Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live

JESHI LA POLISI MKOA WA RUVUMA LAWASHIKILIA ASKARI WAKE WAWILI

$
0
0
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo Msekhela
--------------------------------------------------
Na Nathan Mtega,Songea

JESHI la polisi mkoani Ruvuma linawashikilia askari wake wawili kwa tuhuma za kumjeruhi kwa kumpiga risasi mwendesha piki piki aliyejulikana kwa jina la Salgo Ndunguru(22) mkazi wa Ruvuma mjini Songea.

 Akizungumza kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo Msekhela amesema tukio hilo limetokea Agosti 26 mwaka huu majira ya saa 12 jioni katika mtaa wa Mfaranyaki mjini Songea ambapo askari polisi wawili PC Waziri mwenye namba G 5075 na PC Ayoub mwenye namba G 9800 wakiwa doria na piki piki ya polisi yenye namba za usajili PT 1250 CR aina ya Yamaha CC 250 katika eneo hilo la Kombezi walimjeruhi mwendesha piki piki huyo kwa kumpiga risasi.

 Amesema mwendesha piki piki huyo alijeruhiwa kwa kupigwa risasi na askari PC Waziri katika harakati za kuinsuru silaha hiyo iliyokuwa imebebwa na askari mwenzake PC Ayoub ambaye alizingirwa na baadhi ya waendesha piki piki wakiongozwa na mwendesha piki piki aliyejulikans kwa jina moja la Agrey ambaye alidai kuwa yeye ndiye mmiliki wa piki piki iliyokamatwa na askari hao ikiwa imebeba mzigo wa majiko.

 Ameitaja piki piki iliyokuwa ikiendeshwa na majeruhi huyo kuwa ni aina ya San Lug yenye namba za usajili T 757 CUD ambapo baada ya mwendesha piki piki huyo kukamtwa alimpigia simu mdhamini wake Agrey alipofika alisababisha mkusanyiko mkubwa wa waendesha piki piki maarufu kama Yebo yebo ambao walianza kuwarushia mawe askari hao huku majeruhi akiwa ameshika mtutu wa bunduki iliyokuwa imebebwa na askari PC Ayoub ndipo askari PC Waziri katika kuinusuru silaha isiporwe alimpiga risasi majeruhi kwenye kiganja cha mkono wa kushoto na risasi hiyo kumjeruhi sehemu mbili ambazo ni kiganja cha mkono wa kushoto na paja la mguu wa kushoto.

 Amesema majeruhi amelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma iliyopo mjini Songea kwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri na katika vurugu hizo zilizodumu kwa muda wa nusu saa kabla ya kutulizwa na kikundi cha askari maalumu kilichowahi na kutuliza vurugu hizo kwa kutumia nguvu kidogo hali ikarejea kuwa shwari na hakuna madhara zaidi yaliyojitokeza.

 Aidha kamanda Msikhela amesema uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo unaendelea ili kubaini chanzo halisi cha tukio hilo unaendelea na hatua zitachukuliwa dhidi ya wahusika watakaothibitika na ametoa wito kwa waendesha piki piki kuacha tabia ya kushabikia vurugu ambazo hazina tija na kuwa chanzo cha kusababisha migogoro isiyokuwa na maana na kusababisha madhara kwa jamii.

 Amewataka waendesha piki piki kufuata taratibu zilizopo ikiwa ni pamoja na kuwasilisha malalamiko yao kwa viongozi husika kwa kupitia viongozi wao ili yaweze kufanyiwa kazi amewataka wananchi mkoani Ruvuma kuwa watulivu na kuendelea na shughuli zao bila hofu yoyote kwani jeshi la polisi liko imara kulinda mali na maisha yao.

OFISI YA WAZIRI MKUU YAENDELEA KUTOA MAFUNZO YA KUPUNGUZA ATHARI ZA MAAFA YA UKAME KATIKA NGAZI YA KATA, WILAYANI SAME

$
0
0
Mtakwimu, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Bw. Vilerian Kidole akifafanua juu ya Umuhimu wa Tathmini ya Hali ya Chakula na Lishe Nchini kwa Wataalam kutoka kata za Hedaru, Makanya na Vunta wakati wa mafunzo yanayoendelea Hedaru, Wilayani Same juu ya jinsi ya kutekeleza Mradi Wa Kuijengea Jamii Uwezo wa kupunguza Athari Za Maafa katika kata zao.
Mkuu wa Huduma za Hali ya Hewa kwa Jamii, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Bi. Hellen Msemo akisisitiza juu ya Umuhimu wa Kutumia Taarifa za Mamla ya Hai ya Hewa nchini katika Kupunguza Athari za Maafa kwa Wataalam wa kata za Hedaru, Makanya na Vunta (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Tarehe 25 Agosti, 2014, Hedaru, Wilayani Same (katikati) katika mafunzo yanayoendelea Hedaru, Wilayani Same juu ya jinsi ya kutekeleza Mradi Wa Kuijengea Jamii Uwezo wa kupunguza Athari Za Maafa katika kata zao.
Mratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Jane Alfred akieleza jinsi jamii inavyoweza kukabili Maafa kwa Wataalam wa kata za Hedaru, Makanya na Vunta (hawapo pichani) katika mafunzo yanayoendelea Hedaru, Wilayani Same juu ya jinsi ya kutekeleza Mradi Wa Kuijengea Jamii Uwezo wa kupunguza Athari Za Maafa katika kata zao.
Baadhi ya Wataalam katika Sekta ya Kilimo, Mifugo, Afya, Elimu na Utawala wa kata ya Hedaru, Makanya na Vunta wakinukuu masuala muhimu katika mafunzo hayo yanayoendelea Hedaru, Wilayani Same juu ya jinsi ya kutekeleza Mradi Wa Kuijengea Jamii Uwezo wa kupunguza Athari Za Maafa katika kata zao.

Rais Kikwete azindindua mradi wa ujenzi wa Barabara ya Magole-Turiani –Mziha

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Profesa Juma Kapuya akiweka jiwe la Msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa ujenzi wa Barabara ya Magole-Turiani –Mziha sehemu ya Magole-Turiani (48.6km) inayojengwa kwa kiwango cha lami.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe, mbunge wa Mvomero Amos Makalla, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Profesa Juma Kapuya akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa ujenzi wa barabara ya Magole-Turiani (48.6km).
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale akitoa maelezo ya kina kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu ujenzi wa Barabara ya Magole-Turiani (48.6km).
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wa kwanza kulia akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe kabla ya uzinduzi rasmi wa ujenzi wa barabara ya Magole-Turiani (48.6km) kwa kiwango cha lami.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Profesa Juma Kapuya wakifurahia jamabo na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mheshimiwa Antony Mbasa kabla ya uzinduzi wa Barabara ya Magole-Turiani (48.6km).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kushoto wakifurahia kikundi cha ngoma za asili mara baada ya Mheshimiwa Rais kuwasili Wilaya ya Mvomero kwa ajili ya kuzindua ujenzi wa Barabara ya Magole-Turiani (48.6km).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe wa kwanza (kushoto) akizungumza kabla ya uzinduzi rasmi wa barabara ya Magole Turiani. Wa kwanza kulia kwake ni Mkurugenzi wa Barabara kutoka Wizara ya Ujenzi Mhandisi Ndyamukama pamoja na Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi na Umeme Dkt. Wiliam Nshama.

VIONGOZI WA TAKUKURU WAKUTANA KILIMANJARO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU unaofanyika katika ukumbi wa Kuringe.
Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Dk Edward Hosea akizummza wakati wa Mkutano wa mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU .
Mkurugenzi wa idara ya elimu TAKUKURU ,Marry Mosha akitoa neno la shukurani mara baada ya mgeni rasmi kufungua mkutano huo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

CHUO CHA DIPLOMASIA CHAWANOA MAAFISA KUTOKA JESHI, SERIKALINI NA SEKTA BINAFSI

$
0
0
Katika kuendeleza wajibu wake wa kutoa mafunzo ya muda mfupi, Chuo cha Diplomasia kimeendesha mafunzo ya juma moja ya Itifaki na Uhusiano ‘PROTOCOL AND PUBLIC RELATIONS’ kati ya tarehe 18 – 22 August, 2014. Mafunzo haya yalilenga kuwaongezea uwezo maafisa mbali mbali kutoka serekalini na sekta binafsi. Mafunzo haya ni muendelezo wa mafunzo  ya muda mfupi yatolewayo na Chuo cha Diplomasia kila mwezi, 

katika mafunzo hayo ambayo Kwa kawaida wawezeshaji wa mafunzo hayo ya muda mfupi katika Chuo cha Diplomasia, huwa ni mabalozi na wakufunzi waliobobea katika mambo ya Diplomasia na hivyo kuwapa washiriki uzoefu na mafunzo ya kiutendaji zaidi ili kuwajengea uwezo na ufanisi katika kuboresha majukumu yao. 
 PICHA YA WASHIRIKI WAKIWA NA BALOZI SANGA ‘mwenye Kaunda suti katikati’

Mafunzo hayo yalihusisha maofisa wa kada mbalimbali kutoka idara za Serikali, Chuo cha Ardhi, Jeshi la Wananchi, Magereza, Ubalozi wa Uingereza, na sekta binafsi kama Benki Kuu ya Tanzania, SMART TANZANIA (Telecom), SERENA HOTEL, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Chuo cha Utalii Tanzania,  Idara ya Uhamiaji, Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Umoja wa Mataifa (UN),

Mafunzo hayo ya juma moja yaliyofanyika Kurasini Dar es salaam, washiriki walijifunza jinsi ya kuratibu itifaki za dhifa, sherehe za kitaifa na mikutano mingine mbali mbali. Pia walijifunza Diplomasia, uhuisiano wa umma na namna bora ya kuandaa taarifa kwa ajili ya mawasiliano na umma.
Picha ya Pamoja.

Akifunga mafunzo hayo, Mkuu wa Idara ya Utafiti, Uchapishaji, Ushauri na Kozi fupi, Bw. Juma M. Kanuwa alisisitiza kwamba mafunzo hayo yatawasaidia maofisa hao kuboresha utendaji wa kazi zao.

“Kazi zinazohusiana na itifaki na uhusiano wa umma (Protocol and Public Relations) zinahitaji utaalam ambao utamfanya mtu aweze kutimiza majukumu yake kwa ufasaha na kufikia malengo na matokeo mazuri. Hivyo mafunzo haya ya Itifaki na mengine yote yanayotolewa na Chuo cha Diplomasia yana lengo la kuwajengea uwezo na utaalam washiriki wote ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi na kupata matokeo bora,” alisema.
Akaongeza kuwa, kutokana na uhitaji mafunzo haya  yatarudiwa tena Zanzibar mnamo mwezi wa kumi, yakifuatiwa na ‘INTERNATIONAL SECURITY AND ARMS CONTROL,  FRENCH LANGUAGE na DATA COLLECTION AND ANALYSIS (Using SPSS,SQL and STATA) hapa chuo cha Diplomasia, na kuwataka wale wote wanaohitaji wafike chuoni ama kupiga namba 0713667303 au cfrshortcourse@yahoo.com kwa maelezo zaidi na kupewa utaratibu.

East African Legislative Assembly Session Opens in Dar es salaam

$
0
0
The East African Legislative Assembly (EALA) commenced its 1st Meeting of the 3rd Session of the 3rd Assembly Wednesday  afternoon at the Karimjee Hall in Dar es Salaam. The Speaker of the Parliament of Tanzania, Rt. Hon Anna Makinda remarked that Integration was key and called for concerted efforts to ensure it remains people centred.

“I salute the good work of EALA over the last 13 years when it comes to sensitizing the people of East Africa”, Rt. Hon Makinda remarked. She noted that Parliament of Tanzania was committed to the integration process and termed the recent ratification of the Monetary Union Protocol as a unique example and case in point.  The United Republic of Tanzania is the first country in the EAC region to ratify the Protocol.

Rt. Hon Makinda termed some of the engagements with EALA as the Inter-Parliamentary Games and the Inter-Parliamentary Relations Seminar (Nanyuki) series where Tanzania and other legislators engage and exchange ideas on integration. The Speaker noted that Parliaments in the region had established specific committees to address regional integration matters. She however cited the need to forge closer mechanisms between the two Parliaments.

“We need to find ways to strengthen and effectively communicate about integration for the sake of the citizens”, Rt. Hon Makinda stated. She also reiterated that EALA was now a trailblazer in legislative matters in the continent. 

“I am pleased to note that Pan-African Parliament (PAP), Southern Africa Development Co-operation Parliamentary Forum (SADC-PF) and the ECOWAS Parliament are emulating EALA’s modes and its mandate”, the Speaker said. She remarked that Karimjee Hall where the EALA is meeting was historic having being the location where the Parliament of Tanzania held its legislative business until 20 years ago (1995).

In her remarks, the Speaker of EALA, Rt. Hon Dr. Margaret Nantongo Zziwa stated that Parliament had a key role to play in strengthening integration. The Speaker noted that both EALA and Parliament of Tanzania had continued to foster relations.

“I am confident that the Parliaments shall continue to play a fundamental role in strengthening the integration process through the requisite legislative, oversight and representative framework”, Rt. Hon Zziwa said. She lauded Rt. Hon Makinda for her role in guiding Parliament to greater heights.

“Rt. Hon Speaker, your experience in Parliament goes back several years to 1975 when you were first nominated to the House.  When the annals of history are written, it shall surely be recorded that you were at the helm as the first woman Speaker in the Parliament of Tanzania since the first Speakership of Adam Sapi Mkwawa in 1964” Speaker Zziwa said. 

 In one of the chapters, I am sure it shall also be clearly annotated that in the fullness of time, you were part of the leaders who contributed to a new constitutional dispensation” she added.

The two week Assembly expects to debate on the following Bills and reports:

•           The EAC Integration (Education) Bill, 2014 (2nd & 3rd Reading)
•           receive and consider reports from various Committees of the Assembly.  The Reports include that of the Committee on Regional Affairs and Conflict Resolutions and the African Leadership Centre on East African Societies and Regional Security; Report of the Committee on Agriculture, Tourism and Natural Resources on Regional Parliamentarians’ Workshop on Forests and Climate Change and Report of the Committee on Communication, Trade and Investment on the EAC Aviation Sector.  Other reports include that of the Committee on General Purpose on the capacity building workshop on the legislative process of bills, Report of the Committee on Legal Rules and Privileges and the report of the Committee on Accounts on EAC Audit Process.
•           consider Motions and Questions brought before the House.

The Assembly shall also seize the moment to visit various stakeholders and to sensitise citizens.   Institutions to be visited include the Tanzania Ports Authority on August 29th, 2014 and the Taasisi ya Sanaa na Utamaduni – TASUBA (Institute of Arts and Culture) in Bagamoyo on August 30th, 2014. The visits are expected to enhance the collaboration between EALA and the stakeholders in question.

Last week, EALA paid a courtesy call at the IPP Media where Members held discussions with the Executive Chairman and the Senior Management.
  

 Prayers at the start of the EALA Plenary in Karimjee Hall, Dar es Salaam
 Speaker of the Parliament of Tanzania, Rt. Hon Anna Makinda makes her remarks at the start of the EALA Plenary in Karimjee Hall, Dar es Salaam
The Speaker of EALA, Rt. Hon Zziwa delivers  her remarks
The Speaker of EALA, Rt. Hon Margaret Nantongo Zziwa  leads the procession out of the Chamber as the Speaker of Parliament of Tanzania, Rt. Hon Anna Makinda tags along.

Birthday Wishes to Ankal from Mrs Ankal

$
0
0
Happy birthday to you my better half, my friend, perfect father/daddy to our kids‎. Wish you happiness, wish you success and  contentment in your life. I wish to be there with you but " kazi hizi" I am always thankful to God for you and for every opportunity and everything he has favoured us. His blessings are ever in abundance. I love and  cherish you and will forever do so, in a very special way. Happy birthday.

Mrs Ankal.

introducing francia chengula's new song "Nyumbani ni Nyumbani"


RAIS KIKWETE KATIKA SHEREHE ZA UZINDUZI WA PROGRAMU YA UIMARISHAJI WA MIPAKA YA KIMATAIFA MKOANI KAGERA

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakipokea nyimbo za Taifa za nchi zao eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi wa Tanzania na Burundi katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakiangalia moja ya alama katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. Kushoto kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakizindua kwa pamoja eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.

Balozi Seif Ali Idd akutana na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Tigo

$
0
0
Kampuni ya Mitandao ya simu za Mkononi ya Tigo imejitolea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye sekta ya uwekezaji katika masuala ya mitandao ya mawasiliano sambamba na kusaidia huduma za Kijamii kwa wananchi wa Visiwa vya Unguja na Pemba.

Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo yenye Makao Makuu yake Mjini Stokholmes Nchini Sweeden Bwana Arthur Basting alieleza hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake katika Jengo la Msekwa ndani ya Viunga vya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.

Bwana Arthur Basting ambae anasimamia Kampuni Tigo Barani Afrika alisema Uongozi wa Taasisi hiyo imejikita kutoa ushirikiano huo ikizingatia zaidi umuhimu wa mawasiliano ya Teknolojia yaliopo hivi sasa Ulimwenguni kote.

Bwana Arthur alisema Uongozi wa Kampuni ya Tigo unafurahia kuona kwamba Teknolojia ya Mawasiliano kupitia simu za Mikononi hivi sasa imeenea na kupokelewa vyema na wananchi wa Bara la Afrika.

Naye Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Tigo Hapa Tanzania Bibi Sylvia Balwire alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwamba Kampuni hiyo tayari imeanza mipango maalum ya kusaidia huduma za Kijamii katika maeneo mbali mbali hapa Nchini.

Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliuomba Uongozi wa Kampuni ya Tigo kuongeza nguvu zake zaidi katika kusaidia miradi ya Kijamii ambayo bado inaonekana haijawa na nguvu za kujiendesha yenyewe.

“ Hadi wakati huu tunaozungumza zipo skuli zetu nyingi hazijawa na vikalio, huduma za maabara na Maktaba, hata vifaa katika vituo vyetu vya Afya. Uwepo wenu kama wawekezaji unaweza pia kuyaangalia maeneo hayo muhimu kwa ustawi wa Jamii yetu “. Alisema Balozi Seif.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Tigo yenye makao Makuu yake Nchini Sweeden Bwana Arthur Basting akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Jengo la Msekwa ndani ya Viunga vya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma. Kati kati yao Ni mshauri wa Kampuni hiyo Balozi Ami Mpungwe.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Tigo Bwana Arthur Basting akimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif nia ya Kampuni hiyo ya kutaka kushirikiana na SMZ Katika miradi ya mitandao ya mawasiliano.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Kampuni ya Tigo aliokutana nao kwenye ofisi yake iliyop[o jengo la Msekwa ndani ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano Mjini Dodoma. Kulia ya Balozi Seif ni Makamu wa Rais wa Kampuni ya Tigo Bwana Arthur Basting na kulia yake ni Meneja Uendeshaji wa Tigo Tanzania Bibi Sylvia Balwire, Mshauri wa Kampuni hiyo Balozi Ami Mpungwe na Meneja Mkuu wa Tigo Nchini Tanzania Bwana Diego Gutierrez. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Airtel yazidi kufungua milango ya biashara mikoani

$
0
0
MKUU wa Wilaya ya Bukoba, Mkoani Kagera Bi. Zipora Pangani ameipongeza Kampuni ya Simu za Mkononi Airtel kwa kufungua duka kubwa, ambalo litatoa huduma mbalimbali kwa wateja ikiwemo kutuma na kutoa fedha ya (AIRTEL MONEY).

Akifungua duka hilo lililopo eneo la Mtaa wa Kawawa Mjini Bukoba, alisema litakuwani chachu ya maendeleo, kwa wakazi wa mkoani Kagera ambapo litarahisisha huduma kwa wananachi.

“Ufunguzi wa hili duka hapa kwetu litakuwa ni chachu ya maendeleo kwa wateja wa Air tel na wananchi kwa ujumla hasa kwenye matumizi ya huu mfumo wa air tell money” Alisema Mkuu huyo wa Wilaya.

Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka wakazi wa kagera na maeneo jirani kuhakikisha kwamba wanaitumia hiyo fursa vizuri ili kuhakikisha wanakuza uchumi wao katika ngazi ya familia na taifa kwa ujumla.

Naye Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania alisema ufunguzi wa duka hilo ni mwendelezo wa ufunguzi wa maduka mengine nchi nzima ili kutoa huduma bora kwa wateja wake.

“ Kampuni yetu ya Airtel tuna mpango madhubuti wakuhakikisha maduka yetu yote yanakuwa na mwonekano sawa na kutoa huduma bora zenye kiwango cha hali ya juu kwa wateja wetu kutokana na mahitaji yao” Aliongeza

“ Dhamira yetu ni kuhakikisha tunaendeana na kasi ya uhutaji kwa wateja wetu kwenye mawasiliano ya kisasa na teknolojia, ya hali ya juu” Alisema Mkurugenzi huyo.

Kwa Upande wao wateja wa kampuni hiyo waliojitambulisha kwa majina ya Joseph Kamuntu na Eradius Ernest wakizungumza mara baada ya kufunguliwa kwa duka hilo waliishikuru kampuni hiyo na kwa kuwasogezea huduma hiyo.

“ Tunawashukuru sana hawa watu jamani yaani binafsi nimefurahi sana kupata hii huduma karibu sasa hivi wamefungua nimeingia mara moja nimehudumiwa ni mfano wa kuigwa na makampuni mengine,” Alisema Kamuntu.

Aliyaomba Mkampuni mengine ya simu kuiga mfano wa kampuni ya Airtel kwa kutoa huduma bora ambazo zinamjali mteja ili kuhakikisha maendeleo yanakuwa kwa pande zote.

Kampuni ya Simu za Mkononi Airtel hadi sasa imefungua maduka 11 hapa nchini katika mikoa ya Dar es salaam, Kagera, Dodoma ,Morogoro, Mtwara, Mbeya, lengo likiw ani kuhakikisha wananachi wanapata huduma bora na kwa wakati.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba,Mh. Zipora Pangani akikata utepe kuashiria ufunguzi wa duka jipya la Airtel mkoani Bukoba jana, anaefuata ni Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba (suti nyeusi) na watoa huduma wa duka hilo mkoani hapo wakishudia, duka hilo litakalohudumia wakazi wa mkoa wa Kagera .
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba,Mh. Zipora Pangani akiongea na wananchi na wanahabari waliohudhuria uzinduzi wa duka jipya la Airtel mkoani Bukoba jana, kulia ni Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba (suti nyeusi) pamoja na watoa huduma wa duka hilo mkoani hapo wakishudia, duka hilo litakalohudumia wakazi wa mkoa wa Kagera .
Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba (kushoto) akimuelezwa jambo Mkuu wa Wilaya ya Bukoba,Mh. Zipora Pangani mara baada ya ufunguzi wa duka jipya la Airtel mkoani Bukoba jana.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba,Mh. Zipora Pangani (kati) akikata keki maalum iliyoandaliwa na wafanyakazi wa Airtel huduma kwa wateja Bukoba kwaajili ya hafla ya kusheherekea ufunguzi wa duka jipya la Airtel mkoani hapo. Wakwanza kushoto akishuhudia ni Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Airtel Tanzania Bi Adriana Lyamba na meneja wa duka hilo bukoba bi Anna Mapunda, duka hilo litakalohudumia wakazi wa mkoa wa Kagera .
Picha ya pamoja.

FM ACADEMIA KUTUA ARUSHA KWA KISHINDO KUZINDUA ALBAMU YAO MPYA SEPTEMBER 5 VIWANJA VYA UKUMBI WA TRIPLE A

$
0
0
 wasanii wa bendi ya fm Academia wakiwa jukwaani wanaimba wapili kulia ni Rais wa bendi Nyoshi
Rapa wa bendi  ya Fm Academia akiwa anashambulia jukwaa wakati wa shoo.
wanenguaji wa bendi ya Fm wakiwa kazini  wote hawa watakuwepo katika  uzinduzi huu wa Albamu ya Chuki ya nini usikose ni balaa
Fm  Academia baada ya kukaa kwa muda wa miaka 4 (minne) yaani kuanzia mwaka 2010 mpaka 2013 sasa wanatarajia kuzindua rasmi  album mpya kabisa inayojulikana kwa jina la Chuki ya nini ndani ya jiji la Arusha na vitongoji vyake .

 Album ya chuki ya nini imebeba nyimbo kumi ndani yake,nazo ni:-Chuki ya nini, Fataki ,Otilia ,Ndoa ya kisasa,Neema,Dai chako ulaumiwe,Maisha,Madudu,Miraessa.album ya chuki ya nini ni album yenye kiwango cha kimataifa ambapo nyimbo hizi zote zitazinduliwa rasmi septembar tano mwaka huu ndani ya viwanja vya  ukumbi wa Triple A jijini Arusha

Akizungumza na waandishi  wa habari jijini hapa mkurugenzi wa SB Intamenti Seif Manyota alisema kuwa bendi hiyo inatarajia kutua jijini Arusha kwa kishindo kwa ajili ya uzinduzi huu wa albamu mpya ambapo alibainisha kua tukio hilo litakuwa la kihistoria.

Alisema kuwa  hii ni mara ya kwanza kwa bendi hii  kuzindua albamu  nje ya mkoa wa dar es salaam na kwa hivyo wameamua kuwapa heshima kubwa wapenzi wa bendi hiyo wa mkoa wa Arusha  pamoja na mikoa ya kanda ya kaskazini kwa ujumla hii ikiwa ni heshima ya kipekee.

"uzinduzi huu wa  albamu sio tu tunazindua  nyimbo mpya bali tunazindua pia vyombo vipya na staili mpya za kuicheza gwasuma kama vile mnavyojua bendi ya fm  ni wazee wa pamba wazee wa kushambulia jukwaa"alisema Manyota

Aidha alibainisha kuwa kwa mkoa wa Arusha wameamua kuwapa kipaumbele na pia kwakuwa kunawapenzi wengi wa ngwasuma wameamua kufanya shoo hii nje ambapo ,kutafugwa jukwaa la kisasa  kabisa.

Alitaja baadhi ya nyimbo ambazo zipo katika albamu ambayo inazinduliwa kuwa ni pamoja na Chuki ya nini,ndoa ya kisasa fataki  pamoja na nyinginezo.

Aidha kwa upande  mungine alisema uzinduzi huu autaishia Arusha tu bali wakazi wa Moshi na Tanga nao watapata burudani hii na kuzitambua staili mpya pamoja na nyimbo mpya zilizopo kwenye albamu hii.

Alisema kua pia kutakuwa na CD na DVD za albamu hiyo mpya iliyozinduliwa huku akisema kuwa kwa upande wa Arusha kiingili    akuwa 20000 na unapatiwa CD moja buru mlangoni.

kwa upande wa Rais wa bendi hiyo Nyoshi alisema kuwa timu  yake yote imejipanga vyema kuwapa burudani ya nguvu wakazi wa Arusha  na kuwapa staili mpya ikiwemo ile ya vundesa  ambapo alisema kuwa wameiboresha na imekuwa ya kiufasaha  zaidi  na ina vinjonjo vingi zaidi ,staili tamu  pamoja na maneno matamu.
Alisema kuwa lengola kubwa la kuzindua albaimu hii apa jijini Arusha ni pamoja na kuwaelewesha wapenzi wao nyimbo mpya na kuakikisha wapenzi wao wanajua staili zao zote za  nyimbo hizo na  sio ivyo tu pia alisema kuwa kwa kipindi  hiki wanataka kuwa wakazi wa arusha zawadi ya kuwaletea wasanii wote wa bendi hiyo ambapo alisema wapo 32  na wote watafika jijini Arusha

Vijana wapewa changamoto ya kutumia uzazi wa mpango

$
0
0
Afisa Vijana wa UMATI kutoka Temeke Bibi. Upendo Daud akimkabidhi zawadi ya machapisho kuhusu Afya ya uzazi wa mpango Mwenyekiti wa Mtaa wa Sabasaba ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika Jamvi la Vijana lililofanyika katika mtaa wake. Jamvi la Vijana ni program ambayo inaendeshwa na UMATI kupitia Kituo cha Vijana YAM kutoka Manispaa ya Temeke, Jamvi hilo la vijana limebeba kauli mbiu ya “Kijana ana haki ya juu ya uzazi wa mpango?”
Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Sabasaba wakipata maelezo kuhusu afya ya uzazi wa mpango kutoka kwa waelimisha rika wa UMATI walipokuwa katika Jamvi la Vijana lilioshirikisha Kikundi cha Vijana cha Benki Club kutoka Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam mapema hivi karibuni.
Mmoja wa washereheshaji katika Jamvi la Vijana akimkabidhi mtoto Shani Rajab zawadi ya Jarida la Fema baada ya kujibu swali kuhusu uzazi wa mpango katika Jamvi la Vijana lililofanyika katika mtaa wa Sabasaba na kuhusisha Kikundi cha Vijana cha Benki Club kutoka kata ya Mtoni iliyopo Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam mapema hivi karibuni. Jamvi la Vijana ni program ambayo inaendeshwa na UMATI kupitia Kituo cha Vijana YAM kutoka Manispaa ya Temeke, Jamvi hilo la vijana limebeba kauli mbiu ya “Kijana ana haki ya juu ya uzazi wa mpango?”
Baadhi ya wananchi wakifuatilia igizo kutoka kwa Kikundi cha Vijana cha Benki Club (hakipo pichani) wakati wa Jamvi la Vijana lililofanyika mapema hivi karibuni katika mtaa wa Sabasaba uliopo katika Kata ya Mtoni Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam. Jamvi la Vijana ni program ambayo inaendeshwa na UMATI kupitia Kituo cha Vijana YAM kutoka Manispaa ya Temeke, Jamvi hilo la vijana limebeba kauli mbiu ya “Kijana ana haki ya juu ya uzazi wa mpango?”
Baadhi ya waigizaji wa Kikundi cha Vijana cha Benki Club wakiigiza kuhusu namna ambavyo mwanaume anamshinikiza mke wake abebe mimba mara baada ya miezi michache tokea ajifungue,igizo hilo lilionyeshwa wakati wa Jamvi la Vijana lililofanyika mapema hivi karibuni katika mtaa wa Sabasaba kata ya Mtoni iliyopo Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam. Jamvi la Vijana ni program ambayo inaendeshwa na UMATI kupitia Kituo cha Vijana YAM kutoka Manispaa ya Temeke, Jamvi hilo la vijana limebeba kauli mbiu ya “Kijana ana haki ya juu ya uzazi wa mpango?”
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sabasaba uliopo katika Kata ya Mtoni Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam Bw. Ibrahim Mwita (waliosimama katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kikundi cha Vijana cha Benki Club wakati wa Jamvi la Vijana lililofanyika jijini Dar es Salaam mapema hivi karibuni. Picha zote na Frank Shija, MAELEZO

4TH ANNIVERSARY OF VIJIMAMBO BLOG, PROMOTING TANZANIA TOURISM EXPO IN THE USA

$
0
0
Vijimambo Blog kwa ushirikiano wa pamoja na Ubalozi wa Jamhuri ya Muunagano wa Tanzania ikiwemo Jumuiya ya Watanzania DMV inawaletea miaka 4 ya Vijimambo ikiutangaza Utalii wa Tanzania na kukemea ujangili siku ya September 13, 2014. Njoo ujivunie maliasili na utalii wa nchi yako sote kwa pamoja yunaweza kuitangaza nchi yetu na kukemea ujangili kwa kauli moja yenye nguvu inayosikika kimataifa.
Juu na chini ni Ukumbi wa sharehe ya mchana kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 11 jioni
add ni 3 Reserch  Court, Rockville, MD 20850 na baadae usiku ni Hall la Oxford 9700 Martin Lurthers King Jr HWY, Lanham, MD 20786 kuanzia saa 3 usiku mpaka saa 9 alfajiri
Vyakula vya kitanzania Burudani ya kila aina karibu tuitangaze Tanzania kimataifa. 

Kwa Wajasiliamali watakaopenda kuweka meza zao mwisho wa kujisajili ni Sept 5, 2014 tafadhali wasiliana na wanakamati Baraka Daudi 301 792 8562, Tuma Kaisi 301 433 4311, Iddi Sandaly 301 613 5165, Asha Nyang;nyi 301 793 2833, Mayor Mlima 301 806 8467 na Julius Katanga 202 400 4218

BG Tanzania yawadhamini wanafunzi kumi kupata elimu ya juu ngazi ya stashahada ya uzamili ( Masters of science degree) ya sayansi nchini Uingereza

$
0
0
27 Agosti, 2014, Dar es Salaam, Tanzania–BG Tanzania ilia​ndaa ​hafla kwa ajili ya kuwaaga wanafunzi kumi watanzania wali​o​faulu kupata udhamini wa elimu ya juu ngazi ya stashahada ya uzamili ( Masters of science degree ) ya sayansi kwenye vyuo vikuu nchini Uingereza.

Katika hafla hii, wanafunzi watapata fursa ya kukutana na Meneja Mkuu wa BG Tanzania ( Derek Hudson) pamoja na wafanyakazi na wadau Mbalimbali.

Udhamini huu wa elimu ya juu ni kati ya mpango mkakati wa maendelo ya jamii wa kampuni ya BG Tanzania. Mpango huu unatoa fursa sawa kwa watanzania na taratibu za kutahini na kupata wanafunzi zinafanyika kwa njia ya uwazi na umakini kuhakikisha fursa iliyopo inatolewa kwa wale wenye sifa na kukidhi vigezo. Wanafunzi wote wataenda kusoma kozi zinazohusiana na masuala ya gesi na mafuta kwenye vyuo vya Aberdeen na Robert Gordon.

Mpango huu wa udhamini wa elimu ya juu ulianza mwaka 2012 ambapo wanafunzi 4 hadi sasa wameishafaidi kwenye mpango huu. wanafunzi 2 waliishamaliza masono nakurudi nchini na 2 wanarudi mwishoni mwa mwaka huu.

Kwa kuzingataia umuhimu wa mpango huu, kwa mwaka 2014, BG Tanzania imeongeza udhamini kutoka wanafunzi 4 hadi 10 na idadi hii itaendelea kwa miaka 3.( wanafunzi 30 kufikia 2017) British Council wanatekeleza mradi huu kwa niaba ya BG Tanzania. Ufadhili unaotolewa ni kwa ajili ya ada, usafiri wa kwenda na kurudi, gharama za kuishi, gharama za mafunzo kwa vitendo. Kampuni ya BG itatoa fursa ya wanafunzi kutembelea makao makuu ya BG yaliyoko mji wa Reading- Uingereza ​. ​

Akiongea katika hafra hii, Meneja mkuu wa BG Tanzania, Bwana .Derek Hudson alisema, lengo la udhamini huu ni kuongeza idadi ya Watanzania wenye taaluma ya masuala ya gesi na mafuta nchini. Ni matarajio yetu kuwa, baada ya wanafunzi kumaliza watarudi kusaidia taifa kwa njia moja ama nyingine. BG Tanzania itaendelea kufanya kazi kwa karibu sana na serikali pamoja na wadau wengine kuhakikisha fursa hii inaongezeka iwezekanavyo
Meneja Mkuu wa BG Tanzania,Derek Hudson (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla hiyo ya kuwaaga wanafunzi kumi watanzania wali​o​faulu kupata udhamini wa elimu ya juu ngazi ya stashahada ya uzamili ( Masters of science degree ) ya sayansi kwenye vyuo vikuu nchini Uingereza. Kulia ni Mkurugenzi wa British Council nchini,Bw.Richard Sunderland.
Meneja Mkuu wa BG Tanzania Derek Hudson akiwa na wanafunzi waliodhaminiwa kupata elimu ya juu ya stashahada ya uzamili.

Viongozi wa vyama vya Siasa wakutana kujadili ushiriki wa makundi maalum katika uongozi

$
0
0
Tanzania Center for Democracy (TCD) iliwakutanisha viongozi wa vyama vya Siasa wanachama wa TCD ili kupokea taarifa ya Utafiti wa ushiriki wa makundi maalum katika nafasi za uongozi wa nchi, makundi yaliyojadiliwa ni Wanawake, Vijana na Walemavu ... Mapendekezo na maazimio ya mkutano huo yanafanyiwa kazi na TCD na baadae yatapelewa kwenye vyama kwa ajili ya kutumia Matokeo ya Utafiti huo ili kuongeza ushiriki wa makundi hayo katika uongozi ndani ya vyama na Taifa kwa ujumla!
Kutoka kushoto ni Dr. Alex Makulilo Mtafiti toka UDSM, Mhe. John Mnyika kutoka CHADEMA , Ndg. Phares Magesa (MNEC) kutoka Chama Cha Mapinduzi na kulia ni mwakilishi kutoka NCCR-Mageuzi !

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ziarani nchini Singapore

$
0
0
Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (wa tatu kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mawaziri saba wa Mambo ya Nje wa Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara wakiwa na mwenyeji wa Mkutano huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Singapore Mhe. Kasiviswanathan Shanmugam (wa tano kutoka kushoto).
Mawaziri wa Mambo ya Nje wakiwa kwenye ziara kwenye mojawapo ya vyuo maalum nchini humo Institute of Technical Education ambapo Tanzania inashirikiana nacho kwenye kutoa mafunzo kwa walimu wa VETA.
Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (kushoto) akikata utepe kufungua rasmi ofisi za Ubalozi wa Heshima za Tanzania nchini Singapore akishirikiana na Mhe. S.S. Teo, Balozi wa Heshima. Kulia ni Mhe. John Kijazi, Balozi wa Tanzania nchini India ambaye pia anaiwakilisha Tanzania nchini Singapore.
Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (wa pili kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa kwenye picha ya pamoja na Mhe. John Kijazi (wa kwanza kushoto), Balozi wa Tanzania nchini India ambaye pia anaiwakilisha Tanzania nchini Singapore, Mhe.S.S. Teo, Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Singapore na Balozi Mbelwa Kairuki, Murugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (wa pili kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa kwenye picha ya pamoja na Mhe. Kasiviswanathan Shanmugam, Waziri wa Mambo ya Nje wa Singapore (wa tatu kushoto), Balozi Mbelwa Kairuki na Mhe. John Kijazi, Balozi wa Tanzania nchini India na Singapore.
Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa kwenye mazungumzo na mwenyeji wa Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara Mhe. Kasiviswanathan Shanmugam, Waziri wa Mambo ya Nje wa Singapore.

mambo ya gado leo

IN LOVING MEMORY

$
0
0
THE LATE MRS. ITIKA MWANGASA MWAKILEMA.
(Mama Nkundwe) 28th August 2014

Hours, Days, Months, Years, kept on moving, though with a lot of loneliness and emptiness but we survived the 25 years of sadness since you left us suddenly that 28th August 1989. We, having been raised religiously, believe that it was a call from God, a call that you had to go for because God loved you more.

Ever since you passed life hasn’t been the same, but by God’s grace we survived the agonizing fight, even your two little boys, Nkundwe and Nsaji have grown into great men and we believe that wherever you are, you are watching over us.

You are greatly missed by your husband Thaddeus, sons Nkundwe and Nsaji, Mother Laini, Sisters Jane and Matilda, brothers in law Joseph, William, James, Nico and sister in law Valentine, Friends and Relatives. To all of us there have never been a replacement in our lives and you will always hold that special place in our hearts. We are still fulfilling God's will and purpose on earth until the day when God decides that we join you in the everlasting life that our Lord has prepared for his people.

MAY THE ALMIGHTY GOD CONTINUE TO REST YOUR SOUL IN ETERNAL PEACE
AMEN.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO TAREHE 28.08.2014.

Viewing all 110167 articles
Browse latest View live




Latest Images