WASANII TUSIWE WATU KULAUMIWA KILA WAKATI! BALI KUSHAURIWA,
WASANII LAZIMA WAANGALIE KWA MAKINI MIKATABA NA MUDA KUTUMBUIZA
Baada ya vyombo vya habari kuandikia kwa wingi tukio la fujo zilizotokea wikiendi ya 30.Augost 2014 katika show ya mwanamuziki Diamond, Blog ya jamii na timu ya Michuzi Media imefanya juhudi za kutaka kusikia maoni na mtazamo wa mwanamuziki wa Tanzania aliyeupigania muziki wa Tanzania katika soko la ughaibuni kwa miaka 21 si mwingine bali ni Kamanda ras Makunja wa FFU
au Ngoma Africa Band.
Michuzi media ilianza kwa swali ?: Ras Makunja nini mtazamo wako kwa
Yaliyotokea Stuttgart.?
Kamanda Ras Makunja: " Kwanza nianze kwa kuwapa pole wale wote waliopatwa na usumbufu na maumivu yawe ya mwili,hisia au hali kutokana na tukio lile,kwa kweli tuliposikia tulistuka sana sana" ,Ras Makunja alisema.
Kwa kuwa sisi sote tunajua ugumu wa msanii anapokuwa On Tour hususan ugenini ,kuna taarifa za awali ambazo msanii ni vigumu sana kuzipata,taarifa ambazo ,pengine zinaweza kumsaidia msanii kwa namna moja au nyingine,kwa kweli msanii anapokuwa ugenini ni sawa na usiku wa kiza.Ras Makunja alisisitiza
Tunacho shukuru Mungu pamoja na yote yaliyotokea pale hatukusikia kama kuna mtu aliyepoteza uhai,maana uhai ni zawadi ya Mola kwa viumbe wake.
Wito wangu kwa wadau na washabiki kwa kuwa nyinyi ndio ma-boss zetu,na sisi wasanii au wanamuziki ni watumishi wenu,ningewaomba msichoke kuunga mkono mara mnaposikia msanii au mwanamuziki,au bendi inapiga sehemu fulani,Kwa sababu Chereko Chereko na mwenye mwana.
Fujo zilizotokea pale Stuttgart kila moja kasoma katika vyombo vya habari na nyinyi ndio mahakimu,lakini mimi si msemaji wa upande wowote pale bali kama msanii ningeomba msimuhukumu msanii kwa kosa la mtu mwingine.
MICHUZI MEDIA : Unawashauri nini wanamuziki wenzako kutoka nyumbani wanaokuja kutumbuiza ?
Ras Makunja: Ushauri wangu nimeshausema mara nyingi katika vyombo vya habari kuwa, Wasanii wa nyumbani lazima wanapopata mikataba waipeleke kwa mameneja na mwanasheria ili isomwe na kueleweka kipengele kimoja baada ya kimoja mfano: taratibu za malipo cash au? na muda wa kulipwa kabla au baada ya show: Hotel,Bima ,VAT,Ulinzi na Kingine muhimu ambacho mara nyingi ndicho chanzo cha mizozo ni malipo na muda wa kutumbuiza hili lazima liwe wazi tena ndani ya mkataba,Mfano show inaanza saa 4 usiku hadi 7.usiku basi lilwe wazi.
Unajua kuna baadhi ya mapromota wanapenda sana kutufanya wasanii kuwa mashine, mara nyingi wanavunja utaratibu "anakuweka hoteli na yeye anasubiri watu wajae ukumbini au wanunue vinywaji kwanza ,sasa
watu wakishalewa unategemea nini? ni fujo tu lakini kama mkataba unaeleza time ya kutumbuiza na mwisho wa show,ata kama kuna watu wawili msanii anatumbuiza.
"WASANII WA AFRIKA MASHARIKI WAPENDWA SANA ULAYA"
Ras Makunja alisema baada miaka 21 ya kupigania soko na moyo wa wadau na washabiki wa sanaa za Afrika Mashariki sasa sanaa zetu zimeshika soko na baadhi ya wasiopenda maendeleo wanatutazama kwa macho ya makengeza !
Wasanii lazima tuangalie sana sana nani wa kufanya nae kazi,katika music Industry kuna baadhi ya watu wanamfanya msanii ni kipande cha ndimu "anakamua na kutupa ganda"
Msanii anapata tabu kujenga jina kwa miaka,eti promota anataka kulibomoa kwa dakika usipokubaliana na yake,lazima wasanii wajichunge sana.
Wasanii wa Afrika Mashariki tunawapa wakati mgumu wapinzani wetu,na wapinzani wetu wanajua vema kuwa pia sisi ni wakarimu hapo ndipo wanapojaribu kutumaliza na ukarimu wetu.
Nawashauri wasanii wezangu wale wanaokuja ujerumani,kabla hujasafiri jaribu kuwasiliana na umoja wa waTanzania Ujerumani(UTU) email yao hii kamati.utu@googlemail.com ili upate information muhimu,hakuna
atakaye kuingilia katika biashara au mkataba wako lakini ushauri ni muhimu.
Pia lazima tujijue kuwa kwa sasa tunatishia soko na tayali lipo mikononi mwetu kwa maana hii wapinzani wanajaribu kujifanya wao ndio mapromota lazima tujipange na kutambua nani wa kufanya nae kazi na kwa makubaliano yepi.
Habari za uhakika tunazo kuwa mwaka 2015 wasanii wa Afrika Mashariki ndio wanaotakiwa kwa wingi hapa ughaibuni,tumieni nafasi hiyo.
KARIBUNI SANA KATIKA SOKO LA UGHAIBUNI NA MKIPATA NAFASI ZA
KUTUMBUIZA LAZIMA MKAMUE BILA YA HURUMA.
Asanteni, pia nawashukuru sana Michuzi Media kwa kunipa nafasi.