Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

Southern African Centre for Infectious Disease Surveillance (SACIDS) Summer School announcement


RAIS JK AFUNGUA MKUTANO WA KWANZA WA DIASPORA JIJINI DAR ES SALAAM LEO, WANA-DIASPORA KIBAO WAHUDHURIA

$
0
0
Mratibu wa Diaspora katika Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Suzan Mzee akitoa muhtasari wa mkutano wa Diaspora kabla ya kufunguliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika ukumbi wa Serena Hotel leo Agosti 14, 2014. Anayeangalia mabango ni mjumbe wa kamati ya maandalizi Bw. Constantine Magavilla.
 Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuhutubia na kufungua rasmi Mkutano wa Diaspora.
 Sehemu ya wageni waalikwa akiwemo Balozi Mwanaidi Maajar ambaye anasifika kwa kusimamia mambo ya Diaspora
Mkurugenzi wa Diaspora katika Ofisi ya Rais  Zanzibar Bw. Khamis Mohamed (kushoto)  pamoja na wadau kutoka ughaibuni wakifuatilia
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Mkutano wa Diaspora katika ukumbi wa hoteli ya Serena leo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

NAJUA WAJUA YA CAPTAIN GARDINER G. HABASH NDANI YA MICHUZI TV LEO

Ngoma azipendazo ankal - back by popular demand

$
0
0

Narudi katika safu hii kwa ngoma ya "Kuch Kuch Hota Hai"

Na Sultani Kipingo

Kuch Kuch Hota Hai  (tafsiri yake “kuna vitu hutokea”), ambayo pia ilijulikana kama KKHH, ni filamu ya kuchekesha ya Kihindi iliyotoka India na Uingereza Oktoba 16, 1998. Mwandishi na mwongozaji wake alikuwa Karan Johar na wachezaji wake walikuwa Shahrukh Khan na Kajol, ikiwa ni filamu yao ya nne pamoja. Ilipigwa India, Mauritius na Scotland, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Karan Johar kuongoza filamu, akiwa na lengo la kupiga hatua mpya katika filamu za Kihindi.

Hadithi yake inahusisha pembe tatu za aina mbili za mapenzi. Nusu ya kwanza inahusu marafiki wakiwa chuoni, wakati nusu ingine inaelezea hadithi ya binti wa mjane anayejaribu kuwaunganisha baba yake na rafiki wa zamani.
Filamu hii ilifanikiwa sana India na ulimwenguni kote, ikawa ndiyo filamu iliyoingiza mapato makubwa kwa mwaka huo wa 1998, na pia filamu ya kwanza ya kihindi kuingia katika filamu 10 bora za Uingereza. Wakati muziki wake nao uliuza sana kwa mwaka huo, filamu hii ilijishindia tuzo kibao. Na hadi leo, pamoja kuwa ni ya siku nyingi, bado inatazamwa katika TV za India.



Mwanamuziki kamanda ras makunja afunguka kuhusu mabadiliko ya katiba na pia uraia pacha

$
0
0
Mwanamuziki Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja mtunzi,mwimbaji kiongozi wa bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma africa band aka FFU Ughaibuni yenye makao yake nchini Ujerumani, amefunguka na machache yafuatayo kuhusu mabadiliko ya katiba mpya ya Tanzania na haki za raia wa Tanzania:

Akizungumza kutoka katika makao yake mjini Oldenburg,Ujerumani.
Kamanda Ras Makunja wa kikosi kazi FFU-Ughaibuni alisema
Kuwa: MCHAKATO WA KATIBA MPYA UMEWAFANYA WATANZANIA
WENGI KUSOMA KATIBA YA ZAMANI ! MWANZO WALIKUWA HAWAISOMI NA KULIELWA VEMA ! 
Kwa sasa ! WATANZANIA HATUNA HAJA YA KUOGOPA  MAUMIVU YA 
MABADILIKO YA KATIBA LAZIMA TUENDE KUFUATANA NA WAKATI,
LAZIMA TUWEKE MASALAHI YA TANZANIA NA MTANZANIA KWANZA,

Ras Makunja,alichambua zaidi kwa kusema kuwa watanzania tumekuwa tunatabia za uwoga wa maumivu ya mabadiliko linapokuja swala la kujadili masilahi ya kitaifa na mtanzania,mara nyingine bila ya kujijua tunawapigania
watu ambao sio walengwa katika katiba "Nina maana walengwa wa kunufahika katika katiba hii lazima wawe watanzania wote wa bara na visiwani ambao wanaishi popote pale duniani" bila kujali dini,jinsia au
vyama vyao vya kisiasa.

SWALI: NINI MTAZAMO WAKO NA UNATARAJIA NINI ? KATIKA KATIBA MPYA ?

RAS.MAKUNJA: Mtazamo wa wangu katika kulijadili hili la katiba mpya ningewaomba kwanza wale wabunge walio katika bunge maalumu la katiba
kwamba : WAFANYE KILA HALI KATIKA MJADALA HUU KUPATA KATIBA
YENYE MASILAHI 99% TANZANIA NA MTANZANIA KWANZA

Mfano: Haki za kumiliki Ardhi,tunapoongelea swala la Haki ya mtanzania
basi Ardhi na maslahi yanayo patikana katika Ardhi lazima yamilikiwe na
raia wa Tanzania kwanza,kwa sababu Ardhi ndio msingi au ubongo wa nchi yetu,kwa maana hii asilimia kubwa ya ardhi kama haipo katika miliki ya raia wa Tanzania ,uhuru wetu unatakuwa umepungua maana.
ARDHI NA RAIA WA TANZANIA NDIO MOYO WA TAIFA NA UTAWALA
WA TANZANIA,asilimia 50% ya Adhi ikiwa mikononi mwa watu ambao sio
watanzania,au watu ambao wana offer za kukaa au kufanya jambo katika
ardhi kwa mktaba wa miaka mingi ,wananchi tutajikuta tupo ugenini katika ardhi yetu.HII HAINA MAANA KUWA TUNAWAFUNGIA MILANGO WAWEKEZAJI BALI TUNAWEZA KUINGIA NAO MIKATABA YA MUDA MFUPI .

SWALI:  KUHUSU URAIA PACHA UNALIONAJE HILI?

RAS MAKUNJA: SIO SWALA LA WENGI WAPE, NA WACHACHE WANYIMWE BALI SWALA LA HAKI YA BINADAMU NA URAIA

WATANZANIA LAZIMA TULITAZAME SWALA URAIA PACHA KWA FAIDA YA TANZANIA NA PIA TULICHAMBUE HASARA NA FAIDA ZAKE.
Ras Makunja aliingia kwa kina kwa kusema kuwa kuhusu uraia pacha
walio wengi wanahitaji kuelemishwa faida na hasara zake,pamoja na haki
za msingi kwa watanzania wanaomba hili liwemo katika katiba mpya.
Kwanza tunapolizungumzia hili lazima tujue nini ? maana uraia na nini maana Pasipoti. Historia inaonyesha kuwa matumizi ya PASIPOTI yalianza mapema mwaka 1910 SOVIET UNION (URUSI) ndio walioanzisha kwa nia ya kuwathibiti raia wao katika mfumo wa kikomunisti,baada ya hapo ndipo madola mengine yakafuata; Leo tunapoongelea uraia pacha wengine wanachanganya pasipoti tu za kusafiria na kusahau haki za uraia na binadamu kwa ujumla. Katika kanuni za haki za binadamu hairuhusiwi mtu kunyang'anywa uraia wake, Mimi ningeshauri kuwa katiba mpya iruhusu raia watanzania waweze kuwa na pasipoti zaidi ya tatu,kwa sababu zitawasaidia katika maswala la maendeleo,kama vile uchumi,elimu n.k
MFANO HAI KUNA WATOTO WALIOZALIWA NJE YA NCHI  WAZAZI WAO WOTE NI WATANZANIA LAKINI WANAKOSA HAKI KATIKA NCHI WALIOZALIWA KWA KUWA SI RAIA WA NCHI ILE,NA WANAPOTIMIZA MIAKA 18 WANASHINDWA KUUKANA URAIA WA TANZANIA NA KUOMBA WA NCHI WALIOZALIWA JAPO NCHI WANAYOISHI WANAWEZA KUWA RAIA PACHA.
Watoto hawa wanasulubiwa kwa kuhukumiwa makosa ambayo hawajafanya ! kwani awakuomba wazaliwe ughaibuni, Watanzania katika katiba mpya lazima tuwafikirie watoto hawa wasio na hatia.
Hata katika kanuni za haki za binadamu zinasema kuwa "Si ruhusa kwa binadamu yeyote yule kunyanga'nywa uraia wake.Sasa mtoto wa kitanzania akiwa hana haki ya kuwa mtanzania kwa kuwa kazaliwa nje ya nchi ! hii si haki. 
(B) Muwekezaji wa Kigeni anapokaribishwa Tanzania kwa maneno ya "Jisikie upo Nyumbani ! na mtanzania hakubaliki kwao hapa kidogo pana utata lazima patazamwe upya.

Kwa sasa kuna nchi nyingi duniani ambazo katika katiba zake zinasema kuwa raia wa nchi hizo harusiwi kuny'angwa uraia wake ata kama anaomba uraia wa nchi nyingine,sisi bado tunaogopa kulijadili kwa visingizio vya usalama. Kwa Sasa hatuna adui kama ilivyokuwa zamani tuliofu makaburu n.k Adui wetu wa sasa ni NJAA NA UMASIKINI na Uraia pacha unaweza kuwa silaha kubwa ya kupiga vita adui zetu hawa NJAA,UMASIKINI.

TUNAWEZA KUWEKA MASHARTI KWA WALE WATAKAO KUWA NA URAIA PACHA(Ras Makunja alisisitiza) Mfano: Mtu akiwa na uraia pacha hawezi kugombea nafasi za juu ya uongozi wa taifa kama vile mbunge,diwani, Rais. Au kufanya kazi katika sekta ya usalama na mambo nyeti yanayo husu taifa. huu ni mfano tu. Uraia pacha si swala la kuliogopa bali kuelimishana.

SWALI : MATEGEMEO YAKO KUHUSU KATIBA MPYA?

Ras Makunja: Ni mategemeo yangu kuwa wabunge katika bunge maalumu la katiba wataweka maslahi ya Tanzania na watanzania kwanza na kuondoa itikadi zao za ki-vyama kama tunanyoona sasa. Tunategemea watatuletea rasimu ya mapendekezo ya katiba yenye masilahi ya Taifa na watanzania kwanza si vinginevyo. mwanamuziki huyo alimalizia.

REDIO ZA KIJAMII ZATAKIWA KUTOA ELIMU KWA JAMII

$
0
0
DSC_0323
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, akifafanua jambo kwa Diwani wa kata ya Ololosokwani ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika lisiolo la kiserikali la RAMAT inayomiliki Redio Loliondo FM, Bw. Yannick Ndoinyo (kushoto) wakati wa ziara ya kukagua miradi inayofadhiliwa na UNESCO. Bw. Al Amin aliambatana na wadau wa maendeleo Meneja Mauzo wa Samsung tawi la Tanzania, Bw. Sylvester Nteere (wa pili kushoto) na Mwakilishi wa Ubalozi wa Uswiss nchini, Bw. Erick Kalunga (hayupo pichani). Kulia ni Afisa Miradi kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO, Myoung Su Ko. wengine wakinamama wakikundi cha kimasaia waliofika kupokea ugeni huo.
Na Mwandishi wetu
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni duniani (UNESCO) limezitaka redio za jamii kuendelea kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii hususan ukeketaji kwa akina mama kwa kuelezea athari zitokanazo na ukeketaji ili kuisaidia jamii yenye mila hizo kuachana nazo kabisa.
Hayo yamebainishwa na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph wakati wa ziara ya kutembelea miradi kwenye vijiji vya Ololosokwani wilayani Ngorongoro na kuzitaka redio za kijamii kuwa sehemu ya kutoka elimu ya katiba ili kuiwezesha jamii kufahamu wajibu wao kama raia ili wakati unapofika waweze kufanya maamuzi sahihi ya maendeleo.
Al Amin alisema kuwa vipindi vya elimu ya Afya na masuala ya kijamii yahusuyo serikali na jamii kwa ujumla yanapaswa kupewa kipaumbele na redio hizi katika masuala ya huduma za kijamii hususan ndoa za utotoni, ukeketaji na ajira za utotoni ili ziweze kukomeshwa katika jamii kwani zinarudisha maendeleo ya mtoto hasa wa kike.
DSC_0353
Sehemu maalum ya anayotumia mtoa huduma wa maktaba hiyo inayofadhiliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ambapo kutokana na shida ya umeme katika eneo hilo Kompyuta hiyo inatumia umeme wa jua (solar).
“Kwa sasa hapa nchini kumekuwa na mjadala wa Katiba Mpya mchakato unaoendeshwa na Bunge la Katiba linaloendelea na vikao vyake mjini Dodoma.  Wananchi wana haki ya kujua kila kinachoendelea, kushiriki katika mijadala mbalimbali itakayosaidia kupanua uelewa wao ili mwisho wa siku wanajamii waweze kuwa na maamuzi sahihi na hilo ndio lengo la redio” alisema Al Amin.
Alisema kuwa japo matangazo yamekuwa ya muda mfupi redio Loliondo imekuwa faraja na imetoa mchango mkubwa katika kusaidia jamii kupata uelewa kwenye masuala mbali mbali ya kijamii hususan wizi wa mifugo na utunzaji wa mazingira ya kiikolojia kwenye maeneo husika kwenye  uwanda wa eneo la pori tengefu la Loliondo.
Nae Mkurugenzi wa RAMAT  Yannick Ikayo ambayo inaendesha mradi  wa redio ya kijamii ya Loliondo FM alisema kuwa redio hiyo imekuwa mkombozi kwa kutoa elimu kwa jamii na imesaidia kuongeza uelewa na madhara mbali mbali kwenye masuala ya kijamii hususan ukeketaji na utunzaji wa mazingira ya kijamii.
DSC_0300
Jengo la Maktaba inayofadhiliwa na UNESCO iliyopo kwenye kijiji cha  Ololosokwani wilayani Ngorongoro kwa uangalizi wa Shirika lisiolo la kiserikali la RAMAT.
Loliondo FM Redio ilianzishwa mwaka Oktoba 2013 pamoja na Maktaba na Ujenzi wa Kituo cha Utamaduni ambavyo lengo ni kusogeza elimu kwa jamii ya kifugaji na kupata uelewa wa masuala mbali mbali yanayowazunguka ikiwemo utunzaji wa mazingira.
“Migogoro ya kijamii imekuwa ikipatiwa ufumbuzi hali inayoifanya jamii ya kifugaji kufaidika na redio hii kwani imekuwa na msaada mkubwa kwa jamii yetu na wilaya kwa ujumla hivyo tunaiomba jamii kuipa ushirikiano na kuamini kuwa redio hiyo ni mkombozi wao na kiunganishi kati yao na watawala”, amehitimisha Ikayo.
Wilaya ya Ngorongoro imeonekana kuwa na changamoto katika elimu hasa vijana wa kike kuacha masomo kwa ajili ya kuolewa na wengine kukimbia kukeketwa hali inayohitaji serikali kutoa elimu kubwa kwa jamii ya kifugaji kuachana na mila potofu ikiwemo ukeketaji ulioshamiri.
Wanahabari walitembelea wilayani humo waliwashudiwa wasichana kutoka kabila la kifugaji wakiwa tayari wamekeketwa kwa kuvalishwa mavazi maalum yanaonyesha kutoka kwenye tohara huku wakimshuhudia msichana aliyeshindwa kwenda kujiunga na kidato cha kwanza akiuza mkaa kwa kisingizio cha kukosa ada.
DSC_0283
Mkurugenzi wa Shirika lisiolo la kiserikali la RAMAT inayomiliki Redio Loliondo FM, Bw. Yannick Ndoinyo  (wa pili kushoto) akielezea maendeleo ya miradi mbalimbali inayosimamiwa na Shirika lake ikiwa chini ya ufadhili wa UNESCO kwa ugeni ulioambatana na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (katikati) wakati wa ziara ya kukagua miradi hiyo.
DSC_0959
Baadhi watoto wa jamii za kifugaji wa kijiji cha Ololosokwani ambao wanastahili kupata elimu ya awali lakini wazazi huwaamuru kwenda kuchunga mifugo kama walivyokutwa na mpiga picha wetu kwenye maeneo ya kijiji hicho.

SWAHILI FESTIVAL Community Picnic 2014

Masele aeleza umuhimu wa sayansi Afrika, ataka vijana kushirikishwa katika maamuzi

$
0
0
Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam 
Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Stephen Masele amesema kuwa bara la Afrika linahitaji taaluma ya sayansi kutokana na umuhimu wake kwa maendeleo na ukuaji wa uchumi. Masele ameyasema hayo jijini Dare es Salaam wakati akifunga Mkutano wa Tatu wa Vijana Wanasayansi Duniani (YES), na kuongeza kuwa, Afrika inahitaji sayansi kwa ajili ya kufanya ugunduzi na tafiti ambazo zitachangia katika kuchochea maendeleo barani Afrika. 
Aliongeza kuwa, kutokana na umuhimu huo, Wizara ya Nishati na Madini imedhamiria kuwekeza kwa vijana katika tasnia ya sayansi ikiwemo kuhamasisha Vyuo Vikuu nchini, kuanzisha masomo ya sayansi hususan katika sekta ndogo ya gesi na mafuta jambo ambalo litawezesha kuzalisha wataalam wengi zaidi watakaosaidia kuendeleza taaluma hiyo na rasilimali zilizopo nchini. 
Kutokana na umuhimu huo, aliutaka Mtandao wa Vijana Wanasayansi Duniani (YES), kuhakakikisha unasaidia kuwezesha vijana kuona umuhimu wa kuingia katika taaluma ya sayansi hususan jiolojia ili kuwezesha bara la Afrika kuwa na wataalamu wengi watakaosaidia kuharakisha maendeleo kupitia rasilimali asilia.
 “Mtandao wa vijana mna jukumu la kuchochea taaluma ya sayansi kwa vijana. Afrika inahitaji wanasayansi wakutosha, kwa kuwa, uwepo wao utasaidia kuchochea ukuaji wa viwanda na teknolojia barani Afrika,” alisisitiza Masele. 
Aidha, alieleza kuwa, Afrika inahitaji wataalamu wanasayansi hivyo, alitoa wito kwa kuwashirikisha vijana katika masuala ya kitaaluma ikiwemo kufanya maamuzi.
“Nikiwa kiongozi kijana, nawataka vijana kuona umuhimu wa taaluma hii, hivyo, nawatanguliza ninyi katika hili, nendeni mkawafundishe na kuwahamasisha wenzenu waone umuhimu wa sayansi kwa dunia na kwa Afrika,”alibainisha Masele. 
Aidha, aliongeza kuwa, kama kiongozi kijana, atatumia nafasi yake, kusaidia uwepo wa sera nzuri ambazo zitahamasisha ukuaji wa taaluma ya sayansi na kuwezesha vijana kisayansi. 
Kwa upande wake, Rais wa Vijana Wanasayansi Duniani, Meng Wang alieleza kuwa, mkutano huo wa tatu umeacha historia kwa Tanzania na Afrika kutokana na kupata nafasi ya kukutana, kujadili na wanasayansi wakubwa waliobobea katika masuala ya Jiolojia Afrika na Duniani jambo ambalo litasaidia kuchochea ari ya vijana kuendeleza taaluma hiyo ikiwa ni pamoja na kuhamasisha vijana wengi zaidi kuingia katika sekta hiyo.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Mhe. Stephen Masele akizungumza wakati akifunga Mkutano wa Tatu wa Vijana Wanasayansi Duniani, jijiji Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Mhe. mStephen Masele akimpa zawadi ya kinyago iliyotolewa na mtandao wa Vijana Wanasayansi Duniani (YES), Rais wa Wajilojia barani Afrika Profesa Aberra Mogessie.

 Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Mhe Stephen Masele, katika picha ya pamoja na baadhi  ya Wanasayansi Vijana Duniani waliohudhuria mkutano tatu nchini Tanzania. Wengine katika picha waliokaa kutoka kushoto ni Mtendaji Mkuu Wakala wa Jiolojia Tanzania, Profesa   Abdulkarim Mruma, Rais wa Wajilojia Barani Afrika Profesa Aberra Mogessie, Rais wa  Vijana Wanasayansi Duniani Meng Wang na Mwenyekiti wa Vijana Wanasayansi, Tanzania Steven Nyagonda.


Nimezawadiwa Kitabu: "Picturing Hemingway's Michigan"

$
0
0

Na Profesa Mbele



Leo nimepata zawadi ya kitabu, Picturing Hemingway's Michigankilichotungwa na Michael R. Federspiel. Kinahusu sehemu ya kaskazini ya jimbo la Michigan, ambapo familia ya Ernest Hemingway ilikuwa inakwenda kwa mapumziko. 

Kitabu kina picha na maelezo kuhusu sehemu hiyo, ambapo Hemingway alitembelea tena na tena wakati wa utoto na ujana wake. Hapa ni chimbuko la matukio ya riwaya ya mwanzo ya Hemingway,The Torrents of Spring na hadithi zake ziitwazo Nick Adams Stories. 







Nimeletewa kitabu hiki na Bwana David Cooper wa Ohio na mwanae Clay ambaye ni mwanafunzi wangu aliyekuja Tanzania mwezi Januari, 2013 katika kozi yangu ya "Hemingway in East Africa."

Baba huyu ndiye aliyetupeleka Montana kwa ndege yake mwaka jana,kuonana na Mzee Patrick Hemingway. Hapa kushoto ni picha tuliyopiga mjini Lakeville, Minnesota, kabla ya kuruka kwenda Montana. Bwana Cooper anaonekana kulia kabisa, halafu anafuata mwanae, halafu mwanafunzi wangu mwingine aliyekuwemo katika kozi ya "Hemingway in East Africa," na mimi naonekana kushoto kabisa.




Mwanafunzi aliyeniletea kitabu anaonekana nami pichani hapa kushoto, tukiwa kwenye mpaka baina ya hifadhi za Ngorongoro na Serengeti.

Nilipokipata kitabu hiki, yapata saa saba mchana, nilijawa na furaha, nikaanza kukisoma mara, lakini nikaona nipige kwanza simu kwa walioniletea. Nilimpata Bwana Cooper, nikamshukuru sana. Ameniambia kuwa yeye na mwanae walikiona kitabu hiki katika duka kule sehemu ya Michigan Kaskazini, wakaniwazia. Baada ya maongezi nimeendelea kukisoma, nikamaliza baada ya masaa mawili hivi.. 



Wameninunulia nakala yenye sahihi ya mwandishi, kama inavyoonekana hapa kushoto. (Ninaposema hivi, mawazo yangu yameshakwenda kwenye mazungumzo baina yangu na Ndugu Christian Bwaya kuhusu suala hili la kusainiwa vitabu).

Nilifahamu kuwa sehemu hii ya Michigan Kaskazini ni muhimu katika utoto na ujana wa Hemingway, lakini kitabu hiki kimenifungua macho zaidi kwa kuonyesha sehemu mbali kwa picha na maelezo. Picha nyingi ni za mtoto Hemingway na watoto wengine katika familia yao, picha za wanaukoo, na sehemu mbali mbali. Nyingi katika ya picha hizo sikuwa nimeziona kabla. Kwa yote hayo, nimefurahi sana.


Wachina waonesha nia kuwekeza sekta ya madini, wakutana na Muhongo, Maswi, muhongo asisitiza hakuna kusafirisha madini ghafi

$
0
0
Nuru Mwasampeta na 
Veronica Simba, Dar es Salaam 
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema Wizara yake imejipanga kuhakikisha inajengwa mitambo ya uchakataji madini (Mineral Processing Plants) hapa nchini ili kuondokana na utaratibu wa kusafirisha madini ghafi nje ya nchi na badala yake zisafirishwe bidhaa zitokanazo na madini husika ili kuongeza thamani na hivyo kukuza pato la nchi. 
 Aliyasema hayo  alipokutana na kuzungumza na Wawekezaji wa Kampuni ya Chinalco ya nchini China waliokuja nchini kwa lengo la kujadiliana na Viongozi Waandamizi wa Wizara kuhusu fursa za uwekezaji hususan katika sekta ya madini. 
“Tunahitaji kuwa na mitambo ya uchakataji madini hapa nchini hivyo nawashauri katika uwekezaji wenu mfikirie suala la kujenga mtambo husika kwani hatutaki kusafirisha madini ghafi nje ya nchi,” alisisitiza Profesa Muhongo.
 Katika mazungumzo hayo, Waziri Muhongo aliwashauri wawekezaji hao ambao walioambatana na Balozi wa China nchini, Mhe. Lu Youqing kuhusu fursa muhimu za uwekezaji katika sekta ya madini hapa nchini kuwa ni uwekezaji katika madini yaliyo katika kundi adimu (Rare Earth Elements), madini ya Shaba (Copper) pamoja na madini ya Dhahabu. 
Aliwashauri wawekezaji hao kukutana na Wataalamu kutoka Shirika la Madini la Taifa (Stamico) ambalo limepewa dhamana ya kusimamia maeneo yote ya uwekezaji katika sekta ya madini kwa niaba ya Serikali, ili kujadiliana kuhusu uwezekano wa kuingia ubia katika uwekezaji husika ikiwa ni pamoja na kupata maelezo ya kina kuhusiana na uwekezaji katika sekta ya madini. 
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi aliwaeleza wawekezaji hao kuwa Tanzania inajulikana vizuri kwa kuwa na mazingira mazuri ya kijiolojia yanayofaa kwa uwekezaji hususan kwa madini kama dhahabu, vito, shaba, nickel na cobalt na kwamba aina ya miamba inayopatikana nchini inaruhusu madini ya aina nyingi kupatikana akitolea mfano Tanzanite ambayo inapatikana Tanzania pekee. 
 Aidha, aliongeza kuwa Tanzania inayo sera nzuri ya madini, utawala bora, hali nzuri ya kisiasa (political stability) pamoja na miundombinu bora, ambazo ni miongoni mwa sababu za msingi zinazovutia uwekezaji nchini. Naye Kamishna wa Madini, Mhandisi Paul Masanja aliwakaribisha wawekezaji wa Kampuni ya Chinalco kuja kuwekeza nchini na aliahidi kuwapa msaada utakaohitajika ili kufanikisha azma yao hiyo ikiwa ni pamoja na kuwapa leseni ya kutafuta au kuchimba madini kwa wakati. 
Awali, Mwenyekiti wa Kampuni ya Chinalco, Bw. Xiong Weiping akiinadi Kampuni yake kwa Viongozi wa Wizara alieleza kuwa, Kampuni hiyo ni mali ya Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na inasimamiwa na Serikali Kuu na kwamba inajihusisha na masuala ya maendeleo ya rasilimali za madini, uchakataji wa madini ghafi na masuala ya kiufundi (technical & engineering services). 
Alisema mkakati wa kampuni hiyo ni kuendelea kupanua shughuli za uzalishaji wa madini ya Aluminum, Shaba, Rare Earth Element na uongezaji thamani madini. Ziara ya Kampuni hiyo nchini imekuja kufuatia ziara zilizofanywa awali nchini China kwa nyakati tofauti na Mhe. Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana katika Makao Makuu ya kampuni hiyo mapema mwaka jana na kuuomba uongozi wa kampuni hiyo kupanua mipaka ya biashara hadi Tanzania.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akiongea na Wawekezaji wa Kampuni ya Chinalco ya nchini China waliokuja nchini kwa lengo la kujadiliana na Viongozi Waandamizi wa Wizara kuhusu fursa za uwekezaji hususan katika sekta ya madini. 
Wawekezaji wa Kampuni ya Chinalco ya nchini China wakiongea na Waziri Muhongo
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi katika picha na waekezaji hao pamoja na maofisa wa wizara

WASANII WATUA BUKOBA TAYARI KWA UFUNGUZI WA FIESTA 2014 LEO UWANJA WA KAITABA

$
0
0

Msanii OMMY DIMPOZ na wenzake wakishuka kwenye Ndege aina ya Precision leo asubuhi kwenye Uwanja wa Ndege Mjini Bukoba tayari kwa kukamua vilivyo katika mwendelezo wa Msimu wa Dhahabu na Serengeti Fiesta, Tamasha linalotarajiwa kufanyika leo Ijumaa kwenye uwanja wa Kaitaba hapa Bukoba.
Wasanii hao pamoja na watangazaji na wafanyakazi wengine wameingiatayari Bukoba wakitokea jijini Mwanza. Picha na Faustine Ruta wa bukobasports.com
Wasanii wakishuka kwenye Ndege tayari kwa Fiesta kesho Ijumaa.
Chistian Bella huyoo langoni mwa pipa.

INTRODUCING NEW SONG MAUMIVU -BOB JUNIOR AND ROMA

JARIDA LA NISHATI NA MADINI TOLEO LA 29

Klabu 12 za soka za maveterani kupamba Tamasha la Miaka 16 ya Home Gym

$
0
0
KLABU 12 za timu za soka za maveterani zinazooundwa na nyota wa zamani wa kandanda nchini zinatarajiwa kuchuana katika michezo maalum ya Tamasha la Miaka 16 ya Home Gym, itakayofanyika Septemba 6 kwenye uwanja wa Mwenge, Dar es Salaam.

Aidha zaidi ya klabu 30 za Jogging nazo zinatarajiwa kupamba tamasha hilo ambalo litahusisha pia michezo mbalimbali ikiwamo ya netiboli, kuvuta kamba, kukimbia kwenye magunia na kukimbiza kuku.

Kwa mujibu wa mratibu wa tamasha hilo, Andrew Mangomango, klabu za maveterani zilizothibitisha kushiriki tamasha hilo ambalo litapambwa na burudani ya muziki na shoo ya watunisha misuli, wanyanyua vitu vizito, ngumi na karateka ni Mbagala Veterani, Boko, 501, Break Point, Survey, Mwenge na Msasani.

Mangomango alizitaja nyingine kuwa ni Biafra Veterani, Meeda, Mikocheni, Mbezi, Mabenzi, Segerea na Ukonga Veterani ambazo zinaundwa na nyota wa zamani wa kandanda waliowahi kutamba na timu kama za Simba, Yanga na Taifa Stars.

Juu ya klabu za Jogging mratibu huyo alizitaja kuwa ni pamoja na Temeke Jogging, Mwananyamala, Kingungi, Amani, Magenge, Makuka, 501, Ndiyo Sisi, Wastaarab, Makutanom, Pasada, FBI, Kongowe, Oysterbay Police, Zakheem, Kwa Nyoka, Kawe Beach, Satojio, Kawe Mkwamani na nyingine.

Mangomango aliongeza kuwa baada ya michezo yote wanamichezo washiriki watajumuika pamoja kuwatembelea yatima wanaolelewa kituo cha Chakuhama kwa ajili ya kuwapeleka misaada mbalimbali.

"Ni tamasha ambalo litaambatana na michezo mbalimbali kama ya kuvuta kamba, kukimbiza kuku, kukimbia kwenye magunia, na shoo za watunisha misuli, wanamieleka, mabondia na karateka kisha kwenda kutembelea yatima," alisema.

Mangomango alisema mgeni rasmi wa shughuli zote hizo anatarajiwa kuwa Mkuu wa Kikosi cha Jeshi cha 501, J.B Kapumbe.

Hii ni mara ya pili kwa tamasha hilo kufanyika mwaja jana lilifanyika wakati Home Gym ikiadhimisha miaka 15 tangu kuasisiwa kwake ambapo shughuli zake kuu ni kufanyisha mazoezi na kutoa ushauri juu ya afya ya mwili.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI UTOAJI TUZO WA WANASAYANSI WACHANGA WA TANZANIA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya utoaji Tuzo kwa Wanasayansi wachanga kutoka shule mbalimbali za Sekondari za Tanzania, iliyofanyika jana Agosti 13, 2014 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ilongero, John Andrea (wa pili kulia) na Thobias Clement, wakati wakimuelezea jinsi walivyoweza kufanya utafiti na kugundua matumizi ya Kinyesi cha wanyama kuzalisha Umeme, wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wanasayansi wachanga, yaliyofanyika jana Agosti 13, 2014 sambamba na utoaji tuzo za washindi wa maonesho hayo, katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Lumumba ya mjini Zanzibar, Dhariha Amour (kulia) na Salma Khalfan (wa pili kulia) wakati wakimuelezea jinsi walivyoweza kufanya utafiti wa kutumia Karafuu na Limao kutengeneza dawa ya kufukuza Inzi , wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wanasayansi wachanga, yaliyofanyika jana Agosti 13, 2014 sambamba na utoaji tuzo za washindi wa maonesho hayo, katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwakabidhi Tuzo washindi wa jumla wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Lumumba ya mjini Zanzibar, Dhariha Amour (wa pili kushoto) na Salma Khalfan (wa tatu kulia) baada ya kutangazwa kuwa washindi wa jumla katika maonesho ya Wanasayansi wachanga kwa kufanya utafiti wa kutumia Karafuu na Limao kutengeneza dawa ya kufukuza Inzi , wakati wa halfa ya utoaji Tuzo hizo wa wanasayansi wachanga iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam jana Agosti 13, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia jambo baada ya kuwakabidhi Tuzo washindi wa jumla wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Lumumba ya mjini Zanzibar, Dhariha Amour (wa pili kushoto) na Salma Khalfan (wa tatu kulia) baada ya kutangazwa kuwa washindi wa jumla katika maonesho ya Wanasayansi wachanga kwa kufanya utafiti wa kutumia Karafuu na Limao kutengeneza dawa ya kufukuza Inzi , wakati wa halfa ya utoaji Tuzo hizo wa wanasayansi wachanga iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam jana Agosti 13, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na baadhi ya viongozi kushuhudia zoezi la utoaji tuzo za wanasayansi Wachanga lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jana . P_icha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea mabanda ya maonesho.

18 Tanzanian Students to Participate in Youth Exchange and Study (YES) Program

$
0
0
United States Ambassador Mark Childress met with eighteen secondary school students and four coordinators of The Kennedy-Lugar Youth Exchange and Study (YES) program in Tanzania. The students (15-17 years of age) from Zanzibar and the mainland have been selected to live and study in the United States for up to a full academic year under the YES program.

Among these students 11 are from Zanzibar and 7 from three regions in Mainland Tanzania, including Kilimanjaro, Tanga and Coastal regions. During the program, students will live with host families, attend high school, engage in activities to learn about American society, acquire leadership skills and help educate Americans about their country and culture.

The Kennedy Lugar Youth Exchange and Study (YES) Program was created in 2003 by the U.S. Department of State’s Bureau of Education and Cultural Affairs as a way to build bridges between citizens of the U.S. and countries around the world. The YES program was launched in Tanzania in 2006 and to date 127 Tanzanian students have participated in this program. (Photo courtesy of the U.S. embassy).

SERIKALI YAKANUSHA KUWEPO KWA UGONJWA WA EBOLA NCHINI

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Shaaban Mwinjake (kushoto), akikanusha kuwepo kwa ugonjwa huo kama ilivyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari.Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Dharura na Maafa wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Elias Kwesi.
Mkurugenzi Msaidizi wa Dharura na Maafa wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Elias Kwesi, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati wakikanusha kuwepo kwa ugonjwa wa Ebola nchini. 
Mkurugenzi Mkuu wa Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Suleiman Said Suleiman akizungumza namna TAA ilivyojipanga kuhakikisha hakuna msafiri kupitia viwanja vya ndege mwenye ugonjwa huo atakayeingia nchini bila ya kugundulika.
Msaidizi wa Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Asha Omar akielezea namna Uhamiaji walivyojipanga kuhakikisha inawatambua wageni wanaoingia nchini hasa wale wanaotoka nchi zilizoathiriwa na ugonjwa huo.
Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya na Ubora, Dk.Fausta Mosha (kulia), akitoa ufafanuzi wa kimaabara kuhusu ugonjwa huo.
Maofisa wa JNIA wakiwa kwenye mkutano huo.
Maofisa kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Ofisa Afya Mfawidhi wa JNIA, George Ndaki, Mkurugenzi Msaidi wa Ufuatiliaji wa Ugonjwa, Janeth Nghambi, Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya na Ubora, Dk.Fausta Mosha na Mkurugenzi Msaidizi Afya na Usafi wa Mazingira, Elias Chinamo.
Wanahabari na wadau wengine kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Uwanja wa Ndege wakiwa kwenye mkutano huo.

SHUKRANI KWA WALIOSHIRIKI KUMUUGUZA NA HATA MSIBA WA MPENDWA WETU HAPPY-SIANA APPIA KIRENGA

$
0
0
Happy-Siana Appia Kirenga

19.12.1966 - 5.07.2014


Familia ya Marehemu Mzee Appia Thomas Kirenga wa Machame Kisiki Moshi inayo heshima kubwa kutoa shukrani za dhati kabisa kwa ndugu, jamaa na marafiki ambao walishiriki kwa namna moja ama nyingine kufanikisha msiba, mazishi na hatimaye matanga ya mtoto/Dada yao mpendwa, Happy-Siana Appia Kirenga aliyefariki dunia usiku wa  Jumamosi  ya July 5 kwenye Hospitali ya Taifa  ya Muhimbili na kuzikwa jirani na alipopumzishwa baba yake mzazi, nyumbani, Alhamisi ya July 10, 2014.


Kwa vile walivyotuunga mkono na kutufariji wakati wa kipindi hiki kigumu cha msiba huu mkubwa ni wengi na ni vigumu kuwataja wote kwa majina, Familia, inapenda kwa heshima na taadhima nyingi kutoa shukrani za jumla ikiwaomba wote mkubali kuzipokea kwa moyo ule ule kama mlivyotuunga mkono. Mmetufariji sana, mmekesha nasi, mmeshinda nasi, nyote mmekuwa kimbilio salama kwetu wakati wa kipindi hiki kigumu. 


Mmeonesha upendo wa kweli kweli kwetu kama Familia na kwa mwanetu dada yetu ambaye angerejea kwenye uzima tena, naye bila shaka yoyote angetoa shukrani za dhati ya moyo wake.


                        Hata hivyo, tunapenda kutoa shukurani kwa makundi machache ya marafiki ambao mchango wao utabakia kwenye nyoyo za wazazi na familia yetu  tukianza na majirani na marafiki wa karibu wa Familia walioko Dar es Salaam, Moshi, Arusha, Morogoro, Dodoma, Manyara, Kagera, Mbeya na kwingineko Tanzania, Kenya na nje ya Afrika Mashariki, ambao michango yao kamwe haitasahaulika.


Familia pia inapenda kuwashukuru wanajumuia wa Sayuni Mtaa wa Neema Usharika wa Mbezi Makabe Dar Es Salaam, Uongozi na Washarika wa Makongo Juu Dar es Salaam, uongozi na Washarika wa Kalali Machame Moshi na Watumishi Wengine wa Mungu kutoka sharika mbalimbali wakiongozwa na Askofu Mstaafu Dk Erasto, N. Kweka  kwa huduma kubwa za kiroho wakati wa msiba huo mkubwa uliotufika.


Familia vile vile inapenda kutoa shukrani za dhati kabisa kwa Dr Ayoub Pamba, na kwa Wauguzi na Madaktari wa Hospitali za Tumbi Kibaha na Muhimbili Dar es Salaam kwa juhudi zao za dhati za kutaka kuokoa maisha ya Dada yetu


Aidha, tunatoa shukrani kwa wafanyakazi na uongozi wa Super Sky Aviation,  Regional Air Limited, Wafanyakazi marubani wakiongozwa na Kapten Tatiya Tukero Naikuni, na mfanyakazi mmoja mmoja kwa jumla michango yenu, ilitufariji na tutaendelea kukumbuka ukarimu wenu daima. 


            Vile vile, Familia inawashukuru sana wanakijiji cha Wari, Kata ya Machame, Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, kwa kuupokea vizuri na kuushughulikia kwa heshima zote msiba wa mtoto wao Happy-Siana Appia Kirenga.



Mwisho Tunawashukuru nyote mlioweza kufika nyumbani Machame Kisiki kumhifadhi Dada Happy.  Hatuna cha kuwalipa, Mungu atawalipa.



“Mathayo 5: 8 :- Heri wenye moyo safi;  Maana  hao watamwona Bwana”

RAIS KIKWETE AWAAPISHA MAJAJI WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA WAPYA 20 IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete,  Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda,  Waziri wa Sheria na Katiba Dkt Asha-Rose Migiro, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu,  Katibu Mkuu Kiongozi  Balozi Ombeni Sefue, Mwanasheria Mkuu Jaji  Frederick Werema, Mtendaji Mkuu wa Mahakama Mhe Hussein kattanga  katika picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama kuu ya Tanzania baada ya kuapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu pamoja na  Majaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania wapya
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu pamoja na  Majaji wa Mahakama ya Kuu Tanzania na Majaji  wapya
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu pamoja na  majaji wapya 
  Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu na Jaji Kiongozi   Shaban Ally Lila wakiwa na Majaji wapya 
 Rais Kikwete na Waziri wa Sheria na Katiba Dkt Asha Rose Migiro wakiwa wa wanachama wa Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania wanawake wapya
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu na Jaji Kiongozi   Shaban Ally Lila wakiwa katika pic ha ya jumla na Majaji wapya na wa zamani. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Mh. Lowassa atoa pole msikiti wa Mtambani Kinondoni jijini Dar leo

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipatiwa maelezo na Imam wa Msikiti wa Mtambani,Sheikh Suleiman (mwenye kanzu nyeupe) ya namna moto ulivyoteketeza sehemu ya jengo la shule ya Seminari ya Kiislam ya Mivumoni katika Msikiti wa Mtambani Kinondoni jijini Dar es salaam,wakati alipotembele kuijionea hali hiyo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akitoka kuangalia uharibifu uliotokea kwa kusababishwa na moto uliotokea hivi katibuni na kuteketeza sehemu ya majengo ya shule ya Seminari ya Kiislam ya Mivumoni katika Msikiti wa Mtambani Kinondoni jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiangalia uharibifu uliotokea kwa kusababishwa na moto na kuteketeza sehemu ya majengo ya shule ya Seminari ya Kiislam ya Mivumoni katika Msikiti wa Mtambani Kinondoni jijini Dar es salaam.Kulia ni Imam wa Msikiti huo Sheikh Suleiman akimuongoza Mh. Lowassa.
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images