Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109587 articles
Browse latest View live

BREAKING NYUUZZZZZZ: MABWENI YA SHULE YA SEKONDARI YA MIVUMONI ILIOPO KWENYE MSIKITI WA MTAMBANI KINONDONI YATEKETEA KWA MOTO

0
0
 Moto Mkubwa ukiendelea kuwaka katika eneo la juu la Jengo la Shule ya Sekondari ya Kiislam ya Mivumoni (Mivumoni Islamic Seminary) iliyopo ndani ya Msikiti wa Mtambani,Kinondoni B Jijini Dar es Salaam leo.

Eneo hilo ambalo lilikuwa likitumika kama Mabweni ya Wanafunzi wa Shule hiyo,Maabara na Ofisi za Walimu limeteketea kabisa kiasi kwamba hakuna kitu chochote kilichoweza kuokolewa.

Jitihada za kuuzima moto huo zimekuwa zikiendelea hadi hivi sasa,huku sehemu ya Waumini wa Kiislam wakijitokeza kwa wingi kusaidia juhudi hizo za kuuzima moto huo zilizokuwa zikiendesha na Kampuni ya Kuzima moto ya Ultimate,japo baadae gari hilo liliisha maji,hali iliyowapelekea Waumini hao kulijaza maji gari hilo kwa kurumia ndoo huku kazi ya Uzimaji moto huo ikiendelea.

Chanzo cha Moto huo,inadaiwa ni hitilafu ya Umeme iliyokuwepo kwenye Bweli la Wasichana Wanafunzi wa Shule hiyo.Hakuna mtu yeyote aliepoteza maisha wala kujeruhiwa katika tukio hilo.Picha zote na Othman Michuzi. 
 Moto mkubwa ukiendelea kuwaka kwenye eneo hilo.
 Ulinzi mkali wa Polisi ulitawala katika eneo la Msikiti huo wa Mtambani kuhakikisha Usalama unakuwepo kwenye eneo hilo.
 Sehemu ya Waumini wa Kiislam wakishirikiana kusombelea maji ili kuuzima moto huo. 
 Jitihada zikiendelea. 
  Gari la Zima Moto mali ya Kampuni ya Ultimate Security likijazwa maji kwa ndoo ili kuendelea na zoezi la uzimaji w amoto huo. 
  Likafika na gari hili kwa ajili ya kusaidia kuzima moto huo.


Mashuhuda wakiwa nje ya eneo hilo.

Hon. Prime Minister Mizengo Pinda launches the 6th PACF conference

0
0
Honourable Prime Minister Mizengo Pinda launched the annual Pan African Competitive Forum conference on 13th

The seminar that has been taking place from 11th to 15 August 2014 in Bagamoyo, Tanzania, is jointly organised by the Commission for Science and Technology (COSTECH), PACF-Tanzania and Small Industries Development Organization (SIDO) , The meeting aims to enhance Africa’s social economic development through innovation and cluster based competitiveness as a catalyst for transformation, innovation, entrepreneurship and accelerating regional integration and intra-Africa trade.

 The gathering has brought together the government, academics and the private sectors from Ghana, Senegal, Finland, Kenya, Uganda, Japan, Sweden, South Africa, Botswana Nigeria as well as Tanzania.

“The government is playing an active role in supporting clusters, I believe through program we are going to break through the world market,’’ Prime Minister Mizengo Pinda said during the event adding that the government anticipates having 300 clusters and 500 facilitators by 2020.

Prof Burton Mwamila, the chairman of PACF executive Board said that clusters are seen as excellent vehicles to ensure that there is innovativeness in the products produced in African countries.“Innovation in clusters is vital because it enables value addition, competition, growth and thus enhances development, ’’ he said.

Mwamila said that the cluster initiative programme in Tanzania has been developing since its establishment in 2003.“We started with eight clusters and now we have 70 clusters and 200 cluster facilitators (trainers),’he said.

Meanwhile, Dr Hassan Mshinda the Director General of the Commission for Science and Technology (COSTECH) said that the cluster programme has the potential of transforming the African economy. August 2014, “Through this meeting we expect to exchange knowledge, share experience and build capacity of our cluster programme, ’’ Dr Mshinda said.

Dan Sjögren from Scandinavian Institute for Competitiveness and Development Swedish who represented the Swedish International Development Authority (SIDA) commended PACF-Tanzania for its achievements in reinforcing the cluster programme.SIDA is the major donor of the cluster programmed in Tanzania.

“SIDA has contributed an important part in cluster development but this is a minor part, ’’ he added ‘The big part has been done in Tanzania. Facilitators have worked hard to make the business plan work in reality, ’’ he said.

On his part Prof Makame Mbarawa, the Minister of Communication, Science and Technology urged local governments to promote and engage academics with clusters. ‘‘Innovative clusters should be adopted to create employment,’’ Mbarawa said.
Agroup photo of the PACF meeting participants with the Prime Minister, Mizengo Pinda.

JUMA KASEJA AWA BALOZI MPYA WA NSSF

0
0
Golikipa wa timu ya Yanga, Juma Kaseja, ambaye ni mwanachama wa Hiari wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) akikabidhiwa mkataba kutoka kwa  Mwanasheria wa NSSF, Chedrick Komba kuwa Balozi rasmi wa Shirika hilo katika Huduma Mbalimbali zitolewazo na NSSF.

Golikipa wa Yanga, Juma Kaseja, ambaye ni mwanachama wa Hiari wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) akisaini mkataba wa kuwa balozi wa NSSF katika huduma mbalimbali zitolewazo na Shirika hilo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori na Kulia ni Mwanasheria wa NSSF, Chieldric Komba.

WAZIRI KAMANI ANG'ARA KIMATAIFA, APEWA TUZO

0
0
Na Mwandishi Watu
WAZIRI wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk. Titus Kamani (Pichani), amepewa Tuzo ya Utawala Bora katika kipengele cha Watendakazi Bora Serikali barani Afrika kutokana na wizara yake kuonyesha utendaji kazi wa hali ya juu.

Tuzo hizo ziliandaliwa na Kampuni ya CEO Titans Building Nations ya Afrika Kusini, ambayo imejikita katika kutambua watu na viongozi wanaofanya kazi kwa ufanisi. Hafla ya kukabidhi tuzo hizo ilifanyika hivi karibuni katika Hoteli ya Hilton jijini Nairobi, Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mjini Dar es Salaam, juzi jioni mbali na Dk. Kamani, mwingine aliyepata tuzo hiyo ni Mhariri Mtendaji wa Mwananchi Communications Limited, Bakari Machumu, aliyenyakua tuzo ya Uongozi Thabiti katika Vyombo vya Habari vya Tanzania.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Dk. Kamani alisema hiyo ni ishara ya kuwa serikali na watendaji wa wizara yake wanawajibika kikamilifu.

Alisema wizara yake ina jukumu la kusimamia maendeleo ya mifugo sekta ambayo, imekuwa mkombozi mkubwa wa Watanzania wengi na kuwa, amefarijika kuona utendaji wa wizara yake ukitambulika kimataifa.

“Wakati naalikwa kuhudhuria hafla hii nilijua ni masuala ya utendaji ila sikufahamu kama kuna tukio hili la jitihada za wizara yangu kutambuliwa. “Nimefarijika kuona kazi yetu inatambulika hivyo, tutaendelea kuongeza bidii zaidi ili kutimiza azma yetu ya kuwainua wafugaji na wakulima kwa ujumla kiuchumi,” alisema Dk. Kamani.

Washiriki 100 kutoka taasisi mbalimbali barani Afrika walichaguliwa, ambapo wawakilishi 28 waliingia fainali kuwania tuzo katika nyanja tofauti.

SERIKALI YATAKIWA KUTIMIZA AHADI ZA UJENZI WA ZAHANATI KWA KILA KATA

0
0
DSC_0534
Diwani wa kata ya Ololosokwani na Mkurugenzi wa Irkiramat Foundation (RAMAT) Bw. Yannick Ikayo Ndoinyo akiangalia kitanda cha kujifungulia wakimama kwenye Zahanati ya Sero ambayo kwa siku inatibu wagonjwa 50 na zaidi ikiwa na daktari mmoja huku wakazi wanaofuata huduma hiyo kutoka kata hiyo na ya jirani Soitosambu kutembea umbali mrefu kwa Kilometa 7-15 kupata huduma ya afya.(Picha Zainul Mzige)

Na Mwandishi wetu, Ngorongoro

Wakazi wa vijiji vya Ololosokwan, Soit-Sambu, Njoroi na Loipir kata za Ololosokwana na Soit-Sambu wilayani Ngorongoro wanakabiliwa na changamoto kubwa ya huduma ya Afya kwa kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo kwenye kijiji cha Sero huku waathirika wakubwa ni kinamama na watoto.

Umbali wa zahanati hizo imekuwa sababu kubwa ya vifo hususani kwa akina mama wajawazito wanaotaka kwenda kujifungua na watoto halikadhalika wanapozidiwa hufia njiani kutokana na umbali wa zahanati kutoka kijiji kimoja kwenda kingine wanapotakiwa kuwahishwa hospitalini hali inayowafanya kutembea umbali mrefu kilometa 15 hadi kuipata huduma ya zahanati .

Akizungumza na waandishi wa habari Diwani wa kata ya Ololosokwani na Mkurugenzi wa Irkiramat Foundation (RAMAT) Yannick Ikayo Ndoinyo waliotembelea miradi inayofadhiliwa na Shirika la Elimu na Sayansi (UNESCO) wilayani humo alisema serikali haina budi kutimiza ahadi yake ya kujenga Zahanati kwa kila kata nchini Tanzania kuwapunguzia wagonjwa hususan akina mama waja wazito na watoto adha ya kutembea au kusafiri mwendo mrefu kutafuta huduma za afya.

Ndoinyo alisema kuwa tatizo kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma ya afya lipo na kwamba vifo ya wamama na watoto na kutopata huduma zinazotakiwa kwa wakati. Wananchi hupata huduma za afya kutoka Sero ambayo ina umbali mrefu kutoka Ololosokwang au wakati mwingine mgonjwa hupata rufaa rufaa hadi Hospitali ya wilaya ya Waso na iwapo mgonjwa atakuwa katika hali mbaya ni tatizo.
DSC_0532
Gari la wagonjwa lilitolewa na serikali likiwa limeharibika kutoka na miundo mbinu ya barabara na kushindwa kufanyiwa matengezo kwa muda mrefu hali inayomfanya daktari wa Zahanati hiyo kuwafuata majumbani wagonjwa mahututi kwenda kuwapatia huduma za afya.

BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

MH. LOWASSA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA BALOZI WA JAPAN NCHINI

0
0
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada wakati alipo mtembelea ofisini kwake Jijini Dar es Salaam na kufanya nae mazungumzo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada ofisini kwake,Mwenge jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada akifafanua jambo wakati wa Mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa ofisini kwake,Mwenge jijini Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kushoto) akimtambulisha Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Arusha, Mh. Namelock Sokoine kwa Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada pamoja na Ujumbe wake alioambatana nao.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akielezea jambo kwa Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada na ujumbe wake alioambatana nao wakati wa kikao chao kilichofanyika leo ofisini kwake Mwenge,jijini Dar es saalam.Kulia ni Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Arusha, Mh. Namelock Sokoine.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kushoto) na Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Arusha, Mh. Namelock Sokoine (kulia) wakimsikiliza Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada (wa pili kushoto) wakati alipokuwa akifafanua jambo kuhusiana na namna Ubalozi huo utakavyoweza kufanisha Miradi ya Maendeleo katika Wilaya ya Monduli.Wa pili kulia ni Katibu wa Balozi wa Japan,Bw. Sato Firgt.

TANZANIA YAADHIMISHA MIAKA 100 TANGU KUANZA KWA VITA KUU YA KWANZA YA DUNIA

0
0
Katika kuadhimisha miaka 100 ya kuanza kwa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, Tanzania, Ubelgiji, Ugiriki, Iraki, Kenya, Nigeria na Afrika Kusini zimeungana na India katika hafla iliyoendana na uzinduzi wa kitabu cha picha za kumbukumbu za wapiganaji waliofariki kwenye vita hiyo kuanzia mwaka 1914 – 1918.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, iliyofunguliwa na Mhe. Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mhe. John W. Ashe, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kuhudhuriwa na Wawakilishi wa nchi mbalimbali Wanachama wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Ramadhan M. Mwinyi, Kaimu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania amesema kitabu hicho ni mchango muhimu katika historia ya vita hivyo, vilivyosababisha maafa makubwa katika mabara ya Ulaya, Asia na Afrika, ambapo jumla ya watu milioni 16 walifariki dunia na wengine milioni 20 kupata majeraha makubwa.

Balozi Mwinyi alitumia fursa ya hafla hiyo kuikumbusha jumuiya ya kimataifa, wajibu wa kizazi cha sasa, kuendelea kusisitiza umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya mazungumzo kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 1945.

Akizungumza kwa hisia kali, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alisema hata baada ya athari kubwa za Vita Kuu mbili za Dunia, Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa hazijajifunza umuhimu wa kuepusha vita na migogoro. Matokeo yake, dunia imeendelea kugubikwa na migogoro mbalimbali ambayo imesababisha vifo, majeruhi, uharibifu mkubwa wa miundo mbinu na mazingira.

Naye Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa alihoji kama Vita hivyo vilipaswa kuitwa Vita Vikuu, badala yake alisema vingeitwa Janga Kuu la dunia. Rais huyo alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa nchi zote za Umoja wa Mataifa katika kuzuia na kutatua migogoro.

Tanzania bara, wakati huo ikiwa chini ya himaya ya wakoloni wa Kijerumani, iliguswa na vita hivyo vilivyopiganwa na watawala wa Kijerumani na Waingereza katika maeneo ya Afrika Mashariki. Inakadiriwa kuwa, wanajeshi na raia takriban elfu hamsini wa eneo hilo walipoteza maisha katika vita hivyo. Miongoni mwao ni wanajeshi wa Kihindi ambao walipigana upande wa Waingereza. Minara ya kumbukumbu pamoja na makuburi ya wanajeshi hao ipo Dar es Salaam, Taveta naTanga.

Tanzania ilisisitiza kuwa, ni vyema kuwakumbuka wengine wengi ambao walipoteza maisha wakati na baada ya vita, kutokana na maradhi na njaa. Pia ilitaja maeneo mengine ambayo ni kumbukumbu ya vita hivyo kama vile sanamu ya askari (Askari Monument) iliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam na Kariakoo, ambako waliishi wanajeshi wa Kihindi waliojulikana kwa Kiingereza kama “Carrier Corps”.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwa na Wawakilishi wa Nchi zilizoandaa hafla hiyo.
 Mhe. Ramadhan M. Mwinyi, Kaimu Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwasilisha hotuba yake kwenye hafla hiyo.

washindi wa shindano la uwekezaji “DSE Scholar Investment Challenge 2014” wapatikana jijini dar

0
0
 Mshindi wakwanza wa shindano la uwekezaji “DSE Scholar Investment Challenge 2014” Laurent Dyanko kutoka chou kikuu cha kilimo, Sokoine University of Agriculture (SUA) akikabidhiwa zawadi wa shilingi milioni moja na cheti cha ushindi
 Mshindi wapili wa shindano la uwekezaji “DSE Scholar Investment Challenge 2014” George Firimini kutoka chuo cha usimaniza wa fedha, Institute of Finance Management (IFM) akikabidhiwa zawadi wa shilingi laki sita na cheti cha ushindi
 Mshindi watatu wa shindano la uwekezaji “DSE Scholar Investment Challenge 2014” Godlove Kellya kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam akikabidhiwa zawadi ya shilingi laki nne na cheti cha ushindi


Washindi watatu bora shindano la uwekezaji “DSE Scholar Investment Challenge 2014” Laurent Dyanko, George Firmini na Godlove Kellya katika picha ya pamoja na mwakilishi kutoka benki ya NMB, mkuu kitengo cha njia za huduma mbadala.



Afisa mtendaji mkuu wa Dar es Salaam Stock Exchange akiongea na wanafunzi walioshiriki katika shindano la uwekezaji “DSE Scholar Investment Challenge 2014” wakati wa hafla ya kuwatambua wanafunzi hamsini bora na uandaaji wa mchakato wa kutafuta washindi watatu bora wa shindano hilo. Katikati ni bwana George Kivaria  mwakilishi benki ya NMB (wadhamini wa mashindano) kushoto ni Sosthenes Kewe  Mkurugenzi wa taasisi ya uendelezaji wa huduma za fedha.

Redd's miss Kinondoni 2014 kujulikana kesho ndani ya Escape One mikocheni jijini Dar

0
0

 Mratibu wa shindano la Redd's miss Kinondoni 2014 Innocent Melleck katikati akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar Es Salaam juu ya shindano la kanda ya kinondoni litakalofanyika katika ukumbi wa Escape One ijumaa kwa kiingilio cha 10,000 kwa viti vya kawaida na 30,000 kwa VIP huku burudani za Malaika Bend chini ya Chirstian bella na Young Suma na tayari tiketi zipo mtaani. Baadhi ya warembo wa shoto ni matroni wa kambi hiyo Husna Maulid na kulia ni Mkuu wa itifaki wa kamati ya Miss Tanzania Albert Makoye

Benki ya Diamond Trust (DTB) yatangaza mafanikio yake makubwa kwa nusu mwaka wa 2014

0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Diamond Trust (DTB),Bwa.Viju Cherian akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani),Mapema leo ndani ya moja ya ukumbi wa mikutano Serena Hotel jijini Dar kuhusiana na ripoti ya nusu mwaka wa 2014 kuhusu utendaji wa benki hiyo kwa ongezeko kubwa la faida kabla yakodi (profit before Tax (PBT) ya sh.billioni 10.3 ikiwa ni  asilimia 38 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2013 sambamba na mafanikio makubwa iliyoyapata benki hiyo.

Bwa.Viju alisema kuwa mwaka 2014 unatoa matumaini ya kuwa mwaka mwingine mzuri kibiashara kwa DTB,alisema kuwa mafanikio yalipatikana katika maeneo yote muhimu ya urari wa mahesabu ya mwaka.''Benki yetu inajivunia kwa mara nyingine kupata faida kubwa ikilinganishwa na benki zingine shindani ikiwa na ongezeko la asilimia 44 katika biashara ya fedha za kigeni na ongezeko la asilimia 30 katika mikopo.Pichani shoto ni Mkuu wa kitengo cha Fedha na Utawawala Bwa.Joseph Mabusi pamoja na mwisho kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko Bwa.Sylvester Bahati.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI MHE. STEPHEN MASELE AKUTANA NA RAIS MSTAAFU MHE. BENJAMIN WILLIAM MKAPA

0
0
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa (Kulia) akiwa kwenye mazungumzo na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Stephen Masele ofisini kwake Upanga jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa (kulia) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Stephen Masele (Kushoto) aliyemtembelea ofisini kwake

MADALALI WA KORTI WAKAMATA BASI LA TFF

In Remembrance of Dr. Abdon Ulisaja and Mrs. Catherine Florence Mwangota

0
0
In Rising of the sun and in its going down,  We remember them
In the blowing of the wind and in the chill of winter,  We remember them
In the opening of buds and in the rebirth of spring,, We remember them
In the blueness of the sky and in the warmth of summer, We remember them
In the rustling of leaves and in the beauty of autumn, We remember them
In the beginning of the year and when it ends, We remember them
When we are weary and in need of strength, We remember them
When we are lost and sick at heart And When we have joys we yearn to share,
We remember them
So long as we live, they too shall live, We will continue to remember them

WASANII KUSHIRIKI TAMASHA LA KWANZA LA KIMATAIFA LA MUZIKI LITAKALOFANYIKA MJINI CAIRO, MISRI

Dola za Marekani milioni 53.8 zapatikana kutokana na mauzo ya vito

0
0
 Na Greyson Mwase, Bagamoyo

Jumla ya Dola za Marekani  milioni 53.8  zilipatikana kutokana na mauzo ya vito mbalimbali ndani ya nchi  kwa mwaka wa fedha 2013/2014.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha  Uchambuzi na Uthamini wa Madini ya Almasi na Vito, (TANSORT) kilichopo chini ya Wizara  ya Nishati na Madini   Archard Kalugendo kwenye semina  iliyoshirikisha Makamishna Wasaidizi wa Madini wa Kanda,  Afisa Madini Wakazi na  Wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini inayoendelea Bagamoyo  yenye lengo la  kujadili  utendaji na  uboreshaji wa  shughuli za uthaminishaji wa madini ya almasi na  vito nchini.

Kalugendo alisema kuwa  mauzo hayo  yanatokana na usimamizi mzuri wa Kitengo hicho  katika kuthaminisha  almasi na vito kwa ajili ya kukokotoa mrabaha wa Serikali; Kutayarisha miongozo ya bei (Price Guides)  ya almasi na madini ya  vito inayotumika kukokotoa mrabaha na  Kutoa huduma za kijemolojia (Gemmological Services) kwa wachimbaji wadogo na wa kati na Kusimamia mauzo na kufuatilia mwenendo wa masoko ya almasi na  madini ya vito.

“  Kutokana na  usimamizi mzuri wa  mauzo na kufuatilia mwenendo wa masoko ya almasi na  mad  ini ya vito, ulipelekea wastani wa bei ya almasi za Tanzania katika soko la dunia kupanda hadi  dola za Marekani 286 kwa karati   ikiwa ni ongezeko la  asilimia 13, alisisitiza Kalugendo

Alisema  masoko saba ya kimataifa yalifatiishwa ili kutambua mwenendo wa bei na masoko ya madini ya vito na almasi duniani ambayo ni  Bangkok, Antwerp, Basel, London, Changsha, Las Vegas na Arusha.

Kalugendo aliongeza  kuwa  mafanikio yaliyopatikana kutokana na usimamizi mzuri wa shughuli za uthamini wa almasi na madini ya  vito  ni pamoja na  mauzo ya Tanzanite kuliingizia  Shirika la Madini la  Taifa (Kalugendo aliainisha mafanikio mengine yaliyopatikana kuwa ni pamoja na Kilo 818, gramu 269,211 na carat 40,599 za Tanzanite kuthaminiwa na kuuzwa na mgodi wa TanzaniteOne Minerals Limited (TML) wa Arusha.


Akielezea changamoto za TANSORT  Kalugendo alisema ni pamoja na kada ya  Wajemolojia kutokuwa katika muundo wa Kada za Utumishi wa Umma , kutokuwepo kwa kituo  maalum  cha kufanyia biashara ya almasi na vito nchini na kuendelea kwa vitendo vya wizi, udanganyifu, utapeli na utoroshwaji wa madini ya almasi na vito nchini.


 Kalugendo aliendelea kueleza kuwa  kumekuwepo a  ukwepaji wa kodi na tozo za Serikali miongoni mwa wazalishaji na wafanyabiashara wadogo wa almasi na vito hali inayopelekea taifa kukosa mapato yake stahiki.

Akielezea mikakati katika utatuzi wa changamoto hizo Kalugendo alisema  rasimu ya Kada ya Wajemolojia imekamilika kwa ajili  ya taratibu  zinazofuata pamoja na matayarisho kwa ajili ya  soko rasmi la kuuzia madini ya thamani kubwa hapa nchini  kuendelea kufanyiwa kazi na Wizara.

Alisema  hatua mbalimbali  zinazoendelea ni pamoja na kufanya tathmini za mapato, kutafuta uwekezaji katika jengo hilo, kutathmini namna bora ya kuendesha soko hilo na kujifunza kutoka nchi nyingine juu ya uendeshaji bora wa masoko ya jinsi hiyo.

Aidha, aliongeza kuwa TANSORT imejipanga kuendelea kutoa elimu  juu ya athari za vitendo vya udanganyifu, wizi, ukwepaji kodi, na utoroshaji wa madini ya vito.

TANSORT ni Kitengo cha Uchambuzi na Uthamini wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya Nishati na Madini ambapo uthamini unalenga ukokotoaji sahihi wa mrabaha wa Serikali kama ilivyoelekezwa na Sheria ya Madini ya Mwaka 2010, Vifungu vya 87, 88 na 89.  Kitengo hiki kilichoanzishwa mwaka 1966 kina ofisi tano  sehemu tofauti tofauti ikiwa ni pamoja na Antwerp nchini Ubeljiji,  Kanda ya Mashariki (Dar es Salaam) Kanda ya  Kati- Magharibi (Shinyanga) Kanda ya Kaskazini (Arusha) Kanda ya Kusini (Songea).

TAHLISO WAPINGA MAANDAMANO YALIYOPANGWA KUFANYIKA KESHO IJUMAA

0
0
Makamu Mwenyekiti wa TAHLISO Abdi Mahmoud Abdi akizungumza na Waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar kuhusu kukanusha Taarifa ya Maandamano yaliyopangwa kufanyika hapo kesho. Picha na Makame Mshenga
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 
Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu TAHLISO limekanusha Taarifa zilizosambazwa katika Vyombo vya habari na Mitandao ya Kijamii juu ya kuwepo wa maandamano ya Wanafunzi wa Vyuo vikuu yanayotarajiwa kufanyika hapo kesho Ijumaa. 
Shirikisho hilo pia limesema Taarifa za kuwepo kwa maandamano hayo hazijatolewa na TAHLISO na kuwaomba Wanafunzi kutojaribu kushiriki katika Maandamano hayo. Akizungumza na Waandishi wa habari leo Mjini Zanzibar Makamu Mwenyekiti wa TAHLISO Abdi Mahmoud Abdi amesema aliyesambaza Taarifa za Maandamano hayo ni Mtu ambaye alishavuliwa Nyadhifa za Uongozi wa TAHLISO na kwamba anachokifanya ni Upotoshaji na kujipalilia kisiasa.
 “Anayejiita Mwenyekiti wa TAHLISO Musa Mdede SI MWENYEKITI HALALI kwa sababu vikao halali vya Shirikisho vilivyofanyika May 3,4,2014 katika Chuo cha kodi vilimwondoa madarakani na kwa mujibu wa Katiba nafasi yake ilikaimiwa na Makamu wake ” Alisema Abdi
Amesema sababu ya Msingi ya kumuondoa katika nafasi yake ilitokana na kwenda kinyume na Katiba kwa kujiingiza katika Siasa ambapo aligombea na kuangushwa katika kura za maoni kupitia CHADEMA. Amedai kuwa anachokifanya Mdede kwa sasa ni upotoshaji kwa TAHLISO ambapo anajitangaza kwa malengo ya kugombea uchaguzi mkuu unaokuja wa mwaka 2015. 
Amefahamisha kuwa licha ya kuwepo na Taarifa ya Baadhi ya Vyuo kutokupata Pesa kwa ajili ya Mafunzo ya Vitendo TAHLISO imekuwa bega kwa bega kuhakikisha suala hilo linapatiwa majibu ya haraka. 
Amesema BODI ya Mikopo inaendelea kuchukua hatua za haraka katika kuhakikisha Vyuo husika Vinapatiwa fedha na kwamba siku ya Leo Bodi itatoa Fedha kwa Chuo kikuu Kishiriki cha kumbukumbu ya Stephano Moshi (SMUCCO) na Chuo kikuu cha Jordan Morogoro.
 “Chuoni siyo sehemu ya kufanya Siasa bali ni sehemu ya kusoma, Maandamano siyo suluhu njia pekee ni mazungumzo na tunaendelea kuyafanya” Alifafanua Abdi. 
Aidha Makamu Abdi amesema taratibu zinazohitajika zinaendelea kuchukuliwa ili Vyuo vingine vilivyobakia viweze kupata fedha hizo. Vyuo ambavyo havijapata Fedha za Mafunzo kwa Vitendo ni pamoja na Chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino(SAUT) Mwanza na Tabora, Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM), Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji Mbeya na Chuo kikuu cha Tumaini Makumira-Iringa. 
Katika taarifa zilizosambaa kwenye Vyombo vya habari na Mitandao ya kijamii inadaiwa kesho Ijumaa kutafanyika Maandamano ya amani ya Wanafunzi wa Vyuo vikuu kuelekea Ofisi za Waziri Mkuu kushinikiza Serikali kutoa Shiligi Bilioni 6.6 kwa ajili ya mafunzo ya Vitendo kwa wanafunzi hao. 
Makamu huyo ambaye anashika nafasi ya Uenyekiti kwa sasa amewaomba Wanafunzi ambao hawajapata fedha zao kuwa watulivu wakati wakisubiri kupata fedha zao huku hatua za haraka zikichukuliwa. 

MTUMISHI WA BUNGE MAALUM LA KATIBA AAGWA BAADA YA KUTEULIWA KUWA JAJI WA MAHAKAMA KUU NA RAIS

0
0
 Mwenyekiti wa Kamati namba moja ya Bunge Maalum la Katiba,Mhe. Ummy Ali Mwalimu akimkabidhi kadi ya hongera   mtumishi wa Bunge hilo, Mhe. Leila Mgonya katika shehere ya kumwuaga  baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania. Awali  Mhe. Mgonya alikuwa ni Msaidizi wa  Waziri Mkuu.
 Mwenyekiti wa Kamati namba moja ya Bunge Maalum la Katiba,Mhe. Ummy Ali Mwalimu akimlisha keki mtumishi wa Bunge hilo, Mhe Leila Mgonya katika shehere ya kumwuaga  baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania. 
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. William Lukuvi , akimlisha keki mtumishi wa Bunge hilo, Leila Mgonya katika shehere ya kumwuaga  baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania. Picha na Kamati ya Bunge Maalum la Katiba

MISS ILALA 2013 DORICE MOLLEL ATEMBELEA KAMPUNI YA KUTENGENEZA UMEME WA GESI NA KUTUNZA MAZAO RIELA NCHINI UJERUMANI

0
0
photo
Bw. Karl Heinz Knoop akielezea historia fupi kuhusu kampuni yake kwa wanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu  Nyerere akiwemo Miss Ilala 2013 Dorice Mollel wanaoshiriki program ya mwezi mmoja nchini Ujerumani.

Miss Ilala 2013 Dorice Mollel (kushoto pichani) akiwa kwenye program ya mwezi mmoja, na wenzake 8 kutoka Chuo cha kumbukumbu ya Mwl. Nyerere ambapo wamepata nafasi ya kwenda kutembelea Kiwanda cha Kilimo kilichoanzishwa mwaka 1972 ambacho kinamilikiwa na Bw. Karl Heinz Knoop , mwenye uzoefu wa miaka 50 ambaye anatarajia kujenga kiwanda hiki pia nchini Tanzania mkoani Kilimanjaro Moshi kitakachofahamika kwa jina la Reila amabavyo pia vipo zaidi ya nchi 11 duniani na kwa Afrika ni Tanzania pekee tumepata bahati hiyo ya kuletewa Teknlolojia anayotumia ya kutengeneza umeme wa gesi na pia kutunza mazao, hii itasaidia sana kukuza sekta ya kilimo Tanzania.
Dorice Mollel amesema “ hichi ni kitu cha muhimu sana nikiwa kama mrembo nikirudi nyumbani na kuieleza jamii inayonizunguka ili kutuletee faida baadae nchini kwetu”.
photo (1)

Kamouni ya Huawei yaonesha nia kuwekeza mradi wa umeme jua zanzibar

0
0
 Kampuni ya Mitandao ya Teknolojia ya Kisasa ya Nchini Jamuhuri ya Watu wa China ya Huawei inayoendesha na kusimamia mradi wa Umeme unaotumia jua (Solar Power Solution) imeonyesha nia ya kutaka kuwekeza Visiwani Zanzibar kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Zanzibar (ZECCO).
Ujumbe wa Kampuni Huawei  ulioongozwa na Afisa Mkuu wa Kampuni hiyo Bw.Bruce Zhang ulieleza hayo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake iliyopo katika Jengo la Msekwa ndani ya Viunga vya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.
Akitoa maelezo na ufafanuzi wa kina wa mradi huo Mkurugeni Fedha wa Huawei Bwana Peter Jiang alimueleza Balozi Seif kwamba mradi huo umepangwa kuwa na awamu tatu zitakazojitegemea zenyewe kulingana na mahitaji ya sehemu husika zitazofanikiwa kuwekwa mradi huo.
Bwana Peter alizitaja awamu hizo kuwa ni pamoja na ile ya mwanzo itakaolengwa katika miradi ya Skuli, Hospitali wakati ile ya pili itaelekezwa katika maeneo ya utalii pamoja na bara bara za maeneo ya mji.
Mkurugenzi huyo Fedha  wa Kampuni ya Huawei aliitaja awamu ya tatu ya mradi huo itahusisha maeneo ya visima vya maji itakayokwenda sambamba na uimarishaji wa sekta ya kilimo kwa vile lengo kuu  la mradi huo linategemewa kufaidisha jamii iliyopo vijijini ambayo kwa mazingira ya maisha ya kila siku hukosa huduma za umeme na kudumaza kwa mahitajio yao ya kijamii.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba mradi wa Umeme wa kutumia jua ni muhimu sana kwa vile unaweza kuwa hakiba hasa wakati inapotokea hitilafu ya umeme unaotumika hivi sasa ambao ni chanzo kimoja tuu.
Balozi Seif alisema uanzishwaji wa mradi kama huo Visiwani Zanzibar unaweza kusaidia kasi ya ongezeko la uwekezaji katika sekta ya viwanda vidogo vidogo vitakavyotoa pia ajira kwa wananchi  hasa Vijana na akautaka Uongozi huo wa Kampuni ya Huawei kuwasilisha maombi yake kwa wakati ili Serikali kupitia Taasisi husika zipate fursa ya kuangalia njia ya kufanikisha kuanzishwa kwa mradi huo.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Afisa Mkuu wa Kampuni ya Huawei ya China Bwana Bruce Zhang Ofisini kwake ndani ya Jengo la Msekwa katika Viunga vya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.
 Afisa Mkuu wa Kampuni ya Huawei Bwana Bruce Zhang akimuonyesha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif michoro ya mradi wao wa Umeme wa kutumia jua waliopanga kuuanzisha Visiwani Zanzibar.
Nyuma ya Bwana Bruce ni Mkurugenzi Fedha wa Huawei Bwana Peter Jiang pamoja na Meneja wa mradi wa Solution Bwana Briyan Peng.
 Mkurugenzi Fedha wa Huawei Bwana Peter Jiang kati kati akitoa maelezo mbele ya Balozi Seif hayupo pichani ya jinsi mradi wa umeme wa kutumia jua utakavyoweza kufanya kazi kwa kiwango kinachokubalika.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akibadilishana mawazo na Ujumbe wa Kampuni ya Huawei mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika kwenye Ofisi yake iliyopo Bungeni Mjini Dodoma
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Survey Veterani yatoka sare na Coastal union U-20, yawakubali NSSF

0
0

 Kikosi cha Timu Ya Survey wakiwa katika picha ya pamoja.
 Wachezaji wa Survey Veterani wakiwa katika picha ya
pamoja Wachezaji wa Coastal U 20  kabla ya mechi.

Mchezaji wa Timu ya Survey Veterani Hamad Shaweji
akimtoka mchezaji wa Coastal Union U 20  katika mashindano ya kilele cha nane nanae yaiyofanyika viwanja vya mkwakwani Jijini Tanga.


NA ELIZABETH KILINDI, TANGA

TIMU ya Survey Veteran ya jijini Dar es Salaamu, Jumapili iliyopita ilivuna sare ya bao 1-1 dhidi ya kikosi cha vijana wa chini ya miaka 20 wa timu ya Coastal Union katika mechi ya kirafiki iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga.
Ikiwa ni mechi ya pili kwa Survey katika ziara yao ya jijini hapa, baada ya kuwafunga Veterani Kombaini ya Tanga 2-1 katika mechi yao ya kwanza dhidi ya Kombaini ya Maveterani wa hapa, licha ya kutoka sare walicheza soka ya kueleweka.
Mechi hiyo iliyofanyika chini ya udhamini wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), katika kuadhimisha kilele cha wakulima maarufu kama Nane Nane, imeacha gunzo kubwa kwa wapenzi na mashabiki wa soka.
Mechi hiyo ya Jumapili iliyochezwa katika uwanja wa Mkwakwani, jijini hapa, bao la Survey lilifungwa na Moses Mdamo katika dakika ya 20 kabla ya vijana wa Coastal Union kusawazisha dakika ya 40, likifungwa na Kapamba Kibadeni.
Baada ya filimbi ya mwisho, Kocha Seleman Mgaya ambaye pia ni Katibu wa timu ya Survey Veteran, alisema wamefurahia ushirikiano wa NSSF hasa kuonyesha mchango wao katika kusaidia michezo.
“Tunaishukuru  NSSF kwa moyo wa kutukutanisha kimichezo kwani wameonyesha kututambua. Kwetu hili ni jambo la kujivunia, tunaahidi kuwa tayari kutoa kila aina ya ushirikiano kwao,” alisema Mgaya.
Viewing all 109587 articles
Browse latest View live




Latest Images