Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 550 | 551 | (Page 552) | 553 | 554 | .... | 3286 | newer

  0 0


  Katika siku za hivi karibuni ndege aitwae kware ameanza kuwa ndege maarufu katika baadhi ya wafugaji katika nchi yetu na kwa wale ambao walikuwa wakiwawinda porini enzi hizo bado wana imani kuwa ndege huyu hawezi kufungwa kama hatakimbia basi atajiua, lakini kwa wale wanaotaka kumfuga ndege huyu mdogo mwenye mayai matamu ya madoa doa wanaweza sasa inaweza kugeuka chanzo cha mapato na sehemu ya chakula bora kwa familia.


  Leo ningependa niingie ndani kuwa nini hasa tofauti ya mayai ya kware na yale ya kuku ingawa taarifa nyingi nilizopata kwenye mitandao na kwinginekoinaonyesha tu kwa habari za watu waliopata kutumia mayai kware na kuona umuhimu wake katika afya na baadhi ya tovuti kuongelea tu kwamba mayai haya ni mazuri yanasaidia kwa afya bado kama watu wanaotaka kueleew inakuwa haikidhi haja kuamani tu yakuwa yana saidia katika afya, nikiwa mmojawapo wa watu ambao niliona yanasaidia watu walikuwa na matatizo mbalimbali ya kiafya wakiendelea vizuri.


  Na mpaka sasa mimi napenda kukiita hiki chakula bora na sio dawa kama watu wengi waliotumia wakapata nafuu kwa yale waliokuwa yakiwasibu na wale waliokuwa na dhaifu nyingine katika mwili wakarejea afya maridhawa lakini msimano wangu binafsi napenda kutambua mchango wa haya mayai kama chakula bora.


   Ndio maana hata Mungu aliamua kuwapa wana waisrael kama chakula kwenye Kutoka 16:13 na mtumishi Daudi anakomelezea kwenye Zaburi 105:40. Sasa kwa kuwa siku zote najua kuwa Mungu hapingani na sayansi kitu wanasayansi wanachofanya nikungudua tu mambo ambayo Mungu ameyaweka kwahiyo ikabidi nitafute kisayansi sasa sisi tunaopenda kuoona na kufanya akili zetu zielewe maana ukielewa jambo kwenye akili yako ni rahisi kufanyia kazi.


  Katika kutafuta nikasema pamoja na vyanzo vya wataalamu binafsi ningependa kupata vyanzo vilivyo vya kiserekali ambavyo wao hawana upande waliolalia maana hawa wataalamu binafsi wanaweza kuwa na ajenda zao, Na ndipo nilipopata  utafiti wa USDA (United State Department of  Agriculture) unaonyesha tofauti za mayai haya kwa kina katika category 78 za nutrients  zilizogawanya mayai ya kware yana  vitu 31 zaidi ambayo ya kuku hayana kabisa wakati yale ya kuku ya kitu kimoja tu ambacho hakiko kwenye ya kware ambacho naomba nikitaje nacho ni Vitamin K (phylloquinone) na  katika hizo 45 vilivyobaki vya kware 42 viko juu  na vingine hata mara mbili ya zile za kuku, wakati vya kuku ni 3 vitatu  ambayo vimezidi vile vya kware.  Angalia link hizo hapo chini kwa number kamili


  Faida hizi zote tunaweza kupata kama watu wetu watajiingiza katika ufugaji wa ndege huyu ambaye anapatikana sehemu nyingi unaweza kuanza kidogo kidogo mpaka wakafikia mwengi,na kama unavyooana hapo juu unaweza kutengeneza banda rahisi la mbao laini na wafu na kuanzia hapo, ila wawapo wadogo waweke kwenye box na kuwawekea taa kama ufanyavyo kuku.
  Ufugaji nyuma ya nyumba

  Naomba niwakilishe nakaribisha maswali comment hapo chini ili tuendelee kujifunza zaidi faida ya ndege huyu na manufaa yake katika maisha yetu Ahsanteni.


  0 0

  Bwana Nzumbe Nyanduga (kushoto) amekuwa Mtanzania wa kwanza kupata stashahada ya “International Master (MA) in Management, Law and Humanities in Sports” inayodhaminiwa na FIFA. Pichani ni Bw. Nzumbe Nyanduga anaonekana akipokea stashahada hiyo kwenye Chuo Kikuu cha Neuchatel, Uswiss kutoka kwa Mkuu wa Chuo mbele ya Mchezaji wa zamani wa Real Madrid, Bw. Christian Karambeu ambae alikuwa ndio Patron wa darasa la 2014. Bw. Nyanduga amepata stashahada hiyo yenye distinction akiwa mwanafunzi bora wa 2014.

  0 0

  Mdau Chris Mauki ameibuka na libeneke lake zuri kabisa lenye lengo la kuwahabarisha wadau kuhusu masuala ya saikolojia, familia, mahusiano, na malezi pindi upatapo nafasi ya kutembelea Libeneke lolote lile,basi usisite kutia baraka katika libeneke la Mdau Chris Mauki ili upate uhondo kwa kubofya hiyo Link hapo chini.

  0 0

    
  Marehemu Bi Aziza enzi za uhai wake.
  Kikundi cha Unity Of Women Friends,Kupitia mradi wao wa Mwanamakuka Awards  na Washirika wake,Benki ya Wanawake TWB na Clouds Media Group,Wana tangaza kwa masikitiko makubwa ya kumpoteza mshindi wa mwaka jana 2013,Bi Aziza  Mbogolume (pichani).
  Bi Aziza amefarika mapema jana mchana jijini Dar es salaam,mazishi yake yanatarajiwa kufanyika leo mnamo majira ya saa 9,na msiba upo nyumbani kwake Magomeni mwembechai.Aziza alikuwa ni Mwanamke jasiri mwenye uthubutu wa kufanya biashara kupitia kipaji chake cha Kuchora .
  MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI  PEMA PEPONI-AMIN

  http://1.bp.blogspot.com/-pWV9rBQ6zSU/UTsAJzwBYSI/AAAAAAAEMbs/wIoMPtgWHwc/s1600/03.jpg
  Aziza Mbogolume (wa pili kulia) enzi za uhai wake wakati akipokea mfano wa hundi baada ya kushinda tuzo ya Mwanamakuka 2013 kutoka kwa Mke wa Makamu wa Rais, Aisha Bilal.
  http://4.bp.blogspot.com/-6hZqPBN8luU/UW3H0k0LiQI/AAAAAAACIkY/j9xLijjnl2k/s640/DSC_3104.JPG
  Baadhi ya viongozi waratibu wa shindano la Tuzo za Mwanakuka wakistaajabia kazi za mikono ya Aziza Mbogolume (wa pili toka kushoto) enzi za uhai wake katika maonesho ya mwaka huu yaliyofanyika Escape 1 Mikocheni jijini Dar
  0 0

  Leo Agosti 26 ni siku ya kuzaliwa ya Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Ngoyai Lowassa aliezaliwa tarehe kama ya leo miaka 61 iliyopita.Mh. Lowassa anayo furaha kubwa kuisherehekea siku hii muhimu kwake na kwa familia kwa ujumla.Globu ya Jamii na timu yake inamtakiwa Heri ya siku ya kuzaliwa kwake.
  Mh. Lowassa akiwa shambani kwake wakati alipotembelea kuangalia maendeleo ya mifugo.

  0 0

  DSC_0425
  DSC_0428
  |It's now official launched".....Ofisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mh. Mohammed Dewji "MO" (Mb) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Maendeleo cha IRIS Executive Development Centre ambao ndio wamiliki wa jarida la IRIS Executive, Phylisiah Mcheni wakifurahi pamoja baada ya uzinduzi rasmi wa jarida hilo.
  DSC_0445
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mh. Mohammed Dewji "MO" (Mb) akikata keki maalum iliyoandaliwa kusindikiza uzinduzi huo.
  DSC_0451
  Mgeni rasmi Ofisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mh. Mohammed Dewji "MO" (Mb) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa jarida la IRIS Executive. Kutoka kushoto ni Ofisa uhusiano na raslimaliwatu waIRS Exexcutive, Beatrice Silayo, Jokha Sadiki, Ofisa Mtendaji Mkuu waKituo cha Maendeleo cha IRIS Executive Development Centre ambao ndio wamiliki wa jarida la IRIS Executive, Phylisiah Mcheni, Ofisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mh. Mohammed Dewji "MO" (Mb),Mhariri Mtendaji wa jarida la IRIS Executive, Mike Mina, Meneja Masoko wa jarida la IRIS Executive, Alinda Henry na Ofisa anayeshughulikia masuala ya Fedha wa jarida la IRIS Executive Bw. George Saltai.


  0 0

  Mkurugenzi wa jiji la LAHTI, Kari Porra akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa nyumba hizo za mbao kwa mratibu wa ziara hiyo Godfrey Nyamrunda kutoka taasisi ya Uongozi ya Tanzania, nyuma yao ni Meya wa jiji la Dar Esa Salaam Dk Didas Masaburi.
  Baadhi ya viongozi kutoka majiji sita ya Tanzania wakipata maelezo kuhusu mfumo wa ukusanyaji wa taka na uchujaji wa maji machafu katika jiji la LAHTI, kutoka kushoto ni mratibu wa mtandao wa majiji Tanzania, ( Tanzania Cities Network) Philoteus Mbogoro, Meya wa jiji la Tanga Omary Guledi, Lissa Tervo wa taasisi ya Uongozi ya Tanzania, Johanna Palamoki ambae ni mtaalam wa mipangomiji katika jiji la LAHTI, Mkurugenzi wajiji la Lahti Kari Porra na Meya wa jiji la Mbeya Athanas Kapunga.
  Badhi ya nyumba za ghorofa zilizojengwa kutumia mbao katika jiji la LAHTI nchini Finland ambazo zilitembelewa na madiwani wa majiji sita ya Tanzania waliokuwa katika ziara ya mafunzo nchini humo iliyoratibiwa na taasisi ya Uongozi ya Tanzania. Finland ni miongoni mwa nchi zenye maeneo makubwa ya misitu ya kupandwa dunaini, zaidi ya asilimia 80 ya eneo la nchi hiyo ni misitu na wenyewe wanasema nyumba zinazojengwa kwa kutumia mbao zina gharama nafuu kuliko kujenga kwa matofali au mawe.Picha zote na Vedasto Msungu wa ITV

  0 0

  Katibu Wa Bunge La Tanzania Dr. Thomas Kashililah Alikuja Kuhudhuria Mkutano Wa Chama Cha Bunge La Jumuiya Ya Madola Uliojulikana "Programme For The 3rd Commonwealth Parliamentary Association (Cpa) Africa Region Youth Parliament" Uliofanyika Mjini Lusaka Tarehe 24 Hadi 28 Agosti 2014. Katika Safari Hiyo Ya Kikazi Aliongoza Ujumbe Wa Watanzania 10 Ambao Walihudhuria Mkutano Huo. Aidha Katibu Wa Bunge Alipata Fursa Ya Kuutembelea Ubalozi Wa Tanzania Lusaka Na Kuonana Na Mhe. Balozi Grace Joan Mujuma Na Maafisa Wa Ubalozi Na Kubadilishana Mawili Matatu Kuhusiana Na Nchi Yetu.
  Mhe. Balozi Akiwa Katika Mazungumzo Na Dr. Kashililah Na Wajumbe Waliongozana Nae Waliokaa Upande Wa Kushoto Mwa Balozi Wakimsikiliza Kwa Makini
  Picha Ya Pamoja Kuanzia Kushoto:- Richard Lupembe ( Counselor ) Ubalozi Wa Tanzania Lusaka, Mbarikiwa Masinga, Emmanuel Mpanda, George Seni, Demetrius Mgalami, Justa Nyange (Head Of Chancery) Ubalozi Wa Tanzania Lusaka, Dr Thomas Kashililah (Katibu Wa Bunge La Tanzania) Mhe. Balozi Grace Joan Mujuma, Huddy Kiangi (Finance Attaché) Ubalozi Wa Tanzania Lusaka, Salma Omary, Zuwena Turkey, Katherine Kaikula, Maryam Rajab Na Joseph Lyimo.

  0 0

  website Design & Hosting in Tanzania
  Siku hizi ni kitu cha kawaida kuona vitu vya ajabu vikitumwa tokea akaunti ya mtu unayemuamini sana na haukutegemea kama mtu kama yeye angeweza kutuma (post) vitu kama hivyo, na ikakufanya hata utake kujitoa (Unlike / Unfriend) toka kwenye urafiki au ufuatiliaji kwake. Je unadhani ni kweli kila kitu kinachotumwa kwenye Facebook hutumwa na na muhusika? Jibu ni hapana. Mara nyingi ni wavamizi walioingia kwenye akaunti ya muhusika na kuitumia kadri wawezavyo ama kwakuwa umeruhusu vipachiko (apps) zitume kwa niaba yako.
  Siku hizi, uvamizi wa akaunti kwenye Facebook umekuwa mkubwa, na asilimia kubwa ya uvamizi huu hutokana na ama wahusika kutofahamu athari wa wanachokichagua ama kutokujua jinsi ya kujilinda. Kama ilivyo ada, Dudumizi itakuelezea namna ya kujilinda na uvamizi huo kwenye Facebook.
   Aina za uvamizi:
  Kwenye facebook, kuna aina nyingi za uvamizi, lakini zilizo kubwa ni nne.
  1) Mtu anayekujua kutumia akaunti yako (ana username na password yako)
  2) Mtu asiyekujua kuotea (dictionary attack) namba za siri za akaunti yako (hii ni mra chache sana).
  3) Kujiunga kwenye vipachiko (Apps) vinazonyonya taarifa zako ikiwemo password (Wengi ni wahanga hapa)
  4. Kutumia computer ya mtu mwingine / asiye muaminifu
  Kila aina ya uvamizi ina njia yake ya kujikinga, leo tutaangalia njia moja baada ya nyingine ambazo zitakuwezesha kujikinga na uvamizi huu.


  0 0

   Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB anayeshughulika na huduma ya China Deski, Ibrahim Masahi (kulia), akitoa ufafanuzi kuhusu huduma maalum za kibenki kwa ajili ya kusaidia wafanyabiashara na wawekezaji wa China na Tanzania, wakati wa maonyesho ya bidhaa za China yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.  
   Baadhi ya wateja wakisoma vipeperushi vyenye taarifa muhimu za Benki ya CRDB kuhusu huduma maalum ya China Deski.
   Baadhi ya watu waliofika katika banda la CRDB wakati wa maonyesho ya bidhaa za China wakisoma vipeperushi vyenye taarifa muhimu kuhusu huduma maalum ya China Deski.
   Ibrahim Masahi akitoa ufafanuzi kwa wateja waliotaka kujua huduma za China Deski.

  Na Mwandishi Wetu
    
  BENKI ya CRDB, imeeleza kupata faida baada ya kuanzisha deski la China kwa kuwaunganisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka China na hapa nchini.

  Akizungumza jana katika maonyesho ya bidhaa za China Afrika, yanayofanyika jijini Dar es salaam, Meneja Uhusiano wa Deski hilo, Ibrahim Masahi, alisema kuwa huduma hiyo imerahisisha na kuwasaidia wafanyabiashara kupata mikopo na kufanya huduma za kibenki, kukuza wigo wa kibiashara.

  Masahi alisema kuwa huduma hiyo umuwezesha mteja wa CRDB kutoa hadi kiasi cha sh milioni 40 kwa siku ikiwa atakuwa nchini China au Tanzania kwaajili ya biashara na kuwekeza.

  “Tangu kuanza kwa hudyma hii benki kupitia deski la China imepata faida ya zaidi ya Bilioni 30, na imeunganisha wateja mbalimbali na wawekezaji wanaonunua bidhaa china, lakini kwa upande wa Tanzania Chnagmoto kubwa ni lugha wakiwa kule China na rate imekuwa ikibadilikabadilika,”alisema. 


  Aidha aliwataka watanzania kuchangamikia fursa hiyo ambayo imeondoa madhara ambayo yangeweza kutokea na kueleza kuwa kwasasa wameingia ubia na benki zaidi ya 10 nchini China.


  0 0

  Fatuma Misango mwenye mtandio mweusi kichwani akizungumza na mmoja wa wanawake waliotendwa.
  -------------------------
  Mwandishi HANNAH MAYIGE, wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania – OUT, anaangazia safari ngumu ya mwanaharakati mwanamke mzaliwa wa Namtumbo,  Mratibu wa  Kituo cha wasaidizi wa sheria Songea, Bi. Fatuma Misango katika harakati za kupigania haki za wanawake, watoto na  kupinga ukatili wa kijinsia.

       “Mimi  naitwa  Fatuma  Misango,  ni Mratibu  wa  kituo  cha  wasaidizi  wa sheria  kiitwacho Songea Paralegal  Center  (SOPCE),” Bi  Fatuma alianza kujieleza  kwa mwandishi wa makala haya ofisini kwake mjini Songea.
  Bi. Fatuma Misango anasema yeye ni  mzaliwa  wa  wilaya  ya  Namtumbo  mkoa  wa  Ruvuma,  mwenye  umri  wa miaka  takribani  hamsini sasa.


  0 0


  0 0

   Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa King'ongo, Demetrius Mapesi (kulia),akimtwisha ndoo ya maji Radhia Said baada ya kuzindua mradi wa kisima cha maji mwishoni mwa wiki kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika Kata ya King'ongo, wilayani Kinondoni, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kisima hicho kimejengwa kwa msaada wa TBL. Kushoto ni Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni, Joseph Nicholaus
   Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni, Joseph Nicholaus (kushoto) na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa King'ongo, Demetrius Mapesi wakifunua pazia ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kisika cha maji kiolichojengwa kwa gharama ya sh. mil. 29  kwa msaada wa TBL katika Kata ya King'ongo, wilayani Kinondoni, Dar es Salaam. Wanaopiga makofi ni wananchi wa eneo hilo wakionekana kufurahishwa na msaada huo muhimu kwani wataondokana na tatizo la maji ambapo walikuwa wakitembea zaidi ya KM 2 kununua maji ndoo moja sh. 700. Katika Kisima hicho watakuwa wananunua ndoo moja ya maji kwa sh. 50.
   Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni, Joseph Nicholaus, akifungua maji kwenye bomba lililounganishwa kwenye kisima hicho. Kisima hicho kina uwezo wa  kutoa zaidi ya lita 5000 za maji kwa saa.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   The Deputy Minister for Information, Youth, Culture and Sports, Juma Nkamia (second left) hands over a trophy to Masunga Duba (right) a cyclist from Mwanza shortly after being announced winner of the ABG Cycle Challenge during the 156.6 km men’s race. Looking on at the left is the African Barrick Gold (ABG) Vice President Corporate Affairs Deo Mwanyika and the Cycling Association of Tanzania (CAT) Chairperson Jax Mhagama (second right).
   The African Barrick Gold (ABG) Vice President Corporate Affairs Deo Mwanyika (left) shakes hands with the ABG Cycle Challenge second runner up Simon Mbaruku (second right) during the lake Zone cycling competition sponsored by his company. Looking on second left is the Deputy Minister for Information, Youth, Culture and Sports, Juma Nkamia.
   The ABG Cycle Challenge first runner up Seni Konda (second left) celebrates after receiving a trophy, medal and one million shilling cash prize during the award ceremony to climax the event. Looking on at the left is the African Barrick Gold (ABG) Vice President Corporate Affairs Deo Mwanyika and the Cycling Association of Tanzania (CAT) Chairperson Jax Mhagama (second right).
  The African Barrick Gold (ABG) Executive General Manager Planning and Business Improvement Michelle Ash (second left) poses for a group photo with ABG Cycle Challenge women’s race winners shortly after presenting awards to them. Looking on at the right is the ABG Public & Communications Manager, Nector Foya. Martha Anthony (third left) a cyclist from Mwanza emerged winner of the women’s race.

  0 0

   Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania ( TUCTA )Nicholaus Mgaya akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipowasili kwenye Makao Makuu ya TUCTA kwa mazungumzo na Viongozi wa vyama vya wafanyakazi.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Wanawake,Jinsia na Watoto (TUCTA) Siham Ahmed kabla ya kuanza kwa mazungumzo baina ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi.
    Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania ( TUCTA )Nicholaus Mgaya akizungumza wakati wa kikao cha Viongozi wa vyama vya Wafanyakazi na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye ukumbi wa mikutano TUCTA.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumzwa kwenye kikao na Viongozi wa Vyama Vya Wafanyakazi Tanzania.
   Sehemu ya Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi Tanzania wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
   Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU) Erasto Kihwele akichangia jambo wakati wa kikao hicho. (Picha na Adam H.Mzee)


  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Drive Dentsu, Mr Cheriff Tabet (kushoto)akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ofisi yao Dar es Salaam. Kulia kwake ni Meneja Uendelezaji wa Biashara na Masoko Mapya, Rami El Khalil.

  Mkurugenzi Mkuu wa Drive Dentsu, Mr Cheriff Tabet (katikati)akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ofisi yao Dar es Salaam. Kulia kwake ni Meneja Uendelezaji wa Biashara na Masoko Mapya, Rami El Khalil, na kushoto ni Meneja Mkuu wa Drive Dentsu Tanzania, Terry Greenwood.


  ========  ========  ========= 
               
  Dar es Salaam, 26-August, 2014: Kampuni ya Drive Dentsu, imefungua ofisi zake mpya jijini Dar es Salaam katika jitihada za kusogeza huduma zake kwa wateja wake katika ukanda wa Afrika Mashariki.

  Ikiwa ni kampuni iliyotanda nchi zaidi ya 110, Drive Dentsu ni sehemu ya muunganiko wa kimataifa wenye zaidi ya wafanyakazi 37000 na ofisi 160 duniani kote, muunganiko ambao unaleta pamoja ujuzi, maarifa na vitendea kazi vyenye kuhakikisha inawapa wateja wake huduma zenye ubora wa hali ya juu.

  Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Bw. Cheriff Tabet, Mkurugenzi Mkuu wa Drive Dentsu, amesema ufunguzi wa ofisi mpya ya Drive Dentsu jijini Dar unalenga kutoa suluhisho la ubunifu kwa makampuni na bidhaa za kitanzania.

  Bw. Tabet amesema pamoja na kuwekeza nchini Tanzania, Drive Dentsu imelenga kujipanua katika masoko mengine katika ukanda huu ili kuhakikisha wanakidhi mahitaji yao kwa kutoa suluhu kwa changamoto zote za kibiashara.

   “Katika ukanda wa Afrika Mashariki, uchumi wa Tanzania umekua ukikua kwa kasi kubwa pamoja na ongezeko la uzalishaji wa bidhaa nyingi jambo ambalo linakuza mazingira yenye ushindani hivyo kufanya kuwepo na uhitaji mkubwa wa ubunifu katika kuwafikia wateja’  anasema Bwana Tabet.

  Tabet pia anasema kuwa Drive Dentsu inaleta uzoefu wake mkubwa, nchini Tanzania, ambao umewawezesha kutwaa tuzo 17  za kimataifa na kitaifa katika tasnia ya ubunifu wa matangazo. Naye Bw. Rami El Khalil, Meneja Mkuu wa Masoko na Maendeleo ya Biashara wa Drive Dentsu anasema Tanzania ni nchi yenye fursa nyingi kutokana na uchumi wake kuwa imara hivyo ni sehemu nzuri kuwekeza.

  ‘Drive Dentsu itaweka muhimili mpya katika tasnia hii ikiwa na mtazamo mpya wenye kusaidia chapa kujidhihirisha na kutambulika kwa watumiaji wake’ anasema Bw. Rami. Pia Drive Dentsu wamewekeza katika wataalam mahiri walioko nchini, hili linajidhirisha walipomteua Terry Greenwood kuwa Meneja Mkuu wa kampuni hiyo nchini Tanzania.

  Terry mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 41 katika tasnia ya mawasiliano, amepata uzoefu huo katika makampuni mbalimbali huko Amerika, China na Mashariki ya Kati. Pia kwa miaka saba sasa amekuwa akifanya kazi na Drive Dentsu.

  Kwa uzoefu wake na ushirikiano kutoka kwa mtandao wa Drive Dentsu kimataifa tunaamini ataleta mapinduzi katika tasnia ya utengenezaji matangazo. Wateja wa Drive Dentsu kwa sasa ni kama Zantel, Moov, Moneygram, Radisson Royal Hotel, Daihatsu, Hitachi, Jammal Trust Bank, Toshiba, Lexus, Bridgestone, Jumeirah dot Shabaka, Toyota, Virgin, Abdul Latif Jameel na Vitaene C.

  ‘Ofisi zetu nchini Tanzania zitakuwa ni sehemu ya kuimarisha muunganiko wetu kimataifa, pia itaiwezesha Drive Dentsu kuwasaidia wateja wetu kukabiliana na mabadiliko ya kila siku katika biashara’ anamaliza Bwana Rami. 

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mheshimiwa John Mongela akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uongezaji virutubishi katika ngazi ya jamii mkoani Arusha leo,   kushoto kwake ni Dr. Vicent Assey kutoka Wizara ya Afya –makao makuu na kulia kwake ni  Kaimu Mganga mkuu wa Arusha ,Dr. Omary Chando.Uzinduzi huo ulianza kwa mafunzo maalumu kutoka wizara ya Afya ikishilikiana na taasisi ya chakula na Lishe (TFNC)  kutolewa kwa viongozi wa juu wa Mkoa pamoja na wakuu wa wilaya za Monduli, Karatu na Arumelu. Kushoto kwa mkuu wa wilaya ni Dr. Vicent Assey kutoka Wizara ya Afya –makao makuu na kulia kwake ni Dr. Omar

  0 0

  OFISI ya Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma, imetoa ufafanuzi juu ya taarifa zilizotolewa kwenye vyombo vya habari kuhusu kuchelewa kwa malipo ya posho za Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba.

  Ufafanuzi huo umetolewa leo na Mkurugenzi wa Habari na Itifaki Bw. Jossey Mwakasiyuka wakati alopokutana na waandishi wa habari kwa lengo la kutolea ufafanuzi kuhusiana na taarifa hizo zilizoikera ofisi hiyo ya Bunge Maalum.

  Mwakasyuka amevieleza vyombo vya habari kuwa, ofisi ya Bunge Maalum imekerwa na kuchapishwa kwa taarifa hizo na baadhi ya vyombo vya habari kwani taarifa hizo ni za upotoshaji na zina lengo la kuwadhalilisha Waheshimiwa Wajumbe na kuwafanya waonekane wenye kuishi na kufanya kazi kwa kutegemea posho wanazolipwa.

  “Ni vema ikaeleweka kwamba Wajumbe wa Bunge Maalum wote ni watu wenye nafasi zao katika jamii na ni wenye kazi au shughuli zao mahususi zinazowaingizia kipato na kwamba Ujumbe wa Bunge Maalum ni nafasi ya muda tu ya kutimiza jukumu la kuliandalia taifa Katiba Mpya”. Alisema Mwakasyuka.

  Mwakasyuka ameongeza kuwa, si vema kwa vyombo vya habari kuwadhalilisha Wajumbe hao kwa njia yoyote ile kwani kwa kufanya hivyo kunawavunja moyo na kuwafanya washindwe kuifanya kazi ya Bunge Maalum vizuri kama ilivyotarajiwa na wananchi.

  Akifafanua kuhusiana na malipo ya posho hizo, Mkurugenzi Mwakasyuka ameviambia vyombo vya habari kuwa, Wajumbe wote wa Bunge Maalum ambao wanahudhuria vikao vinavyoendelea wamekwishalipwa posho zao zote kama wanavyostahili.

  “Ni vyema ikaeleweka kwamba malipo ya posho yanafuata taratibu za fedha za umma na yanapita kwenye mchakato maalum unaojumuisha kupata orodha za mahudhurio ya Wajumbe kwenye kikao, upatikanaji wa fedha toka Hazina, na upatikanaji wa fedha toka Benki, hivyo wakati mwingine huchukua siku kadhaa hadi kukamilika.” Alifafanua Mwakasyuka.

  Aidha, Mwakasyuka amevitahadharisha vyombo vya habari vinavyondika habari za Bunge Maalum kuzingatia maadili na kanuni za Uandishi wa habari zinazotolewa katika vikao vya Bunge Maalum ili taarifa kama hizo za upotoshaji zisijirudie tena.

  “Kumbukeni kuwa wajibu wenu ni kuhabarisha umma na sio kupotosha umma na hata kuleta usumbufu kwa jamii kutokana na uandishi usio makini”. Alionya Mwakasyuka.

  Katika kanuni za Bunge Maalum, kanuni ya 77 inawataka waaandishi wa habari kuandika habari za Bunge Maalum kwa weledi mkubwa kwa kuzingatia maadili ya uandishi wa Habari ili kuondoa uandishi wenye kuleta chuki kati ya Serikali na Wananchi wake kwani kinyume na kanuni hiyo, Katibu anaweza wakati wowote kuondoa ruhusa aliyotoa kwa mwakilishi wa chombo chochote cha habari iwapo chombo hicho kitatoa taarifa yoyote kuhusu shughuli za Bunge Maalum ambayo kwa maoni ya Bunge Maalum inapotosha ukweli au vinginevyo inakiuka kanuni, taratibu au haki za Bunge Maalum.
  Mkurugenzi wa Habari na Itifaki, Bw. Jossey Mwakasyuka (kushoto) akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na malipo ya posho za Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba leo katika ukumbi wa mikutano ofisi ya Bunge mjini Dodoma.
  Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wakisikiliza kjwa makini maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari na Itifaki, Bw. Jossey Mwakasyuka wakati alipofanya mkutano na waandishi hao kwa lengo la kutolea ufafanuzi kuhusiana na malipo ya posho za Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba leo katika ukumbi wa mikutano ofisi ya Bunge mjini Dodoma. (Picha zote na Benedict Liwenga-Maelezo).

  0 0

  Na John Gagarini, Kibaha

  RAIA wa nchi ya Ethiopia Dawita Alalo (25) amekufa alipokuwa akipatiwa matibabu kwenye kituo cha afya cha Chalinze kata ya Bwiringu wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

  Marehemu alikuwa ni kati ya raia 48 wa nchi hiyo walikamatwa wakiwa kwenye msitu wa kijiji cha Visakazi Ubena Zomozi tarafa ya Chalinze Agosti 22 mwaka huu, baada ya kuingia nchini bila ya kibali.

  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kibaha kaimu kamanda wa polisi mkoani humo Mrakibu Mwandamizi (SSP) Athuman Mwambalaswa alisema kuwa marehemu ni miongoni mwa wahamiaji haramu 11 waliokuwa wamelazwa kituoni hapo wakipatiwa matibabu.

  Kamanda Mwambalaswa alisema kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 26 majira saa 7:30 usiku alipokuwa akipatiwa matibabu kituoni hapo baada ya kuugua ugonjwa wa malaria.

  Wakati huo huo mlinzi wa baa ya Silent Inn Jamat Mandama (55) amefariki dunia baada ya kunywa pombe nyingi bila ya kula chakula.

  Alisema kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 27 mwaka huu majira ya saa 1 usiku huko Umwe kata ya Ikwiri wilayani Rufiji.

  Aidha alisema kuwa mlinzi huyo alikutwa amekufa akiwa lindoni kwenye baa hiyo.

  0 0

  Na   Magreth Kinabo, Dodoma

  Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Jakaya Mrisho  Kikwete ameahidi kuonana na Viongozi wa Vyama vya Siasa vinavyounda Kituo cha Demkrasia Tanzania(TCD) kabla ya mwisho wa wiki kwa lengo la kushauriana.

   Kauli  hii imetolewa na Mwenyekiti wa TCD,Mhe. John  Cheyo mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi  wa   katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Bunge.

  Mhe. Cheyo alisema Rais Kikwete amekubali kuonana nao kufutia kikao chao walichokaa kwa pamoja ambacho kilihusisha viongozi  wakuu wa vyama hivyo, Agosti 23,mwaka huu, ambapo walijadili na kutafakari maendeleo ya mchakato wa Katiba Mpya.

  Alisema viongozi hao, katika kiako hicho cha  pamoja na mambo mengine waliazimia kutafuta nafasi ya kuonana na Rais Kikwete kwa  ajili ya lengo hilo, ambapo kufutia azimio hilo, Mwenyekiti huyo aliwasiliana  naye  alilipokea  azimio  hilo na kuahidi kufanya hivyo.

  “Tutalishauri taifa kwa maoni tutakayokubaliana na Rais,” alisema Mhe. Cheyo bila ya kutaja agenda  juu ya jambo hilo.

  Aliongeza kuwa  watazunguza na kutafakati ili  kuhimarisha amani na mchakato huo utoe matunda mema.

  Mhe. Cheyo alisema kikao hicho kilifanyika na kuhusisha vyam vyote vilivyoko  katika TCD.

  Alisema hii ni mara ya kwanza kwa TCD  kumwomba Rais Kikwete kuonana naye na kukubali ombi hilo.

older | 1 | .... | 550 | 551 | (Page 552) | 553 | 554 | .... | 3286 | newer