Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109973 articles
Browse latest View live

Makundi kumi yaingia nusu fainali ya Dansi 100%

$
0
0
Jumla ya makundi kumi yamefanikiwa kuingia katika mchuano wa nusu fainali ya shindano la Dance 100% shindano hilo linaloandaliwa na kituo cha (EATV) chini ya udhamini wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania,yanaendelea kupamba moto ambapo hapo juzi hatua ya robo fainali ilifanyika katika uwanja wa Don Bosco Mbuyuni Namanga jijini Dar es Salaam na makundi 10 yalifanikiwa kuchukua tiketi ya kuingia nusu fainali.

Mratibu wa shindano hilo Happy Shame aliyataja makundi yaliyofanikiwa kuingia nusu fainali kuwa ni Wazawa Crew,Best Boys Crew,G.O.P,The WT,Tatanisha Dancers, Quality Boys, Wakali sisi, Mazabe Powder,The Winners Crew, Dar Crew, Mratibu wa mashindano hayo,Happy Shame,alisema kuwa amefuhishwa na juhudi zinazofanywa na washiriki katika shindano hilo na anawapa pongezi sana majaji kwa kuwa makini na kuweza kupata makundi 10 rasmi yaliyoingia moja kwa moja ngazi ya nusu fainali.

“Huu ni mwaka wa tatu East Africa Televisheni tunaandaa mashindano haya kwa udhamini wa Vodacom Tanzania na Mwaka huu tumeungwa mkono na Grand Malt kama kinywaji rasmi cha Dance 100%. Kwa kweli nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitaweza kutoa shukururani zangu kwa wadhamini kwani wasingekuwa wao tusingekuwa hapa tulipo”Alisema Happy.

Happy, aliongeza kwamba kundi litakaloibuka na ushindi katika mashindano haya ambayo pia yamekuwa yakionyeshwa na kituo cha televisheni cha EATV kila jumatano saa moja kamili usiku,litajishindia kitita cha shilingi milioni 5.

Naye Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wakuu wa mashindano haya,Matina Nkurlu alisema kuwa Vodacom inatoa udhamini kwa kutambua kuwa muziki na michezo ni maeneo ambayo yanaweza kutoa ajira sahihi kwa vijana na kuweza kuwakwamua kimaisha.

Alisema kuwa kwa niaba ya Vodacom Tanzania,anayapongeza sana makundi hayo 10 yaliyoingia nusu fainali na kwa kuwa jukumu la kukabiliana na tatizo la ajira hapa nchini sio la serikali peke yake bali pia ni la watu wote ikiwemo makampuni,taasisi za umma na za binafsi basi wanajisikia fahari sana kwa vijana hao kuingia nusu fainali ndio maana siku zote Vodacom imekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono jitihada za kupambana na tatizo la ajira kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo michezo , burudani.

“Vodacom tunaamini kuwa vijana wanaweza kuleta mapinduzi makubwa katika sekta mbalimbali iwapo watawezeshwa hivyo tunadhamini mashindano haya tukiamini kuwa vijana wenye vipaji wanaoshiriki wataweza kujitangaza na kujulikana ambapo katika siku za usoni ni rahisi kujiajiri kupitia katika sanaa”Anasema Nkurlu.

Alisema jinsi siku zinavyoenda ndiyo jinsi anavyowaona vijana wanaoshiriki katika shindano hilo wamekuwa makini kwa kile wanachokifanya kwani wametambua kuwa michezo ni ajira na wanaitumia fursa hii waliyoipata ipasavyo ili waweze kujikomboa kiuchumi “Suala la ajira kwa vijana sio lazima kufanya kazi viwandani au maofisini tu bali kuna njia nyingi za kujiajiri na kujipatia kipato mojawapo ikiwa ni kupitia michezo,muziki na sanaa nyingine na Vodacom siku zote tupo mstari wa mbele kuinua vipaji vya vijana na kuweza kujikwamua kiuchumi”Alisisitiza Nkurlu.
Kundi la W.T la Temeke la jijini Dar es Salaam,wakikonga nyoyo za mashabiki wakati wa robo fainali ya Shindano la Dance% lilifanyika kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay.Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Kikundi cha T.O.P cha Temeke jijini Dar es Salaam,wakiburudisha vilivyo wakati wa robo fainali ya Shindano la Dance% lililofanyika kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay.Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.Mshindi ataondoka na kitita cha shilingi Milion 5.


MH. MWIGULU NCHEMBA ASITISHA SAFARI YAKE KWA MUDA ILI KUOKOA MAJERUHI KATIKA AJALI YA GARI

$
0
0
Naibu Waziri wa Fedha,Mh.Mwigulu Nchemba akiangalia sehemu aliyokuwa amebanwa Kondakta wa Gari hilo (pichani) lililopata ajali jana katika barabara kuu ya Dar - Iringa kutokana na kugonga Ukuta pembezoni mwa Barabara hiyo.
Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Mwigulu Nchemba akizungumza na Kondakta wa  lori hilo lililopata ajali mara baada ya Kumnasua kwenye roli hilo.Kijana anaonekana kuugulia maumivu makali kwenye Mkono.
Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Mwigulu Nchemba akitoka huduma ya Kwanza kwa Majeruhi wa ajali hiyo.Huyu ni Dreva akijaribu kuwasha Gari hilo.
Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Mwigulu Nchemba akiendelea kutoa huduma ya kwanza kwa Majeruhi kabla  ya kumkimbiza kwenda hospitali ya Wilaya ya Mikumi.Picha na Festo Sanga.

KAMATI YA KUWAHOJI WAOMBA HIFADHI (NEC) YAANZA KAZI KAMBI YA WAKIMBIZI NYARUGUSU, KIGOMA

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Kuhoji Waomba Hifadhi (NEC), Faraja Nchimbi (watatu kushoto), Katibu wa Kamati hiyo, Philo Nombo (watatu kulia) ambaye anamwakilisha Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi nchini, wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati hiyo baada ya kuwahoji waomba hifadhi katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, iliyopo Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma. Waombaji hao wanatoka nchi mbalimbali ambapo wengi wao wanatoka nchini Kongo. Zaidi ya waomba hifadhi 300 wanaendelea kuhojiwa na Kamati hiyo ambayo inaongozwa na Taasisi nane za Serikali ambazo ni Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (DPP), Idara ya Wakimbizi, Ofisi ya Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Kiongozi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ofisi ya Inspekta Jererali wa Polisi, Kamishna Mkuu wa Uhamiaji na Shirika la Kimataifa ya Kuhudumia Wakimbizi ambao ni waangalizi wa tukio hilo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Kuhoji Waomba Hifadhi (NEC), Faraja Nchimbi (katikati-meza kuu) akiwa na wajumbe wa Kamati hiyo wakati walipokuwa wanawahoji waomba hifadhi (hawapo pichani) katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, iliyopo Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma. Waombaji hao wanatoka nchi mbalimbali ambapo wengi wao ni Wakongo. Zaidi ya waomba hifadhi 300 wanahojiwa na Kamati hiyo ambayo inaongozwa na Taasisi nane za Serikali ambazo ni Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (DPP), Idara ya Wakimbizi, Ofisi ya Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Kiongozi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ofisi ya Inspekta Jererali wa Polisi, Kamishna Mkuu wa Uhamiaji na Shirika la Kimataifa ya Kuhudumia Wakimbizi ambao ni waangalizi wa tukio hilo.

SUZA Management Team refreshes with leadership skills

$
0
0
The State University of Zanzibar (SUZA) top executives are being enlivened with a four days Leadership Development and Performance Management Training Programme. This programme which is facilitated by Ms. Glynis Rankin, a founding Director and Chief Executive Officer of Creative Metier, UK is taking part at Zanzibar Beach Resort from Saturday 23rd Ms. Jeanette Logney.

Opening the training programme, Dr. Idrissa Muslim Hija, the Unguja South Regional Commissioner clued-up that in his memory within a short period, this is the third time SUZA has been organizing leadership training for its personnel hence places itself among very few institutions offering training opportunities to their human resources.

“In most cases the institutions which disregard training opportunities to their workforce use to point out fund inadequacy being the obstacle of not performing this important undertaking for organizations’ prosperity though in reality this reason is immaterial since some trainings do not cost much”, Dr. Hija cautioned.

He advised that the offered skills should be effectively utilized to spearhead the expected results in the university and the tendency of not employing the available skills in training which is common among many institutions should be avoided.

Dr. Hija urged SUZA community to be creative in order to correspond with the fundamental objective of the government of Zanzibar of establishing the State University of Zanzibar which is to bring about positive changes to Zanzibar society. He added that due to lack of consciousness many researches which are supposed to be conducted by natives are carried out by foreigners and insisted that it is a high time now to expand awareness in doing researches and overlie foreign researchers who have taken over most of the researches which can benefit our situation.

Meanwhile, when introducing the State University of Zanzibar to training programme facilitators, Prof. Idris Rai, the Vice Chancellor informed that the issue of distance nowadays is not a measure of time any more as we are living in a village due to high advancement of technology and we therefore need to be critical thinkers in our ambition to build a knowledge-based society.

Prof. Rai elaborated the vision, mission, slogan, executing principles (core values), priority areas and strategic objectives of the university. He enlightened that this training is aimed at accelerating the speed of implementing SUZA targeted objectives in order not to be left behind.

Creative Metier is a UK based institution which delivers innovative Leadership Development Programmes within institutions, across networks and multi-country institutions to bring about a step change in the development of senior leadership. August, 2014 and will finish on 26th August, 2014. Ms. Rankin is assisted by

Wawili wachomwa moto kwa tuhuma za uwizi huko Tabata jijini Dar

$
0
0
Vijana wawili wamechomwa moto katika eneo la Tabata Liwiti wakituhumiwa kuiba pochi ya mwanamke katika eneo hilo,Walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa lilitokea asubuhi ya jana (Jumamosi) ambapo walikuwa watatu wakafukuzwa na watu mbalimbali.

Alisema kuwa walipokamatwa walipigwa na kisha kuchomwa moto.

"Matukio haya yamekuwa yakitokea mara kwa mara hapa Tabata na wezi wanaoiba kwa kutumia pikipiki wamekuwa ni kero kubwa sasa na kila wakikamatwa na kupelekwa vituoni wanaachiwa na Polisi ila kwa sasa wananchi wameamua kutumia sheria mkononi."
Askari kanzu wa Jeshi la Polisi wakipakia kwenye gari mabaki ya miili ya vijana wawili waliotuhumiwa kuwa ni wahalifu wa uwizi waliochomomwa moto jana maeneo ya Tabata Liwiti,jijini Dar es salaam.
Sehemu ya Wananchi wakazi wa Tabata Liwiti pamoja na Askari Kanzu wa Jeshi la Polisi wakiangalia mabaki ya miili ya vijana wawili waliosadikiwa kuwa ni wahalifu wa uwizi waliochomomwa moto jioni maeneo ya Tabata Liwiti,jijini Dar es salaam.
Hii ndio pikipiki waliokuwa wakiitumia wahalifu hao.
Picha na Evance Ng'ingo wa habari5blog

WAANDISHI WANAWAKE PWANI WAANZISHA CHAMA CHAO

$
0
0
Na John Gagarini, Kibaha

WANAWAKE nchini wametakiwa kutokubali kufumbia macho vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kuhofia kutengwa na familia zao badala yake wawe watoa taarifa ili kuwadhibiti watu wanaoendeleza vitendo hivyo ambavyo ni kinyume cha sheria na uvunjaji wa haki za binadamu.

Tabia ya kuficha ukatili wa kijinsia imesababisha wahusika kujikuta wakiathirika kutokana na vitendo hivyo ambavyo vimeshamiri kutokana na kuendelea kwa usiri ndani ya familia.

Hayo yalisema jana mjini Kibaha na mkurugenzi wa benki ya Wanawake Tanzania Magreth Chacha, wakati wa uzinduzi wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Mkoa wa Pwani (PWMO).

Chacha alisema kuwa baadhi ya wanawake wamekuwa wakificha vitendo hivyo vya kikatili ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya wanaume wasiokuwa na huruma.

“Vitendo vya ukatili wa kijinsi vimekuwa vikifanywa ndani ya familia huku wanawake amabao ndiyo wahanga wa matukio hayo wamekuwa wakikaa kimya kuhofia kutengwa na familia zao jambo ambalo limesababisha vitendo hivi kuendelea,” alisema Chacha.

Alisema kuwa baadhi ya vitendo hivyo vimekuwa vikifanywa na watu wa karibu wa familia wakiwemo wanandoa na ndugu hali ambayo inasababisha taarifa hizo kufichwa huku walengwa wakiendelea kuathiriwa na vitendo hivyo viovu na vya ukatili.

“Baadhi ya vitendo hivyo ni pamoja na wanawake kupigwa, kutumikishwa kingono, kubakwa, watoto kubakwa, kulawitiwa, kufanyishwa kazi licha ya kuwa na umri mdogo na vitendo vingine vinavyokwenda kinyume cha sheria na haki za msingi za binadamu,” alisema Chacha.

Kwa upande wake mwenyekiti wa (PWMO) Mwamvua Mwinyi alisema kuwa lengo la kuanzishwa chama hicho mbali ya kutetea haki za waandishi wanawake pia ni kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ndani ya mkoa huo na Tanzania kwa ujumla.

“Vitendo vya ukatili wa kijinsia vimekuwa vikiongezeka siku hadi siku kutokana na baadhi ya wanajamii hususani wanawake kutokuwa katika kutoa taarifa za vitendo hivyo hali inayofanya kuongezeka kwa ukatili wa kijinsia,” alisema Mwinyi.

Aliiomba jamii kwa kushirikiana na vyombo vya sheria kwa kutoaa taarifa juu ya watu wanaofanya vitendo hivyo vya ukatili hususani maeneo ya pembezoni mwa miji, chama hicho kilianzishwa mwaka jana na kina jumla ya wanachama 15.

Nakumatt wafungua Supermarket nyingine Arusha

$
0
0
Mwonekano wa Supermaket mpya ya mtandao wa maduka ya Nakumatt Holdings Ltd jijini Arusha baada ya kuzinduliwa jana kwenye eneo la TFA Arusha.
Mwonekano wa Supermaket mpya ya mtandao wa maduka ya Nakumatt Holdings Ltd jijini Arusha baada ya kuzinduliwa jana kwenye eneo la TFA Arusha.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)Dk Richard Sezibera(kushoto) akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Nakumatt Holdings Ltd,Atul Shah akiangalia bidhaa mbalimbali kwenye Supermarket mpya ilifunguliwa eneo la TFA jijini Arusha.
Wafanyakazi wa duka jipya la Nakumatt jijini Arusha waki 'pose' kwa picha ndani Supermarket hiyo ambayo ni inaungezea hadhi mji wa Arusha ambao ni kitalii na taasisi za kimataifa.

MH. PINDA AONGOZA HARAMBEE YA MKAPA FELLOWS JIJINI MWANZA

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika harambee ya kuchangia Mradi wa Mkapa Fellows kwenye hoteli ya JB Belmont jijini Mwanza August 23, 2014. Zaidi ya sh. Bilioni 1.3 zilichangwa.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea mchango wa shilingi milioni 15 kutoka kwa Mfanyabiashara wa Mwanza na Dar es salaam Jumanne Kishimba katika harambee ya kuchangia Mradi wa Mkapa Fellows iliyofanyiak kwenye hoteli ya JB Belmont jijini Mwanza August 23,2014. Zaidi ya Shilingi Bilioni 1.3 zilichangwa.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa akimshukuru Mfanyabiashara wa Dar es salaam na Mwanza, Jumanne Kishimba ambaye alichangia Shilingi milioni 15 katika harambee ya kuchangia mradi wa Mkapa Felllows kwenye hotel ya JB Belmont jijini Mwanza August 23, 2014. Zaidi ya Shilingi Bilioni 1.5 zilichangwa. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mkapa HIV/AIDS, Balozi Charles Sanga.
Waziri Mmuu, Mizengo Pinda akipokea kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanal Fabian Massawe Maarufu kwa jina la Mulokozi mchango wa zaidi ya shilingi milioni 100 zilizochangwa na Wanakagera katika harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Mradi wa Mkapa Fellows, kwenye hoteli ya JB Belmont jijini Mwanza August 23, 2014. Zaidi ya Shilingi Bilioni1.3 zilichangwa katika harambee hiyo.
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akipokea mchango wa zaidi ya shilingi milioni 100 kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Shinya, Ali Rufunga zilizotolewa na wanashinyanga kuchangia mradi wa Mkapa Fellows katika harambee iliyoongozwa na Waziri Mkuu kwenye hoteli ya JB Belmont jijini Mwanza August 23, 2014. Zaidi ya shilingi Bilioni 1.3 zilichangwa.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarest Ndikilo ambaye aliwasilisha mchango wa zaidi ya Shilingi milioni 100 zilizochangwa na Wanamwanza katika harambee ya kuchangia Mradi wa Mkapa Fellows iliyofanyika kwenye hoteli ya JB Belmont jijini Mwanza, August 23, 2014. Zaidi ya Shilingi Bilioni 1.3 zilichangwa katika harambee hiyo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa baada ya harambee ya kuchangia Mradi wa Mkapa Fellows iliyofanyika kwenye hoteli ya JB Belmont jijini Mwanza, August 23, 2014. Zaidi ya Shilingi Bilioni 1.3 zilichangwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

ZOEZI LA UHAKIKI WAKIMBIZI KAMBI YA NYARUGUSU LAFIKIA UKIKONGONI

$
0
0
Mratibu wa Idara ya Wakimbizi Kanda ya Kigoma, Tony Laiser akiwaongoza Wakimbizi wazee kutoka nchini Kongo leo kufanyiwa uhakiki wa taarifa zao ili watambulike rasmi kuwa ni wakimbizi katika Kambi ya Nyarugusu, iliyopo Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma. Zaidi ya familia za Wakimbizi 14,000 ikiwa ni sawa na Wakimbizi 68,000 wamefanyiwa uhakiki huo kambini hapo.
Mratibu wa Idara ya Wakimbizi Kanda ya Kigoma, Tony Laiser (kulia) akimuhoji Mkimbizi kutoka nchini Burundi, Bibi Karumere (katikati) wakati wa kufanyiwa uhakiki wa taarifa zake ili aweze kutambulika rasmi kuwa ni Mkimbizi katika Kambi ya Nyarugusu, iliyopo Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma. Zaidi ya familia ya Wakimbizi 14,000 sawa na jumla ya Wakimbizi 68,000 wamefanyiwa uhakiki huo kambini hapo.
Mratibu wa Idara ya Wakimbizi Kanda ya Kigoma, Tony Laiser (kulia) akimkabidhi Mkimbizi kutoka nchini Kongo katika Kambi ya Nyarugusu msaada wa taa inayotumia mionzi ya jua. Taa hiyo pia ina sehemu ya kuchajia simu za mikononi. Maelfu ya wakimbizi katika Kambi hiyo walipewa msaada huo leo ulitolewa na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) kupitia Shirika linalotoa huduma za Kijami na Unyanyasaji wa Kijinsia (IRC) ikiwa ni kawaida yao kutoa misaada mbalimbali ya kuwasaidia wakimbizi hao waliopo katika kambi hiyo, Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.
Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi Nyarugusu, Sospeter Boyo (wapili kushoto) akiwahoji mafundi ujenzi ambao ni wakimbizi kutoka nchini Kongo, wakati wakilijenga darasa la Shule ya Sekondari Fraternite iliyopo katika Kambi ya Nyarugusu, wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma. Shule hiyo inafundisha kwa kutumia Mitahala ya Elimu ya nchini Kongo.
Mama Mkimbizi kutoka nchini Kongo akiwa na mwanae, pamoja na wakimbizi wengine wakisubiria kwenda kufanyiwa uhakiki wa taarifa zao leo ili waweze kutambulika rasmi kuwa ni wakimbizi katika Kambi ya Nyarugusu, iliyopo Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma. Zaidi ya familia ya Wakimbizi 14,000 sawa na jumla ya Wakimbizi 68,000 wamefanyiwa uhakiki huo kambini hapo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Rais Kikwete atunuku Kamisheni Kwa maofisa wapya wa Jeshi

$
0
0
Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi na kumpongeza luteni Usu Mohamed Ramadhani Mgalawe baada ya kuibuka mwanafunzi bora wakati wa hafla ya kuwatunuku kamisheni maafisa wapya 179 wa jeshi la Wananchi waliohitimu vyema mafunzo yao katika chuo cha Jeshi Monduli Mkoani Arusha jana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitunuku kamisheni kwa maafisa wapya 179 wa jeshi waliohitimu vyema mafunzo yao ya muda mrefu katika chuo cha jeshi Monduli Mkoani Arusha jana.
Maofisa wapya wa Jeshi wakila kiapo mbele ya Amiri jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa hafla ya kuwatunuku kamisheni iliyofanyika katika chuo cha jeshi kilichopo Monduli Mkoani Arusha jana.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wapya wa jeshi baada ya kuwatunuku kamisheni katika sherehe zilizofanyika katika chuo cha jeshi Monduli mkoani Arusha jana.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Luteni Usu Mohamed Ramadhani Mgalawe aliyeibuka mwanafunzi bora(Best Oficer Cadet Traineer Overall) wakati wa mafunzo ya muda mrefu ambapo maafisa 179 wa jeshi walihitimu vyema na kutunukiwa kamisheni katika chuocha jeshi Monduli jana.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mwanafunzi Bora katika kozi ya muda mrefu ya jeshi Luteni Usu Mohamed Ramadhani Mgalawe(watatu kushoto) pamoja na wazazi wake muda mfupi baada ya Rais Kuwatunuku kamisheni maofisa 179 wa jeshi katika chuo cha Monduli Mkoani Arusha jana.
Mtoto mdogo akimsalimia Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kumalizika kwa sherehe za kuwatunuku kamisheni Maofisa 179 wa jeshi katika chuo cha jeshi Monduli Mkoani Arusha jana. (picha na Freddy Maro)

MAREHEMU LUCIA KIBUSI AAGWA BOSTON, MASSACHUSETTS NCHINI MAREKANI

$
0
0
Marehemu Mama Lucia Kibusi enzi za Uhai wake.
Watoto wa marehemu Martin na Steven Kibusi kulia wakiwa kwenye chakula cha pamoja baada ya ibada ya kumbukumbu ya kumuaga mama yao kumalizika kushoto ni marafiki wa karibu na watoto wa marehemu wakiwafariji marafiki zao. Pia familia ya marehemu walitoa shukurani za dhati kwa wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine katika msiba huu wa mpendwa mama yao na kuwezesha kukusanya $19,000 ili kuwezesha kusafirisha mwili wa marehemu nyumbani Tanzania " hatuna cha kuwalipa kitakacholingana na hicho kikubwa mlichoifanyia familia hii ya Kibusi, tunawaoombea kwa Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema awazidishie mara dufu"
Dua la kuombea chakula
Mkuu wa Wilaya ya Springfield, Alhaji Isaac Kibodya akiwa na shemeji yake na NY Ebra aliyewakilisha timu ya Vijimambo kwenye msiba huo.
Watanzania wa Massachusetts wakiwa wamejumuika pamoja kwenye chakula cha pamoja  baada ya Ibada ya kumbukumbu kumalizika
Kwa picha zaidi bofya HAPA

TCRA YAKITOZA FAINI KITUO CHA TELEVISHENI CHA CLOUDS TV NA RADIO CLOUDS FM KWA KUKIUKA MAUDHUI YA UTANGAZAJI

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Margaret Munyagi (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Agosti 22, 2014 jijini Dar es Salaam, wakati akisoma maamuzi yaliyofikiwa na Mamlaka hiyo kuhusu shauri la ukiukaji wa kanuni za utangazaji namba 5/2014 dhidi ya Kituo cha Televisheni cha Clouds na Kituo cha Clouds Intertainment FM Radio cha Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati hiyo, Bgoya Walter.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Margaret Munyagi (wa pili kulia), akiwa na wajumbe wenzake wakati wa mkutanmo huo. Kutoka kushoto ni Abdul Ngarawa, Joseph Mapunda, Walter Bgoya na Mkurugenzi wa Utangazaji (TCRA), Habby Gunze.
Wajumbe wa kamati hiyo, Abdul Ngarawa, Joseph Mapunda wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Margaret Munyagi (kushoto), akitia saini maamuzi hayo kabla ya kupewa walengwa. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Utangazaji TCRA, Habby Gunze.
Wawakilishi kutoka Clouds Inertainment FM Radio wakiwa kwenye mkuatno huo.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.Picha na Mdau Dotto Mwaibale.

‘MADINI HOUSE’ KUJENGWA ARUSHA, Kuwa na huduma za kibenki, Helkopita kutua moja kwa moja kituoni

$
0
0
Na Asteria Muhozya, Songea
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Paul Masanja ameeleza kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini itajenga kituo maalum cha kuuza na kununua madini ya vito kutokana na nchi kuwa na hazina kubwa ya madini jambo ambalo pia litachangia katika kuyaongezea thamani madini hayo. 
 Masanja ameyasema hayo  mjini Songea wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Nishati na Madini Eliakim Maswi kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na wizara ikiwemo kuonana na Makamishna Wasaidizi wa Kanda, Maafisa Madini Wakaazi, Watumishi wa Shirika la Umeme Tanzania, kuangalia shughuli za wachimbaji wadogo wakiwemo wafanyabiashara wa madini na wawekezaji katika sekta ya madini. 
 Kamishna aliongeza kuwa, kituo hicho kitakuwa na huduma zote muhimu zikiwemo za kibenki ambazo zitawawezesha wachimbaji na wafanyabiashara kutokutafuta huduma muhimu zinazoendana na shughuli hizo nje ya kituo hicho. 
“Shughuli zote za uuuzaji na ununuzi madini ya vito na usonara zitafanywa katika kituo hicho. 
Kutakuwa pia na helkopita itakayotua moja kwa moja katika jengo hilo jambo ambalo litawezesha uwepo wa usalama katika biashara nzima ya kuuza na kununua madini,” alisisitiza Masanja. 
 Aidha, aliongeza kuwa, ili kuiwezesha sekta hiyo kupaa kwa kasi na kuchangia katika ukuaji wa uchumi, wizara imeamua kuanza kwa kuboresha ofisi za kanda za madini ikiwa ni pamoja na kununua maeneo maalum kwa ajili ya kujenga ofisi hizo ili kuboresha utendaji wa sekta ya madini nchini na kuwa na ofisi za uhakika. 
 “Tunataka kupitia sekta ya madini kuiwezesha serikali kuongeza mapato yake na kutoka hapa tulipo kiuchumi. Jambo hilo linawezekana ndio sababu tunaanza na kuboresha sehemu za kazi ili kuwawezesha watumishi kufanya kazi katika mazingira mazuri zaidi na kuongeza uwajibikaji,”aliongeza Masanja. 
Katika hatua nyingine, Kamishna Masanja amewataka Makamishna Wasaidizi wa Kanda na Makamishna Wakaazi walioteuliwa hivi karibuni kutimiza wajibu wao vizuri na kufikia lengo la makusanyo ambayo wizara imewapangia na kwa wale wasiotekeleza agizo hilo la makusanyo ndani ya kipindi cha miezi mitatu wataondolewa katika nafasi zao. 
“Tumeamua kupaa kupitia sekta hii, asiyeweza kutekeleza jambo hili kama tulivyokubaliana, tutamwondoa na kuwapa wengine wenye uwezo wa kufanya hivyo. Tunataka kufanya kazi kwa kasi na kisasa zaidi,” alisisitiza Masanja. 
Wakati huo huo, aliwata watumishi wote walioko katika ofisi za Kanda kuwa waadilifu, wawajibikaji, wawazi na wabunifu ili kuweza kutekeleza majukumu yao kikamilifu ikiwemo kufuata sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma. 
Vilevile, aliongeza kuwa, wizara imejipanga kuanza kutumia mfumo wa kieletroniki kuanzia mwezi Septemba kwa ajili ya waombaji wa leseni jambo ambalo litasaidia kurahisisha zoezi la uombaji wa leseni na kuondoa manungu’niko miongoni mwa waombaji.
Afisa Madini Mkaazi Tunduru Fredrick Mwanjisi (kushoto) akifurahia jambo wakati akimwongoza Katibu Mkuu Nishati na Madini Eliakim Maswi (wa pili kushoto) kutembelea eneo itakapojengwa ofisi ya Madini Tunduru. Wengine katika picha ni ujumbe wa Maafisa walioongozana na Katibu Mkuu na watumishi wa ofisi ya Madini Tunduru.

Jengo ambalo litatumika kama  Makao Makuu ya Ofisi ya Madini Kanda ya Ziwa Nyasa mjini Songea. Jengo hilo limenunuliwa na Wizara na litaanza kutumika mara baada ya ukarabati. Wengine katikati ni Kaimu MKurugenzi Idara ya Utawala Wizara ya Nishati na Madini, Caroline Msika na wengine ni maafisa wWizara ya Nishati na Madini na Maafisa wa Madini Kanda waliofuatana na Katibu Mkuu.

Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Paul Masanja, (wa kwanza kushoto) akitafakari jambo mara baada ya kukagua kiwanja kitakapojengwa ofisi ya Madini ya Kamishna Mkaazi wa Madini, Nachingwea. Wa pili kushoto ni  Katibu Mkuu  Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, wa kwanza, wengine ni  Afisa Madini Mkaazi Nachingwea, Mhandisi Mayigi Makolobela (wa pili kulia) na wa kwanza kulia ni Mjiolojia kutoka ofisi ya Madini Mtwara.

KAMPUNI YA MSAMA PROMOTION NA JESHI LA POLISI WAKATAMA KAZI FEKI ZA WASANII

$
0
0
1
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari kwenye kituo cha polisi cha Urafiki wakati akitangaza kukatatwa kwa watuhumiwa 17 wanaorudufu kazi za wasanii kinyume na utaratibu yaani kazi feki katika jiji la Dar es salaam na baadhi ya mikoa ambapo kazi feki za wasanii zilizokamatwa thamani yake ni shilingi milioni 12, Kulia ni ASP Denis Moyo mkuu wa upelelezi wa kituo hicho ambaye amesema amethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa 17 ambao wanasubiri kupelekwa mahakamani.
2
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama na KAMASP Denis Moyo mkuu wa upelelezi wa kituo hicho wakionyesha CD feki zilizokamatwa jijini Dar es salaam
4
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama na ASP Denis Moyo mkuu wa upelelezi wa kituo hicho wakionyesha CD feki zilizokamatwa jijini Dar es salaam
5
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akifafanua zaidi kuhusu wizi huo wa kazi a wasanii unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara na kuwanyonya wasanii.
6
Kituo cha polisi cha Urafiki

Benki ya Exim yaijengea maliwato Shule ya Msingi Kilakala

$
0
0

 Mkuu wa matawi (Cluster Head) wa Benki ya Exim Tanzania, Bi Agnes Kaganda (wapili kushoto) na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kilakala, Bw. Abdul Kuratasa kwapamoja wakifungua jiwe la msingi kuonyesha makabidhiano rasmi ya maliwato iliyojengwa na benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia ni Kaka Mkuu wa Shule Seif Ahmed (wa kwanza kushoto), Dada Mkuu wa shule Naomi Shakila (wa kwanza kulia) na mlezi wa shule hiyo Dkt. Ellen Otaru (wa pili kulia). Na mpiga piga wetu.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kilakala, Bw. Abdul Kuratasa akikata utepe kuashiria ufunguzi wa maliwato iliyokabidhiwa na Benki ya Exim Tanzania katika hafla iliyofanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Na mpiga picha wetu.  


MAKANISA SINGIDA YAONYA MATUSI NA UBAGUZI BUNGENI

$
0
0
DSC00479
Askofu wa kanisa la Evanglist Assembels of God Tanzania (E.A.G.T) Singida mjini, John Mafwimbo akizungumza kwenye mkutano wa Injili uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Ukombozi mjini Singida.Pamoja na mambo mengi, askofu Mafwimbo amewasihi wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, kufanya mambo waliyotumwa na Watanzania na si vinginevyo.

Na Nathaniel Limu, Singida
Makanisa ya Kipentekoste mkoani Singida, yameungana na Watanzania wengine kuwaomba wajumbe wa Bunge Maalum la kuandaa Katiba mpya,kujiepusha na mambo/vitendo ambavyo hawakutumwa na wananchi na badala yake washikamane na wavumiliane ili waweze kufanikisha kupatikana kwa katiba itakayoendeleza amani na utulivu uliopo nchini.

Makanisa hayo ambayo ni pamoja na Free Pentekoste Tanzania na Evangelist Assembles of God Tanzania (E.A.G.T.),yamedai kwamba matusi, dharau, ugomvi na kejeli za aina mbalimbali hazitachangia kupatikana kwa Katiba inayotarajiwa na Watanzania.
Wamedai vitendo hivyo, vitachangia pamoja na mambo mengine kubomoa umoja na undugu uliojengeka kwa miongo mingi na vitakaribisha vitendo viouvu kama vinavyofanywa na vikundi vya Boko haramu na Alshabab.

Akizungumza kwenye mkutano mkubwa wa injili uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Ukombozi mjini Singida, Askofu wa E.A.G.T, John Mafwimbo alisema ni wakati sasa kwa waumini wa madhehebu mbalimbali ya dini kufunga kwa ajili ya kufanya maombi kuliombea Bunge Maalum la Katiba,liweze kutekeleza yale yote waliyotumwa na Watanzania.
DSC00490
Mchungaji wa kanisa la Free Pentekoste Tanzania Singida mjini, Boniface Ntandu, akiwahubiria waumini wa madhehebu ya dini mbalimbali waliohudhuria mkutano wa injili uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Ukombozi.

"Tuwaombee bila kuchoka wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba,waweze kututengenezea/kutuboreshea vizuri Katiba na wala wasituchanganye,ili sisi huku waumini wa madhehebu ya dini na Watanzania wengine wasiokuwa na dini tuje tufanye uamuzi sahihi wakati wa kuipigia kura Katiba hiyo",alifafanua.

Akifafanua zaidi, Mafwimbo, alisema kazi ya wajumbe nikuwajengea Watanzania mazingira mazuri ili waje kupigia kura Katiba itakayokidhi mahitaji yao ya zaidi ya miaka 50 ijayo.
Kwa hali hiyo, Askofu Mafwimbo amewashawishi wajumbe hao kuimarisha utamaduni wa kuvumiliana, kupendana na kumaliza tofauti zao wao kwa wao.

"Niwakumbushe tu wajumbe wetu, kwamba Watanzania ni waumini wazuri wa amani na utulivu. Kitendo hicho kimeendelea kuchangia nchi yetu kupaa kimaendeleo na wakati huo huo, sisi waumini tunaendelea kuabudu kwa uhuru mpana bila usumbufu wa aina yo yote",alisema na kuongeza kwa kusema; "Endapo hatutapata katiba stahiki,tutakuwa tunakaribisha vurugu kama zile zinazofanywa na makundi ya boko haramu".
DSC00471
Moja ya kwaya zilizokuwa zikihubiri kwa njia ya nyimbo kwenye mkutano wa injili ulioandaliwa na mwimbaji wa nyimbi za injili mkoa wa Singida, Elineema Babu.
DSC00478
Baadhi ya waumini wa madhehebu mbalimbali ya dini,waliohudhuria mkutano wa injili unaoendelea kwenye viwanja vya shule ya msingi Ukombozi mjini Singida.(Picha zote na Nathaniel Limu).

WAKONGWE WA REAL MADRID WAKWEA MLIMA KILIMANJARO

$
0
0
Wachezaji wakongwe wa Klabu ya Real Madrid wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa TANAPA mara baada ya kumaliza zoezi la matembezi mafupi ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
 Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dk. Fenela Mukangara akitoa cheti cha ushiriki kwa mchezaji Ruben De La Red wa Klabu ya Real Madrid mara baada ya kumaliza zoezi la matembezi mafupi ya kupanda Mlima Kilimanjaro. 
Wakongwe wa Real Madrid wakiwa katikati ya msitu wa Mlima Kilimanjaro.

 Eneo la Maporomoko ya Maji ambapo wachezaji wakongwe wa Real Madrid walifanikiwa kufika Mlimani Kilimanjaro. 
 Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete (mwenye fulana nyeupe na miwani) akiongoza msafara wa wakongwe wa Real Madrid kukwea Mlima Kilimanjaro.




MWIGULU AMSIMIKA SALIM ASAS KUWA KAMANDA WA VIJANA RINGA

$
0
0

MFANYABIASHARA maarufu mkoani Iringa Salim Abri Asas akisimikwa kuwa Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa katika kipindi cha miaka mingine mitano  na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara Mwigulu Nchemba katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Mwembetogwa, mjini Iringa.
Mwigulu Nchemba akizingumza na umati wa watu katika viwanja vya mwembetogwa mwishoni mwa wiki mjini Iringa
MFANYABIASHARA maarufu mkoani Iringa Salim Abri Asas akizungumza na Wananchi mwishoni mwa wiki mara baada ya kusimikwa kuwa Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa katika kipindi cha miaka mingine mitano  na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara Mwigulu Nchemba katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Mwembetogwa, mjini Iringa.
 Salim Abri Asas akiwa na Wazee wa Kimila kabla ya kusimikwa kuwa Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa katika kipindi cha miaka mingine mitano.
 Shughuli za kusimikwa zikiendelea huku wanahabari wakiendelea kurekodi tukio hilo.

Na Denis Mlowe,Iringa

MFANYABIASHARA maarufu mkoani Iringa Salim Abri Asas mwishoni mwa wiki amesimikwa kuwa Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa katika kipindi cha miaka mingine mitano  na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara Mwigulu Nchemba katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Mwembetogwa, mjini Iringa.

 Akimuapisha Asas kuwa Kamanda wa UVCCM Mkoa wa Iringa, Nchemba ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM alisema analitumikia taifa hili akijua sehemu kubwa ya wananchi wake ni masikini na lengo kubwa ni kuwaondoa katika lindi la umaskini.


Nchemba alisema nchi inaliwa na moja ya eneo linalowaweka katika kazi kubwa ya mapambano ni fedha zinazotolewa kwenye halmashauri kwa ajili ya maendeleo ambazo hazitumiki ipasavyo na watendaji kwa kuzitumia katika miradi isiyo endelevu na kusababishia nchi kutokuwa na maendeleo.

“Kuna mambo mengi yanatokea katika halmashauri zetu kwasababu ya kukosa usimamizi unaosababisha watu wetu wakose hali ya kupata huduma zinazotakiwa kutekelezwa katika miradi ya maendeleo hivyo nitahakikisha kuwabana na kuwafuatilia kwa kila halmashauri kuleta mchanganuo wa fedha jinsi zilivyotumika na kuhakikisha mradi umekamilika na sio kusema kiasi Fulani kimetumika.”  Alisema Nchemba.
 
Aliongeza kuwa serikali inaendelea na mikakati ya kuwasaka, kuwakamata na hatimaye kuwafikisha katika vyombo vya dola watumishi wa umma wanaokula kodi za wananchi kwa mikono miwili bila kunawa.

Mwigulu alisema mambo mazuri yanakuja na serikali itaendelea kutengeneza sera  zinazojali watanzania ili keki ya taifa iliwe na watanzania wote na kudhibiti matumizi ya ovyo na fedha tutakazokuwa tunatoa hatutaruhusu zitumike kwa kazi tofauti na ile iliyokusudiwa.

Akimpongeza Asas kwa kuwa kamanda wa UVCCM, Alisema UVCCM wakitimiza wajibu wao ipasavyo watasaidia kupunguza maadui wakubwa wawili wa CCM ambao wameendelea kuwa na athari kubwa wakati wa chaguzi za serikali.

Aliwataja maadui hao kuwa ni pamoja na kujiingiza kwenye makundi ya wagombea na hila zinazosababisha baadhi ya wana CCM wasitendewe haki stahiki kwenye vikao muhimu vya chama.

Kwa upande wake Kamanda Salim Asas alisema baada ya kuapishwa kwa kipindi kingine lengo ni kuwainua vijana kiuchumi na kutaka ushirikiano katika kuleta maendeleo ya wananchi wa mkoa wa Iringa bila kujali itikadi ya vyama na dini. 

Madini Migodini yapo Salama- Maswi

$
0
0
Na Asteria Muhozya, Mbinga

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi amewataka watanzania kuondoa dhana kuwa madini yanayochimbwa katika migodi mbalimbali nchini yanaibwa na wawekezaji wakubwa na kusisitiza kuwa, Wizara kupitia Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), wapo katika migodi yote nchini kuhakikisha kwamba madini hayo hayatoroshwi .

Maswi ameyasema hayo alipotembelea Mgodi wa kuchimba Makaa ya Mawe wa kampuni ya Tancoal eneo la Ngaka wilayani Mbinga inayomilikiwa kwa ubia kati ya Kampuni ya Australia na Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na kuongeza kuwa, TMAA wapo katika kila mgodi kujua kiasi cha madini kinachochimbwa, kinachouzwa na kwa ajili ya kuhakiki vyeti vya mauzo ya madini hayo kuhakikisha kuwa vinakwenda sambamba na kiasi cha mrahaba kinachotolewa na wawekezaji.

Kwa upande wake Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Paul Masanja alisisitiza hoja ya Katibu Mkuu Maswi na kuongeza kuwa, Wizara kupitia maafisa wa TMAA wamekuwa wakifanya ukaguzi kuhakikisha kwamba serikali inapata mrahaba stahili kupitia madini yanayouzwa na kutoa mfano kwa madini ya Makaa ya Mawe ya Ngaka kwamba serikali inapata asilimia 100 ya mrahaba.

“Nawapongeza sana TanCoal ni wasikivu, maafisa wa TMAA huwa wanafanya ukaguzi kila baada ya miezi mitatu kujua kiasi kinachozalishwa na kinachouzwa hivyo, tunakwenda nao vizuri,” alisisitiza Masanja.

Naye Mkurugenzi wa Tancoal Tan Brereton ameeleza kuwa, mgodi wa wa Ngaka ni mradi mkubwa kwa Tanzania na kuongeza kuwa, uwepo wa mgodi wa makaa ya mawe wa Tancoal ni mafanikio na maendeleo makubwa kwa Tanzania kutokana na kuwezesha ajira kwa wataalamu mbalimbali nchini ikiwemo serikali kupata kodi na mirahaba kupitia mgodi huo jambo ambalo litawezesha kuboresha huduma za kijamii.

Aidha, amezitaja faida za nyingine za mgodi huo kuwa, uwepo wa Mgodi huo utawezesha Tanzania kuzalisha kiasi kikubwa cha nishati ya umeme kutokana na uwepo wa kiasi kikubwa cha makaa hayo katika mgodi wa Ngaka na kueleza kuwa, makaa ya mawe kutoka katika mgodi huo yana ubora wa kiwango cha juu tofauti na madini yanayochimbwa nchini Afrika Kusini.

“Makaa ya Ngaka yana ubora wa hali ya juu sana tofauti na makaa ya nayochimbwa Afrika Kusini kwasasabu madini haya hayahitaji kusafishwa kabla ya matumizi tofauti na mengine ambayo husafishwa kabla ya kutumiwa ,alisisitiza Tan.

Aidha ameongeza kuwa, kampuni hiyo ina uwezo wa kuzalisha kiasi cha tani 480,000 za makaa ya mawe kwa mwaka na kuongeza kuwa, tayari kampuni hiyo imesaidia huduma mbalimbali za kijamii katika maeneo ya afya,shule ,maji na kuwaendeleza vijana na kutumia zaidi ya shilingi milioni mia sita na kuongeza kuwa, kampuni hiyo imekwisha toa kiasi za bilioni 2 kama kodi na mrahaba kwa serikali.

Kwa mujibu wa Tan, ameeleza kuwa, makaa yanayozalishwa na kampuni hiyo yanatumika katika viwanda vya saruji vya Mbeya Tanga Lake, kampuni ya METL na viwanda vya karatasi viwanda vya nguo.
Mashine ya kusaga makaa yam awe katika viwango mbalimbali kulingana na mahitaji ya wateja ikiendelea na kazi ya kusaga mawe katika Mgodi wa Mkaa ya Mawe wa Ngaka unaomilikiwa kwa ubia na Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na kampuni ya Australia.
Gari la kubeba makaa ya Mawe katika mgodi wa Ngaka likimwaga makaa sehemu maalum kutoka mgodini kabla ya kusagwa katika viwango mbalimbali kulingana na mahitaji y wateja.
Meneja wa Kampuni ya TANCOAL (wanne kulia) Tan Brereton na Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo Emmanuel Constantinides (wa tatu kulia) wakimwonesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi na ujumbe wake namna shughuli za himbaji Makaa ya Mawe zinavyofanyika.
Gari la kubeba kupakia Makaa ya Mawe likiendelea na kazi hiyo katika Mgodi wa Ngaka unaomilikiwa na kampuni TANCOAL.

WABUNGE WA CCM WAUNGURUMA HUKO MTERA MKOANI DODOMA

$
0
0
Sehemu ya Wananchi wa Jimbo la Mtera,wakiwa wamekusanyika kwa wingi kwenye Mkutano wa hadhara uliofanywa na baadhi ya Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa kuuelimisha umma juu ya masuala ya Maendeleo, Utekelezaji wa ilani Chama, Maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za vijiji na mitaa, Bunge la Katiba na Mambo yanayohusu maendeleo ya katika vijiji na wilaya zetu. Pia waliwakumbusha juu ya thamani ya muungano wetu na vipengele muhimu vinavyojadiliwa ndani ya Bunge la Katiba.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh. Ridhiwani Kikwete akihutubia kwenye Mkutano huo
Mbunge wa Jimbo la Nkenge mkoani Kagera , Asumpta Mshana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Iringa jimbo la Mtera jana nyuma ni mbunge wa jimbo la Mtera Mh. Livingstone Lusinde.
Mbunge wa jimbo la Mtera Mh. Livingstone Lusinde akiwahutubia wananchi wa jimbo lake katika kijiji cha Iringa Mvumi mkoani Dodoma.
IMG-20140824-WA0008
Mbumge wa ji,bo la Sikonge Mh. Said Mkumba akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.
Wananchi wakisikiliza kwa makini Mbunge wa Chalnze Ridhiwani Kikwete alipokuwa akiwahutubia
Viewing all 109973 articles
Browse latest View live


Latest Images