha umma kuwa Mahabusu hao wanaotuhumiwa kwa Makosa ya Ugaidi wapo salama, wana Afya nzuri na hawana tatizo lolote gerezani.


  Imetolewa na;

  John Casmir Minja,
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza,
  20 Septemba, 2014.

  0 0

   Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Pwani Pauline Mrango akisoma Hotuba ya makabidhiano ya mashine 28 za kufyatulia matofali kwa vikundi vya vijana katika halmashauri zote za mkoa wa Pwani.
  Shirika la Nyumba la Taifa limetoa mashine hizo zenye gharama ya zaidi ya shilingi milioni 12 pamoja na mafunzo kwa vijana ya wiki mbili ambapo baada ya kumaliza mafunzo Shirika litatoa msaada wa shilingi laki tano kwa kila kikundi kama mtaji .
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpa mkono wa pongezi Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa pwani Pauline Mrango kwa kutoa mashine 28 za kuwasaidia vijana.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria makabidhiano ya mashine za kufyatulia matofali zilizotolewa na shirika la nyumba la Taifa kwenda kwenye halmashauri zote za mkoa wa Pwani.
  Mashine 28 zitawasaidia vijana mkoa wa Pwani kuondokana na tatizo la ajira, pili litasaidia sana katika utunzaji wa mazingira,zitasaidia wananchi kujenga nyumba za kisasa na kwa bei nafuu.(Adam Mzee)

  0 0

  Rais Jakaya Kikwete akiwa na mtoto wa miaka minane aliejitambulisha kwa jina la Brian ambaye alitoa burudani ya kupiga kinanda wakati wa wimbo wa Taifa na nyimbo nyinginezo katika hafla ya USIKU WA JAKAYA uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya JW Mariott jijini Washington
  Rais Jakaya Kikwete akiongea na Dkt Seche Malecela baada ya kupokea risala ya pongezi kwa uongozi wake nchini Tanzania  katika hafla ya USIKU WA JAKAYA uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya JW Mariott jijini Washington
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipokea makombe toka kwa Balozi wa Heshima wa Tanzania huko California Mhe Ahmed Issa kama pongezi kwa uongozi uliotukuka Rais Jakaya Kikwete akiwa na mtoto wa miaka minane Brian ambaye alitoa burudani ya kupiga kinanda wakati wa wimbo wa Taifa na nyimbo nyinginezo katika hafla ya USIKU WA JAKAYA uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya JW Mariott jijini Washington
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipokea zawadi toka Watanzania kutoka Atlanta  kama pongezi kwa uongozi uliotukuka Rais Jakaya Kikwete akiwa na mtoto wa miaka minane Brian ambaye alitoa burudani ya kupiga kinanda wakati wa wimbo wa Taifa na nyimbo nyinginezo katika hafla ya USIKU WA JAKAYA uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya JW Mariott jijini Washington.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika hafla ya USIKU WA JAKAYA uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya JW Mariott jijini Washington.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Wasanii wa muziki wa Bongofleva Ommy Dimpo na Vanessa Mdee a.k.a Vmoney wakilishambulia jukwaa kwa pamoja mbele ya umati wa mashabiki wa tamasha la Fiesta 2014  lililofanyika jana ndani ya uwanja wa Samora mkoani Iringa,huku miluzi na shangwe zikisikika kila kona ya uwanja.Tamasha la Fiesta linatarajiwa kufanyika kesho mjini Morogoro katika uwanja wa Jamuhuri ambapo wasanii mbalimbali wa bongofleva watatumbuiza.
  Baadhi ya Mashabiki wakishangqweka.
   Msanii Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongofleva,Selemani Msindi a.k.a Afande Sele Mfalme wa Rhymes,akiimba kwa hisia kubwa juu ya jukwaa la tamasha la Fiesta 2014 lililofanyika jana ndani ya uwanja wa Samora mkoani Iringa.
  Msanii wa muziki wa kizazi kipya Linah Sanga akionesha mumahiri wake kucheza jukwaani akiwa sambamba na mmoja wa madansa wake mahiri katika tamasha la burudani la fiesta lililofanyika jana ndani ya uwanja wa samora mkoani Iringa.
  Sehemu ya umati wa watu waliojitokeza kwenye tamasha hilo la Fiesta 2014 ndani ya Samora mjini Iringa hapo jana.
  Anajiita Rais wa Manzese,jina lake la kisanii anajiita Madee kutoka kundi la TIP TOP CONECTIONs,akiimba mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Iringa waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja wa Samora hapo jana.Tamasha la Fiesta kesho linatarajiwa kufanyika ndani ya uwanja wa jamuhuri mkoani Morogoro.
  Wakazi wa mji wa Iringa waliojitokeza ndani ya tamasha la Fiesta wakishangweka kwa raha zao.PICHA NA MICHUZI JR-IRINGA.  0 0

  Mjumbe wa Kamati ya CCM Taifa Bi. Khadija Hassan Aboud akimkaribisha Mbunge ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha FRELIMO cha Msumbiji Bi. Nyeleti Mondlane Ofisi kuu ya CCM Zanzibar.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha FRELIMO cha Msumbiji Bi. Nyeleti Mondlane akisaini kitabu cha wageni alipofika Ofisi kuu ya CCM Zanzibar (kulia) Katibu wa FRELIMO Zanzibar Bw. Agostino Andrea.
  Kiongozi wa Ujumbe wa Chama cha FRELIMO Bi. Nyeleti Mondlane (watatu kushoto) akibadilishana mawazo na wenyeji wake wajumbe wa Chama cha Mapinduzi katika Ofisi Kuu Kisiwandui Zanzibar ikiwa ni mkakati wa kuimarisha Uhusiano wa Vyama vyao na kuzindua Kampeni ya Uchaguzi Mkuu Nchini Msumbiji.
  Picha ya pamoja ya Ujumbe wa Chama cha FRELIMO na baadhi ya wajumbe wa Chama cha Mapinduzi CCM wakiongozwa na Mjumbe wa Kamati ya CCM Taifa Bi. Khadija Hassan Aboud wakatikati. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini Marekani,Mh. Liberata Mulamula na Afisa Mwandamizi wa Mambo ya Nje,Hassan Mwemeta pamoja na wadau wengine wakiwa katika picha ya pamoja na Mwanamama Oprah Winfrey kwenye hoteli ya Fairmount,nchini Marekani leo.

  0 0


  0 0

  Washiriki wa Shindano la Redds Miss Tanzania 2014 walitoa misaada ya kijamii katika Hospitali za Misheni Kilema na ile ya K.K.K.T Marangu baada ya kutembelea Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.
   Warembo waiangalia watoto.
   picha ya pamoja ya warembo na wenyeji Hospitali ya Kilema Moshi.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Na Thomas William,Morogoro.
  Usajili na Utambuzi wa watu katika mkoa wa Morogoro umezinduliwa rasmi Septemba 20, 2014 na Mkuu wa Mkoa wa huo, Joel Bendera katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Morogoro.

  Akizindua zoezi hilo aliwasisitiza wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa mamlaka za Serikali za Mitaa, makatibu tawala wilaya na viongozi wote kufikia ngazi ya kijiji na mtaa kuhakikisha kwamba wanashiriki kikamilifu katika kufanikisha usajili wa watu katika mkoa wake.

  Alisema viongozi na watendaji wote katika mkoa huo wanatakiwa kuweka uzalendo mbele katika suala hilo na kuhakikisha kwamba hakuna wageni wanaopata vitambulisho vya taifa ambayo ni vya raia.

  Zoezi hili ambalo linawahusu wananchi na wakazi wa wilaya zote za Morogoro ambazo ni Morogoro Mjini, Morogoro Vijijini, Mvomero, Kilosa, Kilombero, Gairo, na Ulanga wenye umri wa miaka 18 na zaidi linafanyika kwa siku saba.

  Ili kusajiliwa mwombaji anatakiwa kufika katika kituo cha usajili ukiwa na nyaraka muhimu zinakazokutambulisha mathalan, cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi, Cheti cha Elimu ya Msingi, Sekondari au Chuo, Leseni ya Udereva, Kadi ya kupigia Kura, Pasipoti na Kadi ya Bima ya Afya. Wageni wanatakiwa kuwa nakala ya Pasipoti ya nchi wanazotoka na kibali cha kuishi nchini.

  Aidha, mwombaji anakumbushwa kuhakikisha jina lake limesajiliwa katika rejesta ya makazi iliyopo katika Serikali ya Mtaa/Kijiji kabla ya kuanza taratibu za usajili. Vituo vitafunguliwa asubuhi saa 2:00 hadi saa 11:00 jioni.

  0 0

  Wafanyabiashara wa Namanga na Wilaya ya Longido wameiomba Serikali iwajengee Soko kubwa Namanga ili waepukane na usumbufu wanaoupata wanapokwenda Kenya kuuza mifugo, mazao na bidhaa nyingine.

  Wafanyabiashara hao walitoa ombi lao jana Septemba 19 wakati wa mkutano na Maofisa wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki wanaotembelea mipaka mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu ya Mtangamano wa Afrika Mashariki.

  Baadhi ya manyanyaso wanayopata wanadai ni kuombwa kitu kidogo, kupewa malipo kidogo ya bidhaa zao kuliko bei ya soko na kusumbuliwa kuhusu ubora wa bidhaa wakati bidhaa zao zimetimiza viwango vyote.

  Uongozi wa Wilaya ya Longido umetenga eneo la heka 120 kwa ajili ya soko ili wafugaji na wakulimna wauzie bidhaa zao hapo.

  Hiyo pia itasaidia Wanunuzi kutoka Kenya waje kununua sokoni hapo na hivyo wakulima na wafanyabishara wa Tanzania kupata bei nzuri na kuepuka usumbufu wanaoupata sasa. 

  Wafanyabishara hao pia wamesema ujenzi wa soko utasaidia kuzuia Wakenya kwenda mashambani na kununua mazao moja kwa moja kwa wakulima.

  Akizungumza na wafanyabiashara hao Mkurugenzi Msaidizi wa Masuala ya Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Graceana Shirima alisema Serikali itashugulikia haraka malalamiko yao ikiwa pamoja kuharakisha ujenzi wa masoko mipakani.

  Shirima, ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu Joyce Mapunjo, alishauri uongozi wa Wilaya ya Longido kuanza na utaratibu wa gulio wakati wakiendelea na mikakati ya ujenzi wa soko.

  Mweka Hazina wa Wilaya Issai Mbiru alisema tayari Wilaya imepata fedha Shilingi bilioni 2.3 kutoka kwa wafandhili na ujenzi wa soko hilo utaanza muda si mrefu.
  Mkurugenzi Msaidizi wa Masuala ya Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara Bi. Graceana Shirima (kulia) akimkabidhi machapisho mbalimbali Katibu Tawala wa Wilaya ya Longido Bw. Dunford Peter wakati wa ziara ya kuonana na wafanyabiashara wa Namanga tar. 19-9-2014
  Malori yakisubiri kukamilisha taratibu za kuvuka Mpaka wa Namanga kuingia Tanzania kwa kutumia utaratibu wa zamani. Ujenzi wa OSBP utarahisisha Malori na wasafiri kupita.


  0 0

  Yvonne Chaka Chaka - Thank You Mr DJ

  0 0

  Kituo cha radio kinachokuja kwa kasi jijini Dar es Salaam leo usiku huu kimefanya uzinduzi mkubwa wa radio hiyo mjini Bagamoyo. Pichani Mtangazaji wa michezo wa radio hiyo Maulid Kitenge akiwa na baadhi ya wasikilizaji mara baada ya kuwasili mjini Bagamoyo tayari kwa uzinduzi usiku wa kuamkia leo. Mkude Simba ndani....

  0 0
 • 09/20/14--23:06: iga ufe!


 • 0 0
 • 09/20/14--23:10: ORIJINO KOMEDI NEW SESSION


 • 0 0

   Washiriki wa Shindano la Redd's Miss Tanzania 2014, wakimsikiliza Afisa Mfawidhi, Nisalile Mwangoka aliyekuwa akiwapa maelezo juu ya upimaji wa wageni wanao ingia nchini kupitia viwanja vya ndege unavyofanyika kutumia mashine maalum iitwayo 'Walk Through Thermoscaner', iliyopo uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wakati warembo 30 wanaowania taji la Miss Tanzania walipotembelea uwanja huo na kujifunza mambo mbalimbali . Warembo hao wapo katika ziara ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini.
   Mashine hiyo ikionekana kufungwa juu kuelekea usawa wa kuingilia abiria wanaowasili tka nje ya nchi.
   Namna inavyoonekana baada ya kipimo kuchukuliwa
   Nisalile Mwangoka akionesha kifaa cha zamani cha upimaji ugonjwa wa Ebola ambacho kimeelezwa kuwa licha ya ufanisi lakini kilikuwa kinaweka foleni kwa abiria tofauti na hicho kipya.
   Meneja wa Usalama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Kisusi Makomondi akiwapa maelezo washiriki hao wa shindano la Miss Tanzaniua 2014 juu ya shughuli mbalimbali za uwanja huo. 

  0 0
 • 09/21/14--00:15: Yale yale.....
 • Jamaa akitia upepo katika tairi la lori kwenye foleni ya mataa ya Ubungo jijini Dar es salaam leo. Mdau aliyeleta taswira hii anahoji, je Watanzania tumefikia hatua hii kweli - hata haya hatuna???

older | 1 | .... | 578 | 579 | (Page 580) | 581 | 582 | .... | 3282 | newer