Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 553 | 554 | (Page 555) | 556 | 557 | .... | 3348 | newer

  0 0


  The State University of Zanzibar (SUZA) in collaboration with Eastern and Southern African Management Institute (ESAMI) is inviting qualified applicants to join Master of Business Administration (MBA) evening program to be run at SUZA - Vuga campus located at Stone town starting this academic year (2014/2015).

  This evening course is specifically designed for managers from the public institutions, NGOs and private sectors executives who have full time job responsibilities but can afford to attend an advanced management education on evening. The course is designed to accommodate a mix of professionals with various backgrounds, who manage business entities from various companies, factories and hospitals just to mention a few; as well as public servants, Members of Parliament and entrepreneurs. The program will be run jointly by experienced academics from ESAMI and Tanzania.

  Classes will run from 5.00 pm to 10.00 pm for two weeks in every three months, for a period of two years.

  Total fee for the 2-year degree program is US$7,000, (i.e. US$3,500 per year). Application form and further information can be obtained in the University website www.suza.ac.tz or by collecting a hardcopy at our University premises of Vuga and Tunguu during working hours.

  The application deadline is 25th September, 2015 at 4.00 p.m.

  You may call a Dean - School of Continuing and Professional Education (SCOPE) through his mobile phone 0777 – 667748 directly or send an email to hassan.ali@suza.ac.tz OR hassanrashidali@yahoo.com OR scope@suza.ac.tz for more information.

  The State University of Zanzibar is one of the most preferred and vibrant universities in the region offering over 30 programs. For details of these programs please visit http://www.suza.ac.tz.

  Please be hurry to apply as there is limited number of applicants for this program.

  0 0

  Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akiongea na waandishi wa Habari huku akiwaasa kuacha chuki katika masuala yanayohusu mchakato wa Katiba.
  Mjumbe wa Kamati Namba Nne ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Christopher Ole Sendeka akiongea na wandishi wa Habari kuhusu kazi na majukumu ya Kamati yake leo 28 Agosti, 2014.
  Mjumbe wa Kamati Namba Tatu ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Dkt. Francis Michael akiongea na wandishi wa Habari kuhusu kazi na majukumu ya Kamati yake leo 28 Agosti, 2014.
  Mjumbe wa Kamati Namba Moja ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Ummy Mwalimu Ally akiongea na wandishi wa Habari kuhusu kazi na majukumu ya Kamati yake leo 28 Agosti, 2014.
  Mjumbe wa Kamati Namba Kumi na Moja, Mhe. Hamad Massauni akiongea na wandishi wa Habari kuhusu kazi na majukumu ya Kamati yake leo 28 Agosti, 2014. (Picha zote na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma)

  0 0

  Mheshimiwa Dk. Binilith Mahenge Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira ametoa rai kwa Wananchi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla kuweka juhudi katika kupambana na changamoto za mabadiliko ya Tabia Nchi.

  Alitoa rai hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar-es-salaam kuhusu mkutano wa Mawaziri wa Mazingira na Mambo ya Nje kutoka nchi za kamati ya wakuu wa nchi za Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika jijini Dar-es -salaam katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere Tarehe 29 Agosti 2014.

  Alisema kuwa Tanzania imeandaa mkutano wa Mawaziri wa Mazingira na mambo ya nje kutoka nchi za kamati ya wakuu wa nchi za Afrika kuhusu tabia nchi lengo likiwa ni kutoa mwongozo wa namna ya kushughulikia changamoto na mabadikiko ya tabianchi na namna ambavyo nchi za Afrika zitavyoweza kunufaika na rasilimali zinazotolewa na nchi zilizoendelea ili kukabiliana na mabadiliko hayo.

  Mkutano huo ambao utakuwa ni mwendelezo wa juhudi za viongozi wa Afrika katika kushughulikia na kutoa mwongozo wa namna ya kukabiliana na athari za Mabadiliko ya tabia nchi ambazo zimeendelea kuliathiri Bara la Afrika na Dunia kwa ujumla.

  Anasema kuwa joto la dunia limeongezeka kutokana na kuongezeka kwa gesi joto kama vile hewa ukaa ambayo inatokana na shughuli mbalimbali za uzalishaji na matumizi ya nishati, viwanda na usafirishaji.

  "Mabadiliko haya ya tabianchi yanaathiri zaidi watu ambao ni maskini zaidi na wengi ni wale waishio bara la Afrika.Hivyo basi nchi za Afrika zinahitaji rasilimali fedha za kutosha ili kukabiliana na madhara hayo ambayo yanatokana na Mabadiliko ya tabianchi" Alisema Dk.Mahenge.

  Aliongeza kuwa mkutano huo utajadili zaidi mambo yanayoathiri kwa kiasi kikubwa Mazingira , hivyo utapendekeza masuala muhimu kwa bara la Afrika hasa upatikanaji wa fedha na tekinolojia katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko hayo barani Afrika.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais –Mazingira Mh. Dk. Eng. Binilith Satano Mahenge (kushoto), akiwa pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya makamu wa Rais, Bwana Sazi Saula wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano utakaofanyika jijini Dar es Salaam Tarehe 29 Agosti 2014 .
  Sehemu ya waandishi wa habari wakisikiliza hotuba inayotolewa na Mheshimiwa Dk. Eng. Binilith Satano Mahenge (hayupo pichani).

  0 0

  Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo ya Mabadiliko ya Tabianchi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Pius Yanda (wa pili kushoto) akifungua Mafunzo ya uwezeshaji kuhusu mabadiliko ya Tabianchi na athari zake kwa walimu wa somo la Jiografia kutoka Manispaa ya Kinondoni. Kushoto ni kiongozi wa walimu wanaopata mafunzo Mwl. Nesta Mwamfupe. Mafunzo hayo ya siku mbili yanafanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
  Walimu wa Shule za Msingi Manispaa ya Kinondoni wakisikiliza muwezeshaji wakati wa mafunzo ya uwezeshaji kuhusu mabadiliko ya tabia nchi kwa walimu wa Jiografia, mafunzo yanaratibiwa na Kituoa cha Mafunzo ya Tabianchi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
  Kielelezo cha mafunzo kuhusu ongezeko la gesi joto duniani.

  0 0

   Meneja Mkuu msaidizi wa Biolands(Kulia) akimkabidhi na kupongezana  na Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mh. Magreth Ester Malenga ufunguo wa Gari la Wagonjwa katika Sherehe zilizofanyika kwenye viwanja vya Halmashauri ya Wilaya Kyela.
   Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mh. Magreth Malenga akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Gari la Wagonjwa walilokabidhiwa na kampuni ya Biolands , akisaidiwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt. Seif Mhina 
   Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mh. Magreth Ester Malenga  akifungua Mlango wa Gari la Wagonjwa Kuashiria Uzinduzi.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Na Faki Mjaka - Maelezo Zanzibar

  Jumuiya ya Maradhi yasiyo Ambukiza Zanzibar (Z-NCDA) inatarajia kuzindua Kampeni ya Uchunguzi wa Maradhi ya Kansa ya Shingo ya Kizazi Agosti 30-31 mwaka huu.

  Uzinduzi huo utafanyika katika Kituo cha Afya Mpendae mjini Zanzibar ambapo Wanawake wenye dalili za Maradhi hayo watafanyiwa uchunguzi bure kituoni hapo.

  Akizungumza na Waandishi wa habari Ofisini kwao Mpendae, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Ali Mansour Vuai amesema lengo la uchunguzi huo ni kuisaidia Serikali katika mapambano dhidi ya Ugonjwa huo hatari ambao ni vigumu kujua dalili zake.

  Amezitaja dalili za Saratani ya Shingo ya Kizazi kuwa ni pamoja na Maumivu makali sehemu ya kiuno hadi mapajani pamoja na kutokuwa na mpangilio maalum wa Hedhi.

  Dalili zingine ni kutokwa na Damu wakati wa tendo la ndoa, kutokwa na maji maji Ukeni yanayowasha kwa muda mrefu na kujiskia maumivu makali wakati wa tendo la ndoa.

  Mwenyekiti Ali amewaomba Wanawake ambao watakuwa na moja kati ya dalili hizo waweze kufika Mpendae ili kufanyiwa uchunguzi zaidi. Amesema Jumuiya yao itakapogundua Muathirika wa Tatizo la Kansa ya Shingo ya Kizazi watamsaidia kwa kumkutanisha na Madaktari wa Mnazi mmoja au Muhimbili ili kusaidiwa matibabu ya Afya yake.

  “Zanzibar kumefanyika uchunguzi wa magonjwa mengi ikiwemo Kansa lakini hakujawahi kufanyika Uchunguzi wa Kansa ya Shingo ya Kizazi kwa Wanawake..hili ni tatizo ambalo linawamaliza wanawake wengi ndio maana Jumuiya ikaamua kufanya kazi hiyo” Alisema Mwenyekiti Ali.

  Kwa upande wake Katibu wa Z-NCDA Ali Zubeir amesema ni Vyema watu wakajenga mazingira ya kupima afya zao mara kwa mara hasa ikizingatiwa kuwa baadhi ya Magonjwa ikiwemo Saratani ya Shingo ya Kizazi huchukua muda mrefu kabla ya kumuathiri mgonjwa.

  Amesema kwa vile maradhi hayo huathiri sana sehemu za siri wameandaa mazingira mazuri ambayo mgonjwa atafanyiwa uchunguzi wake na Wataalamu Wanawake ili kulifanya zoezi hilo kuwa rahisi kwao.

  Katibu huyo amesema malengo yao ni kufanya uchunguzi wa Kansa ya Shingo ya kizazi katika kila Jimbo Zanzibar, lakini kwa sasa hawana pesa za kugharamia Uchunguzi huo na kwamba wanaishukuru Asasi ya Kiraia ya nchini Denmark kwa kuchangia jumla ya Shilingi Milion 7 na nusu kwa ajili ya zoezi hilo.
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maradhi yasiyo Ambukiza Zanzibar (Z-NCDA) Ali Mansour Vuai katikati akizungumza na Wanahabari (hawapo pichani) kuhusu kuzindua Kampeni ya Uchunguzi wa Maradhi ya Kansa ya Shingo ya Kizazi itakayofanyika Agosti 30-31 mwaka huu Mpendae mjini Zanzibar.
  Katibu wa Jumuiya ya Maradhi yasiyo Ambukiza Zanzibar (Z-NCDA) Ali Zubeir kushoto akizungumza na Wanahabari (hawapo pichani) kuhusu kuzindua Kampeni ya Uchunguzi wa Maradhi ya Kansa ya Shingo ya Kizazi itakayofanyika Agosti 30-31 mwaka huu huko Mpendae mjini Zanzibar. 

  0 0

  Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya Oilcom imezindua promosheni ya jishindie mtungi wa gesi, ambapo wateja wa Vodacom watakaojaza mafuta kwa huduma ya M-pesa kwenye vituo vya kampuni ya mafuta ya Oil Com watajishindia mtungi wa gesi.

  Akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hii leo katika kituo cha Oilcom cha mtaa wa Libya jijini Dar es Salaam ,Meneja Uhusiano wa Masuala ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim,alisema kuwa promosheni hii imewalenga watumiaji wa mafuta ya magari watakaojaza mafuta kwenye magari yao kwa kutumia huduma ya M-pesa.

  “OilCom ni moja ya makampuni ambayo yalijiunga katika mtandao wa M-pesa siku chache zilizopita na tunashirikiana nao katika promosheni hii ambapo wateja watakaojaza mafuta katika vituo vya mafuta vya Oilcom vilivyopo mtaa wa Libya,Kipawa na TMJ wataingia kwenye promosheni hii ambapo droo itakuwa ikifanyika mara moja kwa wiki na mshindi atakayekuwa ameweka mafuta mengi kwenye gari kwa kutumia huduma ya M-Pesa atajishindia mtungi wa gesi wa O-Gesi wenye thamani ya shilingi 52,500”Alisema Mwalim.

  Mwalim alisema kwamba promosheni hii itadumu kwa kipindi cha miezi mitatu kwa kuanzia itafanyika katika kituo cha mafuta cha Oilcom cha mtaa wa Libya na mwezi utakaofuata itafanyika katika kituo cha Oilcom cha Kipawa na itamalizikia katika kituo cha mafuta cha Oilcom TMJ.

  Kwa upande wake Meneja wa maswala ya kompyuta wa kampuni ya OilCom Abubakar Mwita,ameishukuru kampuni ya Vodacom kwa kubuni promosheni hii ambayo inahamasisha wateja wa mafuta kutumia huduma ya M-pesa na kuwapunguzia usumbufu wa kutembea na hela mfukoni wanapohitaji kujaza mafuta kwenye magari yao.

  Alisema tangu OilCom izindue huduma ya wateja wao kulipia mafuta kwa njia ya M-pesa watumiaji wa huduma hii wamekuwa wakiongezaka siku hadi siku na kuifurahia kwa kuwa inawarahisishia maisha na kuwaondolea usumbufu “Tuko mbioni kuhakikisha vituo vyetu vyote vya mafuta viwe na huduma ya kulipia kwa M-Pesa”.Alisema Mwita.

  Hivi karibuni kampuni ya Vodacom Tanzania na Oilcom ziliingia ubia ambapo wateja wa pande zote mbili wamewezeshwa kulipia mafuta kwa kupitia huduma ya M-Pesa popote kwenye vituo vya kampuni hiyo ya mafuta. Mpaka sasa huduma hii iko katika vituo vya mafuta vya TMJ Msasani,Kipawa na Oilcom kilichopo mtaa wa Libya na upo mkakati unaoendelea kuhakikisha vituo vyote vya Oilcom nchi nzima vinakuwa na huduma ya kulipia kwa M-Pesa.
  Meneja Uhusiano wa Masuala ya Nje wa Vodacom Tanzania,Salum Mwalim akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu promosheni mpya ya jishindie mtungi wa gesi kwa kujaza mafuta kwa Mpesa inayoendeshwa na Vodacom kwa kushirikiana na kampuni ya mafuta ya Oil Com,kulia ni Menaja Msaidizi wa kituo cha Oilcom mtaa wa Libya jijini Dar es Salaam Abubakar Kaburu ,Katikati ni Meneja wa masuala ya kompyuta na ufundi wa Oil com,Abubakar Mwita.
  Meneja Msaidizi wa kituo cha Oilcom mtaa wa Libya jijini Dar es Salaam Hussein Kaburu kulia pamoja na Meneja Uhusiano wa Masuala ya Nje wa Vodacom Tanzania,Salum Mwalim wakionesha moja ya mtungi wa O-Gas utakaoshindaniwa katika promosheni mpya ya jishindie mtungi wa gesi kwa kujaza mafuta kwa M-pesa inayoendeshwa na Vodacom kwa kushirikiana na kampuni ya mafuta ya Oil Com,kushoto ni Meneja wa masuala ya kompyuta na ufundi wa Oil com,Abubakar Mwita(kushoto)
  Meneja Uhusiano wa Masuala ya Nje wa Vodacom Tanzania,Salum Mwalimo(kushoto) pamoja na Meneja wa masuala ya kompyuta na ufundi wa Oil com,Abubakar Mwita. Wakionesha waandishi wa habari hawapo pichani moja ya mtungi ambayo itakuwa inatolewa kwa washindi wa promosheni mpya ya jishindie mtungi wa gesi kwa kujaza mafuta kwa M-pesa inayoendeshwa na Vodacom kwa kushirikiana na kampuni ya mafuta ya Oil Com.

  0 0

  Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania- Dubai, leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Iran ya Dubai, Dr. Asghar Fashad. Katika mazungumzon hayo, Mhe. Mjenga alimuomba Dr asghar kuangalia uwezekano wa kuwa na makubaliano kati ya hospitali yake na Ubalozi Mdogo kwa ajili ya kutoa huduma za afya kwa Watanzania kwa gharama nafuu ukilinganisha na gharama zake za sasa.

  Baada ya mazungumzo na mashauriano ya muda wa saa moja, Uongozi wa Juu wa Hospitali, ulikubali ombi la Mhe. Mjenga la kupunguza gharama za matibabu kwa Watanzania kwa asilimia 40 (40%). Mwanzo, Uongozi ulipendekeza asilimia 20, ambayo Mhe. Mjenga aliwaeleza kuwa bado ilikuwa ni punguzo dogo na bado ingekuwa ni mzigo mkubwa kwa Watanzania. Hatmaye, ndio maafikiano hayo yakafikiwa ya asilimia 40.

  Mpango wa huu utajumuisha Watanzania wote waishiyo UAE na wale wanaoishi nje ya UAE ikiwa ni pamoja na wale wanaoishi Tanzania. Hospital ya Irani ni moja ya hospitali zenye huduma za hali ya juu kwa hapa Dubai na UAE kwa ujumla.

  Uongozi wa Hospitali umekubali kuanza kutoa Vitambulisho Maalum kwa ajili ya Watanzania wote kuanzia Jumapili tarehe 1 Septemba. Mkataba wa Makubaliano haya utatiwa saini Jumatatu tarehe 2 Septemba.

  Aidha, Mhe. Mjenga, amemuomba Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hii, kuangalia uwezekano wa kujenga Hospitali kubwa yenye hadhi kama hii, nchini Tanzania. Kimsingi, Mkurugenzi Mkuu amekubali ombi hili, na ameahidi kumuomba Rais wa Hospitali kufanya ziara nchini Tanzania mwezi ujao ili kuona na uongozi husika na kuanza mazungumzo ya kuanzisha Hospitali kama hiyo. Ameeleza kuwa Tanzania na Iran na nchi marafiki wa siku nyingi, na hivyo Iran inafarijika sana kuwa karibu na Tanzania kimahusiano.
  Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania- Dubai akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Iran ya Dubai, Dr. Asghar Fashad pamoja na ujumbe wake wakati alipowa
  Mhe. Omar Mjenga akiwa akiwa katika picha ya pamoja na mwenyeji wake Dk. Asghar Fashad.

  0 0
 • 08/28/14--09:06: TAARIFA YA MSIBA
 • Ndugu Timothy Kulewa wa Manchester Uingereza, anasikitika kutangaza kifo cha Mke wake Maryam Nassoro Jaffuru kilichotokea juzi 26/08/2014 kwa Ajali ya gari Morogoro akitoken safarini mwanza. Mazishi yanafanyika kesho Ijumaa 29/08/2014 saa Tisa alasiri katika Makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam, Baada ya Misa itakayofanyika Kanisa la kilutheri Mbezi Beach ( Tangi Bovu) saa Saba mchana.

  Bwana ametoa Bwana ametwaa Jina lake lihidimiwe.

  0 0

  Wiki hii imekuwa njema kwa mustakabali wa jimbo la Darfur ambalo kwa muda mrefu limeshuhudia mgogoro wa wenyewe kwa wenyewe. Hizi ni taarifa za kujumuishwa kwa waasi wa zamani wa kikundi cha JEM-SUDAN kwenye jeshi la kitaifa nchini Sudan kufuatia hatua ya kikundi hicho kutia saini makubaliano ya Doha kuhusu amani Darfur.

  Kwa mujibu wa Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika huko Darfur, UNAMID umesema hilo ni kundi la kwanza kutoka takribani askari 2700 ambao hatimaye watajiunga na jeshi la kawaida.

  Kufuatia hatua hiyo Joseph Msami wa idhaa hii amezungumza na Mkuu wa vikosi vya UNAMID Luteni Jenerali Paul Mella na kwanza amenza kumuuliza wamepokeaje hatua hiyo.

  (SAUTI MAHOJIANO)
  Kusikiliza bofya hapo chini

  0 0

  Na Faki Mjaka Maelezo Zanzibar

  Wizara ya Afya Zanzibar imekabidhi kifaa cha THERMAL SCANNER kwa ajili ya kuchunguza Wagonjwa wa EBOLA watakao ingia nchini kutoka mataifa mengine.

  Kifaa hicho kilichowekwa katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume kitatumika kwa ajili ya kuwachunguza zaidi Wageni ambao watatoka katika nchi zilizoathiriwa na Ugonjwa wa Ebola.

  Akikabidhi kifaa hicho Mkuu wa kitengo cha kufuatilia mwenendo wa Maradhi Zanzibar Dkt Salma Masauni amesema THEMO SKAN kitasaidia katika kuwabaini watu ambao wameathirika au kuwa na dalili za Ungojwa wa Ebola na kuchukuliwa hatua zaidi.

  Dkt Salma amesema iwapo mgonjwa atabainika hatua zaidi zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kupelekwa katika kituo cha Afya cha Chumbuni ambacho kimetayarishwa kwa ajili hiyo.

  Aidha Dkt Salma amefahamisha kuwa Kituo cha Afya cha Chumbuni kimetengwa kama eneo litakalotumika kwa ajili ya Matibabu kwa mgonjwa atakayebainika kuambukizwa Ugonjwa wa Ebola nchini.

  Amesema Wizara ya Afya katika kukabiliana na Ugonjwa huo wa kuambukiza imekuwa ikifanya Jitihada mbalimbali za kutoa elimu na njia mbali mbali za kinga kabla ya Zanzibar kuathirika na Ebola.

  Amesema licha ya Vifaa hivyo vilivyotolewa Vifaa vingine vitakuja wiki inayokuja ili viendelee kutumika katika maeneo ya Bandarini na Viwanja vya ndege Unguja na Pemba

  Dkt. Salma amesema Ugonjwa huo haujaingia nchini bali Serikali inajiandaa na juhudi zake za kukabiliana na Ugonjwa huo ili usiweze kuingia na kuathiri Zanzibar.
  Mkuu wa kitengo cha kufuatilia mwenendo wa Maradhi Zanzibar Dkt Salma Masauni akionesha Kifaa “THERMAL SCANNER” kwa Wafanyakazi wa Kituo cha Afya cha Uwanja wa ndege wa Zanzibar. Kifaa hicho kitatumika kusaidia kuwabaini Wagonjwa wa EBOLA watakao ingia nchini kutoka mataifa mengine.
  Mkuu wa kitengo cha kufuatilia mwenendo wa Maradhi Zanzibar Dkt Salma Masauni na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji Zanzibar wakionesha baadhi ya Vifaa Vitalavyotumika kuwachunguza Wagonjwa wa EBOLA watakao ingia nchini kutoka mataifa mengine.
  Mkuu wa kitengo cha kufuatilia mwenendo wa Maradhi Zanzibar Dkt Salma Masauni akionesha matumizi ya Kifaa cha “THERMAL SCANNER” kwa Wafanyakazi wa Kituo cha Afya cha Uwanja wa ndege wa Zanzibar. Kifaa hicho kitatumika kusaidia kuwabaini Wagonjwa wa EBOLA watakao ingia nchini kutoka mataifa mengine.

  0 0

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM.


  STAILI ile ile waliyotumia Yanga SC kumpata mshambuliaji Emmanuel Arnold Okwi ndiyo ambayo klabu yake ya zamani, Simba SC inaitumia kumrejesha kundini Mganda huyo.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari jioni hii mjini Dar es Salaam, Okwi amesema kwamba amesaini Simba SC mkataba huru wa muda, baada ya Yanga SC kumpa barua ya kusitisha mkataba naye jana pamoja na kumshitaki Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).


  Okwi amesema ameamua kuomba kuichezea Simba SC kipindi hiki ambacho ana matatizo na Yanga SC ili kulinda kipaji chake, kwa kuwa hata FIFA haitaki mchezaji akae bila kucheza.

  Msimbazi ni nyumbani; Okwi akiwa na jezi ya Simba SC baada ya kurejea timu yake ya zamani leo  “Sasa wakati Yanga wanaendelea na kesi yao, mimi ninaomba nichezee Simba SC ili kulinda kipaji changu. Nimewaandikia barua TFF na FIFA pia na nina matumaini usajili wangu utaidhinishwa, kwa sababu mimi si tatizo katika hili,”amesema.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba wamemsaini mchezaji huyo baada ya kupitia kwa kina suala lake na Yanga SC na kugundua haki ipo upande wa mchezaji.
  “Baada ya kulipitia suala lake na Yanga kwa undani kabisa na vielelezo ambavyo mchezaji mwenyewe ametupatia, tumejiridhisha tuko sahihi kumsaini ili acheze mpira kunusuru kipaji chake kipindi hiki ambacho ana matatizo na Yanga SC,”amesema Poppe.  

  Yanga mtanikoma; Okwi akiwa ameshika jezi yake nbamba 25 kwa pamoja na Hans Poppe  Tayari Simba SC imetuma jina la mchezaji huyo katika usajili wake TFF na ataungana na Mganda mwenzake, Joseph Owino, Warundi Pierre Kwizera na Amisi Tambwe na Mkenya, Paul Kiongera katika wachezaji watano wa kigeni. 
  “Tumewaandikia barua TFF kuomba kumtumia mchezaji huyu kwa muda wakati kesi yake na Yanga inaendelea, tumeambatanisha na barua yake ambayo yeye anatuomba kucheza kwetu kulinda kipaji chake,”amesema Poppe.  Okwi aliichezea Simba SC tangu mwaka 2009 kabla ya Januari mwaka jana kuuzwa kwa dola za Kimarekani 300,000 Etoile du Sahel ya Tunisia. Etoile haikulipa fedha hizo Simba SC na baadaye ikaingia kwenye mgogoro na Okwi, aliyedai hakulipwa pia mishahara yake kwa miezi mitatu. Okwi akawafungulia Etoile kesi FIFA na akaomba wakati mgogoro wao unaendelea, aruhusiwe kuchezea timu yoyote kulinda kipaji chake, ndipo akajiunga na SC Villa ya kwao.

  Akiwa SC Villa ndipo aliposaini Yanga SC Desemba mwaka jana na pamoja na mapingamizi yaliyoanzia ndani, na baadaye klabu yake, Etoile- lakini Okwi aliidhinishwa kuichezea timu hiyo ya Jangwani.  Okwi aliichezea Yanga SC mechi 11 na kuifungia mabao matano- lakini kuelekea mechi tano za mwisho za Ligi Kuu msimu uliopita akaingia kwenye mgogoro na klabu hiyo. Okwi alisusa kushinikiza amaliziwe fedha zake za usajili na mgogoro wao umeendelea huku mchezaji huyo akiwa amesusa tangu Machi, miezi minne tu baadaye tangu asajiliwe.  Vikao kadhaa vimekwishafanyika baina ya Okwi na Yanga SC tangu hapo kutafuta suluhu ya suala hilo na kikao cha mwisho leo baina ya mchezo huyo na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Manji matokeo yake ni nyota huyo kurejea Msimbazi.  Kuhusu deni lao la dola 300,000 kumuuza mchezaji huyo Etoile, Poppe amesema haihusiani kabisa na usajili wake huu wa sasa. “Ile kesi yetu ya madai ya fedha zetu kule FIFA ilikwishamalizika na vielelezo vyote vilipelekwa, bado kutolewa hukumu tu,” amesema. 

  0 0

  Na Mwene Said wa Blogu ya Jamii 


   Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Nchini (TBS), Charles Ekelege amehukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwenda jela miaka mitatu na kuilipa serikali Dola 42,543 za Kimarekani, baada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka kwa kutoa asilimia 50.


  Kadhalika, Ekelege anadaiwa kutoa asilimi hiyo ya  punguzo la tozo ya utawala kwa Kampuni mbili  Kampuni ya Jaffar Mohamed Ali Garage na Kampuni Quality Motors na kulisababishia shirika hilo hasara ya dola hizo.

  Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi  Augustina Mmbando baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili na mahakama yake kumuona mshtakiwa bila kuacha shaka ana hatia.

  Hakimu alisema ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri ulieleza mahakama kwamba mshtakiwa kupitia wadhifa wake alifanya maamuzi bila kinyume na sheria za TBS zinazomwelekeza kuwasilisha masuala yote ya kiutendaji kwenye Bodi ya Wakurugenzi.

  Alisema kitendo cha kutoa msamaha kwa kampuni hizo bila kuacha shaka moja kwa moja mahakama imeona alitumia madaraka yake vibaya.

  “Kwa upande wa  shitaka la pili, kiongozi yeyote katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anapokuwa madarakani ni kwa ajili ya maslahi ya taifa, lakini mshtakiwa alikosa uzalendo na kutumia madaraka yake vibaya kuhujumu uchumi” alifafanua hakimu kuhusu ushahidi wa Jamhuri.

   “Mahakama inamuona mshtakiwa ana hatia katika kosa hili la pili la kujumu uchumi … pia mshtakiwa amesababisha watanzania waliompa dhamana kukosa kula keki ya taifa lao kwa kujinufaisha yeye binafsi” alisema hakimu huyo na kuongeza kuwa.

  “Katika ushahidi uliotolewa na mshtakiwa alikiri kufanya maamuzi bila kupata baraka na kibali cha Bodi ya Wakurugenzi na kwamba aliidanyanya mahakama” alisema Hakimu Mmbando.

  0 0


  0 0

  Dear All,

  We are writing to remind you about the DICOTA 2014 Convention – themed “Empowering Tanzanian Diaspora for Socio-Economic Transformation: At Home and Abroad” – to be held at the Millennium Hotel Durham, 2800 Campus Walk Avenue, Durham NC 27705, U.S.A. from 2nd to 5th of October, 2014. We have 34 days before the Convention and only 20 days before the early Bird discounted registration fee ends.
   
  Ambassador Ombeni Sefue, the Chief Secretary is the Guest of Honor
   
  The convention brings together members of the Tanzanian Diaspora in the United States America, Tanzanian private sector and government officials; key decision makers from Tanzania and U.S. businesses; financial institutions, and international organizations with vested interest in investment and growth in the country. 

  The conference presents attendees with the latest trade and investment opportunities in all sectors of the economy, while providing a forum for potential partnership formation through many networking opportunities. Based on this year’s theme, all topics and discussion will be centered towards empowering ourselves for Socio-Economic transformation abroad and in Tanzania. Among the invitees, H.E. Amina Salum Ali, the African Union Ambassador to the United States confirmed to be with us and deliver a Keynote Speech for the second day of the convention. 

  If you are considering to be one of the sponsors for the DICOTA 2014 Convention, Click here for the details on sponsorship opportunities. Please plan to attend this extraordinary Convention. Click here to register, early Registration with Great discount Ends September 18, 2014. For more Information about Convention Registration, Hotel Discount Ratesand Program visit us at www.dicotaus.org. You can also contact us by email dicota@dicotausa.orgor call 1-952-217-0265 to reach a convention steering committee representative. For hotel reservation with special rates for the convention, click here.
   
  Looking forward to seeing you all in Durham, North Carolina.
   
  With Kind Regards,
   
  Dr. Ndaga Mwakabuta,
  DICOTA President.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakwanza kushoto akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi pamoja na Mbunge wa Kongwa ambaye pia ni Naibu Spika Job Ndugai wakifurahia mara baada ya Rais kuweka jiwe la Msingi Ujenzi wa Barabara ya Mbande-Kongwa 16.5Km .
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi, Mbunge wa Kongwa ambaye pia ni Naibu Spika Job Ndugai, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Profesa Juma Kapuya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe, akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa barabara ya Mbande-Kongwa 16.5Km.
  Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma pamoja na kikundi cha ngoma za asili cha Kibaigwa kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuhutubia mamia ya Wakazi wa Kibaigwa.
  Sehemu ya barabara Mbande-Kongwa 16.5Km ambayo ujenzi wake umewekwa jiwe la Msingi.
  Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kulia akizungumza na Mbunge wa Kibakwe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa George Simbachawene huku Mbunge wa Kongwa ambaye pia ni Naibu Spika Job Ndugai akishuhudia kushoto.
  Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akizungumza na Mbunge wa Kongwa ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Profesa Juma Kapuya(kulia) kabla ya uzinduzi wa barabara ya Mbande-Kongwa 16.5Km.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya uzinduzi na ufunguzi wa barabara ya Mbande-Kongwa 16.5Km.
  Viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Ujenzi pamoja na Taasisi zake wakimsubiri Rais Dkt. Jakaya Kikwete kuzindua rasmi mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Mbande-Kongwa 16.5Km. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi

  0 0

  Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu wa Maafa imesema itawatumia Wataalam waliopo katika Ngazi ya Kata katika Mradi wa kuzijengea uwezo jamii wa kuzuia, kupunguza na kukabiliana na maafa yanayotokana na ukame. Kauli mbiu ya Mradi huo ni “Athari za Ukame Zinapunguzika, Jamii ikielimishwa.”

  Akiongea wakati wa Mafunzo juu ya Utekelezaji wa Mradi huo kwa Wataalam wa Sekta ya Kilimo, Mifugo, Afya, Elimu na Utawala wa kata ya Hedaru, Makanya na Vunta, Wilayani Same, Mratibu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wa Mradi huo Bw. Harrison Chinyuka alifafanua kuwa lengo la Mafunzo hayo ni kuwajengea Uwezo wataalam hao wa kutambua viashiria na vihatarishi vinavyoweza kusababisha maafa ili waweze kutoa elimu sawia kwa vikundi vinavyotekeleza mradi huo katika kata zao.

  “Kutokana na mabadiliko ya Tabia Nchi yameleta athari nyingi ikiwemo ukame, kupitia mradi huu ulioanza kutekelezwa kwa majaribio katika Wilaya ya Same hasa katika Kata ya Hedaru, Makanya na Vunta, hivyo wataalam kupitia mafunzo haya wataweza kuvieimisha vikundi vya kata zao husika juu ya kuzuia, kupunguza na kukabiliana na maafa yanayotokana na ukame.” Alisema Chinyuka.

  Chinyuka alifafanua kuwa Wataalamu hao katika ngazi ya kata ndio waratibu katika kuijengea jamiii uwezo wa kukabiliana na kupunguza vihatarishi vinavyoweza kusababisha maafa ya ukame kwakuwa Wataalam hao hutoa mafunzo kwa wadau kuhusu matumizi ya mbegu na pembejeo za kilimo, mifugo na misitu pamoja na upatikanaji wa maji safi na salama kwa matumizi ya binadamu na mifugo.

  Wakitoa mada wakati wa mafunzo hayo Wakufunzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika walibainisha kuwa Wataalam katika Sekta ya Kilimo, Mifugo, Afya, Elimu na Utawala wa kata ya Hedaru, Makanya na Vunta wanalo jukumu la kuelimisha jamii juu ya matumizi ya Taarifa za Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini pamoja na Umuhimu wa Tathmini ya Hali ya Chakula na Lishe Nchini katika kata zao.

  Akiongea wakati wa kufunga mafunzo hayo Afisa Mtendaji Kata Hedaru, Bw. Jackson Mbwambo alibainisha kuwa mafunzo hayo yamewajengea uwezo wataalam wa ngazi ya kata wa kuweza kupunguza athari za maafa ya ukame na kuahidi kushiriki kikamilifu katika kuijengea jamiii uwezo wa kukabiliana na kupunguza vihatarishi vinavyoweza kusababisha maafa ya ukame katika kata zao.

  Mikoa ya Kilimanjaro na Shinyanga ndio inayotekeleza mradi huo, wilaya zinazoshiriki katika mradi huo ni pamoja na Same, Hai na Mwanga kwa mkoa wa Kilimanjaro na Wilaya za Kishapu, Shinyanga Vijijini na Shinyanga Mjini kwa mkoa wa Shinyanga.

  Mradi Wa Kuijengea Jamii Uwezo Wa Kupunguza Athari Za Maafa Kwa Mikoa Iliyoathirika Zaidi Na Ukame umefadhiliwa na Benki ya Dunia na kusimamiwa na UNICEF chini ya Uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Halmashauri husika wakiwa Watendaji Wakuu wa Mradi huo. Mradi huo unatekelezwa kwa kipindi uliozinduliwa Wilayani Same, mkoani Kilimanjaro tarehe 11 Desemba2013.
  Baadhi ya Wataalam katika Sekta ya Kilimo, Mifugo, Afya, Elimu na Utawala wa kata ya Hedaru, Makanya na Vunta Wilayani Same, wakinukuu masuala muhimu wakati wa mafunzo ya jinsi ya kutekeleza Mradi Wa Kuijengea Jamii Uwezo wa kupunguza Athari Za Maafa katika kata zao, mafunzo hayo ya muda wa wiki moja yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu wa Maafa.

  0 0

  Mwenyekiti wa Mtandao wa Mashirika yanayofanya kazi na Watoto Tanzania ambaye pia ni Mratibu Miradi, Kituo cha Watoto wa Mtaani cha Dogodogo Kigogo (Dogodogo Centre Street Children Trust), Sabas Masawe. Mwenyekiti wa Mtandao wa Mashirika yanayofanya kazi na Watoto Tanzania ambaye pia ni Mratibu Miradi, Kituo cha Watoto wa Mtaani cha Dogodogo Kigogo (Dogodogo Centre Street Children Trust), Sabas Masawe.

    MCHAKATO wa kujadili na kuandika Katiba Mpya unaendelea bungeni mjini Dodoma, licha ya kuwepo kwa mvutano na mgawanyiko wa makundi ya wabunge wa bunge maalumu wanaojadili Rasimu ya Pili iliyowasilishwa kwao. 

  Wakati hayo yakiendelea viongozi, wanaharakati na wadau wa watoto wanapendekeza masuala ya haki za msingi za watoto yatambulike vizuri katika katiba ijayo.

   Mwenyekiti wa Mtandao wa Mashirika yanayofanya kazi na Watoto Tanzania ambaye pia ni Mratibu Miradi, Kituo cha Watoto wa Mtaani cha Dogodogo Kigogo (Dogodogo Centre Street Children Trust), Sabas Masawe anashauri ibara ya 43 ambayo inataja haki za msingi za watoto iendelee kuwepo mpaka Katiba inakamilika na iboreshwe zaidi katika mchakato unaoendelea Bungeni.

   Nasema haya maana tayari kuna baadhi ya watu wameanza kuhoji kwamba kwanini hata watoto wanaingia kwenye katiba ilhali wao ni sehemu ya watu kama wazazi wao. Anasema pamoja na kuingizwa kipengele cha mtoto kwenye rasimu ya pili ya katiba bado kuna mambo ambayo wao kama wadau wangependa yaingizwe tena hivi sasa katika mchakato wa majadiliano unaoendelea.

   Anasema baadhi ya mambo hayo ni kama umri wa mtoto mwenyewe kutaja wazi kwamba ni kuanzia umri gani. "...Unaweza ukaangalia hili ni suala la msingi sana kutaja umri wa mtoto mwenyewe anayezungumziwa...kwa sisi wadau wa watoto tunashangaa sana kwa maana nyingine tunaona suala hilo ni kama linaongeza utata, kumuweka mtoto kwenye katiba ilhali umeshindwa kumtambua (kiumri) mtoto ni yupi ni sawa na vichekesho...tunashauri mtoto huyu umri utajwe wazi kuondoa utata...," anasema. 

   Mfano ukisema wazee wana haki ya kutibiwa bure lazima useme huyu mzee anaanzia umri gani na kuishia wapi. Huwezi kusema wazee watibiwe bure alafu unashindwa kuainisha vitu vya muhimu kama umri wao, bila hivyo utaleta mkanganyiko wa tafsiri...ndiyo maana hata sasa mtoto anayetajwa tunataka tujue anaanzia umri gani na kuishia umri gani. Sasa hili pekee linatushangaza watu wasomi wanajadili bila kuliona hili.Mkuu wa Mkoa wa Tabora Fatma Mwasa akizungumza na mwandishi wa makala haya. 
  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Fatma Mwasa akizungumza na mwandishi wa makala haya.

   Huyu mtoto akiingia kwenye mgongano katika sheria anashughulikiwa namna gani kwasababu hili linaweza kuwa na mgongano kama pia litashindwa kutajwa kwenye katiba chombo ambacho ni sheria mama ya nchi. Masawe anasema mambo mengine ambayo yanatakiwa kuainishwa ni pamoja na kuelekeza namna ya kuwawajibisha wazazi ambao wamekuwa wakikimbia majukumu yao ya kulea watoto na kuwapeleka katika vituo vya yatima eti kwa madai wamewashinda.


  0 0

  Majaji Bw. Venance Bahati (kushoto) na Bi. Costansia Gabusa (kulia) wakijadiliana jambo wakati wa kufanya tathmini ya mradi wa ukingo uliojengwa pembezoni mwa bahari kwa ajili ya kuzuia mmomonyoko katika eneo la Mwarongo jijini Tanga. Ukingo huo umejengwa kwa msaada wa kampuni ya utafutaji wa mafuta na gesi ya Afren PLC.
  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Tongoni Bw. Mzihili Abeid (kushoto) akitoa maelezo mbele ya majaji waliotembelea maabara ya shule hiyo. Maabara hiyo imejengwa na kampuni ya utafutaji wa mafuta na gesi ya Afren PLC.
  Msimamizi wa kampuni ya utafutaji wa mafuta na gesi ya Afren PLC Bw. Ahmed Omar (kulia) akizungumza na jopo la majaji na sektretarieti kwenye maabara ya shule ya sekondari ya Tongoni iliyofadhiliwa na kampuni hiyo.
  Jaji Venance Bahati (katikati) akiteta jambo na msimamizi wa kampuni ya utafutaji wa mafuta na gesi ya Afren PLC Bw. Ahmed Omar (kulia). Kushoto ni Jaji Costansia Gabusa.
  Msimamizi wa kampuni ya utafutaji wa mafuta na gesi ya Afren PLC Bw. Ahmed Omar (kushoto) akizungumza na majaji walipotembelea maabara ya Shule ya Sekondari ya Mabokweni jijini Tanga ambapo kwa sasa kampuni hiyo imejitolea kuwajengea maabara ya kisasa.
  Mkurugenzi wa kampuni ya Dawson Food Products Ltd iliyopo wilayani Mkinga mkoani Tanga Bw. Burhani Taibali (kulia) akizungumza na majaji pamoja na sekretarieti iliyotembelea kampuni hiyo.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki Mkombozi Commercial, Edwina Lupembe akiongea na waandishi wa habari waliofika katika hafla ya benki hiyo kufikisha miaka mitano tokea imeanzishwa. Aliongeza kuwa benki hiyo ilianzishwa kwa lengo la kutoa huduma za kibenki sanjari na kushughulika na matatizo ya kiuchumi kwa jamii katika nyanja mbalimbali.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Edwina Lupembe akikazi msisitizo mbaye ya waandishi wa habari.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki Mkombozi Commercial, Edwina Lupembe akiwatambulisha mbele ya wageni waalikwa na wafanyakazi, watoto wanaosomeshwa na benki hiyo.

older | 1 | .... | 553 | 554 | (Page 555) | 556 | 557 | .... | 3348 | newer