Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 543 | 544 | (Page 545) | 546 | 547 | .... | 3285 | newer

  0 0

  The EU Ambassador to Tanzania Mr Filiberto C. Sebregondi listens to a a group of people living with albinism who called on him at his office in Dar es salaam, exasperated by the very recent violent attacks on persons with albinism which resulted in the killing of  one Mapambo Mashiri (53), a husband who died defending his wife who lives with albinism, Mungu Masaga (35). Sadly, despite his valiant efforts the perpetrators still cut-off her arm and harmed her children. 
   The EU Ambassador to Tanzania Mr Filiberto C. Sebregondi with the group


  0 0  0 0
 • 08/19/14--18:22: mambo ya nathan mpangala


 • 0 0

  Naomba unipe nafasi nitoe maoni yangu kuhusu Uraia pacha nikijbu maoni yaliyoandikwa kwenye gazeti la mwananchi na bwana Humphrey Polepole. 
  Maoni yake yamenishangaza sana na mtu huyu anaonekana ana hujuzi kidogo katika mambo ya uandishi na ameamua kutumua ujuzi wake kudanganya watu kuhusu swala hili la urahia pacha kwa watanzania.

  Napenda iheleweke kwamba urahia pacha sio kitu kigeni Tanzania. 
  Kimsingi na kimazingira Tanzania inaruhusu urahia pacha. 

  1.kwa watanzania wote walio na wazazi wenye urahia tofahuti mpaka watakapofikisha miaka ishrini na moja. 
  2.Kwa wanzanzibar wanye urahia wa zanzibar na urahia wa Tanzania.  Tatizo lililopo sasa ni watanzania wanataka wanufaike na urahia wa nchi nyingine pia na sio watu wengine wanufaike na urahia wa Tanzania. Hofu inayowekwa na wasiopenda maendeleo ya watanzania ni kudanganya kuwa wakongo, wamarekan, wasomali  na wengineo ndio watanufaika na urahia pacha. 
  Kitu ambacho sio kweli mkongo atakapotaka kuwa rahia wa tanzania lazima aombe kupitia uhamihaji ya tanzania urahi huo. Na kira nchi inasheria zake kuhusu uraia  wa kuomba, nchi kama tanzania inabidi huwe umekaa ndani ya nchi kwa miaka isiyopungua kumi.na bado uchunguzi utafanywa kuhusu tabia zako na huko ulikokuwa kabla ya kupewa urahia wa Tanzania. 
  Kwani hata ukikamilisha taratibu zote hizo bado idara ya uhamiaji inaweza kukukatila kuwa rahia wa Tanzania . Sasa ofu ya kusema wageni wengi watanufaika na  urahia wa tanzania. Inatoka wapi.


  0 0

   Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba Mhe Samwel Sitta alioowasili kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwenye ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM Dodoma Agosti 19, 2014. Kulia ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda, kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora), Mhe George Mkuchika akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi
   Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwenye ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM Dodoma Agosti 19, 2014. Kushoto ni Makamu wa Mwenyekiti wa CCM (Visiwani) na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein. Kulia ni Makamu wa CCM (Bara) Ndg Philip Mangula akifuatiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana
   Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa katika Uwanja wa ndege wa Dodoma na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Dkt Emmanuel Nchimbi
  Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikweteakiagana na wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mbunge wa Songea mjini Dkt Emmanuel Nchimbi, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Mbunge wa jimbo la Peramiho Mh. Jenista Mhagama, na Naibu Waziri wa Fedha na mbunge wa Iramba Magharibi Mhe Mwigulu Nchemba 

  0 0
 • 08/19/14--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Msikilize Mwanaid Shaabani katika ngoma hii yab " Viumbe wazito "

  0 0
 • 08/19/14--21:00: Mh.Magufuli umeliona hili?

 • 0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweha saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Lewis Makame Masaki jijini Dar es salaam aliyefariki  katika Hospitali ya AMI Trauma Centre Jijini Dar es Salaam tarehe Agosti 19, 2014.
   Mama Salma Kikwete akiweha saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Lewis Makame,  Masaki jijini Dar es salaam aliyefariki  katika Hospitali ya AMI Trauma Centre Jijini Dar es Salaam tarehe  Agosti 19, 2014.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwafariji wafiwa walipokwenda kutoa pole nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Lewis Makame,  Masaki jijini Dar es salaam aliyefariki  katika Hospitali ya AMI Trauma Centre Jijini Dar es Salaam  Agosti 19, 2014.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na watoto wa marehemu pamoja na Jaji Mstaafu Mark Bomani alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Lewis Makame Masaki,  jijini Dar es salaam aliyefariki  katika Hospitali ya AMI Trauma Centre Jijini Dar es Salaam tarehe Agosti 19, 2014.

  0 0

  Watu  zaidi ya 17 wanadaiwa kufariki dunia na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa  baada ya mabasi waliokuwa wakisafiria kugongana katka k ijiji  cha Mlogolo wilayani Sikonge mkoani Tabora.

  Ajali hiyo imetokea leo hii jioni majira ya saa 11 jioni baada ya Basi la Kampuni ya Sabena lenye namba za usajiri T 110 ARV lililokuwa likitokea Mbeya kwenda  Mwanza kumegongana uso kwa uso na basi la AM Dreamline lenye namba za usajiri  T 803 ATN lililokuwa likitokea Mwanza kupitia Mpanda.

  Ajali hiyo imetokea maeneo ya Mlogolo takribani kilometa 3 kutoka wilayani   Sikonge.Pia inadaiwa kuwa dereva wa basi la Sabena aliyefahamika kwa jina la James Kombe amepoteza maisha baada ya kukatika kiwiliwili na kufa papohapo a kuwa jitihada za kutafuta kiwiliwili chake zilikuwa zikifanyika baada ya kupondeka vibaya.

  Mashuhuda wa ajali hiyo wamedai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni madereva hao kuwa ni wasaidizi ( Day-worker).Inakadiriwa kuwa karibu robo tatu ya basi la sabena imeharibiwa vibaya sana.Mabasi yaliyohusisha ajali hiyo ni basi la  Sabena lililokuokea  Mbeya kwenda -Mwanza na AM Dreamline lililokuokea  Mwanza kwenda Mpanda.

  Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP). Suzana Kaganda ili kuzungumzia ajali hiyo bado zinaendelea.

  0 0

   Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange  akifungua kiwanja kipya cha Michezo kitakachotumika kwa ajili ya michezo ya Majeshi ya Shirikisho la Jumuia ya Afrika Mashariki, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi na kushoto ni Mkuu wa Brigedi ya Nyuki, Brigedia Jenerali Sharif  Sheikh Othman.
   Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange akimpongeza Mkandarasi wa kiwanja hicho kutoka Kampuni ya M. S Maya Heardwere ya Zanzibar Bw. Abdallah M. Salim.
  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange akizungumza na wanahabari mara baada ya ufunguzi wa kiwanja hicho Migombani Zanzibar jana Agosti 19. (Picha na Makame-Maelezo Zanzibar).
   Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange akipokea saluti mara baada ya kuwasili kwenye  ufunguzi wa kiwanja kipya cha Michezo kilichopo Makao Makuu ya Brigedi ya Nyuki Migombani.

  0 0

  DAR ES SALAAM INSTITUTE OF TECHNOLOGY

  INDIA-TANZANIA CENTRE OF EXCELLENCY IN ICT (ITCoEICT).


  Entrepreneurship E-Learning Training Opportunity run by DIT and ILO

  ILO-Start and Improve Your Business (SIYB) program is a materials-based training program for potential and established entrepreneurs who want to improve the management processes of their business. The training is modular in order to meet the specific needs of the target group. 

  The Start and Improve Your Business (SIYB) is based on advanced participatory adult training methodologies. In order to supplement this training, YEF has developed an online SIYB program that creates an additional channel to deliver training to young existing and potential entrepreneurs in the region.


  The SIYB E-learning and Mobile learning program is aimed at delivering a marketable business training course following the course content of SIYB to as wide an audience as possible, using ICT (e-learning and mobile learning) to scale up outreach, whilst increasing convenience, accessibility and user satisfaction for the targeted beneficiaries. With regard to business development services, the benefits from the introduction of the SIYB E-learning program are numerous. 

  Potential and existing entrepreneurs will have an opportunity to access the program through an additional channel. This will provide an environment of flexible learning as well as cross culture learning, leading to new perspectives. The SIYB trainers will, also, have an opportunity to share experiences and resources with other through the e learning and mobile platform forums.  For more information and Registration visit:

  NB: After registration notify Admin by sending Email to daudi.mboma@gmail.com with subject: "SIYB registered trainee" for enrollment.


  For more details:

  Contact:  0715316162


  Published by;


  Director ITCoEICT  0 0


  Naomba kutambulisha kwenu tovuti mpya ya www.kariakootz.com inayofahamika kama Kariakoo Digital ambayo imejikita katika kukusanya orodha ya maduka ya wafanyabiashara wa Kariakoo pamoja na bidhaa wanazouza, mawasiliano yao na mitaa wanayopatikana na kuyaweka sehemu moja ili kukupa urahisi wa kutafuta bidhaa unayohitaji.

  Sasa unawaweza kuokoa muda na pesa zako kwa kutumia tovuti hii mpya ya www.kariakootz.com kupata orodha ya maduka mengi yanayouza bidhaa kariakoo kisha unaweza kuwasiliana moja kwa moja na mwenye duka/biashara hiyo kujua/kulinganisha bei na hata kuagizia bidhaa unayohitaji ukiwa nyumbani au mikoani.

  Kariakoo Digital inalenga kuwaunganisha wafanyabiashara wa Kariakoo na wateja wao ndani na nje ya nchi.

  Karibuni sana!  0 0

  Kutoka kulia ni Mhe. Balozi Dr. Batilda S. Burian akifanya mazungumzo ofisini kwake na Mkurugenzi Mkuu Mpya wa taasisi ya  Shelter Afrique  Bw. James Mugerwa(Katikati) ambaye aliambatana na afisa wake  Bw. Vipya Harawa(Kushoto) ambaye ni Mkurugenzi wa masuala ya ushirikiano katika taasisi hiyo.

  =======  =======  ======= =======

  Bw. James Mugerwa, Mkurugenzi Mkuu Mpya wa Taasisi ya Shelter Afrique  yenye makao yake makuu hapa jijini  Nairobi alimtembelea  Mhe. Balozi Batilda ofisini kwake  kwa ajili ya kujitambulisha kutokana na kuchaguliwa kwake hivi karibuni kuwa Mkurugenzi Mpya wa Taasisi hii muhimu ambayo imekuwa ikijishughulisha na utoaji wa mikopo nafuu kwa nchi wanachama wake kwa ajili uendelezaji wa miji na makazi bora nafuu, ambapo Tanzania ni moja ya nchi mwanachama katika taasisi hii. 

  Mhe. Batilda ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya ambaye pia ni Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya  UN-Habitat na UNEP yenye makao yake makuu hapa Nairobi.

  Katika mazungumzo, Bw. Mugerwa alitoa shukrani za pekee kwa Tanzania kwa jinsi ambavyo imekuwa ikitoa ushirikiano mkubwa kwa Taasisi hii na kuahidi kudumisha na kuendeleza ushirikiano ambao umekuwepo. 

  Kwa upande wa Mhe. Balozi Batilda sambamba na kumpongeza  Bw. Mugerwa kwa kuchaguliwa kwake kuongoza taasisi hii muhimu, alitoa shukrani za pekee kutokana na mikopo nafuu ambayo imekuwa ikitolewa na taasisi hii kwa Tanzania kwenye sekta ya uendelezaji wa  makazi nafuu ikiwa ni pamoja na kumhakikishia kumpa ushirikiano wa Tanzania katika kutekeleza majukumu yake. Bw, Mugerwa ameahidi kuitembelea Tanzania siku za karibuni kwa ajili ya kuendeleza na kukuza ushirikiana ambao umekuwepo baina ya Tanzania na Taasisi hii.

  Imetumwa na  
  Kiyavilo A. Msekwa
  ICT Officer
  Tanzania High Commission,
  Nairobi, Kenya

  0 0

  Ushirikishaji wa wananchi nguzo ya kutekeleza BRN

  TAASISI za Serikali zinazohusika katika utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) zimetakiwa kuhakikisha kuwa wananchi wanaelezwa mafanikio na changamoto za utekelezaji wa Mpango huo.

  Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam leo Jumatano na Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Rais-Usimamizi wa Utekelezaji wa Miradi (PDB) inayosimamia utekelezaji wa BRN, Bw. Omari Issa alipokuwa akifungua Mkutano wa Kwanza wa Watendaji wa Serikali Kutathmini Utekelezaji wa BRN.

  BRN ilianza kutekelezwa Julai mwaka jana ikisimamiwa na Kitengo kipya cha Rais kinachoshughulikia Usimamizi wa Miradi (PDB).

  Akifungua mkutano huo uliohusisha Wakurugenzi wa Wizara zinazohusika na BRN na taasisi zingine za utekelezaji, Bw. Issa alisema kuwa katika mwaka mmoja uliopita BRN imeweza kuleta mageuzi makubwa katika utendaji na utekelezaji wa miradi.

  Hata hivyo alisema mafanikio hayo na changamoto zake vinapaswa kuelezwa kwa umma ili kuwashirikisha wananchi wafahamu na kutoa mchango wao.

  "Natoa rai kwa Wizara na taasisi zinazohusika na utekelezaji wa BRN kuimarisha mawasiliano kwa umma ili wananchi wawe na taarifa na pia tuweze kupata mrejesho wa kuwahudumia zaidi siku zijazo," alisisitiza Bw. Omari akifafanua kuwa PDB iko tayari kufanyakazi na Wizara kusaidia mawasiliano.

  Akizungumzia mwaka mmoja wa utekelezaji wa BRN, Bw. Issa alisema moja ya mafanikio ni BRN kuimarisha ari ya watendaji wa Serikali katika kila mmoja kufanya maamuzi na utekelezaji wa haraka unaojali muda na matokeo.

  "Wizara ya Maji ni moja ya mfano mzuri wa taasisi za Serikali ambako dhana ya BRN imeonekana kuleta mafanikio. Tulipoanza tu kutekeleza miradi ya kupeleka maji vijijini wataalamu waliokuwa makao makuu ya Wizara walihamishiwa mikoani na baadhi ya taratibu za manunuzi zikapunguzwa.

  "Leo ninayofuraha kuwaeleza kuwa mfumo huu wa nidhamu ya utekelezaji wa BRN umefanyakazi kubwa. Katika wizara hiyo zaidi ya wananchi milioni mbili wamepatiwa maji vijijini ndani ya mwaka mmoja ikilinganishwa na idadi ya watu 500,000 (laki tano) tu waliokuwa wakipatiwa maji kwa mwaka kabla ya mfumo wa BRN kuanza," alisema.

  Katika mkutano huo wa tathmini, watendaji hao wa Serikali watatumia muda huo kuchambua changamoto zilizoikabili BRN katika mwaka mmoja uliopita, kuainisha mikakati ya kushughulikia changamoto hizo na watendaji hao kuweka kiapo cha kujituma zaidi katika utekelezaji siku zijazo ili kupata matokeo makubwa zaidi.

  0 0

   Deputy Permanent Secretary President's Office-Public Service Management Mr.HAB Mkwizu (left) speaking at a farewell ceremony of departing JICA Senior Representative Mr.Hajime Iwama (second left) at the President's Office - Public Service Management yesterday.
   Deputy Permanent Secretary President's Office-Public Service Management Mr.HAB Mkwizu (left) present a gift to outgoing JICA Senior Representative Mr. Hajime Iwama during a farewell ceremony held at the President's Office-Public Service Management yesterday.
  Deputy Permanent Secretary President's Office-Public Service Management Mr.HAB Mkwizu (second left) in a group photo with JICA staffs, and President's office officials after a farewell of departing JICA Senior Representative Mr.Hajime Iwama (right,first line) held at the President's Office-Public Service Management yesterday.

  TANZANIA TO BENEFIT FROM ABE INITIATIVES


  By Happiness Shayo.


  The Government of United Republic of Tanzania is among four African countries that benefits from Master’s Degree and Internship Program of the African Business Education Initiative for Youth (ABE Initiative) initiated by Japanese Government through Japanese Prime Minister Abe.


  Speaking yesterday during a farewell ceremony at the President’s Office, Public Service Management the departing JICA Senior Representative Mr. Hajime Iwama said that the program supports youth who have potential to contribute to their countries.“This program will support young men and women from Private and Government Sectors to study Master Courses in Japanese Universities as international students and experience internships at Japanese enterprises.”

  He said the aim of the program was to develop effective skills and knowledge so that they can contribute to the development of their societies. He listed other countries which benefits from the program as Republic of Kenya, Republic of Mozambique and Republic of South Africa.

  Mr. Iwama explains that the implementation of the program started this year whereby 33 Tanzanians have been selected to attend Master’s Degree Program in Japan.Meanwhile, Deputy Permanent Secretary; President’s Office Public Service Management Mr.HAB Mkwizu said that JICA has been very instrumental in supporting Tanzania’s development through soliciting and allocating volunteers and experts to serve the needs of the people in different parts of the country.

  He mentioned among the sectors supported by government of Japan through JICA as health, education and infrastructure development among others.Mr. Mkwizu assured JICA Reprentatives that Tanzania will continue to sustain the programmes and projects initiated by JICA in order to deliver desired benefits to the intended communities.

  0 0


   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu (katikati) akiingia katika kongamano la majadiliano kuhusu changamoto za kufikika kwa huduma za fedha kwa wajasiriamali wadogo na wa kati Tanzania jijini Dar es Salaam Jumanne wiki hii.  Wengine ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC), Bw. Raymond Mbilinyi (kushoto) na  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bw. Godfrey Simbeye (Kulia).  Kongamano hilo lilitayarishwa na TPSF pamoja na Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT).

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bw. Godfrey Simbeye (Kushoto) akitoa hotuba yake wakati wa kongamano la majadiliano kuhusu changamoto za kufikika kwa huduma za fedha kwa wajasiriamali wadogo na wa kati Tanzania jijini Dar es Salaam Jumanne wiki hii.  Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu; Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC), Bw. Raymond Mbilinyi (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa VICOBA na Mbunge Viti Maalum, Bi. 
  ========  ========  ==========
  Taasisi za fedha nchini zimeshauriwa kulegeza masharti ya utoaji mikopo ili wajasiriamali nchini waweze kupata fursa zaidi ya kupata mitaji kuendeleza biashara zao na kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa nchi.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua Kongamano la majadiliano kuhusu changamoto za kufikika kwa huduma za fedha kwa wajasiriamali wadogo na wa kati Tanzania jijini Dar es Salaam. Waziri huyo alisema Jumanne wiki hii kuwa taasisi za fedha nchini zilegeze masharti ili wajasiliamali waweze kupata mitaji ya biashara zao.
  Kongamano hilo lilitayarishwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kwa kushirikiana na Financial Sector Deepening Trust (FSDT). “Ninayo furaha kubwa kuona TPSF na wadau wengine wameandaa kongamano hili ambalo linalenga kutafuta suluhisho la wajasiliamali kupata mitaji kutoka taasisi za fedha,”alisema.
  Alisema moja ya changamoto ambazo wajasiriamali wanakumbana nazo ni namna ya kupata mitaji kutoka katika taasisi hizo, jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya biashara. Alisema mikopo kutoka benki inatolekewa kwa masharti makubwa na riba kubwa jambo ambalo ni kikwzo kwao na taifa pia.
  “Sera ya nchi inaruhusu sekta binafsi kuendesha uchumi kupitia kampuni ndogo, za kati, na wajasilimali, sasa mitaji kwa wajasiriamali ni jambo ambalo haliepukiki,”alisema. Alisema serikali inashirikiana na TPSF kuhakikisha mazingira ya biashara yanaimarika na kongamano hilo ni moja ya hatua muhimu katika kuondoa vikwazo hivi.
  Aidha alisema wakati nchi inasubiri kuingia katika uchumi mkubwa kutokana na gesi na mafuta ni lazima wajasiriamali wadogo wawezeshwe ili pia wawe na uwezo wa kutoa huduma kwa kampuni kubwa. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji TPSF, Bw. Godfrey Simbeye alisema kongamano hilo ni la muhimu katika kutafuta ufumbuzi wa mitaji  kwa wajasiliamali ambao ni tegemeo kubwa katika kuendeleza nchi.
  “Nchi zilizofanikiwa zimewekeza katika maendeleo ya wajasiriamali wao, hatuna budi kufanya hivyo,” alisema. Alifafanua kuwa wajasiriamali wakipatiwa huduma za fedha na kukuza mitaji yao, wana nafasi kubwa ya kuleta maendeleo.“Tumeshuhudia ukuaji wa mitaji na uchumi wetu unakwamishwa na mambo mengi mojawapo ni namna ya kupata mitaji,”alisema.
  Alisema mitaji mingi inatoka benki lakini kwa  mazingira yaliyopo ni vigumu kwa biashara inayoanza kupata mitaji kutokana na masharti ambayo siyo rafiki. Alisema sekta hiyo lazima iwezeshwe sababu ndiyo yenye uwezo wa kutoa jira kubwa na kuleta mapinduzi ya uchumi.
  Naye Mtaalamu wa Maswala ya Wajasilimali, kutoka FSDT, Bw. Peter Kingu alisema kuna kila sababu taasisi za fedha kupanua wigo kwa wajasilimali kupata mitaji bila ya kuweka masharti magumu. “Taasisi yetu inafanya kazi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo TPSF katika kuhakikisha wajasiriamali wanaimarika kibiashara,” alisema.
  Kongamano hilo lilishirikisha wadau mbalimbali toka sekta binafsi, sekta ya umma, taasisi za utafiti, kampuni mbalimbali pamoja na benki miongoni mwa wadau wengine. Kampuni ya simu za mkononi ndiyo iliyodhamini kongamano hilo. Inatarajiwa kuwa maazimio ya kongamano hilo yatasaidia katika juhudi za kurahisisha upatikanaji wa huduma za fedha miongoni mwa wajasiriamali wadogo na wa kati hapa nchini.

  0 0

   
   Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania ,Kelvin Twissa akitoa mada juu ya huduma zinazotolewa na kampuni yake wakati wa Warsha ya kushirikishana uzoefu kuhusu njia za kuboresha na kupanua huduma za kifedha kwa biashara ndogo na za kati hapo jana. Warsha hiyo iliandaliwa na Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) na kudhaminiwa na Vodacom.Kushoto ni muongozaji  wa mada Felix Mlaki  na Katikati ni Mtaalamu toka Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE)Moreme Marwa. 
   Mmoja wa washiriki wa Warsha ya kushirikishana uzoefu kuhusiana na njia za kuboresha na kupanua huduma za kifedha kwa biashara ndogo na za kati iliyoandaliwa na Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania, akisoma moja ya jarida la Vodacom  wakati wa warsha hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam hapo jana. 
  Baadhi ya washiriki wa Warsha ya kushirikishana uzoefu kuhusu njia za kuboresha na kupanua huduma za kifedha kwa biashara ndogo na za kati iliyoandaliwa na Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania,wakifuatilia mada kwa makini  zilizokuwa zikitolewa  wakati wa  warsha hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam hapo jana. 

  0 0

   Timu ya Airtel wakiongozwa na Emanuel Rafael zone Businnes Manager mara baada ya uzinduzi wa mnara wa kampuni ya mawasiliano ya airtel katika kijiji cha Sigunga wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma hafla ya uzinduzi imefanyika jana kijijini humo
   Mkuu wa wilaya Khadija Nyembo akiongea wakati wa uzinduzi wa mnara wa airtel katika kijiji cha Sigunga wilaya ya Uvinza mkoani kigoma hafla ya uzinduzi imefanyika jana kijijini humi
   Kikundi cha Ngoma kikiburudisha katika sherehe za uzinduzi wa mnara wa Airtel kijiji SIGUNGA wilaya ya Uvinza mkoani  Kigoma.
  =======  =======  =========
  Airtel yawafikishia Wanakijiji wa Sigunga Kigoma huduma za mawasiliano
  ·         Yazindua mnara wa mawasiliano katika kijiji cha Sigunga mkoani Kigoma, wanakijiji Kunufaidika na huduma za mawasiliano ya simu za mkononi toka Airtel
  Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel leo imezindua rasmi huduma za mawasiliano katika kijiji cha Sigunga wilaya ya  Uvinza mkoani Kigoma

  Uzinduzi huo unafatia jitihada za kampuni ya Airtel kuendelea kuboresha mawasiliano ya huduma za simu za mkononi katika maeneo mbalimbali nchini husasani katika maeneo ya vijijini huku lengo likiwa ni kuzifikia jamii zinayoishi pembezoni mwa nchi huduma bora ya Airtel Money.

  Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma za mawasiliano Sigunga,  Meneja Mauzo kanda ya Ziwa bwana Raphael Daudi alisema “ Airtel inatambua adha wanayoipata wakazi wa kijiji cha Sigunga na maeneo ya jirani katika kupata huduma za mawasiliano kwa muda mrefu sasa,  hivyo tumeonelea ni vyema basi tukachukua hatua ya kuboresha huduma hizi muhimu kwa kuwafikishia wanakijiji hawa  mawasiliano yatakayowawezesha kufanya shughuli zao za kila siku kwa ufanisi zaidi

  Kupitia mnara huu sasa tunaweza kuwaunganisha wanakijiji hawa na maeneo mengine ya nchi, tutawawezesha kupata masoko ya kuuza biashara zao kwa urahisi, tumewawezesha kupata huduma za kifedha kupitia huduma yetu ya Airtel Money ambapo sasa wataweza kupokea na kutuma pesa kwa ndugu jamaa na marafiki pia kupokea malipo ya biashara zao na kuweza kufanya malipo mbalimbali ya huduma muhimu wakiwa majumbani mwao. Sambamba na hilo mawasiliano jijini hapa yamekuwa chachu ya maendeleo na ukuaji wa shughuli za kiuchumi kwa ujumla.

  Kwa upande mkuu wa wilaya ya Uvinza Khadija Nyembo alisema” Tunawashukuru sana Airtel kwakutambua kwa vitendo umuhimu wa mawasiliano kwa kutufikishia mawasiliano kijijini hapa. Kupitia mawasiliano ya Airtel tumeweza kuboresha usalama wa raia na mali zao, kuwezesha kufanyika kwa  shughuli za kiuchumi kiufani , wakulima sasa wanauhakika wa kupata masoko na kupata malipo kwa kupitia simu ya mkonono.  sambamba na hilo mawasiliano hayo yamewezesha huduma muhimu za  kijamii kuboreshwa zaidi.

  Natoa wito kwa wakazi wa Sigunga Na vijiji vya jirani kutumia mawasiliano haya katika kukuza uchumi wao na wa jamii kwa ujumla.

  Wakiongea kwa wakati tofauti wakazi wa Sigunga wameishukuru Airtel kwa kuwafikishia  mawasiliano hayo nakusema , tumekuwa na adha kubwa ya huduma za simu kabla ya mawasiliano haya kufikishwa kijijini hapa lakini kwa sasa kero hiyo imekwisha kabisa hivyo tunaipongeza sana kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa juhudi zao.

  0 0

   Warembo watakaoshiriki mashindano ya Redd's  Miss Temeke, wakiwa katika picha ya pamoja na Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Khalid Mohamed (TID), anayemiliki bendi ya  Top in Town,itakayotoa burudani katika mashindano hayo.
  Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Khalid Mohamed (TID), anayemiliki bendi ya  Top in Town, akielezea katika mkutano na waandishi wa habari, katika  klabu ya City Sports & Lounge jinsi alivyojiandaa kutoa burudani katika mashindano ya Redd's Miss Temeke yatakayofanyika ijumaa ndani ya TCC Club,Chang'ombe, Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mwandaaji wa mashindano hayo, Benny Kisaka.Nyuma yao ni baadhi ya warembo watakaoshiriki mashindano hayo. 

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0


older | 1 | .... | 543 | 544 | (Page 545) | 546 | 547 | .... | 3285 | newer