Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 576 | 577 | (Page 578) | 579 | 580 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalum Mhe. Andrew Chenge (mjumbe) akiongoza kikao cha kamati hiyo jana ambapo kamati hiyo inamalizia uandishi wa Katiba pendekeze inayotarajiwa kuwasilishwa Bungeni Jumatatu wiki hii. Kamati hiyo inachambua maoni ya taarifa za Kamati pamoja na michango ya Wajumbe wakati wa Mjadala na kuyaweka maoni hayo pamoja na kisha kuandaa katiba inayopendekezwa. picha na Owen Mwandumbya.


  0 0

  Mkuu wa Majeshi Nchini Tanzania Davids Mwamunyange akisalimiana na Mwenyekiti wa Shirika la Nyumba la Serikali ya Dubai (NAKHEEL) Mhe. Ali Rashid Ahmed Lootah alipo mtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam.
  Mh. Davis Mwamunyange akifanya mazungumzo na Mhe. Lootah mara tu baada ya kuwasili ofisini kwake, Mhe. Lootah katika ziara yake anaangalia fursa za uwekezaji katika uchumi, ujenzi wa nyumba na makaazi
  Afisa Mambo ya Nje Bw. Hangi Mgaka akifuatilia kwa makini mzungumzo kati ya Mhe. Davis Mwamunyange na Mhe. Lootah (Hawapo pichani) na (wakwanza na wapili kutoka kulia) ni wajumbe walioambatana na Mhe. Lootah katika ziara
  Kulia ni Balozi Mdogo Omar Mjenga akizungumza jambo huku Mhe. Davis mwamunyange (wakwanza kushoto) na Mhe. Lootah (katikati) wakimsikiliza wakielekea nje mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo. 
  Katikati ni Mkurugenzi wa Nyumba kutoka Dubai Mhe. Ali Rashid Ahmed lootah, nawa kwanzakushoto ni Mkuu wa Majeshi nchini Tanzania Mhe. Davis Mwamunyange na wakwanza kulia ni Balozi mdogo wa Tanzania, Dubai Mhe. Omar Mjenga wakiwa katika picha ya pamoja.
  Picha ya Pamoja.
  Picha na Reginald Philip.

  0 0

   Kamishna wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (Tacaids), Daniel Machemba katikati akikata utepe kaushiria uzinduzi wa mabango ya kuelimisha Ukimwi na masuala mbalimbali ya kuwajengea uwezo vijana yatakayosambazwa katika vyuo vikuu mbalimbali na Shirika la Vijana Tayoa. Anayefuata kulia ni kamishna mwingine Diana Chilolo, Mkurugenzi wa Tayoa Peter Masika. Kulia ni Mhadhiri wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM, Emmanuel Mushi na Kamishna wa Tacaids, Faraja Kotta Nyalandu.
   Kamishna wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi, Diana Chilolo akimkabidhi zawadi Mhadhiri wa Chuo cha IFM, Emmanuel Mushi kwa chuo hicho kushirikiana na Shirika la Vijana tayoa katika mapambano dhidi ya Ukimwi. Nyuma yake ni kamishna mwingine, Faraja Kotta Nyalandu, Kamishna Daniel  Machemba na Mkurugenzi Mkazi wa Tayoa Peter Masika.
  Kamishna wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi, Diana Chilolo akimkabidhi zawadi Mhadhiri wa Chuo cha IFM, Emmanuel Mushi (mbele shati la bluu) kwa chuo hicho kushirikiana na Shirika la Vijana tayoa katika mapambano dhidi ya Ukimwi. Pembeni yake ni kamishna mwingine, Faraja Kotta Nyalandu, Kamishna Daniel  Machemba na Mkurugenzi Mkazi wa Tayoa Peter Masika.

  0 0

  Maandamano ya CHADEMA Mkoa wa Dodoma yamedhibitiwa kwa Mkoa mzima.
  Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi wa Polisi EMMANUEL G. LUKULA (ACP) (pichani) amesema katika hilo kuna gari lenye namba za usajili T.792 CAX aina ya Pick up Ford Ranger nyeupe mali ya CHADEMA iliyokuwa ikiendesha na CHRISTOPHER NYAMWINJA, Mweneye miaka 52, Mgogo, Mkristo Mratibu wa CHADEMA Kanda ya magharibi ambapo makazi yake ni TABORA mjini limekamatwa mtaa wa KUU karibu na kituo cha mafuta cha GAPCO jirani na WIMPI RESTAURANT likiwa na watu wengine watatu ambao ni:-

  1.     LAURENT S/O MANGWESHI mwenye miaka 36, Mkristo, Msukuma Mkulima wa Wialya ya Mpanda Mkoa wa Katavi.

  2.     AGNES D/O STEPHANO mwenye miaka 26, Mhehe, Mkristo Mfanyabiashara Mkazi Ubungo MAziwa Dar es Salaam.

  3.     ELISHA S/O DAUDI mwenye miaka 49, Msukuma, Mkristo Fundi umeme Mkazi wa TAbora.

  Kamanda LUKULA – ACP amesema gari hilo lilikuwa na bango lenye maandishi “TUNAPINGA UFISADI UNAOFANYWA NA BUNGE LA KATIBA”. Likiwa na maandishi ubavuni mbele na nyuma M4C.

  Aidha Kamanda LUKULA – ACP ameongeza kuwa kabla ya kukamatwa kwa gari hilo Polisi walilikimbiza na katika kupita kwenye kona/mtaa watu wawili waliruka kutoka kwenye gari hilo na kukimbia kusikojulikana na bango hilo. Watu waliobaki ndani ya gari hilo ambao ni wanne ndio waliokamatwa.
  Askari Polisi wakiwa kwenye zoezi la kuzuia Maandamano ya Chadema Mjini Dodoma.

  0 0

  Asasi Nne zisizo za kiserikali zinazojishughulisha na kupambana na mabadiliko ya tabianchi nchini ForumCC, CAN, YouthCAN na Oxfam Tanzania zimetoa tamko la pamoja kuhusiana na Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika huko New York-Marekani tarehe 23/09/2014.

  Katika tamko hilo ambalo pia limewasilishwa kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Dr. Eng. Binilith Mahenge, mambo matano yamependekezwa kuzingatiwa wakati wa mkutano huo ambao Rais wa Tanzania DK. Jakaya Kikwete pia atatoa hotuba yake.

  Mambo hayo ni pamoja na kupunguza utoaji wa hewa ukaa (Emission Reduction), Misaada ya Fedha za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi (Climate Finance), Kuongeza mapambano ya mabadiliko ya tabianchi kwa vitendo, Matumizi ya teknolojia na Nishati Mbadala na Kilimo.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Dr. Eng. Binilith Mahenge(katikati) akiwa na Viongozi wa Forum CC, kutoka kulia ni Oscar Munga, Mjumbe wa bodi ya wadhamini ya ForumCC, Vera Mugita, Afisa Miradi, Fazal Issa na Adam Anthony.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Dr. Eng. Binilith Mahenge wa kwanza kushoto akizungumza na Mjumbe wa bodi ya wadhamini ya ForumCC, Vera Mugita na Afisa Miradi wa ForumCC Fazal Issa


  0 0

  Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai kamishina wa polisi Isaya Mngulu akizungumza na waandishi wa habari leo mjini mjini Songea mkoani Ruvuma
  ---------------------
  Na Nathan Mtega wa demasho.com,Songea

  JESHI la polisi chini limethibitisha kuwa kitu kilichokuwa kinadaiwa kuwa nio bomu lililorushwa mjini Songea mkoani Ruvum Septemba 16 mwaka huu majira ya saa 1.25 usiku katika eneo la Misufini na kuwajeruhi askari polisi watatu kati ya wanne waliokuwa doria kuwa ni bomu la kutupwa kwa mkono lililotengenezwa kienyeji.

   Akitoa taarifa ya uchunguzi wa tukio hilo kwa waandishi wa habari mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai kamishina wa polisi Isaya Mngulu amesema bomu hilo lilirushwa na watu wasiojulikana na kuwajeruhi askari polisi watatu waliokuwa doria siku hiyo wa kituo kikuu cha polisi cha mjini Songea ambao ni G.5515 PC John,G7351 PC Ramadhan na WP 10399 Felista ambao baaada ya kujeruhi kwa bomu hilo walikibizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma iliyopo mjini Songea kwa matibabu.

  Amesema askari PC John aliyepata majeraha kiasi alipatiwa matibabu siku hiyo na kuruhusiwa huku askari wawili PC Ramadhan na WP Felista wakiendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo na hali zao zinaendelea vizuri.
  Aidha amesema jeshi las polisi makao makuu kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoani Ruvuma na vyombo mbali mbali vya ulinzi na usalama vinaendelea na uchunguzi zaidi ikiwa ni pamoja na kutafuta taarifa za waliohusika na tukio hilo ambalo mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana nalo.

  Amesema jeshi la polisi linaamini kuwa wahusika waliofanya tukio hilo ni sehemu ya jamii inayoishi mjini Songea au yenye mahusiano na wenyeji wa Songea na mtu aliyetengeneza bomu hilo lazima kuwa kuna  mtu au watu walioshuhudia au wanaomjua kwa maana kwamba hakuwa pekee yake na ni imani ya jeshi la polisi kuwa kuna baadhi ya wananchi wanaweza kuwa wanawafahamu wahusika wa tukio hilo wasisite kushirikiana na jeshi la polisi kuwafichua ili kuendeleza ushirikiano mwema na jeshi la polisi kwa ulinzi.

  Katika hatua nyingine mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai Kamishina wa polisi Isaya Mngulu ametoa wito kwa wananchi kuendeleza ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na timu ya upelelezi kutoka makao makuu ya jeshi la polisi kwa ajili ya kuwapata wahusika wa tukio hilo ambalo limetokea kwa mara ya kwanza mkoani Ruvuma na lisipofanyiwa kazi ipasavyo linaweza kutoa mwanya kwa wahalifu wa aina hiyo kuendeleza uhalifu huo kwa wananchi pamoja na jeshi la polisi.

  0 0

  The East African Community (EAC) Secretary General Amb. Dr. Richard Sezibera has encouraged journalists from East Africa to promote positively the regional integration process.

  “Be pro-EAC integration by reporting objectively about the EAC integration, on its huge benefits and enormous opportunities that exist for the people of the region and for our common good,’’ Dr. Sezibera told Thursday about 15 senior journalists and editors attending a week-long advance training on reporting inter-religious conflicts in the EAC Region, in Kigali, Republic of Rwanda.

  The training is running parallel to the on-going five-day EAC conference on inter-religious collaboration to strengthen peace and security in East Africa. The EAC chief said that the role of the media in EAC integration should be to change the mindsets of people so as to easily and happily embrace the regional integration process. “But to do this, you yourselves need to develop a pro-East African mindset because with it, you will be able to see and write positively from the regional perspective” affirmed Amb. Sezibera.

  Media houses and editors, he added, have unique opportunity to swing the pendulum of integration by telling accurately and in balanced way the so many positive work carried out in the Partner States.
  “It is extremely important that EA journalists assisted in the EAC’s goals,” he stressed.

  The Secretary General later responded to myriad of questions from the journalists on the EAC integration process. The Secretary General was accompanied by the EAC Deputy Secretary General (in charge of Political Federation), Mr Charles Njoroge.

  Also present at the occasion was Miriam Heidtmann, GIZ’s Manager responsible for Peace and Security. The GIZ has facilitated both the inter-religious conference and the training of the journalists.
  The scribes Thursday afternoon toured Nyamata Genocide Memorial site; a church where around 2,500 people were killed and it has become emblematic of the barbaric treatment of women during the 1994 genocide.

  In the church, the scribes viewed the graphic and audio-visual displays focused particularly on the mass rape, brutalization of women and the use of HIV as a deliberate weapon of genocide. Earlier on Tuesday, addressing the opening of the journos training, the Head of EAC Corporate Communications and Public Affairs, Mr Owora Richard Othieno, said that religious issues were sensitive and must be handled with a lot of care and understanding for the unity of the East Africans.

  “Your journalistic skills, experience, patience and mutual respect are absolutely necessary to report fairly on religious-related issues and events,” he counselled.

  The advance training is conducted by veteran journalists and consultants, Dr. Christopher Kayumba from Republic of Rwanda and Dr. Haron Mwangi from Republic of Kenya. The inaugural inter-religious conference, which is attended by over 150 delegates from the Partner States, will close on Saturday.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki akizungumza na wajumbe hao katika Manispaa ya Kinondoni kabla ya kuanza kwa ziara. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda.
  Wajumbe wakiwasili Kata ya Mabwepande kukagua ujenzi wa Hospitali ya Mabwepande.
  Mhandisi wa Majengo wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Brighton Kimaro akiwaongoza Meya wa Manispaa hiyo Yusuf Mwenda (kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki na wajumbe hao kukagua jengo la hospitali ya Mabwepande.
  Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida (kushoto kwake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki na wajumbe hao kuhusu maendeleo ya ujenzi wa soko la kisasa la wafanyabiashara ndogo lililopo ndani ya kituo kipya cha daladala cha Sinza.
  Wajumbe wakiingia kukagua kituo cha kisasa cha polisi kilichofungwa CCTV Camera kilichopo ndani ya kituo cha daladala cha Sinza.
  Kaimu Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni, Ismail Mafita akitoa maelezo kwa wajumbe wa kamati hiyo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa kituo cha daladala cha Sinza. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida (wa pili kulia) na Meya wa Manispaa hiyo, Yusuf Mwenda.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Rais wa Serikali ya JamhurI ya Muungano wa Comoro Dr.Ikililou Dhoinine wakiagana katika ukumbi wa Ikulu ya Comoro wakati Rais Shein alipomaliza ziara yake na ujumbe aliofuatana nao nchini humo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Comoro Mohamed Ali Soilihi katika uwanja wa Ndege wa Comoro wakati Dk.Shein alipomaliza ziara yake ya siku nne nchini Comoro.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakiagana na Viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Comoro katika Uwanja wa Ndege wa Comoro baada ya kumaliza Ziara ya siku nne kwa mualiko wa Serikali hiyo.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu Zanzibar.

  0 0

  Siku kama ya leo 19 September ndio siku ya kuzaliwa mkuu wa bendi ya Ngoma Africa aka FFU ya kule ujerumani, kamanda Ras Makunja (pichani) alizaliwa mjini Dar-es-Salaam, akiwa mtoto wa kwanza wa kiume wa Bw.Jumanne Saleh Makunja Ngayonga (RIP) na Bi.Moza Hassan Seifu Mpili (Mama Makunja), Mwanamuziki Kamanda Ras Makunja leo ndio Happy Birthday !!!!! yake pia unaweza kuburudika na kusherekea naye katika kambi yao FFU-Ughaibuni at http://www.ngoma-africa.com au www.ngoma-africa.com

  0 0

  Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick (wa tatu kushoto), wakiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam leo. Daraja hilo linajengwa kwa  ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF). Wa nne kushoto ni Meneja Mradi ujenzi wa daraja hilo, Mhandisi John Msemo. Picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0  Mmiliki wa Jossekazi Auto garage ambao ndiyo waandaaji wa tamasha akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamasha la kwanza la Magari la aina yake, linalojulikana kwa jina la Automobile Clinic, ambalo linatarajiwa kufanyika kwa siku mbili Septemba 27 na 28, 2014 katika viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam. Ambapo alisema kuwa tamasha hilo limelenga katika kutoa huduma ya kitaalamu ya kiufundi kwa wenye magari (Checkup and Fix) kutoka kwa mafundi stadi ambao wamebobea katika fani ya ufundi wa makenika katika aina tofauti tofauti za magari. Pembeni kulia ni Mkurugenzi wa Jast Tanzania Limited, Jahu Mohammed Kessy, Mratibu wa Tamasha hilo na Mwakilishi toka Mwambi Lube Distributor, Jonathan Mwanayongo.

  Na Mwandishi Wetu. 

  Kampuni ya Jast Tanzania Limited kwa kushirikiana na Jossekazi Auto Garage and General supplier wameandaa tamasha la kwanza la Magari la aina yake, linalojulikana kwa jina la Automobile Clinic, ambalo linatarajiwa kufanyika kwa siku mbili mfululizo katika viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam. Tamasha hilo limelenga katika kutoa huduma ya kitaalamu ya kiufundi kwa wenye magari (Checkup and Fix) kutoka kwa mafundi stadi ambao wamebobea katika fani ya ufundi wa makenika katika aina tofauti tofauti za magari.

  Akizungumza na vyombo vya habari, kwenye ukumbi wa habari Maelezo, Joseph Mgaya mmiliki wa Jossekazi Auto garage amesema tamasha hili lina lengo kuwakutanisha mafundi stadi na wenye magari, kwa gharama nafuu sana ya shillingi elfu ishirini tu.
  Mkurugenzi wa Jast Tanzania Limited, Jahu Mohammed Kessy, Mratibu wa Tamasha hilo akielezea machache juu ya tamasha hilo.

  BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

  0 0

   Warembo wanaoshiriki shindano la Redd's Miss Tanzania 2014 wametembelea hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) na kujifunza mambo mengi kuhusiana na hifadhi hiyo ya mlima kilamanjaro. Pichani ni warembo hao wakipiga picha na mdau mkubwa wa masuala ya urembo mkoani Kilimajaro, Athena Mawalla wa mgahawa wa Meku's Bistro wakati warembo hao walipomtembelea wakiwa njiani kwenda KINAPA.
   Warembo wakiwa katika gari njiani kuelekea KINAPA. 

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (katikati) akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Maneromango leo wakati wa ziara yake wilayani Kisarawe, Pwani ya  kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kuata Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho pamoja na kusikiliza kero za wananchi kwa lengo la kuzipatia ufumbuzi.PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
   Wananchi wa Kata ya Maneromango wakisikiliza kwa makini hotuba ya Kinana katika mkutano huo. ambapo aliwananga wapinzani kuwa wapo kwa ajili ya kupanga maandamano, kutukana, kutoa manaeneo machafu klwa Serikali wakati CCM ipo kiutendaji zaidi katika masuala ya maendeleo ya wananchi.
   Kinana akihutubia baada yakuweka jiwe la msingi katika jengo la Zahanati ya Palaka Kata ya Malumbo wakati wa ziara yake wilayani Kisarawe.


  0 0

  Ndugu zangu,

  LEO ni Septemba 19, ni Siku ya Kuzaliwa Mtandao wa Mjengwablog.

  Kwa mwanadamu, hakupaswi kuwapo na ukomo wa kujitahidi kufanya yalo mema kwa jamii yako.

  Na katika kujitahidi kuyafanya yalo mema, basi, mwanadamu uwe tayari kukumbana na changamoto nyingi. Na kama ilivyo kwa maji ya mto, yanapokutana na mwamba, basi, kasi yake huongezeka maradufu.

  Leo blogu yako hii ya Mjengwablog imetimiza miaka minane. Miaka minane si haba. Kwa mtoto, aweza kuwa darasa la Pili. Na kwetu wa Mjengwablog ni miaka minane ya kujifunza, kukosea, kujifunza kutokana na makosa, na kisha kusonga mbele.

  Kwa niaba ya timu nzima ya Mjengwablog nachukua fursa hii kuwashukuru, kwanza kabisa, mke wangu mpenzi, Mia, ambaye, bila yeye, kazi hii yangu ya kuitumikia jamii ingelikuwa ngumu sana. Pili, niwashukuru kwa dhati wanangu wanne, Olle, John, Manfred na Gustav. Wanawangu hawa wamekuwa na mchango mkubwa pia, ikiwamo kufanya utani na mimi baba yao, ilimradi niwe na wakati wa kucheka, hata pale nilipoona kazi ni ngumu na kukutana na vikwazo.


  0 0

  Waziri wa Habari,Utalii na Utamaduni nchini Malawi Mheshimiwa Kondwani Nankhumwa alisema kuwa Serikali ya Malawi haina mgogoro na Serikali ya Tanzania kuhusiana na mpaka wa ziwa Nyasa.


  Aliyasema hayo baada ya kukutana na Jopo la Waandishi Habari wa Mkoa wa Mbeya waliotembelea ofisini kwake katika mfululizo wa ziara ya waandishi waliofanya ziara ya juma moja nchini humo katika ziara ya kubadishana uzoefu baina ya Waandishi wa Nchi hizo.


  Waziri Nankhumwa alisema  kuwa Mtoto wa Rais  wa Malawi Profesa Ather Muthalikana  anasoma Dar es Salaam naye Rais amekuwa Muhadhiri wa chuo kikuu na kwamba Watanzania wengi wanaishi na kufanya biashara nchini Malawi hivyo hakuna sababu za kuwepo kwa tofauti za aina  yoyote ile itayowapelekea kuwagawa wananchi wa pande hizo.


  Aidha alisema kuwa ili kuonesha hakuna tofauti baina ya wananchi wa pande hizo Marais wa nchi hizo watapaswa kuchukua ndoano na kuvua samaki pamoja katika ziwa hilo ili kuionesha Dunia kuwa wananchi wa pande hizo ni wamoja na kuna mwingiliano wa makabila.


  Kauli hiyo iliungwa mkono na Balozi wa Tanzania nchini Malawi Patrick Tsere ambaye alisema kuwa hakuna mgogoro wa mpaka katika Ziwa Nyasa baina ya Tanzania na Malawi.


  Aliyasema hayo alipotembelewa na waandishi wa Habari wa Mkoa Mbeya walipotembelea ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Malawi katika mfulizo wa ziara ya waandishi hao nchini Malawi ili kubadilishana mawazo na changamoto mbalimbali zikiwemo za mazingira,utalii na Elimu juu ya Ukimwi ambazo zinafanana katika nchi hizo.


  Balozi Tsere alisema hivi sasa si wakati wa marumbano kwani inahitajika subira katika mzungumzo yaliyonza baina ya viongozi wa nchi hizo na kwamba si wakati wa kuupeleka mgogoro huo katika mahakama ya  kimataifa ambapo utazigharimu fedha nyingi nchi hizo katika utatuzi wa mgogro huo.


  Hata hivyo Waandi wa Habari wa nchi hizo walifanya makubaliano ambayo yatasaidia kuzitangaza nchi hizo kimataifa ikiwa ni pamoja na mbuga za wanyama zilizopo  Malawi na Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe ili utumiwe na wananchi hizo ili kukuza uchumi wan chi hizo.


  Katika ziara hiyo Waandishi  wa vyombo mbalimbali walishiriki ikiwa ni pamoja na Tone Multimedia Group, Mbeya yetu Blog,Chanel Ten,Mwananchi,Jambo leo,Bomba Fm,Majira na Raia Mwema.  Vingine na Tanzania Daima,Baraka FM na Mwandishi Rais mstaafu Ulimboka Mwakilili ambaye alikuwa Mwenyekiti wa safari na Mhandisi wa Ujenzi Claudio  Lusimbi ambaye ni Mlezi Katika Safari hiyo
  Waziri wa Habari , Utalii na Utamaduni Nchini Malawi Mh. Kondwani Nankumwa akiongea na waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya Ofisini kwake.
   Baadhi ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya wakifuatilia Hotuba ya Waziri wa Habari, Utalii na Utamaduni Mh. Kondwani Nankumwa


  0 0

  Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba ncini Tanzania Mhe. Nehemia Mchechu (wakwanza kushoto), watatu kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Shirika la Nyumba la Serikali ya Dubai Mhe. Ali Rashid Ahmed Lootah, wapili kutoka kulia ni Bwa. Issack Peter, na wakwanza kutoka kulia ni Balozi Mdogo Mhe. Omar Mjenga, watembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu za Kigamboni zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mapema leo asubuhi jijini Dar es salaam. 
  Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa Mhe. Nehemia Mchechu akimwelezea Mhe. Lootah ubora wa nyumba za mradi wa gharama nafuu (hazipo pichani) zilizojengwa katika eneo hilo la Kigamboni jijini Dar es Salaam
  Baadhi ya Nyumba za mradi za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika eneo la Kigamboni.
  Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai Mhe. Omar Mjenga akizungumza mara baada ya kumaliza kuangalia mradi wa nyumba hizo za gharama.Picha na Reginald Philip

  0 0

  Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa mwezi wa Septemba, Muwakilishi wa Kudumu wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Balozi Samantha Power akizungumza wakati wa Mkutano wa Dharura wa Baraza Kuu la Usalama, uliofanyika Alhamisi kwa lengo la kukusanya nguvu za Jumuiya ya Kimataifa katika kuukabili mlipuko wa Ebola ambao sasa unaangaliwa katika jicho la kuwa tishio la amani na usalama wa Kimataifa.
  Wajumbe wa Baraza Kuu la Usalama wakipiga kura ya kuunga mkono azimio namba 2177( 2014) kuhusu ugonjwa wa Ebola, azimio hilo linaelezwa kuwa huenda ndio likawa azimio la aina yake kupata uungwaji mkono mkubwa. Zaidi ya Mataifa 131 yameunga mkono azimio hilo ambalo linaweka mikakati ikiwamo ya vitendo na kisiasa ya kushughulikia mlipuko wa Ebola

  Na Mwandishi Maalum, New York

  Katika hali isiyokuwa ya kawaida katika historia ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo limekasimiwa majukumu na dhamana ya masuala yote yanayohusiana na Amani na Usalama wa Kimataifa, jana alhamisi limelazimika kukutana kwa dharura kujadiliana na kuweka mikakati ya kuukabili mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.

  Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa na ambalo kwa mwezi huu wa Septemba lipo chini ya Urais wa Marekani, lilikutana chini ya kichwa cha habari kilichosema “ Amani na Usalama katika Afrika: Ebola”.

  Kwa tafsiri ya haraka ni kuwa, Ugonjwa huo wa Ebola ambao umeshapoteza idadi kubwa ya maisha ya watu katika nchi kadhaa za Afrika ya Magharibi kwamba, sasa siyo tu unachukuliwa kama janga la kiafya, kibinadamu na kiuchumi bali umekuwa ni tishio kwa Amani na Usalama wa Jumuiya ya Kimataita.

  Ni kwa sababu hiyo basi, Jumuiya ya Kimataifa kwa maana ya Umoja wa Mataifa wenyewe wanachama 193 imeamua kuuangalia kwa jicho pana zaidi mlipuko huo wa Ebola na kuutafutia ufumbuzi.

  Katika mkutano huo wa dharura na ambao kama ilivyoelezwa hapo juu uliandaliwa na Rais wa Baraza hilo kwa mwezi huu (Marekani), licha ya kusikiliza hotuba au maelezo kutoka kwa baadhi ya wajumbe wa Baraza hilo akiwamo katibu Mkuu wa Umoja wa Mataita, Mkurugenzi Mkuu wa WHO na wawakilishi kutoka mataifa ambayo yameathiriwa na mlipoko huo, Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja Azimio namba 2177.

  Azimio hilo ambalo limeungwa mkono na zaidi ya mataifa 131 ikiwamo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaelezwa kama Azimio ambalo limepata uungwaji mkono mkubwa zaidi pengine kuliko azimio lolote ambalo limewashi kuwasilishwa katika Baraza hilo.

  Nchi ambazo hadi sasa zimeathirika kwa kiasi kikubwa na mlipuko huo wa Ebola ni Liberia, Sierra Leone na Guinea. Zikiwamo Nigeria na nchi nyingine Cote d’ Ivoire na Senegal ambazo nazo zimeeleza kukumbwa na mlipuko wa Ebola

  Inaelezwa kuwa asilimia zaidi ya 50 ya wahanga wa mlipuko huo ni wanawake, ambao kimsingi kutokana wa majukumu yao ndio walezi na watoa huduma ya kwanza kwa wanafamilia wanaokumbwa na ugonjwa huo.

  Katika mkutano huo wa dharura kila mjumbe aliyepata nafasi ukiacha wale waliotoa ahadi za kutoa misaada ya hali na mali ikiwamo ya kibinadamu na fedha kwa nchi ambazo zimeathirika na mlipuko huu, wametoa wito kwa kuitaka Jumuiya ya Kimataifa na nchi zote bila ya kujali ukubwa au udogo wake kuchukua hatua madhubuti za muda mfupi na muda mrefu kuukabili mlipuko wa Ebola ambao hadi sasa hauna tiba.

  Vile vile, wazungumzaji kadhaa wamezipongeza nchi ambazo zimekabiliwa na mlipuko huo kwa hatua mbalimbali ambazo hadi sasa zimechukua katika kuukabili ugonjwa Aidha baadhi ya wazungumzaji wamesisitia haja na umuhimu wa kutozitenga au kuzinyanyapaa nchi ambazo zimeathirika kwa kile walichosema kinachotakiwa si kuzitenga bali kuzisaidia ili kupunguza kasi ya kusambaa kwa ugonjwa huu hatari.

  Mwakilishi wa Tanzania akichangia majadiliano hayo, alirejea ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aliyoitoa hivi karibuni katika mkutano wa Umoja wa Afrika uliofanyia Malabo, Equitoria Guinea kuwa Tanzania iko tayari kushirikiana kwa hali na mali na AU na washirika wengine katika kuukabili mlipuko wa Ebola.

  Umoja wa Mataifa umekwenda mbali zaidi kwa kuanzisha Kituo cha Kwanza cha aina yake kuratibu dharura ya Mlipuko wa Ebola na kuipandisha hadhi Misheni ya Kulinda Amani nchini Liberia ili pamoja na mambo mengine iweze kuratibu na kusimamia misaada inayohusiana na Mlipuko wa Ebola.

  Katika kile kinachoonekana kwa Ebola ni tishio kwa amni na usalama , nchi kama vile Marekani, Uingereza na Cuba na nyinginezo zenyewe zimeamua kuyahusisha majeshi yake katika utoaji wa misaada, mafunzo na ujenzi wa vituo vya afya kama hatua ya kukabiliana na Ebola.

  0 0
 • 09/19/14--01:38: SHUKRANI
 • Familia ya marehemu Stephen E.M Ngereza wa Ilala D'salaam inapenda kutoa shukrani zake za dhati kwa ndugu, jamaa, marafiki na majirani kwa jinsi mlivyoshirikiana bega kwa bega katika kumuuguza mpaka umauti ulipompata ndugu yetu Joyce Stephen katika hospitali ya taifa Muhimbili tarehe 07 septemba 2014 na kupumzishwa katika nyumba yake ya milele tarehe 10 Sept 2014 kijijini Maramba Tanga.

  Ni wazi kuwa katika kufanikisha kumuuguza mpaka msiba huo mzito mlitumia raslimali zenu kubwa ambazo hazirejesheki kwa namna yoyote ile.

  Familia kwa pamoja haina cha kuwalipa kwa moyo wenu wa upendo mliouonyesha zaidi ya kusema neno ahsanteni.

  Familia hiyo inawaombea kwa mwenyezi mungu mzidi kubarikiwa na kupewa ziada...Bwana alitoa na bwana ametwaa, jina la bwana lihimidiwe...
  amen

  0 0
 • 09/19/14--02:00: CHICKEN WINGS BONANZA


older | 1 | .... | 576 | 577 | (Page 578) | 579 | 580 | .... | 3285 | newer