Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel Catalog



Channel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 564 | 565 | (Page 566) | 567 | 568 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Mussa Jallow (katikati) Meneja Masoko wa Benki ya NBC, Alina Maria Kimaryo (kushoto) Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa Binafsi na Bidhaa za Kuwekeza, Andrew Massawe wakionyesha vipeperushi kuashiria uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya Weka Upewe ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo.
  Meneja Masoko wa Benki ya NBC, Alina Maria Kimaryo (kushoto) akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Weka Upewe ya mwaka 2014 jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Mussa Jallow na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa Binafsi na Bidhaa za Kuwekeza, Andrew Massawe.
  Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa Binafsi na Bidhaa za Kuwekeza, Andrew Massawe (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Weka Upewe ya mwaka huu jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Masoko wa benki hiyo, Alina Maria Kimaryo na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Mussa Jallow.
  Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano wa Benki ya NBC, William Kallaghe (kushoto) akizungumza katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam leo.
  Baadhi ya maofisa wa benki hiyo na waandishi wa habari waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

   Uongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa na wa wilaya ya Namtumbo ukitoka nje ya Ofisi ya Mkuu hiyo, baada ya kufanya mazungumzo ya kina ya mpango ya kujenga nyumba za gharama nafuu.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw.  Nehemia Mchechu na ujumbe wake wakiwa na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Bw. Abdulah Lutavi akiwatembeza kwenye eneo lililotengwa na Wilaya hiyo kwa ajili ya kujengewa nyumba na NHC. Shirika la Nyumba litajenga nyumba za gharama nafuu katika halmashauri hiyo hivi karibuni.

   Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw.  Nehemia Mchechu, Mkuu wa Wilaya Natumbo, Bw. Abdulah Lutavi na ujumbe wao wakijadiliana kwenye eneo litakalojengwa nyumba za gharama nafuu na Shirika la Nyumba.


  0 0

  Naomba kutumia fursa hii kuitambulisha kwenu rasmi official website yangu ambayo ni http://www.profesajay.com
  Kwa habari zangu za uhakika, kuhusu MUZIKI, VIDEOS, SHOWS, INTERVIEWS, PHOTOS na kila kinachonihusu... Kuwa wa kwanza kupata taarifa zangu, Asanteni sana kwa kunisupport siku zote!! LOVE..

  0 0

  Msemaji wa Wizara ya Kazi na Ajira Bw Ridhiwan Wema pichani, akiongea na Wanahabari hawapo pichani katika ukumbi wa Habari –Maelezo kuhusiana na Suala la la Wakala wa Huduma za Ajira nchini. Kushoto pichani ni Kamishna wa Kazi Bw.Saul Kinemela na kulia pembeni ni Bw Ally Msaki Mkurugenzi wa Ajira wote kutoka Wizara ya Kazi na Ajira.

  0 0

  Ajali nyingine mbaya:Basi la Abiria linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam - Tabora limepata ajali mbaya sana mchana huu katika eneo la  Kiegeya,Gairo na kupelekea zaidi ya watu wanne kupoteza maisha huku wengine wakiwa wamejeruhiwa vibaya sana.Ni majonzi makubwa yametawala katika eneo hilo hivi sasa,huku juhudi za kuokoa miili na majeruhi zikiendelea kama inavyoonekana pichani.ni siku tatu tu zimepita toka ajali nyingine mbaya itokee huko Musoma na kupoteza maisha ya zaidi ya Watanzania 35.Ripota wa Globu ya jamii yupo eneo la tukio hivi sasa na taarifa kamili itawajia baadae kidogo.


  0 0

  MKURUGENZI mtendaji wa Azania benki,Charles Singili amewataka wananchi kuwa na mazoea ya kujiwekea akiba kwa manufaa ya baadae.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa akauni mpya ya benki hiyo iitwayo Dhamira, Singili amesema kuwa utaratibu wa kujiwekea akiba utapunguza tatizo la umasikini kwa wananchi.

  Aliongezea kuwa, endapo wananchi wakipatiwa elimu kuhisu faida za kutunza fedha zao,itasaidia kupunguza hali ya umasikini uliopo sasa.

  "Kwa kutambua matatizo yanayoikabili nchi yetu, Azania bank imeamua kufungua akaunti ambayo itamwezesha mwananchi kutunza fedha bila makato ya aina yeyote" alisema Singili.

  Singili aliongezea kuwa, akaunti ya Dhamira, itamsaidia mwananchi yeyote kutunza fedha kuanzia Sh. 50,000 na atapatiwa riba ya asilimia 8 kila mwenzi.

  Aliongezea kuwa, akaunti hiyo inatafunguliwa na mtu ambae ametimiza miaka 18 na kuendelea na itamsaidia kuweka riba kadri awezavyo.

  "Dhamira akaunti itamsaidia mwananchi kutimiza malengo au ndoto zao, pia kipindi cha chini kuweka akiba ni miezi 12," alisema.
  Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Azania,Charles Singili akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa akauni mpya ya benki hiyo iitwayo Dhamira (Dhamira Account) uliofanyika kwenye Makao Makuu ya Benki hiyo,Ubungo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Waandishi wa habari waliohudhuria kwenye uzinduzi huo wakimsikilizwa kwa makini Mkurugeni Mkuu wa Benki ya Azania,Charles Singili.
  Mkurugeni Mkuu wa Benki ya Azania,Charles Singili akimuelekeza namna ya kujaza fomu,Bi. Naomi Mapunda ambaye alikuwa mteja wa kwanza kufungua akauni hiyo ya Dhamira.
  Baadhi ya Maofisa wa Benki ya Azania.

  0 0


   Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF na wadau wa Maendeleo kutoka ndani na nje ya nchi wameanza Mkutano wa kupitia mafanikio na changamoto za utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini,PSSN unaoratibiwa na Mfuko huo nchini. 


  Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango huo unaowahusisha wataalamu mbalimbali kutoka Taasisi za Fedha na mashirika ya misaada ya kimataifa utawawezesha pia wataalamu hao kutembelea maeneo kadhaa ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru kaya maskini  katika mikoa y Dodoma, Lindi na Zanzibar.


  Akitoa tathmini ya utekelezaji wa Mpango  wa kunusuru kaya maskini Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga amesema tayari kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 13 kimetumika katika kutoka ruzuku kwa walengwa wa Mpango huo na kuwa katika maeneo ambako ruzuku hiyo imetolewa kumekuwa na mafanikio makubwa ya uboreshaji wa maisha ya kwalengwa wa  mpango huo.


  Kwa Upande wao wadau wa Maendeleo kutoka BENKI YA DUNIA , UNICEF,ILO, UNPF,na  DFID,,wameonyesha kuridhishwa kwao na namna TASAF inavyotekeleza Mpango wa kunusuru kaya maskini na kuonyesha kuwa kazi hiyo itakamilimka kwa mafanikio makubwa .

   Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF bwana Ladislaus Mwamanga akiongoza Mkutano wa wadau wa maendeleo na maafisa wa TASAF juu ya utekelezaji wa mpango wa kunusuru Kaya maskini nchini ,PSSN ulioanza leo Jijini DSM.
   Baadhi ya wadau wa Maendeleo wakiwa katika mkutano wa kutathmini  utekelezaji wa shughuli za Mpango wa kunusuru Kaya Maskini, unaoratibiwa na TASAF.
   Baadhi ya wadau wa maendeleo  na watendaji wa TASAF wakiwa katika mkutano wa kutathimini utekelezaji wa mpango wa Kunusuru kaya maskini PSSN.
  Baadhi ya wadau wa maendeleo wakiongozwa na mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, aliyevaa tai  walipotembelea chumba cha kurekodi takwimu za walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini  ambacho kimefungwa zaidi ya kompyuta 100.




  0 0



  0 0

   Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu, Mhe. Benjamini Wiliam Mkapa akiwahutubia Wajumbe waliohudhuria mkutano wa Jiolojia uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa J.K Nyerere Jijini Dar es Salaam.
   Baadhi wa Wajumbe waliohudhuria mkutano wa Jiolojia wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na mgeni rasmi katika Ukumbi wa Kimataifa wa J.K Nyerere Jijini Dar es Salaam.
  Wanasayansi Vijana wakifuatilia mada wakati wa mkutano wa tatu wa Wanasayansi Vijana Duniani wenye lengo la kuhakikisha kuwa vijana wanashiriki vyema katika rasilimali za duniani kwa ajili ya maendeleo na ukuaji wa uchumi thabiti. (Picha na Makala na Benedict Liwenga, Maelezo-DSM)

  0 0
 • 09/08/14--23:09: Article 20


 • 0 0

  Mgodi wa dhahabu wa Geita Gold Mine uliopo mkoani Geita. Mgodi huu ni moja ya makampuni yanayowania tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji.
  Mshauri wa Mkurugenzi Mtendaji wa Geita Gold Mine katika masuala ya serikali na jamii Bw. Clement Msalangi (mbele kwa mbali) akielezea mafanikio ya mgodi wa Geita Gold Mine katika utoaji wa huduma bora kwa jamii na uwezeshaji kwa timu ya majaji na sektretarieti iliyofanya ziara katika mgodi huo.
  Meneja Mahusiano ya Jamii Bw. Manase Ndoloma akisisitiza jambo katika kikao kilichoshirikisha uongozi wa mgodi wa Geita Gold Mine na jopo la majaji na sekretarieti kwa ajili ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji iliyotembelea mgodi huo.


  0 0



  0 0

  The Cyber Defense East Africa 2014 will take place on 16th to 19th September next week with the MAIN theme “Fighting against Financial and Data privacy crime. The guest of honor in this event will be the Minister of Home Affairs, Hon Mathias Chikawe. Speakers from BOT, TCRA, Police Cyber Crime unit, Legal Sector Reform and international experts in forensic science and defense in depth from Europe will attend the event.   To get your ticket call +255719233037 or send email to registration@nrd.no  


  0 0

  Vijimambo Blog kwa ushirikiano wa pamoja na Ubalozi wa Jamhuri ya Muunagano wa Tanzania ikiwemo Jumuiya ya Watanzania DMV inawaletea miaka 4 ya Vijimambo ikiutangaza Utalii wa Tanzania na kukemea ujangili siku ya September 13, 2014. Njoo ujivunie maliasili na utalii wa nchi yako sote kwa pamoja yunaweza kuitangaza nchi yetu na kukemea ujangili kwa kauli moja yenye nguvu inayosikika kimataifa.
  msanii wa Bongo Flava Kassim Mganga kunogesha tamasha la Utalii na miaka 4 ya Vijimambo
  Aunty Ezekiel Msanii wa Bongo movie kutoka Bongo kunogesha Tamasha la Utalii na miaka 4 ya Vijimambo kaa mkao wa kula


  0 0

   Mbunge wa Jimbo la Morogoro kusini Mh Innocent Kalogeris (kulia) Ahimkabidhi Pikipiki 11 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Vijijini Mh Jazar Ikiwa Ni ahadi yake aliyoitoa ya Kukusaidia chama cha Mapinduzi Kujitegemea Kiuchumi.Mh Kalogeris Amekabidhi pikipiki hizo akiwa na Lengo Kila kata Kuwa na Pikipiki MMoja uwe Mradi wa Chama ili kuwezesha Kila kata Kuendesha Shuguli za Chama Bila kuwa wategemezi .Mbunge Kalogeris amehadi kuhakikisha kata zote za jimbo hilo zinapatiwa Pikipiki.Mh Kalogeris amesisitiza Pikipiki hizo ni mali ya CCM Wilaya ya Morogoro Vijijini na si mali ya watu binafsi. 
   Wanachama na wapenzi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Morogoro vijijini waliojitokeza wakati wa Kupokea Msaada huo.

   Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Vijijini Mh Jazar (Kulia) Akikabidi Pikipiki kwa Mmoja wa Mwakilishi wa kata zinazounda Wilaya ya Morogoro mjini Ikiwa kama mrdi wa kukiwezesha chama hicho kujitegemea

  0 0


  0 0


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni (pichani), anatarajiwa kuwasili nchini siku ya Jumatano asubuhi, tarehe 10 Septemba, 2014 kwa ziara ya kikazi ya siku moja.

  Katika ziara hiyo nchini, Mhe. Museveni atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu, Dar es Salaam. Rais Museveni ataondoka baadaye siku hiyo hiyo kurejea nyumbani.

  IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI,
  WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

  0 0

  Mkaguzi msaidizi wa Polisi,Inspekta Sospeter Laban Akeyo akiingia ukumbini na mkewe Fidea Laban wakati wa sherehe ya kumuaga iliyoandaliwa na wakazi wa mji wa Himo katika ukumbi wa King Size In.
  Afande Laban na mkewe wakiwa meza kuu na wageni wengine waalikwa.
  Champegne zikafunguliwa maalumu kwa ajili ya wageni waalikwa.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu -Tamisemi, Mh. Hawa A. Ghasia, akitoa neno kwa wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya mkopo wa elimu ya juu(‘Piga Kitabu na LAPF’)
   Uzinduzi rasmi wa Piga Kitabu na LAPF ulipambwa na shamrashamra za aina yake.
   Waziri Wa Nchi, Ofisi Ya Waziri Mkuu -Tamisemi, Mh. Hawa A. Ghasia, akimkabidhi mfano wa hundi Bwana Rolland Lyamuya mmoja wa wanachama wa mfuko wa pensheni wa LAPF ambaye amenufaika na huduma mpya ya mkopo wa elimu ya juu(‘Piga Kitabu na LAPF’)  iliyozinduliwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
    Mgeni rasmi wa hafla ya uzinduzi wa Piga Kitabu na LAPF Mh. Hawa A. Ghasia akipokea zawadi ya kitabu cha Nelson Mandela kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa  Pensheni wa LAPF. 
   Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi huo.
    Baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa ‘Piga Kitabu na LAPF’ Mkopo wa elimu ya juu kwa wanachama wa LAPF iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 

older | 1 | .... | 564 | 565 | (Page 566) | 567 | 568 | .... | 3272 | newer