Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 542 | 543 | (Page 544) | 545 | 546 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'  kushoto akiwaelekeza mabondia jinsi ya kupiga ngumi ya mkunjo wa chini 'upper-cut' wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya Ilala iliyopo  Amana CCM, Dar es salaam
  Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'  kushoto akimwelekeza bondia Lulu Kayage jinsi ya kupiga ngumi kwa kuingia ndani bila woga wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya Ilala.

  0 0

   HUAWEI Technologies (T) Limited Channel Executive, Mr. Moses Hella (left) explains to the President of the United Republic of Tanzania, Hon. Dr. Jakaya Kikwete on the company’s latest introduced latest smart phone called Ascend P7 when he visited the company’s booth during a two-day Tanzania Diaspora Initiative conference held in Dar es Salaam recently. Second left is the Prime Minister, Mizengo Pinda and Huawei Terminal Marketing Manager Lydia Wangari (third left).
  HUAWEI Technologies (T) Limited Channel Executive, Mr. Moses Hella (left) explains to the President of the United Republic of Tanzania, Hon. Dr. Jakaya Kikwete on the company’s latest introduced technology called Enhanced LTE (eLTE) when he visited the company’s booth during a two-day Tanzania Diaspora Initiative conference held in Dar es Salaam recently. Looking on second left is the Prime Minister, Mizengo Pinda.

  HUAWEI Technologies (T) Limited, a leading global information and communications Technology (ICT) company, has introduced in the Tanzania market a new technology called enhanced LTE, which will boost the government’s anti-poaching campaign as well as critical communication and video trunking or video surveillance for enterprises.

  Speaking during a two-day Tanzania Diaspora Initiative conference held in Dar es Salaam recently, Huawei Technologies Channel Executive, Mr. Moses Hella said the new device enables fast restoration of communication at critical times, having a video trunking (WALKI-VIDEO) for quick and accurate dispatch decision making, which can be effective in the current Tanzania anti-poaching campaign. 

  “We have introduced into the Tanzania market our latest technology called ‘enhanced LTE’ which is a state of the art mobile solution for critical communication as well as mobile video surveillance especially in transporting of important goods or people.

  “With this device, problems like illegal poaching in the country can be minimized if not eradicated. We believe that by installing this device in areas where illegal poaching is rampant will boost the ability of game wardens to monitor and track activities going on in the game parks/national reserves. 
  “Installing wireless cameras and deploying mobile surveillance system in different national game reserves will greatly support the government’s anti-poaching campaign,” said Mr. Hella.

  He reiterated that the eLTE technology has been deployed in more than 30 countries mostly in Armies, Police, Power Grids, Ports, Airports, Oil and Gas fields as well as Security Companies. Mr. Hella said that Huawei being the main sponsor of the fast Diaspora conference; it helped the company showcasing several other latest technologies such as smart-phones, modems and home devices that helps Tanzanians to catch up with technological advancement.

  “We have also introduced our latest smart phone called Ascend P7 which is an outstanding artwork with 5.00-inch 1080x1920 High Definition display powered by 1.8GHz processor alongside 2GB RAM and 13-megapixel rear camera, the gadget was also handed over to the President who visited our Huawei booth making him to be among the first Huawei Ascend P7 user in Tanzania,” he added.

  Commenting on Huawei’s eLTE technology President Jakaya Kikwete said; “this is good technology, did you show to Kova, the Special Zone Police Commander?”

  Meanwhile, during the meeting the president encouraged the Tanzania Diaspora to bring technologies in Tanzania.  The President urged for the Tanzania Diaspora to bring technologies in Tanzania. He said "Today Huawei gave me their latest smart phone P7, this shows Huawei is keeping up with competition and innovations, so Diaspora have to cooperate with these giants to bring technologies in Tanzania."

  Likewise, Mr. Hella mentioned that Huawei for more than ten years in Tanzania has been working hand in hand with the community to bridge the digital gap through ICT training to subcontractors and telecom operators.

  “We hope we can cooperate further with the Government and Diaspora society in bridging digital gap in Tanzania especially in the area of capacity building,” he said.


  Huawei is the leading telecommunication solution provider in the world with operations in more than 170 countries. The company has 150,000 staffs globally, and they have more than 120 staff in Huawei Tanzainia company, in which more than 65% are Tanzanians. 

  0 0
 • 08/18/14--23:38: IGA UFE!

 • 0 0  Marehemu Jaji Mstaafu,Lewis Makame enzi za uhai wake

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za  Rambirambi Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, National Electoral Commission (NEC) kufuatia taarifa za kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Lewis Makame kilichotokea katika Hospitali ya AMI Trauma Centre Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Agosti, 2014. 

  “Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Tanzania na Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) chini ya Mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa, Mheshimiwa Lewis Makame ambaye amelitumikia Taifa letu katika Utumishi wa Umma kwa uaminifu, uadilifu, bidii na umahiri mkubwa”, amesema kwa masikitiko Rais Kikwete katika Salamu zake. 

  Katika utumishi wake, Marehemu Jaji Lewis Makame, enzi za uhai wake, alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kabla ya kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa na baadaye Mwenyekiti wa NEC ambayo aliiongoza kwa miaka 17 mfululizo hadi alipostaafu mwaka 2011.  Uongozi wake ulichangia sana kuimarisha amani, utulivu, umoja na mshikamano wa kitaifa katika mazingira mapya ya demokrasia ya vyama vingi vya siasa hapa nchini.

  “Ni kwa kutambua kipaji kikubwa cha uongozi alichokuwa nacho Marehemu Jaji Lewis Makame, Taifa letu limepoteza mtu muhimu sana kwani hata baada ya kustaafu kwake alikuwa bado anahitajika sana kutokana na mchango wake wa ushauri katika mambo mengi yanayohusu maendeleo ya nchi yetu”, amesema Rais Kikwete na kuongeza,

  “Kutokana na msiba huu mkubwa, nakutumia Salamu za Rambirambi kwa kumpoteza aliyekuwa Kiongozi Mahiri wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Kupitia kwako, naomba Salamu zangu za Rambirambi na pole nyingi ziifikie Familia ya Marehemu kwa kumpoteza Kiongozi na Mhimili Madhubuti.  Namuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aipokee na kuilaza Mahala Pema Peponi Roho ya Marehemu, Jaji Lewis Makame, Amina”, amesema Rais Kikwete akiomboleza msiba huu.   

  Amewahakikishia Wanafamilia kuwa yuko pamoja nao katika kuomboleza msiba huu mkubwa, na anamuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema awape moyo wa uvumilivu, ujasiri na subira Wanafamilia wote, ndugu na jamaa wa Marehemu, ili waweze kuhimili machungu ya kuondokewa na Mpendwa wao kwa kutambua kuwa yote ni Mapenzi yake Mola.  

  Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu.
  Dar es Salaam.
  19 Agosti, 2014


  0 0

  Wazazi wana wajibu na ulazima wa kuhakikisha kwamba watoto wao wanawasimamia vyema katika kupata elimu bora itakayotoa mwanga wa kimaisha katika hatma yao ya baadaye. 

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa nasaha hizo wakati akizunghumza na Uongozi wa Kamati ya Skuli, walimu, Wazazi na Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Kinyasini Wilaya ya Kaskazini “A “ mara baada ya kuikagua na kuangalia maendeleo na changamoto zinazoikabili skuli hiyo. 

  Balozi Seif alisema elimu ndio ufunguo pekee pekee utakaowapa njia watoto hao kukabiliana na mazingira ya kimaisha yanayokwenda kwa kasi na haraka ndani ya mfumo wa sasa wa sayansi na Teknolojia. 

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliipongeza Kamati ya Uongozi ya Skuli hiyo kwa jitihada zake kubwa inazochukuwa kwa kushirikiana na walimu na kuleta maendeleo makubwa. Mapema Mwenyekiti wa Kamati ya Wazee wa Skuli ya Sekondari ya Kinyasini Nd. Simba Haji alimuomba Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kufuatilia ahadi iliyotolewa na aliyekuwa Waziri Kiongozi wa Mwisho wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kutafuta mbinu za kulitengeneza Jengo la madarasa manne la Skuli ya Msingi ya Kinyasini ambalo liko katika hali mbaya. 

  Skuli ya Kinyasini ikiwa ni miongoni mwa skuli kongwe ndani ya Mkoa wa Kaskazini Unguja iliasisiwa mnamo mwaka 1946 kwa Darasa la Quran na kuanza kwa darasa la kwanza mwaka 1947 lililoendelea hadi darasa la kumi na moja kwamba 1973.
  Mwalimu Mkuu wa SDkuli ya Sekondari ya Kinyasini Mkoa wa Kaskazini Unguja Mwalimu Haroun Juma akimkaguza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefanya ziara fupi kuangalia maendeleo ya changamoto zinazoikabili Skuli hiyo.
  Balozi Seif akibadilishana mawazo na walimu wa Skuli ya Kinyasini Sekondari alipokfanya ziara fupi skulini hapo.
  Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Kinyasini Sekondari Haroun Juma akimuonyesha Balozi Seif Vikalio vilivyotengenezwa kwa zege ndani ya madarasa ya Sekondari ya skuli hiyo.
  Balozi Seif akishangaa mabadiliko makubwa ya majengo ndani ya Skuli ya Sekondari ya Kinyasini ambapo ndipo alipoanzia kupata elimu ya msingi katika miaka ya 46. Kushoto ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Skuli ya Kinyasini Sekondari Nd. Simba Haji.
  Balozi Seif akiangalia kisima cha Skuli hiyo ambacho kilipata hitilafu ya mafuta baada ya bomba la mafuta lka kituo cha Petroli kiliopo katibu na skuli hiyo kupasuka na kutembea katika miamba hadi eneo hilo la kisima. Kushoto ya Balozi Seif ni Mwalimu Mkuu wa Skuli hiyo ya Kinyasini Sekondari Mwalimu Haroun Juma.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizunguma na wazazi, kamati ya skuli, walimu na wanafunzi wa skuli ya sekondario ya Kinyasini mara baada ya kukaguzwa kuona maendeleo na chngamoto zinazoikabili. Picha na Hassan Issa wa –OMPR – ZNZ.

  0 0

  Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amekubali kumuondolea sakramenti ya upadri, Padri Raymond Mosha wa Jimbo la Katoliki la Moshi ikiwa ni miaka 20 tangu padri huyo aombe kujiondoa kwenye daraja hilo. 

  Barua ya uamuzi wa Papa Francis ilisomwa jumapili ya juzi katika parokia na vigango vyote vya Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi wakati wa ibada za jumapili zilifanyika katika makanisa ya jimbo hilo. 

  Miongoni mwa parokia ambazo barua hiyo ilisomwa ni Parokia ya Karanga ambako Paroko wake, John Matumaini alitoa tangazo hilo katika ibada zote. Uamuzi huo ambao ni nadra sana kutolewa na Papa, unamaanisha kuwa sasa hivi padri huyo yuko huru kuoa na kuwa na familia kama Wakristo wengine. 

  Hata hivyo, wakati uamuzi huo ukitangazwa rasmi juzi, tayari Padri Mosha ambaye ni profesa wa falsafa na maadili katika Chuo Kikuu cha Nelson Mandela Arusha, ana mke na watoto watatu ambao kwa sasa wako vyuo vikuu. 

  Padri Mosha alisema aliandika barua kuomba kuondolewa daraja hilo mwaka 1994 kabla ya uamuzi kutolewa juzi. 

  Katika orodha ya mapadre 185 wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi iliyopo katika tovuti ya jimbo hilo, jina la Padri Mosha linaonekana likiwa ni namba 23. 

  Akizungumzia hatua hiyo, Padri Mosha alisema: “Ninafurahi kufunguliwa kifugo hiki na hii itanifanya niishi kama Mkristo. Kwa vile hawajaniondolea sifa ya kutoa huduma kama vile ibada za mazishi, sakramenti ya mwisho na ubatizo, nitaendelea kutoa kwa wahitaji kwa sababu ninaupenda ukristo. 

  “Nashukuru sasa nimekuwa muumini wa kawaida nitaweza kufunga ndoa kanisani kwa kuwa nilikuwa nimefunga ndoa ya kisheria tu kwa DC.” 

  Kuhusu kwa nini aliamua kuacha upadri, Profesa Mosha alisema ni baada ya kufanya kazi hiyo kwa miaka 20 na akaona ipo haja ya kuwa na familia lakini kanisa lilikuwa haliruhusu. 

  “Sasa kwa kuwa kanisa haliruhusu mapadri kuoa ndiyo maana nikaamua kuandika barua ambayo hata hivyo, imechukua muda mrefu kujibiwa na tayari nina watoto watatu wako chuo kikuu.

  0 0

  Mkurugenzi Msaidizi Habari, Elimu na Mawasiliano toka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw. Cosmas Mwaisobwa akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu maandalizi ya utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2014/2015, wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa.
  Baadhi ya Waaandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi Habari, Elimu na Mawasiliano toka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw. Cosmas Mwaisobwa wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Na Rose Masaka - MAELEZO

  Serikali ya Tanzania imesaini mkataba wa kupokea mkopo nafuu wa shilingi bilioni 203 kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya kuendeleza sekta ya elimu katika mpango wake wa matokeo makubwa sasa(BRN).

  Mkataba huo umesainiwa na Katibu mkuu wa wizara ya fedha Dk. Servacus Likwelile huku ukiwashirikisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Elinu na Naibu Katibu Mkuu kutoka TAMISEMI leo jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza wakati wa hafla hiyo fupi ya kusaini mkataba Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dk. Servacus Likwelile ameishukuru Benki ya Dunia kutoa mchango huo kusaidia sekta ya elimu nchini na kuwataka TAMISEMI na Wizara ya Elimu kusimamia vizuri pesa hizo ili kuleta mafanikio zaidi kufikia malengo ya matokeo makubwa sasa.

  Aidha Dk. Likwelile amewataka waajiri wote katika sekta ya elimu kutoa kipaumbele kwa walimu ili waweze kuboresha elimu nchini na kuwataka kupeleka majina na akaunti namba za walimu wote Hazina ili Hazina iweze kuwawekea mishahara yao katika akaunti zao kwa wakati.

  Naye Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Prof. Sifuni Mchome amesema kuwa Wizara ya Elimu kwa sasa imepiga hatua kubwa katika kufanikisha lengo la matokeo makubwa sasa linalolenga kukuza na kuendeleza elimu katika ngazi ya shule za msingi na sekondari hivyo fedha hizo zinatumika kutatua matatizo katika sekta ya elimu ambapo kwa sasa shule nyingi zimeanza kuonesha matokeo mazuri.

  Akitoa mchango wake wakati wa hafla hiyo Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier amesema kuwa Benki ya Dunia imeona kuna umuhimu wa kuisaidia Tanzania katika sekta ya elimu ili kuleta ujuzi na kuvumbua vipaji kwa vijana wadogo watakaosaidia kuleta maendeleo hapo baadae.

  Naye Naibu Katibu Mkuu wa TAMISEMI Dk. Deo Mtasiwa ameahidi kusimamia fedha hizo kwa ufanisi na kuhakikisha kuwa zinawafikia walengwa wote hadi ngazi ya chini waweze kufaidika na pesa hizo.
  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dk. Servacius B. Likwelile akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kusaini mkataba wa kupokea mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya kusaidia sekta ya Elimu, kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier.
  Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Prof. Sifuni Mchome akifafanua jambo wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba wa kupokea mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia kuisaidia sekta ya Elimu nchini, katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dk. Servacius B. Likwelile na kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier.
  Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Dk. Deo Mtasiwa akichangia wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba wa kupokea mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya kusaidia sekta ya Elimu, kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Prof. Sifuni Mchome.
  Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Dk. Deo Mtasiwa (kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Prof. Sifuni Mchome (wapili kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dk. Servacius B. Likwelile (wapili kulia) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier (kulia) wakijadiliana wakati wa kusaini mkataba wa kupokea mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia kuisaidia sekta yaElimu leo jijini Dar es Salaam. Picha na Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikalini - WHVUM

  0 0

  Waziri wa Uwezeshaji katika ofisi ya Waziri Mkuu Mary Nagu akiongea jambo na mshauri wa Tanzania Private Sector Foundation(TPSF) Dk.Donath Olombi (Kulia ) na Meneja Biashara wa M-pesa wa Vodacom Tanzania,Asia Mhina (katikati) kwenye warsha ya kushirikishana uzoefu kuhusiana na kuboresha huduma za Kifedha kwa wafanyabiashara ndogo na za kati uliofanyika kwenye Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam leo na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
  Mkurugenzi mtendaji Mkuu wa Tanzania Private Sector Foundation Godfrey Simbeye wa pili kutoka (Kushoto) Meneja Biashara wa M-pesa wa Vodacom Tanzania Asia Natalia Mhina(kushot) na Mshauri wa mshauri wa Tanzania Private Sector Foundation Dk.Donath Olombi (Kulia) wakimsikiliza jambo Waziri wa Uwezeshaji katika Ofisi ya Waziri Mkuu Mary Nagu, baada ya kuzindua warsha ya kushirikishana uzoefu kuhusu njia za kuboresha huduma za Kifedha kwa wafanyabiashara ndogo na za kati uliofanyika kwenye hotel ya Serena jijini Dar es Salaam leo na kudhamini na Vodacom Tanzania.
  Waziri wa Uwezeshaji katika ofisi ya Waziri Mkuu Mary Nagu, akisalimiana na Meneja Biashara wa M-pesa wa Vodacom Tanzania Asia Mhina,katika warsha ya kushirikishana uzoefu kuhusiana na kuboresha huduma za Kifedha kwa wafanyabiashara ndogo na za kati.Warsha hiyo imefanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.Katikati ni Meneja Uhusianoa wa Umma wa Vodacom Matina Nkurlu.
  Mkurugenzi mtendaji Mkuu wa Tanzania Private Sector Foundation(TPSF) Godfrey Simbeye akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusiana na warsha ya kushirikishana uzoefu kuhusu njia za kuboresha huduma za Kifedha kwa wafanyabiashara ndogo na za kati katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
  Waziri wa Uwezeshaji katika ofisi ya Waziri Mkuu Mary Nagu, akiongea na waandishi wa Habari kuhusiana na warsha ya kushirikishana uzoefu katika kuboresha huduma za Kifedha kwa wafanyabiashara ndogo na za kati ulioandaliwa na Tanzania Private Sector Foundation na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania uliofanyika kwenye hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Uwezeshaji katika ofisi ya Waziri Mkuu Mary Nagu akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Warsha ya kushirikishana uzoefu kuhusu njia za kuboresha huduma za Kifedha kwa wafanya biashara ndogo na za kati ulioandaliwa na Tanzania Private Sector Foundation na kudhaminiwa Vodacom Tanzania.
  Baadhi ya washiriki wakifatili mada wakati wa warsha ya kushirikishana uzoefu katika kuboresha njia za huduma za Kifedha kwa wafanyabiashara ndogo na za kati ulioandaliwa na Tanzania Private Sector Foundation(TPSF)na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.

  0 0

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Stephen Masele (kulia ) akizungumza na balozi wa China nchini Tanzania Dr. LU Youqing (kushoto) aliyemtembelea ofisini kwake leo kwa ajili ya maandalizi ya kongamano la China – Afrika linalotarajiwa kufanyika mkoani Arusha, Tanzania mapema Machi, 2015.
  Balozi wa China nchini Tanzania Dr. LU Youqing (kushoto) akizungumza na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Stephen Masele (kulia) juu ya hatua iliyofikiwa ya maandalizi ya kongamano hilo.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Stephen Masele (kulia ) na Balozi wa China nchini Tanzania Dr. LU Youqing (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kikao hicho.

  0 0

  DIWANI wa Viti Maalum Msasani, Kuluthum Sagamiko ameandaa warsha kwa ajili ya wenyeviti na makatibu wa Umoja wa Wanawake (UWT) wilaya ya Kinondoni kwa ajili ya mafunzo ya kujiimarisha kichama na ujasiriamali kwa wanawake.

  Warsha hiyo ilifanyika Dar es salaam jana, ambapo jumla ya viongozi hao kutoka kwenye kata 34 za wilaya hiyo walishiriki na kuweka mikakati ya pamoja.

  Akifungua warsha hiyo, Naibu Katibu Mkuu Bara, Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Eva Mwingizi, aliwataka kuwa mstari wa mbele na kusimama katika nyanja zote ikiwemo siasa na biashara bila woga.

  Alisema uwiano sawa wa asilimia 50 kwa 50 katika uongozi hauwezi kufikiwa endapo wanawake wenyewe watasita kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali.

  "Nimefurahi leo kuwaona wanawake wamekutana pamoja, kwa sababu warsha kama hizi zinawajengea uwezo,kina mama wanaweza na wakijengewauwezo basi wanafanya vizuri katika nyanja zote.

  "Kina mama ni mtaji mkubwa popote pale, ni tegemeo kwenye maeneo mengi, hawa ni jeshi,ukitaka kufanikisha jambo, na kuwatumia kinamama basi jambo hilo lazima lifanikiwe, kwahiyomafunzo ya kufanya wajitambuezaidi ni muhimukwao,"aliongeza.

  Alisema ingawa UWT ipo kisiasalakini walifikiria kuwainua kina mama kwa kuanzisha kitengo cha miradi, ambapopamoja namambomengine kinawaunganisha na taasisi mbalimbali za mikopo ilikuinua biashara zao.

  Naye muandaaji wa warsha hiyo, Diwani wa Viti Maalum Msasani, Kuluthum Sagamiko,alisema lengo ni kuwajengea uwezo wanawake hao wanaotoka katika kata, kwakuwandiowenye watu .

  "Pia wajitambue nakujipanga nachangamoto hususan cha uchaguzi na maisha kwa ujumla, hasa wakati huukuelekea katikachaguzi za kitaifa,"aliongeza.

  Licha ya kupata mafunzo ya kisiasa,Kuluthum alisema pia kunamkufunzi wa mamboya biashara, ili kuleta msukumozaidi,kwa kuamini kuwa mwanamke mwenye uchumi ananguvu zaidi.

  "Kwenye wilaya yetuyaKinondoni, tumepoteza majimbo mawili na kata 11, kupitia wanawake hawa, wenye nguvu nauelewa itakuwa rahisi kurudisha maeneo tuliyopoteza kwa upinzani,"alisema.
  viongozi hao wakisikiliza watoa mada (hawapo pichani) wakati wa warsha hiyo
  Meza kuu

  0 0

  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr.Seif Rashid(mb), amehudhuria hafla ya utoaji tuzo kwa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Singida.tuzo hiyo inahusiana na mafanikio yaliyokwisha na hospitali hii katika kuinga na kudhibiti maambukizi kutoka kwa magonjwa Kwenda kwa mtoa huduma na vile vile kutoka kwa mtoa huduma Kwenda kwa magonjwa.mradi huu unasimamiwa na wizara ya Afya na ustawi wa Jamii chini ya ufadhili wa mashirika ya kimarekani ambayo ni PEPFAR, JHPIEGHO na CDC. Tuzo hiyo hutolewa kwa hospitali au Kituo cha kutolea huduma za Afya baada ya kuikodi vigezo na kupata alama kuanzia asilimia 80 na kuendelea ya vigezo vinavyotumika katika kutathmini utekelezaji wa programme hiyo.

  0 0


  0 0

  Katibu Mtendaji Katibu Mtendaji wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na masuala ya kilimo (Ansaf), Audax Rukonge akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu uzinduzi wa  Jukwaa la Wadau watakaoangalia mazao ya mikunde na nafaka litakalofanyika Agosti 20 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Masoko wa Taasisi ya Rudi, Sebastian Sambuo na Ofisa Programu wa Women & Youth Development Foundation, Luke Daniel Kifyasi.
  Ofisa Masoko wa Taasisi ya Rudi, Sebastian Sambuo  akizungumza wakati wa mkutano huo.
  Na Clezencia Tryphone

  Waziri Mkuu Pinda, Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Jukwaa la wadau watakaoangalia mazao ya mikunde na nafaka mara baada ya kuvunwa.

  Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mtendaji wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na masuala ya kilimo (Ansaf), Audax Rukonge amesema katika uzinduzi huo utafanyika katika hoteli ya Golden Tulip Agosti 20 na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda atakuwa mgeni rasmi.
  Alisema lengo la kufanya uzinduzi huu ni kutokana na changamoto mbalimbali juu ya mazao hayo, ambazo uwakumba wakulima na wafanyabiashara kwa ujumla.
   
  Miongoni mwa changamoto hizo, ni utuzwaji wa mazao hayo baada ya kuvunwa, hasa kwa wakulima wadogo wadogo na wale wa kati na wafanya biashara huku changamoto nyingine ikiwa ni upotevu wa Mbegu pamoja na matumizi ya tekinolojia ya utunzaji na takwimu.

  “Tunatarajia kufanya uzinduzi wa jukwaa la wadau wanaoangalia mazao ya mikunde na nafaka mara tu baada ya kuvuna, na lengo kubwa ni kuwaamasisha pia watunzaji wa nafaka hizo, ili kuepuka upotevu, na tumefikia hatua hii baada ya kufanya utafiti,”amesema Rukonge.

  Amesema, mara baada ya kufanywa kwa takwimu wamegundua kuwepo kwa upotevu mkubwa wa mbegu za mazao hayo na hiyo ndiyo sababu iliyowafanya kuzindua jukwaa hilo.

  0 0


  0 0

  H.E Tanzania Ambassador to The USA, Ambassador Liberata Mulamula Introducing The Ministers who Participated at The Ministerial Breakfast Meeting Organised By TIC And Attended By The Us Multi National Corporations in Washington DC.
  TIC Executive Director,Juliet Kairuki and The Vice President Of Marriott International Hotels Kathleen Williams During the Ministerial Breakfast Meeting Organised By TIC at The Washington DC.
  TPDC Managing Director James Mwainyekule Speaking to one of Theus Investor Interested In Tanzania's Oil And Gas Sector
  A Session of US Investors Who Attended The Ministerial Breakfast Meeting Organised By TIC at The Grand Hyatt In Washington DC.

  0 0

  Mtaalamu wa kujadili mikataba kutoka World Trade Organization (WTO), Prof. Dickson Yeboah akitoa mada jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa Kimataifa wa kuwajengea uwezo maofisa wa serikali kutoka nchi 15 za Afrika Mashariki, Afrika ya Kati na Afrika Kusini kuhusu uandikaji wa mikataba inayohusu Uwekezaji na Biashara. Mkutano huo umeandaliwa na Chuo Kikuu cha Bagamoyo.
  Baadhi ya washiriki wa mkutano huo.

  Na Happiness Katabazi

  CHUO Kikuu cha Bagamoyo (UB), kimesema kitaendelea kuandaa mafunzo  ya jinsi ya Kutengeneza mikataba na wawekezaji  kwa maofisa wa serikali za nchi zinazoendelea ili serikali hizo ziondokane na tatizo la kuandika mikataba ya uwekezaji ambayo haiziletei faida nchi zao.

  Akizungumza na Katika  Mafunzo yanayoshirikisha wataaluma wa masuala ya Biashara toka nchi 15 yanayofanyika Katika Hotel ya Habour View Dar Es Salaam ambapo Mafunzo hayo yameandaliwa na Chuo Kikuu Cha Bagamoyo na kufadhiliwa na Chuo Kikuu Cha Nordic Africa Institute of the University of Uppsala Cha nchini Sweden, Mkuu wa Shule ya Biashara na Utawala (UB), Dk.Lenny Kasoga Alisema Mafunzo ya wiki mbili yameusisha  maofisa wa juu wa serikali mbalimbali ambao ni wataalamu wa fani ya Biashara toka nchi 15.

  Dk.Kasoga alisema Leo Dunia ipo Karne  ya 21 lakini bado nchi  zinazoendelea ambazo  zimegundulika Kuwa na utajiri  mkubwa  zimejikuta zikiingia mikataba mibovu na wawekezaji KWA Sababu tu nchi hizo Hazina wataaluma serikalini ambao wamebobea Katika kufanya mijadala ya Kibiashara na wawekezaji na jinsi ya kuandika mikataba hiyo.

  "Kwa kukuona tatizo Hilo sisi UB, tumeandaa Mafunzo haya ambayo yamewapa mwanga maofisa Hao waandamizi toka serikali za nchi 15 ambapo Mafunzo tuliyowapatia watayapeleka Katika serikali zao na vyuo vyao ili waweza kuandaa mitaala Katika vyuo vikuu vyao NGazi ya Shahada ya Pili ili watu wasome' Alisema Dk.Kasoga.

  ALizitaja nchi zinazoshiriki Mafunzo ambayo ni ya kwanza kufanyika nchini  ambayo yanatarajiwa Kufungwa Ijumaa ya wiki hii na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk.Shukuru Kawambwa  Ni Mwenyeji Tanzania na Zanzibar, Madagascar,Mozambique, Rwanda,Malawi,Zambia, Burundi, Uganda, Ethiopia ,Kenya, Kongo, Malawi na Lesotho.

  Kwa upande wake Profesa Francis Matambalya toka Chuo Kikuu Cha NAI, Uppsalla nchini Sweed, alisema chuo chao wameamua kufadhili UB iendeshe Mafunzo hayo kwasababu wanaamini UB ninauwezo wa kuendesha Mafunzo na kwamba Tanzania pia ambayo Katika Mafunzo hayo wamewasilisha na maofisa Biashara toka Wizara ya Viwanda na Biashara nayo inamkabili na Changamoto hiyo.

  0 0

   Afisa Mnadhimu namba wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Japhet Lusingu akitoa ufafanuzi wa mada mbalimbali zilizojadiliwa kati ya Jeshi hilo na wadau wa Polisi Jamii Mkoa wa Arusha katika kikao kilichofanyika ukumbi wa Bwalo la Afisa wa Polisi (Police Officers Mess) mwishoni mwa wik
   Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha Mrakibu wa Polisi (SP) Francis Duma akitoa elimu ya Polisi Jamii katika kikao kilichowajumuisha viongozi wa Jeshi la Polisi na Wadau wa Polisi Jamii Mkoa wa Arusha.
    Katibu wa kikao cha Viongozi wa Polisi na Wadau wa Polisi Jamii ambaye pia ni Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Arusha Bw. Adolph Olomi akitoa mwongozo kwa wadau juu ya uendeshaji wa kikao hicho kilichofanyika Ukumbi wa Bwalo la Polisi mwishoni mwa wiki.
   Mdau wa Polisi Jamii ambaye pia nin Mwanasheria wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Bw. Kiomoni Kibamba akisisitiza jambo wakati anachangia mada ya Usalama mkoa wa Arusha katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Bwalo la Polisi mwishoni mwa wiki iliyopita
  Picha ya pamoja kati ya baadhi ya viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha na wadau wa Polisi Jamii mkoani hapa mara baada ya kikao cha kujadili usalama kilichofanyika ukumbi wa Bwalo la Polisi habari.picha na woindeshizza blog

  BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

  0 0

   TUNALETA CAMERA HII  (USED) KWA SPECIAL ORDER KWA YEYOTE ATAKAYEHITAJI KWA BEI YA SH 450,000/- TU. INAKUWA NA LENZI YAKE NA MKOBA. KWA ORDER NA MAWASILIANO ZAIDI WASILIANA KWA NUMBER HIZI 0656564648/0753739163  AMA KWA EMAIL macamaca97@outlook.com  0 0

  WATANZANIA WA NEW JERSEY, NA MAENEO YA KARIBU (NY, CT, MA, PA, MD, DE) Mnakaribishwa wote kwenye Community Barbeque ya Watanzania siku ya Jumamosi, Agosti 23, 2014, kuanzia saa tisa alasiri katika viwanja vya Lincoln Park, West Side Avenue, Jersey City, New Jersey. Lengo letu ni kujumuika pamoja, kufahamiana zaidi na kula nyama. Kufika kwako ndio mafanikio ya jumuiko letu sote. Ahsanteni.


older | 1 | .... | 542 | 543 | (Page 544) | 545 | 546 | .... | 3284 | newer