Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 53 | 54 | (Page 55) | 56 | 57 | .... | 3285 | newer

  0 0


  0 0

    Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA,Mama Salma Kikwete akipokelewa na Mkuu wa Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule,kwenye Zahanati ya Nyamisati , iliyopo wilaya Rufiji Mkoa wa Pwani akiwa ni  Mgeni rasmi kwenye hafla fupi ya  makabidhiano ya msaada wa vifaa vya tiba na dawa wenye thamani ya shilingi Mil 20 kutoka Vodacom Foundation kwa ajili ya wakazi wa eneo hilo.
   Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA,Mama Salma Kikwete,akiongea na baadhi ya wakazi wa Nyamisati wilaya Rufiji Mkoa wa Pwani wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya msaada wa vifaa vya tiba na dawa wenye thamani ya shilingi Mil 20 katika Zahanati ya Nyamisati, iliyopo wilayani humo vilivyotolewa na Vodacom Foundation hapo jana.
    Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA,Mama Salma Kikwete(katikati) pamoja na Mganga Mkuu wa Zahanati ya Nyamisati, iliyopo wilaya Rufiji Mkoa wa Pwani Bw.Haruna Mhina,wakipokea msaada wa vifaa vya tiba na dawa wenye thamani ya shilingi Mil 20 kutoka kwa Mkuu wa Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule.
   Baadhi ya wakazi wa Nyamisati wilaya Rufiji Mkoa wa Pwani wakimsikiliza Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA,Mama Salma Kikwete,akiongea nao wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya msaada wa vifaa vya tiba na dawa wenye thamani ya shilingi Mil 20 katika Zahanati ya Nyamisati, iliyopo wilayani humo vilivyotolewa na Vodacom Foundation hapo jana.
   Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,mara baada ya makabidhiano ya msaada wa vifaa vya tiba na dawa wenye thamani ya shilingi Mil 20 kutoka Vodacom Foundation kwa ajili ya wakazi wa eneo Nyamisati  iliyopo wilaya Rufiji Mkoa wa Pwani.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa wamebeba mabox yenye vifaa tiba na dawa vyenye thamani ya shilingi Mil 20 kwa ajili ya kutoa msaada katika Zahanati ya Nyamisati, iliyopo wilayani Rufiji vilivyotolewa na Vodacom Foundation hapo juzi.

  0 0


  Are you passionate about young Tanzanians making waves in their respective fields? 
  Ndovu Special Malt is proud to support the nation’s most promising talent through its social media Spotlight campaign
  To find out more about the campaign, head to theNdovu Special Malt Facebook Page, or to chat live today (3PM to 4PM) with Tanzanian success, Evans Bukuku about his journey to success, and the inspiration behind his career to date, follow this link here to join the live chat at 3PM “  0 0
 • 02/25/13--00:26: umbea wa nathana mpangala


 • 0 0
 • 02/25/13--02:51: Article 11


 • 0 0


   Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue (wa tatu kulia) akisikiliza maelezo Kibenki kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania,Sabasaba Moshingi (kulia) wakati wa ziara ya Balozi Sefue kutembelea Matawi ya Benki ya Posta ya Jijini Dar es Salaam leo,ambapo ametembelea Matawi ya Kariakoo,Mkwepu na Makao Makuu ya Benki ya Posta.

  Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akizungumza na Wakurugenzi wa Benki ya Posta Tanzania katika makao makuu ya Benki hiyo yaliopo mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam,mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea matawi ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi wa Uendeshaji na Teknohama wa Benki ya Benki ya Posta Tanzania,Jema Msuya (kushoto) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati alipotembelea Tawi la Mkwepu jijini Dar es Salaam leo.
   Meneja wa Benki ya Posta Tanzania Tawi la Mkwepu jijini Dar es Salaam,Ayub Sapi Mkwawa (kushoto) akisalimia na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue ( wa pili kulia) wakati alipowasili kwenye tawi hilo leo.kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania,Sabasaba Moshingi.


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza  na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu Nchini Tanzania  Mhe. Mallallah  Mubarak Alameri,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajili  ya kumuaga Rais,baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchin

  0 0

  Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba (kushoto) akiongea na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba ya Kenya Prof. Yash Pal Ghai katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Feb. 25, 2013). Prof. Ghai amekutana na Wajumbe na kubadilishana nao uzoefu kuhusu uandishi wa Katiba Mpya.
  Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba (kulia) na Mjumbe wa Tume Bw. Simai Mohamed (katikati) wakiongea na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba ya Kenya Prof. Yash Pal Ghai katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Feb. 25, 2013). Prof. Ghai amekutana na Wajumbe na kubadilishana nao uzoefu kuhusu uandishi wa Katiba Mpya.
  Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Assaa Rashid (kushoto) akiongea na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba ya Kenya Prof. Yash Pal Ghai katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Feb. 25, 2013). Prof. Ghai amekutana na Wajumbe na kubadilishana nao uzoefu kuhusu uandishi wa Katiba Mpya.
  Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Prof. Palamagamba Kabudi (kushoto) akiongea na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba ya Kenya Prof. Yash Pal Ghai katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Feb. 25, 2013). Prof. Ghai amekutana na Wajumbe na kubadilishana nao uzoefu kuhusu uandishi wa Katiba Mpya.
  Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba ya Kenya Prof. Yash Pal Ghai (kulia) akibadilishana mawazo na Naibu Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Casmir Kyuki (kushoto) na Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume Bw. Joseph Ndunguru katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo (Feb. 25, 2013). Prof. Ghai amekutana na Wajumbe na kubadilishana nao uzoefu kuhusu uandishi wa Katiba Mpya.

  0 0

  Akhil Gupta, Deputy Group CEO & Managing Director,cBharti Enterprises Segun Ogunsanya, CEO, Airtel Nigeria, Manoj Kohli,MD & CEO International, Bharti Airtel, Sunil Bharti Mittal, Chairman,Bharti Airtel with H.E. Omobola Johnson, Hon. Minister of Communication Technology, Government of Nigeria at the inauguration of the Airtel Pavilion at the Mobile World Congress 2013

  0 0


   Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani,Dk Selassie Mayunga akiwa amejumika na wananchi wa kijiji cha Sale,wilayani Ngorongoro  kwenye mkutano uliokuwa unahutubiwa na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa Anna Tibaijuka  kwenye ziara ya kutatua migogoro ya ardhi wilayani humo.
  Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa Anna Tibaijuka ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)akizungumza na wananchi wa vijiji vya Olorien Magaiduru na kijiji cha Mgongo,Kata ya Samunge katika ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi wilayani Ngorongoro

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akimkaribisha ikulu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufalme wa Oman Mhe.Yousuf bin Alawi bin Abdullah wakati waziri huyo alipomtembelea na kufanya naye Mazungumzo.
  Rais Dkt,Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya nje wa Oman Mhe.Yousuf Bin Alawi bin Abdullah ikulu jijini Dar es Salaam leo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Mhe.Yousuf Bin Alawi bin Abdullah(kushoto) baada ya kufanya naye mazungumzo ikulu jijini Dar es Salaam leo.Wengine ni wajumbe waliofutana na Waziri huyo(picha na Freddy Maro)

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (kushoto) akiwa na Naibu wake Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) walipokutana kwa mazungumzo  na ujumbe kutoka Jamhuri ya Watu wa China ukiongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Zhai Jun (hayupo pichani)


  Mhe. Membe na Mhe. Maalim wakiendelea na mazungumzo na ujumbe huo kutoka China kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na China. Kulia kwa Mhe. Membe ni Balozi Rajabu Gamaha, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

  Mhe. Zhai Jun (katikati), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa China akimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo yao. Wengine katika picha ni Mhe. Lu Youqing (kulia), Balozi wa China hapa nchini na Bi. Zhang Jing, Mkalimani wa ujumbe huo.

  Mhe. Zhai Jun, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China akizungumza na Mhe. Membe (hayupo pichani) na wajumbe wengine.

  Mhe. Membe na Mhe. Maalim wakimsikiliza Mhe. Zhai Jun (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo yao. Wengine katika picha ni Wajumbe  wa Tanzania wakati wa mazungumzo hayo.

  Mhe. Membe akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo hayo huku Mhe Zhai Jun na wajumbe wengine wakisikiliza

  Wajumbe wa China na Tanzania kwa pamoja wakimsikiliza Mhe. Membe wakati wa mazungumzo hayo.


  Wajumbe wengine wa Tanzania waliokuwepo kwenye mazungumzo hayo. Kulia ni Bw. Assah Mwambene, Mkurugenzi wa Idara ya Habari katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

  Mhe. Membe akimsindikiza Mhe. Zhai Jun mara baada ya mazungumzo yao

  Mhe. Membe akiagana na Mhe. Zhai Jun.

  Mhe. Membe akiteta jambo na Balozi Lu Youqing mara baada ya mazungumzo huku Mhe. Maalim akisikiliza kwa makini.

  0 0


  Mama Salma Kikwete (MNEC) Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Tanzania (WAMA) akisalimiana na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Rukwa mara baada ya kushuka katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga leo. Anaemuongoza ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. Atakuwepo Mkoani Rukwa kwa ziara ya siku tatu ambapo atakabidhi msaada wa vifaa vya hospitali kutoka WAMA, atafanya mkutano na wanawake, atakabidhi pikipiki za mradi wa PMTCT katika tarafa ya Matai Wilaya mpya ya Kalambo, atakabidhi pia vitambulisho vya matibabu ya wazee wa Manispaa ya Sumbawanga, na vilelvile kabla ya kuondoka atafanya mkutano na wanajumuiya wa shule ya St. Theresia ya Mjini Sumbawanga.

  Mama Salma akiveshwa Skafu na moja ya Skauti mara baada ya kuwasili Mkoani rukwa.

  Mama Salma akifurahi na vikundi vya ngoma. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.
  Mama Salma akisalimiana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) Mkoa wa Rukwa Aeshi Hillal ambae pia alikuwa Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini CCM. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kwela Ignas Malocha.
  Mama Salma Kikwete akijadili jambo na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya katika Ikulu ndogo ya Sumbawanga Mkoani Rukwa leo mara baada ya kuwasili katika ikulu hiyo kwa ajili ya mapumziko mafupi, chakula na kusomewa taarifa ya Mkoa.
  Mama Salma Kikwete Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitaka ufafanuzi wa jambo kutoka Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya wakati akimsomea taarifa ya Mkoa wa Rukwa katika sekta ya afya.
  Kutoka kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima, wa tatu ni Ndugu Aeshi Hillal Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) Mkoa wa Rukwa, Iddi Kimanta Mkuu wa Wilaya ya Nkasi na Mussa Chang'a Mkuu wa Wilaya ya Kalmbo wakifuatilia taarifa hiyo iliyokuwa ikiosmwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
  Mganga Mkuu Hospitali Kuu ya Mkoa Rukwa Dkt. Gurisha Richard akifafanua jambo kwa Mama Salma Kikwete juu ya vifo vya mama na mtoto Mkoani Rukwa.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa InjiNIA Stella Manyanya akimkabidhi Mama Salma Kikwete taarifa hiyo ya Mkoa wa Rukwa kuhusu sekta ya Afya. Katika taarifa hiyo Mama Salma kikwete aliutaka uongozi wa Mkoa wa Rukwa kuendelea kutoa elimu kwa kina mama kabla na baada ya kujifungua ili kupunguza vifo vya mama na mtoto ambavyo vingi husababishwa na uelewa mdogo wa akinamama juu ya afya zao na watoto. SOMA TAARIFA HIYO HAPA CHINI. Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa.


  0 0
 • 02/25/13--12:33: KUMBUKUMBU

 • Ilikuwa saa 11.00 jioni, siku kama ya leo tarehe 27 February, 2006 ulipotutoka. Wakati bado tulikuhitaji sana, tulidhani ni ndoto tu.Japo sote tuliamini kuwa siku moja ungeamka ukiwa mzima.Mama,japo leo ni miaka saba tangu ututoke,bado tunahisi tuko ndotoni na tumeshindwa kabisa kukubaliana na ukweli kwamba haupo nasi. Mara kwa mara nakuona ndotoni, lakini ninapoamka nagundua ni ndoto tu,na hiyo inazidisha uchungu na majonzi.

  Japo siku zote tangu ututoke tumekuwa na wakati mgumu sana ,siku hii ya leo tunapoadhimisha miaka saba ya kifo chako ni ngumu zaidi kwetu.Inaleta kumbukumbu zisizoelezeka na zisizostahimilika.
    
  Kazi ya Mungu haina makosa.Tukijiuliza sana kwanini alikuchukua wakati bado tunakuhitaji sana tutakuwa tunakufuru.Tunajaribu kujifariji kwa kuamini kuwa alikuchukua kwa vile alikupenda zaidi yetu.Na tunajitahidi pia kujiridhisha kuwa huko ulipo unapata pumziko la amani na unaangaziwa mwanga wa milele ukistarehe kwa amani.Japo haupo nasi kimwili lakini siku zote tupo nawe kiroho

  Unakumbukwa sana na watoto wako wapendwa Bupe, Lilian na Shirima, Fred na Furaha bila kuwasahau wajukuu zako Irene-Kanyampa, Aziz-Elian, Rose, Junior-Ereneus na Katarina.


  Pumziko la Milele Akupe Ee Bwana na Mwanga wa Milele Akuangazie Ustarehe Kwa Amani,  AMEN

  0 0


  Wafanyabiasha Wakitanzania washio jiji la London siku ya Jumamosi, tarehe 23, mwezi 2  walitembelewa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Peter Kallaghe.
   
  Lengo la ziara hiyo ni kubadilishana nao mawazo na kuangalia jinsi gani wafanyabiashara hao wanavyoweza kutumia fursa za kiuchumi zinazojitokeza nchini Tanzania.
   
  Katika ziara hiyo wafanyabiashara hao walimueleza Balozi Kallaghe mafanikio yao na changamoto zinazowakabili kwanye uendeshaji wa shughuli zao za kila siku.
   
  Wafanyabiashara waliotembelewa ni pamoja na Bi. Jennifer Wright anayemiliki biashara ya kuuza na kununua nyumba pamoja na Soloon za nyele, Bw. Augustino Msey mwenye kampuni ya Swahili Travel and Tours, Moona Store (dukani kwa Sadi) wauzaji wa vifaa vya umeme na wakala wa Westen Union, Salumu wa Barking anayemiliki Foro Barbeque Food, na pia Balozi Kallaghe alipata fursa ya kuhudhuria uzinduzi wa kikundi cha jamii cha Istiqama UK. Balozi Kallaghe aliambatana na wanajumuia ya Kitanzania Bw. Haruna Mbeyu na Bi. Mariamu Mungula.
   
  Balozi Kallaghe alipokutana na mmoja wa wafanyabiashara Bi. Jeniffer Wright alisema kuwa yupo tayari kuwasaidia Watanzania waishio Uingereza na waliokuwepo nyumbani kwa kuwapa mafundisho na maelekezo ya kibiashara kutokana na ujuzi aliokuwa nao. Pia Bi. Wright aliomba serikali ya Tanzania ipunguze vizuizi vya biashara ili waweze kuwekeza nchini Tanzania. Nae Mwenyekiti wa Swahili Group Bw. Augustino Msey alisema kuwa kampuni yake inajitahidi kuitangaza Tanzania katika sekta ya utalii. Bw. Msey aliendelea kusema kuwa kampuni yake inafanya mikakati mikunbwa ya kuwekeza nchini Tanzania. Vilevile Forodhani Barbeque Food waliomba serikali waliangalie suala zima la uraia pacha, kwani Watanzania wanapata tabu sana na vizuizi vingi wanapotaka kuwekeza nchini.
   
  Balozi Kallaghe aliwashauri Watanzania wote wajumuike kwa pamoja, na washirikiane kuleta maendeleo na kuwekeza nchini Tanzania na vilevile wanapopata matatizo wasisite kwenda ubalozini kutaka ushauri na kuomba msaada.  0 0


  Hon. Bernard K. Membe (MP) (2nd left), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation together with H.E. Yousuf bin Alawi bin Abdullah, Minister Responsible for Foreign Affairs of the Sultanate of Oman signing Agreed Minutes of the Areas for Cooperation between Tanzania and Oman.  The two Ministers also signed Memorandum of Understanding on Political Understanding Exchange, today at Hyatt Regency (Kilimanjaro) Hotel in Dar es Salaam.  Others in the photo are Mr. Benjamin Msuya (left), Legal Service Officer in the Ministry of Foreign Affairs (Tanzania) and his counterpart Mr. Isaka (right) from the Sultanate of Oman. 

  Hon. Membe and H.E. Abdullah exchanging Agreed Minutes of the Areas for Cooperation that included sectors of agriculture, infrastructure, railway, trade, industry, trade, investment, energy and minerals, livestock production and fisheries development, and others.  The two countries engaged in the first meeting of Joint Permanent Commission of Cooperation held for two days from February 24 to 25, 2013 in Hyatt Regency (Kilimanjaro) Hotel in Dar es Salaam.
    
  Hon. Membe and H.E. Abdullah shake hands, cementing further economic and political cooperation between the two countries.

  Hon. Membe and H.E. Abdullah exchanging Memorandum of Understanding between the United Republic of Tanzania and the Sultanate of Oman on Political Consultation Exchange.

  Delegates from both countries that comprised of Government and Private Sectors  were in attendance to witness the signing of Agreed Minutes and the MoU on Political Consultation Exchange .

  Mr. John M. Haule (2nd right), Permanent Secretary of the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation exchanges views with Ambassador Simba Yahya (right), Director of the Department of Middle East in the Ministry of Foreign Affairs.  Also in the photo is H.E. Ali Ahmed Saleh (left), Ambassador of the United Republic of Tanzania to Oman welcomes H.E. Abdullah.

  Hon. Bernard K. Membe (MP) (left), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation presents a gift of a mural depicting parts of Zanzibar's buildings and streets to H.E. Yousuf bin Alawi bin Abdullah, Minister Responsible for Foreign Affairs of the Sultanate of Oman.  

  A group photo with Delegates comprised of both Government and Private Sectors from both countries.  Standing in the front role is Hon. Bernard K. Membe (MP) (left - 1st row), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation and H.E. Yousuf bin Alawi bin Abdullah (right - 1st row), Minister Responsible for Foreign Affairs of the Sultanate of Oman.  

  All photos by Tagie Daisy Mwakawago of the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation.


  0 0

  Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Maadili ya Mkoa wa Mara wakiwa Katika Mkutano na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, Mhe. Mohamed Chande Othman Hayupo pichani lengo likiwa ni kusikia na kutafuta njia ya jinsi ya kutatua changamoto mbalimbali zilizopo Katika Kamati hizi. (Picha na Mary Gwera, Mahakama ya Tanzania)

  0 0

  20
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Balozi Charles Sanga katikati wa tatu kutoka kulia, Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania Dk. Aloyce Nzuki kushoto na Zaida Enver Mkurugenzi Mtendaji wa Witch & Wizard Creative (PYT) Ltd wakisaini mkataba wa makubaliano ya kuanzisha onesha la Utalii litakalojulikana kwa jina la Swahili Tourism Fair kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam, ambalo kwa mara ya kwanza litafanyika nchini Tanzania kwenye ukumbi huohuo wa Mlimani City Dar es salaam kuanzia Oktoba 2-5 mwaka huu, Wanaoshuhudia tendo hilo la kusainiwa kwa mkataba huo nyuma ni Mh. Thanduyise Hery Chiliza Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania na kulia ni Ian Kaduma Mwanasheria wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Kampuni ya Witch & Wizard Creative (PYT) Ltd Pia ndiyo inayoandaa maonyesho makubwa ya utalii nchini Afrika Kusini yanayojulikana kama Indaba 21Guido Ceruti Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni ya Witch& Wizard Creative (PYT) Ltd akisaini mkataba huo huku Mh Thanduyise Hery Chiliza Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania akishuhudia tukio hilo kushoto ni Ian Kaduma Mwanasheria wa TTB
  22
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB Balozi Charles Sanga na Zaida Enver Mkurugenzi Mtendaji wa Witch& Wizard Creative (PYT) Ltd wakibadilishana mikataba mara baada ya kusainiwa katikati wanaoshuhudia ni Mh Thanduyise Hery Chiliza Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania Dk. Aloyce Nzuki 


  0 0

  Afisa Elimu mkoa wa Dar es Salaam Raymond Mapunda (kushoto) akimkabidhi hivi karibuni katika ukumbi wa Karimjee zawadi ya redio (music sytem) Winfrida Leonard kutoka shule ya Sekondari ya wasichana ya WAMA – Nakayama iliyopo Rufiji mkoani Pwani ambaye alishika nafasi ya tatu katika mashindano ya kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa Tanzania. Mashindano hayo yaliandaliwa na umoja wa wanafunzi wa Tanzania waliosomeshwa kwa ufadhili wa Japan (JATA) ambapo jumla ya wanafunzi 32 kutoka shule nane walishiriki.
  Faiza Ussi kutoka shule ya Sekondari ya Sunni Madressa ya mjini Zanzibar alifurahia zawadi ya laptop aliyopewa hivi karibuni katika ukumbi wa Karimjee mara baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa Tanzania. Mashindano hayo yaliandaliwa na umoja wa wanafunzi wa Tanzania waliosomeshwa kwa ufadhili wa Japan (JATA) ambapo jumla ya wanafunzi 32 kutoka shule nane walishiriki.
  Meneja wa shule ya Sekondari ya wasichana ya WAMA-Nakayama Ali Mindria (kulia) akipokea kombe la ushindi hivi karibuni katika ukumbi wa Karimjee kutoka kwa Afisa Elimu mkoa wa Dar es Salaam Raymond Mapunda (kushoto) baada ya shule hiyo kuibuka mshindi wa jumla katika shindano la kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa Tanzania lililoandaliwa na umoja wa wanafunzi wa Tanzania waliosomeshwa kwa ufadhili wa Japan (JATA). Wanafunzi wane kutoka shule hiyo waliingia kumi bora kwa kushika nafasi ya tatu, sita, saba na tisa kati ya wanafunzi 32 walioshiriki shindano hilo.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) wakiwa katika picha ya pamoja hivi karibuni na wanafunzi wanne kutoka shule ya Sekondari ya wasichana ya WAMA-Nakayama walioshiriki shindano la kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa Tanzania lililoandaliwa na umoja wa wanafunzi wa Tanzania waliosomeshwa kwa ufadhili wa Japan (JATA) nakushika nafasi ya tatu, sita, saba na tisa. Wanafunzi 32 kutoka shule nane walishiriki katika mashindano hayo yaliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza ambapo shule ya WAMA-Nakayama aliibuka mshindi wa jumla.
  Washindi kumi walioshiriki shindano la kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa Tanzania lililoandaliwa na umoja wa wanafunzi wa Tanzania waliosomeshwa kwa ufadhili wa Japan (JATA) wakiwa katika picha ya pamoja hivi karibuni katika ukumbi wa Karimjee na baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo. Wanafunzi 32 kutoka shule nane walishiriki katika mashindano hayo yaliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza ambapo mshindi wa kwanza alipata laptop yenye thamani ya dola 600 za kimarekani. Picha na Anna Nkinda – Maelezo

  0 0

  Jaji Mkuu wa Tanzania, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, Mhe. Mohamed Chande Othman akiwa Katika mkutano Wajumbe wa Kamati za Maadili za MKOA wa Mara (hawapo pichani) kulia kwa Mhe. Chande (mwenye suti ya dark blue) ni Mkuu wa MKOA wa Mara. Walioketi meza Kuu ni baadhi ya Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama. Tume ya Utumishi wa Mahakama ipo Katika ZIARANI ya MKOA ya kanda ya ziwa (Mwanza, Mara na Kagera) lengo likiwa ni kuimarisha mahusiano mazuri na Kamati za Maadili za mikoa hiyo Katika utendaji kazi wa Tume ya Utumishi wa Mahakama na Mahakama kwa ujumla. (Picha na Mary Gwera, Mahakama ya Tanzania).

older | 1 | .... | 53 | 54 | (Page 55) | 56 | 57 | .... | 3285 | newer