Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

BRN champions challenged to deliver

0
0
NEW staffs employed to monitor implementation of the Big Results Now (BRN) Programme have been challenged to do away with the tendency of working in business as usual model.

The call was issued yesterday in Dar es Salaam by the Deputy Chief Executive Officer of the President's Delivery Bureau (PDB) which oversees the BRN Programme, Mr. Peniel Lyimo during the opening of the First Annual Strategic BRN Staff Retreat in Dar es Salaam.

The meeting which will include presentations on the one year of implementing the transformation Programme from the PDB CEO, Mr. Omari Issa and case studies on project implementation from Malaysia will also expose the champions to best ways to oversee the BRN.

"BRN has introduced its own way of doing things. Much as we have to abide by the laws and regulation, we also need to introduce a system of working the business unusual way," said Mr. Lyimo insisting, that is the best way to deliver.

He highlighted that one of the challenges in the one year of BRN implementation was the business as usual mind-set to some of the public servants. "This is why we are meeting today to reflect upon how best we, as champions of that change, ought to behave. The changes begins with us," stressed Mr. Lyimo.

PDB was established in July, 2013 to oversee the BRN Programme that seeks to transform the delivery of government projects in the selected National Key Results Areas. The six primary sector under BRN area agriculture, education, transport, energy, water and resources mobilization.

A new sector on strengthening business environment has also been included in the BRN Programme while plans are under way to include health sector.  

MDAU ABUU MAIGE AFUNGA NDOA NA ZAINAB AHMED

0
0
Bwana Harusi Abuu Almas Maige akiwa amepozi na Mkewe,Bi.Zainab Binti Ahmed Lukuta mara baada ya kufunga ndoa yao huko Kigamboni mwishoni mwa wiki. 
 Bwana Harusi akiwa na Wazazi wake Mzee Maige na Mkewe.
 Bwana Harusi Abuu Almas Maige akiwa amepozi na Mkewe,Bi.Zainab Binti Ahmed Lukuta mara baada ya kufunga ndoa yao huko Kigamboni mwishoni mwa wiki,pichani nyuma wakiwa na Wazazi wao katika picha ya pamoja mara baada ya ndoa kufungwa.

Bujora mabingwa Balimi Ngoma Kanda ya Ziwa 2014

0
0
KIKUNDI cha Ngoma za asili cha Bujora cha jijini Mwanza kimefanikiwa kuchukua ubingwa wa fainali za mashindano ya Ngoma za asili kanda ya ziwa mwishoni mwa wiki kwa pointi 87.5 zilizofanyika katika Uwanja wa Mabatini kwa kushirikisha mabingwa wawili kutoa katika mikoa mitano ambayo ni Tabora, Shinyanga, Kagera,Mara na Mwanza.

Kwa ubingwa huo kikundi cha Bujora kilizawadiwa pesa taslimu shilingi 1,100,000/= , kikombe pamoja na medali za dhahabui cha Mwanalyaku ambao walipata pointi .

Nafasi ya Pili katika fainali hizo ilichukuliwa na kikund Mwanalyaku cha jijini Mwanza pia kwa pointi 79.5 na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu shilingi 850,000/=, Nafasi ya tatu ilichukuliwa na kikundi cha Bugoloile cha Kagera kwa pointi 79.3 na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 600,000/=.Nafasi ya nne ilikwenda kwa kikundi cha Mabulo ya Jeshi cha Sinyanga kwa pointi 76.7 na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 500,000/=.

Nafasi ya tano mpaka ya kumi ni kikundi cha Rugu kagera pointi 75.2,Musoma One cha Mara 73.8,Wanunguli Shinyanga pointi 73.1,Magereza Tabora 70.1,Kiwajaki Mara 69.6 na cha mwisho ni kikundi cha Bugobogobo cha Tabora pointi 59.3.

Mgeni rasmi katika fainali hizo alikuwa Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Christopher Fuime ambaye aliishukuru Kampuni ya Bia Tanzania kwa kuzamini mashindano ya ngoma ambayo hufanyika kila mwaka wakati wa mavuno ambapo aliwaomba waendelee kudhamini kwani yanatukumbusha asili yetu tulikotoka na pia zawadi wanazopata zinaongeza kipatao kwa washiriki.

Nae Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager, Edithi Bebwa aliwashukuru washiriki wote kwa kuwa mabingwa wa mkoa yao huko wanakotoka na pia aliwashukuru kwa kushiriki fainali za Kanda na kuwaahidi kuboresha zaidi mashindano mwaka ujao hasa upande wa zawadi.

Edithi alisema sababu msinigi ya kuwepo kwa Mashindano ya Balimi Ngoma za Asili ni kuenzi na kulinda utamaduni wa Kitanzania. Kampuni ya Bia nchini ni sehemu yao ya kurudisha fadhila kwa watumiaji wa Kinywaji cha Balimi Extra Lager pamoja na vinywaji vyote vya Kampuni ya Bia Tanzania(TBL).
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Christopher Fuime(kulia) akimkabidhi kikombe kiongozi wa kikundi cha ngoma cha Bujora mara baada ya kuibuka mabingwa wa Kanda ya Ziwa wa fainali za mashindano ya Ngoma za Asili yalifanyika katika Uwanja wa Mabatini jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wacheza ngoma wa kikundi cha Bujora wakishangilia na kikombe pamoja na pesa taslimu shilingi 1,100,000/= mara baada ya kuibuka mabingwa wa Kanda ya Ziwa wa fainali za mashindano ya Ngoma za Asili yalifanyika katika Uwanja wa Mabatini jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.

Court delivers three rulings on Burundi Journalists Association; creation of Burundi’s National Commission for Lands; and travel ban imposed on Rufyikiri

0
0
East African Court of Justice Arusha, 15 August 2014: The First Instance Division today delivered three rulings in the Application matters, one allowed and other two dismissed.

The First Ruling of the Court

The First Instance Division allowed Civil Society groups and Non- Governmental Organizations operating with and without the borders of the Republic of Burundi to participate in the case filed by Burundi Journalists Association as amicus curiae (Friends of the Court) pursuant to Rule 36 of the East African Court of Justice Rules of procedure. 

Rule 36 provides that “an application for leave to intervene under Article40 of the Treaty and an application for leave to appear as amicus curiae shall be by notice of motion”.

The main case challenges inter-alia Law which governs the Press Sector in Burundi which was amended and in their case that numerous provisions of that law are contrary to the freedoms of expression and of the press within the meaning of Article 6 (d) and 7 (2) of the Treaty for the Establishment of the East African Community.

VIJANA WAZIDI KUJIFUA KWA ROBO FAINALI YA DANCE 100% INAYODHAMINIWA NA VODACOM TANZANIA

0
0
Hassan Tofi mmoja wa washiriki wa Shindano la Dance 100% wa Kundi la Best Boys la Kigamboni jijini Dar es Salaam,akiwaongoza wenzake katika mazoezi yao yanayofanyika katika Viwanja vya Don Bosco Upanga ikiwa ni sehemu ya kujindaa na robo fainali ya shindano hilo itakayofanyika Agosti 23 mwezi huu. Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Washiriki wa shindano la dance 100% wa kundi la Best Boys la Kigamboni jijini Dar es Salaam,wakiwa mazoezini katika viwanja vya Don Bosco Upanga wakijiandaa kwa mchuano wa robo fainali utakaofanyika Agosti 23 mwezi huu. Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
NISIKILIZENI KWA MAKINI:Mshindi wa Dance 100% mwaka 2012 Fred Julius wa kundi la T. Africa la Chang’ombe jijini Dar es Salaam, akiwapa mbinu za kuweza kuibuka washindi vijana wa kundi la Best Boys la Kigamboni jijini Dar es Salaam alipowatembelea kambini kwao Don Bosco Upanga ,walikoweka kambi kwa ajili ya kujiandaa na robo fainali ya shindano hilo litakalofanyika Agosti 23 mwezi huu. Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Baadhi ya washiriki wa shindano la Dance 100% wa kundi la Best Boys la Kigamboni jijini Dar es Salaam, wakiwa katika mazoezi Don Bosco Upanga ambapo wameweka kambi yao kujiandaa na robo fainali ya mashindano hayo yatakayofanyika Agosti 23 mwezi huu. Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu(kulia)akiongea na washiriki wa Dance 100% wa Kundi la Best Boys la Kigamboni jijini Dar es Salaam, wakati alipowatembelea kambini kwao Don Bosco Upanga ,wanakojiandaa na na robo fainali ya mashindano hayo yatakayofanyika Agosti 23 mwezi huu. Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.

UONGOZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA WALIOSOMA KOREA (KAAT) YAFANYA MAZUNGUMZO NA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR

0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (Kushoto) akiwakaribisha viongozi wa KAAT walipokwenda kumtembelea na kufanya nae mazungumzo nyumbani kwake. Katikati ni Rais Mpya wa KAAT, Bw. Stephen Katemba na Kulia ni Bw. Bukheti Juma ambaye ni Makamu wa Rais, KAAT (Zanzibar).
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (Kushoto) akifurahia jambo na viongozi wa KAAT, Bw. Stephen Katemba (Katikati) na Bw. Bukheti Juma (Kulia). Viongozi hao walipokwenda kumtembelea na kufanya nae mazungumzo nyumbani kwake mjini Zanzibar.
 Rais Mpya wa KAAT, Bw. Stephen Katemba (Katikati) akiongea na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (Kushoto) wakati walipokwenda kumtembelea na kufanya nae mazungumzo nyumbani kwake mjini Zanzibar. Kulia ni Bw. Bukheti Juma ambaye ni Makamu wa Rais, KAAT (Zanzibar).
 Bw. Bukheti Juma (Kulia) ambaye ni Makamu wa Rais, KAAT (Zanzibar) akiongea na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (Kushoto) wakati walipokwenda kumtembelea na kufanya nae mazungumzo nyumbani kwake mjini Zanzibar. Katikati ni Rais Mpya wa KAAT, Bw. Stephen Katemba akiwasikiliza.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (Kushoto) akitilia mkazo umuhimu wa jamii kusaidia wazee wasiojiweza, wakati alipofanya mazungumzo na viongozi wa KAAT, Bw. Stephen Katemba (Katikati) na Bw. Bukheti Juma (Kulia). Viongozi hao walipokwenda kumtembelea na kufanya nae mazungumzo nyumbani kwake mjini Zanzibar.
Baadhi ya wanachama wa KAAT wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (Katikati).

NEWS ALERT: Jaji Lewis Makame afariki Dunia

0
0
 Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde,inaeleza kuwa aliewahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini,Jaji Mstaafu Lewis Makame (pichani) amefariki dunia mchana huu katika hopitali ya Hospital ya AMI Trauma Center, Masaki jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu ya maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.

taarifa kamili itakuja baadae.

SEMINA YA WATENDAJI WA BRN YAFUNGULIWA LEO

0
0
Naibu Mtendaji Mkuu, Ofisi ya Rais-Usimamizi wa Utekelezaji wa Miradi (Presidents Delivery Bureau - PDB) inayosimamia Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now! - BRN), Bw. Peniel Lyimo, akifungua semina ya siku nne, ya tathmini ya Utekelezaji wa BRN kwa Mwaka wa kwanza; inayohusisha watendaji kutoka wizara na sekta mbalimbali zinazotekeleza BRN. Semina hiyo imefunguliwa leo Jumatatu jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya washiriki wakifuatilia mada katika semina hiyo ya tathmini inayohusisha watendaji wa BRN iliyofunguliwa jijini Dar es Salaam leo Jumatatu. Semina hiyo inayowakutanisha watendaji wapya wa PDB na BRN pia inahudhuriwa na maofisa wanahohusika na utekelezaji katika ngazi ya Wizara, Taasisi na Mikoa.
Watendaji kutoka Ofisi ya Rais-Usimamizi wa Utekelezaji wa Miradi (PDB) wakijadiliana jambo wakati wa semina ya tathmini inayohusisha watendaji wa BRN iliyofunguliwa jijini Dar es Salaam leo Jumatatu. Kutoka kushoto ni Meneja Mawasiliano na Utetezi, Bw. Hassan Abbasi, Mkurugenzi wa Huduma za Utawala wa PDB, Bw. Maharage Chande na mtaalamu wa PDB kutoka PEMANDU Malaysia, Bw. Marc Shien Loong.
Naibu Mtendaji Mkuu wa PDB, Bw. Peniel Lyimo (kulia) akijadiliana jambo na baadhi ya watendaji wake wanaosimamia sekta ya kilimo katika BRN. Kutoka kushoto ni James Ngwira kutoka PDB, Bw. January Kayumbe Mkuu wa Kitengo cha Utekelezaji wa BRN katika Wizara ya Kilimo na Bw. Henry Kinyua, Mkurugenzi wa Idara ya Kilimo - PDB.

BARAZA LA MADIWANI CHATO LATOA TUZO ZA ELIMU

0
0
Baraza la madiwani la halimashauri ya wilaya ya chato katika kikao chake robo ya nne, limetunuku vyeti, ngao na pesa Taslimu ikiwa ni pongezi kwa shule na kata zilizofanya vizuri katika mtihani wa darasa la saba 2014.

Shule binafsi zilizoongoza ni shule ya msingi Kadama (Kadama English medium), ikifuatiwa na shule ya msingi Emau ( Emau english medium) zote zipo wilayani Chato. Shule za serikali zilizoongoza ni shule ya msingi Magiri iliyoshika nafasi ya kwanza, nafasi ya pili ilimeshikwa na shule ya msingi Minkoto “A”, na kufuatiwa na shule ya msingi Imalabupina iliyoshika nafasi ya tatu, huku shule ya msingi Kamanga iliyopo kata ya Makurugusi ikishika nafasi ya mwisho na kukabidhiwa kinyago.

Kata zilizofanya vizuri katika tuzo hizo ni pamoja na Kasenga, Muganza na Buziku. Katika hatua nyingine Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Chato limewatunuku vyeti vya pongezi wananchi wawili wa kata ya Nyamirembe Ndg. Rajabu Athumani Ndugala na Abdu Ibrahimu Mpisi ambao walifanikisha ujenzi wa madarasa mawili na ofisi ya mwalimu shule ya msingi Nyamirembe B kwa gharama ya Tshs.16,000,000, huku halmashauri ya Wilaya ya chato ikikamilisha madarasa na fisi hizo kwa kwa thamani ya Tshs.15,000,000.

Afisa elimu wa wilaya ya Chato Bw. Angasirini Obedi Kweka akitoa maelezo kwa baraza la Madiwani kabla ya kukabidhi tuzo hizo alisema, Ufauru mzuri wa wanafunzi huchangiwa na uwepo wa walimu wakutosha na wenye kuwajibika, chakula kwa wanafunzi wawapo shuleni na ushirikiano baina ya wanajamii.

Bw. Kweka aliendelea kuelezea changamoto zilizopo mashuleni, hususa ni madawati ambayo yamekuwa changamoto kubwa hasa shule za msingi ambapo alisema idadi ya wanafunzi inazidi kuwa kubwa ukilinganisha na idadi ya madawati yaliyopo , hivyo aliliomba baraza la madiwani kulifanyia kazi tatizo hil.la
bi. Leticia Pastory wa Kadama English medium akipokea ngao na cheti kwa kuwa mshindi wa kwanza katika mtihani wa darasa la saba wilayani Chato.
bw Edward Leornad mratibu wa elimu kata ya Kasenga akipokea cheti cha kata ya kwanza kiwilaya katika mtihani wa darasa la saba 2013.
Bw. Lucas Nicholaus mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Kamanga shule iliyokuwa ya mwisho katika mtihani wa darasa la saba 2013 akipokea kinyago, ambacho hukabidhiwa kwa shule inayofanya vibaya kila mwaka.
baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Chato katika kikao cha robo ya nne.

Serikali yaendelea kusimamia urutubishaji wa vyakula

0
0
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Gaudensia Simwanza(kushoto) akiwaeleza waandishi wa kuhusu udhibiti wa vyakula vilivyoongezwa virutubisho wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) leo Jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa.
Na Frank Mvungi
Serikali imejipanga kufanikisha mpango wa Kitaifa wa urutubishaji vyakula na kusimamia usalama wa vyakula vilivyoongezwa virutubishi kwa lengo la kulinda afya ya walaji.
Hayo yamesemwa na Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) bi Gaudensia Simwanza wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Akifafanua Gaudensia amesema TFDA imeandaa kanuni za uongezaji virutubishi kwenye vyakula (Tanzania food, Drugs and Cosmetics (food fortification) Regulations 2012)
Alisema kuwa hatua nyingine ni kuandaa miongozo ya udhibiti wa ubora na usalama wa vyakula vilivyoongezwa virutubishi ili kuwajengea uwezo wasindikaji kuweza kutekeleza matakwa ya kanuni za uongezaji virutubishi kwenye vyakula.
Akifafanua  Gaudensia alisema kuwa  upo mwongozo wa uhakiki wa ubora na usalama katika usindikaji wa mafuta ya kula yaliyoongezwa virutubishi na mwongozo wa uhakiki wa ubora na usalama katika usindikaji wa unga wa mahindi ulioongezwa virutubishi ili kuliunda afya ya mlaji.
Katika hatua nyingine Gaudensia alibainisha kuwa mwongozo wa usimamizi wa Kanuni za uongezaji virutubishi na mwongozo wa ukaguzi wa vyakula vilivyoongezwa virutubishi ambapo pamoja na mambo mengine mwongozo huu umeainisha taratibu za kufuata katika udhibiti wa vyakula vilivyoongezwa virutubishi muhimu katika chakula.
Vilevile  alisisitiza kuwa utoaji wa mafunzo kwa wadau kuhusu uhakiki na udhibiti wa ubora na usalama wa vyakula vilivyooongezwa virutubishi kama vile wataalamu kutoka katika viwanda ni muhimu kwa vile vinavyoongeza virutubishi kwenye vyakula.
Katika hatua nyingine, jukumu jinguine  la TFDA ni kusambaza vitendea kazi vinavyotumika katika uhakiki na udhibiti wa ubora na usalama wa vyakula na kusimamia utekelezaji wa kanuni za uongezaji wa virutubisho kwenye vyakula.
Aidha, Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inafanya majaribio katika Halmashauri 6 za Mikoa ya Iringa, Kilolo, Iringa Vijijini, Njombe, Arusha, Karatu, Meru na Monduli ambapo kwa upande wa mafuta ya kula majaribio yanafanyika katika Mikoa ya Manyara, Singida na Dodoma.

Vodacom, FSDT yakutanisha wafanyabiashara na watoa huduma sekta ya fedha

0
0
Mkurugenzi wa Huduma za Uanachama wa Tanzania Private Sector Foundation (TPSF)Louis Accaro akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam(hawapo pichani) kuhusiana na warsha ya kuboresha na kupanua huduma za kifedha itakayofanyika kesho/leo Serena Hotel jijini Dar es Salaam, wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Mshauri wa TPSF Dk.Donath Olomi, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia na Kulia ni Mtaalamu wa Biashara wa FSDT Peter Kingu,Warsha hiyo imedhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Mtaalamu wa Biashara wa Financial sector Deepening Trust(FSDT)akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusiana na warsha ya kuboresha na kupanua huduma za kifedha itakayofanyika kesho/leo Serena Hotel Dar es Salaam.Katikati ni Mkurugenzi wa Huduma za Uanachama wa Tanzania Private Sector Foundation (TPSF)Louis Accaro na kushoto ni Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia.Warsha hiyo inadhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Mkurugenzi wa Huduma za Uanachama wa Tanzania Private Sector Foundation (TPSF)Louis Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia, Mshauri wa TPSF Dk.Donath Olomi na Mtaalamu wa Biashara wa FSDT Peter Kingu(kulia) mara baada ya mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam(hawapo pichani) kuhusiana na warsha ya kuboresha na kupanua huduma za kifedha itakayofanyika kesho/leo Serena Hotel Dar es Salaam na kudhamiwa na Vodacom Tanzania.

Zaidi ya wafanyabiashara 100 wadogo na wa kati wanakutanishwa na watoa huduma sekta ya fedha kesho (Jumanne Agosti 19, 2014) jijini Dar es salaam katika semina maalum iliyoandaliwa na Taasisi ya sekta bianfsi Nchini (TPSF) iliyofadhiliwa na Vodacom na FSDT.

Mkutano huo unaofanyika chini ya ufadhili wa Kampuni ya Vodacom na Taasisi ya ukuzaji sekta ya fedha nchini (FSDT) unafanyika katika hoteli ya Serena chini ya Uenyekiti wa Mwenyekiti wa TPSF Dk. Reginald Mengi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Huduma za Uanachama wa TPSF Luis Akaro amesema shabaha ya  semina hiyo ni kujadili vikwazo vya upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wafanyabiashara  na kubadilishana uzoefu.

Tabora,Kagera,Arusha,Kilimanjaro na Ilala zapata Mabingwa Safari Pool

0
0
FAINALI za mashindano ya Safari Pool Taifa yajulikanayo kama “Safari National Pool Competition 2014”, mikoa ya Tabora ,Kagera, Arusha,Kilimanjaro na Mkoa wa kimichezo wa Ilala zimefanikiwa kupata mabingwa wa mikoa zilizomalizika mwishoni mwa wiki katika mikoa hiyo.

Mkoa wa Tabora mabingwa ni Tiptop Pool Klabu,Kagera ni Bilele Pool Klabu,Arusha ni Ngarenaro Pool Klabu,Kilimanjaro ni Mboya Pool Klabu na Mkoa wa Kimichezo wa Ilala ni Mashujaa Pool Klabu ambavyo kwa kutwaa ubingwa huo walizawadiwa pesa taslimu kila klabu Shilingi 800,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha mikoa yao katika fainali za kitaifa zinazotarajiwa kufanyika Mkoani Kilimanjaro.

Upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume, Tabora ni Omary Hassan, Kagera ni Roberth Butasigwa, Arusha ni Richard Daudi, Kilimanjaro ni Baraka Jackson na Ilala ni Yasin Athuman ambao walizawadiwa pesa taslimu Shilingi 400,000/= kila mmoja katika mikoa yao pamoja na tiketi ya kuwakilisha mikoa yao katika fainali za kitaifa Mkoani Kilimanjaro.

Upande wa mchezaji mmoja mmoja Wanawaake, Tabora ni Happiness Morgan, Kagera ni Sajida Saidi, Arusha ni Merry Gumbo, Kilimanjaro ni Reticia Kileo, na Ilala ni Recho Kihupi ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi 300,000/=.

Fainali za kitaifa za 2014 za “Safari National Pool Competion” zinatarajiwa kufanyika Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa kushilikisha Mikoa 17 ambayo ni Tabora,Shinyanga,Dodoma.

 Mbeya,Iringa,Morogoro,Mwanza,Kagera,Manyara,Arusha,Tanga,Pwani,Ilala,Lindi,Temeke,Kinondoni na wenyeji wa mashindano kwa mwaka huu mkoa wa Kilimanjaro.
Diwani wa Kata ya Vingunguti, Asaa Simba(kulia) akimkabidhi nahodha wa klabu ya Mashujaa, Said Miraji(Babu Jee) pesa taslimu Shilingi 800,000/= mara baada ya uibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa yaliyofanyika Ilala Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Katikati ni Katibu wa Chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga.
Wachezaji wa timu ya klabu ya Mashujaa wakishangilia na kitita cha pesa taslimu Shilingi 800,000/= /= mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa yaliyofanyika Ilala Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Kulia ni Diwani wa Kata ya Vingunguti, Asaa Simba na Katibu wa Chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga.

INTRODUCING NEW SONG KITENGE BY WABIBI FT MENSEN SELEKTA

Sporah ku-host Africa Gospel Music Awards jumapili Agosti 24, 2014

0
0
Sporah atakua ana Host Africa Gospel Music Awards jumapili hii ya tarehe 24 mwezi wa nane. Atakua ana HOST hii award na muimbaji maarufu wa nyimbo za injili kutoka Ghana Mr Sonnie Badu.
Sonnie is a multiple award winning Gospel singer, songwriter, philanthropist, producer, TV presenter and author. He is arguably the most successful gospel export to emerge out of Africa in recent years. 
Tunawakaribisha Watanzania woote wanaoishi Europe, wote wanakaribishwa.
Information zaidi ziko kwenye www.africagospelawards.com

BARAZA LA MADIWANI CHATO LATOA TUZO ZA ELIMU

0
0
Baraza la madiwani la halimashauri ya wilaya ya chato katika kikao chake robo ya nne, limetunuku vyeti, ngao na pesa Taslimu ikiwa ni pongezi kwa shule na kata zilizofanya vizuri katika mtihani wa darasa la saba 2014. 
 Shule binafsi zilizoongoza ni shule ya msingi Kadama (Kadama English medium), ikifuatiwa na shule ya msingi Emau ( Emau english medium) zote zipo wilayani Chato. Shule za serikali zilizoongoza ni shule ya msingi Magiri iliyoshika nafasi ya kwanza, nafasi ya pili ilimeshikwa na shule ya msingi Minkoto “A”, na kufuatiwa na shule ya msingi Imalabupina iliyoshika nafasi ya tatu, huku shule ya msingi Kamanga iliyopo kata ya Makurugusi ikishika nafasi ya mwisho na kukabidhiwa kinyago. 
 Kata zilizofanya vizuri katika tuzo hizo ni pamoja na Kasenga, Muganza na Buziku. Katika hatua nyingine Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Chato limewatunuku vyeti vya pongezi wananchi wawili wa kata ya Nyamirembe Ndg. Rajabu Athumani Ndugala na Abdu Ibrahimu Mpisi ambao walifanikisha ujenzi wa madarasa mawili na ofisi ya mwalimu shule ya msingi Nyamirembe B kwa gharama ya Tshs.16,000,000, huku halmashauri ya Wilaya ya chato ikikamilisha madarasa na fisi hizo kwa kwa thamani ya Tshs.15,000,000. 
 Afisa elimu wa wilaya ya Chato Bw. Angasirini Obedi Kweka akitoa maelezo kwa baraza la Madiwani kabla ya kukabidhi tuzo hizo alisema, Ufauru mzuri wa wanafunzi huchangiwa na uwepo wa walimu wakutosha na wenye kuwajibika, chakula kwa wanafunzi wawapo shuleni na ushirikiano baina ya wanajamii. 
 Bw. Kweka aliendelea kuelezea changamoto zilizopo mashuleni, hususa ni madawati ambayo yamekuwa changamoto kubwa hasa shule za msingi ambapo alisema idadi ya wanafunzi inazidi kuwa kubwa ukilinganisha na idadi ya madawati yaliyopo , hivyo aliliomba baraza la madiwani kulifanyia kazi tatizo hil
 Bi. Leticia Pastory  wa Kadama English   medium akipokea  ngao na cheti  kwa  kuwa mshindi wa kwanza katika mtihani wa darasa la saba wilayani Chato.

 Bw. Edward Leornad  mratibu wa elimu kata ya Kasenga   akipokea cheti cha kata ya kwanza kiwilaya katika mtihani wa darasa  la saba 2013

 Bw. Lucas Nicholaus mwalimu mkuu  wa shule ya Msingi Kamanga shule iliyokuwa ya mwisho katika mtihani wa darasa la saba 2013 akipokea kinyago, ambacho hukabidhiwa kwa shule inayofanya vibaya kila mwaka

 Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Chato katika kikao cha robo ya nne 

Sehemu ya wajumbe wa Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Chato katika kikao cha robo ya nne 


ngoma azipendazo ankal

0
0
Ngoma ya "Wahoi" iliyomtoa Malkia wa Mipasho Khadija Omar Kopa enzi hizoo

Mambo yapamba moto kuelekea fainali za Miss Temeke 2014

0
0
 Vimwana wa Miss Temeke 2014 wakiwa kwenye pozi la picha,ikiwa ni sehemu ya maandalizi yao ya kuelekea kwenye kinyang'anyiro chao kitakachofanyika kwenye Ukumbi wa TCC klabu Chang'ombe jini Dar es Salaam Agosti 22,2014.Jumla ya washiriki 17 watapanda jukwaani siku hiyo kuwania taji hilo huku Globu ya Jamii ikimzawadia kitita cha Sh. Mil 1 Mrembo atakaeonekana ana mvuto wa picha (Miss Photogeni 2014).
Wakiwa wamepozi wenyewe.
Watembea kwa mwendo wa madaha mithili ya Twiga mbugani.

BUSINESS SEMINAR

Mazungumzo na Liberatus Mwang'ombe na Solomon Chris baada ya Uchaguzi DMV

0
0
Mubelwa Bandio kati akiwa na aliyekuwa mgombea wa nafasi za Mwenyekiti wa Jumuiya DMV Liberatus Mwang'ombe (L) na mgombea nafasi ya Katibu Msaidizi Solomon Chris (R0 wakati wa mahojiano
Agosti 9, 2014, Jumuiya waTanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia nchini Marekani ilifanya uchaguzi wake mkuu.
Matokeo yake yamekuwa yakipingwa na waliokuwa wagombea wa uchaguzi huo kutokana na sababu mbalimbali.
Wamaketi na Vijimambo Blog na Kwanza Production kueleza sababu hasa za kupinga matokeo hayo siku ya Jumatano ya Agosti 13, 2014.
Karibu uungane nasi kusikia wanachopinga

Mazungumzo na Salma Moshi kuhusu uchaguzi DMV

0
0
 Salma Moshi akizungumza na Mubelwa Bandio kwenye mahojiano haya

Agosti 9, 2014, Jumuiya waTanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia nchini Marekani ilifanya uchaguzi wake mkuu.
Matokeo yake yamekuwa yakipingwa na waliokuwa wagombea wa uchaguzi huo kutokana na sababu mbalimbali.
Mmoja wa wagombea hao, Salma Moshi amaketi nasi kueleza sababu hasa za kupinga matokeo hayo siku ya Jumatano ya Agosti 13, 2014 chini ya utayarishaji wa Vijimambo Blog
Karibu uungane nasi kusikia anachopinga
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images