Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109981 articles
Browse latest View live

MH,MAGUFULI UMEIONA HUJUMA HII INAYOFANYIKA KIVUKO CHA KIGAMBONI


MSOSI TIME KABLA YA MECHI

$
0
0
Wachezaji wa timu ya Mbeya City, wakipata chakula kwenye moja ya mgahawa katika mji wa Majimoto Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi, wakati timu hiyo ilipokwenda kucheza mechi ya kirafiki ya dhidi ya kombanini ya timu za City na Shinyanga United za wilayani humo. Mechi hiyo ilichezwa kwenye Uwanja wa Majimoto na timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1. PICHA: GODFREY KAHANGO

KAMATI KUU YA CCM YAHIMIZA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA KUHUDHURIA VIKAO NA KUSHIRIKI KATIKA MIJADALA

$
0
0
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Sekretarieti Makao Makuu ya CCM Dodoma.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Dodoma ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi alisema,Kamati Kuu pamoja na mambo mengine, ilipokea taarifa na kufanya tathimini juu ya maendeleo ya mchakato wa mabadiliko ya Katiba nchini, ndani na nje ya Bunge.

Kamati Kuu vilele imepokea na kujadili taarifa kuhusu mazungumzo na mashauriano kati ya vyama vya CUF, CHADEMA, NCCR-MAGEUZI  na CCM. Mazungumzo ambayo yalisimamiwa na Msajili wa vyama vya siasa nchini.

Aidha Kamati Kuu ilipokea pia taarifa ya kikao cha Baraza la Vyama vya siasa na pia taarifa ya kikao cha Kituo Cha Demokrasia nchini (TCD). Vikao hivyo vyote vilihusu maendeleo ya mchakato wa Katiba nchini.


Kuhusu mwenendo wa Bunge la Katiba, Kamati Kuu imearifiwa maendeleo ya majadiliano na upigaji kura katika kamati za Bunge hilo. Kwa ujumla Kamati Kuu imeridhishwa na namna wajumbe wa Bunge Maalum wanavyoshiriki katika kujadili na kujenga hoja na wanavyoshughulikia tofauti za kimtazamo na kimawazi katika vikao vyao na hatimaye uhutimishaji wa majadiliano kwa kura.

Kamati Kuu inawahimiza wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, kuhudhuria vikao vya kamati na vile vya Bunge na kushiriki katika mijadala kwa kutanguliza masilahi mapana ya taifa na hatimae kuipatia nchi katiba inayotarajiwa na watanzania wote. Chama Cha Mapinduzi kinautakia kila lakheri mchakato huu.


Aidha Kamati Kuu imeridhishwa na juhudi za vyama na wadau mbalimbali katika kujenga na kuimarisha maridhiano na mshikamano kwa lengo la kupata muafaka. Hata hivyo Kamati Kuu imesikitishwa na kuvunjika kwa mazungumzo kati ya CCM, CUF,CHADEMA na NCCR-MAGEUZI yaliyokuwa yanasimamiwa na Msajili wa vyama vya siasa nchini kwa kengo la kujenga na kuimarisha maridhiano na mshikamano ili kupata muafaka.


Kamati Kuu imepokea na kuridhishwa na taarifa kuhusu juhudi zinazofanywa na Kituo Cha Demokrasia nchini (TCD) pamoja na vyama vinavyounda TCD katika kutafuta muafaka wa kisiasa kwa lengo la kuimarisha amani, utulivu, mshikamano na kuaminiana kati ya wadau mbalimbali na hasa kati ya vyama vya siasa.

Kamati Kuu inaunga mkono juhudi za TCD za kuendeleza mashauriano kati ya vyama na ndani ya vyama kwa lengo la kupunguza mivutano, kujenga uaminifu na ustahimilivu na umoja kati yao.

Hivyo Kamati Kuu imempongeza Katibu Mkuu wa CCM kwa namna alivyoshiriki na kukiwakilisha Chama kwenye vikao hivyo.

Kamati Kuu imemuagiza Katibu Mkuu aendelee kukutana na vyama na wadau wengine katika kufanikisha lengo la maridhiano hayo.

Mwisho Kamati Kuu inaendelea kuwasihi Watanzania wote kuendelea kushikamana na kuvumiliana pale wanapopishana kimtazamo juu ya hoja mbalimbali za katiba kwani Amani,  Utulivu na Utanzania wetu ni muhimu kuliko tofauti zetu za kimitazamo. Mchakato wa Katiba nchini uendelee kuwa fursa ya kuijenga nchi yetu badala ya kutumika kutugawa na kututenganisha.

Nakumatt set to celebrate golden milestone with opening of 50thbranch in Arusha, Tanzania this Saturday

$
0
0
Regional retailer, Nakumatt Holdings, will this weekend kick-off a series of consumer reward programmes to celebrate the opening of its 50thBranch in Arusha, Tanzania, this Saturday.

The opening of Nakumatt Arusha, formerly operated by South African Retailer- Shoprite- is a major milestone for the retailer, as it had earlier set a corporate target to open its 50thbranch by February 2015 under its Nakumatt 2.0 Corporate Development Strategy.

Having started its supermarket operations in 1992 with its pioneer Nakumatt Mega store located along Nairobi’s Uhuru Highway opposite Nyayo Stadium, Nakumatt has been enjoying steady growth for the last 20 years.

Under the stewardship of its Managing Director Mr. Atul Shah, Nakumatt has over the last two decades managed to revolutionalise East Africa’s formal retail operations having pioneered several retail concepts. Among other retail concepts, Nakumatt was the first retailer to unveil The 24 hrs shopping across the region.

With a staffing force of more than 7000 across the region, Nakumatt is perhaps now the leading formal sector employer in Retail sphere in East Africa.

Across the region, Nakumatt has been at the forefront in the promotion of regional retail trade integration and currently operates 8 branches in Uganda, 4 in Tanzania and 2 in Rwanda alongside its 36 Kenya stores.

“This weekend, we shall be opening our 50thbranch in Tanzania which will also symbolically confirm our commitment to expand our services beyond East Africa in the next five years,” Shah affirmed.

And added: “As we celebrate this golden milestone, we are also kicking off a variety of consumer reward programmes to express our corporate appreciation to our smart shoppers across the region.”

Currently enjoying a more than US$650million turnover for its regional operations, Shah confirmed that Nakumatt’s future looks bright with its  expansion plans now trained on such markets as, South Sudan and Burundi among others.

With the opening of Nakumatt Mlimani, Pugu road and Nakumatt Arusha Shah, pointed it out that Nakumatt now has four running stores in Tanzania. The three new stores are the latest additions to the existing Nakumatt Moshi store which opened its doors in 2011 in the bustling town at the foot of Mt Kilimanjaro.

In Kenya, Nakumatt is also gearing up for the opening of two new stores in Kenya by the end of the year. 

Alongside the store openings, Nakumatt is also actively enhancing its private brands (Nakumatt Select and Nakumatt Blue Label) roll-out across the East Africa region, to offer the best value proposition to its loyal shoppers.

Zuriel Oduwole Celebrated in Washington DC at Various Events

$
0
0
As the maiden US - Africa Leadership summit with more than 50 African heads of state in attendance enters its last official day in Washington DC, Zuriel Oduwole was being celebrated by women's groups across the city at the high profile side events. After the busy First ladies summit in the center of Washington DC, she was formally received by the director of the US Peace Corp organization; Carrie Hessler - Radelet, back in her office [see attached images]

She mentioned how she has watched many of Zuriels international news interviews on video, and was very inspired by her work, her steps, and her accomplishments at such a young age, with very little budget. Zuriel shared the footprints of her journey, supported by Ethiopian Airlines across the continent. Director Radelet then indicated her readiness to partner with Zuriels inspirational projects on Girls Education, especially across the African continents, as the peace corps already has projects and volunteers across more than 24 African countries.

In honor of her warm reception, Director Radelet then signed one of Zuriels project footballs, as part of her #FollowTheBallForEducation project. It is the very last stop on the project - the USA. The footballs had traveled more than 24,000 miles to many countries across 3 continents, including the USA, Brazil, Ethiopia, South Africa, Mauritius and Nigeria to bring awareness to the issues of Girls education in Africa.

A documentary of the footballs journey is due at the end of 2014
Zuriel Oduwole arrivers peace Corp.
Director of the US Peace Corp organization; Carrie Hessler - Radelet welcomes Zuriel Oduwole.
Director Carrie signs Zuriel Education Project Footbal.

UBORA WA MAGARI YA ENZI HIZOOOOO

$
0
0
SIKU HIZI MNA VIGARI VYENU VYA CEILINGBOARD MNARIIIINGA, MAGARI YALIKUA ENZI ZETU BANA, ANGALIA TANGU 1910 HADI LEO HII BODI IPO VILEVILE MPAKA MTI UMEOTA HUMO HUMO, HAPANA CHEZEA JEREMANI..... UKIITAKA TAFADHALI USIKATE MTI BALI CHOMOA GARI ! VINGEVYO AFISA MISITU ATAKUFIKISHA MAHAKAMANI

RAIS KIKWETE AANZA ZIARA MKOANI MOROGORO

SHIRIKA LA MAGEREZA KUINGIA UBIA WA UCHIMBAJI MADINI YA CHOKAA NA KAMPUNI YA TWIGA CEMENT YA JIJINI DAR

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Jeshi Magereza John Casmir Minja(kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Bw. Alfonso Rodrudges(kulia) kabla ya kusaini Makubaliano ya ubia kati ya Shirika la Magereza na Kmapuni hiyo ya uchimbaji madini ya chokaa katika eneo la Gereza Wazo Hill leo Agosti 21, 2014 Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza John Casmir Minja(kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Bw. Alfonso Rodrudges(kulia) wakisaini nyaraka muhimu za Makubaliano ya ubia katika mradi wa uchimbaji madini ya chokaa katika eneo la Gereza Wazo Hill.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Bw. Alfonso Rodrudges(kulia) wakibadilishana nyaraka muhimu za Makubaliano ya ubia kati ya Shirika la Magereza na Kampuni ya Twiga Cement katika mradi wa uchimbaji madini ya chokaa katika eneo la Gereza Wazo Hill Jijini Dar es Salaam.


Mamlaka ya Elimu Tanzania inatarajia kukabidhi madawati 2000 kwa shule za Msingi 10

$
0
0
Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano toka Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi Sylvia Lupembe akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu jitihada wanazofanya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kukabiliana na changamoto katika sekta ya elimu,wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Masoko na Uhusiano toka benki ya KCB Bi. Christina Manyenye.
Meneja Sheria na Uhusiano toka kampuni ya uuzaji na usambazaji wa mafuta ya TOTAL Bi. Masha Msuya Akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mpango wao wa kutoa zaidi ya madawati 1000 kwa kushirikiana na wadau wengine , mpango huu utaanza kutekelezwa kwa kuanzia na mkoa wa Dar es Salaam.kulia ni Mkuu wa kitengo cha Masoko na Uhusiano toka benki ya KCB Bi. Christina Manyenye.
Afisa Rasilimali Fedha toka taasisi isiyo ya kiserikali ya Social Action Trust Fund (SATF) Bw. Timotheo Tenga akiwaeleza jambo waandishi wa habari( hawapo pichani) wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Sheria na Uhusiano toka kampuni ya uuzaji na usambazaji wa mafuta ya TOTAL Bi. Masha Msuya.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wakiwasikiliza wawasilishaji toka Mamlaka ya Elimu Tanzania, KCB, TOTAL, Social Action Trust Fund (SATF) leo Jijini Dar es Salaam. PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

Robo fainali Dansi 100% kufanyika Jumamosi

$
0
0
Kinyang’anyiro cha mashindano yanayokuwa kwa kasi hapa nchini ya Dance 100% yanayoandaliwa na kituo cha televisheni cha East Africa(EATV) chini ya udhamini wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania,yanaendelea ambapo hapo kesho hatua ya robo fainali inafanyika katika uwanja wa Don Bosco Mbuyuni Namanga jijini Dar es Salaam na kushirikisha makundi 16 kutoka wilaya 3 za mkoa wa Dar es Salaam.

Makundi ya wachezaji wa miondoko mbalimbali ya muziki ambao yamefanikiwa kuingia ngazi ya robo fainali ni Wazawa Crew,Best Boys Crew,G.O.P,The W-T,Best Love,Tatanisha Dancers,Bustani,Quality Boys,Pambana Fasaha,Wakali sisi,Tamtam, Mazabe,TWC,B2K na Winners Crew.

Mratibu wa mashindano hayo,Happy Shame,alisema kuwa katika kinyang’anyiro cha robo fainali hiyo watapata makundi 10 yatakayoingia moja kwa moja ngazi ya nusu fainali hapo baadaye.

“Huu ni mwaka wa tatu East Africa Televisheni tunaandaa mashindano haya kwa udhamini wa Vodacom Tanzania na kinywaji cha Grand Malta na mwaka hadi mwaka yamekuwa yakiongezeka kupata umaarufu na kuwavutia vijana wengi ambao hujitokeza kushiriki”Alisema Shame.

Shame, aliongeza kwamba kundi litakaloibuka na ushindi katika mashindano haya ambayo pia yamekuwa yakionyeshwa na kituo cha televisheni cha East Afrika kila jumatano saa moja kamili usiku,litajishindia kitita cha shilingi milioni 5.

Naye Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wakuu wa mashindano haya,Matina Nkurlu alisema kuwa Vodacom inatoa udhamini kwa kutambua kuwa muziki na michezo ni maeneo ambao yanaweza kutoa ajira kwa vijana na kuweza kuwakwamua kimaisha.

Alisema kuwa Vodacom inatambua kuwa jukumu la kukabiliana na tatizo la ajira hapa nchini sio la serikali peke yake bali pia ni la watu wote ikiwemo makampuni,taasisi za umma na za binafsi na ndio maana siku zote imekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono jitihada za kupambana na tatizo la ajira kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo michezo , burudani na huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo.

“Vodacom tunaamini kuwa vijana wanaweza kuleta mapinduzi makubwa katika sekta mbalimbali iwapo watawezeshwa,hivyo tunadhamini mashindano haya tukiamini kuwa vijana wenye vipaji wanaoshiriki wataweza kujitangaza na kujulikana ambapo katika siku za usoni ni rahisi kujiajiri kupitia katika sanaa”Anasema Nkurlu.

Aliwataka vijana waamke wasibaki nyuma na watumie fursa kama hizi ili waweze kujikomboa kiuchumi “Suala la ajira sio kufanya kazi ofisini tu bali kuna njia nyingi za kujiajiri na kujipatia mapato mojawapo ikiwa ni kupitia michezo,muziki na sanaa nyingine na Vodacom siku zote tutakuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za vijana kujikwamua kiuchumi”Alisisitiza Nkurlu.
Vijana wanaounda Kundi la Mob Squad Kutoka Wilaya ya Temeke wakionyesha umahiri wao katika shindano la Dance miamia hivi karibuni,liloandaliwa na East Africa TV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Baadhi ya mashabiki waliofurika katika mashindano hayo hivi karibuni.

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MKUU WA MKOA WA TABORA KUFUATIA AJALI ILIYOTOKEA HIVI KARIBUNI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mheshimiwa Fatma Mwasa kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea tarehe 19 Agosti, 2014 katika Kijiji cha Mlogolo, Wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora.

Ajali hiyo iliyotokea katika Kijiji cha Mlogolo Wilayani Sikonge, ilihusisha basi la abiria la Kampuni ya Sabena lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Mwanza ambalo lililogongana uso kwa uso na basi lingine la Kampuni ya AM Coach lililokuwa likitokea Mwanza na kusababisha vifo vya watu 19 na kujeruhi wengine 81.

“Nimeshtushwa na kusikitishwa na ajali hii iliyogharimu maisha ya watu 19 na wengine 81 kujeruhiwa” amesema Rais.

“Pokea Salamu zangu za Rambirambi kutokana na ajali hiyo, na kupitia kwako naomba unifikishie Salamu za Rambirambi na pole kwa wafiwa wote kwa kupotelewa ghafla na wapendwa wao. Namuomba Mwenye Mungu, Mwingi wa Rehema azipokee na kuzilaza Roho za Marehemu wote mahala pema peponi, Amina”.

Rais Kikwete amewaomba wafiwa wote wawe na moyo wa uvumilivu na ujasiri wakati huu ambao ni mgumu sana kwao wanapoomboleza vifo vya ndugu na jamaa zao.

Aidha amesema anawaombea kwa Mola majeruhi wote wa ajali hiyo waweze kupona haraka na kurejea tena katika hali zao za kawaida na kuungana tena na familia, ndugu na jamaa zao.

Kwa mara nyingine Rais Kikwete ameendelea kusisitiza umakini na usimamizi mzuri wa Sheria ya Usalama Barabarani kutoka kwa mamlaka zinazohusika, ili maisha ya wananchi wasio na hatia yasiendelee kupotea na kusababisha simanzi kwa familia, na kupotea kwa nguvu kazi muhimu ya Taifa.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
21 Agosti,2014

TDL YAZINDUA KINYWAJI KIPYA CHA KIMATAIFA, FYFE'S SCOTCH WHISKY KATIKA SOKO LA TANZANIA

$
0
0
KAMPUNI ya Tanzania Distilleries Ltd (TDL) imeendelea kujitanua katika soko nchini baada ya kuzindua kinywaji kipya cha kimataifa kiitwacho Fyfe's Scotch Whisky.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kinywaji hicho Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa TDL, David Mgwassa alisema Fyfe's ni kinywaji maridhawa kinachoandaliwa kikamilifu kikiwa na radha murua na ya kipee.

"Ubora wa kinywaji hiki unatokana na umahiri mkubwa wa waandaaji na pia unatokana kimea na nafaka bora zilizotumika na kuwa Fyfe's Whisky huvundikwa kwa miaka kadhaa katika mji Loch Lomond, Scotland ili kuongeza ubora wake kabla ya kuwa tayari kwa matumizi" alisema Mgwassa.

Mgwasa aliongeza kuwa kampuni yao imekuwa ikiwaletea watanzania vinywaji mbalimbali ambavyo vimekuwa chachu katika kusherehekea hatua tofauti za mafanikio yao na kuendelea kuwaletea ladha tofauti za vinywaji bora.

Alisema kinywaji hicho ni zawadi ya pekee katika soko na kuwa Tanzania imekuwa nchi ya kwanza ulimwenguni kuzinduliwa na baadaye kitazinduliwa nje nyingine.
Mkurugenzi Mtendaji wa TDL, David Mgwassa, akizungumza na wadau mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi wa kinywaji hicho.
Langa Khanyile akitoa ufafanuzi wa Whisky hiyo kabla ya uzinduzi.
Sehemu ulipo fanyika uzinduzi huo katika Hoteli ya Serena.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd (TDL), David Mgwassa (wa pli kushoto), akiwa na baadhi ya wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa kinywaji kipya kiitwacho Fyfe’s Scotch whisky, iliyofanyika Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL), Kushila Thomas.

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Waziri Mkuu kuwa mgeni rasmi mashindano ya Kimataifa ya Wushu

$
0
0
Na Daud Manongi, WHVUM

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mashindano ya Kimataifa ya mchezo wa Wushu (Kung fu) yatakayofanyika hapa nchi kuanzia tarehe 30 hadi 31 katika viwanja vya Mnazi Mmoja.

Hayo yamebainishwa na Rais wa Chama cha Mchezo wa Wushu nchini Mwalami Mitete alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

Katika taarifa yake Mwalami alisema kuwa mashindano hayo yatajumuisha vilabu vyote vya mchezo huo hapa nchini ambapo alitaja idadi yake kuwa 23 na kuongeza kuwa kutakuwa na timu shiriki kutoka nchi mbalimbali zikiwemo China, Kenya, Uganda, Zimbabwe, Ethiopia, Libya na Iran.

“Tunatarajia kufanya mashindano ya Kimataifa ambayo yatajulikana kama 2nd Wushu Competition na yatafanyika kuanzia tarehe 30 na 31 kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 12 jioni katika viwanja vya Mnazi Mmoja”. Alisema Mwalami.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Michael Kagondela amesema kuwa ni fursa nzuri kwa wadau wa michezo hapa nchini hasa wa mchezo wa Wushu kwa kuaandaa mashindano makubwa yanayoshirikisha timu kutoka sehemu mbalimbali kwani kufanya hiyvo kutaongeza hamasa kwa wanamichezo wa Tanzania kujifunza kutoka kwao Aidha Kagondela ameupongeza umoja wa wafanyabiashara wa China hapa nchini kwa hatua yao ya kudhamini mashindano hayo na kuomba wadau wengine wajitokeze katika kusaidia kukuza michezo hapa nchini.

Mshauri wa Masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China hapa nchini Liu Pong mshindano hayo kufadhiliwa na Jumuiya ya wafanyabiashara wa China hapa nchini ni matunda ya ushirikiano wa muda mrefu baina ya Tanzania na China na kuongeza kuwa michezo ni njia ambayo itaendeleza uhusiano huo.

Hii ni mara ya pili kwa chama hicho kuandaa michuano mikubwa ya mchezo huo baada ya awali kuandaa michuano ya taifa iliyohusisha klabu pekee za Tanzania iliyofanyika Ufukwe wa Coco mwaka 2011.
Tanzania International
Mshauri wa masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania wa pili kutoka kulia Bw.Liu Pong akiongea na wanahabari hawapo pichani kuhusu mashindano ya kimataifa ya mchezo wa WUSHU yatakoayofanyika kwenye viwanja vya mnazi mmoja mwezi wa nane jijini Dar es Salaam mwaka huu.
Mwakilishi wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Michael Kagondela watatu kutoka kulia akiongea na wanahabari hawapo pichani kuhusu mashindano ya kimataifa ya mchezo wa WUSHU yatakoayofanyika kwenye viwanja vya mnazi mmoja mwezi wa nane jijini Dar es Salaam mwaka huu
Rais wa Chama cha WUSHU nchini wapili kutoka kushoto akiongea na wanahabari hawapo pichani kuhusu mashindano ya kimataifa ya mchezo wa WUSHU yatakoayofanyika kwenye viwanja vya mnazi mmoja mwezi wa nane jijini Dar es Salaam mwaka huu

BALOZI KAMALA ATEMBELEA MTAA UNAOITWA TABORA ULIOPO JIJINI BRUSSELS UBELGIJI

$
0
0
Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiwa katika picha ya pamoja na Bwana. Rodgriguez Lionel anayemiliki duka katika mtaa unaoitwa Tabora uliopo jijini Brussels Ubelgiji. Mtaa huo ulipewa jina la Tabora mwaka 1916 kama ishara ya kumbukumbu ya ushindi wa majeshi ya nchi mbalimbali dhidi jeshi la Ujerumani katika mapigano ya Tabora - Tanzania ya vita Kuu ya Kwanza ya Dunia.

Flightlink waendelea kutanua mbawa,waleta ndege nyingine

$
0
0
Ndege ya Kampuni ya Flightlink iliyowasili nchini hivi karibuni,ikiwa imeegeshwa katika eneo lake kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere jijini Dar es salaam.Ndege hii aina ya Embraer 120 inauwezo wa kubeba abiria 30 na itakuwa ikifanya safari zake katika Mikoa ya Dar es salaam, Dodoma, Zanzibar,Arusha na Pemba.
Muonekano wa siti ndani ya Ndege hiyo.

Balozi wa Uholanzi azungumza na Rais Dk.Shein,Ikulu Zanzibar leo

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Bw.Jaap Frederiks alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa mazungumzo leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Bw.Jaap Frederiks alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Bw.Jaap Frederiks alipofika Ikulu Mjini Zanzibar baada ya mazungumzo leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

SHUKRANI

$
0
0
BIBI. URSULA SABINUS KWEKA
 1944 - 2014.

Kwa niaba ya Familia ya Mzee Sabinus Kweka, napenda kutoa shukrani za dhati kwa matendo, majitoleo na upendo wenu usiku na mchana kwa ajili ya mama yetu Mpendwa URSULA KWEKA kuanzia ugonjwa hadi kifo chake ambacho kilitokea usiku wa kuamkia tarehe 30/07/2014 na kuzikwa tarehe 05/08/2015 kijijini kwake NARUMU,wilaya ya HAI,mkoa wa KILIMANJARO. 

Kwa kuwa siyo rahisi kumshukuru kila mmoja kipekee, tunaomba mpokee nyote shukrani hizi kwa moyo mkunjufu. Kweli tumeuona utukufu wa Mungu. Ila tutakuwa Wachoyo wa fadhila kama hatutashukuru watu au vikundi vifuatavyo:-

1.Uongozi wote wa Mkoa wa Kilimanjaro ukiongozwa na  Mkuu wa Mkoa,Mhe.L.GAMA kwa kuwa nasi siku ya Mazishi 

2.Madaktari na Wauguzi wote wa Hospital za Dr.Mohamed,Selian – Arusha,pamoja na Bugando Medical Centre alikofia marehemu kwa huduma zao za kuokoa maisha ya marehemu bila mafanikio.

3.Majirani wa zamani wa Capripoint na wakazi wote wa Calfonia Nyegezi alikokuwa akiishi Marehemu

4.Ndugu,Jamaa na Marafiki popote walipo hasa wanarumu wa Mwanza na Watanzania waishio Marekani kwa michango yao ya hali na mali pamoja na maombi

5.Vikundi mbalimbali vilivyosaidia kuomboleza msiba K.m Jumaki, Umamwa,Ukiki,Tupendane,wafanyakazi wa Benki kuu Mwanza,Kweka Law Chambers,Kituo cha Utafiti Selian,Kwaya ya Mt.Augustino ya Parokia ya Mkolani kwa mkesha siku zote za maombolezo.

6.Mwisho,wanavijiji wote wa NARUMU, Waombolezaji  wote toka sehemu mbalimbali za Nchi, Mapadri na Masista wote walioshiriki Ibada ya Mazishi…………………………………………………………….

RAHA YA MILELE UMPE Eee BWANA………………………………

“HERI KUIENDEA NYUMBA YA MATANGA, KULIKO KUIENDEA NYUMBA YA KARAMU KWA MAANA HUO NDIO MWISHO WA WANADAMU WOTE” MHUBIRI 7:2

Mh. Kigoda afungua maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini China leo jijini Dar

$
0
0
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda na Balozi wa China Nchini Dkt. Lu Youqing wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa maonyesho ya siku nne ya bidhaa zinazotengenezwa nchini China.
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Shenzhen Yingli New Energy Resources Honglin Hui (Kulia) akimueleza Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda (kushoto) jinsi Solar Panel inayotengenezwa na kampuni hiyo inavyofanya kazi wakati wa maonyesho ya bidhaa zinazotengenezwa nchini China yaliyofunguliwa leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee uliopo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda akiangalia pikipiki aina ya SWAN inayotengenezwa na kampuni ya Honda ambayo inayotumia mafuta ya Petrol na Umeme wakati wa maonyesho ya bidhaa zinazotengenezwa nchini China. Kulia kwake ni Balozi wa China nchini Dkt. Lu Youqing na kushoto ni Juwes Wang ambaye ni mfanyakazi wa kampuni hiyo.

Article 7

MAMA DORCAS MEMBE AFUNGUA KITUO CHA KUSAMBAZIA MATREKTA WAKULIMA CHA KARIATI MATRACTOR KILICHOPO KINONDONI JIJINI DAR

$
0
0
MKE wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dorcas Membe amekitaka kituo cha kusambaza Matrekta kwa wakulima cha Kariati Matrekta kupunguza tena bei za bidhaa hizo ili kuwa kimbilio kwa wakulima.

Kauli hiyo ameitoa leo jijini  Dar es Salaa wakati akizindua kituo hicho ambapo alisema ingawa bei zao zipo chini wapunguze tena ili hata mkulima wa chini aweze kumudu kununua au kukopa trekta hiyo imuwezeshe kuondokana na umasikini.

Akizungumza katika uzinduzi huo alisema anapongeza uanzishwaji wa kituo hicho kwani ni kazi inayowahusu wakulima ambao idadi yake ni takribani asilimia 80.

''Nakupongeza Mkurugenzi kwa jitihada za kuanzisha kituo hiki chenye lengo la kuwawezesha wakulima kupata matrekta na zana zake kwa fedha tasilimu au mkopo, mpango huo utawakomboa wakulima wengi kuondokana na jembe la mkono'' alisema

Mkurugenzi Mtendaji wa Kariati Matrekta, Alhaji Omary Kariati alisema jambo ambalo wanalifanya ni kuunga mkono mpango wa Kilimo Kwanza wa serikali ya awamu ya nne  ya Rais Jakaya Kikwete kwa vitendo.

Aidha alisema kwa kuhakikisha wakulima wanapata dhana za kilimo hadi sasa tayari wamesambaza matrekta 80 ambapo wamekuwa wakikopesha bila ya dhamana.

''Nimeisikia mama akisema kuwa tupunguze bei na namuhakikishia hapa hapa kwamba tumepunguza tena bei   trekta la milioni 23 litanunuliwa kwa shilingi milioni 20''alisema

Mbali na hayo Meneja wa Uhusiano kwa Wateja Wakubwa wa Benki ya KCB, Victor Malewo amesema wanashirikiana vema na kituo hicho hivyo wakulima wategemee mambo mengi mazuri.
 Mke wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikianmo wa Kimataifa, Mama Dorcas Membe (katikati), akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Kituo cha Kusambaza Matrekta cha Kariati Matractor kilichopo Kinondoni Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho, Omary Kariati na Meneja wa Uhusiano kwa Wateja Wakubwa wa Benki ya KCB, Victor Malewo, ambapo wamekiwezesha kituo hicho kupata mikopo ya kununulia matrekta hayo.
 Mke wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikianmo wa Kimataifa, Mama Dorcas Membe na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kusambaza Matrekta kwa Wakulima ya Kariati Matractor , Omary Kariati wakionesha tovuti ya kituo hicho baada ya kufungulia. Tovuti hiyo ya www.kariatimatractor.com itamsaidia mkulima yeyote aliopo nchini kupata fomu kwa ajili ya kununua matrekta hayo.
Mke wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikianmo wa Kimataifa, Mama Dorcas Membe akisoma taarifa yake kwa wanahabari.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kusambaza Matrekta kwa Wakulima ya Kariati Matractor , Omary Kariati (kulia), akizungumza na wanahabri na wageni waalikwa kwenye ufunguzi huo wa ofisi yake.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Viewing all 109981 articles
Browse latest View live




Latest Images