Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

WASHIRIKI WA DANCE 100% WAADHIMISHA SIKU YA VIJANA VODACOM

0
0
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia akifafanua jambo kwa washiriki walioingia robo fainali katika shindano la Dance 100% walipotembelea makao makuu ya Vodacom Tanzania yaliyopo Mlimani City jijini Dar es Salaam na kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya Vijana duniani jana.Shindano hilo litakalofanyika Agosti 23 limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania na Mshindi wa shindano hilo atajinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5.
Washiriki walioingia robo fainali ya shindano la Dance 100% wakimsikliza kwa makini Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa walipotembelea makao makuu ya Vodacom Tanzania yaliyopo Mlimani City jijini Dar es Salaam na kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya Vijana duniani jana.Shindano hilo litakalofanyika Agosti 23 limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania na Mshindi wa shindano hilo atajinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa akipozi kwenye picha na baadhi ya washiriki walioingia robo fainali ya shindano la Dance 100% litakalofanyika Agosti 23 walipotembelea makao makuu ya Vodacom Tanzania yaliyopo Mlimani City jijini Dar es Salaam na kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya Vijana duniani jana.Shindano hilo limeandaliwa na EATV na Mshindi wa shindano hilo atajinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5.
Baadhi ya washiriki walioingia robo fainali ya shindano la Dance 100% wakifurahi jambo pamoja na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu wakati walipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Mlimani City jijini Dar es Salaam kwaajili ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya Vijana duniani jana.Shindano hilo litakalofanyika Agost 23 limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.Mshindi wa shindano hilo atajinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5.


WIZARA YA MAMBO YA NDANI YABADILI ANWANI YAKE

Mama Tunu Pinda atunukiwa Cheti cha Ubalozi wa Amani Duniani

0
0
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akiwa na Rais wa Universal Peace Federation (UPF), Dk. Thomas Walsh (kushoto) na Mwenyekiti wa UPF, Dk. Charles Yang mara baada ya kutunukiwa cheti cha kumtambua kama Balozi wa Amani Duniani katika hafla ya kufunga Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama uliomalizika jana usiku (Agosti 12, 2014) jijini Seoul, Korea Kusini.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (wa pili kulia mstari wa mbele) katika picha ya pamoja viongozi wenzake 10 waliotunukiwa vyeti vya kuwatambua kama Mabalozi wa Amani Duniani katika hafla ya kufunga Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama uliomalizika jana usiku (Agosti 12, 2014) jijini Seoul, Korea Kusini.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (wa pili kulia mstari wa mbele) katika picha ya pamoja viongozi wengine waliotunukiwa vyeti vya kuwatambua kama Mabalozi wa Amani Duniani katika hafla ya kufunga Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama uliomalizika jana usiku (Agosti 12, 2014) jijini Seoul, Korea Kusini. Walioshika vyeti kutoka kushoto ni Mke wa Rais wa visiwa vya Samoa, Bibi Filifilia Tamasese , Mke wa Rais wa visiwa vya Marshall, Bibi Lieom Anono Loeak na Mke wa Rais wa Fiji, Bibi Koila Nailatikau. (PICHA NA IRENE BWIRE WA OWM).

Matumizi bora ya Facebook kwa Biashara

0
0
Mitandao jamii imekuwa moja ya nyenzo imara kabisa ya kujitangaza na kuwafikia walengwa wengi kwa uharaka na mapana zaidi kwa njia ya mtandao. Jiulize swali dogo tuu, je kwa siku za karibuni umekuwa ukitumia njia gani kufahamu juu ya bidhaa au huduma fulani.

Je kwa kutumia tangazo la kwenye TV au Radio ambapo hauna uhakika hata saa ngapi wataonesha tangazo unalohitaji? Au kwa kupitia gazeti ambapo wengi wetu sasa inapita hata mwezi bila kusoma gazeti lililochapishwa? Au ni mara ngapi umetumia muda wako kusoma lundo la emails kwenye sanduku la email za matangazo (Junk emails)?

Matumizi ya facebook kwa Biashara

Siku hizi watu wamebadilika sana, wateja hupendelea kutafuta huduma toka mahali ambapo wanapata taarifa zote kwa upamoja tena pindi wanapohitaji, baadhi ya njia watumiazo kwa sana ni kama; kwa kutumia mitambo ya utafutaji (search engines) au toka kwa marafiki zao walio kwenye mitandao jamii (Social networks). Na huko ndiko kunakoshibisha njaa ya huduma na kujibu maswali yao yote.

Je wewe ni mmoja wa watoa huduma wanaoshibisha njaa ya taarifa za huduma au kujibu maswali ya wateja? Facebook siyo sehemu ya kupotezea muda kama wengi wanavyofikiria, pia siyo sehemu ya vijana peke yake na wala siyo sehemu ya kukimbiwa na wafanyabiashara makini.Facebook ni sehemu inayounganisha watu pamoja, na wewe kama mfanyabishara makini,Facebook ni sehemu sahihi itakayokuwezesha kujitanua na kukutana na wateja wengi wa sasa na wa baadae.

 Twende kazi, ili kuwasaidia wafanyabiashara na Wakurugenzi juu ya matumizi thabiti ya Facebook kibiashara, Dudumizi Technologies imeandaa kitabu kifupi juu ya matumizi ya Facebook kwa biashara,kitabu hiki kimelenga na kujikita moja kwa moja kukuongoza kwenye kila kitu muhimu unachotakiwa kukifahamu kwenye matumizi thabiti ya Facebook kwa biashra yako. Utakapomaliza kitabu hiki, basi utakuwa na uelewa mzuri siyo tuu kuhusu mitandao Facebook yenyewe kama Facebook, bali mahusiano yake na biashara yako
 



Kwa makala zaidi za IT fuatilia kurasa wetu wa Facebook http://www.facebook.com/dudumizi

KIKAO CHA MKAKATI WA UJENZI WA MAABARA ZA SHULE ZA SEKONDARI ZA KUDUMU KATA CHAFANYIKA DAR ES SALAAM

0
0
 Naibu Meya Manispaa ya Kinondon,Songoro Mnyonge (katikati), akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani), Agosti 12, 2014 jijini Dar es Salaam mara bara baada ya kufungua kikao kilichowakutanisha wakuu wa shule, watendaji wa mitaa, kata pamoja na wenyeviti wa bodi za shule chenye lengo la kuangali namna ya kupatikana kwa fedha za kujenga zinajenga  maabara katika shule  za Sekondari ifikapo Novemba Mwaka huu (kushoto), Afisa Uhusiano Manispaa ya Kinondoni, Sebastian Mhowera, na kulia. Diwani Kata ya Kawe Othmani Chipeta.
 Mchumi, wa Manispaa ya Kinondoni, Bw.Salm Hamisi Msuya akielezea mchakato wa uchangiaji wa ujenzi wa maabara katika shule 18 za sekondari zilizokuwa na maabara za kudumu wakati wa kikao hicho.
 Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Bw.Sanga Omari akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho.
 Diwani kata ya Manzese, Mhe.Eliam Manumbu akichangia mada.
 Wakuu wa shule, watendaji wa mitaa, kata pamoja na wenyeviti wa bodi za shule wakiwa kwenye kikao chenye lengo la kuangali namna ya kupatikana kwa fedha za kujenga maabara katika shule  za Sekondari ifikapo Novemba Mwaka huuHABARI PICHA- NA PHILEMON SOLOMON


MANISPAA  ya Kinondoni inahitaji jumla ya kiasi cha Sh Bilioni 1.3 ili kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete aliyezitaka Halmashauri zote kuhakikisha zinajenga  maabara katika shule  za Sekondari ifikapo Novemba Mwaka huu.

Hayo yamebainishwa jana Jijini Dar es salaam na Naibu Meya wa Manispaa hiyo Songoro Mnyonge  wakati akizungumza katika kikao kilichowakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wakuu wa shule, watendaji wa mitaa, kata pamoja na wenyeviti wa bodi za shule chenye lengo la kuangali namna ya kupatikana kwa fedha hizo.

Huku akiwaomba wadau mbalimbali yakiwemo mashirika, taasisi, watu binafsi pamoja na wafanyabiashara kujitokeza kuchangia upatikanaji wa fedha hizo, Songoro alisema ushirikiano wao katika suala hilo utaipa  faraja manispaa hiyo kutokana na umuhimu wa elimu kwa taifa.

“Tunawaomba mjitokeze kwa wingi ili kuunga mkono juhudi za Rais Kikwete anayetaka kuona shule zote za sekondari zinakuwa na maabara za kudumu ili kusaidia kupanua wigo wa ufundishaji kw wanafunzi mashuleni, jitihada zetu pekee hazitotuwezesha kufikia malengo hayo kutokana na ufinyu wa bajeti” alisema Mnyonge.

Aidha alisema manispaa hiyo inahitaji maabara za kudumu 114 kukidhi mahitaji katika kata 32 huku sekondari 14 ndizo pekee katika zilizo na maabara hizo kati ya 46 zilizopo katika manispaa hiyo suala alilosema linahitaji kutafutiwa ufumbuzi wa haraka.

Alisema kila chumba kimoja cha maabara ya kudumu ujenzi wake unakadiriwa kufikia kiasi cha Sh Milioni 75 na kwa jumla ya vyumba vote 114 inahitajika kiasi hicho cha zaidi ya Sh Billioni 1,suala alilosema haliwezi kufanikiwa bila nguvu za wadau mbalimbali.


Alisema malengo ya baadae ya manispaa hiyo ni kujenga vyumba vitatu vya maabara ya fikizia, kemia na baiolojia ifikapo mwaka 2016 hatu aliyosema kwa kiasi kikubwa itamaliza tatizo la ugumu wa masomo ya sayansi kwa wanafunzi sambamba na kuongeza wataalam wa baadae wa Taifa hili.

michuano ya Airtel Rising Stars Yaendelea kurindima uwanja wa karume jijini dar

0
0
 Nahodha wa Timu ya Ilala, Maisala Adam (kulia) akimiliki mpira asinyang'anywe na mshabuliaji wa Kinondoni, Ibrahimu Chuli wakati wa michuano ya Airtel Rising Stars inayofanyika katika Kiwanja cha Karume jijini Dar es Salaam jana. Timu ya Ilala ilishinda 1-0.
 Mchezaji wa Timu ya Ilala, Hussein Rashid (kulia) akipimana ubavu na Beki wa Timu ya Kinondoni, Miraji Kwangaya wakati wa michuano ya Airtel Rising Stars inayofanyika katika Kiwanja cha Karume jijini Dar es Salaam jana. Timu ya Ilala ilishinda 1-0.
 Mabeki wa Timu ya Kinondoni Fredy Mazuri (Kushoto) na Miraji Kwangaya wakimzuia mshambuliajai wa Timu ya Ilala,Hussein Rashid wakati wa michuano ya Airtel Rising Stars inayofanyika katika Kiwanja cha Karume jijini Dar es Salaam jana. Timu ya Ilala ilishinda 1-0.
Naodha wa Timu ya Kinondoni, Fredy Mazuri (aliyeanguka) akijaribu kumzuia naodha wa Ilala,Shabani Ally (Aliyeruka) asipite wakati wa michuano ya Airtel Rising Stars inayofanyika katika Kiwanja cha Karume jijini Dar es Salaam jana. Timu ya Ilala ilishinda 1-0. 

TEAM LIBE FOR DMV COMMUNITY PRESIDENT 2014 HAITAMBUI UONGOZI MPYA WA ATC METRO 2014

0
0
Tunapenda kutoa taarifa kwa Umma wa DMV kuwa, Team Libe for DMV Community President 2014 hatutambui uongozi mpya ulio tangazwa na Tume ya Uchaguzi jana August 11, 2014.   Msimamo wetu ni kuwa; tunapinga matokeo ya uchaguzi ulio fanyika August 9, 2014 kwani ulikuwa sio wa haki na ni BATILI.  

“Team Libe for DMV Community President 2014” haitatoa ushirikiano wowote na uongozi wa Jumuia ya Association of Tanzania Community in DMV.  Pia tunawaasa wale wapenzi wetu kuto kutoa ushirikiano wowote na uongozi huu batili hadi pale madai yetu yatakapo sikilizwa na kutatuliwa.  Tunaomba wapenzi wetu ambao walijitokeza kupiga kura wawe wavumilivu na watulivu katika kipindi hiki kigumu cha kunyang’anywa haki yao ya kimsingi ya kumchagua kiongozei wanao mtaka.  

Mwisho, “Team Libe for DMV Community President 2014” inaitaka “Board of Directors” kutengua uongozi huu uliopatikana kwa njia ya dhulma.  Ieleweke kuwa, Team Libe for DMV Community President 2014” na wafuasi wake hatutatoa ushirikiano wowote na uongozi wote wa jumuia.

Fuata hii link kusoma maelezo juu ya ubatili ya huu uchaguzi;


Imetolewa August 12, 2014
Team Libe for DMV Community President 2014

PINDA AFUNGUA MKUTANO WA PACF- BAGAMOYO, AADHIMISHA SIKU YA KUZALIWA

0
0
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama dawa mbali mbali  zilizotengenezwa kwa kutumia Karafuu kabla ya kufungua  mkutano wa Pan African Competitiveness  Forum (PACF)  kwenye hoteli ya Stella Maris mjini Bagamoyo leo Agosti 13, 2014. Kulia ni Waziri wa Sayansi na Tekinolojia  Profesa Makame Mbarawa
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu  Mahiza (kushoto) na Waziri wa Sayansi na Tekinoloji, Profesa  Makame Mbarawa baada ya kufungua Mkutano wa Mwaka wa  Pan African Competitiveness Forum (PAC) mjini Bagamoyo  Agosti 13, 2014. Watatu Kulia ni Profesa Burton Mwamila.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na baadhi ya washiriki wa  Mkutano wa Mwaka wa  Pan African  Competitiveness Forum,  baada ya kufungua mkutano wa kwenye hoteli ya  Stella Maris Mjini Bagamoyo, Agosti 13, 2014. Kulia ni Waziri wa Sayansi na Tekinolojia, Profesa Makame Mbarawa  na Wavpili kulia ni Mhandisi Mohammed Jibrin kutoka Nigeria na kushoto ni General Garbal kutoka Nigeria
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akigomganishiana glasi na mjukuu wake Nicole katika mkusanyiko mdogo  na mfupi  sana wa kifamilia wa  kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwake  kwenye makazi yake  kwenye hoteli ya Stella Maris mjini `Dodoma Agosti 12, 2014. Wengine pichani ni binti zake, Namsi (kulia) na Yusta. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Airtel na GSMA waandaa semina kuhamashisha matumizi ya Nishati mbadala rafiki wa mazingira Dar es Salaam - Green Power Energy

0
0
Bharti Airtel, kampuni ya mawasiliano ya kimataifa yenye shughuli katika nchi 20 mbalimbali Asia na Afrika, leo imeshiriki kuandaa semina ya GSMA inayofanyika Dar es Salaam kwa siku mbili mfululizo tarehe 12 na 13 Agosti 2014 katika hoteli ya Serena. 
 Semina hiyo ya kimataifa ya GSMA inalenga zaidi kutazama maendelea ya sekta ya Mawasiliano kwa kuangalia Zaidi mipango, mafanikio na fursa ya baadaye ya mawasiliano ya nishati mbadala rafiki kwa mazingirana yaani –green telecoms, pia itaendesha majadiliano juu ya mikakati inayowezekana kuongeza maendeleo katika sekta ya mawasiliano kwa kuzingatia matumizi ya nishati rafiki kwa mazingira (green power energy). 
 Semina hiyo inahudhuriwa na makampuni kutoka mataifa yapatayo 60 ikiwemo Tanzania, ambapo wanajadiliana na kubadilishana mawazo katika sekta ya mawasiano. Sunil Colaso, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel alisema, “tunajisikia fahari sana kushiriki katika mabadiliko ya nishati ya kijani yenye lengo la kutunza mazingira ambayo yataleta faida kubwa katika jamii yetu. 
Ushirikiano wetu na GSMA katika kuandaa tukio hili kutatuwezesha pia kuanzisha na kuleta technolojia mpya ambapo tutachangia kwa kutoa mawazo yetu katika mijadala inayohusiana na mawasilano endelevu nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla sehemu yetu ya kwa jamii (CSR)”. 
 “Mjadala iliyoandaliwa itajikita zaidi katika mambo yanayohusu teknolojia na maendeleo yake kama vile ufahamu kwenye teknolojia ya nishati ya jua, yaani (solar hybrid technologies) au fuel cell technology na nyingine nyingi. 
Baadaye, wasemaji mbalimbali wataangazia fursa za uwekezaji na miundombinu ya biashara ambazo zitaweza kunufaika na uvumbuzi huu wa matumizi ya teknolojia ya nishati mbadala–rafiki wa mazingira kutumika kwa maendeleo ya nchi ya Tanzania”.aliongeza Colaso Akiongea katika ufunguzi rasmi wa shughuli hiyo, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa aliwapongeza GSMA na Airtel kwa kazi yao nzuri katika juhudi za kuleta maendeleo kwa jamii kwa kupitia teknolojia ya mawasiliano. vile vile alishukuru sana GSMA kuipa nafasi nchi ya Tanzania kuwa muandaaji wa semina hiyo muhimu kwa mwaka huu. 
Pia kwa kutambua changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya mawasiliano hasa kwenye swala la nishati ya kuwezesha minara nchini Tanzania, Prof. Mbarawa alifurahishwa sana na mtazamo wa fulsa hiyo ya utumiaji wa teknolojia ya nishati mbadala rafiki wa mazingira. “kunachangamoto kubwa katika Kuanzisha na kuendeleza miundombinu kwa kizazi kipya hasa kwa nchi zetu zinazoendelea. 
Hivyo, tuna kila sababu ya kukaa na kushirikiana jinsi ya kutumia teknolojia mbadala ili kwa pamoja kupunguza changamoto za ukosefu wa nishati, na kuendeleza ufanisi wa huduma na uhifadhi wa mazingira utakaofaidisha Afrika katika miaka ijayo” , aliongea Mheshimiwa Mbarawa.
 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa  (wa pili kushoto), akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso, baada ya kuzindua warsha ya siku mbili ya Nishati ya mbadala kwa wadau wa Mawasiliano ya simu ya GSMA, inayofanyika jijini Dar es Salaam leo.  Kulia ni Meneja wa Programu wa GSMA Mobile, Ferdous Mottakin na Afisa Mtendaji Mkuu wa Airtel Africa Towers Services Ltd, Prakash Ranjalkar.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa  (kushoto), akijadiliana jambo na  Mkurugenzi  wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya, baada ya kuzindua warsha ya siku mbili ya Nishati ya Kijani kwa Mawasiliano ya simu ya GSMA, inayofanyika jijini Dar es Salaam jana. 

ELIZABETH TARIMO NDIYE MSHINDI WA MISS KANDA YA MASHARIKI 2014

0
0
Mshindi wa Taji la Redd’s Miss Kanda ya Mashariki 2014 ,  Elizabeth  Tarimo (18) ambaye pia ni Miss Lindi akiwa mwenye uso wa furaha na tabasamu la ushindi sambamba na  mshindi wa pili  Nidah Katunzi (19) ( kulia) ,ambaye ni Miss Mtwara pamoja na wa tatu, Lucy Julius Diyu  (21) (kushoto) Miss Morogoro baada ya kutangazwa kuwa washindi kwenye nafasi hizo wakati  kinya’ganyiro cha kuwania taji hilo  kilichofanyika juzi usiku kwenye ukumbi wa Hoteli ya Nashera ya mjini Morogoro.

Rais Kikwete, Mgeni Rasmi katika Mkutano wa Diaspora jijini Dar es salaam

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika mkutano wa Watanzania wanaoishi ughaibuni (Diaspora) ambao umepangwa kufanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam tarehe 14 na 15 Agosti 2014.

Mkutano huo ambao umeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Taasisi ya Diaspora Tanzania (Tanzania Diaspora Initiative-TDI), unalenga kuwahamasisha Watanazania wanaoishi ughaibuni wenye utaalamu na mitaji kurudi nchini au kuwekeza katika shughuli mbalimbali kwa madhumuni ya kukuza uchumi wa nchi.

Aidha, Mkutano huo ambao ni wa kwanza kufanyika nchini, wenye kaulimbiu “Unganisha, Shiriki, Toa taarifa na Wekeza” (Connect, Engage, Inform and Invest) utatoa nafasi kwa washiriki kutambua vyema fursa za uwekezaji na ajira zinazopatikana Tanzania.


Imetolewa na: Wizara ya Mambo ya Nje 
na Ushirikiano wa Kimataifa, Dar es salaam. 
13 Agosti, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, AFUNGUA MKUTANO WA SITA WA VYUO VIKUU MJINI ARUSHA LEO

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua Mkutano wa Sita wa Vyuo Vikuu uliofanyika leo Agost 12-2014 katika Hoteli ya Naura Spring mjini Arusha. Mkutano huo umewakutanisha washiriki mbalimbali wakiwemo, wanazuoni, wanasayansi, watunga sera na wawakilishi wa wafanyabiashara kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Senegal, Canada, Ujerumani, maofisa wa Benki ya Dunia na wadau mbalimbali wa maendeleo. Lengo la Mkutano huo ni kujadili nafasi ya Elimu ya Juu katika utekelezaji wa Malengo ya Milenia (MDGs)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Sita wa Vyuo Vikuu uliofanyika leo Agost 12-2014 katika Hoteli ya Naura Spring mjini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia vitabu vya aina mbali mbali alipotembelea mabanda ya maonesho yaliyoandaliwa na Vyuo Vikuu baada ya kufungua Mkutano wa Sita wa Vyuo Vikuu wenye lengo la kujadili nafasi ya Elimu ya Juu katika utekelezaji wa Malengo ya Milenia (MDGs) Mkutano huo umefunguliwa leo Agost 12-2014 katika Hoteli ya Naura Spring mjini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijadiliana jambo na baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Sita wa Vyuo Vikuu wenye lengo la kujadili nafasi ya Elimu ya Juu katika utekelezaji wa Malengo ya Milenia (MDGs) Mkutano huo umefunguliwa leo Agost 12-2014 katika Hoteli ya Naura Spring mjini Arusha. (Picha na OMR)

Mahabusu ya watoto Tanga kupatiwa fedha

0
0
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO

Serikali imetenga fedha zitagawiwa kwenye vituo vyote vinavyotoa ushauri nasaha na kurekebisha watoto walio chini ya umri wa miaka 18 vilivyo chini ya Idara ya Ustawi wa jamii nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii  Nsachris Mwamwaja kufuatia habari iliyochapishwa na gazeti la Majira toleo Na. 7524 Vol.II/5624 la Jumatano Agosti 13, mwaka huu yenye kichwa cha habari “Mahabusu ya watoto yadaiwa mil. 1/=”.

“Ni kweli tatizo hilo lipo ndio maana Serikali imetenga fedha tayari ambazo zitagawiwa kwenye vituo vyote nchi nzima” alisema Mwamwaja.

Mwamwaja alisisitiza kuwa deni hilo litalipwa kweye mahabusi hiyo iliyoko Tanga.

Mahabusi hiyo ni miongoni mwa vituo kadhaa vilivyo chini ya Idara ya Ustawi wa Jamii ndani ya Wizara ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. 

Matumizi ya fedha hizo ni pamoja na kushughulikia tatizo la maji na uhaba wa chakula kituoni hapo ili kuendelea kutoa huduma stahiki kwa watoto hao na kufikia lengo la kuwarekebisha tabia zao ili wawe raia wema nchini.  

Aidha, Mwamwaja aliongeza kuwa fedha zilizotengwa  si za Mkoa wa Tanga tu bali ni kwa ajili ya vituo vya nchi nzima zikiwemo makambi ya wazee wasiojiweza, mahabusi za watoto na kambi za kutibu wagonjwa wa ukoma.

NEWS ALERT: Rais Kikwete ateua Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania wapya 20

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, baada ya kushauriana na Tume ya Utumishi wa Mahakama, amewateua wafuatao kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzaniakuanzia tarehe 13 Agosti, 2014.


WATUMISHI WAMAHAKAMA


(i)                 Bw. Penterine Muliisa KENTE, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani, Dar es Salaam.


(ii)               Bw. Benedict Bartholomew MWINGWA,ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Msajili wa Mahakama Kuu, Dar es Salaam.


(iii)             Bw. Edson James MKASIMONGWA, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Katibu wa Jaji Mkuu.


(iv)             Bw. David Eliad MRANGO, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Msajili, Baraza la Ushindani, Dar es Salaam.


(v)               Bw. Mohamed Rashid GWAE, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Msajili, Mahakama Kuu, Kitengo cha Kazi, Dar es Salaam.


(vi)             Dkt. John Eudes RUHANGISA, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Msajili, Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Arusha.


(vii)           Bw. Firmin Nyanda MATOGORO,ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Naibu Mwenyekiti, Baraza la Rufaa la Kodi, Dar es Salaam.


MAWAKILI WA SERIKALI NA TAASISI MBALIMBALI ZA SERIKALI


(i)                 Dkt. Eliezer Mbuki FELESHI,ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Mkurugenzi wa Mashitaka, Dar es Salaam.


(ii)               Bi. Barke Mbaraka Aboud SEHEL, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Kaimu Mkurugenzi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dar es Salaam.


(iii)             Bi. Winfrida Beatrice KOROSSO ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Katibu Mtendaji, Tume ya Kurekebisha Sheria, Dar es Salaam.


(iv)             Bi. Lilian Leonard MASHAKA,ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa,                      (TAKUKURU), Dar es Salaam.


(v)               Bi. Leila Edith MGONYA, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Msaidizi wa Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dar es Salaam.


(vi)             Bw. Awadhi MOHAMED, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Mchunguzi Mkuu, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, (TAKURURU), Dar es Salaam.


MAWAKILI WA KUJITEGEMEA


(i)                 Bw. Lugano J.S. MWANDAMBO, kutoka REX Attorneys, Dar es Salaam.


(ii)               Bw. Amour Said KHAMIS, kutoka AKSA Attorneys, Dar es Salaam.


(iii)             Dkt. Paul KIHWELU, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Wakili wa Kujitegemeana na Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu Huria, Dar es Salaam.


(iv)             Bi. Rose Ally EBRAHIMU, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Wakili wa Kujitegemea, Bulyankulu Gold Mine Ltd, Shinyanga.


(v)               Bi. Salma MAGHIMBI, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Mjumbe, Tume ya Ushindani, (FCC), Dar es Salaam.


WATUMISHI WA VYUO VIKUU


(i)                 Dkt. Mary Caroline LEVIRA, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Kaimu Mkuu wa Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu Kishiriki cha Ruaha.


(ii)               Dkt. Modesta Opiyo MAKOPOLO, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu, Mzumbe, Morogoro.


Wateuliwa wote wataapisha tarehe 15 Agosti, 2014 Saa 05.00 asubuhi katika Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam.


Imetolewa na Mkurugenzi Idara ya habari Maelezo

13 Agosti, 2014

HIVI NDIVYO MSIKITI WA MTAMBANI KINONDONI JIJINI DAR ULIVYOKUWA UKITEKETEA KWA MOTO JIONI HII.


MH. SITTA ATEMBELEWA NA JUKWAA LA KATIBA NA JUKWAA LA WAHARIRI MJINI DODOMA LEO

0
0
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta, akizungumza na Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba (JUKATA), Deus Kibamba, alipomtembelea ofisini kwake Bungeni Dodoma leo. Kushoto ni mjumbe wa Jukwaa hilo Hezron Kaaya.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta akizungumza na Viongozi wa Jukwaa la Wahariri (TEF), walipomtembelea ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma leo. Picha na Owen Mwandumbya.

video ya uzinduzi wa studio mpya ya BBC idhaa ya kiswahili Mikocheni jijini dar es salaam

UNILEVER LAUNCHES OMO FAST ACTION IN DAR ES SALAAM, TANZANIA

NAJUA WAJUA YA CAPTAIN GARDINER G. HABASH NDANI YA MICHUZI TV LEO

TANZANIA INVESTS IN EMPOWERING WOMEN - JULIET KAIRUKI

0
0
Women empowerment will be front and centre in 2014 as more companies, communities and countries invest in women's entrepreneurship. CNBC Africa spoke to Juliet Kairuki, Executive director at the Tanzania Investment Center (TIC), in the sidelines of the just ended US Africa investment summit hosted by US President  Barack Obama in Washington DC.
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images