Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

WENGI WAJITOKEZA KATIKA BANDA LA UTT ASSET MANAGEMENT

$
0
0
Ofisa Mwendeshaji Mafunzo  UTT Asset Management, Hilder Lyimo (kulia),  akitoa maelezo kwa mwananchi aliyefika katika banda la UTT jinsi mifuko ya Uwekezaji wa pamoja inavyoweza kumpa fursa ya kushiriki katika Masoko ya Fedha na Mitaji ili kukuza pesa zake. 
Ofisa Mwendeshaji wa UTT Asset Management, Ahmed Salmin Mabrouk akielezea faida za kuwekeza katika mifuko ya uwekezaji wa pamoja inayoendeshwa na utt asset managenet  kwa wananchi waliotembelea banda lao katika viwanja vya Nanenane  Lindi.
Hekaheka za wananchi zikiendelea wakati wanajaza fomu za kujiunga na mifuko ya UTT Asset Management huku wakisaidiwa na maofisa wa taasisi hiyo.


MH. PINDA AFUNGA MAONYESHO YA NANENANE KANDA YA ZIWA JIJINI MWANZA

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea tuzo ya Kilimo Kwanza kutoka kwa Yusuf Sinare Yusuf ambayo imetolea na Baraza la Taifa la Kueneleza Wakulima (ACT) kwa niaba ya wakulima, wafugaji na wavuvi nchini katika monyesho ya wakulima Nanenane yaliyofanyika kikanda na kufungwa na Waziri Mkuu jijini Mwanza August 8, 2014.
Waziri Mkuu, izengo Pinda akitazama batamzinga kwenyebanda la wilaya ya Ukerewe katika maonyesho ya wakulima Nanenane ya kanda ya ziwa yaliyofanyika jijini Mwanza August 8, 2014 na kufungwa na Waziri Mkuu. 

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAZINDIUA MSIMU WA FIESTA 2014

$
0
0
Mmoja wa wasanii watakaotoa burudani katika matamasha ya mwaka huu ya Serengeti Fiesta, Vanessa Mdee akizungumza wakati wa uzinduzi wa  tamasha la muziki la mwaka huu la Serengeti Fiesta litakaloanza kutimua vumbi leo katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapo. Kushoto kwake ni Meneja wa Bia ya Serengeti, Rodney Rugambo na mmoja wa waratibu wa tamasha hilo, Sebastian Maganga . 

Fiesta ya mwaka huu inadhaminiwa na kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager. Baadhi ya wasanii watakaotumbuiza katika onyesho la leo ni, Diamond Platinum, Ommy  Dimpos, Linah, Chenge, Temba, Shilole, Ally Kiba, Mr. Blue, Mwana FA, Young Killer, Ben Pol, Christian Bella, Roma, Ney wa Mitego, Mkubwa na wanae, Barnaba, Belle 9, Rachel na Madee. 

MARAIS WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA WA WAWEKEZAJI MAREKANI

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Marais wa nchi za Jumuiya ya Mashariki, Mhe Paul Kagame wa Rwanda, Mhe Yoweri Museveni wa Uganfda, Mhe Uhuru Kenyatta wa Kenya na MhePierre Nkurunzinza wa Burundi wakati wa mkutano wao na wawekezaji wa Kimarekani uliofanyika katika makao makuu ya chama cha wafanyabiashara (US Chamber of Commerce) jijini Washington DC. PICHA NA IKULU

AJALI ENEO LA AFRIKANA, MBEZI BEACH MCHANA WA LEO

$
0
0
 Gari aina ya Nissan Hard Body yenye Namba za Usajili T 524 ALW likiwa limetupwa mtaroni na trela la lori (halipo pichani) ambalo lililigonga gari hilo na kutumbukia mtaroni eneo la Afrikana Mbezi Beach Mchana wa leo. Katika Ajali hiyo iliyohusisha Lori na gari aina ya Nissan Hard Body hakuna mtu yoyote aliyepoteza Maisha
 Wananchi wakisaidia Kulifunga minyororo gari aina ya Nissan Hard Body ambayo imetumbukia mtaroni mara baada ya Kugongwa na trela la lori (halipo pichani) mchana wa leo katika Eneo la Mbezi Afrikana

Wananchi wakisaidia kuligeuza gari ndogo aina ya Nissan Hard Body iliyotumbukia mtaroni eneo la Afrikana Mbezi Beach mara baada ya Kugongwa na trela la lori (halipo pichani) mchana wa leo, katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha. Picha zote na Josephat Lukaza Wa Lukaza Blog

NHIF yaibuka Mshindi wa kwanza Nane Nane Kitaifa

$
0
0
 Makamu wa Rais Dk. Mohamed Ghalib Bilal akiwa na ngao ya ushindi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ambao uliibuka kuwa mshindi wa kwanza katika sekta ya Mifuko wa Hifadhi ya Jamii, anayejiandaa kuipokea ni Meneja wa NHIF Mkoa wa Lindi, Fortunata Raymond.
 Meneja wa NHIF Mkoa wa Lindi, Fortunata Raymond akionesha ngao ya ushindi baada ya kuipokea.
 Ofisa Matekelezo wa NHIF Mkoa wa Lindi, Paul Marenga akitoa elimu ya umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii kwa wananchi waliofika katika banda la NHIF.
 Ofisa Matekelezo wa CHF, Nicolous Mwangomo akitoa darasa kwa wananchi waliozunguka banda la Usajili wa wanachama wa CHF.

MAGUFULI AKAGUA UJENZI WA KIVUKO CHA MSANGAMKUU (MV. MTWARA), DARAJA LA KIGAMBONI PAMOJA NA UKARABATI WA KIVUKO CHA MV. KIGAMBONI

$
0
0
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli leo amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni ambalo ujenzi wake utakamilka ifikapo Juni mwaka 2015.

Awali, Dkt.Magufuli alianza kwa kukagua ujenzi wa kivuko kipya cha Msanga Mkuu maeneo ya Kurasini, kivuko hiki kinajengwa na mkandarasi mzalendo na kitakamilika ndani ya kipindi cha miezi miwili.

Aidha, Waziri wa Ujenzi amefanya ukaguzi wa ukarabati wa matengenezo makubwa ya kivuko cha MV.Kigamboni huko Kigamboni, ukarabati huo unafanywa na Wakandarasi Wazalendo kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania - Kamandi ya Jeshi la Majini. 

Kivuko cha MV.Kigamboni kilijengwa mwaka 2009 na kwa taratibu za vivuko vinavyofanya safari zake katika maji ya chumvi hutakiwa kufanyiwa ukarabati mkubwa kila baada ya miaka mitano. 

Hata hivyo, Dkt.Magufuli amewahakikishai wananchi wa Kigamboni kuwa mwaka wa fedha 2014/15 Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 3.7 kwa ajili ya kununua kivuko kipya kitakachofanya safari zake maeneo ya Kigamboni.

Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wa kwanza kulia akipewa maelezo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe kuhusu ujenzi wa kivuko cha Msanga Mkuu(MV Mtwara) kilicho katika hatua za mwisho za matengenezo chini ya Kampuni ya Sangoro Marine Transpot Limited. 

Luteni Kanali Abel Gwanafyo akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu ukarabati wa Kivuko cha MV. Kigamboni kinachofanyiwa ukarabati na Jeshi la Wananchi wa Tanzania kupitia kikosi cha Wanamaji (Nav) Kigamboni jijini Dar es Salaam. 

Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoka katika kivuko cha MV. Kigamboni mara baada ya Ukaguzi. 

WABUNGE MASHABIKI WA YANGA WAONYESHANA UBABE NA WENZAO WA SIMBA

$
0
0
 Kikosi cha timu ya Wabunge mashabiki wa Yanga kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao na Wabunge mashabiki wa Simba. 
Beki wa timu ya Wabunge wa Simba, Wiliam Ngeleja akichuana na mshambuliaji wa Wabunge wa Yanga, Mwigulu Nchemba.
Mshambuliaji wa timu ya Wabunge mashabiki wa Yanga, Ridhiwan Kikwete (kushoto), akimtoka beki wa timu ya Wabunge mashabiki wa Simba, Adam Malima katika mchezo wa Matumaini uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Mashabiki wakifuatilia mchezo huo.(Picha zote na Francis Dande)

HAFLA YA MEET AND GREAT YAFANA NDANI YA UFUKWE WA CLUB YA JEMBE NI JEMBE JIJINI MWANZA.

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Bwa.Joseph Kusaga a.k.a Joe sambamba na Mkurugenzi wa kampuni bingwa ya Burudani hapa nchini,Prime Time Promotions ,Bi Juhayna Kusaga ambao ndio waandaaji wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 wakiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL),Bwa.Ephraim Mafuru  ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo wakiwa ndani ya hafla ya Meet&Great ya Wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya (watakaoshiriki tamasha la fiesta) na wadau wengine ndani ya Ufukwe wa Club ya Jembe ni Jembe,ilioko nje ya mji wa Jiji la Mwanza.

Tamasha la Serengeti Fiesta linatarajiwa kuzinduliwa leo ndani ya uwanja wa CCM Kirumba,huku Wasanii mbalimbali wakiwa wamekwishawasili tayari kwa onesho hilo ambalo linasubiriwa kwa hamu kubwa na Wakazi wa jiji hilo la Miamba.
 Baadhi ya Wasanii bongofleva na Wadau wengine mbalimbali wa muziki wakiwa wamujumuika kwa pamoja kwenye hafla ya meet&great iliyofanyika usiku wa kumkia leo kwenye kiota cha maraha cha Jembe ni Jembe,jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2014,pichani kulia Sebastian Maganga akiwa na baadhi ya Watangazaji wa Clouds FM,kwenye hafla hiyo ya Meet&Great.Pichani shoto ni B Dozen,Nikson pamoja na Millard Ayo.
Baadhi ya Wasanii watakaoshiriki tamasha la Fiesta wakiwa wamejichanganya na wadau wengine wakibadilishana mawazo na kufahamiana pia.PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

NEWS ALERT: Kibonde wa Clouds FM atiwa mbaroni leo

$
0
0
Mtangazani Mahiri wa Redio 88.5 Clouds FM kupitia kipindi cha Jahazi, Ephrahim Kibonde akipingana na Askari wa Usalama barabarani wakati alipotakiwa kutii sheria bila shurti,mapema asubuhi hii jijini Dar es salaam.

Kibonde anadaiwa kusababisha ajali asubuhi hii eneo la Makumbusho, ikiwa gari aliyokuwa akiendesha kuigonga gari ya dereva mwingine kwa nyuma. Trafiki walifika eneo la tukio na kupima ajali, Kibonde alipoona hivyo akarudi nyuma na kuendesha gari lake kuondoka eneo la tukio bila kufuata taratibu za usalama barabarani,hali iliyomlazimu yule Trafiki katumia gari lililogongwa kumfukuzia. 

Walifanikiwa kumkamata eneo la Mwenge na Trafiki aliingia katika gari lake na kumwomba arudi eneo la ajali ili wakapime na kuchora mchoro wa ajali. Kibonde aligoma na kumtaka trafiki ashuke katika gari lake,Trafiki naye hakutana kufanyi kwa maana ya kuwa aligoma kushuka na kumuamuru Kibonde arudi eneo la tukio. 

Kibonde aliondoa gari na kuendelea na safari yake huku yule Trafiki akiwa ndani ya gari hiyo, Trafiki aliwasiliana na wenzake ambao walianza kuifuatilia gari hiyo ya Kibonde kama walivyopewa maelekezo na mwenzao aliopo ndani ya Gari hiyo.

Mara Kibonde akatokea maeneo ya mataa ya Ubungo, hapo kulikuwa na Trafiki mwingine aliyekua eneo hilo akaipiga mkono gari ya Kibonde na ambapo inasemekekana hakusimama na badala yake ikaja gari nyingine na kuichomekea kwa mbele na hapo ndipo alipotiwa mbaroni! Aligoma kuendesha gari ikabidi livutwe hadi polisi Urafiki na yeye kuwekwa chini ya ulinzi na baadae akahamishiwa Kituo cha Oystabay ambako yupo mpaka sasa.

Inadaiwa kuwa Kibonde alikuwa amelewa,hali iliyopelekea kufanya hayo yote ikiwa ni pamoja na kuwajibu vibaya Askari hao.

Prof. Gabriel afunga Kambi ya Kimataifa ya Vijana ijulikanayo kama International Youth Fellowship jijini dar

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akitoa hotuba wakati wa kufunga Kambi ya Kimataifa ya Vijana International Youth Fellowship (IYF) katika Ukumbi wa Milimani City leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akipokea tuzo kwa niaba ya Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kama waziri mwenye dhamana ya kusimamia masuala ya Vijana kutoka kwa Meneja wa IYF kanda ya Chungcheong China Bw. Jung Soo Park wakati wa kufunga Kambi ya Kimataifa ya Vijana katika Ukumbi wa Milimani City leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akizungumza na Makamu Mwenyekiti kutoka kampuni ya Acona .Bw. David K.S. Kim wakati wa kufunga Kambi ya Kimataifa ya Vijana katika Ukumbi wa Milimani City leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (watatu kulia) akipeana mikono na Makamu Mwenyekiti kutoka kampuni ya Acona Bw. David K.S. Kim baada ya mazungumzo wakati wa kufunga Kambi ya Kimataifa ya Vijana katika Ukumbi wa Milimani City leo Jijini Dar es Salaam. Wakwanza kulia ni Mwenyekiti wa IYF Tanzania Dr. Kansolele Ntevi, na wapili kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Vijana Dr. Kisui S. Kisui, wakwanza kushoto ni Makamu wa Rais kutoka kampuni ya Acon Bw. Wan Gi. Kim na anayefuatia ni Rais wa kampuni ya Uhandisi na Ujenzi kutoka Korea Bw. KI TAE, KIM.
Baadhi ya Vijana kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania na nje ya nchi wakifuatilia kwa makini matukio yaliyokua yakiendelea wakati wa kufunga Kambi ya Kimataifa ya Vijana katika Ukumbi wa Milimani City leo Jijini Dar es Salaam.
Vijana kutoka Graciosas Kwaya kutoka Korea wakitoa burudani wakati wa kufunga Kambi ya Kimataifa ya Vijana katika Ukumbi wa Milimani City leo Jijini Dar es Salaam. Picha zote na Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikalini - WHVUM

WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA YASHIRIKI KIKAMILIFU MAONESHO YA WAKULIMA NANE NANE KITAIFA MKOANI LINDI

$
0
0
Naibu Katibu mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Maria Bilia akiwa anatembelea mabanda ya maonesho.


Naibu Katibu mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Maria Bilia akipiga picha ya pamojanaViongozi mbalimbali waserikali katika maonyesho ya Nanenane 2014, Lindi.

Naibu Katibu mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Maria Bilia akipokea zawadi baada ya kutembelea mabanda.
Naibu Katibu mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Maria Bilia akiwa anatembelea mabanda ya wadau.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Rais Kikwete atembelea Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (Bush Presidential Library) mjini Dallas,Marekani

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete walitembelea Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (Bush Presidential Library) na kujionea nafasi kubwa iliyotolewa kwa Tanzania na zawadi ambazo Rais Bush alizipata katika ziara yake rasmi ya Tanzania wakati akiwa Rais wa Marekani. Maktaba hiyo ya kuvutia inaendeshwa kwa teknolojia ya kisasa kabisa ya habari na mawasiliano.

Rais Kikwete alikuwa amesimama mjini Dallas kwa muda akiwa njiani kutoka Washington D.C., kwenda Houston, jimbo hilo hilo la Texas kuhudhuria mkutano wa wafanyabiashara wa mafuta na gesi ambao wanataka kuwekeza katika sekta hiyo katika Tanzania.

Rais Kikwete amekuwa katika Marekani kwa ziara ya kikazi ya siku tisa, ambako miongoni mwa mambo mengine, amehudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Marekani na Afrika uliofikia kilele chake jana kwa kikao kilichoendeshwa na Rais Barack Obama wa Marekani katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani mjini Washington D.C.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (Bush Presidential Library) sehemu ambayo imejengwa kwa mfano wa Ikulu ya Marekani, White House, hususan katika bustani ya Waziri (Rose Garden) pamoja na ofisi ya Rais wa Marekani, Oval office.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea na kujionea vitu mbalimbali ambavyo Rais mstaafu George W. Bush alipewa kama zawadi kutoka Tanzania ambavyo vimehifadhiwa katika Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (Bush Presidential Library).
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea sehemu ya mfano wa ofisi ya kupangia mikakati ya Ikulu ya Marekani iliyotumika na Rais MStaafu George W. Bush kwenye Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (Bush Presidential Library). PICHA NA IKULU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitoka kwenye Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (Bush Presidential Library).

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL MGENI RASMI MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE KITAIFA MKOANI LINDI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Waziri wa Kilimo Maendeleo ya chakula na Ushirika, Eng. Christopher Chiza, na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Lindi wakati akitembelea katika Mabanda ya Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo Mkoa wa Lindi, jan Agosti 8, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea baadhi ya mashamba ya mfano kujionea kilimo cha umwagiliaji wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho katika Kilele cha sikukuu ya Wakulima Nanenane iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo, mkoani Lindi jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia jambo na Mbunge wa Kilwa Murtaza Mangungu, wakati walipokutana kwenye viwanja vya Ngongo katika maonesho ya sikukuu ya wakulima Nanenane iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo, mkoani Lindi jana Agosti 8, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea Jarida la Kilimo la Nanenane kutoka kwa Iman Kajula, kwa ajili ya kuzinduliwa wakati wa Kilele cha Sikukuu ya Wakulima Nanenane iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo, Mkoani Lindi jana Agosti, 8, 2014.

OFISI YA WAZIRI MKUU WAIBUKA KIDEDEA KWA WIZARA ZA SERIKALI NANE NANE, 2014

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu(Uhusiano na Uratibu) Mh. Stephen Wasira akimkabidhi Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Ofisi ya Waziri Mkuu , Bw. Issa Nchasi, kombe na cheti cha mshindi wa Pili katika kundi la Wizara za Serikali kwenye Sherehe za Sikukuu ya Wakulima Nane Nane, 2014 zilizofanyika kwenye Uwanja wa Nzuguni Dodoma.
Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifurahi mara baada ya kukabidhiwa kombe la mshindi wa Pili katika kundi la Wizara za Serikali kwenye Sherehe za Sikukuu ya Wakulima Nane Nane, 2014 zilizofanyika kwenye Uwanja wa Nzuguni Dodoma.
Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa kombe na cheti cha mshindi wa Pili katika kundi la Wizara za Serikali kwenye Sherehe za Sikukuu ya Wakulima Nane Nane, 2014 zilizofanyika kwenye Uwanja wa Nzuguni Dodoma.

Wadau David Kapungu na Vailet Ndimbo wameremeta

$
0
0
Maharusi David Kapungu (kushoto) akiwa na mkewe Vailet Mateso Ndimbo mara baada ya kufunga ndoa katika kanisa la Mt Kilian mjini Mbinga na kufuatiwa na sherehe iliyofanyika katika ukumbi wa kahawa club mjini Mbinga.
Maharusi David Kapungu na Vailet Mateso Ndimbo wakinyweshana champen wakati wa sherehe yao ya kuwapongeza mara baada ya kufunga ndoa katika kanisa la Mt Kilian Mbinga mjini na kufuatiwa na sherehe ya kuwapongeza iliyofanyika katika ukumbi wa kahawa club mjini humo ,maharusi wote ni wafanyabiashara.

MAMA MARIA NYERERE AWAOMBA WAKE WA VIONGOZI KUENDELEA KUIOMBEA NCHI IENDELEE KUWA NA AMANI NA MAENDELEO

$
0
0
Mama Maria Nyerere akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wana kikundi cha (NEW MELLENIUM WOMEN GROUP) ambao ni wake wa viongozi kushoto ni Mke wa Waziri wa Utalii na Maliasili Faraja Kota kulia ni Mke wa Waziri wa Ulinzi na jeshi la Kujenga Taifa Mariam Mwinyi walifika nyumbani kwake Msasani kumtembelea nakumjulia hali kutokana na mchango wake mkubwa ambao aliutoa katika kumsaidia Baba wa taifa Mwalimu Juliasi Nyerere kuwaongoza Watanzania nakudumisha amani na upendo kwa makabila yote ya Tanzania.
Mama Maria Nyerere akifurahia jambo na Mariam Mwinyi ambaye ni Mke wa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mariam walifika Msasani na wenzake wake wa viongozi kumjlulia hali Mama Maria Nyerere.Picha na Chris Mfinanga

MAKAMU WA RAIS DK. BILAL NDANI YA TAMASHA LA MATUMAINI 2014

$
0
0
Makamu wa Rais wa Tanzania, Mohamed Ghalib Bilal amelipongeza wazo la Tamasha la Usiku wa Matumaini lililoandaliwa na Kampuni ya Global Publishers, jana kuwa ni zuri.

Alimpongeza Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo kwa kuandaa tamasha hilo kwani linaunganisha Watanzania wote.
Mgeni rasmi katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014, Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Ghalib Bilal akitoa hotuba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd ambao ndiyo waandaaji wa Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014, Eric Shigongo naye akitoa neno la matumaini kwa maelfu ya Watanzania waliofurika Uwanja wa Taifa, Dar.
Mgeni rasmi Dk. Ghalib Bilal akikakua timu ya wabunge wa Simba.
Dk. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na wabunge wa Yanga.
Dk. Mohammed Gharib Bilal akiongea jambo na refa wa mchezo wa mechi ya wabunge akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa GlobalEric Shigongo.

Maofisa wa kuwasili nchini kesho

$
0
0
Maofisa wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) wanawasili nchini kesho (Agosti 10 mwaka huu) kuangalia jinsi mchezo huo unavyoondeshwa nchini.

Ujumbe huo wa FIFA utakaokuwa na maofisa sita, baada ya ziara yake utashauri jinsi ya kuboresha uendeshaji huo katika kikao cha pamoja kati yake na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kitakachofanyika mwishoni mwa wiki ijayo.


BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO

SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

KONGAMANO LA KWANZA LA TANZANIA DIASPORA INITIATIVE KUFANYIKA AUGUST 14 - 15,2014 JIJINI DAR

Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images