Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 549 | 550 | (Page 551) | 552 | 553 | .... | 3286 | newer

  0 0

   Wafanyakazi wanaume wa Kampuni ya Toyota Tanzania, wakishindana kukuna Nazi wakati wa Bonanza maalumu la kuwapongeza wafanyakazi lililoandaliwa na Kampuni hiyo lililofanyika kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam, juzi Agosti 23, 2014. Katika Bonanza hilo timu ya Rav 4 iliibuka mshindi wa jumla katika michezo yote iliyochezwa ikifuatiwa na timu ya Hilux, VX na Prado. 
   Wafanyakazi wanaume wa Kampuni ya Toyota Tanzania, wakishindana kukuna Nazi wakati wa Bonanza maalumu la kuwapongeza wafanyakazi lililoandaliwa na Kampuni hiyo lililofanyika kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam, juzi Agosti 23, 2014. Katika Bonanza hilo timu ya Rav 4 iliibuka mshindi wa jumla katika michezo yote iliyochezwa ikifuatiwa na timu ya Hilux, VX na Prado.
   Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Toyota Tanzania,  Bw. Vinod Rustagi, akimkabidhi Kombe la ushindi wa jumla katika michezo yote mwakilishi wa timu ya RAV 4, Mumma Nyamhanga, wakati wa hafla ya Bonanza maalum la kuwapongeza wafanyakazi wa Kampuni hiyo lililofanyika kwenye ufukwe wa Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es salaam, mwishini mwa wiki. Kushoto ni mwamuzi wa michezo hiyo, Othman Kazi. 

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Johstone Frank Maunda akimvisha pete mkewe kipenzi Noela Julian Kaigwa katika ibada takatifu iliyofanyika Agosti 23, 2014 katika Kanisa la MT. Albano Dar es Salaam. Ndoa hiyo ilifuatiwa na tafrija kubwa iliyofanyika katika ukumbi wa Coco Beach. 


  0 0

  Waziri wa Maji,Mhe. Prof. Jumanne Maghembe akikagua ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita million 5.5 kwa ajili ya kuhudumia wakazi wapatao 20,000 katika eneo la Itege mjini Dodoma. Tanki hilo ni miongoni mwa matenki manne yanayoendelea kujengwa. Ujenzi wa mradi huu unajengwa kwa ushirikiano wa Serikali za Tanznia na Jamhuri ya Korea kwa gharama ya Sh. Billion 78. 
  Mkandarasi wa Ujenzi wa Matanki hayo akimuelekeza kitu Waziri wa Maji,Mhe. Prof. Jumanne Maghembe wakati alipofika kukagua ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita million 5.5 kwa ajili ya kuhudumia wakazi wapatao 20,000 katika eneo la Itege mjini Dodoma.


  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard K. Membe akitoa hotuba kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Michezo ya shule za Sekondari za Afrika Mashariki yajulikanayo kama FEASSSA (Federation of East Africa Secondary Schools Sports Association), jana katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) Mhe. Hawa Ghasia akiwakaribisha wanamichezo kutoka Afrika Mashariki katika mashindano ya Michezo ya shule za Sekondari za Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 22 Agosti hadi 1 septemba mwaka huu 2014.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (wakwanza kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (kulia) wakifuatilia kwa makini matukio yaliyokuwa yyakiendelea wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Michezo ya Shule za Sekondari za Afrika Mashariki yajulikanayo kama FEASSSA jana katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Pwani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Maandalizi ya FEASSSA Bi.Mwantumu Mahiza akielezea jinsi Tanzania ilivyojiandaa kufanikisha mashindano hayo wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Michezo ya shule za Sekondari za Afrika Mashariki jana katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar esSalaam.
  Timu ya Mpira wa Miguu kutoka Shule ya Sekondari Makongo Tanzania katika picha ya pamoja kabla ya mechi na Timu ya Mpira wa Miguu kutoka Uganda wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Michezo ya shule za Sekondari za Afrika Mashariki yajulikanayo kama FEASSSA jana katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
  Wanafunzi wa shule za Sekondari kutoka Tanzania ambao wanashiriki mashindano ya Shule za Sekondari za Afrika Mashariki wakiwa kwenye maandamano ya uzinduzi wa mashindano hayo jana katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Meneja Masoko wa Airtel Bi Prisca Tembo na Meneja Biashara wa Techno bw, Marco Wang wakionyesha simu mpya ya TechoH5 iliyoingizwa sokoni ikiwa na ofa kabambe itakawawezesha wateja wa Airtel kupata simu ya kisasa pamoja na vifurushi vya internet ya kudumu kwa muda wa mienzi mitatu kuanzia leo.
  Afisa Mauzo wa airtel Nizar Aladawy na Afisa Mauzo wa Techno bi, Lolinda Joshman wakionyesha simu mpya ya TechoH5 iliyoingizwa sokoni ikiwa na ofa kabambe itakawawezesha wateja wa Airtel kupata simu ya kisasa pamoja na vifurushi vya internet ya kudumu kwa muda wa mienzi mitatu kuanzia leo. Meneja Masoko wa Airtel Bi Prisca Tembo na Meneja Biashara wa Techno bw, Marco Wang wakionyesha simu mpya ya TechoH5 iliyoingizwa sokoni ikiwa na ofa kabambe itakawawezesha wateja wa Airtel kupata simu ya kisasa pamoja na vifurushi vya internet ya kudumu kwa muda wa mienzi mitatu kuanzia leo.

  Airtel kupitia huduma ya Switch on yazindua ofa kambabe ya simu ya Tecno H5 Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia huduma yake ya Switch on leo imezindua ofa kabambe itakayowawezesha wateja wa Airtel kupata simu ya kisasa ya TECNO H5 pamoja na vifurushi vya internet ya kudumu kwa muda wa mienzi mitatu.

  Akiongea wakati wa uzinduzi, Meneja Masoko wa Airtel Bi Prisca Tembo alisema" ofa hii maalumu itawawezesha wateja kununua simu hii ya TECNO H5 na kupata simcard ya bure pamoja na kifurushi cha internet cha muda wa mienzi mitatu kitakachomuwezesha kupiga simu katika muda huu wa mienzi mitatu kwa gharama nafuu ya shillingi 1 kwa sekunde".

  "TECNO H5 ina vitu vinavyovutia ndani ya simu kama vile , camera aina ya Mega pixel yenye uwezo wa kutoa picha nzuri, nafasi ya kutunza data wa kiasi cha 4GB, pamoja na memory card yenye ukubwa wa mpaka 32GB, simu hii pia inatumia technologia ya android na pia ni raisi kuibaba kwani ina ukubwa wa kati.

  Simu ya TECNO H5 inapatikana katika maduka yote Tanzania kwa kiasi cha gharama ya shilingi 129,000/= "aliongeza Tembo.

  TECNO H5 itawapa nafasi wateja wa Airtel kupata huduma ya internet na kuunganishwa na huduma ya SWITCH ON iliyowekwa maasusi kwa watumiaji wa huduma ya internet Tanzania, na kuwapatia internet ya kasi kwa bei nafuu. Kupata huduma hii ya SWITCH ON ni rahisi mteja anatakiwa kupiga *148*22# na kuchagua kifurushi cha internet na kisha kupata ujumbe utakao muhakikishia kuunganishwa na huduma ya SWITCH ON na kuanza kufurahia intenet bila kikomo.

  Ofa hii ni kati ya ofa nyingi zinazotolewa na Airtel kwa wateja wake, sambamba na ofa hii ya TECNO H5 Airtel pia inatoa vifurushi vya YATOSHA vya kupiga simu,ujumbe mfupi , internet na pamoja na ofay a HAKATWI MTU HAPA inayowawezesha wateja wake kutuma na kupokea pesa kwa nusu gharama.

  0 0

  Na Andrew Chale,Dodoma.

  MAONYESHO ya wafanyabiashara kipindi cha Bunge Maalum la Katiba yanaendelea kwa kasi mjini hapa na kuwakutanisha wajasiriamali zaidi ya 100 katika viwanja vya Mashujaa.

  Akizungumza katika maonyesho hayo,Mwenyekiti wa wajasiriamali, Dokta Haruna Kifimbo, alisema lengo kuu la maonyesho hayo ni kutoa fursa kwao kuuza na kunadi bidhaa zao kwa watu mbalimbali wakiwemo wajumbe wa Bunge hilo.

  “Mpaka sasa tuna wajasiriamali 100, ambao wanaendelea na maonyesho yao kwenye viwanja hivi vya Mashujaa kuanzia Agosti 10 mwaka huu, na maonesho yataendelea mpaka litakapomalizika Bunge la Katiba, hivyo bado tunaendelea kupokea wajasiliamari wengine zaidi,” alisema Dk. Kifimbo.

  Alisema kuwa maonyesho hayo yanajumuisha wauzaji wa bidhaa za tiba mbadala, bidhaa za majumbani, kazi za mikono kutoka ndani na bidhaa zingine mbalimbali.

  Kifimbo ambaye ni mganga wa tiba mbadala alisema maonyesho hayo yatazinduliwa rasmi Agosti 21, mwaka huu, na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi, na kutoa rai kwa wananchi kushiriki.

  Lengo ya maonyesho ni kutoa fursa kwakuuza na kunadi bidhaa zao kwa watu mbalimbali wakiwemo wajumbe wa Bunge hilo.
  Mwenyekiti wa wajasiriamali, Dokta Haruna Kifimbo (Kulia) akipata maelezo ya moja ya banda linaloonyesha na kuuza bidhaa zake za madishi na vifaa vya umeme, kwenye maonesho ya biashara za wajasiriamali yanayoendelea katika viwanja vya Mashujaa, mjini Dodoma.
  Baadhi ya wateja wakichagua moja ya bidhaa za dvd na cd zinazouzwa kwenye mabanda hayo.

  Baadhi ya wakina mama wakiwa wanaangalia bidhaa mbali mbali zinazouzwa katika mabanda ya wajasiriamali hao yanayoendelea hivi sasa mjini Dodoma.

  0 0

  Waziri wa Vijana,Utamaduni na Michezo Dk Fenera Mkangara akiongoza ugeni toka klabu ya Real Madrid ulipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA.)

  Baadhi ya wachezaji wa zamani wa klabu ya Real Madrid wakiwasili katika uwanja wa Ndege wa KIA .

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Balozi Mdogo wa Tanzania-Dubai,Mhe. Omar Mjenga akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wakuu wa benki ya UBL ya Dubai,Bw. Shaikh Muhammad Liaque, Makamu wa Rais wa UBL (kushoto) na Bw. Syed Abbas Bokhari walipomtembelea ofisini kwake leo.
  Wakiwa katika mazungumzo,ambapo Mhe. Mjenga amewaomba kuangalia uwezekano wa kuajiri Watanzania kwenye Benki hiyo kuja kufanya kazi Dubai. Mwaka jana, UBL ilifungua ofisi zake jijini Dar es salaam. Mh. Mjenga amewaomba pia kuifanya ofisi ya Dar es salaam kuwa ofisi ya Kanda ya Afrika. Aidha, wamegusia suala la kufungua matawi zaidi Arusha, Moshi, Mwanza, Mbeya na Matawi mengine zaidi Jijini Dar es salaam. Hii yote itafanikisha kuongeza nafasi za ajira kwa Watanzania .

  0 0

   Ms. Esra Esriti Managing Director of Aydin logistics joined by The Ambassador of Turkey to Tanzania Mr. Ali Davudoglu and Vingunguti primary school officials Mr. Calist Chuwa during the handover of the desks at Vingunguti.

  Students of Vingunguti primary school sitting down during the donation ceremony.


   =========   =========    =======

  The education system in Tanzania has been criticized however there are various efforts put in place to reform the sector by both the government and the private corporation.  Consequently, Aydin Logistics joined by the Ambassador of Turkey to Tanzania, Mr. Ali Davudoglu donated 100 desks worth 10 Million Shillings to Vingunguti Primary School during the weekend. 

  We believe that it is obvious that the pupils of Vingunguti cannot perform well if they do not have desks or chairs. We understand that education plays a crucial role in the social and economic development of the community hence this is part of our corporate social responsibility (CSR) through which we support the community around us.

  According to the Managing Director, Ms. Esra Esriti, “We feel proud to be part of the school in endeavoring education system and Aydin Logistics is focusing on improving the education system in Tanzania, as it is key to breaking out of the cycle of poverty.  In order to improve the learning environment we have begun this new bond between Vingunguti Primary School and Aydin Logistics; these 100 desks is the beginning of our relationship and we will continue to support this school so that we can have a conducive environment of learning for the pupils.”

  Vingunguti Primary School Head teacher Mr. Calist Chuwa thanked Aydin Logistics and the Ambassador for their generous donation pledging to make good use of the desks. “Not all classrooms in schools with a good pupil to classroom ratio are healthy environments for learning. 
  Our school has 2350 pupils, but all are seated in only 16 classrooms, whose capacity can only accommodate 720 pupils at the average of 45 in one class. So, for the given data of 2350 the class now accommodating up to 147 pupils at a go. In this case the school needs extra 37 classes to be 53 classrooms and that will fill the gap and lead to a better learning environment for Vinguguti primary School children,” said Mr. Chuwa.

  0 0

  Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

  Jopo la majaji lililoundwa kwa ajili ya kumtafuta mshindi wa tuzo ya Rais ya huduma za jamii na uwezeshaji katika miradi ya madini, gesi na mafuta linatarajia kuanza kazi yake kesho, imeelezwa.

  Akizungumza katika kikao na majaji watakaoshiriki katika zoezi hilo kilichofanyika kwenye ofisi za Wizara ya Nishati na Madini Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava amesema kuwa kazi hiyo inayotarajiwa kukamilika Septemba 24, 2014 itahusisha mikoa yote ambayo miradi ya madini, gesi na mafuta inaendesha shughuli zake.

  Mhandisi Mwihava alisema lengo la zoezi hilo ni kushindanisha makampuni yanayoendesha shughuli za madini, mafuta na gesi katika utoaji wa huduma bora kwa jamii.

  Alieleza kuwa mara baada ya jopo la majaji kumaliza kazi yake, litawasilisha ripoti kamili ya zoezi hilo ambayo itadurusiwa kabla ya kukabidhiwa rasmi kwa ajili ya maandalizi ya halfa ya utoaji tuzo inayotarajiwa kufanyika mapema Novemba mwaka huu.

  “Tanzania imewaamini katika kazi hiyo, hivyo ni imani yangu kubwa mtatumia utaalamu na uzoefu wenu katika zoezi hilo pasipo kupendelea kampuni yoyote. “ Alisisitiza Mhandisi Mwihava.

  Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Uunganishaji na Shirikishi Wadau katika Tasnia ya Uziduaji (Extractive InterStakeholders Forum, EISF) Bi. Catherine Lyombe aliainisha maeneo yatakayoangaliwa kama mchango wa makampuni yanayoendesha shughuli za madini, gesi na mafuta kuwa ni pamoja na elimu, maji, afya, ajira na miundombinu.

  Akielezea zoezi litakavyofanyika Bi. Lyombe alieleza kuwa majaji watatembelea maeneo yote yenye makampuni yanayoendesha shughuli za madini, gesi na mafuta na kuzungumza na wahusika pamoja na kuzungumza na wananchi ili kupata picha kamili ya mchango wa makampuni husika kwa jamii.

  Bi. Lyombe alisisitiza kuwa mbali na kupata taarifa kutoka katika makampuni na maelezo kutoka kwa wananchi kama wataalamu watafanya ulinganisho wa maelezo yanayotolewa na wananchi na tathmini halisi ya utekelezaji wa miradi iliyotekelezwa na kampuni husika.

  Aliongeza kuwa lengo la utoaji wa tuzo hizo ni mkakati wa kuhamasisha makampuni ya madini, mafuta na gesi kuboresha huduma zake kwa jamii. “ Mshindi wa tuzo ya Rais ya huduma za jamii na uwezeshaji katika miradi ya madini, mafuta na gesi anapopatikana, anatia hamasa kwa makampuni mengine kuboresha huduma zake na wananchi kuendelea kunufaika na uwepo wa makampuni hayo” alisisitiza Bi. Lyombe.

  Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji (Presidential Award on Corporate Responsibility and Empowerment –CSRE in Extractive Industry) katika miradi ya madini, gesi na mafuta ilizinduliwa mwaka 2012 na Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kama mkakati wa kuhamasisha makampuni ya madini, gesi na mafuta kuboresha huduma zake kwa jamii hususan katika maeneo ya elimu, maji, miundombinu, ajira na afya.

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava akizungumza na jopo la majaji na sekretarieti inayotarajia kuanza kazi ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji (Presidential Award on Corporate Responsibility and Empowerment –CSRE in Extractive Industry).
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Uunganishaji na Shirikishi Wadau katika Tasnia ya Uziduaji (Extractive InterStakeholders Forum, EISF) Bi. Catherine Lyombe akielezea jinsi zoezi la kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji (Presidential Award on Corporate Responsibility and Empowerment –CSRE in Extractive Industry) litakavyoendeshwa katika kikao hicho.

  0 0

  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpokea Mama Graca Machel aliyemtembelea kwenye ofisi za WAMA tarehe 25.8.2014.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na mgeni wake Mama Graca Machel wanaonekana wakifurahia jambo kabla ya kupiga picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya WAMA.
  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mgeni wake Mama Graca Machel na wajumbe wawili wa Bodi ya WAMA. Wajumbe hao ni Mheshimiwa Sophia Simba,Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto (kulia) na Mama Hulda Kibacha (wa kwanza kushoto).
  Mama Garaca Machel akiweka saini kitabu cha wageni wakati alipotembelea ofisi za WAMA tarehe 25.8.2014.
  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Bodi ya WAMA akimkabidhi zawadi ya picha mgeni wake Mama Graca Machel aliyemtembelea ofisini kwake tarehe 25.8.2014.


  0 0

  Na Veronica Kazimoto,Ludewa

  Wito umetolewa kwa wamiliki wote wa viwanda waliopo katika wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe kutoa taarifa sahihi na ushirikiano wa kutosha kwa wadadisi wakaopita katika viwanda vyao ili kufanya zoezi la Uorodheshaji wa Viwanda kwa ajili ya maandalizi ya Sensa ya Viwanda inayotarajia kufanyika mwezi Septemba, 2014.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo mkoani Iringa, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Meneja Takwimu mkoa wa Iringa na Njombe Fabian Fundi amesema zoezi hilo linaanza rasmi leo tarehe 25 Agosti, 2014 na litamalizika siku ya Jumapili tarehe 31 Agosti, 2014.

  “Zoezi la Uorodheshaji wa Viwanda wilaya ya Ludewa linaanza rasmi leo na litahusisha jumla ya kata kumi na sita ambazo ni pamoja na Ludende, Lugarawa, Ruhuhu, Lupanga, Lwela, Mavanga na Mundindi”, amesema Fundi.

  Amezitaja kata nyingine kuwa ni, Ibumi, Mlangali, Kilondo, Madope, Lupingu, madilu, Makonde, Mkongobaki na Lifuma.

  Fundi amefafanua kuwa taarifa zinazokusanywa katika zoezi hili kutoka viwandani ni pamoja na jina la kiwanda, anuani za kiwanda, mahali kiwanda kilipo, aina ya umiliki na utaifa wa mmiliki.

  Taarifa nyingine ni gharama za malipo mbalimbali kwa wafanyakazi, mwaka kiwanda kilipoanzishwa, aina ya bidhaa zinazozalishwa, idadi ya wafanyakazi na gharama za uzalishaji.

  Zoezi hili la Uorodheshaji wa Viwanda lilianza tarehe 8 Aprili, 2014 kwa Tanzania Bara na mpaka sasa karibu maeneo yote zoezi hili limekwisha kamilika.
  Meneja Takwimu Mkoa wa Iringa na Njombe Fabian Fundi akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu zoezi la Uorodheshaji wa Viwanda limeloanza rasmi leo wilayani Ludewa kwa ajili ya maandalizi ya Sensa ya Viwanda inayotarajia kufanyika mwezi Septemba, 2014.
  Meneja Takwimu Mkoa wa Iringa na Njombe Fabian Fundi akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa waandishi wa habari (hawapo pichani) uliofanyika leo Mkoani Iringa kuhusu zoezi la Uorodheshaji wa Viwanda limeloanza rasmi leo wilayani Ludewa kwa ajili ya maandalizi ya Sensa ya Viwanda inayotarajia kufanyika mwezi Septemba, 2014. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO - LUDEWA)

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Anna Maembe akizungumza katika uzinduzi wa kampeni maalumu za kitaifa za kupinga ndoa za utotoni (National Ending Child Marriage Campaign), zitakazo endeshwa Mkoani Mara. Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Anna Maembe akizungumza katika uzinduzi wa kampeni maalumu za kitaifa za kupinga ndoa za utotoni (National Ending Child Marriage Campaign), zitakazo endeshwa Mkoani Mara.Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Nsoka (kwanza kulia) akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni maalumu za kitaifa za kupinga ndoa za utotoni (National Ending Child Marriage Campaign), zitakazo endeshwa Mkoani Mara. Kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi nchini (UNHCR), Bi. Joyce Mendez Kole. Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Nsoka (kwanza kulia) akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni maalumu za kitaifa za kupinga ndoa za utotoni (National Ending Child Marriage Campaign), zitakazo endeshwa Mkoani Mara. Kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi nchini (UNHCR), Bi. Joyce Mendez Kole.Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi nchini (UNHCR), Bi. Joyce Mendez Kole akizungumza katika hafla hiyo. Kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), Dk. Natalia Kanem. Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi nchini (UNHCR), Bi. Joyce Mendez Kole akizungumza katika hafla hiyo. Kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), Dk. Natalia Kanem.Mwakilishi Mkazi wa UN Women nchini Tanzania, Anna Collins (wa kwanza kushoto) akizungumza katika hafla hiyo. Mwakilishi Mkazi wa UN Women nchini Tanzania, Anna Collins (wa kwanza kushoto) akizungumza katika hafla hiyo.


  0 0

  African ladies are otherwise known for other things than Boxing, except for this one who is changing and making the story looks different.
  Ms.Bintou Yawa Schmill, 29 years young, a totally black African breed  1.71m, Togo born and based in Germany, started her boxing career at a tender age. Something she did as an Amature has become a success story. She wickedly punched competitors, messlessly and won 24 fights ,and 2 draw in the category welterweight -64Kg.

  Her fingerprint show her since 2007, to have been a professional boxer with unbeatable record of 4 fights, 4wins in a package including 3 K. O

  Her case study is exceptional, she has not only broken the gender rule, she’s representing the African continent in a Boxing ring , punching evil out the brains of her competitors, Bintou is the Lioness that roars and the Lions make a way. Now she´s back on stage, live and ready for a face2face catch, one on one.


  Any brave hearted out there to sponsor and make a name with Bintou? Bintou needs you to make it happen… a man is a man because of another man –UBUNTU
  For more information write to

   Africans support your children and make them proud NOW!


  0 0

  Spika wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA) Dk. Margaret Nantongo Zziwa  akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dar es Salaam leo juu ya mkutano wa kwanza wa Bunge la tatu unaotaraji kuanza leo katika ukumbi wa Karimjee na kufunguliwa na Rais Jakaya Kikwete kesho kutwa. 
   Spika wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA) Dk. Margaret Nantongo Zziwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dar es Salaam jana juu ya mkutano wa kwanza wa Bunge la tatu unaofanyika ukumbi wa Karimjee. Wengine kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Amantius Msole, wabunge wa EALA kutoka Tanzania Twaha Taslima na Shy Rose Banji
  Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Wabunge kutoka Tanzania, Adam Kimbisa, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika ofisi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dar es Salaam leo, juu ya mkutano wa kwanza wa Bunge la tatu unaofanyika ukumbi wa Karimjee. Kushoto ni Spika wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA) Dk. Margaret Nantongo Zziwa,wabunge wa EALA kutoka Tanzania, Twaha Taslima na Shy Rose Banji. PICHA ZAIDI --FATHER KIDEVU BLOG 

  0 0

  Baada ya kuona kuwa kuna maeneo mbalimbali ya vivutio vya kitalii muhimu na ambavyo vimesahaulika kwa njia moja au nyengine na pengine hakuna pa kuvitangaza ili watanzania na Dunia kwa ujumla wapate kuvifahamu kwa ukaribu , Tone Multimedia Group kupitia mtandao wake wa Mbeya yetu Blog wameamua kuanza rasmi kuvitembelea na kutangaza kwa Jamii kwa ujumla  wapate kuvifahamu ili nao waje kuvitembelea.

  Safari hiyo ambayo moja kwa moja ilianzia Mkoa wa Mbeya Wilaya ya Rungwe-Tukuyu kwenda kujionea vivutio hivyo mbalimbali kikiwepo cha kwanza kabisa ambacho ni Kijungu eneo ambalo ni la kipekee na lenye historia ya aina yake.

  Hivi ndivyo safari ilivyokuwa Fuatilia hapa kwa makini.
  Kwanza kabisa tulifika katika kibao hiki ambacho kimetoa maelezo ya awali ikiwa ni pamoja na Bei ambazo mtu anatakiwa kutozwa wakati anapotaka kuingia katika eneo hilo, Bei hizo zimewekwa na uongozi wa Serikali ya Kijiji ambapo fedha hizo zinasaidia katika mambo mbalimbali za kuendeleza kijiji hicho ingawa hata hivyo kuna changamoto kadha wa kadha ambazo zinawakabili ikiwa ni pamoja ni Gharama kubwa za kuingia katika eneo hilo kwa wazawa ambapo haichagui kwamba umetoka nje ya nchi au ndani  Jambo ambalo Serikali inapaswa kutazama kwa sababu ni zaidi hata ya kuingia katika Hifadhi za Taifa.
  Picha hii ilipigwa kwa juu kabisa kuonesha Jinsi eneo la Kijungu linavyo onekana 
  Hapa ni eneo ambalo Maji ya mto huo yanatokea katika eneo linaitwa Namba One eneo la ukanda wa juu kabisa wa eneo hilo, Majihayo pamoja na mengine mengi hata wakati wa mvua kubwa ni lazima yazunguke yanapo kwenda lakini mwisho wa siku ni lazima yaishie hapa, Pia hapa ndipo maji haya yanapoanza kutililikia moja kwa moja katika kijungu.


  0 0

  FAINALI za mashindano ya Safari Pool Taifa yajulikanayo kama “Safari National Pool Competition 2014”, mkoa wa kimichezo wa Temeke jijini Dar es Saalaam na Dodoma zimefanikiwa kupata mabingwa wa mikoa mwishoni mwa wiki.

  Mkoa wa kimichezo wa Temeke mabingwa ni klabu ya Mpo Afrika walifanikiwa kutetea ubingwa wao wa mwaka jana wakati mkoani Dodoma Klabu ya Delux ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa mkoa huo.

  Klabu ya Mpo Afrika na Delux kwa kutwaa ubingwa huo zilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 800,000/= kila klabu pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa katika fainali za kitaifa zinazotarajiwa kufanyika Mkoani Kilimanjaro.

  Upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume, Temeke; Innocent Sammy alifanikiwa kutwaa ubingwa na Dodoma ni Rgnald Kassimu, ambao walizawadiwa pesa taslimu Shilingi 400,000/= kila mmoja katika mikoa yao pamoja na tiketi ya kuwakilisha mikoa yao katika fainali za kitaifa Mkoani Kilimanjaro kwa mchezaji mmoja mmoja Wanaume.

  Upande wa mchezaji mmoja mmoja Wanawaake,Temeke; Rebeca Magaigwa alitwaa ubingwa na Dodoma ni Rehema Mussa, ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi 300,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha mikoa yao katika fainali za kitaifa Mkoani Kilimanjaro kwa mchezaji mmoja mmoja upande wa Wanawake.

  Wiki hii fainali za Safari Pool Competition 2014,ngazi ya mikoa zinatarajiwa kuhitimishwa na mikoa ya Morogoro, Iringa na Mbeya.

  Fainali za kitaifa za 2014 za “Safari National Pool Competion” zinatarajiwa kufanyika Septemba 14 mwaka huu, Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa kushilikisha Mikoa 17 ambayo ni Tabora,Shinyanga,Dodoma Mbeya,Iringa,Morogoro,Mwanza,Kagera,Manyara,Arusha,Tanga,Pwan i,Ilala,Lindi,Temeke,Kinondoni na wenyeji wa mashindano kwa mwaka huu mkoa wa Kilimanjaro.
  Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo(wa pili kulia) akimkabidhi kikombe nahodha wa timu ya klabu ya mchezo wa Pool ya Mpo Afrika, Charles Vernance mara baada ya kutetea ubingwa wa fainali za mchezo huo ujulikanao kama “Safari National Pool Competition 2014” ngazi ya mkoa mkoa wa Temeke uliofanyika Kurasini City Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Kulia ni Katibu wa Chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga na Kocha wa timu ya Taifa, Denis Rungu.
  Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo(wa pili kulia) akimkabidhi pesa taslimu Shilingi 800,000/= nahodha wa timu ya klabu ya mchezo wa Pool ya Mpo Afrika, Charles Vernance mara baada ya kutetea ubingwa wa fainali za mchezo huo unaojulika kama “Safari National Pool Competition 2014” ngazi ya mkoa mkoa wa Temeke uliofanyika Kurasini City Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Kulia ni Katibu wa Chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga na Kocha wa timu ya Taifa, Denis Rungu.
  Baadhi ya wachezaji wa Pool wa klabu ya Mpo Afrika na mashabiki wakishangilia na kikombe mara baada ya kutetea ubingwa wa fainali za mchezo huo unaojulika kama “Safari National Pool Competition 2014” ngazi ya mkoa mkoa wa Temeke uliofanyika Kurasini City Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Dk.Sira Ubwa Mamboya kuwa Waziri wa Kilimo na Maliasili katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar kabla Dk.Sira alikuwa Naibu Waziri wa Afya.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Juma Duni Haji kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar kabla alikuwa Waziri wa Afya.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri wa Afya,awali alikuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano hafla ya kiapo imefanyika katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo.


  0 0
 • 08/25/14--13:52: Article 0


 • 0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua jengo la mihadhara la Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro akisaidiwa na uongozi wa chuo hicho alipotembelea hapo na kuzindua ukumbi wa huo jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wanafunzi, wahadhiri na wananchi katika Chuo Kikuuu cha Mzumbe Morogoro baada ya kuzindua ukumbi wa mihadhara na jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya picha yake ya kuchorwa wakati alipotembelea Chuo Kikuu cha mzumbe ambapo walihutubia wanafunzi, wahadhiri na wananchi katika chuo hicho baada ya kuzindua ukumbi wa mihadhara na jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014.
  Meza kuu ikifurahia jambo wakati Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Mvomero Mhe Amos Makalla akipohutubia wanafunzi, wahadhiri na wananchi katika chuo hicho wakati Rais Kikwete alipotembelea na kuzindua ukumbi wa mihadhara na jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea risala toka kwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Mzumbe Mhe Boniface Maiga wakati Rais Kikwete alipotembelea na kuzindua ukumbi wa mihadhara na jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014.
  Rais wa Serikali ya Wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Mzumbe Mhe Boniface Maiga akisoma risala wakati Rais Kikwete alipotembelea na kuzindua ukumbi wa mihadhara na jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014.
  Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro wakiweka kumbumbuku ujio wa Rais Kikwete alipotembelea hapo na kuzindua ukumbi wa huo jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014.
  Umati wa wanafunzi, wahadhiri na wananchi wakimsikiliza Rais Kikwete akiwahutubia alipotembelea hapo na kuzindua ukumbi wa huo jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa serikali ya wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Mzumbe mjini Morogoro baada ya kuwahutubia chuoni hapo Agosti 25, 2014.

older | 1 | .... | 549 | 550 | (Page 551) | 552 | 553 | .... | 3286 | newer