Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 551 | 552 | (Page 553) | 554 | 555 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Muwasilishaji Toka Mfuko wa Pensheni wa NSSF Bw. Feruzi Mtika akiongea na waajiriwa wapya wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuhusu aina ya Mafao wanayotoa iwapo watajiunga na Mfuko huo, wakati wa Semina iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
  Muwasilishaji toka Mfuko wa Pensheni wa GEPF Bi. Evelyne Kusenga akiwaeleza waajiriwa wapya wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo  kuhusu Mafao na faida wanayotoa iwapo watajiunga na Mfuko huo, wakati wa Semina iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
  Meneja Masoko Toka Mfuko wa Pensheni wa PPF Bw. Martin Modigadi akiwaleza jambo watumishi wapya wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati wa semina elekezi kuhusu mifuko ya pensheni leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Afisa Toka Mfuko huo Bi Abela Luo.
  Afisa Toka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bi. Hawa Kikeke akiongea na Waajiriwa wapya wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuhusu Faida watazopata iwapo watajiunga na mfuko huo, leo Jijini Dar es Salaam.
  Kaimu Meneja Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. Arnold Kagaruki akiongea na watumishi wapya wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati wa semina elekezi kuhusu mifuko ya pensheni leo Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Msaidizi Rasilimali watu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo akiwaeleza jambo waajiriwa wapya wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo  wakati wa semina elekezi kuhusu mifuko ya pensheni leo Jijini Dar es Salaam.

  0 0
 • 08/26/14--13:30: Simu.tv mpya!


 • 0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete anatarajia kuwa mgeni rasmi katika  uzinduzi wa programu ya  uimarishaji wa mipaka ya kimataifa kwa lengo la kuhuisha alama zilizopo na kuweka mpya katika maeneo ya  mipaka ya Tanzania ambayo awali yalikuwa yametengwa na mito na baadaye mito hiyo kukauka .

    Programu hiyo inayofanywa na wataalam wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi itazinduliwa rasmi Agosti 28, katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare  kwa upande wa Burundi.

    Aidha, itahusisha ujenzi na uwekaji wa vigingi vya mipaka, Marais wa nchi za Burundi na Tanzania kutembelea baadhi ya maeneo yenye alama za mipaka na kisha kuzungumza na wananchi waishio mpakani. Katika tukio hilo Rais Jakaya Kikwete anatarajia kumpokea mwenzake wa Burundi, Rais Pierre Nkurunziza atakayewasili nchini Tanzania kushuhudia zoezi hilo akitokea nchini Burundi kupitia mpaka wa Kabanga ulioko wilayani Ngara.

    Kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Ngara Bw. Hussein Seif akizungumzia maandalizi ya shughuli hiyo amesema kuwa wilaya hiyo imejipanga kuhakikisha kuwa programu hiyo inatekelezwa kwa ufanisi katika maeneo yote ya wilaya ya Ngara yanayopakana na nchi ya Burundi.

  Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Topographia na Giodosia wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. James Mtamakaya akizungumzia zoezi hilo amesema kuwa tayari maeneo mbalimbali ya mipaka ya Tanzania yameshapitiwa na zoezi hilo likiwemo eneo la mpaka kati ya Tanzania na Uganda.

   Ameyataja maeneo mengine kuwa ni eneo la Tanzania na Rwanda ambalo bado linatenganishwa na mto Kagera, eneo la mpaka kati ya Tanzania na Msumbiji, Tanzania na Kenya pamoja na zoezi la uimarishaji wa mpaka kati ya Burundi na Tanzania ambalo linaendelea kufanyika.
  Kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Ngara Bw. Hussein Seif akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa maandalizi ya shughuli ya uzinduzi wa Programu ya uimarishaji wa mipaka ya Kimataifa wa wilaya ya Ngara itakayozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete eneo la Mugikomero mpakani mwa Tanzania na Burundi. Wanaoonekana nyuma ni raia wa Burundi waishio mpakani.
  Raia wa Burundi wakiwa nyuma ya alama ya mpaka inayotenganisha Tanzania na Burundi. Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inaendelea na zoezi la kuhuisha mipaka hiyo ya kimataifa.
  Moja ya Shamba la ndizi lililopandwa katikati ya eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi ambalo kwa sheria za kimataifa haliruhusiwi kufanyiwa shughuli yoyote.
  Bw. Israel Paul akipaka rangi moja ya alama ya mpaka unaotenganisha Tanzania na Burundi eneo la Mugikomero, wilayani Ngara kufuatia Programu inayoendelea ya uhuishaji wa mipaka ya kimataifa.

  Viongozi wa wilaya ya Halimashauri ya Wilaya ya Ngara wakikagua moja ya eneo la mpaka wa Kabanga unaotenganisha Tanzania na Burundi ambapo Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania atampokea Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza.
  Moja ya alama ya mpaka unaotenganisha Tanzania na Burundi ikiwa imekamilika katika eneo la Mugikomero, wilayani Ngara kufuatia Programu inayoendelea ya uhuishaji wa mipaka ya kimataifa.

  0 0  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU unaofanyika katika ukumbi wa Kuringe.
  Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Dk Edward Hosea akizummza wakati wa Mkutano wa mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU .
  Mkurugenzi wa idara ya elimu TAKUKURU ,Marry Mosha akitoa neno la shukurani mara baada ya mgeni rasmi kufungua mkutano huo.

  Baadhi ya washiriki katika mkutano huo.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  Rais Kikwete, Waiziri wa Ujenzi Dkt.Magufuli, Naibu Waziri wa Maji Amos Makalla, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Musa Iyombe, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera, M/Kiti Kamati ya Miundombinu Profesa Kapuya, M/kiti Bodi Mfuko wa Barabara Dr.Wanyancha, M/kiti Bodi ya Makandarasi Consolata Ngimbwa, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mhandisi Mfugale na Wakandarasi wa mradi wa Magole - Turiani.
  Nyumba za Makandarasi zitakazokabidhiwa kwa wananchi wa Wilaya ya Mvomero baada ya mradi kuisha.

  Rais Jakaya Kikwete amemshuhudia Waziri wake Dkt.Magufuli akiitwa Jembe Jembe! na wananchi wa Gairo kutokana na utendaji kazi wake, hayo yametokea Kata ya Gairo Wilayani Gairo kwenye Mkutano wa hadhara.

  Rais Kikwete yupo Morogoro katika ziara ya siku tano akikagua miradi ya maendeleo, awali aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Magole - Turiani yenye urefu wa kilomita 48.6, inayogharimiwa na Serikali kwa shilingi bilioni 41.891 kule Mvomero na baadae akaendelea na ziara Wilayani Gairo. Ilifika kipindi Dkt.Magufuli aliitwa katika jukwaa kwa ajili ya kusalimia na kutoa neno ndipo wananchi walishangilia kwa nguvu huku wakiita Jembe Jembe!

  Mara kwa mara Dkt.Magufuli amekuwa akiitwa Jembe kutokana na uchapaji kazi wake tangu awe Waziri miaka ya 1995. Hilo pia limeshuhudiwa wakati Rais Kikwete alipomsifu yeye (Dkt.Magufuli) pamoja na timu yake kwa uchapaji kazi katika wizara ya ujenzi.

  Katika hatua nyingine Waziri wa Ujenzi ameruhusu kuzikabidhi nyumba za Makandarasi kwa wananchi wa Wilaya ya Mvomero pindi mradi utakapoisha ili zitumike kwa shughuli za maendeleo ya wanamvomero.

  1995 -2005: Rais Mstaafu B.Mkapa alimpachika Dkt.Magufuli jina la askari wa mwamvuli kutokana na utendaji kazi wake mzuri

  2005 - Todate: Wananchi wamempachika jina la Jembe! Ikiwa ni pamoja na Rais Kikwete kumsifia kwa uchapakazi wake!

  0 0

  Gwiji la muziki wa kizazi kipya, Alikiba, akitoa burudani kwa Wanatanga kwa wimbo wake mpya-Mwana Dar es salaam- usiku wa Fiesta Tanga, katika viwanja vya Mkwakwani jinjini Tanga.

  Akiwa jukwaani, Alikiba alilazimika kuuruduia wimbo huo kwa zaidi ya maramoja kwani pindi alipoonyesha dalili ya kumaliza kuimba, mashabiki zake walipiga kelele kuomba arudie kwa mara nyingine.

  Alikiba ameahidi makubwa zaidi jumamosi hii,  Fiesta Moshi.


  0 0
 • 08/27/14--02:33: SELFIE
 • Ankal akipata selfie na wadau wa Globu ya jamii uwanja wa ndege wa Geita gold mines asubuhi hii.

  0 0

  Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Dkt. Nyamajeje Weggoro wapili kutoka (kulia) akifafanua jambo kwa wajumbe wenzake juu ya ujenzi wa Chuo chake cha Usafiri wa Anga (CATC) wakati walipotembelea eneo la mradi huo uliopo Fukayose Bagamoyo mkoa wa Pwani .Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi Mbwana J Mbwana (tikakati)ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Charles Chacha,wengine kutoka kushoto ni wajumbe Hanif M. Malik ,Yussuf M. Ali na katibu wa Bodi Vallery Chamulungu.

  0 0


  0 0  0 0

  WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe amekutana na Mwanaharakati wa Kimataifa wa haki za wanawake na watoto, Graca Machel na kujadili masuala mbalimbali ya haki za wanawake na watoto katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo.

  Katika mazungumzo yao, Waziri Chikawe alimwambia mke huyo wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, juhudi zake za kuingiza katika Katiba Mpya kifungu cha kuzuia mtoto wa chini ya miaka 18 asioe wala asiolewe.

  Hata hivyo, Mama Machel kwa upande wake alimshukuru Waziri Chikawe kwa maoni yake na kusema kuwa ni muhimu kwa wadau wote wa haki za watoto wakashinikiza wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba na watunga sheria wote wahakikishe kipengele hicho kinaingia ndani ya Katiba. Mama Machel yupo nchini kuhudhuria mkutano wa ufunguzi wa Kampeni ya Kitaifa ya kutokomeza ndoa za utotoni.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (Kushoto) akizungumza na Mwanaharakati wa Kimataifa wa haki za wanawake na watoto, Graca Machel katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo. Waziri Chikawe alimueleza Mama Machel, juhudi zake za kuingiza katika Katiba Mpya kifungu cha kuzuia mtoto wa chini ya miaka 18 asioe wala asiolewe.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akiagana na Mwanaharakati wa Kimataifa wa haki za wanawake na watoto, Graca Machel baada ya kikao chao kifupi kilichofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo. Waziri Chikawe alimueleza Mama Machel, juhudi zake za kuingiza katika Katiba Mpya kifungu cha kuzuia mtoto wa chini ya miaka 18 asioe wala asiolewe. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  Kampuni ya Vodacom Tanzania imekuja na Fistula Ice Bucket Challenge ‘#BongoIce’ yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya matibabu ya akina mama wajawazito wenye ugonjwa wa Fistula. Hii ni kufuatia kampeni inayoendelea mitandaoni ikijulikana kama #ALSIceBucketChallenge ambapo Vodacom Tanzania kwa kutambua kuwa kuna wanawake wengi Zaidi ya 30,000 wanaogua ugonjwa huu hapa nchini imeanzisha kampeni inayoitwa #BongoIce.

  Mkurugenzi wa Vodacom, Rene Meza amekuwa wa kwanza kushiriki kampeni hii na kuwateua Naibu Waziri wa Mawasiliano Mhe January Makamba, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Tigo Diego Gutierrez na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Airtel ndugu Sunil Colaso kushiriki kampeni hii. Fuatilia kupitia:

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Bi. Hawa Ghasia ameridhishwa na tathimini ya mkutano wa mashauriaono wa awamu ya kwanza wa Mradi wa Mabasi yaendeyo Haraka (DART) uliofanyika hivi karibuni na wa kampuni ya Simon Group inayomiliki mabasi ya UDA na wamiliki wa usafirishaji jijini Dar es Salaa( Daladala) kuungana kwani italeta maendeleo katika sekta ya usafiri jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam hivi karibuni kuhusu maendeleo ya   ya sekta ya usafiri pamoja na majadiliano yanayoendelea kufanyika wakati huu wa kuelekea katika mfumo mpya wa Mabasi yaendeyo Haraka,Waziri Ghasia aliunga mkono jitihada zote zinazofanywa na wadau katika sekta ya usafiri.

  “Kwa jinsi ambavyo mfumo unatakiwa uendeshwe na kwa jinsi  zabuni zitakapo tangazwa bila kua na umoja itakuwa ni vigumu watanzania kupata kazi,”alisema na kuunga mkono makubaliano ambayo yameshafikiwa baana ya pande husika.

  Bi. Ghasia alisema uzoefu unaonyesha kuwa watazania wamezoea kufanya kazi mtu mmoja mmoja hivyo basi wakati  umefika wakati kuwa na kampuni moja itakayokuwa na nguvu katika sekta ya usafirishaji.“Imani walioijenga kwa kuungana italeta tija kubwa kiuchumi katika sekta ya usafiri katika  jiji la Dar es Salaam na wengine nao wataiga,” alisema Ghasia.

  Alisema  kuwa mfumo  mpya utakaokuwa unatumika katika uendeshaji utakuwa wa kisasa zaidi na kwa mfumo wetu wa kuchukua nauli ndani ya daladala hautakuepo tena hivyo ni lazima kuwa kitu kimoja.

  “Mimi ni ningefurahi sana kama huu mfumo ungeshikiliwa na watanzania kuliko wageni,” Waziri Ghasia alisisitiza, na kuongeza kuwa wakati umefika kwa watanzania wabadilike na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

  Bi. Ghasia alisema anaamini wawekezaji wa ndani wanauelewa mzuri na mfumo huu mpya hasa kutokana na kushirikishwa toka mwanzo wa mradi hadi kufikia sasa kutokana na kujifunza mambo kadha wa kadha nje ya nchi.“ Ninashukuru tumekuwa na wamiliki wa usafiri toka zoezi hili linaanza, DARCOBOA tumeenda nao mapaka Bogota nchini Colombia na wameona namna mfumo unavyofanya kazi” aliongeza Waziri Ghasia.

  Alisema kuungana kwao ni ishara na namna walivyojifunza nchini Colombia jinsi wenzao walivyohama kutoka katika mfumo kama tulionao sisi na kuingia katika mfumo mpya wa mabasi yaendayo haraka.

  “Wawekezaji wetu waliona namna mfumo ulivyomzuri na rahisi katika jiji lile hivyo ni somo tosha kwa wamiliki wetu wa hapa nchini, nashukuru wameliona hilo,” alisema.

  0 0

  SERIKALI imepokea msaada wa magari manne na pikipiki 20 zenye thamani ya sh. .261,105,615 kutoka Shirika la Wahisani la Kijerumani linalohudumia Ukoma na Kifua Kikuu (GLRA) kwa ajili ya kusaidia sekta ya afya.

  Akipokea msaada huo Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid alisema Tanzania imefikia lengo la kimataifa la kutokomeza ukoma kwa kuwa chini ya mgonjwa mmoja katika watu 10,000 hivyo kufanya ukoma kutokuwa tatizo kubwa la afya nchini.

  Alisema pamoja na kupokea msaada huo bado kumekuwa na changamoto ikiwemo za ukosefu wa magari na pikipiki kwa mikoa na wilaya mpya ambapo Serikali kupitia mpango huo unafanya jitihada za kupata vyombo vya usafiri katika mikoa hiyo.

  Alisema vyombo hivyo vya usafiri vitapelekwa katika mikoa ya Kigoma, Tanga, Halmashauri za Ilala na Kinondoni ambapo aliomba  vitumika vizuri kulingana na malengo yaliyokusudiwa.

  "Napenda kuuwaasa waganga wakuu wa mikoa na wilaya kusimamia kikamilifu matumizi ya vyombo hivi vya usafiri kwa kuhakikisha wale wote watakaokabidhiwa wanavilinda kwa kuvitumia vizuri kulingana na malengo yaliyokusudiwa na kwa kufuata taratibu za serikali na si vinginevyo," alionya.

  Dk. Rashid alitoa wito kwa Halmashauri zote nchini kuangalia namna ya kuchangia gharama za matengenezo ya vyombo hivyo ili kuziba pengo la kupungua kwa misaada inayotolewa na wahisani.

  Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Wahisani la Kijerumani linalohudumia Ukoma na Kifua Kikuu (GLRA), Burchard Rwamtoga (wa pili kushoto), akimkabidhi  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid (kulia),moja ya ufunguo wa gari kati ya magari manne na pikipiki 20 vyote vikiwa na thamani ya sh.261,105,615, Dar es Salaam leo, zilizotolewa na shirika hilo kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kupambana na magonjwa hayo nchini. Wanashuhudia kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Charles Palanjo na Naibu Waziri, Dk. Steven Kebwe.
  Naibu Waziri, Dk. Steven Kebwe (wa pili kulia), na viongozi wengine wa wizara hiyo wakiwa kwenye hafla hiyo. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Charles Palanjo, Mganga Mkuu wa Serikali Donan Mmbando na Mkurugenzi Msaidizi Afya na Usafi wa Mazingira, Elias Chinamo.
  Pikipiki zilizotolewa kwa serikali.
  Magari yaliyotolewa kwa Serikali.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Balozi Mdogo wa Tanzania- Dubai, mhe. Omar Mjenga, leo amemtembelea na kufanya mazungumzo na Bw. Rashid Lootah, Mwenyekiti wa Nakheel, Shirika la Nyumba la Serikali ya Dubai.

  Katika mazungumzo yao, wamezungumzia ziara ya Mwenyekiti huyo pamoja na ujumbe wake kuitembelea Tanzania, itakayofanyika kuanzi tarehe 16-20 Septemba, ambako anatarajia pamoja na kuonana na baadhi viongozi wa Serikali, watafanya mazungumzo na Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) yatakayowezesha kusainiwa makubaliano ya ushirikiano kwenye sekta ya nyumba kati ya mashirika hayo mawili.

  Aidha, watapata fursa ya kukitembelea kituo cha uwekezaji - TIC ili kupata taarifa muhimu za uwekezaji.

  Aidha, Mhe. Mjenga amemuomba Mwenyekiti huyo kufadhili mkutano wa Uwekezaji kwenye Sekta ya Utalii utakaofanyika Novemba hapa Dubai. Mkutano huo unaandaliwa na Ubalozi Mdogo kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii ya Tanzania-TTB pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii.
  Mhe. Mjenga akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Lootah mbele ya baadhi ya miradi inayojengwa na Nakheel.
  Mazungumzo yakiendelea kati ya Mhe. Mjenga na Mwenyekiti Lootah, katika ofisi za Nakheel.

  0 0

  Na Tamimu Adam – Jeshi la Polisi

  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imekabidhiwa msaada wa vifaa vyenye thamani zaidi ya milioni mia moja kutoka kwa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kwa ajili ya matumzi ya ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Mambo ya ndani na ukumbi wa mikutano wa Jeshi la Polisi Tanzania.

  Msaada huo, ulitokana na Ziara ya Naibu Waziri wa Usalama wa raia wa Jamhuri ya watu China aliyoifanya hapa nchini mwezi mei mwaka jana ambapo aliahidi misaada mbalimbali kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Jeshi la Polisi.

  Miongoni mwa vifaa vilivyokabidhiwa na Balozi wa Jamhuri ya watu wa China hapa nchini Mhe. Xu Youqing kwa Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mhe. Pereira Silima ni pamoja na Kompyuta Thelasini (30), Viti tisini na mbili (92), Meza hamsini (50) na PA System kwa ajili ya kumbi mbili za mikutano.

  Aidha, Balozi wa Jamhuri ya watu wa China hapa nchini Mhe. Xu Youqing alikabidhi Pikipiki hamsini (50) kwa Jeshi la Polisi ambazo zilipokelewa rasmi na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima. Pikipiki hizo zilitolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya watu wa China kwa niaba ya jumuiya ya wafanyabiashara wa kichina walipo Afrika wakati wa ziara yake aliyoifanya hapa nchini mwezi juni mwaka huu.

  Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. Pereira Silima baada ya kupokea vifaa hivyo, alimshukuru Balozi huyo wa China na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Pamoja na Wafanyabiashara wa Kichina waliopo Afrika kwa msaada walioutoa kwa Serikali ya Tanzania, na kueleza kuwa vifaa hivyo vyote vitakuwa ni chachu katika kuzuia, kupambana na kukabiliana na uhalifu hapa nchini.

  Naye, Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki alisema kuwa mbinu za kutenda uhalifu hubadilika mara kwa mara kulingana na mabadiliko ya kiteknolojia, na katika kukabiliana na mabadiliko hayo Jeshi la Polisi liko kwenye utekelezaji wa Maboresho yaliyojikita katika mihimili mikuu mitatu ambayo ni kulifanya Jeshi kuwa kisasa, lenye weledi na linaloshirikiana na wananchi katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu, hivyo vifaa vilivyokabidhiwa vitalisaidia Jeshi la Polisi katika mpango huo unaolenga kuzuia uhalifu.
  Balozi wa Jamhuri ya watu wa China akipokea cheti kinachoonyesha ushirikiano mzuri baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mhe. Pereira Silima wakati wa kukabidhi msaada wa kutoka Serikali ya watu wa China.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi , Mhe. Pereira Silima amekaa juu ya pikipiki,(kushoto kwake) Balozi wa China hapa nchini Mhe. Xu Youqing (kulia) (katika) Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi,Abdulrahman Kaniki wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa vya ukumbi , pikipiki pamoja na kompyuta zilizotolewa na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Picha na Hassan Mndeme- Jeshi la Polisi.

  0 0

  M-Net has announced that it will be launching a new East African focussed TV brand, Maisha Magic tailored to meet DStv subscriber local viewing needs from Monday 1 September and will be closely followed by Maisha Magic Swahili on September 24. This exciting channel will be screened to Premium, Compact Plus and Compact subscribers on channel 161.

  “M-Net has been building steadily on its investment in the East African market, centralized in Kenya but with outreach across the region. We have recognized that whilst the Africa Magic brand has come to represent a powerful philosophy about pan-African cohesion, there is definitely great potential for a customized East African television brand. As such, M-Net put in place a detailed project a few years ago to carefully build its technical, staffing and content capacity so that when Maisha Magic is officially launched, it would be the culmination of all these investments,” says M-Net East Africa Regional Director Michael Ndetei.

  He goes on to say, “We have always believed that East African talent, East African stories are as vital and as compelling as those found anywhere else in Africa. This is a fact proven by the success of East African content at the first two Africa Magic Viewers’ Choice Awards. Now with our studio fully functioning, the Africa Magic Original Films Project well underway producing made-for-TV titles and our flagship show Mashariki Mix well established, we are ready to launch Maisha Magic, both the channel and the brand.”  

  It will be made up of East African content, though the channel will also include some international programming that have resonance with East African audiences, such as South American telenovelas, dubbed into English.  Ndetei confirms the combination strategy saying, “Our research demonstrated clearly that our audiences want home-grown entertainment, with very specific kinds of international content, so we’re working on getting that balance right to ensure that this is in fact a channel made in East Africa, to meet East African tastes.”

  Programming on the Maisha Magic channel will cover multiple genres including sitcoms, telenovelas, reality, drama and music. Highlights to look out for include; Comedy shows Mr & Mrs Singh and Mazagazaga and Comedy Club Uganda hosted by Ann Kansiime; the dramas Rush and The Tendo Sisters; the music shows Wakilisha and Beyond the Beat; the Mexican soaps A Love To Remember and Loving You Is All I Want as well as recent hits such as Kona and Noose of Gold. Notably the channel will screen Original Films from East Africa as part of the Africa Magic Original Films Project. The Maisha Magic channel will also be the home for all daily highlight programs from the up-coming Big Brother Hotshots, plus all the live Sunday eviction shows.  

  For more information log onto www.dstv.com

  0 0

  Spika wa Bunge la Tanzania Anne Makinda akihutubia Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) la kwanza kufanyika Dar es Salaam, tangu utaratibu wa kufanyika kwa bunge hilo kwa mzunguko kwa kila nchi mwanachama wa Jumuiya.
  Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Margaret Zziwa akizungumza kwenye ufunguzi wa bunge hilo.
  Spika wa Bunge la Tanzania Anne Makinda (kushoto) akiwa na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Margaret Zziwa wakati wa ufunguzi wa vikao vya bunge hilo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
  Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Dkt. Abdullah Juma Saadala (wa pili kushoto), akifuatilia ufunguzi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki.Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki, Phyllis Kandie (Waziri kutoka Kenya) Shem Bagaine (Waziri kutoka Uganda), Leontine Nzeyimana (Waziri kutoka Burundi), Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Richard Sezibera na kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa Jumuiya hiyo Wilbert Kaahwa.
  Wabunge wa Tanzania wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia hutuba ya Spika wa bunge hilo (hayupo pichani) kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
  Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) wakiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge hilo Dkt. Margaret Zziwa (wa nne kutoka kulia waliokaa) na Spika wa Bunge la Tanzania Anne Makinda, mara baada ya ufunguzi wa bunge hilo.
  Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdullah Jumaa Saadala akizungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki leo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Na Veronica Simba

  Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi, Mhe. Côme Manirakiza na Ujumbe wake wako katika ziara ya siku tano (24 – 28 Agosti, 2014) hapa nchini kwa lengo la kujifunza namna Sekta za Nishati na Madini zinavyofanya kazi.

  Katika ziara yake, Waziri Manirakiza ametembelea Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini – Dar es Salaam na kukutana na Wataalamu mbalimbali wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake wakiongozwa na Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje.

  Wakiwa Wizarani, Waziri na Ujumbe wake walipata fursa ya kusikiliza mada zinazohusu Sekta za Nishati na Madini zilizowasilishwa na Wataalamu wa Wizara.

  Ujumbe huo pia umepata nafasi kutembelea Taasisi na Mashirika mbalimbali yaliyo chini ya Wizara na yale yenye uhusiano na Wizara ikiwemo Mpango wa Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji Tanzania (Tanzania Extractive Industry Transparency Initiative – TEITI), Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasimali Madini (SMMRP) na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA).
  Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje akiwasilisha mada kuhusu Sekta ya Madini – Tanzania kwa Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi, Mhe. Côme Manirakiza (wa kwanza kulia) na Ujumbe wake (Kulia kwake) waliofika Makao Makuu ya Wizara – Dar es Salaam, Agosti 26, 2014 kujifunza namna Sekta za Nishati na Madini zinavyofanya kazi. Upande wa kushoto ni Wataalamu mbalimbali wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake.
  Mtaalamu kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Wellington Hudson akitoa mada kuhusu Rasilimali za Gesi na Mafuta kwa Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi, Mhe. Côme Manirakiza (Wa kwanza Kulia) na Ujumbe wake. Ujumbe huo ulifika Makao Makuu ya Wizara – Dar es Salaam, Agosti 26, 2014 kujifunza kuhusu Sekta za Nishati na Madini zinavyofanya kazi. Wengine pichani ni Wataalamu wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake wakiongozwa na Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje (wa kwanza kushoto).
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Profesa Abdulkarim Mruma (aliyeinua mikono), akitoa ufafanuzi kuhusu GST kwa Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi, Mhe. Côme Manirakiza (Wa kwanza Kulia) na Ujumbe wake waliofika Makao Makuu ya Wizara - Dar es Salaam, Agosti 26 kujifunza namna Sekta za Nishati na Madini zinavyofanya kazi.
  Mtendaji Mkuu wa Jiolojia na Migodi (Geology and Mines) wa Burundi, Emmanuela Ngenzebihoro (mwenye kilemba) akiuliza swali kwa Wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini – Tanzania (Walioketi Kushoto), wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi, Mhe. Côme Manirakiza (Wa kwanza Kulia) na Ujumbe wake Makao Makuu ya Wizara - Dar es Salaam, Agosti 26, 2014. Waziri Manirakiza na Ujumbe wake walifika wizarani kujifunza namna Sekta za Nishati na Madini zinavyofanya kazi.
  Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi Mhe. Côme Manirakiza (aliyeinua mkono), akiomba kupewa ufafanuzi kuhusu sekta ya madini hapa nchini, baada ya uwasilishwaji mada zilizohusu sekta za nishati na madini za Tanzania. Waziri Manirakiza na Ujumbe wake walitembelea Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini - Dar es Salaam, Agosti 26, 2014 kwa lengo la kujifunza namna sekta husika zinavyofanya kazi. Wengine pichani ni Wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini - Tanzania (kushoto) na Ujumbe ulioongozana na Waziri (Kulia).

older | 1 | .... | 551 | 552 | (Page 553) | 554 | 555 | .... | 3270 | newer