Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

WAKULIMA WA SHAYIRI MONDULI JUU WALIOFADHILIWA NA TBL WAPATA MAVUNO MENGI

$
0
0
 Mkulima (wa pili kulia) wa Shayiri katika mashamba ya Monduli Juu, wilayani Monduli mkoani Arusha akiendelea na uvunaji wa Shayiri kwa kutumia mashine ya kisasa ambapo wameweza kuvuna hadi gunia 1o kwa hekari moja. Wakulima wa Monduli Juu wameanza kuvuna mazao yao, baada ya kuwezeshwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) iliyowapatia mafunzo, mikopo ya mbolea na dawa. Pia shayiri hiyo hununuliwa na TBL kwa ajili ya kutengenezea kimea katika kiwanda kilichopo Moshi, mkoani Kilimanjaro.
 Afisa Ugani wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Monduli Juu na West Kilimanjaro, Editha Temu akipima kuangalia ubora wa Shayiri iliyoanza kuvunwa katika mashamba ya Monduli Juu. Kushoto ni  ni Mwenyekiti wa wakulima wa Shayiri Monduli Juu Bariki Kivuyo.


 Mkulima wa Shayiri Goigoi Kivuyo akionyesha sehemu ya shamba linalotarajiwa kuvunwa Shayiri eneo la Monduli Juu, wilayani Monduli mkoani Arusha, baada ya kulima kwa kufuata maelekezo na mkopo  wa mbegu na dawa kutoka Kampuni ya TBL
: Mkulima wa mfano Mepoloo Lolosi aliyelima hekari 180 za Shayiri katika eneo la Monduli Juu wilayani Monduli, mkulima huyo alikuwa akionyesha baadhi ya zana za kilimo ambazo aliwezeshwa kuzipata kwa njia ya mkopo ili kufikia malengo yake ya kulima kisasa.  Tayari amekwisha kumaliza kuzilipia zana hizo pamoja na nyingine.
Meneja wa Barley kutoka  Kiwanda cha Bia nchini (TBL) Dk. Bennie Basson akiwaonyesha waandishi wa habari hawao pichani namna Kampuni hiyo inavyowawezesha wakulima wa Shayiri katika kulima kilimo bora chenye tija.

RPC NJOMBE APATA AJALI NA MLINZI WAKE AFARIKI DUNIA

$
0
0
Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe ASP Fulgence Ngonyani.
Na James Festo, Njombe.

KAMANDA wa polisi Mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani  pamoja na dereva wake Nuaka Seme  wamelazwa katika hispitari ya Mkoa wa Njombe ya kibena ambako wanaendelea  kupatiwa matibabu kufuatia ajali iliyotokea usiku wa kuamkia  jana katika eneo la kiwanda cha Miwati (TANWAT) ambapo katika ajali hiyo askari mwenye cheo cha "constable" alifariki dunia papo hapo.

Akiongea na vyombo vya habari  huku akipatiwa matibabu katika hospitari ya Mkoa kutokana na Mnadhimu wa Jeshi la polisi Mkoa wa Njombe ASP Yahaya  rajab kushindwa kuongea kwa madai kuwa hanaruhusa Kamanda Ngonyani alisema kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa tatu hadi saa nne za usiku katika barabara ya  Makambako hadi Njombe.

Aidha Jeshi la Polisi  limesema kuwa  katika ajali hiyo aliyefariki dunia ni George  Stephano  Matiko (24)

 H580 Pc George  Enzi za uhai wake.

Nuaka Sema aliyekuwa dereva wa gari hilo lenye namba za usajili PT 2058  alisema kuwa kutokana  gari hilo la mizigo kukaa katikati ya barabara walishindwa kupishana kwa wakati na kuligonga kwa nyuma na baadae kukutana uso kwa uso na nguzo ya umeme iliyowasababishia ajali.

"ghafla niliona gari mbele likiwa limewasha taa zote za mbele (full light) likiwa upande wetu na nilivyoona hivyo niliwasha taa kuashiria hatari  na ndipo mwenye gari la mizigo alianza kukwepa kuelekea upande wake na wakati tukipishana mwishoni kwa kuwa lilikuwa refu tulienda tukakwanguana ndipo tulipoteza mwelekeo" alisema dereva huyo.

Aliongeza kuwa " mara baada ya kukwanguliwa tukilikwepa lori tukaigonga nguzo ya umeme na hapo hapo mwenzetu akafariki na tunashukuru sana wafanyakazi wa kampuni ya tanwat ambao waliwahi kuja kutusaidia... na lile lori hatukuweza kuchukua namba zake na liliendelea na safari".

Kwa upande wake  Afisa muuguzi wa hospitari hiyo  Bw. Denis Haule alisema kuwa majeruhi wawili  walipokelewa majira ya saa tano usiku na mwingine  alikuwa amekwisha fariki dunia na kubainisha kuwa hali ya majeruhi hao inaendelea vizuri na  Kamanda wa Polisi anaweza kuruhusiwa muda wowote.

"tumewapokea jana usiku  majeruhi  wawili na mmoja  akiwa amekwisha fariki dunia , hali yao kwa sasa inaendelea vizuri  na kamanda anaweza kuruhusiwa wakati wowote....lakini dereva wake anatakiwa kuendelea kupewa matibabu kutokana na maumivu mbalimbali katika mwili wake.

MADA MAUGO ALIPA KISASI CHA KUPIGWA NA THOMASI MASHALI

$
0
0
Bondia Thomasi Mashali (kushoto) akionyeshana umwamba wa kutupiana makonde na Mada Maugo wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana.Maugo alishinda kwa point mpambano huo.
Bondia Thomas Mashali (kulia) akimrushia konde la mkono wa kushoto bondia Mada Maugo wakati wa mpambano wao uliofanyika jana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.Maugo alishinda kwa point mpambano huo.
Mabondia Mada Maugo (kushoto) na Thomas Mashali wakipambana ulingoni.
Bondia Said Memba (kushoto) akionyeshana umwamba wa kutupiana makonde na Bondia Khalid Chokoraa wakati wa mpambano wao uliofanyika jana .Chokoraa alishinda kwa point.
Bondia Khalid Chokora akipangua konde lililorushwa na Saidi Memba wakati wa mpambano wao chokoraa alishinda kwa point.Picha na Superd Blog

TEKNOLOJIA YA MIWANI YA KISASA YAWA TISHIO

$
0
0
 Kumekua na wimbi la ukuaji wa teknolojia kila kukicha, Ukuaji huu wa teknolojia umepelekea matumizi makubwa ya mitandao maeneo mengi na hili linaenda sambamba na ukuaji wa kasi wa uhalifu mtandao hivi sasa. Mbali na "MIWANI" pamoja na"MAGARI YASIYO NA DEREVA" kutoka Google, pia kumekua na aina nyingine ya miwani maarufu kama “Spy glasses” ambayo awali iliaminika inatumiwa zaidi na wahalifu ( wadukuzi) wa taarifa za watu.

Miongoni mwa maswala yaliyo umiza vichwa wataalam wa maswala ya usalama mitandao katika mijadala ni pamoja na kupima athari za miwani hii ya kisasa ambayo inakua imeambatanishwa na kifaa chenye uwezo wa kuona, na kusafirisha taarifa upande wa pili huku pande zote mbili kuweza kusafirisha sauti kupitia mawani hiyo.

Aina tatu za mawani hizi za kisasa ziliweza kuangaziwa macho na wataalam wa maswala ya usalama mitandao ili kujua ni athari kiasi gani zinaweza kuleta kwa jamii na badae katika kampeni ya kukuza uelewa wa maswala ya usalama mitandao kwa msaada wa tasnia ya uigizaji, Hollywood kupitia Tamthilia ya "NIKITA" kwenye kipengele chake cha mwisho sehemu ya kwanza naya tatu walitolea ufafanuzi aina mbili za miwani na uwezo wake.


Aina hiyo ya mawani sasa imeonekana kuchukua sura mpya pale Polisi nchini uchina kukamata wanafunzi waliyokuwa wakitumia miwani hiyo wakati wakifanya mitihani ilikuwasiliana na walio nje kupatiwa majibu ya mtihani. Uchunguzi huo uliambatana na tahadhari kuwa miwani hiyo iko kawaida sana na kwa haraka haraka si rahisi kuitambua hivyo wasimamizi mitihani kutakiwa kuwa makini sana kwa wavaaji miwani.


Aidha, aina hii ya miwani pia imehofiwa kuenea zaidi ambapo inaaminiwa kwa kushirikiana na teknolojia ya simu zinazo tumiwa na wahalifu kufatilia watu kwa pamoja zinategemewa kutumiwa vibaya na hatimae kusababisha wimbi la uhalifu mtandao lililoboreshwa zaidi kuleta madhara makubwa kwa mataifa mbali mbali.

ZESCO YAICHAPA SIMBA 3-0

$
0
0
 Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji na viongozi wa Simba pamoja na Rais wa TFF, Jamal Malinzi. (Picha na Francis Dande)
 Kikosi cha Simba kikiwa na Kocha Mkuu, Zdravko Logarusic (kulia), pamoja na Rais wa Simba, Evans Aveva.
Kikosi cha Zesco.
 Ramadhani Singano 'Mess' akiwatoka wachezaji wa Zesco.
Mshambuliaji wa Simba, Raphael Kiongera (kushoto), akimtoka beki wa Zesco United ya Zambia, Bernad Mapili katika mchezo maalumu wa kirafiki wa kimataifa wa Simba Day uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Zesco ilishinda 3-0.
Golikipa wa Zesco, Lameck Nyangu akiokoa moja ya hatri zilizoelekezwa langoni mwake.
Amis Tambwe akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Zesco, Bernad Mapili.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

BALOZI LIBERATA MULAMULA APIGA KURA YAKE DMV

$
0
0
 Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwasili kwenye kituo cha kupigia kura katika uchaguzi wa DMV unaoendelea sasa hivi Wheaton, Maryland nchini Marekani hapa mhe. Liberata Mulamula akilakiwa na mgombea makamu wa Urais Bi. Salma Moshi na Bwn. Idd Sandaly, Rais wa Jumuiya ya Wtanzania anyaemariza muda wake na ambaye pia anagombea tena nafasi hiyo katika uchaguzi huo.
Mhe. Libarata Mulamula akisalimiana na kampeni meneja wa mgombea wa Urais Liberatus Mwang'ombe Bi. Muna
 Mgombea wa Urais Liberatus Mwang'ombe akimsindikia Mhe. Balozi kuahakiki jina lake.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akihakiki jina lake.

Mhe. Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na mmoja wa Wajumbe wa kamati ya uchaguzi Bwn. Sunday Shomari.

Mhe. Balozi akipiga kura yake.

 Mhe. Balozi akitumbukiza kuara yake.
Balozi akiwahutubia wanaDMV Hebu msikilize hapo chini.

USHIRIKA VETERAN BINGWA WA BONAZA LA NANENANE ARUSHA

$
0
0
Mahmoud Ahmad,Arusha
Timu ya Ushirika Veteran ya mkoani Kilimanjaro imeibuka bingwa wa Bonanza la Nanenane kwa kuifunga timu ya Kivule veteran ya ukonga jijini Dar es salaam kwa magoli 3-0  katika mchezo wa fainali ya mashindano hayo yaliondaliwa na timu ya Arusha All Stars kwenye uwanja wa sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Michezo hiyo ya nanenane iliyozishirikisha timu kutoka mikoa ya Arusha,Dodoma, Mwanza,Dar es salaam na Kilimanjaro ambao timu yao ndio waliibuka mabingwa wa mashindano hayo kwa timu za ushirika veteran na kivule kucheza fainali

Hata hivyo wenyeji wa mashindano hayo waliambulia nafasi ya nne baada ya kufungwa katika mechi ya kugombea nafasi ya tatu na timua ya Dodoma veteran iliyokuwa inaongozwa na mkongwe wa soka hapa nchini Charles Mgodo.

Akizungumza baada ya mechi hiyo mgodo aliwataka wachezaji wa sasa kuangalia michezo ya maveterani katika mabonanza mbalimbali kwani watajifunza kitu kutoka kwao ikiwemo nidhamu ya michezo na kujituma kama walivyoonyesha baadhi ya wachezaji wa miaka ya nyuma wa timu zilizotamba kwenye ligi kuu.

Pia Mgodo alisema kuwa maandalizi ya timu za vijana wa sasa na wazamani ni tofdauti huku akisema kuwa vijana wa sasa wanataka kucheza kama mchezaji Fulani baada ya kuangalia tv huku hawajitumi hili ni tatizo na kuwataka kuanza kujituma na kutoweka maslahi mbele na kuuvaa uzalendo.

Akalishauri shirikisho la michezo hapa nchini Tff kurudi mashuleni au kuanzisha Academy ilkuweza kuibua vijapaji na sio kuviacha vikielea bila ya kuviendeleza hili ni tatizo kwa ukuaji wa michezo hapa nchini.

“Tunataka vijana wakija kwenye mabonanza waje kujifunza mpira na kuangalia tofauti ya mpira wanaocheza wao na wa wazee wao hapa umeona wachezaji wa zamani wakijituma tokea mwanzo wa mchezo hadi mwisho na wao wanatakiwa kuwa kama hivi ila kikubwa wawe wazalendo kwa taifa lao hapo tutafanikiwa”alisema Mgodo.

Mh. Zitto atikisa Mwidau CUP Pangani

$
0
0
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), amesema hatua ya Tanzania kutofanya vizuri katika michenoa ya kimataifa ni kukosekana misingi imara wa kuinua vipaji kuanzia ngazi ya chini.

Hayo alisema leo mjini Pangani alipokuwa akizindua mashindano ya Mwidau CUP, ambapo asema hatua ya Tanzania kutoka patupu katika mashindano ya Olimpiki ni kielelezo tosha cha kuhitaji maandalizi ya kina.

“Nchi yetu haijapata bahati ya kufanya vizuri kwenye michezo kwani hivi juzi timu zetu zilikuwa katika michuano ya Olimpiki nchini Scotland lakini hatukupata medani hata moja.

“Wiki iliyopita tulikuwa Maputo Msumbiji timu yetu ya Taifa imetolewa kwenye mashindano ya Mataifa huru. Tanzania kwa mara ya mwisho ilishiriki mashindano ya mataifa huru tangu mwaka 1980. Hatujawahi kushiriki tena na sababu kubwa tumesahau kujenga vipaji,” alisema Zitto.

Alisema ni vigumu kumnenepesha ng’ombe siku ya moja ya mnada ila kinachotakiwa ni juhudi kama zilizonzishwa na Mbunge wa Viti Maalum Amina Mwidau (CUF), kuibua vipaji kuanzia ngazi za chini. Alimtaka mbunge huyo kuhakikisha mashindani yajayo yakuwa na timu za chini ya miaka 17 ambazo zinatasaidia katika kuibua vipaji zaidi.

“Hii itatusaidia kuwajua watoto bado wadogo kwani hapa Pangani wapo kina Ulimwengu na kina Mbwana Samatta. Ninatoa wito kwa mashirika ya umma kuwa na timu zao kama ilivyokuwa miaka ya nyuma kwani hii itasaidia kuinua soka letu na hata michezo mingine katika Taifa letu,” alisema.

Kwa upande wake mbunge wa Viti Maalum, Amina Mwidau (CUF), alisema mashindano ya mwaka huu yamekuwa na maboresho makubwa ambapo mshindi wa kwanza atapata zawadi ya Sh 500,000 wa pili 400,000, wa tatu Sh 300,000 huku mshindi wa nne akijinyakulia Sh 100,000.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), akizungumza na wananchi katika uzinduzi wa mashindano ya soka ya Mwidau CUP leo mjini Pangani.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), akiingia uwanjani kuzindua mashindano ya Mwidau CUP .Kushoto ni mdahamini wa mashindano hayo ambaye pia ni mbunge wa Viti Maalum Amina Mwidau.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), akiwa ameshika ngao ya hisani ambayo iliwania katika mchezo wa ufunguzi wa Mwidau CUP, ambapo timu ya Torino iliibamiza APL ya Mwera bado 2-0.

NAIBU SPIKA ALIPOKUWA ZIARA YA KIKAZI NCHINI MALAYSIA

$
0
0
 Naibu Spika Mheshimiwa Job Ndugai akiwa na waheshimiwa  Saleh Ahmed Pamba, (Pangani),Abdulkarim Esmail Hassan Shah (Mafia) walipokuwa kwenye ziara ya kikazi nchini Malaysia. Katika picha ya pamoja na Afisa wa Bunge, Afisa wa Ubalozi Bwana Dismas Assenga na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Ponary Mlima.

Rais wa Zanzibar Dk.Shein akutana na Diaspora wa Zanzibar Ikulu

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Wazanzibari wanaoishi   nchi za nje (Diaspora)  wakati alipowaalika katika chakula maalum leo katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar (kushoto) Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
 Baadhi ya Wazanzibari wanaoishi nje ya Nchi (Diaspora)wakiwa katika chakula walichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.
 Wazanzibari wanaoishi nje ya Nchi (Diaspora) wakichukua chakula walichoaandaliwa na   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar
 Wazanzibari wanaoishi nje ya Nchi (Diaspora) wakichukua chakula walichoaandaliwa na   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


RAIS KIKWETE AKUTANA NA RAIS UHURU KENYATTA MJINI DUBAI WAKIWA NJIANI KUREJEA NYUMBANI

$
0
0
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Uhuru Kenyatta walipokutana katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dubai waliposimama kwa muda wakiwa njiani kuelekea nyumbani wakitokea Washington DC, Marekani, walikohudhuria Mkutano wa Marekani na Wakuu wa nchi wa Afrika ulioandaliwa na Rais Barack Obama.
 Mama Salma Kikwete akisalimiana na Rais Uhuru Kenyatta walipokutana katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dubai waliposimama kwa muda wakiwa njiani kuelekea nyumbani wakitokea Washington DC, Marekani, walikohudhuria Mkutano wa Marekani na Wakuu wa nchi wa Afrika ulioandaliwa na Rais Barack Obama. Kulia  ni Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe Omari Mjenga
 Balozi wa Tanzania  katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Mhe.Mbarouk Nassor Mbarouk akiwa na balozi wa Kenya katika UAE Mhe Mohamed Gello katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dubai ambapo mabalozi hawa walifika kuwapokea Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Uhuru Kenyatta waliosimama kwa muda mjini hapo wakitokea Washington DC, Marekani, walikohudhuria mkutano wa Marekani na Wakuu wa nchi za Afrika ulioandaliwa na Rais BArack Obama wa Marekani. Picha na IKULU

DEREVA TEXI ATOWEKA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA

$
0
0
Na John Gagarini,Kibaha.

DEREVA wa Texi wa Maili Moja Richard Ponera (36) mkazi wa Mwendapole wilayani Kibaha mkoani Pwani amepotea katika mazingira ya kutatanisha baada ya kukodishwa na watu wasiofahamika.

Ponera alikodishwa na watu wawili ambao hawakufahamika  Agosti 5 mwaka huu majira ya saa 2:30 usiku akiwa anaendesha gari lenye usajili na T 905 BHT aina ya Corolla nyeupe.

Akizungumza na mjini Kibaha kuhusina na tukio hilo katibu wa Umoja wa madereva Texi Kibaha Mjini (KITAGURO) Fadhil Kiroga alisema kuwa dereva huyo tangu alipoondoka siku hiyo hadi leo hakurudi na hakuna taarifa yoyote  iliyopatikana juu yake.

Kiroga alisema kuwa siku ya tukio hilo Ponera alionekana akipatana na watu hao kwa muda kidogo kama dakika 10 hivi kisha akaondoka na watu hao ambao walikuwa wawili.

“Baada ya mapatano licha ya kuwa madereva wengine hawakuweza kujua walichokuwa wakiongea na Ponera waliondoka na alipofika Mlandizi aliwasiliana na mwenzetu ambaye ni Salum Mbawala na kumwambia kuwa kwa sasa yuko Mlandizi,” alisema Kiroga.

Alisema kuwa baada ya hapo simu yake haikuweza kupatikana tena kwani baada ya kuona harudi wenzake walijaribu kumpigia lakini simu yake haikupatikana tena.

“Ponera hapa alikuwa hana muda mrefu tangu aanze kazi na alipata gari hilo ambalo alikuwa amekabidhiwa kama wiki mbili zilizopita na gari lenyewe halikuwa kwenye hali nzuri sana kusema labda ilikuwa ni kishawishi cha watu labda kutaka kuliiba gari hilo, hatujui kilichomtokea mwenzetu,” alisema Kiroga.

Aidha alisema kuwa wamefanya jitihada mbalimbali ambapo walikwenda polisi kutoa taarifa juu ya tukio hilo na kupewa namba KMM/RB/847/2014 pia walitoa taarifa kwenye vituo vya Mlandizi na Tumbi kisha kutembelea maeneo ya Yombo, Miswe na Mzenga bila ya mafanikio.

Kwa uapande wake mke wa dereva huyo Rosemary Urasa (31) alisema kuwa siku ya tukio hilo alikuja naye hadi Maili Moja yeye akenda sokoni kununua vitu vya nyumbani akamwacha stendi kwa ajili ya kuendelea na shughuli zake kama kawaida.

“Nakumbuka majira ya saa 5 asubuhi nilimpigia simu baada ya gari linguine ambalo liko hapa nyumbani lilikuwa linapiga honi lenyewe nikamwambia aje alizime lakini kwa bahati nzuri kuna mtu alifanikiwa kulizima nikamjulisha alikuwa njiani kuja lakini akarudia eneo linaloitwa Picha ya Ndege, toka hapo kila nikipiga simu simpati,” alisema Urasa.

Alibainisha kuwa mumewe ambaye wamezaa naye watoto wawili walihamia Kibaha baada ya kufanikiwa kujenga na kuzaa watoto wawili ambao ni Ruben (14) anayesoma kidato cha kwanza St Anne na Kontrada anayesoma darasa la sita shule ya Msingi Jitegemee.

Aidha alisema kuwa wakati mwingine mumewe hufanya kazi na kukesha hivyo siku hiyo usiku alijua kuwa atakesha lakini ilipofika asubuhi alishangaa kutokumwona kwani endapo anakuwa amekesha asubuhi ni lazima arudi lakini siku hiyo hakumwona ikambidi aje kwenye eneo analopaki lakini alipouliza wakasema tangu alivyoondoka jana hajaonekana tena.

Naye mmiliki wa gari hilo Athuman Kimia alisema kuwa siku hiyo ya tukio aliwasiliana na Ponera ambapo kulikuwa na tatizo la kulipia gari linapokuwa barabarani na kumpa 170,000 kwa ajili ya kulipia.

Kimia alisema kuwa baada ya kama saa moja alimpigia na kumwambia kila kitu kashalipia hivyo mambo mazuri na ndipo alipoendelea na shughuli kama kawaida.

“Tumekubaliana kila baada ya wiki awe ananipa malipo ya kazi lakini nilipigiwa simu kuambiwa kuwa Ponera aonekani na nilipojaribu kumpigia simu yake haipatikani sijui kilichomtokea ninini kwani yeye huwa ananipigia endapo kumetokea tatizo kwani sasa hivi ni wiki ya pili tangu nimkabidhi gari ,” alisema Kimia.

AZANIA BANK ILIVYOSHIRIKI MAONESHO YA NANE NANE JIJINI ARUSHA

$
0
0
Afisa Masoko wa Kanda ya kaskazini wa Benki ya Azania ,Bhoke Makore akizungumza na baadhi ya wananfunzi waliotembelea banda la Azania Benki katika maonesho ya Nane nane kanda ya ksakazini yaliyofanyika katika viwanja vya Themi jijini Arusha.
Mmoja wa Staff wa Azania Bank tawi la Arusha Jovin Joseph  akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa wateja waliotembelea banda la Bank hiyo katika viwanja vya Nane nane.
Afisa Masoko wa Kanda ya kaskazini wa Benki ya Azania ,Bhoke Makore akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo walipotembelea banda la Azania Benki katika maonesho ya Nane nane kanda ya ksakazini yaliyofanyika katika viwanja vya Themi jijini Arusha.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

VODACOM ILIVYONOGESHA TAMASHA LA MATUMAINI JIJINI DAR

$
0
0
Mmoja wa Mashabiki akiwa na furaha katika Tamasha la Usiku wa Matumaini lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam juzi.
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya, Ahmad Alli (maarufu) Madee akiwapagawisha mashabiki wake wakati wa Tamasha la Usiku Matumaini lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam juzi.
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya, Roma Mkatoliki akiwapagawisha mashabiki wake wakati wa Tamasha la Usiku wa Matumaini lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam juzi.
Bondia Said Membe (kulia)akijiandaa kumsukumia konde bondia, Kharid Chokoraa wakati wa Tamasha la Usiku wa Matumaini lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam juzi.

Msanii muvi JB akimwangalia msaanii mwenzake, Kraud baada ya kumuangusha chini wakati wa pambano lao la ngumi wakati wa Tamasha la Usiku wa Matumaini lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam juzi.
Bondia Mada Maugo (kulia) akiangalia namna ya kumsukumia konde bondia, Thomas Mashali wakati wa Tamasha la Usiku wa Matumaini lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam juzi.
Mshabiki wa bondia, Mada Maugo wakimwagia maji baada ya mwanamasumbwi huyo kushinda pambano lake zidi ya bondia Thomas Mashari wakati wa Tamasha la Usiku wa Matumaini lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam juzi.

WANAWAKE WOTE DUNIANI TUNALILIA AMANI - MAMA PINDA

$
0
0
MKE WA WAZIRI MKUU, Mama Tunu Pinda amesema wanawake wote duniani wanalilia amani na hawapendi vita wala machafuko kwani husababisha amani kutoweka kwenye familia na vifo vya watu wasio na hatia.

Ametoa wito huo leo mchana (Jumapili, Agosti 10, 2014) wakati akitoa mada kama mzungumzaji mkuu (keynote speaker) kwenye Mkutano wa Dunia wa siku tano ulioanza leo jijini Seoul, Korea Kusini.

Mkutano huo ambao umeandaliwa na taasisi ya Universal Peace Federation (UPF) ambayo inatoa ushauri kwenye Baraza la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Uchumi na Kijamii unajadili masuala ya Amani, Usalama na Maendeleo.

Akiwasilisha mada yake kuhusu usalama, amani na maendeleo barani Afrika, Mama Tunu Pinda alisema: “Ninaiomba jamii ya Kimataifa duniani kote tusimamie amani na usalama kwani kinyume na hapo ni kuleta machafuko na vita. Wanawake hatupendi vita wala machafuko...,” alisema huku akishangiliwa.

Aliwataka washiriki wa mkutano huo wasimame katika nafasi zao kama baba na mama, kama kaka na dada na kuhakikisha kuwa dunia inakuwa ni mahali pazuri pa kuishi. “Ninawasihi tuendeleze maono ya Muumba wetu, tuweke utu mbele kwa kuwajali wengine na tuache kutanguliza maslahi yetu binafsi,” alisema.

Mapema, akiwakaribisha wajumbe zaidi ya 500 kutoka nchi 68 wanaoshiriki mkutano huo, Rais wa UPF, Dk. Thomas Walsh alisema taasisi hiyo inasimamia misingi ya amani, usalama na maendeleo ya jamii kwa nia ya kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa mataifa mbalimbali.

Alisema anatumaini uwepo wa wakuu wa nchi mbalimbali na viongozi mashuhuri, utasaidia kupata majibu ya changamoto inayoikabili dunia juu ya upatikanaji wa amani ya kudumu.

Naye, Mfalme Letsie Mswati III kutoka Lesotho, akizungumza katika mkutano huo alisema dunia inakabiliwa na changamoto nyingi za ukosefu wa amani kubwa ikiwa ni uharibifu wa mazingira. Aliwataka wajumbe wa mkutano huo kuhakikisha wanahimiza utunzaji wa mazingira kama njia ya kupunguza matatizo yanayojikeza kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

Alionya kwamba kuna haja ya kuweka mifumo madhubuti ya kuhakikisha kuwa dunia haiendelei kuwa na matukio ya kigaidi na matumizi ya silaha za maangamizi. “Kama tutakubali vita viendelee kutokea, na migogoro isiyokwisha barani Afrika na nchi za Uarabuni, ni lazima tukubali kuwa hakutakuwa na maendeleo katika mabara haya,” alisema.

Uchaguzi DMV 2014

Timu ya Quebec Yatwaa Ubingwa wa Mbagala Cup

$
0
0
Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa pamoja na Mlezi wa Mashindano hayo, Emmanuel John wakikabidhi zawadi ya mbuzi kwa washindi.  
Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa pamoja na Mlezi wa Mashindano hayo, Emmanuel John wakikabidhi zawadi ya mbuzi kwa washindi timu ya QuebecMgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa akikabidhi zawadi ya jezi na mpira kwa washindi. 
Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa akikabidhi zawadi ya jezi na mpira kwa washindi. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

SHUKRANI ZA DHATI KWA WANA-DMV

$
0
0
Ndugu zangu WanaDMV, mimi Harriet Shangarai nakuja mbele yenu kuwashukuru kwa kujitokeza kwa wingi ili kushiriki katika zoezi la kidemokrasia -
Kupitia  kura, sauti za wanaDMV  zimesikika. 

Ushirikiano na Upendo mlio onyesha ndio msingi utakaotuletea maendeleo ya kweli.
Mbele yetu tuna kazi kubwa, lakini kwa moyo  mliyoonyesha nina imani tutaweza.
Asanteni saana. 
Palipo na Umoja pana  Ushindi. PS

NAJUA WAJUA YA CAPTAIN GARDINER G. HABASH NDANI YA MICHUZI TV LEO

MASHIRIKA MBALIMBALI YAOMBWA KUDHAMINI PIA MATAMASHA YA MUZIKI WA INJILI

$
0
0
1
Meya wa jiji la Mwanza ya Mhe.Stanslaus Mabula akinyanyua juu albam za mwimbaji Rose Muhando wakati alipozindua albam hiyo mkoani Mwanza leo kwenye uwanja wa CCM Kirumba. 

 Albam hiyo imezinduliwa na Meya wa jiji la Mwanza Mhe.Stanslaus Mabula ambaye alimwakilisha Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mh. Januari Makamba. Akizungumza katika uzinduzi huo wakati akitoa ujumbe aliouwakilisha katika uzinduzi huo kutoka kwa Mh. Januari Makamba,Mabula ameuelezea ujumbe huo kuwa Serikali inafanya kila liwezekanalo kushawishi makampuni ili yadhamini pia matamasha ya muziki wa injili ka ambavyo yamekuwa yakifuturisha vikundi na waumini mbalimbali wakati wa mfungo wa ramadhan.

'' kwakuwa muziki wa injili pia unaeneza amani na upendo kwa jamii ya watanzania, Hii itasaidia kupunguza gharama za uandaaji, jambo ambalo kwa namna moja au nyingine litakuwa linarahisisha uandaaji wa matamasha hayo ambayo yamekuwa ni chachu ya watu kuachana na maovu na kuwa watu wema katika jamii'',alisema Mabula.
01
Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akiimba pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama kulia na mwimbaji wa muziki wa injili Bonny Mwaiteje katikati na Mwimbaji Chengula kushoto wakati wa tamasha la uzinduzi wa Albam ya Shikilia Pindo la Yesu uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mwishoni mwa wiki akisindikizwa na waimbaji malimbali wa muziki huo akiwemo Ephraimu Sekereti kutoka nchini Zambia.
5
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bwa. Alex Msama akigawa albam ya Rose Muhando kwa Mh. Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula na Maaskofu waliohudhuria kwenye uzinduzi huo.
6
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza machache katika uzinduzi huo. 
2
Meya wa jiji la Mwanza Mhe.Stanslaus Mabula kulia akiwa amesimama na Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion wakati wa uzinduzi huo kutoa kulia ni waimbaji Chengula Bony Mwaiteje , Tumaini Njole na Rose Muhando.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images