Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109984 articles
Browse latest View live

JESHI LA POLISI MKOA WA DODOMA LAZUIA MAANDAMANO YALIYOPANGWA NA CHADEMA

$
0
0
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) EMMANUEL G. LUKULA
Na Sylvester Onesmo wa Jeshi l
a Polisi Mkoa wa Dodoma.Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limetoa tamko la kuzuia maandamano ya Chama cha CHADEMA hapo tarehe 18/09/2014 na kuwataka wananchi kuyapuuza.
Akiongea na waandishi wa habari, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi wa Polisi EMMANUEL G. LUKULA (ACP) alisema kuwa; Kufuatia Viongozi wa CHADEMA kutaka kufanya maandamano kuelekea viwanja vya Ofisi za Bunge Mkoani Dodoma kwa ajili ya kupinga Bunge la Katiba siku ya tarehe 18/09/2014 linaloendelea, kuwa maandamano hayo ni batili na akiwataka wananchi wakazi wa Dodoma kuyapuuza kwa kuwa yanakiuka Sheria iliyoliweka Bunge hilo.

Kamanda LUKULA  alitaja sababu za msingi za kuzuia maandamano hayo kuwa ni:-
1. Siku ya maandamano ya tarehe 18/09/2014 ni siku ya kazi ikiwa ni pamoja na muda wa maandamano hayo ni masaa ya kazi saa 04:00 asubuhi hadi saa 06:00 mchana yataathili ufanisi wa watu waliopo makazini/maofisini.
2. Bunge maalumu la Katiba linaloendelea kwa sasa lipo Kisheria na hakuna tamko lolote lililotolewa na Mahakama yoyote kulisitisha, hivyo moja ya kazi ya Jeshi la Polisi ni kulinda Sheria na wale wanaofuata sheria. Hivyo kufanya maandamano yanayopinga Bunge la Katiba ni kukiuka Sheria iliyoliweka Bunge hilo.
3. Kuna kesi Mahakamani ya kupinga Bunge hilo kuendelea, hadi sasa shauri hilo linaendelea Mahakamani. Hivyo kwa CHADEMA kuandamana ni kuingilia Uhuru wa Mahakama.
4. Baadhi ya Wilaya barua za kufanya maandamano zimechelewa kufika kwa Wakuu wa Polisi Wilaya kabla ya saa 24 kisheria.

Aidha Kamanda Lukula  alitoa wito kwa wananchi wa Dodoma kupuuza maandamano yoyote ya kupinga uwepo wa Bunge la Katiba kwani ni batili. Aidha aliwashauri viongozi wa CHADEMA Mkoa na Wilaya za Dodoma wayasitishe maandamano hayo na wasipo ridhika, wakate rufaa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwa maelekezo zaidi.


JK awasili Marekani kuhudhuria mkutano wa 69 wa Umoja wa Mataifa

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini usiku wa jana, Jumatatu, Septemba 15, 2014, kuanza ziara ya wiki mbili katika Marekani ambapo atahutubia Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN General Assembly) New York. Mbali na kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Rais Kikwete pia atahudhuria mikutano muhimu katika mji mkuu wa Marekani, Washington, D.C.
Rais Kikwete akiagana na viongozi mbalimbali waliofika kumuaga katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Septemba 15, 2014. Kushoto ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali
Rais Kikwete akiagana na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama waliofika kumuaga katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Septemba 15, 2014. Kulia ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali
Rais Kikwete akisindikizwa na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali wakati alipokuwa anaondoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kuelekea Marekani Septemba 15, 2014. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili New York, Marekani. Kulia Mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi akifuatiwa na Mama  Upendo Manongi Septemba 16, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakilakiwa na maofisa mbalimbali wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa baada ya kuwasili New York, Marekani, Septemba 16, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakilakiwa na maofisa mbalimbali wa Tanzania  baada ya kuwasili New York, Marekani, Septemba 16, 2014.  PICHA NA IKULU

Changia mafunzo ya wakunga, okoa maisha ya mama na mtoto - Amref health africa

$
0
0
Mkurugenzi mkazi wa Amref Health Africa Dkt. Festus  Ilako akizungumzia maendeleo ya kampeni hiyo toka ilipozinduliwa mwaka 2011 na  uwatangaza mabalozi wapya wawili wa kampeni hiyo kuwa ni wasanii mashuhuri, Banana Zoro na Mwasiti Almasi 
 Nchini Tanzania, wanawake 7,900 hupoteza maisha kila mwaka wakati wa kujifungua. Zaidi ya asilimia 80 ya vifo hivi vingeweza kuepukika endapo wahudumu wa afya  wenye utaalamu wangetoa huduma kwa wakina mama wajawazito wakati wa kujifungua.  
Kwa kuamini kuwa hakuna mwanamke anayepaswa kufa wakati wa kujifungua, Shirika la Amref Health Africa Tanzania kwa kushirikiana na Bank za Barclays na Bank M leo wametangaza nia ya kuongeza nguvu na  juhudi za kutunisha mfuko wa kusaidia mafunzo ya wakunga kupitia kampeni yake ya Stand up for African Mothers.
 Kampeni hiyo ya kimataifa inalenga katika kuongeza uelewa juu ya   mchango unaotolewa na wakunga wenye ujuzi katika kupunguza vifo vya wajawazito wakati wa kujifungua na watoto wachanga. 
Kampeni hii pia inalenga kukusanya fedha kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wakunga 15,000 katika nchi 13 za Afrika,  kati yao wakunga 3800 wanatarajiwa kupata  mafunzo nchini Tanzania ifikapo mwaka 2015/2016. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Changia mafunzo ya wakunga , okoa maisha ya mama na mtoto” kwa kuunga mkono nia hii njema unasaidia kuwapatia mafunzo wahudumu wa afya walio mstari wa mbele kuokoa maisha ya mama na mtoto nchini Tanzania

Mmoja wa mabalozi wapya wawili wa kampeni hiyo Mwasiti Almasi akiongea na waandishi wa habari .
 Nchini Tanzania kampeni hii ilizinduliwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete tarehe 15Mei mwaka 2012. 
Mke wa Raisi amekuwa balozi wa kampeni hii akiongoza juhudi za kuwaokoa kina mama wa kiafrika. 
Tunayo furaha pia ya kuwatangaza wanamuziki wa kizazi kipya nchini Tanzania  Banana Zoro na Mwasiti Almasi ambao wamejitoa katika kushiriki na Amref Health Africa kuelimisha jamii  juu ya afya ya mama na mtoto kupitia kampeni hii ya Stand up for African Mothers.

Mpaka sasa, fedha zilichongishwa kupitia kampeni hii zimewezesha  kusomesha wakunga 80 kwa kiwango cha cheti; wakunga 10 wanatarajiwa kuhitimu mwezi wa 11 mwaka huu na 70 wanaingia mwaka wa pili wa mafunzo yao. 
Jumla ya wanafunzi 176 wanaongeza ujuzi kwa kupata mafunzo  ya ukunga   kwa njia ya masafa, ili kuongeza elimu kutoka kiwango cha cheti hadi diploma. 
Mafunzo hayo yanaendeshwa kati ka vituo kumi vilivyo katika mikoa ya Mbeya, Dodoma, Tanga, Kilimanjaro, Mwanza, Mara, Zanzibar and Mtwara. Na kiasi cha fedha kilichopatikana mwaka 2013 kinatarajia kusaidia wanafunzi 60 watakaoanza masomo yao mwezi wa 10 mwaka huu.


Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari mapema leo Mkurugenzi wa Amref Tanzania Dr. Festus Ilako alisema “Tunatoa mchango wetu katika kulisaidia Taifa kufikia malengo yake ya millennia (MDGs) yanayohusiana na afya kwa kuboresha huduma za afya na kuchangia katika kuboresha hali ya sasa ya afya ya uzazi. Mafunzo ya ukunga yatawaongezea ujuzi wakunga walioko na kufundisha wakunga zaidi ambao baada ya kuhitimu  watatoa huduma za afya ya uzazi  katika zahanati hivyo kuchangia katika kupunguza vifo vya kina mama vinavyoweza kuzuilika. Tunatoa rai kwenu kuunga mkono na kubadilisha maisha ya kina mama”


Tunawashukuru wadhamini wote walio pamoja nasi katika kufanikisha juhudi hizi. Bank M na Barclays bank  wamekuwa mstari wa mbele katika kusaidia mafunzo ya wakunga kuanzia mwaka 2013 mpaka sasa. Pia tunatambua mchango mkubwa uliotolewa na Benki ya Authetic Media Group, BG, Coca Cola Excel Management, FBME,KPMG,NBC, MICHUZI Blog, Mohan’s LTD, Jaffsher foundation LTD, Jamii forums, KCB bank, UCHUMI supermarket, IPP media, Push Mobile, , PWC, Pyramid Pharma, Southern Sun Hotel, Songas, SERENA Hotels, Serengeti Breweries, Stanbic Bank and TCRA. 
Ombi letu kwa mashirika, makampuni ya uma na yale ya binafsi, pamoja na watu binafsi ni kuunga mkono jitihada hizi kwa kudhamini mafunzo ya wakunga (mafunzo ya mkunga mmoja yanagharimu dola 3000). Unaweza kuchangia kwa njia mbali mbali, ikiwa ni pamoja na kupitia 
·         Account ya benki National Bank of Commerce (NBC), Corporate Branch, Akaunti Namba 0111030004548

·         Mpesa Namba 0762 22 33 48

·         Tigo pesa Namba 0716 032 441

·         Airtel money Namba 0685 506306.


Kuhusu Amref Health Africa.

Amref Health Africa ni Taasisi kongwe ya afya  ya  kimataifa  isiyo ya kiserikali , inayotoa mafunzo na  huduma za afya  kwa zaidi ya nchi 30  barani  Africa.   Shirika hili lilianzishwa mwaka 1957 kama “ AMREF flying Doctors”  kwa ajili ya kutoa huduma  muhimu za kiafya katika jamii iliyokuwa katika  maeneo magumu kufikiwa.  

Kwa sasa , Amref Health Africa  inatoa huduma nyingi za afya katika jamii na  hasa kwa kuzingatia  wanajamii wahitaji ambao wengi wanaishi katika maeneo magumu kufikika barani Afrika. 
Amref Health Africa imejikita  katika uimarishaji wa mifumo ya utoaji wa huduma za afya, mafunzo, mikakati ya utoaji wa huduma/miradi ya afya ya mama na mtoto, UKIMWI, kifua kikuu, malaria, maji safi na usafi wa mazingira,  huduma za madaktari bingwa na maabara.


Amref Health Africa inabaki kuwa  Taasisi ya mfano na   kuaminika  kimataifa kwa  kutoa huduma bora za afya  na endelevu kwa  miaka 57 toka kuanzishwa kwake.

WASHINDI WA TUZO ZA HABARI ZA TANAPA WATEMBELEA KIJIJI CHA UTALII WA UTAMADUNI AFRIKA KUSINI CHA LESEDI

$
0
0
Mshindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 Gerald Kitabu (The Guardian) akisalimiana na kijana wa Kizulu katika kijiji cha Utamaduni cha Lesedi walipotembelea ili kujifunza utalii wa kiutamaduni nchini Afrika Kusini.
Mshindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 Vedasto Msungu (ITV) akisalimiana na kijana wa Kizulu katika kijiji cha Utamaduni cha Lesedi walipotembelea ili kujifunza utalii wa kiutamaduni nchini Afrika Kusini.
Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 kutoka kulia Gerald Kitabu, David Rwenyagira na Vedasto Msungu wakifurahi pamoja na wanakijiji cha Wazulu cha Lesedi walipowatembelea ili kujifunza utamaduni wao.
Mshindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 David Rwenyagira (Radio Five) akishika ngao kwa ajili ya kujikinga na adui ambao ni mojawapo ya utamaduni wa Wazulu.
Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 wakiendelea kupata somo juu ya tamaduni mbalimbali zinaopatikana nchini Afrika Kusini.
Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Kituo cha Utamaduni cha Lesedi, Afrika Kusini.
Lugha ya Kiswahili nayo yafahamika vema Afrika Kusini kama inavyoonekana hapa katika picha iliyopigwa na Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013.

MSTAHIKI MEYA WA ILALA JERRY SILAA ASHUSHA NEEMA KWA SHULE YA MSINGI KIVULE

$
0
0
Meya wa manispaa ya Ilala Jerry silaa akabidhi msaada wa madawati mia moja katika shule ya msingi kivule iliyopo jijini dar es salaam ikiwa ni mpango aliouanzisha na kuanza kuutekeleza kupitia (meya boll) katika mpango huo madawati hayo yamekabidhiwa kwa mwalimu mkuu wa shue hiyo pamoja na diwani wa kata ya kivule na afisa elimu wa manispaa ya ilala walikuwepo katika shuguli hiyo ya kupokea msaada huo Jana
 Meya wa Ilala Mstahiki Jerry Silaa akizungumza mara baada ya kupokea risala iliyo somwa na Mkuu wa shule ya kivule
 Mh.Akifurahi na wanafunzi wa shule hiyo ambapo walikuwa na furaha wa kupokea msaada huo
 Mstahiki Jerry Silaa meya wa Ilala akimkabidhi msaada huo wa madawati mia moja (100) mwalimu mkuu wa shule ya msingi kivule.

BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI KAMILI

Mwenyekiti wa Shirika la Nyumba Serikali ya Dubai afanya ziara nchini

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya akisalimiana na Mkurugenzi wa Nyumba kutoka Dubai Mhe. Ali Rashid Ahmed Lootah walipokutana kwa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Kampuni inayojishughulisha na masuala ya Nyumba ya OYO. Bw. Lootah yupo nchini kwa ziara ya siku mbili ya kuangalia fursa za uwekezaji katika Sekta ya Nyumba na Makazi.
Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai Bw. Omar Mjenga (katikati) akimtambulisha Mhe. Lootah (wa kwanza kulia) kwa Mkurugenzi wa IPP Media Bw. Reginald Mengi walipokutana katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam
Bw. Mjenga (wa kwanza kulia) akimtambulisha Bw. Harbert Marwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya OYO kwa Mhe. Ali Rashid Ahmed Lootah mara baada ya kuwasili nchini. 
Bw. Mjenga akiwa na mmoja wa wajumbe waliofutana na Mhe. Lootah wakati wa chakula cha jioni kwa wageni hao katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

HAPPY BESDEI MDAU FATHER KIDEVU!!

$
0
0
LEO ni siku ya kuzaliwa ya mpiganaji Mroki Mroki 'Father Kidevu' ambapo leo anaadhimisha miaka kadhaa hapa duniani. Anasema Sifa na Utukufu anazirudisha kwa Mungu maana yeye ndie ajauae sababu ya kumuacha hadi hii leo na hakuna alicho mpa. Pia anashukuru wazazi hasa mama yake, familia yake ikiongozwa na mkewe pamoja na watoto wao. 

"Ndugu zangu mbali na hao niliowataja hapo juu, lakini ninyi marafiki zangu, Wadau wangu, ndugu na jamaa wote popote pale mlipo hapa duniani ni watu muhimu sana sana, hadi kufika hapa leo ninyi mnachango wenu wa namna moja au nyingine. Sina la zaidi ya kusema Asanteni sana na Mungu awazidishie na tukazidi kuishi kwa amani na Upendo."

HAPPY BIRTHDAY FATHER KIDEVU!! HAPPY BIRTHDAY MROKI MROKI!!

WAZIRI CHIZA ATEMBELEA SOKO LA MAHINDI NFRA DODOMA

$
0
0
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika,Mhe. Eng Christopher Chiza (Mb) akijibu kero za wakulima na wafanyabiashara waliopeleka mahindi NFRA Dodoma kwa ajili ya kuyauza,Wakati alipowatembelea jana.
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika,Mhe. Eng Christopher Chiza akionyesha uchafu uliokuwa kwenye magunia ya mahindi yaliyopelekwa na wakulima na wafanyabiashara NFRA Dodoma kwa ajili ya kuyauza.
Mahindi yaliyonunuliwa na kituo cha NFRA Dodoma yakipangwa nje kitaalamu kwa ajili ya kuhifadhiwa.

MWENYEKITI WA CHADEMA,FREEMAN MBOWE AFIKA MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI KWA MAHOJIANO LEO

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe akiwasili kwenye makao makuu ya Jeshi la Polisi nchini,Mapema leo asubuhi tayari kwa kwenda kuhojiwa juu kauli aliyoitoa kwenye Mkutano Mkuu wa chama hicho hivi karibuni,kuwa watafanya maandamano nchini nzima bila kikomo.
 Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),John Mnyika akizungumza na waandishi wa habari waliokuwepo kwenye eneo la makao makuu ya Jeshi la Polisi,juu ya kile kilichokuwa kikiendelea kwenye mahojiani kati ya Mwenyekiti wa Chama hicho na Jeshi la Polisi.Picha na Othman Michuzi.
 Makamu Mwenyekiti wa Chadema,Prof. Abdallah Safari na Wakili wa Chama,Wakili Mabele Marando wakiwasili kwenye Makao Makuu wa Jeshi la Polisi mapema leo.
 Baadhi ya Wachama na Wafuafi wa Chadema wakishangilia wakati Mwenyekiti wao akiwasili kwenye Makao Makuu ya Jeshi la Palisi leo.

Kamishna wa Polisi,CP Paul Chagonja akiwataka wanachana na wafuasi wa Chadema kuondoka eneo hilo kwani hakuna sababu ya kufanya fujo.
 Ulinzi mlali katika eneo hilo.

SERIKALI, MAKAMPUNI YA MADINI ‘KUWANOA’ WAZAWA KATIKA USHIRIKISHWAJI SEKTA YA MADINI

$
0
0
Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje akiwakaribisha wajumbe wa mkutano wa kujadili ushirikishwaji wazawa (local content) katika sekta ya madini uliofanyika jijini Mwanza hivi karibuni. Waliokaa meza kuu kutoka kushoto ni Kamishna Msaidizi Kitengo cha Uchumi na Biashara, Salim Salim, Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Ndalo Kulwijila na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, John Henjewele.
Mwanasheria wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Rose Mponguliana akiwasilisha mada kuhusu uwajibikaji wa Shirika hilo katika suala la ushirikishwaji wazawa wakati wa mkutano baina ya Serikali na Makampuni ya Madini uliofanyika hivi karibuni jijini Mwanza.
Wajumbe wa Mkutano baina ya Serikali na Makampuni ya Madini uliojadili ushirikishwaji wazawa katika sekta ya madini wakisikiliza hotuba ya Mgeni Rasmi, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Ndalo Kulwijila (hayupo pichani).
Wajumbe wa Mkutano baina ya Serikali na Makampuni ya Madini uliojadili ushirikishwaji wazawa katika sekta ya madini wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo katika Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza hivi karibuni. Kutoka Kushoto waliokaa ni Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Sehemu ya Uongezaji Thamani Madini Latifa Mtoro, Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje, Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndalo Kulwijila na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, John Henjewele.

Training on intervention techniques for Maritime Police and Crime Investigation Officers in Zanzibar ends today

$
0
0
September 17th, marked the end of a police training course provided by EUCAP Nestor held at Zanzibar’s Police Academy. This week long training course was an opportunity for Tanzanian Maritime Police and Crime Investigation Officers to learn from EUCAP Nestor’s trainers on a wide range of activities with a focus on maritime intervention security techniques, police practices and boarding intervention. The courses were designed to develop existing skills and progress students to the next level.

They were combined with new techniques and scenarios such as ‘empty hands’ defensive techniques. It was the first time for the participants to be actually trained in a maritime environment, using their own boats. Another aim of the course was to provide techniques to increase the security of the officers whilst on duty and to minimize the potential impact of their actions on the population and environment.
“The goal of this course was to enhance the individual capacity of our Tanzanian counterparts, who clearly demonstrated their high level of professionalism and determination in fighting maritime crimes in the region” said Dag Hjulstad, the EUCAP Nestor training coordinator. “The trainees were so enthusiastic that they even requested an additional 2 hours of training which the training team was happy to deliver.”

At the closing ceremony, Eisso Kronenberg, EUCAP Nestor’s Head of Country Office Tanzania, said “The police college was so cooperative, we did not have to worry about anything. All logistical issues were solved in no time.”

The closing ceremony was attended by several dignitaries from Tanzania and Zanzibar, amongst them the Chief of Maritime Police of Zanzibar, Chief Superintendent Martin Mpembe, Director of Criminal Investigation Salum Msangi, the Director of the Zanzibar Police College and other ranking Police officers.
As part of the European Union’s comprehensive approach to secure the waters in the region, the strengthening of Maritime security and therefore Tanzania Maritime Police plays a vital role in combating piracy and other maritime crimes in the region.

EUCAP Nestor is a civilian EU mission, under the Common Security and Defence Policy, that assists host countries in the Horn of Africa and Western Indian Ocean region to develop a self- sustainable capacity for enhancement of the maritime security, including counter-piracy and maritime governance.

TAMASHA LA UTALII NA MIAKA 4 YA BLOG YA VIJIMAMBO

$
0
0
Mhe. Lazoro Nyalandu Waziri wa Maliasili na Utalii akiingia ukumbini huku akiongozana na Mhe. Liberata Mulamula, Balozi wa Tanzania nchini Marekani kushoto ni Luke Joe ambaye ni mwendeshaji wa Blog ya Vijimambo siku ya Jumamosi Sept 13, 2014 katika ukumbi wa Crowne Plaza iliyopo Rockville, Maryland nchini Marekani.
Mhe. Lazaro Nyalandu ambaye ndiye aliyekua mkeni rasmi akifurahi jambo siku ya Tamasha la Utalii na miaka 4 ya Blog ya Vijimambo kulia ni Luke Joe mwendeshaji wa Blog ya Vijimambo.
Kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu na Luke Joe wakibadilishana mawili matatu siku ya Tamasha la Utalii na miaka 4 ya Blog ya Vijimambo iliyofanyika Jumamosi Sept 13, 2014 Rockville, Maryland nchini Marekani.
Mhe. Lazaro Nyalandu, Mhe. Liberata Mulamula na Luke Joe wakipitia vibanda vya wajasiliamali mara na kuangalia kazi zao wazifanyazo.
Mhe. Lazaro Nyalandu akiongozana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Luke Joe wakipitia vibanda vya wajasilia mali mara tu Waziri wa Maliasili na Utalii alipoingia kwenye Tamasha la Utalii na miaka 4 ya Blog ya Vijimambo.Picha zote na Iska Jojo
Kwa picha zaidi bofya HAPA

Big Brother Hotshots revealed

$
0
0
Fans of Africa’s biggest reality show, Big Brother Africa, will no longer have to wait in anticipation until the launch on the 5th of October to meet the Big Brother Hotshots. 

In a bold and ground breaking move, M-Net and series producers Endemol SA will be delivering a new world first by unveiling the names of the participating housemates live on the official Big Brother website which launches at 14h00 CAT on  Wednesday 17 September.

Three Big Brother housemates will be introduced on a daily basis starting from the 18th September. This will be followed by regular updates on social media.

During the 8th season of Big Brother, over 6 million fans interacted with the show via the Website, Twitter, and Facebook, with the website generating just over 200 million impressions. 

“We are breaking new ground and the website and social media are the perfect platforms to engage with the fans in real-time”, says M-Net Africa Regional Director (West Africa) Wangi Mba-Uzoukwu. “The show will go on, and both fans and housemates are in for some riveting television, coupled with all the drama, intrigue and heart-stopping twists that have long become synonymous with the reality show”. 

The new and undoubtedly glamourous Big Brother house is in the process of being designed and fitted with cutting edge camera equipment and broadcast technology that makes the show unique in its format. 

Catch the live eviction shows as well as the best of the live daily and weekly highlights on Africa Magic Family, and Africa Magic World on GOtv

Follow the action leading up to the premiere night on social media by visiting the official Big Brother website at www.bigbrotherafrica.com from 14h00 on the 18 September, liking facebook.com/BigBrotherAfrica and follow @BigBroAfrica

Mwandishi chipukizi kutoka Zanzibar aja na ‘Paka wa Binti Hatibu’

$
0
0
Na Ali Othman Ali.

Mwandishi anayechipukia kwa kasi katika tasnia ya fasihi ya Kiswahili ambaye pia ni Mhadhiri wa Kiswahili katika Chuo Kikuu Cha London, SOAS na Cambridge nchini Uingereza, Bwana Yussuf Shoka Hamad, hivi karibuni anatarajia kutoa kitabu chake kipya na cha kwanza kuchapishwa kinachoitwa; ‘Paka wa Binti Hatibu na Hadithi Nyingine’.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii kwa simu kutoka nyumbani kwake jijini London, Bwana Yussuf alisema; ‘ Msomi kama binadamu hufa, huzikwa na husahaulika kama watu wengine wengi. Lakini msomi kama mwanataaluma na mwandishi hafi, hazikwi, na wala hawezi kusahaulika kwani mawazo, fikra na falsafa zake hubakia katika maandishi anayoyaacha. Na maaandishi hayo huwa ukumbusho na urithi auachiyao jamii yake milele na milele.’

Bwana Yussuf pia alifafanua kwa upana kwanini ameamua kuandika kitabu chake kwa kutumia lugha ya Kiswahili kwa kusema kwamba hadithi zilizomo humo zinawalenga waswahili wenyewe na sio watu wa jamii nyengine. Kwa hivyo, sambamba na kukuza na kukitangaza Kiswahili kimataifa, kitabu hicho kitatumika kuufiskisha ujumbe uliokusudiwa kwa jamii kwa urahisi na kwa wepesi kwani lugha iliyotumika ni nyepesi na yenye kufahamika kwa walengwa.

Alipoulizwa kwanini alichagua kukipa kitabu chake hicho jina la ‘Paka wa Bini Hatibu’ mwandishi alisema; ‘ Paka wa Binti Hatibu ni usemi uliozoeleka na wengi. Ingawa kufahamika kwake kimaana na kimantiki kumekuwa kukileta mashaka yatokanayo na bezo, kebehi na dharau, usemi huu unabaki kuwa na maana pana, tena zaidi ya ile iliyozoeleka kimazowea ya kuukamilisha usemi wenyewe. Jina la Paka wa Binti Hatibu, halimmuliki paka kama paka peke yake na Binti Hatibu kama tumjuavyo, bali kinaimuilika jamii yote na wanajamii, wote kwa ujumla.’

Akitoa ufafanuzi kuhusu kitabu chake hicho ambacho utangulizi wake umeandikwa na Mhadhiri wa masomo ya Fasihi wa Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA) Bi Asha Khamis Hamad, mwandishi huyo alisema kitabu chake kina hadithi saba na kila hadithi kama kawaida yake ina ncha nyengine saba zinazoimulika jamii kwa undani na kwa kina kipevu cha udadisi na upekuzi. Kila hadithi imebeba mikasa, vitimbi na viteweji kedekede ambavyo kwa ujumla hutoa ujumbe na kuleta ladha ya ucheshi usio kikomo.

Akijibu suala la vipi na wapi aliuota ujuzi huo wa uandishi, mwandishi alisema kuwa. Amekuwa akisoma kazi mbali mbali za waandishi, na pia ametembea sana na kusikia mengi kutoka kwa magwiji wa simulizi na uandishi wakiwemo waandishi nguli katika fasihi ya Kiswahili kama vile Professa Said Ahmed, Farouk Topan na Ali Mwalimu Rashid ambao kwa pamoja walimpa moyo na ari ya kuandika.

Kitabu cha Paka wa Binti hatibu kinachapishwa na ‘The Jomo Kenyatta Foundation’ ya Nairobi nchini Kenya na kitatumika kama kitabu cha kiada katika masomo ya Fasihi katika chuo kikuu cha London, SOAS nchini Uingereza mara tu baada ya kutoka hivi karibuni.

Mbali na kitabu hiki, mwandishi huyu pia amekamilisha miswada mengine minne ya riwaya na Hadithi fupi zinazosubiri kuchapishwa. Mwandihi hivi sasa anaandika vitabu vya kitaaluma vya kufundishia Kiswahili shuleni na vitabu vitokanavyo na utafiti wa mambo mbali mbali yahusuyo jamii na utamaduni wa watu wa Pemba. Moja ya muswada wa kitabu kitokanacho na utafiti wake ni kile cha ‘Watu 40 Mashuhuri kutoka Pemba’ ambacho utafiti wake unaendelea hivi sasa.

Mwandishi Yussuf Shoka Hamad (kulia) akiwa na Professa Said Ahmed Muhamed alipomtembelea nyumbani kwake Limbani Wete hivi karibuni.

Tume kujumuika na Wadau kulaani mauaji dhidi ya watu wenye Ualbino

$
0
0
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kushirikiana na Chama cha Albino Tanzania (TAS), Under The Same Sun (UTSS) Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu ( SHIVYAWATA), taasisi za kiraia na wadau wengine wameandaa maandamano ya amani sanjari na maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani Duniani (International Day of Peace) yatakayofanyika Jumapili Septemba 21,2014 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Kauli Mbiu ya maadhimisho haya ya kitaifa ni “Haki ya Amani kwa wote: Komesha Ukatili na Mauaji Dhidi ya Watu Wenye Ualbino.”

Lengo la maadhimosho haya ya amani ni kulaani vikali vitendo vya ukatili na mauaji dhidi ya watu wenye ualbino na kuhamasisha wadau mbalimbali ikiwemo Serikali, jamii, na jumuiya za kimataifa kuchukua hatua kukomesha vitendo hivyo.

Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye atawakilishwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii. Wadau mbalimbali wanatarajiwa kushiriki ikiwemo Serikali, asasi za kiraia, taasisi za dini, vyama vya siasa na jumuiya za kimataifa.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bibi Mary Massay akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo uliofanyika leo katika ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam ,Kushoto kwake ni Bibi Ziada Ally Nsembo, Katibu Mkuu wa Chama cha Albino Tanzania.
Bibi Ziada Ally Nsembo( katikati) Katibu Mkuu wa Chama cha Albino Tanzania akiongea na waandishi wa habari, kulia kwake ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bibi Mary Massay na kushoto kwake ni Afisa kutoka Under The Same Sun (UTSS).
Meneja uendeshaji wa Under The Same Sun (UTSS), Bwana Gamariel Mboya akitoa maelezo mbele ya waandishi wa habari katika mkutano na waandishi hao uliofanyika leo katika Ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bibi Mary Massay, na Bibi Ziada Ally Nsembo, Katibu Mkuu wa Chama cha Albino Tanzania.
Sehemu ya waandishi wa habari na wadau wengine waliohudhuria mkutano huo.

WAKALA WA AJIRA TANZANIA WAELEZA MIKAKATI YAO YA KUWASAIDIA VIJANA WANAOKUBWA NA JANGA LA KUKOSA AJIRA

$
0
0
Afisa Habari wa Wakala wa Ajira Tanzania (TaESA) Jamilah Mbarouk akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuelezea mkakati wao wa kuanzisha mafunzo ili kuweza kuwasaidia vijana wahitimu ili wakabiliane na soko la ajira, Wakala umekuwa ukitoa mafunzo ya namna ya kushindania fursa za ajira. Mafunzo haya yamevutia watafutakazi wengi ambao tayari wako sokoni na walioko vyuoni. Aidha mafunzo haya yamewabadilisha vijana wengi waliohudhuria kuhusu suala zima la kuajiriwa na kujiajiri na kupelekea uhitaji wa mafunzo haya kuongezeka. Pembeni yake Afisa Utawala, Peter Ugata.

kumbukumbu

$
0
0
Mama Fortunata Joseph Msoka. Hatimaye leo umetimiza mwaka mmoja tangu ulipotuacha Watoto wako, Wadogo zako, Shemeji, Wifi, Wajukuu zako, Wakwe zako, Wanajumuia wenzako na majirani zako kwa majonzi makubwa yasiyoelezeka.

Lakini Tunaamini kwamba yote ni mapenzi ya Mungu aliyekupenda zaidi. Ibada ya kumwombea itafanyika Jumapili 21/09/2014 Kanisa Katoliki la Mt. Augustino Ukonga saa 2:30 Asubuhi.

Kwa hakika pengo lako halizibiki. Unakumbukwa na watoto wako wapendwa Paul Msoka, Rose Mdami, Constantine Msoka, Jackline Msoka,Wajukuu zako, kaka zako, wadogo zako, shemeji zako, wifi zako, wakwe wako, WAWATA Ukonga, Jumuia yako na Parokia yako penzi ya Mt. Augustino Ukonga.

Tunafarijika sana na Zaburi ya 147 na Zab 148 inayotutaka kumsifu, kumwabudu, na Kumshukuru Mungu daima kwa ajili yako. “Mungu akulaze mahali pema mbinguni, Upumzike kwa Amani. Amina”

RENATUS MALULU NA IMERESIANA CHARLES WAMEREMETA

$
0
0
Bwana harusi Renatus Malulu akimvisha pete ya ndoa mkewe Imeresiana Charles wakati wa ibada ya ndoa yao iliyofanyika katika kanisa katoliki la Mtakatifu Mashahidi wa Uganda la Magomeni jijini Dar es Salaam, na kufuatiwa na sherehe kubwa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Msimbazi center.
Wakiwa na nyuso za furaha bwana harusi Renatus Malulu na mkewe Imeresiana Charles wakiwa kwenye pozi la picha baada ya kufunga pingu za maisha katika kanisa la Mtakatifu Mashahidi wa Uganda la Magomeni jijini Dar es Salaam, nakufuatiwa na sherehe kubwa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Msimbazi center.
Renetus Malulu na Imeresiana Charles wakinyweshana shampeni wakati wa sherehe yao ya ndoa iliyofungwa katika kanisa katoliki la Mtakatifu Mashahidi wa Uganda la Magomeni jijini Dar es Salaam, nakufuatiwa na sherehe kubwa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Msimbazi center.
Bwana harusi Renatus Malulu na Mkewe Imeresiana Charles wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufunga ndoa yao katika kanisa katoliki la Mtakatifu Mashahidi wa Uganda la Magomeni jijini Dar es Salaam, nakufuatiwa na sherehe kubwa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Msimbazi center.

CHAMA CHA WANASHERIA TANZANIA CHAIOMBA MAHAKAMA KUU KUWARUHUSU KUFUNGUA MAOMBI YENYE MWELEKEO WA KUPINGA BUNGE LA KATIBA

$
0
0
Na Mwene Said wa Blogu ya Jamii

CHAMA cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) kimeiomba Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam kuwaruhusu kufungua maombi yenye mwelekeo wa kupinga mwenendo wa Bunge Maalum la Katiba unavyoendelea mjini Dodoma.

Wakili wa TLS Mpale Mpoki alilieleza jopo la majaji watatu linalioongozwa na Mwenyekiti Jaji Augustine Mwarija akisaidiana na Aloysius Mujulizi na Fauz Twaib kuwa kuna mambo kadhaa yanayobishaniwa ambayo yanahitaji Mahakama hiyo kuingilia na kutolea ufafanuzi.

Wakili Mpoki anayesaidiwa na wakili Fulgence Massawe, alieleza kuwa kwa kuangalia nyaraka mbalimbali walizowasilisha mahakamani hapana shaka kuwa mwenendo wa Bunge la Katiba unaovyoendelea hivi sasa unahitaji kutazamwa.

“Katika kutenda haki, haitapendeza mwananchi ambaye anaona haki zake zinaporwa azuiliwe kufungua malalamiko yake mahakamani. Hivyo itakuwa ni haki kama mahakama hii itaruhusu maombi yetu ili tuweze kuwasilisha kesi ambayo inakusudiwa,” wakili huyo alisema.

Hata hivyo, naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju anayesaidiwa na mawakili wa serikali Gabriel Malata na Sylvia Matiku, aliiomba mahakama kutupilia mbali maombi hayo kwa vile hayana msingi.

Masaju alipinga uhalali wa maombi hayo kuwasilishwa kwa vile Mahakama Kuu haina mamlaka kwa sababu sheria ambayo inabishaniwa inahusu serikali toka pande mbili za muungano, yaani serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

“Ukiangalia kwa makini nyaraka zilizowalishwa zinaonyesha uwepo wa serikali mbili. Lakini sheria ambayo mwombaji ameitumia inatumika Tanzania bara tu,” alisema.

Masaju aliongeza kuwa katika shauri lililopo Serikali ya Zanzibar haijaunganishwa na hivyo kama mahakama itatoa amri itakayoiathiri kutatoke nini. “Hii inaweza kusababisha mgogoro wa kikatiba,” alibainisha.

Mara baada ya kusikiliza pande zote mbili, majaji hao walisema kuwa watatoa uamuzi wa juu ya maombi hayo Jumatatu ijayo.

Baraza la ushindani: Tutumieni kwa manufaa ya Taifa na ustawi wa uchumi nchini

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Masuala ya Uchumi wa Baraza la Ushindani (FCT) Bw. Nzinyangwa Mchany akiwaeleza waandishi wa Habari (Hawapo pichani)Kuhusu majukumu ya Baraza hilo na kutoa wito kwa wananchi kulitumia baraza hilo pale itakapohitajika kwa madhumuni ya ustawi wa uchumi wa Jamii na Taifa kwa ujumla.wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Sheria wa Baraza hilo Bi. Hafsa Said. Hassan Silayo MAELEZO.

Na Hassan Silayo-MAELEZO

Baraza la ushindani limewataka wananchi kulitumia Baraza hili kwa manufaa ya Taifa na ustawi wa uchumi nchini.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Masuala ya Uchumi Nzinyangwa Mchany wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. “Baraza la ushindani lipo kwa ajili ya watu wote hivyo wananchi hawana budi kulitumia kwa manufaa ya Taifa”. Alisema Nzinyangwa.

Aidha, Nzinyangwa alisema kuwa baraza la ushindani ni chombo maalum cha rufaa za maamuzi au amri za Tume ya Ushindani na mamlaka za udhibiti kwenye sekta za Miundombinu,huduma za maji na nishati.

Pia alisema kuwa kesi zinazosikilizwa kwenye baraza zinahakikisha uzingatiaji wa misingi ya udhibiti ili kuleta umakini katika kusimamia sekta husika na ushindani wa haki sokoni.

Akizungumzia kuhusu rufaa zilizowahi kusikilizwa na baraza hilo Nzinyangwa alisema kuwa rufaa zinazosikilizwa na baraza la Ushindani zimegawanyika katika makundi manne.

Akizitaja rufaa hizo Nzinyangwa alisema ni rufaa kati ya mtoa huduma na mlaji, hii ni pale mlaji anapopewa huduma mbovu au hafifu kwenye sekta inayosimamiwa na mdhibiti kama maji, simu, nishati ya umeme pamoja na bidhaa za mafuta ya nishati.

Pia kuna aina ya rufaa kati ya wauzaji wawili wa bidhaa ya aina moja ama mbadala wake kama kampuni za usafirisha au kampuni za simu ambapo shauri hili litapelekwa kwa mdhibiti wa sekta husika na iwapo upande mmoja hautaridhika na uamuzi unahaki ya kuombea rufaa uamuzi huo kwenye baraza la ushindani.

Akiendelea kutaja Rufaa hizo Nzinyangwa alisema kuwa pia ipo rufaa kati ya mtoa huduma na mdhibiti wa sekta na hii ni pale mdhibiti wa sekta anapoandaa utaratibu wa kudhibiti sekta na ikiwa mdau anaona utaratibu huo hautoshelezi au haukufuata sheria mdau ana haki ya kuwasilisha malalamiko kwenye chombo kilichotoa uamuzi huo.

Pia mdau wa soko anaweza kukata rufaa kwenye Baraza la ushindani ikiwa tume ya ushindani imetoa amri kwenye soko au kutunga kanuni Fulani juu ya utaratibu kuhusu usimamizi wa ushindani kwenye soko ambao mdau anaona uamuzi huo haukuwa sawa.

Tume ya ushindani ina jukumu la kukataza uzalishaji na uuzaji wa bidhaa bandia sokoni,katika jukumu hilo maamuzi hayo yanaweza kukatiwa rufaa na mdau kwenye Baraza la Ushindani
Viewing all 109984 articles
Browse latest View live




Latest Images