Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

Mdahalo wa Pili wa Wagombea Urais Nchini Kenya


KUMBUKUMBU

$
0
0
ROSE KAPYA MWAILENGE

Ilikuwa saa 11.00 jioni, siku kama ya leo tarehe 27 February, 2006 ulipotutoka. Wakati bado tulikuhitaji sana, tulidhani ni ndoto tu.Japo sote tuliamini kuwa siku moja ungeamka ukiwa mzima.Mama,japo leo ni miaka saba tangu ututoke,bado tunahisi tuko ndotoni na tumeshindwa kabisa kukubaliana na ukweli kwamba haupo nasi. Mara kwa mara nakuona ndotoni, lakini ninapoamka nagundua ni ndoto tu,na hiyo inazidisha uchungu na majonzi.

Japo siku zote tangu ututoke tumekuwa na wakati mgumu sana ,siku hii ya leo tunapoadhimisha miaka saba ya kifo chako ni ngumu zaidi kwetu.Inaleta kumbukumbu zisizoelezeka na zisizostahimilika.
  
Kazi ya Mungu haina makosa.Tukijiuliza sana kwanini alikuchukua wakati bado tunakuhitaji sana tutakuwa tunakufuru.Tunajaribu kujifariji kwa kuamini kuwa alikuchukua kwa vile alikupenda zaidi yetu.Na tunajitahidi pia kujiridhisha kuwa huko ulipo unapata pumziko la amani na unaangaziwa mwanga wa milele ukistarehe kwa amani.Japo haupo nasi kimwili lakini siku zote tupo nawe kiroho

Unakumbukwa sana na watoto wako wapendwa Bupe, Lilian na Shirima, Fred na Furaha bila kuwasahau wajukuu zako Irene-Kanyampa, Aziz-Elian, Rose, Junior-Ereneus na Katarina.


Pumziko la Milele Akupe Ee Bwana na Mwanga wa Milele Akuangazie Ustarehe Kwa Amani,  AMEN

Ngoma azipendazo ankal

cheka unenepe...

maisha ni safari ndefu

$
0
0
 Mdau Said Yakub  ana urefu wa futi 6 na inchi 2. Lakini alionekana si lolote alipokutana na jamaa huyu toka Pakistan mwenye urefu wa futi nane mjini Dubai. Yeye anajipatia riziki kwa urefu wake maana ukitaka kupiga naye picha lazima zikutoke dola 3 za kimarekani. Na jinsi inavyoonekana huwa halali njaa....

LIBENEKE LA CHADEMA UK LIPO HEWANI

$
0
0

Timu inayolisuka tawi la Chadema UK imekuwa ikifanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kwamba uongozi utakaochaguliwa una vitendea kazi vya kisasa ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi. Kwa hali hiyo basi tungependa kuitangaza rasmi website ya Chadema UK :

Pia kwa kuzingatia kwamba dunia ya sasa mawasiliano ya jamii ni kupitia njia mbalimbali za kiteknolojia, tunawatangazia wanaChadema UK wote kuwa sasa Chadema inapatikana facebook:

Jina: Chadema UK

Umuhimu wa mawasiliano kwa njia ya simu pia nao umepewa kipaumbele. Hata hivyo tunadhamiria kuhakisha mawasiliano hayo hayamgharimu mwanachadema. Kwa hivyo tunashughulikia kupata mobile phone yenye free text messages and calls applications (Viber, Whatsapp na Tango). Hii itarahisisha namna tunavyowasiliana na wapenda maendeleo.

Mambo yote haya yanafanyika ili kuongeza ufanisi lakini pia ni katika kuhakikisha kwamba Chadema iko karibu sana na wanachadema na watanzania wote kwa ujumla.

Hatutalala mpaka kieleweke!

People’ssss Power

TANGAZO LA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA TAWI LA CCM DMV

$
0
0

Email address:ccmwashdc@gmail.com


Ndugu Wana CCM DMV mnaombwa kuhudhuria mkutano wa uchaguzi bila kukosa,
 Ni nafasi ya kuwachagua viongozi wako utakao wapenda kujenga Chama imara.

SIKU: JUMAMOSI Machi 16, 2013

MUDA:  SAA 10 JIONI (4pm)

MAHALI: TUTAWATANGAZIA

 Ili uweze kupiga kura hakikisha una kadi yako ya Chama na uwe mwanachama hai, na kama huna kadi au umepoteza tafadhali wasiliana na Katibu wa Tawi wa muda

Yacob Kinyemi, Simu (202)-629-7841, email: yacob1972@yahoo.com


Nafasi zinazowaniwa ni:

1) Mwenyekiti wa tawi

2) Katibu wa Tawi

3) Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wa Tawi

4) Katibu wa Fedha na Uchumi wa tawi

5) Mwenyekiti wa Vijana wa Tawi (UVCCM)

6) Katibu wa Vijana wa Tawi (UVCCM)

7) Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake (UWT)

8) Katibu wa Jumuiya ya Wanawake ya Tawi (UWT)

9) Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Tawi

10) Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya Tawi


SIFA ZA MGOMBEA:

1.      Awe na umri kuanzia miaka 18

2.      Awe mwachama wa CCM mwenye kadi

Fomu za kugombania nafasi za uchaguzi ziwakilishwe kwa M/Kiti ( HIDAYA MAHITA)wa Kamati ya Uchaguzi kwa njia ifuatayo:

Fax: 1(888)835-5784     Email: ccmwashdc@gmail.com

Mailing address: 1709 HAMPSHIRE GREEN LANE#33 SILVER SPRING MD 20903

  
MWISHO WA KUCHUKUA NA KURUDISHA FOMU HIZO NI  TAREHE 8 MARCH 2013


MSD YAWEKA WAZI WANAOWALINDA WANAOTOROSHA DAWA NJE YA NCHI

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani akielezea kuhusu utendaji wa bohari hiyo pamoja na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo, zikiwemo za vyombo vya dola kuwafumbia macho baadhi ya wafanyabiashara wanaouza dawa za serikali kiholela pamoja na wanaokamatwa kwa kutorosha dawa hizo nje ya nchi. Taasisi zilizomwagiwa lawama hizo ni baadhi ya maofisa kutoka vyombo vya dola, serikalini na wafanyabiashara. Mwaifwani alidokeza hayo wakati wa Kongamano la Nane la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) la kujadili tafiti zilizofanywa na wanahabari kuhusu matumizi ya fedha zinazochangwa na wananchi kwa ajili ya masuala ya afya katika halmashauri 26 nchini.
 Meneja wa Ufuatliaji wa Mipango Kazi na Mpango Mkakati wa Bohari ya Dawa (MSD),  Cosmas Nalimi akielezea jinsi MSD ilivyojidhatiti kuboresha huduma nchini, wakati wa Kongamano la Nane la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) la kujadili tafiti zilizofanywa na wanahabari kuhusu matumizi ya fedha zinazochangwa na wananchi kwa ajli ya masuala ya afya katika halmashauri 26 nchini. Kongamano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki mjini Mtwara. Baadhi ya dawa za msd inadaiwa zinauzwa nje ya nchi ikiwemo Cameroon.
Msajili wa Baraza la Pharmacy Tanzania, Dk. Midred Kinyara, akielezea mikakati ya usajili wa maduka ya dawa  baridi vijijini wakati wa kongamano hilo.

Tanzania yasaini bil 90/- za maji ili kupanua Miundombinu ya Maji katika Miji mbalimbali nchini

$
0
0
Wizara ya Maji imesaini mikataba ya upanuzi wa miradi ya maji katika mikoa ya Kigoma, Lindi na Halmashauri ya mji wa Sumbawanga ,makubaliano hayo yaliyofanywa kati ya wizara na Wakandarasi watano.

Akisaini mikataba hiyo jana Makao Makuu ya Wizara Ubungo , Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Chistopher Sayi aliwataka wakandarasi hao kutekeleza miradi hiyo kwa wakati kama mikataba inavyoeleza.

“Natumia nafasi hii kupongeza wakandarasi wote walioshinda zabuni za kutekeleza miradi hii, lakini pia ni mategemeo yangu miradi yote itafanywa kwa wakati kama ambavyo tumekubaliana katika mikataba hii”. Alisema Mhandisi Sayi.


Wakandarasi waliopata fursa ya kutekeleza ujenzi wa miradi hiyo ni Spencon Services Ltd ambao watahusika na usambazaji na mifumo ya majisafi mkoani Kigoma; Jandu Plumbers na Metito Overseas watahusika na uchimbaji wa visima katika Halmashauri ya mji wa Sumbawanga. 


 Jandu Plumbers na Metito Overseas watahusika na uchimbaji wa visima mkoani Lindi na Technofab-Gammon Joint usambazaji na mifumo ya majisafi katika Halmashauri ya mji wa Sumbawanga, na Overseas Infrastructure Alliance watahusika na usambazaji wa maji na mifumo ya majisafi mkoani Lindi.

Miradi hiyo ambayo itagharimu takriban shilingi bilioni 90 za kitanzania ambayo imefadhiliwa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya Serikali ya Ujerumani.

WAFANYAKAZI WA AIRTEL WATOA MSAADA KWA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUMU SHULE YA MSINGI MSASANI

$
0
0
Msimamizi wa miradi kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Mubaraka Kibarabara akimkabithi mwalimu mkuu wa kitengo cha watoto wenye mahitaji maalumu wa shule ya msingi ya Msasani Lessy Nyambo vitabu vya wanafunzi na vya walimu ikiwa ni sehemu ya shughuli zinazofanywa na wafanyakazi wa Airtel katika kusaidia shule za watoto wenye mahitaji maalumu.
Afisa Rasilimali watu wa Airtel Bi Doris Kibasa akikabithi vitabu kwa mwalimu mkuu wa kitengo cha watoto wenye mahitaji maalumu wa shule ya msingi ya Msasani Lessy Nyambo mchango uliotolewa na wafanyakazi kwa watoto wa shule yenye mahitaji maalumu. wafanyakazi wa Airtel walitoa mchango huo walipotembelea shule ya msasani Jana
Afisa Rasilimali watu wa Airtel bi Monica Mbwilo vitabu kwa mwalimu mkuu wa kitengo cha watoto wenye mahitaji maalumu wa shule ya msingi ya Msasani Lessy Nyambo mchango uliotolewa na wafanyakazi kwa watoto wa shule yenye mahitaji maalumu. wafanyakazi wa Airtel walitoa mchango huo walipotembelea shule ya msasani Jana.
watoto wenye mahitaji maalumu wa shule ya msingi ya msasani wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya simu ya mkononiya Airtel mara baada ya kupokea msaada wa vitabu kwa walimu na wanafunzi wa shule hiyo vilivyotolewa kwa ushirikiano wa wafanyakazi wa Airtel ili kusaidia ufundishaji wa masomo ya elimu kwa watoto wa mahitaji maalumu shuleni hapo

katika kuchangia shughuli za kijamii, wafanyakazi wa Kampuni ya simu za mkoni Airtel kwa pamoja wameshiriki katika kuchanga na kusaidia wanafunzi wa shule ya watoto wenye mahitaji maalumu iliyopo Msasani jijini Dar es salam.

Wafanyakazi hao wamekusanya kiasi cha shilingi milioni 3 zilizotumika kununua vifaa mbali mbali vya kufundishia.

Akizungumzia mpango huo maalum wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo Afisa Rasilimali watu wa Airtel Bi Doris Kibasa alisema “mkakati huu umewahusisha wafanyakazi wa Airtel katika vitengo tofauti, ninawashukuru kwa kujipanga wao wenyewe na kutumia muda wao kwa kuwakumbuka watoto hawa kwa namna hii

Zoezi hili limewezesha upatikanaji wa jumla ya vitabu vyenye thamani shilingi milion 3 kwa shule ya msasani na kupunguza uhaba wa vitabu kutoka kitabu kimoja kwa watoto watatu hadi kitabu kimoja kwa kila mtoto mmoja.

“tumeona mahitaji ya wanafunzi hawa tulipotembelea shule hii mwishoni mwa mwaka jana. Na kuamua kujipanga ili kuweza kuwasaidi wadogo wetu na majirani zetu ili waweze kufika hapa tulipo sisi leo. Tunaamini kwa kufanya hivi tutakuwa tumeweza kuinua maisha ya watoto hawa na kiwango cha Elimu hapa Tanzania” alisisitiza Bi Doris

nae Mwalimu Mkuu wa kitengo cha watoto wenye mahitaji maalum Bw, Lessy Nyambo alisema msaada huo ni mkombozi kwa wanafunzi hao kwani utawawezesha wanafunzi hao kuwa na kitabu kimoja kimoja badala yakutumia kitabu kimoja wanafunzi wawili mpaka watatu. Amesema kwamba wanafunzi hao wanakabiliwa na uhaba wa vitendea kazi vitakavyowawezesha kuendelea na masomo bila tatizo lolote na hivyo amewahasa mashirika ya umma na wadau mbalimbali kushirikiana na Serikali katika kusaidia shule za watoto wenye mahitaji maalumu.

Nae mwanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi Msasani Fatuma Ally aliishukuru Airtel kwa kuweza kuwapatia Vitabu ambavyo vitaweza kuwasaidia katika masomo yako.

Airtel chini ya mpango wake wa shule yetu imedhamiria kuendelea kuboresh kiwango cha elimu nchi na kuleta mabadiliko katika masomo ya sayansi ili kupata wataalamu wengi wasayansi nchini.

Wiki mbili zilizopita tumetoa msaada wa Vitabu na sare za shule katika shule ya msingi ya Kiromo iliyopo mjini Bagamoyo vyenye dhamani ya shilingi milioni 50 , huku ikitoa msaada wa vitabu kwa shule 4 za sekondari kwa kila mkoa ikiwemo mikoa ya Kagera na Mwanza Lengo ni kufikia shule nyingi zaidi nchini Nzima

TIB na SIDO yasaini makubaliano ya kujenga maeneo ya viwanda

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) Bw. Peter Noni (wapili Kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda vidogo vidogo nchini (SIDO), Bw Michael Laizer, ambayo yanalenga ujenzi wa maeneo ya viwanda kwa wajasiliamali wadogo na wakati. Hafla iliyofanyika jana katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia ni Mwanasheria na Katibu wa Bodi wa TIB Bi. Martha Maeda, na kulia ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Bulilo Mafwimbo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) Bw. Peter Noni (Kushoto) wakibalishana mawazo na Mkurugenzi wa Shirila la Maendeleo ya Viwanda vidogo vidogo nchini (SIDO), Bw Michael Laizer kabla ya kusaini hati ya makubaliano. Makubaliano hayo yanalengaujenzi wa maeneo ya viwanda kwa wajasiliamali wadogo na wakati. Hafla iliyofanyika jana katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) Bw. Peter Noni (wapili Kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano na Mkurugenzi wa Shirila la Maendeleo ya Viwanda vidogo vidogo nchini (SIDO), Bw Michael Laizer, ambayo yanalenga ujenzi wa maeneo ya viwanda kwa wajasiliamali wadogo na wakati. Hafla iliyofanyika jana katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

======

Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) imesaini makubaliano na shirila la maendeleo ya viwanda vidogo vidogo nchini (SIDO) yenye lengo la kushirikiana kuweka miundombinu ya viwanda kwa ajili ya kuwasaidia wajasiriamali wadogo wadogo. Mpango huu wa ushirikiano utawezesha ujenzi wa maeneo ya viwanda (industrial areas), ambao utaanza na mkoa wa Dar es Salaam, kabla ya kutanuka katika miji mingine.  

Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano hayo jana katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Peter Noni, alisema kuwa lengo ni kuwasaidia wajasiriamali kuweza kuzalisha bidhaa za viwandani.

“Hapa benki tumebaini kwamba kunamatatizo makubwa sana kwa mjasiriamali Mtanzania anapojaribu kuwekeza kwa ajili ya uzalishaji. Vita vya kuondoa umasikini nchini vinategemea uzalishaji. Uzalishaji pia unategemea uwezo wa kupata mikopo kutoka benki.

“Benki yetu ya Rasilimali Tanzania imekuwa ikiwafikia wajasiriamali ili kuwapa mikopo kwa ajili ya kuendeleza biashara zao, lakini wengi wao wanashindwa kufikia vigezo, vinayotokana na gharama kubwa inayohitajika ili kuwekeza katika kiwanda.

“Kwa hiyo, benki yetu kwa kushirikiana na SIDO tumeweza kupanga mkakati wa kuwawezesha wajasiriamali kuondokana na tatizo hilo. Tumekubaliana kuanza kushirikiana kutafuta maeneo ambayo tutayawekea miundombinu ya viwanda ambayo itawasaidia hawa wazalishaji wadogo wadogo kuja kukodi, hatua ambayo itawapunguzia gharama za uendeshaji.

“Huu utaratibu pia utamwezesha mjasiriamali huyu aweze kukopesheka na taasisi za kibenki, kwa sabau atakuwa na mahala maalum pa kuzalishia kwa gharama ndogo,” alisema Noni.Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa SIDO Michael Laizer alisema riba ya  mikopo inayotolewa na mabenki hapa nchini bado ni changamoto kwa wajasiriamali wadogo kwa sababu ni kubwa mno.

“Riba ya mikopo kutoka katika benki za kibiashara hapa nchini bado ni changamoto kwa wajasiriamali wadogo. Riba hizo zinawakwamisha wajasiriamali, zinawaruduisha nyuma na pia wanashindwa kupanua biashara zao,” alisema Bw Laizer.

Alisema ushirikiano wa SIDO na TIB utawasaidia wajasiriamali watakaoingia katika mpango huu kupata maeneo ya kuanza uzalishaji kwa gharama nafuu, alisema kuwa utakuwa ni mkombozi kwa wazalishaji wadogo wadogo nchini. “Tunashukuru uongozi wa TIB kukubali kushirikiana na SIDO katika kusaidia kuwapa maeneo ya kuzalishia bidhaa kwa wingi zaidi ambayo yatasaidia kuwaondolea umasikini na kusaidia kuondoa janga la ukosefu wa ajira nchini,” alisema Bw. Laizer.

MKUTANO WA WALIOSOMA KIBOSHO GIRLS

$
0
0


KWA WANAFUNZI WOTE WALIOSOMA KIBOSHO GIRLS WANATAKIWA KATIKA MKUTANO UTAKAOFANYIKA SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 2 MACHI 2013 KATIKA KLABU YA BRAJEC  TPDC FLATS MIKOCHENI JIJINI DAR ES SALAAM KUANZIA SAA TISA MCHANA. 

TAFADHALI ATAKAYESOMA UJUMBE HUU AMTAARIFU MWINGINE. TANGAZO  LIMETOLEWA NA MWENYEKITI DR FLORA ISMAIL.

HOTELI YA DOUBLETREE BY HILTON KUGAWA TAA 200 KILA MWEZI ZINAZOTUMIA NISHATI YA JUA KWA SHULE ZA MSINGI ZA MKOA WA DAR ES SALAAM

$
0
0
Mwl. Salome Makanza wa Shule ya msingi Oysterbay akisoma risala kwa niaba ya Mwl. Mkuu Msaidizi Janeth Mdingi ambapo ameishukuru Hoteli ya DoubleTree by Hilton kwa kubuni kampeni kama hiyo ya kugawa taa zinazotumia Nishati ya Jua kwa Wanafunzi wa Darasa la Saba ambao wanakabiliwa na Mitihani kwani zitawasaidia hata Umeme utakapokatika majumbani mwao.
Mwl. Salome Makanza akikabidhi risala yake kwa Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Mh.Dkt. Terezya Huvisa. Kulia ni Mkurugenzi wa kanda wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton Dar es Salaam Bw. Judd Lehmann. Kuhsoto ni Kushoto ni Afisa Elimu Msaidizi wa Wilaya ya Kinondoni Faustin Kikove na Mwl.Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Oysterbay Bi. Janeth Mdingi (wa pili kushoto).  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Mhe. Membe apokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Uingereza hapa nchini

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Uingereza hapa nchini, Mhe. Dianna Melrose. Hafla hiyo fupi ilifanyika Ofisini kwa Mhe. Membe, tarehe 27 Februari, 2013.
Mhe. Waziri Membe akionesha Nakala hizo mara baada ya kuzipokea.
Mhe. Membe akizungumza na Mhe. Melrose masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uingereza mara baada ya kupokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi huyo.
Mhe. Balozi Melrose akimsikiliza Mhe. Membe wakati wa mazungumzo yao. Wengine katika picha ni Balozi Dora Msechu (wa pili kutoka kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Bi. Zainab Angovi (kushoto), Afisa katika Idara ya Ulaya na Amerika.
Mhe. Membe akimsikiliza Balozi Melrose alipokuwa akifafanua masuala mbalimbal ya ushirikiano.
Mhe. Membe akiagana na Mhe. Balozi Melrose mara baada ya mazungumzo yao.

UZINDUZI WA UKRAINIAN - AFRICAN ACADEMIC CENTER, KHARKOV NATIONAL UNIVERSITY NAMED AFTER VN KARAZIN:

$
0
0

Sherehe katika mji wa Kharkiv, Ukraine, hivi karibuni ambapo kituo hicho kimeanzsihwa kuimarisha uhusiano wa Elimu, Utamaduni na Maendeleo kwa ujumla kati ya Ukraine na Afrika.
Mhe. Balozi Jaka Mwambi aliweza kuzungumza na wataalamu wa mambo ya Elimu kuhusu kusaini mkataba wa Elimu kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Ukraine ambapo wamekubaliana kuhuisha mkataba huo katika vipingele kadhaa kwa upande wa Ukraine.
Mkataba huo utaruhusu Watanzania wengi kusoma vyuo vya Ukraine, wanafunzi wa Ukraine kusoma Tanzania pia, maprofessa kwenda kufundisha Tanzania, kubadilishana uzoefu wa tafiti (research) mbalimbali na hata kubadilishana mambo ya kiutamaduni.

 Wanazuoni wa kiTanzania waishio Ukraine katika picha na Balozi wa Tanzania nchini Urussi, Mhe. Jaka Mwambi na Msaidizi wake - Mhe. Mbarouk N. Mbarouk.
 Mhe. Vil Bakirov - Rector wa Kharkiv National University named after V.N. Karazin, Mhe. Irina Gagarina - Director of Ukrainian State Centre of International Education of Ukraine, Balozi wa Angola nchini Urussi, Mhe. Jaka Mwambi - Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini  Urussi wakipongezana kwa uzinduzi wa kituo cha UKRAINIAN - AFRICAN EDUCATION CENTRE.
Wanazuoni kutoka Nigeria, Tanzania, Tunisia na Kenya.



MAMLAKA YA HALI YA HEWA NCHINI YATOA TAARIFA YA MWELEKEO WA MVUA ZA MSIMU WA MACHI-MEI 2013

BUNGE LA TANZANIA KUSHIRIKIANA KWA KARIBU NA BUNGE LA NAMIBIA

$
0
0
Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne S. Makinda (kushot) akimkaribisha Balozi wa Jamhuri ya Namibia nchini Tanzania Balozi Japhet Issack alipomtembelea ofisini kwake leo.Pamoja na mambo mengine Balozi huyo amemuomba Spika Makinda kuimarisha uhusiano na Bunge la Namibia kwani kuna mambo mengi Bunge hilo linaweza kujifunza kutoka Tanzania.
Spika Makinda akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Balozi wa Namibia nchini Tanzania ambapo amemhakikishia Balozi huyo kuwa Bunge la Tanzania lipo tayari kushirikiana na Bunge la Namibia na kuona ni maeneo yapi ambayo yatawafaidisha wananchi wa nchi mbili hizi. Aliainisha maeneo ya mafunzo na kujenga uwezo kuwa ya kipaumbele. Na Prosper Minja-Bunge.

MAMA SALMA KIKWETE AKABIDHI MSAADA WA VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 700 KWA HOSPITALI KUU YA MKOA WA RUKWA

$
0
0
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dr. John Gurisha orodha ya vifaa mbalimbali vya tiba kwa ajili ya hospitali ya Mkoa wa Rukwa tarehe 26.2.2013 hospitalini hapo. Vifaa hivyo vimeletwa nchini na Taasisi ya WAMA kwa kushirikiana na Kampuni ya Project C.U.R.E kutoka Marekani na vina thamani ya shilingi milioni mia saba.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dr. John Gurisha moja ya vifaa mbalimbali vya tiba kwa ajili ya hospitali ya Mkoa wa Rukwa tarehe 26.2.2013. Baadhi ya vifaa hivyo ni mashine za Ulta Sound, X-Ray, Upasuaji, tiba ya macho, tiba ya kinywa na meno, mgongo, mifupa, mashine ya dawa za usingizi, vitanda maalum (TCU beds) n.k. Kushoto anaeshuhudia makabidhiano hayo ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.
Baadhi ya vifaa tiba alivyokabidhi Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete vikiwa na thamani ya shilingi milioni mia saba. Vifaa hivo pamoja na vingine ambavyo bado vipo kwenye kontena vimeletwa nchini na Taasisi ya WAMA kwa kushirikiana na Kampuni ya Project C.U.R.E kutoka Marekani.
Mama Salma Kikwete akiongea na wadau wa sekta ya afya na wananchi waliokusanyika katika viwanja vya hospitali kuu ya Mkoa wa Rukwa muda mfupi kabla ya kukabidhi vifaa tiba kwa hospitali hiyo vyenye thamani ya shilingi milioni mia saba.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akimkaribisha Mama Salma Kikwete kuzungumza na wadau wa afya katika viwanja vya hospitali kuu ya Mkoa wa Rukwa ambapo alikabidhi vifaa tiba kwa hospitali hiyo vyenye thamani ya shilingi milioni mia saba. Mkuu huyo wa Mkoa alimshukuru Mama Salma kwa jitihada anazozifanya yeye na taasisi yake katika kuunga mkono juhudi za Serikali kuboresha huduma za afya nchini, alimuhakikishia kuwa Serikali yake ya Mkoa itahakikisha inasimamia vizuri sekta ya afya kutimiza ahadi za Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2010-2015 ambazo ni pamoja na kuimarisha huduma za afya nchini.
 Katibu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Daudi Nasib akielezea kwa kifupi kazi na majukumu ya taasisi hiyo kwa wadau wa afya waliohudhuria hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa tiba kutoka WAMA kwa uongozi wa hospitali kuu ya Mkoa wa Rukwa. Miongoni mwa malengo makuu ya taasisi hiyo ni kuimarisha afya ya mama na mtoto na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha huduma ya afya nchini.
 Ndugu Abdul Kimario wa shirika la Project C.U.R.E kutoka Marekani ambae shirika lake limeshirikiana na WAMA kuleta vifaa tiba hivyo hapa nchini akitoa ufafanuzi wa matumizi ya baadhi ya vifaa hivyo kwa wadau wa afya waliokusanyika kushuhudia makabidhiano hayo.
Mama Salma Kikwete akimkabidhi Mzee Protas Kimario kitambulisho cha matibabu ya uzeeni kuwakilisha wazee wengine 458 zoezi lililoenda sambamba na kukabidhi vifaa vya tiba kwa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa tarehe 26.02.2013. Jumla ya vitambulisho 4356 sawa na asilimia 96% katika Manispaa ya Sumbawanga vimeshatengenezwa kwa ajili ya matibabu ya wazee.
Mama Salma Kikwete akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta funguo za pikipiki kwa ajili ya vituo vya afya vya Wilaya hiyo katika jitihada za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT). Jumla ya Pikipiki kumi kutoka Water Rid zilikabidhiwa kwa ajili ya huduma hizo katika Mikoa ya Rukwa na Katavi.(Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

RAIS KIKWETE ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JKT JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na uongozi wa juu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) jijini Dar es salaam alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo leo February 27, 2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange pia walihudhuria.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia makamanda wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alipotembelea makao makuu yao leo February 27, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya saa toka kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael Muhuga huku Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange wakishuhudia. Saa hiyo imeandaliwa na makamanda wa JKT kumpongeza Rais Kikwete kwa kurejesha mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kuanzia mwaka huu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa juu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) jijini Dar es salaam alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo leo February 27, 2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange pia wapo.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

MUHIMBILI YAFANYA MABADILIKO YA MFUMO WA UKUSANYAJI MAPATO

Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images