Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110151 articles
Browse latest View live

clouds Fm yaibuka na tuzo ya ubora (superbrands) kwa mara ya tatu mfululizo.

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk Mary Nagu (kati) pamoja na Mkurugenzi wa Mradi wa Superbrands Afrika Mashariki, Bw Jawad Jaffer kwa pamoja wakimkabidhi cheti Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Bwa.Joseph Kusaga kwa Couds Fm redio kuibuka na tuzo hiyo ya ubora kwa mara ya tatu mfululizo. Tukio hilo lilifanyika hivi karibuni katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mradi Superbrands Afrika Mashariki, Bw Jawad Jaffer akimkabidhi cheti kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Media Group,Bwa. Joseph Kusaga mara baada ya Clouds Fm Radio kuibuka na tuzo hiyo ya Superbrand kwa mara ya tatu mfululizo. Hafla hiyo ilifanyika hivi karibuni katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

INVITATION FOR APPLICATION FOR ADMISSIONS TO VARIOUS CERTIFICATE AND DIPLOMA PROGRAMMES FOR THE 2012/2013 ACADEMIC YEAR FOR MARCH INTAKE

$
0
0

Tumaini University Makumira – Iringa University College invites applications from qualified Tanzanian and non-Tanzanian candidates for admissions to various certificate and diploma programmes for MARCH INTAKE in the 2012/2013 academic year in all her centres – Iringa, Mbeya and Njombe. For full details CLICK HERE

SHINDANO LA KUTAFUTA NEMBO YA BAVICHA

$
0
0

Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) liko kwenye mchato wa kutafuta nembo yake ambayo itakuwa kielelezo cha vijana ndani ya CHADEMA. Nembo hii itakuwa alama ya utambulisho na inatarajiwa kutumika katika shughuli na mambo mbali mbali ya vijana ndani ya CHADEMA.


Katika kufanikisha upatikanaji wa nembo, BAVICHA inatambua uwepo wa vipaji mbalimbali vikiwemo vya ubunifu miongoni mwa vijana wa Tanzania ambao baadhi yao ni wanachama na wafuasi wapenda mabadiliko wa Chadema.


Ili kutoa fursa kwa vijana hawa kutumia vipaji vyao na kutoa mchango wao kwa Chama na Baraza lao, BAVICHA imeandaa shindano maalumu la ubunifu wa NEMBO YA BAVICHA na hivyo kukaribisha wale wote ambao wangependa kushiriki kwa kubuni nembo hii.


VIGEZO MUHIMU VYA KUZINGATIWA

Kwa wale wote wenye kipaji cha ubunifu na wangependa kushiriki shindano hili watapaswa kuzingaztia vigezo vifuatavyo katika ubunifu wao;

1.    Rangi zitakazotumika ni lazima ziwe zinatokana na rangi kuu za CHADEMA

2.    Nembo kuu ya Chama inaweza pia kutumika kubuni nembo ya BAVICHA

3.    Mbunifu atoe maana halisi ya nembo atakayoibuni kwa mukhtadha wa vijana na maudhui mapana ya CHADEMA


MUDA WA SHINDANO

Muda wa shindano hili la kupata nembo ya BAVICHA utakuwa ni mwezi mmoja yaani kuanzia tarehe 26/02/2013 - 26/03/2013. Mbunifu anaweza kuwasilisha ubunifu wake moja kwa moja ofisi za BAVICHA zilizopo mtaa wa Togo Kinondoni – Manyanya, au kwa kutumia barua pepe: bavicha.chadema@gmail.com


MCHAKATO WA UCHAMBUZI

Baada ya wadau mbalimbali kuwasilisha nembo walizozibuni, Sekrataiati ya BAVICHA itazichmbua na hatimaye kupata nembo tatu bora ambazo zitawekewa utaratibu wa kushindanishwa na baadae kuingizwa kwenye vyombo vya kimaamuzi ili kupata nembo moja itakayotumiwa na Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA)


ZAWADI

Kwa kuwa shindano hili linalenga kuwapatia vijana wa CHADEMA na wasio wa CHADEMA lakini wenye mapenzi na CHADEMA fursa ya kutumia na kuvitangaza vipaji vyao na hivyo kutoa mchango wao katika ujenzi wa BAVICHA imara, mshindi wa shindano hili atapewa Shilingi 500,000/=  kama zawadi na pia cheti maalumu cha kutambua mchango wake kwa BAVICHA.


WALENGWA

Walengwa wa shindano hili ni vijana wote wa CHADEMA pamoja na wanachama na wafuasi wa CHADEMA wenye ujuzi/kipaji cha ubunifu.


WITO

BAVICHA inawahamasisha vijana wa CHADEMA na wote wanaopenda mabadiliko kushiriki shindano hili ikiwa ni sehemu ya kuijenga taasisi hii ya vijana ndani ya CHADEMA


Imetolewa na:

Deogratias Munishi

Katibu Mkuu - BAVICHA

Article 1

Article 0

$
0
0

"Mikono Business Consult inwaletea Semina kabambe ya kukuwezesha wewe mjasiriamali kutengeza mfumo imara kwa ajili ya mafanikio ya kibiashara. Semina hii itafanyika mnamo tarehe 22 Machi kwenye hoteli ya Holiday Inn iliyopo katikati ya Jiji la Dar Es Salaam. Kiingilio ni Tsh 30,000/= tu ikiwemo vinywaji. Wasiliana nasi leo kupitia namba 0717 109362 au anuani ya barua pepe info@mikono.biz."

Kwa maelezo zaidi tafadhali piga simu namba 0717 109362 au 0712 453493.

Mikono Business Consult

MNADA MNADA

lady jay dee kama kawa ndani ya nyumbani lounge.

NBC APPOINTS NEW MANAGING DIRECTOR

$
0
0
The National Bank of Commerce (NBC) has today announced the appointment of Mizinga Melu as its new Managing Director, subject to regulatory approval. The appointment is with effect from 20th May 2013.

Mizinga is joining NBC from Standard Chartered Bank Zambia where until now she has been Managing Director since 2007. She takes over from Lawrence Mafuru, who left the bank in December, 2012.

Mizinga has previously served in senior roles at Standard Chartered, including as Global Head of Development Organisations in the United Kingdom where she was responsible for strategy development and implementation as well as Africa Regional Head of Financial Institutions in Kenya and South Africa where she led formulation of Standard Chartered’s FI business strategy in Africa. Prior, she served as Head of Treasury at Standard Chartered Bank Tanzania between 2000 and 2003.

Mizinga holds a Masters in Business Administration (MBA) from Henley Management College (UK) and is an Associate of the Chartered Institute of Bankers (A.C.I.B). She holds numerous other banking qualifications.

Commenting on the appointment, Barclays Africa Chief Executive Officer and Head of Africa Group Strategy, Kennedy Bungane said: “The appointment of Mizinga reiterates the importance of NBC to our ‘One Africa Strategy’ and we are excited that she is joining us at a time we are making steady progress towards our goal of becoming the go-to bank in Africa.”

Dr. Mussa Juma Assad, Chairman of NBC commented: “The board welcomes Mizinga to NBC and looks forward to working with her in maintaining the position of NBC as a leading bank in Tanzania.”

Commenting on her appointment, Mizinga said: “NBC has over the years proven to be an important financial services provider in Tanzania. I am privileged to have the opportunity to lead this great bank at this important moment and I am looking forward to working with every colleague in NBC as we continue on our journey of transforming the bank in the market.”

Mizinga will report directly to Kennedy Bungane, Barclays Africa Chief Executive Officer and will be a member of the Barclays Africa Executive Committee.

SAFARI LAGER YAFUNGA ZOEZI LA FOMU ZA PROGRAMU YA “SAFARI LAGER WEZESHWA”.

$
0
0
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kufunga zoezi la kuchukua na kurudisha fomu za kuomba ruzuku ya Safari Lager Wezeshwa Dar es Salaam jana.Kulia ni Jaji Mkuu wa Programu hiyo, Joseph Migunda.
Jaji Mkuu wa Programu ya Safari Lager Wezeshwa, Joseph Migunda (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kufunga zoezi la kuchukua na kurudisha fomu za kuomba ruzuku ya Safari Lager Wezeshwa Dar es Salaam jana.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.

SHUKRANI

$
0
0

Familiya ya Alhaji Hassan Kippingu ya  Kiluvia Dar Es Salaam, wanatoa shukurani zao za dhati kwa Ndugu , Jamaa na Marafiki wa marehemu Farida Hassan Kipingu, kwa kushiriki kwa Hali na mali wakati wa kipindi kigumu cha kumuuguza mpendwa mtoto wao, mpaka umauti ulipo mkuta na kushiriki pamoja katika
Mashishi yake. 

Nivigumu kumtaja mtu mmoja mmoja, ila shukurani za pekee ziwaendee wauguzi wa Hospt. Ya Agakhan pamoja na marafiki zake wote.

Tunapenda kuwataarifu kutakuwa na Arubaini itakayo fanyika tarehe 10/03/13 saa 03:00 Asubuhi nyumbani kwao Kiluvya wote mna karibishwa

INNA  LILLAH WAINNA  ILAYHI RAAJIUN

UTEUZI WA WAJUMBE WA BODI YA SHIRIKA LA VIWANGOTANZANIA TBS

Zanzibar nayo Yaingia Digitali hivi sasa

$
0
0
Wazizi wa Habari,Utalii Utamaduni na Michezo Said Ali Mbarouk akizungumza na wandishi wa habari jinsi ya utaratibu wa Digital utavyoanza na upatikanaji wa Ving'amuzi huko ktk ukumbi wa salama holl Bwawani Mjini Zanzibar.
Waandi wa habari wa vyombo mbali mbali wakimsikilaza Wazizi wa Habari,Utalii Utamaduni na Michezo Said Ali Mbarouk hayupo pichani akizungumzia jinsi ya utaratibu wa Digital utavyoanza na upatikanaji wa Vingamuzi huko ktk ukumbi wa salama holl Bwawani Mjini Zanzibar.

Na Ali Issa Maelezo Zanzibar 28/2/2013

Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imetangaza rasmi, kuazia leo Matangazo ya dijital yatakuwa hewani kutoa huduma zake kwa majaribio ili kuona wananchi watao pata ving’amuzi wana faidika na huduma hiyo muhimu ya matangazo.

Amesema matangazo hayo ya taenda hewani baada ya kukamilika miundo mbinu ya kufanikisha urushaji wa mangazo ya dijital na yale matangazo ya analog yataendelea kuwepo mpaka wana nchi walio wengi kuweza kumiliki vingamuzi na ndipo serikali kutangaza kuyafunga mangazo ya analojia.

Hayo yamesemwa leo huko Hoteli ya Bwawani na Waziri wa Habari Utalii,Utamaduni na Michezo Saidi Ali Mbaruok wakati wa uzinduzi wa matangazo ya dijital na upatikanaji wa ving’amuzi mbele ya waandishi wa habari walio fika Hotelini hapo.

Amesema matangazo hayo yako tayari kurushwa hewani leo kwamajaribio baada ya kukamilika miundo mbinu ya matangazo ambapo kwa ujumla miundo mbinu hiyo inamilikiwa na serikali na wateja wao kwa sasa walio nunua vingamuzi , watakuwa wana ipata huduma hiyo bila pingamizi yoyote.

“wananchi wa Zanzíbar walishamiliki miundo mbinu ya digital ,jambo ambalo ni lakujivunia sana kwani karibu nchi zote jirani miundo mbinu yao ya dijitali inamilikiwa na kampuni kutoka nje ,sisi Zanzíbar miundo mbinu yetu ya dijitali ni mali ya serikali ya Zanzíbar.alisema waziri.

Aidha waziri huyo alisema kuwa matangazo hayo yataruka yakiwa chini ya utalaamu wa kamuni ya Agape kwa muda wa miaka miwili kwa masharti walioekeana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzíbar, huku ikiwafundisha watalamu wazalendo na mna ya kuitumia mitambo hiyo ya kisasa pamoja na uendeshaji vipindi vilivyo kubaliwa na serikalini yao.

“Serikali imetiliana mkataba wa uendeshaji wa miundo mbinu wa miaka miwili na kampuni ya Ágape katika kipindi hicho cha miaka miwili kampuni ya Ágape itaendesha mitambo hiyo kwa masharti atayo pewa na serikali yetu na wakati huo huo wakiwafundisha wataaalamu wetu ili baada ya muda huo kumalizika wataalamu wetu wa weze kuindesha wenyewe. Alisema waziri.

Waziri huyo alisema kuwa wana nchi wasihamanike juu ya bei ya kingamuzi ni ileile ya shilingi elfu hamsini 50000 ambayo ni rahisi kwani ilizingatia halizao , ispokuwa kilicho ongezeka ni gharama za usajili shilingi 1500 na shilingi 8000 ni malipo ya awali ya mwezi kituambacho ni cha kawaida.

Serikali imekusudia kuleta vingamuzi laki tatu 300000 ifikapo mwezi wa tatu mwaka huu lakini kwa sasa jumla ya vingamuzi 5000 tayari vimeshawasili zanzbar natayari kuzwa katika maeneo yalio sajiliwa ikiwemo raha leo Studio.

Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzíbar.

Samsung yazindua aina Mpya Viyoyozi (Air Conditioners) jijini Dar leo

$
0
0
 Mgeni Rasmi katika hafla ya Uzinduzi wa aina mpya ya Viyoyozi (Air Conditioners) vya kutoka Kampuni ya Samsung,Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara,Mh. Gregory Teu,akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya Uzinguzi huo wa aina ya Viyoyozi vifahamikavyo kama DVM S (Digital Variable Multi System) iliyofanyika usiku huu katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro Kempisk,jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Viyoyozi (Air Conditioners) vya Samsung katika nchi za Afrika Mashariki na Kati,George Kesabo akizungumzia namna walivyojipanga kuhimarisha huduma zao kwa wateja wote wa bidhaa za Samsung wakati wa hafla ya Uzinduzi wa aina mpya ya Viyoyozi (Air Conditioners) vya Kampuni hiyo, iliyofanyika usiku huu katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro Kempisk,jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa Usimamizi wa Vifaa mbali mbali vya Majumbani kutoka Kampuni ya Samsung,Sunny Sharma akifafanua jambo wakati wa hafla hiyo Uzinduzi wa aina mpya ya Viyoyozi (Air Conditioners) viitwavyo DVM S (Digital Variable Multi System) vya Kampuni hiyo, iliyofanyika usiku huu katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro Kempisk,jijini Dar es Salaam.
 Kiyoyozi (Air Condition) Kipya kikizinduliwa.

MTENDAJI MKUU TAZARA AACHIA NGAZI

$
0
0

Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) Bw. Akashambatwa Mbikusita-Lewanika (pichani), hatimaye ameachia ngazi baada ya kuendesha kampeni kali ya miezi kadhaa kutaka aendelee kuongoza Mamlaka hiyo kwa miaka mingine mitatu.

Hatua hiyo ya kuachia ngazi imekuja baada ya Bodi ya Wakurugenzi na Baraza la Mawaziri la Mamlaka hiyo kuonyesha dhahiri kutotaka Mzambia huyo aendelee na uongozi wa TAZARA kutokana na utendaji wake mbovu na uongozi mbaya uliowabagua wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kwa misingi ya utaifa wao.

Habari za ndani za Mamlaka hiyo zimesema Bw. Akashambatwa ambaye kipindi chake cha uongozi kiliisha tarehe 22 Januari, 2013 kiliongezwa kwa maombi maalum ya Serikali ya Zambia kwamba Serikali hiyo ilihitaji muda mrefu kidogo kumpata mbadala wake, licha ya Serikali ya  Tanzania kutoridhishwa na utendaji wake.

Katika kikao chake cha tarehe 20 Februari, 2013 jijini Lusaka, Zambia, Baraza la Mawaziri lilijadili kwa siri na kwa kirefu suala la mtendaji Mkuu huyo ambaye inasemekana aliombewa tena na Serikali ya Zambia kipindi cha nyongeza, ombi ambalo inadaiwa lilipingwa vikali na ujumbe wa Serikali ya Tanzania.

Taarifa za uhakika ndani ya Wizara ya Uchukuzi zinasema Serikali ya Tanzania haikumtaka Mtendaji Mkuu huyo kwa sababu kadhaa zikiwemo :uwezo mdogo, ubadhirifu, kuchochea ubaguzi kati ya Watanzania na Wazambia, ukaidi na uchochezi. Inadaiwa kuwa Mtendaji Mkuu huyo alizuia kuanzishwa kwa mradi wa usafiri jijini Dar es Salaam bila sababu yoyote ya msngi na kuishia kusambaza taarifa za uongo na uchochezi Zambia na magazeti mbalimbali nchini.

Tarehe 25 Februari, 2013 Gazeti la kila siku la Zambia, Zambia Daily Mail, liliripoti tukio hilo la kuachia ngazi kwa kiongozi huyo ambaye anajulikana sana nchini Zambia kama mfanyabiashara na kiongozi wa kimila (chief),                                              

Gazeti hilo lilinukuu barua ya Bw. Akashambatwa ya tarehe  22 Februari, 2013 kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Ujenzi, Ugavi na Mawasiliano ya Zambia, akielezea kuwa hakuna faida ya kuomba kurefushwa kwa mkataba wake wakati vyombo vikuu vya uongozi vya TAZARA, Bodi ya Wakurugenzi na Baraza la Mawaziri, havionyeshi kumkubali.

Kuondoka kwa Bw. Akashambatwa kwenye uongozi wa TAZARA kunatarajiwa kupokewa na wafanyakazi wa TAZARA kwa nderemo na vifijo.

Tanzania DMV kushiriki Diaspora World Cup 2013

$
0
0
Kama Watanzania tuishio USA kwa pamoja tuko kwenye kushiriki diaspora world cup soccer kwa nia ya kufanikiwa kwenye medali za kimataifa, ili kuitangaza Tanzania katika miundo mbinu, utalii na vyote vinavopatikana nchini kwetu. 

Katika ushiriki wetu wa mwaka Jana tulianzisha timu na tulikuwa tunajulikana Kama Tanzania team tuliweza kushiriki kwenye Vijimambo Cup kama Tanzania DMV timu zilizoshiriki ni Malawi, Burundi, Atlanta Georgia, Star United na Tanzania DMV, tuliweza kuibuka washindi wa mashindano hayo na balozi wetu wa Tanzania nchini Marekani alitukabidhi kombe la ushindi, tembelea www.diasporaworldcup2013.com kwa matukio hayo.

Mwaka 2012 tulishiriki kwenye diaspora world cup na tukaweza kufika robo fainali na tuliweza kuzifunga timu kubwa kama Malawi, Spain, Cameroon na Ghana. Tumejifunza vitu vingi kwa mataifa mengine walivyo weza kuzitangaza nchi zao vikiwemo vyama vya michezo kutoka nchini kwao vilivosimamia katika uboreshaji wa nchi zao ili zifanye vizuri. Sisi kama waTanzania tunayo haki ya kupeperusha na kuitangaza nchi yetu kwa umoja na tukafanikiwa. Tunaomba Ushirikiano wenu.

Natanguliza shukurani zetu
Jabiri Jongo
Team Manager

mtanange wa NMB vs Marafiki wa Imani

$
0
0
Mechi kati ya NMB na marafiki wa Imani Kajula iliisha kwa NMB kushinda goli 4 – 3 dhidi za marafiki wa Imani. Mechi hiyo maalum ya kumuaga Imani ilifanyika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam ikishuhudia katibu mkuu wa zamani wa TFF Fredrick Mwakalebela akiibuka nyota wa mchezo.

Timu ya marafiki wa Imani ikiwa tayari kwa mechi na NMB.



Nyota wa mchezo wa leo kipa wa marafiki wa Imani, Fredrick Mwakalebela akiwa na kipa ya NMB Richard Mwalibwa.



Nahodha wa Timu ya marafiki wa Imani Shaffy Dauda akitoa maelekezo wakati wa mapumziko.



Moja ya hekaheka za mechi hiyo, Imani Kajula akimtoka Erick Ruyangi.

Article 13

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA
(PSPF)
TAARIFA KWA UMMA
Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) unawajulisha kwamba Mkutano Mkuu wa wadau utakaofanyika tarehe 07 na 08 Machi 2013 kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa kumi jioni katika Ukumbi wa JB Belmont uliopo ghorofa ya 6 ya Jengo la Maegesho la PSPF - Golden Jubilee Towers , Dar es Salaam.
Madhumuni ya Mkutano huu ni kutoa taarifa ya hesabu ya mwaka na utendaji wa Mfuko na kutathmini mafanikio na changamoto zinazoukabili Mfuko na Sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa ujumla.
Tafadhali thibitisha ushiriki wako kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu Makao Makuu, Dar es Salaam au Ofisi za PSPF mikoani kabla ya tarehe 05 Machi 2013.
“PSPF - Tulizo la Wastaafu”
Kaimu Mkurugenzi Mkuu
Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma,
Golden Jubilee Towers, Ghorofa ya 6-13, Mtaa wa Ohio/Kibo,
Central Area, Kiwanja Na. 8, 9, 12 na 15,  S. L. P 4843. Dar-es-Salaam.
Simu: +255 22 2120912/52 au +255 22 2127375 /6
Nukushi: +255 22 2120930.

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Mdau Mesiaki asante sana kwa kuendeleza libeneke hili. Hizi ngoma zako zinakosha mno. Globu ya Jamii inakaribisha 'Special requests' kwa ngoma za enzi hizo na za sasa. Usisahau Cheka Unenepe..

Article 11

Moto wateketeza maduka zaidi ya kumi Tegeta kwa mujibu wa ITV

Viewing all 110151 articles
Browse latest View live




Latest Images