Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

WAJAWAZITO WAKIJIFUNGUA KATIKA MAZINGIRA SALAMA VIFO VYAO VITAPUNGUA - SALMA KIKWETE

$
0
0
 Ili kuhakikisha vifo vya kina mama wajawazito vinapungua ni lazima wajifungue katika mazingira salama huku kukiwa na upatikanaji wa kutosha wa vifaa tiba.

Hayo yamesemwa jana na Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Mama Salma Kikwete wakati akiongea na viongozi wa Bohari ya Dawa (MSD) iliyopo Keko Jijini Dar es Salaam.

Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alitembelea makao makuu ya MSD kwa ajili ya kuangalia vifaa tiba ikiwa ni pamoja na vifaa vya kujifungulia  kina mama wajawazito.

Alisema kama mama atajifungua katika mazingira salama nchi itaweza kuvuka malengo ya milinia ya kupunguza vifo vya kina mama wajawazito ambavyo kwa sasa vimepungua kutoka 452 kwa kila vizazi hai 100000 hadi kufikia 432 kwa kila vizazi hai 100000 jambo ambalo litasababisha maisha ya mama kuwa bora. 

“Moja ya kazi zinazofanywa na taasisi ya WAMA ni kuboresha afya ya mama na mtoto hapa nchini, katika hili tunatoa vifaa tiba vikiwemo vitanda vya kujifungulia kina mama wajawazito katika Hospitali, vituo vya Afya na Zahanati  ili kuhakikisha kina mama wanajifungua katika mazingira salama” .

Wakati wa ziara ya Rais Kikwete  mkoani Morogoro niliahidi kutoa vitanda vya kujifungulia ili kina mama waweze kujifungua salama, nimekuja hapa na nimejionea vitanda vizuri na vya kisasa vya kujifungulia pamoja na vifaa vingine ambavyo vinatumika kwa mama mjamzito naahidi nitawapelekea vifaa hivyo”, alisema Mama Kikwete.

Aidha Mama Kikwete pia aliwataka viongozi hao kuongeza juhudi  katika utendaji wao wa kazi  ya kuokoa maisha ya binadamu na kuhakikisha dawa wanazozipokea zinafika kwa mlaji kwa wakati kwani kama zitafika kwa wakati vifo vitapungua.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa MSD Cosmas Mwaifwani alisema tangu mwaka wa fedha uliopita wameanza kupeleka dawa na vifaa tiba moja kwa moja katika ngazi ya vituo vya afya na kuvifikisha kwa mlaji nia ikiwa ni kufikisha huduma hii kwa mlengwa kwa ubora unaotakiwa na kwa wakati.

“Dhina ya MSD ni  kuwezesha upatikanaji wa vifaa tiba vyenye ubora kwa bei naafuu kwa watanzania wote, ndiyo maana tunafika Tanzania nzima na hata kule ambako kuna ugumu wa kufika zinaangaliwa njia mbadala za kufika huko”. 

Hivi sasa tunaweza kusimama na kuizungumzia dhina hii bila wasiwasi kwani kwa sasa tafiti zinaonyesha kuwa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba umeongezeka kutoka asilimia 45 hadi kufikia asilimia 85”, alisema Mwaifwani.

Alisema pamoja na kwamba MSD inashughulikia Hospital, Zahanati na Vituo vya afya vya Serikali na taasisi zilizoidhinishwa na wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii bado ipo tayari kutoa huduma kwa  makundi mengine ambayo yanatuma maombi kwa ajili ya kununua vifaa tiba kwa matumizi ya wananchi.

Mwaifwani alisema, “Pale ambapo kundi la watu ama mtu binafsi anapohitaji vifaa tiba kwa ajili ya matumizi ya wananchi na vifaa hivyo vikiwepo MSD, hatutakuwa na hiyana ya kutompatia huduma hiyo kwani tumedhamiria kuokoa maisha ya watanzania”.

Bohari ya Dawa ni moja ya Idara inayojitegemea chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inajiendsha chini ya Bodi ya wadhamini yenye majukumu makuu matatu ambayo ni kununua, kuhifadhi na kusambaza dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa Hospitali za Serikali na zile zilizoidhinishwa na wizara.

MSHINDI WA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) 2014, MWANAAFA MWINZAGO APOKELEWA KWA SHANGWE NA NDELEMO MKOANI KWAO MTWARA

$
0
0
Mara baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara, Mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 Mwanaafa Mwinzago akitoa Maneno ya Shukrani kwa Wakazi wa Mtwara waliojitokeza kuja Kumpokea uwanja wa Ndege wa Mtwara mapema Leo. Vilevile alitoa Shukrani zake zote kwa Watanzania Wote kwa Kuweza umpigia Kura na Kumfanya aibuke mshindi wa Milioni 50 za Tanzania katika fainali ya Shindano la  Kusaka vipaji vya Kuigiza lijulikanalo Kama Tanzania Movie Talents (TMT).
Wapenzi, Mashabiki na wana Mtwara wakiwa Nje ya Uwanja wa Ndege wa Mtwara wakisubiri Kumpokea Mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 Mwanaafa Mwinzago kwaajili ya Kumpongeza kwa Kuibuka MShindi wa SHilingi Milioni 50 za Kitanzania katika Fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT)lililofanyika Mwisho wa Mwezi wa nane katika Ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar Es Salaam.
Wakazi wa Mkoa wa Mtwara wakimpongeza Mshindi wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago ambaye amewasili Mkoani Mtwara ambapo ndio Nyumbani Kwao akitokea Dar Es Salaam mara baada ya Kuibuka Mshindi na Kujinyakulia Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania.
Ndugu, Jamaa na Marafiki wa Mshindi wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago wakipiga picha ya Pamoja mara baada ya Kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara akitokea Dar Es Salaam.

North Eastern Kenya and the Media

TANCIS KUPUNGUZA MUDA NA KUIONGEZEA MAPATO SERIKALI

$
0
0
MAMLAKA mbalimbali ambazo zinawajibika kwa namna moja au nyingine katika kuwezesha mizigo mbalimbali inayoingia nchini kutolewa bandarini zitaunganishwa na mfumo mpya wa kisasa wa kutumia mtandao wa kompyuta wa Tanzania Customer Integrated System (TANCIS) kwa lengo la kuharakisha uondoaji wa mizigo hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa elimu kwa walipa kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Diana Masalla wakati akitoa mada katika kongamano lililoandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali inayoendeshwa bila faida ikiwa na lengo la kupiga vita umaskini Actionaid Tanzania (AATZ) ikishirikiana na Kikundi cha haki kwenye kodi (Tanzania Tax justice Group).

Kongamano hilo ambalo linahusu haki kwenye kodi ni sehemu ya mpango wa asasi ya Action Aid Tanzania kuleta uelewa na weledi katika masuala ya kodi miongoni mwa watanzania na walipa kodi ili kufanikisha ukusanyaji wa raslimali zinazowezesha serikali kutoa huduma za msingi na pia kutengeneza fursa za wananchi kujiendesha kiuchumi.

Masalla alisema mfumo huo mpya ambao utamfanya mwenye mzigo kutoa maelezo ya mzigo wake kidigitali na maofisa forodha nao kushughulika na mzigo wake bila kukutana naye ana kwa ana, umeonesha ufanisi mkubwa hasa wa ufuatiliaji wa hatua kwa hatua tangu mzigo umeingia nchini hadi unamfikia mhusika.Aidha mfumo huo umebana uchepushaji wa mizigo hiyo kutokana na ufuatiliaji wa kidigitali unaofanywa na mfumo huo.
DSC_0002
Mkurugenzi Mkazi wa ASASI isiyo ya kiserikali ya kupiga vita umaskini Actionaid Tanzania (AATZ), Yaekob Metena akifungua kongamano la siku tatu kwa asasi zisizo za kiserikali, wawakilishi kutoka makundi ya vijana na waandishi wa habari juu ya masuala ya haki kwenye kodi linaloendelea kwenye hoteli ya Seascape jijini Dar.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog)

WAZIRI NAGU AHUTUBIA WAFANYABIASHARA WA UBELGIJI NA LUXEMBOURG

$
0
0
Aliyeshika karatasi ni Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji Mhe. Dr. Mary Michael Nagu akibainisha fursa mbalimbali  za Uwekezaji zilizo Tanzania. Akihutubia Wafanyabiashara hao  amewashauri kuchangamkia fursa mbalimbali katika sekta za kilimo, gesi, utalii, madini na ujenzi. Kongamano la Biashara limeandaliwa na Ubalozi wa Tanzania Ubelgiji kwa kushirikiana na Taasisi ya Biashara ya Ubelgiji na Luxembourg.
Pichani ni sehemu ya Wafanyabiashara wa Ubelgiji na Luxembourg wakimsikiliza Mhe. Dr. Mary Michael Nagu Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji. Mhe. Nagu amehutubia Wafanyabiashara hao leo hii Brussels kwenye Kongamano la Biashara lililoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania Ubelgiji kwa kushirikiana na taasisi ya Biashara ya Ubelgiji. 
Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji Dr. Mary Michael Nagu (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kaamala (wa kwanza kulia) na Bwana Maurice Vermeesch Mwenyekiti wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Ubelgiji. Wa kwanza kushoto ni Bwana Christopher Mramba Msaidizi wa Mhe. Nagu.

Article 9

BIA YA KIBO GOLD LAGER YA SERENGETI BREWERIES LTD YASHINDA TUZO YA MEDALI YA DHAHABU YA UBORA DUNIANI YA MONDE SELECTION.

$
0
0


BIA ya Kibo Gold Lager imechaguliwa kuwa mshindi wa medali ya dhahabu kwa ubora duniani inayotolewa na ‘Monde Selection’. Kibo ilipokea utambulisho huo wa kimataifa wakati wa sherehe za 53 za kila mwaka zilizofanyika huko Bordeaux, Ufaransa.  

‘Monde Selection’ ni tuzo zinazotolewa kila mwaka tangu mwaka 1961, kwa ajili ya bidhaa za vinywaji na chakula. Huendeshwa na kampuni ya Biashara ijulikanayo kama ‘International Institute for Quality Selections’ ya Brussels, Ubelgiji. Bidhaa hizo huonjwa na kujaribiwa ili ziweze kupewa alama ya ubora.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries Ltd (SBL), Bw. Steve Ganon, alisema: “Kama familia ya SBL, tumefarijika sana kusikia habari hii kubwa inayoihusu bidhaa yetu, kitu kama hiki huwa hakitokei hivi hivi; tumekifanya kitokee... Kwa hiyo ninaipongeza timu nzima ya SBL kwa juhudi zao za kujenga imani kwa watumiaji.” 

Bia ya Kibo Gold ilizinduliwa miaka 15 iliyopita chini ya Kibo Breweries. Kwa bahati mbaya, bidhaa hiyo haikudumu sana sokoni kutokana na kufungwa kwa kampuni ya Kibo Breweries. Nembo hiyo ilichukuliwa na Serengeti Breweries Ltd na kuzinduliwa upya Juni 2012 katika kiwanda cha SBL kilichopo Moshi Brewery ambako ndiko huzalishwa na kusambazwa sehemukubwa ya kaskazini mwa Tanzania katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Tanga na Manyara, kati ya mingine mingi.

Lengo la bia ya Kibo Gold ni kutanua wigo wa vinywaji vya Serengeti Breweries Ltd na kuwashika watumiaji wa daraja la kati katika soko la kaskazini mwa nchi.  Agosti 2013, Kibo Gold ilibadilishwa na kuwekwa katika chupa yenye shingo ndefu maarufu kama ‘mwanamke nyonga’ ili kwenda na wakati na matakwa ya soko la kisasa.  

Sasa Kibo ipo katika chupa yenye shingo ndefu ya milimita 500 ikiwa na asilima 5.5 ya kileo inayodumu kwa kipindi cha miezi sita. Kauli mbiu ya Kibo ni ‘Yaone maisha katika mwanga bora.’Bia hii kwa sasa inauzwa rejareja kwa Sh 1,800. 

TAMISEMI YATAKA KUONGEZA ZAIDI KIWANGO CHA TAHADHARI YA UGONJWA WA EBOLA.

$
0
0
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Hawa Ghasia, amewaagiza  Waganga Wakuu wa Mikoa , na Halmashauri za wilaya nchini kuongeza zaidi kiwango cha kuchukua tahadhari katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ukiwemo wa Ebola.
Waziri Ghasia alitoa agizo hilo jana mjini hapa wakati wa  hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Waganga wakuu wa mikoa, Halmashauri za wilaya na wakurugenzi wa Hospitali za rufaa kutoka mikoa yote ya Tanzania bara.
Kwa mujibu wa Waziri huyo kuwa, hapa nchini ugonjwa huo  haujathibitika kuingia na Serikali imechukua tahadhari zote kuhakikisha kuwa ugonjwa huo hauingii  nchini na endapo utathibikika kuingia uweze kudhibitiwa kikamilifu.
Hata hivyo alisema , mwaka huu kumekuwepo na matukio ya hapa nchini na nje ya nchi yaliyotufanya tuongeze zaidi kiwango cha tahadhari , na tukio la kwanza ni la mlipuko wa ugonjwa wa Dengue , ambao uliwapata wagonjwa 1,384 kote nchini, na kusababisha vifo vya watu wanne , sehemu kubwa ya wagonjwa walikuwa ni wa Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Waziri huyo , tukio la pili ni la ugonjwa wa ebola ,ambao kwanza ulianzia nchi za Afrika Magharibi,  na kati ya Machi hadi Agosti mwaka huu , watu 3,069 waliungua ugonjwa huo.
Hivyo  hadi kufikia Agosti 28, mwaka huu ,ugonjwa huo umeua watu 1,552 na hivi karibuni umeingia nchi ya Congo DRC na kufikia mwishoni mwa mwezi uliopita watu 24 wameripitiwa kuugua .
“ Ni matumaini yangu kuwa katika mkutano huu  , suala la magonjwa ya mlipuko kama haya yatajadilikwa kikamilifu ili kila mmoja wenu awe katika tahadhari kubwa” alisisitiza Waziri Ghasia
Hata hivyo , Waziri Ghasia alitumia fursa hiyo kutoa shukrani za Serikali ya Tanzania kwa Watu wa Marekani kupitia Shirika lao la CDC na Shirika la Afya Duniani kwa kutoa vifaa na vifaa tiba kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo wa ebola.
Mbali na tahadhari ya magonjwa ya mlipuko, Waziri Ghasia alisema , katika ziara zake sehemu mbalimbali hapa nchini ameshuhudia juhudi zinazofanywa na wadau katika kuboresha upatikanaji  na utoaji wa huduma za afya na ustawi wa jamii.
Kwa mujibu wa Waziri huyo kuwa juhudi hizo ni  kujenga vituo vipya vya huduma za afya , kukarabatiwa vituo ambavyo havipo katika hali nzuri  kuongeza watumishi na upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na kuimalisha utaratibu wa kukusanya mapato katika vituo.
Pia ulimalishaji wa utoaji wa huduma kwa makundi maalumu hususan , wanawake wajawazito, watoto chini ya miaka mitano na  wazee  katika baadhi ya maeneo husika.
Hata hivyo alisema ,kutokana na juhudi hizo, malalamiko kuhusu uhaba wa dawa na vitendo vya rushwa yamepungua katika maeneo ambako juhudi hizo zimekwishafanyika.
“ Nimefurahishwa  na kasi ya ujenzi mpya wa Zahanati na Vituo vya Afya .... juhudi hizi zinapaswa kupongezwa  kwa vile ni utekeleaji wa Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)” alisema Waziri Ghasia .
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali , Dk Donan Mmbando, kabla ya kumkaribisha waziri , alisema lengo la mkutano huo ni kujadili masuala muhimu yanayolenga kuboresha huduma za afya na ustawi wa jamii hapa nchini na pia kuainisha changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi wa wizara hiyo.
Hata hivyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wataalamu hao wa sekta ya afya kujipanga kukabiliana magonjwa ya mlipuko ukiwemo wa ebola na kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya kutolea huduma endapo kutakuwa na udhibitisho wa dalili za wagonjwa katika maeneo yao.
Pamoja na kuzungumzia changamoto zilizopo ikiwemo ya ya  usimamizi wa utendaji bora na uboreshaji wa  mazingira ya kazi na y a watumishi , pia aliwataka wataalamu wao kuangalia namna ya kukabiliana na ongezeko la magonjwa yasiyoambukizwa ukiwemo wa saratani.
Kwa mujibu wa Manga Mkuu wa Serikali, kuwa vituo vingi vya Afya vilijengwa kwa kuangalia upande mmoja wa kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza na kusahau mengine yasiyoambukizwa na kwamba hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa ili kukabiliana nayo na kutaka yaingizwe kwenye mpango kazi wa mwaka 2016.
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Godfrey Mtei akipokea zawadi ya saa ya ukutani kutoka kwa Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia, juzi mjini hapa.
 Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia akikambishi zawadi ya saa ya ukutani Mganga Mkuu wa Serikali,Dk Donan Mmbando,saa hiyo iliyolewa na Taasisi ya Lab Eguip Limited.
 Baadhi ya waganga wakuu wa wilaya na Mikoa ya Tanzania Bara wakisiliza hotuba ya Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia ( hayupo pichani).
Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia, akiwa na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Donan Mmbando , baada ya waziri kufungua mkutano.

KIVUKO CHA MV. KIGAMBONI KUANZA KAZI KESHO KUTWA

$
0
0
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Watendaji mbalimbali hawapo pichani kutoka, Wizara ya Ujenzi, TEMESA na Kikosi cha Maji cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambao wamefanya kazi kubwa ya ukarabati wa Kivuko cha MV Kigamboni.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipanda ngazi kwenda kukagua Kivuko cha MV Kigamboni ambacho matengenezo yake makubwa yanakamilika leo.
Luteni Kanali Gwanafi kulia akimuongoza Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwenda kukagua Kivuko cha MV Kigamboni sehemu ya chini mara baada ya kukamilika kwa ukarabati wake.
Luteni Kanali Gwanafi wapili kutoka kulia akitoa maelezo kuhusu ukarabati mkubwa wa Kivuko cha MV Kigamboni kama inavyoonekana.
Taswira-Kivuko cha MV Kigamboni kinavyoonekana mara baada ya Ukarabati wake.

NBC appoints Pius Tibazarwa as Interim Managing Director

$
0
0
NBC Tanzania announces the appointment of Pius Tibazarwa as Interim Managing Director of NBC Tanzania. Effective 1 October 2014, Pius will succeed Mizinga Melu, who has been appointed Chief Executive of Barclays Africa Regional Management. NBC Tanzania is a subsidiary of Johannesburg listed Barclays Africa Group Limited (BAGL).
Pius is currently the Treasurer for NBC Tanzania and has recently been on secondment to BAGL in Johannesburg.  Previously he was Head of Global Markets, Head of Trading and Head of Global Markets Sales for Standard Chartered Bank Tanzania.

In his banking career, Pius has pioneered the introduction of several new products into the Tanzanian market including FX Options, Structured Deposits and Interest Rate Derivatives.

He holds a Bachelor of Science in Engineering Degree from the University of Dar es Salaam and is a member of the ACI Tanzania Association.

NBC Board Chairman Dr Mussa Assad said: “As Managing Director of NBC Tanzania, Mizinga has built a strong team which is truly transforming our business. She is leaving the business in a much stronger position from where the team will continue to build on under Pius’s leadership. I wish Pius and Mizinga both well in their new endeavours.”
Pius will report to Mizinga in her new role as Chief Executive of Barclays Africa Regional Management, as will the country Managing Directors of all BAGL’s businesses outside South Africa.

WASANII KASSIM MGANGA, AUNTY EZEKIEL NA AJ UBAO KUNOGESHA TAMASHA LA UTALII NA MIAKA 4 YA VIJIMAMBO MGENI RASMI MHE. LAZARO NYALANDU

$
0
0
Vijimambo Blog kwa ushirikiano wa pamoja na Ubalozi wa Jamhuri ya Muunagano wa Tanzania ikiwemo Jumuiya ya Watanzania DMV inawaletea miaka 4 ya Vijimambo ikiutangaza Utalii wa Tanzania na kukemea ujangili siku ya September 13, 2014. Njoo ujivunie maliasili na utalii wa nchi yako sote kwa pamoja yunaweza kuitangaza nchi yetu na kukemea ujangili kwa kauli moja yenye nguvu inayosikika kimataifa.
Msanii wa Bongo Movie Aunty Ezekiel kunogesha tamasha la utalii siku ya Jumamosi Sept 13, 2014
Msanii wa Bongo flava Kassim mganga nae kuwepo.
AJ Ubao

Mbunge wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa achangia bati 100 ujenzi wa shule ya msingi lukwambe na zahanati ya kijiji cha mlangali

$
0
0
Mbunge wa  jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa  (kulia) akikabidhi ahadi ya bati 100 alizokuwa ameziahidi mbunge aliyepita marehemu Dr  Wiliam Mgimwa kwa  viongozi wa kijiji cha Mangalali kwa ajili ya ujenzi  wa vyumba vya madarasa  shule ya msingi Lukwambe hadi  sasa ni asilimia 90 ya ahadi binafsi za mbunge aliyefariki  zimetekelezwa jimbo la Kalenga na mbunge Mgimwa.


Mbunge wa  jimbo la Kalenga Bw Godfrey Mgimwa kulia akikabidhi mchango wake wa Tsh 250,000 kwa ajili ya kusaidia kazi ndogo ndogo  za ujenzi wa zanahati ya kijiji cha Mangalali 
mbunge wa Kalenga Godfrey Mgimwa akiongoza viongozi kutembelea  ujenzi wa zahanati kijiji cha Mangalali 
Diwani wa kata ya Ulanda kulia  akitoa ufafanuzi kwa mbunge wa  jimbo la Kalenga Bw Mgimwa  kuhusu maendeleo ya ujenzi wa zahanati kijiji cha Mangalali .
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Rais Yoweri Museveni Awasili Nchini kwa Ziara ya siku moja

$
0
0
 Rais wa Uganda Yoweri Museveni akiteremka katika ndege iliyomleta leo jijini dar es Salaam kwa ajili ya  ziara yake ya siku moja nchini Tanzania .
 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akikagua Gwaride la Maaskari pamoja na Mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni baada ya kuwasili  leo jijini  katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili ya ziara ya siku moja.
 Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete (Kulia) pamoja na mgeni wake Rais wa  Uganda Yoweri Museveni (kushoto) wakiangalia ngoma za utamaduni baada ya kuwasili  katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa  Mwalimu Julius  Nyerere Leo jijini Dar es Salaam ,kwa ajili ya ziara ya siku moja hapa nchini.
Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete (Katikati)akipata maelekezo kutoka kwa mwongoza msafara na kushoto ni  Rais wa  Uganda Yoweri Museveni  ambaye amewasili nchini leo  kwa ajili ya ziara ya siku moja . ( Picha na Lorietha Laurence-Maelezo).
 Ndege iliyomleta Rais wa Uganda Yoweri Museveni ikiwa imetua katika Kiwanja cha Ndege cha  Kimataifa  Mwalimu Julius Nyerere tayari kwa ziara yake ya kikazi ya siku moja ambapo alipokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete leo jijini Dar es Salaam. 

Mkutano wa 24 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF waanza rasmi leo jijini Arusha

$
0
0
Mgeni Rasmi katika Mkutano wa 24 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Mwigulu Nchemba akitoa hotuba yake wakati akifungua mkutano huo unaofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,jijini Arusha kwa siku tatu mfululizo kuanzia leo Septemba 10 mpaka Septemba 12,2014.Katika hotuba yake hiyo,Mh. Nchemba wameutaka Mfuko wa PPF kuhakikisha wanapanua wigo kwa kuongeza wanachama wengi kutoka kwenye setka binafsi hasa wananchi wa kipato cha chini ikiwemo wajasiriamali.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF,Alhaj Ramadhan Khijja akitoa hotuba yake mapema leo asubuhi wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 24 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF unaofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,jijini Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,William Erio akizungumza leo kwenye Mkutano wa 24 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa PPF,unaofanyika leo kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,Jijini Arusha.
Mgeni Rasmi katika Mkutano huo,Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,William Erio wakati wa Mkutano wa 24 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa PPF,unaofanyika leo kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,Jijini Arusha.
Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk. Titus Kamani (kushoto) akikabidhi Mfano wa Cheti,Muwakilishi wa Chama wa Wavuvi kutoka Ukerewe,Alphonce Mukama wakati wa Mkutano wa 24 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa PPF,unaofanyika leo kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,Jijini Arusha. Wapili kushoto ni Mgeni Rasmi katika Mkutano huo,Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Mwigulu Nchemba.
Picha ya pamoja na Baadhi ya Washindi wa tuzo mbali mbali za uchangiaji wa Mfuko wa PPF.

Mjadala: kifanyike nini kupunguza ama kukomesha ajali barabarani??

$
0
0
Taswira hii inayosambaa kila pembe katika mitandao ya jamii na Globu ya Jamii kuipata ndiyo chachu ya mjadala wetu ambao mdau unaombwa kuchangia bila kuchafua hali ya hewa. Ukweli ni kwamba THIS IS TOO MUCH! Ni lazima kifanyike kitu ama lifanyike jambo kukomesha maafa ya kila mara nchini kutokana na ajali za barabarani.

Waziri Nagu akiwa nchini Ubelgiji

$
0
0
Waziri wa Uwekezaji na Uwezashaji Mhe. Dr Mary Michael Nagu akibadilishana mawazo na wamiliki wa Viwanda wa Wetteren Ubelgiji baada ya kumaliza ziara ya kutembelea baadhi ya Viwanda. Jana Waziri Nagu alibainisha fursa mbalimbali za uwekezaji zilizo Tanzania katika Kongamano la Biashara liloandaliwa na Taasisi ya Biashara ya Ubelgiji kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania Ubelgiji. Kongamano hilo lilifanyika jijini Brussels Ubelgiji.
Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji Dr. Mary Michael Nagu akipokea zawadi kutoka kwa Bwana Peter Doclo Meneja wa Mauzo na Masoko wa kiwanda cha Vandamme Marshamallows cha Wetteren Ubelgiji baada ya kutembelea kiwanda hicho.

NEWS ALERT:Watu wawili wanaidaiwa kufariki kufuatia ajali ya Basi la Super Feo kuacha njia na kugonga mti

$
0
0
Watu wawili Wanadaiwa kupoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa vibaya kufuatia ajali mbaya iliyotokea leo  katika  eneo la  Sanangula nje kidogo ya mji wa Songea mkoani Ruvuma,ikilihusisha basi la Super Feo linalofanya safari zake kati ya Songea - Makambako lililoacha njia na kugonga mti. Aidha inaelezewa kuwa chanzo cha ajali hiyo kinadaiwa kuwa ni mwendo kasi.
 Sehemu ya basi hilo la Super Feo lionekanavyo pichani likiwa limepondeka pondeka baada ya kuacha njia na kugonga mti
Baadhi ya Wasomalia wema wakiwasaidia majeruhi waliopatwa na ajali ya basi hilo

WANAFUNZI WANAOMALIZA DARASA LA SABA TUWATUNZE KIMAADILI WAKISUBIRI MATOKEO

$
0
0
LEO watoto wetu wapatao 808,111 wanamaliza elimu yao ya msngi ya Darasa la Saba nchini kote.

Hii ni idadi tu ya wale ambao wamejisajili kufanya mitihani hiyo kwa mawa huu na Baraza la Mitihani kuwatambua katika takwimu zao hapa nchini kwa mwaka huu wa 2014 lakini huenda vijana waliostahili kumaliza elimu hiyo ingekuwa kubwa zaidi ukilinganisha na wale waliojindikisha darasa la kwanza 2007.

Nimesema watoto wetu wanamaliza kwakua tu na mimi katika hao 808,111 bimnti yangu ni mmoja wapo wa wanaomaliza leo na kwa enzi zetu sisi wazazi wao tungejitapa kuwa ni LY ambayo kimsingi kipindi ile tupo ambao tulikua hatuji maana yake bali ni kufuata mkumbo tu kutokana na viingereza vyetu vya Ugoko kutoka Shule ya Msingi Chini ya Mti.

Hahahaaaa! Mimi nilikuwa nafahamu maana yake ni Last Year! Na hii ni kwasababu tu kaka zangu walikuwa wananifundisha watokapo likizo.

Hoja yangu hapa ni juu ya vijana wetu hawa zaidi ya laki nane ambao kesho wanaingia mtaani na kuazia septemba 12 ni raia na wanarudi mtaani. Soma zaidi : FATHER KIDEVU BLOG

WAKALA WA TAIFA WA HIFADHI YA CHAKULA (NFRA) KANDA YA DODOMA INAKABILIWA NA UFINYU WA ENEO LA KUHIFADHIA MAZAO MSIMU HUU WA UNUNUZI WA MAZAO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi ameitaka Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma kuhakikisha inatafuta suluhisho la haraka la changamoto ya maghala na mifumo ya kuhifadhia mazao inayoikabili taasisi hiyo wakati huu wa msimu wa kununua mazao.

Vilevile Dr. Nchimbi ameelekeza ukarabati wa Maghala ya hifadhi ya “National Milling” yaliyopo eneo la Makole ambayo uwezo wake ni kuhifadhi takribani tani elfu 10 kwa ghala uwekewe mkakati ili kusaidia kuleta suluhisho la haraka la ukosefu wa maeneo ya kuhifadhia mazao yanayoendelea kununuliwa hivi sasa.

Alitoa maelekezo hayo jana alipotembelea kituo cha NFRA Dodoma kukagua maendeleo ya zoezi la ununuzi na uhifadhi wa mahindi na Mtama ambapo alijionea maghala yaliyopo kwa ajili ya kuhifadhia mazao yamejaa na foleni kubwa ya magari yaliyoleta mahindi na mtama kutoka kwa wakulima yakiwa yanasubiri kushusha mazao huku changamoto kubwa ikiwa sehemu ya kuyahifadhi mazao hayo.

Meneja wa NFRA Kanda ya Dodoma Ndg. Mambali alisema kuwa kwa sasa NFRA inanunua mahindi na Mtama kutoka kwa walulima, na kwa mwaka huu, NFRA Kanda ya Dodoma imepanga kununua tani elfu 15 na mpaka sasa tani elfu tatu tu ndio zimeshanunuliwa ambapo tani elfu moja ndio zimefanikiwa kuhifadhiwa kwenye maghala hivyo kunahitajika suluhisho la haraka la sehemu ya kuhifadhi mazao ili zoezi la ununuzi lifanyike kama lilivyopangwa.

Katika hatua nyingine Dr. Nchimbi amepongeza NFRA kwa kutoa kipaumbele kwa vyama vya ushirika vya wakulima kwa kununua mazao yao kwa bei maalumu tofauti na inavyonunua kwa wafanyabiashara wengine ambapo bei inayonunua kwa vyama vya ushirika vya wakulima kwa kilo moja ya mahindi ni shilingi 530 wakati kwa wafanyabiashara wengine inanunua kwa shilingi 500.

Akiwasilisha ombi la vyama vya ushirika vya wakulima kuongezewa kiwango cha tani wanazoruhusiwa kuuza kwa NFRA, Mwenyekiti wa kikundi cha wakulima cha Matumaini Kongwa Ndg. Stanley Machakala amemuomba Mkuu wa Mkoa Dodoma kuwasaidia waongezewe tani zaidi za kuiuzia NFRA kwani huko vijijini bado wakulima wamebakiza mahindi mengi yanayohitajika kuuzwa.

Akitoa ufafanuzi juu ya ombi hilo, Dr. Nchimbi ameahidi kuwasaidia vyama hivyo vya ushirika vya wakulima kulifikisha suala hilo ngazi husika na kusimamia hadi watakapoongezewa kiwango cha mahindi na mtama wanachorususiwa kuiuzia NFRA.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akikagua shughuli za ufungashaji mahindi na Mtama kwenye magunia tayari kwa kuhifadhiwa kwenye maghala wakati alipotembelea kituo cha NFRA Kanda ya Dodoma.
Wakinamama kwenye kituo cha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma wakipeta mahindi na kuyaondoa uchafu tayari kwa ajili ya kuyafungasha kwenye magunia na kuyahifadhi ghalani, mahindi hayo yananunuliwa kutoka kwa wakulima na wafanyabiashara mbalimbali.
Vijana kwenye kituo cha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma wakiendelea na shughuli za kufungasha mahindi na mtama kwenye magunia kwa ajili na kuyahifadhi ghalani, mazao hayo yananunuliwa kutoka kwa wakulima na wafanyabiashara mbalimbali, changamoto kubwa kituoni hapo ni uchache wa maghala ya kuhifadhia mazao.

ngoma azipendazo ankal - Kindly sponsored by Isumba lounge

$
0
0
Eddie grant - "Gimme hope Joanna"
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images