Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 565 | 566 | (Page 567) | 568 | 569 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Shirika la Majisafi na Majitaka limeanza operesheni kata Maji katika jiji la Dar kufuatia madeni sugu yanayodaiwa wateja kufikia zaidi ya billion 44 zinazowahusisha taasisi mbalimbali za serikali, watumiaji wa majumbani na wafanyabiashara mbalimbali.

  Akizungumza na gazeti hili, Ofisa Uhusiano wa Dawasco, Bi Everlasting Lyaro alisema operesheni hiyo inatarajiwa kuanza mapema wiki ijayo na lengo kuu ni kuweza kupata fedha hizo ambazo ni malimbikizo ya muda mrefu.

  “operesheni hii itaanza wiki ijayo yaani sept 15 na mteja yeyote mwenye deni sugu na la muda mrefu na asiyekamilisha malipo ya Ankara za nyuma atasitishiwa huduma mara moja na kulazimika kulipa faini” alisema Lyaro.

  Aliitaja faini ambayo wahusika watalazimika kulipia baada ya kukatiwa Maji kuwa ni Tsh 50,000 kwa wateja wakubwa na 15,000 kwa wateja wadogo.

  “pia majina ya wateja wanaodaiwa na kiwango wanachodaiwa imebandikwa katika ofisi zote za kanda za  Mamlaka hizo hivyo mteja akifika katika ofisi zetu ataona jina lake na kiwango anachodaiwa” aliongeza Lyaro.

  “Tumewatumia ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) wateja wetu juu ya kuanza kwa operesheni hii hivyo hatutegemei mwananchi kujitokeza tena na kulalamika kuwa ameonewa kwa kutopata taarifa kabla zoezi halijaanza” alisema Lyaro.

  Alisema timu ya Dawasco itakuwepo katika maeneo mbalimbali ikipita nyumba kwa nyumba na shirika kwa shirika kusaka wote wanaodaiwa na watalazimika kulipa bili zao.


  0 0

  Barclays Africa Group announces the appointment of Mizinga Melu as Chief Executive of Barclays Africa Regional Management. Effective from 1 October 2014, Mizinga will be responsible for the group’s businesses outside of South Africa.

  Commenting on the appointment, Barclays Africa Group Chief Executive Maria Ramos said: “I am excited that we were able to appoint someone with such breadth of skills and experience into this role. Her appointment will be instrumental in executing our strategy on the continent.”

  Mizinga joined the then Absa Group in March 2013 as Managing Director of NBC Tanzania, where she built a strong team who are transforming that business. She is leaving the business in a much stronger position from where the team will continue to build.

  Previously Mizinga held a number of roles at Standard Chartered including: CEO of Standard Chartered Zambia, Global Head of Development Organisations in the UK, and Africa Regional Head of Financial Institutions in both South Africa and Kenya.

  With an MBA from Henley Management School and deep experience across many countries in Africa, Mizinga brings a wealth of expertise and experience to the role.

  The country Managing Directors of all Barclays Africa’s businesses outside South Africa will report to Mizinga, who will co-ordinate integrated planning and ensure the development of product-led and country-specific strategies, as well as support their execution. In addition, Mizinga will oversee the development of stakeholder relationships with governments, regulators, the Boards and customers in the countries.

  Mizinga will report to David Hodnett, Deputy CEO of Barclays Africa Group.

  0 0

  Na Mahmoud Ahmad,Arusha

  Mahakama ya Afrika ya haki za binadamu imemteua Jaji mkuu mstaafu wa Tanzania Agustino Ramadhan kuwa rais wa mahakama hiyo kwa kipindi cha miaka miwili uteuzi huounaanza mara moja baada ya aliyekuwa rais wa mahakama hiyo Sophia Akuffo wa Ghana kumaliza muda wake.

  Jaji Ramadhani Mtanzania wa kwanza kushikilia kiti hicho tangia kuanzishwa kwa mahakama hiyo baada ya kupata kura 7 kwa kura nne dhidi ya mpinzania wake katika nafasi hiyo ya rais wa mahakama hiyo huku nafasi ya makamu wake ikichukuliwa na jaji  Eisie Thompson kutoka nchi ya Nigeria.

  Katika nafasi hiyo ya makamu walikuwepo majaji watatu waliokuwa wakiwania nafasi hiyo na baada ya upigaji wa kura mara ya kwanza wawili walifungana kwa kura 4 na mmoja kupata kura tatu ndipo uchaguzi ulirudiwa na jaji Thompson kuibuka mshindi kwa kupata kura 6 dhidi ya tano za mpinzani wake.

  Akizungumza na vyombo vya habari baada ya uteuzi huo jaji Ramadhan alisema kuwa ni heshima kwa Taifa la Tanzania kwani ndio mara yake ya kwanza kupata nafasi hiyo huku akisema kuwa nafasi hiyo ni heshima kwake na kwa taifa lake.

  “Kesi yeyote inayohusu nchi yangu mimi sitakuwepo kutokana na sheria zetu za mahakama hii na kuwa tayari watanzania watano wamefungua kesi kwenye mahakama hii na kesi mbili zimetolewa hukumu ya mchungaji mtikila na Zongo”alisema jaji Ramadhan

  Alisema kuwa mpaka sasa ni kesi 5 zimefunguliwa  katika mahakama hiyo na mbili teyari zimetolewa ikiwemo dhidi ya serekali ya Tanzania kesi iliyofunguliwa na mchungaji Christopher Mtikila iliyohusu mgombea Binafsi huku akisema kuwa kuchukuwa hatua kwa utekelezaji wa hukumu kunategemea na serekali kama imejiunga na mikataba ya kimataifa.

  Alitanabaisha kutokana na sheria za mahakama hiyo wakati wa usikilizaji wa kesi zinazoihusu nchi yetu yeye hawezi kuisikiliza na kuwa Atajitoa kuisikiliza kama shiria ilivyo ya mahakama hiyo huku akisema mahakama hiyo inaundwa na majaji 11 kutoka nchi tofauti za bara hili .

  Aidha mahakama hiyo iliwaapisha majaji watatu wa mahakama hiyo kabla ya kuanza mchakato wa upigaji kura kumteuwa jaji wa mahakama hiyo huku ripoti ya mahakama hiyo kila mwaka ikipelekwa kwa umoja wan chi za Afrika.

  Uchaguzi huo huwa ni vipindi vya miaka miwili miwili na iwapo ukimaliza muhula wa kwanza kama utateuliwa tena kushika nafasi hiyo utakuwa ndio kipindi chako ya mwisho kushikilia nafasi hiyo.

  0 0


  Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji Dr. Mary Michael Nagu akimsikiliza Meneja wa kiwanda cha kutengeza mitambo  ya kutumika kwenye viwanda  vidogo vya bia, maziwa ya kawaida na maziwa ya soya. Mitambo hii ni kwa ajili ya kuanzisha viwanda vidogo vidogo kwa nia ya kuwezesha watu kiuchumi, kutoa ajira kwa vijana na kuongeza thamani mazao ya kilimo. Serikali ya Ubelgiji inagharamia asilimia hamsini ya ununuzi wa mitambo hiyo. Mhe Nagu ametembelea kiwanda hicho leo Ghent Ubelgiji.

  0 0

  Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji Dr. Mary Michael Nagu akimsikiliza Meneja wa kiwanda cha kutengeza mitambo ya kutumika kwenye viwanda vidogo vya bia, maziwa ya kawaida na maziwa ya soya. Mitambo hii ni kwa ajili ya kuanzisha viwanda vidogo vidogo kwa nia ya kuwezesha watu kiuchumi, kutoa ajira kwa vijana na kuongeza thamani mazao ya kilimo. Serikali ya Ubelgiji inagharamia asilimia hamsini ya ununuzi wa mitambo hiyo. Mhe Nagu ametembelea kiwanda hicho leo Ghent Ubelgiji.

  0 0


  0 0

  Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma

  BUNGE Maalum la Katiba leo tarehe 9 Septemba, 2014 limeanza kazi yake ya kusoma na kujadili taarifa za Kamati mbalimbali zikiwemo Kamati namba Kumi na Mbili, Kamati namba Mbili, Kamati namba Moja, Kamati namba Nne, Kamati namba Nane, Kamati namba Tano, Kamati namba Tisa, Kamati namba Tatu, Kamati namba Sita pamoja na Kamati namba Kumi na Moja.

  Baadhi ya mambo yaliyojadiliwa katika Bunge hilo ni pamoja suala la baadhi ya viongozi kumiliki akaunti zao za fedha nje ya nchi, haki za makundi mbalimbali nchini, haki za binadamu, masuala ya ndoa ya jinsia moja, haki za wafanyakazi na ajira, wajibu wa Waajiri nchini, haki za uzazi kwa wanawake, haki ya kuishi na sheria ya kunyonga, pia mambo yanayohusu Muundo wa Baraza la Usalama la Taifa.

  Akizungumza wakati wa mjadala huo katika Bunge hilo, mjumbe wa Kamati namba Sita, Mhe. Charles Mwijage amesema kuwa si vema kwa viongozi nchini kujenga tabia ya kufungua akaunti na kuweka fedha zao nje ya nchi kwani kunakaribisha masuala ya wizi wa fedha toka ndani ya nchi kwenda nje ya nchi.

  “Ni vema kiongozi yoyote anayetaka kumiliki fedha nje ya nchi aeleze ni wapi anamiliki hizo akaunti na nini anamiliki”, alisema Mhe. Mwijage.


  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akifanya mazoezi katika mitaa ya mji wa Dodoma mapema leo asubuhi kabla ya kwenda kuhudhulia vikao vya Bunge maalum la Katiba vinavyoendelea mjini Dodoma.Mh. Lowassa aliwahi kutamba sana kwenye mchezo wa mpira wa kikapu zamani.


  0 0

  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango), Bi Joyce Mkinga (Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati alipokuwa akitoa taarifa ya kufanyika kwa Mkutano wa Maafisa Mipango unaotarajiwa kufanyika Mwezi wa Oktoba mwaka huu. Kulia ni Mchumi Mkuu (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango), Bw. Omary Juma.

  0 0

  Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Ngao ya Jamii kuashiria uzinduzi wa msimu mpya wa Ligi kati ya Azam na Yanga itakayochezwa Jumapili (Septemba 14 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000.

  Mechi hiyo itaanza saa 10 kamili jioni, na kiingilio hicho cha sh. 5,000 ni kwa viti vya rangi ya kijani na bluu vitakavyochukua jumla ya watazamaji 36,000 katika uwanja huo wenye viti 57,558.

  Viingilio vingine katika mechi hiyo ambayo itatumia tiketi za elektroniki ni sh. 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 20,000 kwa viti vya VIP C na B wakati viti vya VIP A kiingilio ni sh. 30,000.

  MWAMUZI LUGENGE KUAGWA LEO
  Mwamuzi wa daraja la kwanza (class one), Luteni Godwill David Lugenge aliyefariki dunia juzi (Septemba 7 mwaka huu) kwa ajali ya gari katika Wilaya ya Handeni mkoani Tanga anaagwa leo (Septemba 9 mwaka huu).

  Mwili wa marehemu ambao umehifadhiwa katika Hospitali Kuu ya Jeshi (GMH) Lugalo, baadaye leo saa 6 mchana utapelekwa nyumbani kwa kaka yake Kimara Bucha jijini Dar es Salaam ambapo shughuli za kuaga zitafanyika kabla ya safari ya kwenda mkoani Njombe kwa ajili ya mazishi.

  Luteni Lugenge ambaye mwishoni mwa wiki alishiriki mitihani ya utimamu wa mwili kwa waamuzi wa Ligi Kuu, akiwa na ndugu yake Christopher Alexander Lunyungu katika gari dogo walipata ajali hiyo wakati wakienda mkoani Kilimanjaro.

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ambalo limetoa ubani wa sh. 200,000 kwa familia ya marehemu kwenye shughuli ya kuaga itawakilishwa na mjumbe wake wa Kamati ya Utendaji ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi, Saloum Umande Chama.

  TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Luteni Lugenge, Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu nchini (FRAT) na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito. Bwana ametoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe

  BONIFACE WAMBURA
  KNY KATIBU MKUU
  SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

  0 0

  Inner Circle - "Sweat (A La La Long)"

  0 0
 • 09/09/14--20:00: KUMBUKUMBU
 • Kwa namna ya pekee tunakukumbuka mtoto wetu FLORA FLOWIN MKANULA kwa kuitwa na Mwenyezi Mungu tarehe 10 Septemba, 2013.

  Ni mwaka mmoja sasa tangu ututoke. Upendo wako, ucheshi wako, ushauri wako, uvumilivu wako utakumbukwa daima na sisi wazazi wako Baba FLOWIN na Mama ALICE.

  Unakumbukwa pia na wadogo zako, IRENE na CARRINE, Marafiki, Wanafunzi wenzio wa ‘PCB’ pamoja na familia ya ST. JOSEPH CATHEDRAL HIGH SCHOOL. Kwa hiyo siku ya Jumatano tarehe 10 Septemba, 2014 itaazimishwa Misa Takatifu Kinondoni Makaburini tukiwa na familia ya ST. JOSEPH CATHEDRAL HIGH SCHOOL saa 3.00 asubuhi, na baadae tutaenzi siku yake kwa maadhimisho yatakayofanyika mchana saa 7.30 ST. JOSEPH CATHERDRAL HIGH SCHOOL kwa nia ya kumshukuru Mungu kwa zawadi ya FLORA FLOWIN MKANULA.

  “Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lipewe sifa”.

  “AMINA”

  0 0

   ·        Wadai fidia ya shilingi bilioni 500

  Kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na wadai wengine wawili wamefungua kesi ya madai katika Mahakama Kuu dhidi ya Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe na wengine wawili wakitaka kulipwa fidia ya Shilingi bilioni 500 kwa kashfa alizotoa kimaandishi dhidi yao.

  Mbali na IPTL,  wengine waliofungua kesi hiyo mnamo tarehe 4, Septemba kupitia wakili Melchisedeck Lutema wa Asyla Attorneys na  Kay Felician Mwesiga wa Bulwark Associates Advocates, ni kampuni ya Pan Africa Power Solutions Tanzania Limited (PAP) na Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni hayo mawili, Bw. Harbinder Sing Seth.

  Wadai hao watatu, miongoni mwa mambo mengine wanahitaji malipo ya fedha kutoka kwa Bw. Kabwe na washtakiwa wengine watatu ambao ni mhariri wa gazeti la Raia Mwema, Kampuni ya Raia Mwema na kampuni ya Flint Graphics, kuwa kama fidia itokanayo na makala ya kuwachafua iliyochapishwa kwenye gazeti hilo, iliyosababishwa na washitakiwa hao.

  Pamoja na hayo, pia wanahitaji tamko rasmi toka mahakamani kwamba makala iliyokuwa na kichwa cha habari "Fedha za IPTL ni Mali Ya Umma" iliyochapishwa katika kurasa wa 7 na 14 za gazeti la tarehe 13 Agosti, 2014 ilikuwa ni ya kupotosha na kuchafua kwa kudhamiria na kuhitaji washitakiwa kuomba radhi kwa kuandika na kuchapisha katika kurasa za mbele kichwa cha habari ya kuomba msamaha katika matoleo mawili mfululizo ya gazeti hilo.

  0 0


  0 0  0 0

  Mkurugenzi wa Idara ya Hospitali ya Mnazimmoja Dkt. Jamala Adam Taib akimueleza Waziri wa Afya Mh. Rashid Seif kazi zinazofanywa na Idara hiyo alipofika ofisini kwake kuanza ziara ya kutembelea Hospitali hiyo.
  Waziri wa Afya Mh. Rashid Seif akiongozana na Naibu wake Mh. Mahmoud Thabit Kombo wakitembelea eneo la Hospitali ya Mnzammoja katika ziara yake ya kutembelea Hospitali hiyo.
  Mkuu wa kitengo cha maradhi ya kisukari katika Hospitali kuu ya Mnazimmoja Dkt Miskia Ali akitowa maelezo kwa Waziri wa Afya juu kadhia ya maradhi hayo.
  Waziri wa Afya akipata maelezo ya shughuli za Maabara kutoka kwa mtaalamu wa Maabara wa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja Dkt. Marijani. Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar.

  NA RAMADHANI ALI – MAELEZO ZANZIBAR

  Mkurugenzi wa Idara ya Hospitali ya Mnazimmoja inayojumuisha Hospitali tatu, Hospitali ya Rufaa ya Mnazimmoja, Hospitali ya wagonjwa wa akili Kidongo chekundu na Hospitali ya Wazazi ya Muembeladu Dkt. Jamala Adam Taib amesema kazi kubwa inayofanywa na Idara hiyo katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2010 ni kuimarisha Hospitali ya Mnazimmoja ifikie kiwango cha Hospitali ya rufaa.


  0 0
 • 09/09/14--23:46: Remembering
 • The late Mama  Elsie Nantume Beatrice Uriyo.

  Even though it seems like time froze it has been two years since you suddenly left (10/09 2012)., yet you vividly remain engraved in our hearts, mind and thoughts,timeless & priceless. We your Husband, Children & Grandchildren miss& love you always.

  0 0
 • 09/09/14--23:55: dar es salaam ya kijani
 •  Sehemu  kubwa ya jiji la Dar es salaam ni ya kijani kama zinavyoonesha taswira hizi zilizopigwa jana kutoka angani.


  0 0

  Waziri wa Ujenzi  Dkt. John Magufuli  akiongea na wajumbe mbalimbali waliofika katika  uzinduzi wa kivuko cha kigamboni  leo jijini Dar es  Salaam kinachofanyiwa matenganezo  na Jeshi la Wanamaji maeneo ya kurasini ,ambacho kinatarajiwa kuanza kutumika rasmi alhamisi wiki hii.
   Mtendaji  Mkuu  Temesa Injinia  Marceline Magesa akitoa neno la shukrani  kwa Jeshi la Wanamaji waliwezesha matengenezo ya Mv Kigamboni  leo jijini Dar es Salaam ambapo kinatarajiwa kuanza kutumiwa na wananchi wiki hii.
   Waziri wa Ujenzi  Dkt. John Magufuli ( kushoto) na Katibu Mkuu wa Ujenzi  Injinia Mussa Iyombe(kulia) wakisikiliza kwa makini maelekezo yaliyokuwa yakitolewa katika ufunguzi wa kivuko cha Mv Kigamboni leo jijini Dar es Salaam kinachofanyiwa matenganezo  na Jeshi la Wanamaji maeneo ya kurasini  na kinatarajiwa kuanza kutumika wiki hii.
   Waziri wa Ujenzi  Dkt. John Magufuli ( katikati) akipata maelekezo kutoka kwa  Msimamizi wa matengenezo  Luten Kanali Abel Gwanafyo (Kushoto), kulia  ni  Mkuu wa Jeshi nla Maji Brigadia Jenerali Rostian Laswai wakati wa ufunguzi wa kivuko hicho leo jijini Dar es Salaam ,amabapo  kinatarajiwa kuanza kutumika wiki hii kurahisisha usafiri kwa watu wa  Kigamboni.
   Kivuko cha Mv Kigamboni kinavyoonekana kwa ndani, kinatarajiwa kuanza kutumika siku ya alhamisi baada ya matengenezo yalifanywa na Jeshi la Wanamaji  kwa mda wa wiki tatu tangu kilipoaacha kufanya kazi Agosti 14 mwaka huu.
   Kivuko cha Mv Kigamboni kinavyoonekana  upande wa mbele na ubavuni , kikiwa katika hatua za mwisho tayari kwa kuanza  kutumiwa na wananchi siku ya alhamisi baada ya matengenezo yaliofanywa na Jeshi la Wanamaji  kwa mda wa wiki tatu tangu kilipoaacha kufanya kazi Agosti 14 mwaka huu.( Picha na Lorietha Laurenc eMaelezo).

  0 0

  Bw. Julius Mziray mkaguzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) akizungumza na waandishi wa habari katika hospitali ya Regency ya jijini Dar es salaam. Baada ya kumkamata mtu mmoja anayetuhumiwa kutumia kadi ya bima ya afya yenye namba 02-HCTP1801 ambayo inamilikiwa na Bw. Terry J. Maona kinyume na utaratibu.

  Mtu huyo alikamatwa jana katika hospitali hiyo wakati akitaka kufanya vipimo vya (CityScan), ndipo mmoja wa wafanyakazi wa hospitali hiyo alipogundua na kupiga simu makao makuu ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuwataarifu kuhusiana na tukio hilo, ambapo maofisa walifika na kukamata nyaraka hizo huku mgonjwa akitokomea kusikojulikana baada ya kugundulika, Bw. Julius Mziray amewaasa wamiliki wa kadi za Bima ya Afya kutozitumia watu tofauti badala yake zitumie kwa wahusika walioorodheshwa katika bima hiyo tu Jambo ambalo kuwaigiza katika mikono ya sheria na kupata adhabu kali. 2Bw. Julius Mziray mkaguzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF akiwasomea waandishi wa habari maelezo yaliomo katika nyaraka hizo 3 
  Baadhi ya wgonjwa mbalimbali wakisubiri huduma katika hospitali hiyo4 

older | 1 | .... | 565 | 566 | (Page 567) | 568 | 569 | .... | 3286 | newer