Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 562 | 563 | (Page 564) | 565 | 566 | .... | 3285 | newer

  0 0

   Bondia Bonans Samweli (kushoto) akimrushia konde Bondia mwenzake Julius Kisalawe wakati wa mpambano wao uliofanyika katika GYM ya Ndame jijini Dar es salaam jana.Bondia Kisalawe alishinda kwa point mchezo huo.


   Bondia Julius Kisalawe akinyooshwa mkono juu kuashilia ushindi wake
   Mabondia Ally Yusuph (kushoto) na Sadam Manjepa wakionyeshana umwamba wakati wa mpambano wao uliofanyika jana katika GYM ya Ndame manzese jijini Dar es salaam. Yusuph alishinda kwa point.
  Mabondia Tasha Mjuaji (kushoto) na Hamisi Kicheba wakirushoana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika katika GYM ya Ndame Manzese Midizini Dar es salaam jana. PICHA NA SUPER D BLOG

  0 0

   Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Mohamed Aziz Abood  Akimkabidhi cheti Kada UVCCM Wilaya ya Morogoro mjini CCM,Wakati wa kufunga kambi ya UVCCM kutoka kata za Manispaa ya Morogoro eneo la Morning Site kata ya Milimani
   Mbunge wa Jimbo la Morogoro mjini Mh Aziz Abood akiwaongoza vijana wakati wa kula kiapo mara baada ya kumalizika kwa kambi ya umoja wa vijana CCM wilaya ya Morogoro mjini Akiwa sambamba na Katibu wa CCM wilaya ya Morogoro mjini nyuma,Pamoja na Katibu wa UVCCM wilaya ya morogoro mjini Kulia.
  Washiriki wa Kambi ya Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Morogoro wakila Kiapo Mbele ya Mbunge wa jimbo la Morogoro Mjini
    Mbunge wa Jimbo la Morogoro mjini Mh Aziz Abood  akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kambi ya UVCCM Wilaya ya Morogoro Mjini.
   Mbunge wa Jimbo la Morogoro mjini Mh Aziz Abood  akitangaza rasmi kumalizika kwa kambi hiyo

  0 0

  Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wahandisi mbalimbali hawapo pichani kuhusu umuhimu wa Taaluma ya Uhandisi na Maendeleo nchini kabla ya kufunga mkutano huo wa mwaka uliondaliwa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi(ERB).
  Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wapili kutoka kulia akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Profesa Ninatubu Lema wakawanza kushoto pamoja na Mbunge wa Tunduru kaskazini, Mheshimiwa Ramo Makani wakikagua baadhi ya kazi zinazofanywa na wahandisi nchini.

  Wahandisi zaidi ya 200 wakila kiapo cha Uhandisi mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Kisutu Waliyarwande Lema, huku viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akishuhudia tukio hilo.
   Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akikagua moja ya mabanda mbalimbali katika maadhimisho ya Siku ya Wahandisi Tanzania.

   Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhi zawadi ya kompyuta laptop  kwa mmoja kati ya wanafunzi wakike waliofanya vizuri katika masomo ya kihandisi nchini.

  Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akipewa maelezo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Ujenzi la Taifa (NCC) Dkt. Leonard Madaraka Chamuriho wakwanza kushoto kuhusu kazi mbalimbali za Baraza hilo.

  Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi mbalimbali katika picha ya pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya Uhandisi nchini. Picha zote kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini–Wizara ya Ujenzi

  0 0

  Na Edwin Moshi, Makete

  Walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari Iwawa iliyopo Makete mkoani Njombe wametakiwa kutoridhika na kubweteka na shule hiyo kushika nafasi ya nne kitaifa katika matokeo ya kidato cha sita 2014 yaliyotangazwa miezi michache iliyopita


  Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro katika hafla ya kuwapongeza walimu wa Iwawa sekondari baada ya shule hiyo kushika nafasi ya 4 kitaifa, nafasi ya 2 kikanda na nafasi ya 1 kwa mkoa wa Njombe katika matokeo ya kidato cha sita mwaka huu

  Amewapongeza walimu kwa jitihada zao za kufundisha pamoja na moyo wa wanafunzi katika kujisomea ambavyo kwa pamoja vimepelekea kuitangaza wilaya ya Makete kielimu na kuwataka kupanda na kushika nafasi za juu katika mitihani inayofuata
  "Ni kweli mnastahili pongezi lakini nawaombeni ongezeni bidii ili mitihani inayokuja mwakani mpande zaidi ya hapa, muitangaze wilaya yetu, tukishirikina pamoja tunaweza" amesema Matiro

  Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya amewataka wananchi kushirikiana katika kuchangia maendeleo ya shule kwani serikali inaunga mkono jitihada zao pale tu inapoona wamechangia

  Amesema kumekuwa na kasumba ya watu wachache kuwakatisha tamaa wananchi wengi wenye moyo wakuchangia miradi ya shule, na kusema wananchi wasikatishwe tamaa na watu wa aina hiyo kwani serikali haiwaachii peke yao, wao wakichangia kwa kiasi fulani serikali nayo humalizia palipobakia huku akisisitiza kuwa kwa shule zenye upungufu wa walimu, serikali inalitambua tatizo hilo na ndiyo maana inapanga walimu wapya kila mwaka katika shule hizo na mwishowe upungufu huo utamalizika


  Awali akisoma taarifa ya shule kwa mkuu wa wilaya, mkuu wa shule hiyo Mwl. Antony Ng'wavi amesema shule yake inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa pamoja na walimu jambo ambalo linachangia kupungua kasi ya ufaulu kwa kiasi kikubwa zaidi, huku akiahidi kuwa mwakani shule yake itafanya vizuri kuliko mwaka huu

  0 0

  s

  0 0

   
   MKurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi,Bwa.Ruge Mutahaba (Wanne kulia) kwa niaba ya uongozi wa Clouds Media Group na PrimeTime Promotions  Ltd ambao ndio waandaaji wa Tamasha la Fiesta 2014,ametangaza rasmi kuwa onesho la tamasha hilo lililobeba ujumbe murua kabisa wa sambaza upendo, litafanyika kesho jumapili ndani ya uwanja wa Karume.

  Tamasha hilo la Fiesta lilipangwa kufanyika JANA ijumaa mjini Musoma mkoani Mara lakini kufuatia ajali mbaya iliyotokea mkoani humo jana na kusababisho vifo vya watu zaidi ya 40,iliyotokea katika kijiji cha Sabasaba,wilaya ya Butiama mkoani Mara lilisitishwa ili kwenda sambamba na tukio zima katika kuwafariji wakazi wa Musoma na vitongoji vyake,kutoa mkono wa pole,ambapo Wasanii waliotarajiwa kushiriki tamasha hilo na Waandaaji walitoa msaada wa vifaa tiba kwa hatua za awali kusaidia majeruhi waliokuwa wakipelekwa hospitali ya rufaa mjini Musoma.

  0 0

  Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania,Salum Mwalim (kushoto)akiongea jambo kwa Wafanyakazi wa Kampuni ya Corona (T) Ltd baada ya kampuni hiyo kuibuka kinara wa utumiaji wa huduma ya M-pesa wanapojaza mafuta kwenye vituo vya OilCom( wapili kutoka kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Raphael Habiyaremye ,Meneja uendeshaji wa Corona Faiza Kijangwa ,Meneja Utawala wa Corona Norah Christopher, Meneja wa Maswala ya Kompyuta wa OILCOM Tanzania Abubakar Mwita.Hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha mafuta cha oilcom mtaa wa Libya jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa OILCOM Tanzania Mohamed Said (kushoto) Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania,Salum Mwalim wakimsikilza kwa makini ) Meneja Utawala wa Corona Norah Christopher alipokuwa akiongea kuhusiana na kampuni yao ya Kampuni ya Corona (T) Ltd kuibuka kinara wa utumiaji wa huduma ya M-pesa wanapoja za mafuta kwenye vituo vya OilCom,Kutoka kulia ni Meneja wa Maswala ya Kompyuta wa OILCOM Tanzania Abubakar Mwita, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Corona (T) Ltd Raphael Habiyeremya ,meneja uendeshaji wa Corona Faiza Kijangwa ,Meneja Utawala Norah Christopher hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha mafuta cha oilcom mtaa wa Libya jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa OilCom Tanzania Mohamed Said akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Corona (T) Ltd Raphael Habiyaremye baada ya kampuni yake kuibuka kinara wa uwekaji wa mafuta katika kituo cha Oilcom cha Libya jijini Dar es Salaam,kwa kutumia huduma ya M-pesa ambapo kila wiki wateja wanajishindia mtungi wa O-Ges wenye ujazo wa kilo 6. katikati ni Meneja Uhusiano wa nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim na Meneja wa maswala ya Kompyuta wa Oilcom Tanzania Abubakar Mwita.
  Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Corona (T) Ltd Raphael Habiyaremye baada ya kampuni yake kuibuka kinara wa uwekaji wa mafuta katika kituo cha Oilcom cha Libya jijini Dar es Salaam,kwa kutumia huduma ya M-pesa ambapo kila wiki wateja wanajishindia mtungi wa O-Ges wenye ujazo wa kilo 6 .Kulia ni Meneja wa maswala ya Kompyuta wa Oilcom Tanzania Abubakar Mwita.

  0 0

  MBUNGE MTANDA KUFUNGA KOZI YA LESENI A
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, Mheshimiwa Said Mtanda anatarajia kufunga kozi ya ukocha ya Leseni A ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) inayomalizika kesho (Septemba 7 mwaka huu).

  Hafla hiyo ya ufungaji wa kozi hiyo iliyoshirikisha makocha 22 itafanyika saa 7 mchana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, jijini Dar es Salaam.

  Kozi hiyo ya siku tano iliyokuwa chini ya wakunzi wa CAF, Moatasim Mohamed Nasr kutoka Sudan na Sunday Kayuni wa Tanzania.

  KOZI YA UKUFUNZI WA UTAWALA YA FIFA KUFANYIKA DESEMBA
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) wameandaa kozi ya ukufunzi wa utawala itakayofanyika Desemba mwaka huu.

  Kozi hiyo itakayoendeshwa na wakufunzi kutoka FIFA itafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Desemba 1 hadi 5 mwaka huu, ambapo sifa ya chini ya elimu kwa wanaotaka kushiriki ni kidato cha nne.

  Kwa wanaotaka kushiriki kozi hiyo wanatakiwa kutuma maombi yao kwa Katibu Mkuu wa TFF. Mwisho wa kupokea maombi hayo ni Septemba 12 mwaka huu ambapo wanatakiwa pia kuwasilisha nakala za vyeti vyao vya kitaaluma.

  TFF YARUDISHA LIGI DARAJA LA PILI
  Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana hivi karibuni imekubali mapendekezo ya Kamati ya Mashindano ya kurejesha michuano ya Ligi Daraja la Pili (SDL).

  Lengo la kurejesha ligi hiyo ni kuongeza wigo wa mashindano kitaifa ambapo itasaidia kushirikisha kundi kubwa zaidi la wachezaji kwenye mashindano makini yanayozingatia viwango na vigezo ili kuwapa wachezaji maendeleo ya kiuchezaji ikiwemo kuendelezwa vipaji vyao kitaalamu.

  Ligi hiyo yenye timu 24 itachezwa katika hatua ya makundi manne ya timu sita sita kwa mtindo wa nyumbani na ugenini ambapo mshindi wa kila kundi atapanda kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL). Timu ya mwisho kila kundi itarudi kwenye ligi ya mkoa wake.

  Hatua ya pili ni kutafuta bingwa wa SDL ambapo timu zilizoongoza makundi (nne) zitacheza kwa mtoano nyumbani na ugenini. Utakuwepo mchezo wa fainali ambapo mshindi atkuwa bingwa wa SDL msimu wa 2014/2015.

  Timu zitakazocheza SDL kwa msimu huu ni zile zilizoshika nafasi ya pili hadi ya nane katika Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) katika makundi yao msimu uliopita, na tatu zilizoshuka kutoka FDL msimu uliopita.

  Kundi A litakuwa na timu za Milambo FC (Tabora), Mji Mkuu FC (Dodoma), Mpanda United (Mpanda), Mvuvumwa FC (Kigoma), Singida United (Singida) na Ujenzi (Rukwa). Kundi B ni Arusha FC (Arusha), Bulyanhulu FC (Shinyanga), Eleven Stars (Kagera), Mbao FC (Mwanza), Pamba FC (Mwanza) na Rwamukoma JKT (Mara).

  Timu za kundi C ni Abajalo (Dar es Salaam), Kiluvya United (Pwani), Kariakoo FC (Lindi), Mshikamano FC (Dar es Salaam), Navy FC (Dar es Salaam) na Transit Camp (Dar es Salaam). Kundi D ni Magereza FC (Iringa), Mkamba Rangers (Morogoro), Njombe Mji (Njombe), Town Small Boys (Ruvuma), Volcano FC (Morogoro) na Wenda FC (Mbeya).

  Ligi itachezwa kuanzia Novemba mwaka huu.

  FDL KUCHEZWA MAKUNDI MAWILI
  Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2014/2015 itachezwa katika makundi mawili kwa mtindo wa nyumbani na ugenini kuanzia Oktoba 11 mwaka huu.

  Kundi A lina timu za African Lyon, African Sports, Ashanti United, Friends Rangers, Kimondo SC, Kurugenzi Mafinga, Lipuli, Majimaji, Mlale JKT, Polisi Dar es Salaam, Tessema FC na Villa Squad.

  Wakati kundi B lina timu za Burkina Faso, Geita Veterans SC, Green Warriors, Kanembwa JKT, Mwadui SC, Oljoro JKT, Panone FC, Polisi Dodoma, Polisi Mara, Polisi Tabora, Rhino Rangers na Toto Africans.

  0 0

  Viongozi wa vilabu vya timu zinazotarajia kushiriki kwenye Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayotarajiwa kuanza Septemba 27 mjini Morogoro wametakiwa kusajili timu zao mapema ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza hapo baadae wa kushindwa kusajiliwa kutokana na mapungufu ya timu zao.

  Mwenyekiti wa SHIMIWI Taifa Bw. Ally Katembo aliyasema hayo alipokuwa akifungua mkutano maalumu wa kupanga ratiba ya mashindano ya SHIMIWI uliofanyika ukumbi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam mapema leo.

  Bw.Katembo alizitaka timu zinazotumia wachezaji walioajiriwa kwa mkataba wa miezi mitatu kuacha tabia hiyo na badala yake watumie wachezaji wenye mikataba ya mwaka mmoja na kuendelea ili kuepuka tatizo la kutumia mamluki kwenye timu zao.

  "Tafuteni wachezaji ambao ni wafanyakazi katika Ofisi nyingine za Serikali kama timu zenu zina mapungufu ya wachezaji" alisema Bw. Katembo.

  Naye Katibu wa SHIMIWI Bw.Moshi Makuka aliwataka viongozi hao kutoa taarifa ya timu ambazo hazitashiriki mashindano hayo mapema iwezekanavyo ili kuepuka gharama zinazotumika katika maandalizi ya timu zao.

  "Timu ambazo hazitaweza kushiriki ziwe wazi kusema hazishiriki kwa sababu SHIMIWI inatumia gharama nyingi kwenye maandalizi" alisema Bw.Makuka.

  Mkutano huo ulihudhuriwa na wajumbe wa SHIMIWI na viongozi wa vilabu vya timu mbalimbali kutoka katika Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa, Mashirika ya Umma na Halmashauri za Wilaya.
  Mwenyekiti wa SHIMIWI Taifa Bw. Ally Katembo akifungua mkutano maalumu wa kupanga ratiba ya Mashindano ya SHIMIWI uliofanyika katika ukumbi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam mapema leo. Kushoto kwake ni Katibu wa SHIMIWI Bw. Moshi Makuka (wa pili) na wajumbe wa SHIMIWI wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa.
  Katibu wa SHIMIWI Bw.Moshi Makuka (wa pili kutoka kushoto) akitoa mada wakati wa mkutano maalumu wa kupanga ratiba ya timu zitakazoshiriki kwenye SHIMIWI mwaka huu katika ukumbi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam mapema leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa SHIMIWI Taifa Bw. Ally Katembo na wengine ni wajumbe wa SHIMIWI Taifa wakifuatilia mada.
  Mmoja wa Wajumbe wa SHIMIWI akishiriki katika zoezi la kupanga makundi mbalimbali katika ratiba ya michezo ya SHIMIWI.
  Kamati maalumu ikipanga ratiba ya makundi mbalimbali katika michezo ya mpira wa miguu,mpira wa pete, bao,karata, riadha,kuvuta kamba na kurusha tufe katika michezo ya SHIMIWI.
  Baadhi ya wajumbe wa SHIMIWI na Viongozi wa Vilabu vya Michezo wakifuatilia mada.

  0 0

  Mkurugenzi wa Habari, Elimu kwa Umma na Itifaki wa Bunge Maalum la Katiba, Bw. Jossey Mwakasyuka (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa semina iliyoandaliwa kwa ajili ya waandishi wa habari kuhusu kuimarisha Uandishi wa Habari za shughuli za Bunge iliyofanyika tarehe 6 Septemba, 2014 katika Ukumbi wa African Dreams Conference mjini Dodoma. Kulia ni Mshauri wa mambo ya Kiufundi toka Shirika la UNDP, Bi. Anna Kochannesyan.
  Mhariri Mtendaji Jamhuri Media Limited, Bw. Deodatus Balile akitoa mada mbele ya waandishi wa habari (hawako pichani) inayohusu Athari za Siasa katika uandishi wa Habari za Bunge, Madhara ya Vyombo vya habari kutumika, Miiko na Maadili ya kuzingatia wakati wa semina kwa ajili ya waandishi wa habari iliyofanyika tarehe 6 Septemba, 2014 katika Ukumbi wa African Dreams Conference mjini Dodoma.
  Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Kamati za Bunge Maalum, Bw. Athumani Hussein akitoa mada inayohusu Uandishi wa habari za Bunge na Siasa wenye tija kwa Taifa wakati wa semina iliyoandaliwa kwa ajili ya waandishi wa habari iliyofanyika tarehe 6 Septemba, 2014 katika Ukumbi wa African Dreams Conference mjini Dodoma.

  BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI KAMILI

  0 0

  Wachezaji wa Simba wakishangilia ushindi wa timu yao baada ya kuifunga Gor Mahia ya Kenya 3-0 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 
  Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Gor Mahia ya Kenya, Kennedy Opiyo katika chezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba ilishinda 3-0.
   Ramadhani Singano 'Messi' akichuana na beki wa Gor Mahia ya Kenya.
  Golikipa wa Gor Mahia, Fredrick Onyango akiokoa moja ya hatari langoni mwake.


  0 0

  Pichani ni sehemu mojawapo ya mitaa ya Musoma mjini ikiwa na muonekano wa watu wachache mara baada ya kunaswa na Camera ya Globu ya Jamii mapema leo mchana,mji huo umegubikwa na simanzi na manjonzi makubwa kufuatia ajali mbaya ya mabasi mawili yaliyogongana uso kwa uso likiwe gari ndogo,na kupelekea kuondoa uhai wa watu takribani 40 na zaidi katika kijiji cha Sabasaba wilayani Butiama mkoani Mara.

  0 0

  TUNAUNGANA NA WATANZANIA WOTE KATIKA KUOMBOLEZA MSIBA MKUBWA WA TAIFA
  "Jana September 5 2014 kwenye eneo la Sabasaba Mjini Musoma ilitokea ajali mbaya sana ya mabasi mawili yakiwa na abiria na kulihusisha gari jingine dogo ambapo majeruhi ni zaidi ya 70 na waliofariki ni 39 Wanawake kwa Wanaume kwa mujibu wa taarifa mpya za vifo zilizotoka."
  JUMUIYA YA WATANZANIA ITALIA IMEPOKEA TAARIFA ZA AJALI KWA MASIKITIKO  NA MSHITUKO MKUBWA SANA.
  TUNAWAPA POLE NDUGU JAMAA NA MARAFIKI WOTE WALIOPOTEZA WAPENZI WAO KATIKA AJALI HIYO,TUNATOA POLE KWA WATANZANIA WOTE NYUMBANI NA UGHAIBUNI KWA TUKIO  HILI LA KUSIKITISHA.  MWENYEZIMUNGU AWALAZE MAHALA PEMA PEPONI NDUGU ZETU, NA WALE AMBAO NI MAJERUHI MWENYEZIMUNGU AWAJAALIE NAFUU YA HARAKA NA WARUDI KATIKA SHUGHULI ZAO ZA KILA SIKU.
  INASIKITISHA SANA KUONA AJALI KAMA HIZI ZA BARABARANI ZIMEKITHIRI SASA NA TAKWIMU YAKE NI KUBWA KWA MWAKA INATISHA. NI MATUMAINI YETU SOTE  ZITACHUKULIA HATUA KALI ZA KUDHIBITI HALI  HII YA KUTISHA NA KUSIKITISHA SANA.
  TARATIBU ZIFUATWE ZA UKAGUZI WA VYOMBO VYA USAFIRI NA WAFANYAKAZI WOTE WA MAKAMPUNI YA USAFIRI.  MAKAMPUNI YENYEWE NAYO YAKAGULIWE KWAKINA SANA.
  TUNAMPONGEZA MH WAZIRI MWAKYEMBE KWA HATUA ZA AWALI ALIZOCHUKUA KWANI SASA BASI WANANCHI HATUTAKI KUSIKIA AJALI HIZI ZA AJABU AMBAZO NYINGI ZINATOKEA KIZEMBE PASIPO NA UNGALIFU WA MADEREVA.
  NA WATAKAO BAINIKA KUWA NA MAKOSA BASI WACHUKULIWE HATUA STAHIKI.
  KATIKA KIPINDI HIKI CHA KUOMBOLEZA YA  MSIBA HUU MKUBWA TUNAMUOMBA MUNGU ATUPE UVUMILIVU NA  UPENDO ZAIDI KWETU SOTE.

  MUNGU IBARIKI AFRIKA
  MUNGU IBARIKI TANZANIA


  Kagutta N.Maulidi
  Katibu mkuu
  Jumuiya ya Watanzania Italia.

  0 0

  Rais Jakaya Kikwete akimtunuku nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Jeshi la Wanachi wa Tanzania JWTZ, Mkuu wa majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange katika sherehe za kutunuku nishani zilizofanyika kwenye ukumbi wa Jenerali Kiwelu wa Chuo cha Mafunzo ya Maafisa wa Jeshi Tanzania, Monduli, Septemba 6, 2014.
   Amiri Jeshi Mkuu  Rais Jakaya Kikwete akimtunuku nishani  ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Jeshi la Wanachi wa Tanzania  JWTZ, Mnadhimu Muu wa majeshi  ya Ulinzi nchini, Luteni Jenerali Samuel Albert Ndomba   katika sherehe  za kutunuku nishani zilizofanyika kwenye ukumbi wa   Jenerali Kiwelu wa Chuo cha Mafunzo ya Maafisa  wa Jeshi Tanzania, Monduli
   Amiri Jeshi Mkuu  Rais Jakaya Kikwete akimtunuku nishani  ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Jeshi la Wanachi wa Tanzania  JWTZ Luteni Jenerali Charles Lawrence Mkakala
   Amiri Jeshi Mkuu  Rais Jakaya Kikwete akimtunuku nishani  ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Jeshi la Wanachi wa Tanzania  JWTZ  Meja Jenerali Salum Mustafa Kijuu
   Amiri Jeshi Mkuu  Rais Jakaya Kikwete akimtunuku nishani  ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Jeshi la Wanachi wa Tanzania  JWTZ Meja Jenerali Raphael Mugoya Muhuga
   Amiri Jeshi Mkuu  Rais Jakaya Kikwete akimtunuku nishani  ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Jeshi la Wanachi wa Tanzania  JWTZ Meja Jenerali Joseph Furaha Kapwani

  Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ baada ya kuwatunuku nishani katika sherehe zilizofanyika kwenye ukumbi wa Jenerali Kiwelu wa Chuo cha Mafunzo ya Maafisa wa Jeshi Tanzania, Monduli, Septemba 6, 2014. Kulia kwake ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jeneral Davis Mwamunyange.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue katika sherehe za kutunuku nishani zilizofanyika kwenye ukumbi wa Jenerali Kiwelu wa Chuo cha Mafunzo ya Maafisa wa Jeshi Tanzania, Monduli, Septemba 6, 2014.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ baada ya Rais Jakaya Kikwete kutunuku nishani katika sherehe zilizofanyika kwenye ukumbi wa Jenerali Kiwelu wa Chuo cha Mafunzo ya Maafisa wa Jeshi Tanzania, Monduli, Septemba 6, 2014. Kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa na wapili kushoto ni waziri Mkuu Mstaafu John Maelecela. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  RATIBA ya msiba wa Ruth KASHASHA:

  Tutaaga kuanzia saa 6 mchana leo Jumapili, September 7, 2014 hapa nyumbani kwangu Segerea mwisho.

   Mazishi yatafanyika kesho Jumatatu, yatatanguliwa na Ibada ya kumuombea marehemu ktk kanisa Katolki la St. Peter's Oysterbay saa 7:00 mchana na baadaye kuelekea makaburi ya K'ndoni kwa mazishi saa 9 mchana. 

  Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake litukuzwe.

  0 0


  Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma.


  Kanuni za Bunge Maalum hususani Kanuni ya 77 inawataka waandishi wa habari kuandika habari za Bunge Maalum kwa weledi mkubwa na kuzingatia maadili ya uandishi wa habari ili kujiepusha na uandishi wenye utashi na ushabiki wa kisiasa, msukumo binafsi, chuki ama uchochezi na wakati mwingine uongo wa makusudi.

  Aidha, katika Kanuni hiyo hiyo ya 77(3) inatamka bayana ya kuwa “Katibu anaweza wakati wowote kuondoa ruhusa aliyotoa kwa mwakilishi wa Chombo chochote cha habari iwapo chombo hicho kitatoa taarifa yoyote kuhusu shughuli za Bunge Maalum ambayo kwa maoni ya Bunge Maalum inapotosha ukweli au vinginevyo inakiuka Kanuni, taratibu au haki za Bunge Maalum”.

  Vyombo vya habari vina haki ya kupata habari ili viweze kuhabarisha umma juu ya mambo mbalimbali yanayoendelea nchini has katika Bunge Maalum la Katiba, lakini katika kufanya hivyo waandishi wa habari wanapaswa kutenganisha kati ya siasa na uandishi wa habari, hivyo wanapaswa kubainisha na kuainisha dhana ya uandishi wa habari za kibunge wenye tija kwa taifa ambayo ni weledi katika uandishi wa habari, uelewa kuhusu matarajio ya wananchi pamoja na uelewa juu ya dhima na dhamira ya Bunge katika taifa.

  Uandishi wa habari ni vema usitumiwe kama njia ya kufikia malengo ya kisiasa ama mtu binafsi, makundi au chama na kitendo cha mwanasiasa kuvaa koti la uandishi wakati ni mwanasiasa kunajenga chuki, kunaharibu heshima ya uandishi wa habari na maisha ya waandishi.

  Endapo siasa zitaingizwa katika uandishi wa habari basi kuna hatari ya kuilisha jamii yetu uongo. Mfano, kifungu cha 25 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kinavyotafsiriwa kisiasa.


  0 0

   Mstafa Yahaya mmoja wa washiriki wa Shindano la Dance 100% wa Kundi la “Tatanisha Dancers” la Mabibo  jijini Dar es Salaam,akiwaongoza wenzake katika mazoezi yao ikiwa ni sehemu ya  kujiandaa na nusu fainali ya shindano hilo litakalofanyika Septemba 13 mwaka huu  kwenye  Viwanja vya Don Bosco Oysterbay. Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
   Mshiriki wa shindano la Dance 100% Isyaka Ramadhan wa Kundi la”Tatanisha Dancers” la Mabibo jijini Dar es Salaam,akiwaongoza wenzake katika mazoezi yao ikiwa ni sehemu ya  kujindaa na nusu fainali ya shindano hilo litakalofanyika Septemba 13 mwaka huu kwenye viwanja vya  Don Bosco Oysterbay. Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
   Washiriki wa shindano la dance 100% wa kundi la”Tatanisha Dancers” Mabibo jijini Dar es Salaam,wakiwa mazoezini kujiandaa kwa mchuano wa nusu fainali ya shindano hilo lililoandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania litakalofanyika Septemba 13 mwaka huu  kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay .
   Mshiriki wa shindano la  Dance 100% wa kundi la”Tatanisha Dancers” la Mabibo jijini Dar es Salaam Mstafa Yahaya akionesha umahiri wake wa kudansi wakati wa mazoezi yao ya  kujindaa na nusu fainali ya shindano hilo litakalofanyika Septemba 13 mwaka huu kwenye viwanja vya  Don Bosco Oysterbay. Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania. 
  Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu(kushoto)akiongea na baadhi ya washiriki wa Dance 100% wa Kundi la Tatanisha Dancers wa Mabibo jijini Dar es Salaam, wakati alipowatembelea kambini kwao Mabibo,wanakojiandaa na nusu fainali ya shindano hilo litakalofanyika Septemba 13 mwaka huu kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay.Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.

  0 0


  Chama cha Ujenzi wa Taifa cha NRA ,(National Reconstruction Alliance); kinatoa salamu za pole/rambirambi kwa Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mhe Jakaya Kikwete, Waziri za Uchukuzi, Mkuu wa mkoa wa Mara na Wafiwa kwa ajali mbaya ya Basi iliyopelekea kupotea kwa maisha ya watanzania zaidi ya 40, akiongea kwa njia ya simu akiwa katika ziara ya kikazi mkoani  kigoma Naibu KATIBU MKUU NA KATIBU MKUU wa BODI ya chama Mhe Hassan Kisabya (pichani) , ametoa salamu hizo kwa niaba ya Chama chake.

  Mhe kisabya amesema, amepokea kwa masikitiko na mstuko Mkubwa taarifa za ajali hiyo,na kuongeza kuwa ,ajali ni miongoni kwa majanga makubwa kitaifa yanayopoteza maisha ya watanzania na kuwaomba madereva kuwa waangalifu wakati wate ili kuokoa nguvu kazi ya taifa.
  Pia ,amewataka walinzi wa usalama barabarani kuongeza juhudi ili kuzuia ajali hizo.
  Mhe Hassan Kisabya, Amewataka wafiwa kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu na kuacha wahusika kufanya kazi Yao ya uchunguzi wa ajaili hiyo KISHERIA.
  Mhe kisabya,pia amezitaka kampuni husika za mabasi kuhakikisha wanaajiri madereva wenye sifa ili kuifanya huduma hii ya usafiri wa mabasi kuwa kimbilio la wengi kwa kuwa njia hii Ndio imekuwa nafuu na haraka na inawafaa watu wa hali zote.
  Katika salamu hizo, mhe kisabya ameomba watanzania hususani wasafiri kutoa taarifa kwa vyombo husika pale wanapokuwa na mashaka na uendeshaji wa dereva wawapo safarini ili kuwa msaada kwa  wasimamizi wa usalama wao,hasa tukizingatia ulinzi na usalama ni jukumu letu sote(ibara ya 26(1),(2) ya katiba ya Tanzania ,1977),pia UTII WA SHERIA BILA SHURUTI unatutaka kuwajibika  na kuifanya Tanzania kuwa mahala salama.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Chifu Kishosha Mabiti (wa tatu kutoka kulia) akimwonesha Mwenyekiti wa Jopo la Majaji kwa ajili ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji Prof. Samwel Wangwe (wa pili kutoka kushoto) ramani ya kijiolojia ya mkoa huo mara timu hiyo ilipomtembelea ofisini kwake.
  Mkuu wa wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza Mhe. Mariam Lugaila (mbele kwa mbali) akizungumza na jopo la majaji na sekretarieti kwa ajili ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji iliyomtembelea ofisini kwake kabla ya kuanza zoezi hilo katika wilaya yake.
  Afisa Madini Mkazi wa Bariadi Bw. Nyaisara Mgaya ( wa pili kutoka kushoto) akimwonesha Mwenyekiti wa Jopo la Majaji kwa ajili ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji Prof. Samwel Wangwe (kulia) moja ya aina ya mawe yenye madini ya ulanga kwenye ofisi za kampuni ya utafutaji wa madini hayo ya African Eagle Resource Ltd.
  Mtaalamu kutoka katika kampuni ya Kassco Limited inayojihusisha na madini ya ujenzi Bw. Japhes Gerase (kulia) akielezea mchango wa kampuni yake katika ukarabati wa shule ya msingi ya Ntende (inayoonekana pichani) majaji, sekretarieti na wajumbe waliofanya ziara katika shule hiyo.
  Mtaalamu kutoka katika kampuni ya Kassco Limited inayojihusisha na madini ya ujenzi Bw. Japhes Gerase (kulia) akionesha moja ya kisima kilichochimbwa na kampuni hiyo kwa ajili ya wakazi wa kijiji cha Ntende mbele ya timu ya majaji na sekretarieti iliyotembelea visima hivyo kama moja ya ufanyaji ya tathmini ya miradi iliyofadhiliwa na kampuni hiyo.
  Mmoja wa wajumbe wa timu ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji Mhandisi Moses Ndalahwa (kushoto) akiwahoji vijana wa kijiji cha Ntende kuhusiana na mchango wa makampuni ya madini ya ujenzi katika kijiji hicho.

  0 0


older | 1 | .... | 562 | 563 | (Page 564) | 565 | 566 | .... | 3285 | newer