Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109594 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU PINDA AWASILI MWANZA KUFUNGA MAONYESHO YA NANENANE

0
0
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mwanza, Dr. Anthony Diallo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza  August 7, 2014  ambako anatarajiwa kuwa  mgeni rasmi katika kilele cha sherehe za wakulima Nanenane mjini Mwanza August 8, 2014.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi, Evarest Ndikilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula  na Ushirika, Erasto Zambi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege  wa Mwanza August 7, 2014 ambako August 8,2014 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika  kilele cha sherehe za  wakulima Nanenane  jijini Mwanza . Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mwanza, Dr. Anthony Diallo na kulia ni mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarest Ndikilo
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na viongozi wa mkoa wa Mwanza baada ya kuwasili kwenye  uwanja wa ndege wa Mwanza  August 7, 2014 kwa  ajili ya kufunga maonyesho ya wakulima Nanenane  jijini Mwanza  August 8, 2014.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarest  Ndikilo kwenye  Ikulu ya Mwanza August 7, 2014 ambako August 8 anatarajiwa kufunga maonyesho ya wakulima Nanenane   jijini Mwanza August 8, 2014.

BODI MPYA YA BARAZA LA HABARI YAZINDULIWA

0
0
codes:
Jaji Kiongozi Shaban Ally Lila akihutubia katika uzinduzi wa Bodi mpya ya Baraza la Habari Tanzania kwa niaba ya Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman kwenye Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam, Agosti 7,2014.
 Rais  wa Baraza la Habari aliyemaliza muda wake  Jaji Mstaafu Dk. Robert Kisanga  akihutubia katika uzinduzi wa Bodi mpya ya Baraza la Habari Tanzania ambapo alisisitiza umuhimu wa Baraza la habari na kutaka liungwe mkono kufanikisha malengo yake .Dar es Salaam, Agosti 7,2014.
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Kajubi Mukajanga akizungumza wakati wa kutambulisha Bodi mpya ya Baraza la Habari Tanzania kwenye Hoteli ya Blue Pearl Dar es salaam,Agosti 7,2014.
 Baadhi ya wageni waalikwa na waandishi wa habari wakiwa katika uzinduzi wa Bodi mpya ya Baraza la Habari Tanzania. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

KATIBA HAITAPATIKANA KWA MALUMBANO,MABISHANO WALA MAANDAMANO - KISABYA

0
0
Akiongea na waandushi wa habari Ofisini kwake, NAIBU KATIBU MKUU TAIFA NA KATIBU WA BODI YA CHAMA (NRA), mhe HASSAN KISABYA ALMAS, amewaonya viongozi wenzake wa kisiasa kuacha malumbano na badala yake wajikite kuhakikisha Taifa linapata katiba,

Mhe Kisabya alisema, "mpaka sasa wajumbe wa bunge wanasiasa wamekuwa wakijadili nafasi za kisiasa za utawala na kusahau kuwa kuna mambo mazuri muhimu yanayohusu wananchi"Akitoa mfano kuwa suala la idadi ya SERIKALI ni jambo la kuamua lakini masuala kama Tume huru ya UCHAGUZI, suala la mawaziri kutokuwa wabunge, haki za binadamu,mahakama huru,kupungua kwa madaraka ya Rais , matokeo Rais kupingwa mahakamani na haki ya umiliki wa ardhi, haki za wakulima na mengine mengi ni baadhi ya mambo muhimu kwa ukuaji wa demokrasia na maendeleo ya wananchi, mhe Kisabya alishauri kuwa suala la Katiba ni suala nyeti hivyo viongozi wenzake wa vyama walichikulie kwa umakini na kulipa uzito wa kipekee.

Ndugu Kisabya aliongeza kuwa , ikiwa Katiba hii itakwama basi watanzania wajipange kuwaadhibu baadhi ya wanasiasa kwa kuwanyima kura katika chaguzi zijazo,"ikiwa sisi wanasiasa Ndio tuliokuwa kila siku tunadai katiba iweje Leo Sie Ndio tuwe mstari wa mbele kugomea, ama sivyo hatukuwa wamoja katika kudai katiba Bali wengine walikuwa na ajenda zao"
Mhe kisabya alisema, kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya Katiba inaelekeza kuwa ,iwapo katiba hii mpya itakwama basi tutarejea kuongozwa na katiba ya mwaka 1977;katiba ambayo tumekuwa tikiikataa kuwa inatunyiwa wigo wa kidemokrasia.

Mbali na taarifa pia mhe kisabya aliwaeleza wanahabari kuacha kuiandikia mabaya ya Tanzania na kuvisifia vyama vya siasa kwa kuwa Hakuna chama nje ya taifa, na vyama vinaweza kuondoka ila taifa litabaki ,hivyo hakuna chama kinaweza kuwa na umaarufu kuliko taifa, na kusisitiza kuwa NRA inaamini kuwa sera yake ya Taifa Kwanza vyama baadae ni msingi wa AMANI ya taifa hili, kwani wao wapo tayari kukosa nafasi za utawala ilimradi Usalama,umoja wa taifa na mshikamano wa watanzania na utulivu wa Taifa ubakie imara.

Kuhusu, CHAGUZI ZIJAZO, NRA wamejipanga kusimama katika chaguzi za SERIKALI za mitaa na chaguzi Kuu ya mwaka2015 katika nafasi zote za udiwani, ubunge na Urais kwa kusimamisha watu Makini wanaokubalika na wananchi.alisema, NRA inategemea kuvuma watu maarufu kuelekea 2015 watakaogombea nafasi mbali mbali. 

Pia mhe kisabya, aliwaeleza wanahabari kuwa NRA , itaandaa kumbukumbu ya kuwaenzi waasisi wake, Hayati Prof. Kighoma Ali Malima na Hayati Aboubakar Ulotu ,maandalizi yake yanaendelea.

Mhe kisabya, alimalizia kwa kuwataka wabunge wengine walio nje ya bunge kurejea bungeni kumalizia kazi waliyoianza vizuri ,na kuwasisitiza kuwa wanayo nafasi ya kusimamia fikra zao wakiwa bungeni na watanzania watawasikia ili kupata mwisho mzuri, alisema nchi haitapenda kuona damu za watanzania zikimwagika kwa ajili ya katiba hii Bali katiba hii iwe ni chanzo cha maendeleo amani na utulivu wa taifa.

Guardian and Daily News journalists to participate at the Nile Basin Journalist training in Entebbe, Uganda

0
0
United States Embassy Public Affairs Officer (PAO) Ms. Marissa Maurer (right), presents tickets to Tanzanian journalists, Ms. Beatrice Philemon (left), a journalist with the Guardian Newspaper and Mr. Ludovick Kazoka (center), a journalist with Daily News, who will participate at the Nile Basin journalist training to be held in Entebbe, Uganda from August 10 - August 15, 2014 under the Development and International Media Training.
Ms. Philemon and Mr. Kazoka will join 21 other journalists from Egypt, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Sudan, South Sudan, Uganda, Burundi, and Democratic Republic of Congo, to participate in the program focusing on the technical/scientific aspects of reporting on water resources – especially trans boundary waters – in order to promote more, and more accurate, reporting throughout the Nile Basin on these issues. In addition to the technical substance, it will aim to develop collaborative relationships among journalists from various Nile countries. The workshop will be followed by a 12-month mentoring period during which journalists will receive support and advice on story development.
Commenting on the program during a pre-departure orientation with PAO Ms. Maurer at the U.S. embassy in Dar es Salaam recently, Ms. Philemon and Mr. Kazoka mentioned that, the training would be helpful in enhancing their journalistic competence in key areas like reportage and feature writing on water and environmental issues so that people can be aware on how to keep the river’s environment clean and addressing the problems caused by illegal dumping, the discharge of industrial and domestic effluence into the River and that Tanzanian community be part of the global campaign on climate change mitigation across the country and environmental conservation. In addition, when back home they will share the knowledge with colleagues at work. (Photo Courtesy of the United States Embassy).

Wanasayansi Duniani kukutana Dar es salaam katika kongamano la 25 la Wajiolojia

0
0
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST ) na Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya makongamano ya Wajiolojia Afrika na wanasayansi vijana Duniani, Profesa Abdulkarim Mruma (katikati) akisisitiza jambo wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu kongamano la 25 la Wajiolojia Afrika na mkutano wa tatu wa vijana wanasayansi kutoka nchi mbalimbali duniani. Makongamano hayo yanatarajiwa kufanyika tarehe 11- 16 Agosti, 2014 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud. Wengine, kwanza kulia ni Mwenyekiti wa mtandao wa Vijana wanasayansi kwa upande wa Tanzania Steven Nyagonda, Rais wa Vijana wanasayansi Duniani Meng Wang na Katibu wa Kamati ya Maandalizi, Profesa Nelson Boniface.
Rais wa Wanasayansi Vijana duniani, Meng Wang (wa pili kulia) akiongea jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuelezea kuhusu mkutano wa tatu wa wanasayansi vijana kutoka nchi mbalimbali duniani, kulia ni Mwenyekiti kongamano la vijana wanasayansi upande wa Tanzania Steven Nyagonda, wengine wanaosikiliza ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) na Katibu wa kamati ya maandalizi, Profesa Nelson Boniface.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali, Wizara ya Nishati na Madini Badra Masoud akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wakitoa taarifa kuhusu kufanyika kwa kongamano la 25 la Wajiolojia Afrika na kongamano la tatu la wanasayansi vijana kutoka mataifa mbalimbali duniani. Kushoto ni Michael Msambi mjumbe wa kamati ya maandalizi na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) na Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya makongamano hayo, Profesa Abdulkarim Mruma (kulia).

WANAFUNZI WA SEKONDARI YA WASICHANA MAKETE WATAKIWA KUWA MFANO BORA KIELIMU NA KITABIA

0
0
Na Edwin Moshi,Makete.

Wanafunzi wa kike wanaosoma katika shule pekee ya wasichana iitwayo Makete girls secondary School iliyopo wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kuzingatia masomo na kuwa mfano bora wa kuigwa toka shuleni hadi sehemu wanazotoka

Aidha kwa kufanya hivyo kutapelekea wafaulu vizuri masomo yao na kuhakikisha lengo la serikali kuanzisha shule hiyo linafikiwa hasa kuinua kiwango cha ufaulu kwa wasichana katika wilaya hiyo

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro wakati alipofanya ziara katika shule hiyo hii leo kwa lengo la kujionea maendeleo na changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo ili zitafutiwe ufumbuzi ikizingatiwa shule hiyo ni mpya, ambapo akiwa shuleni hapo pamoja na mambo mengine amekula chakula cha mchana na wanafunzi hao

Akizungumza na wanafunzi hao Mh. Matiro amewataka wanafunzi hao kuepuka wanaume walaghai ambao hutumia njia mbalimbali kuwarubuni hasa wanaporudi majumbani mwao wakati wa likizo na kusema kuwa hategemei tatizo la ujauzito kuwakumba wanafunzi hao endapo watakuwa msimamo wa kuzingatia masomo tu

"Tunategemea shule hii iwe ya mfano na ninyi ndio wenye uwezo wa kuifanya hivyo, hii shule ni mpya na ninyi ndio wanafunzi wa kwanza kusoma hapa, tunategemea mfaulu vizuri, sisi tunajitahidi kwa kila namna kuboresha shule hii, ninyi kazi yenu ni kusoma tu, acheni mzaha someni kwa bidii, kila jambo na wakati wake, wakati mlio nao sasa ni wa kusoma tu na si vingine" amesema Matiro
 
Kwa upande wa wanafunzi hao akiwemo Prisila Haule, Jema Kyando na Florida Ngogo wametaja changamoto zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa vifaa vya michezo, ukosefu wa waalimu wa sayansi, shule kukosa gari, pamoja na shule kukosa matroni.

Mkuu wa shule hiyo Bi. Sayuni Sanga amesema ni kweli shule ina wajibu wa kumuajiri matroni lakini kwa sasa haiwezi kufanya hivyo kwa kuwa shule hiyo ni changa na haina uwezo wa kumlipa ila kwa sasa mwalimu mmoja amejitolea kuwa matroni hadi hapo atakapopatikana matroni halisi

Kuhusu michezo mwalimu wa michezo shuleni hapo Bw. Japhet Mwile amesema wanashindwa kuainisha maeneo ya viwanja vya michezo kutokana na maeneo hayo kuwa na mazao ambayo hayajavunwa na kwa sasa wanasubiri yakishavunwa waanze kuandaa viwanja kwa kuwa walikubaliana na wazazi kuwa wakishavuna mazao yao hawatalima tena mashamba hayo kwa kuwa kwa sasa ni mali ya shule

Shule hiyo imeanza rasmi Aprili 22 mwaka huu na ina wanafunzi 36 na walimu wanne, huku changamoto kubwa inayoikabili shule hiyo ni ukosefu wa mabweni ambapo serikali imeahidi kupambana kuitatua changamoto hiyo kwani kwa sasa wanafunzi hao wanalala madarasani.
 Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akizungumza na wanafunzi wa Makete Girls Sekondari (hawapo Pichani)
Maktaba ya shule hiyo.
 Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi na walimu wa shule hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro (wa tatu kushoto) akiwa na walimu wa shule hiyo, wa kwanza kulia ni Afisa Taaluma sekondari wilaya hiyo.

Salam za Nane Nane kutoka Rahman Nursery School,Segerea jijini Dar

0
0
Shule ya chekechea na madrasa  Rahman ya Segerea jijini Dar-es-salam inatoa salam za sikuu ya Nane Nane kwa wadau na waTanzania wote.
Karibuni sana tupo segerea mwisho.

RWANDA AWARDS 50 MW METHANE GAS TO ELECTRICITY PROJECT ON LAKE KIVU TO U.S. SYMBION POWER

0
0
During the U.S. Africa Head of State Summit this week in Washington, D.C., the Government of Rwanda’s Energy Water and Sanitation Authority (EWSA) awarded Symbion Power a 50 megawatt Independent Power Production (IPP) project using methane gas from Lake Kivu, it was announced today by Paul Hinks, Chief Executive Officer, Symbion Power.

Symbion will build, own and operate a 50 MW power station by constructing gas extraction facilities to lift, separate, and process methane gas, which is dissolved in the deep waters of Lake Kivu, and then deliver it to an on-shore generating facility located at Cape of Busororo in the Nyamyumba area of Rwanda.  Lake Kivu contains 300 km3 of dissolved carbon dioxide and 55 to 60 km3 of methane gas accumulated and trapped at significant depth in the lake.  

"We're very excited that with President Obama's recent announcement of tripling Power Africa's goals to now add 30,000 megawatts to sub-Saharan Africa, partners such as Symbion Power are exploring new opportunities in countries like Rwanda where they have never worked before," said USAID Administrator Dr. Rajiv Shah.  "Through this new model of public-private partnership, we can expand opportunity for millions and drive growth at home and abroad."

In a meeting with Symbion’s Mr. Hinks and USAID Administrator, Dr. Rajiv Shah during the African leaders summit, Rwanda’s President Kagame expressed his enthusiasm for the Lake Kivu project and also acknowledged the successful developments that President Obama’s Power Africa initiative has already realized.

Symbion Power is an American company in the electricity generation, transmission and distribution industry with an established presence in Tanzania, Nigeria, South Africa and operations throughout Africa; this is the company’s first project in Rwanda.  Paul Hinks,

Symbion CEO said, “Rwanda is an amazing investment destination.  What President Kagame and his government have achieved over the past 20 years must represent the most incredible example of nation building in recent history.  We have worked towards investing in Rwanda for the past three years and we are delighted by this new development.  We hope other US companies will follow us.”

“Symbion’s IPP project will use Lake Kivu’s methane resources for a commercial benefit for the people of Rwanda, but it will also reduce the risk of an environmental disaster,” said Hinks.  “Without the removal of methane and carbon dioxide, there is a risk of a sudden release of large quantities of these gases with a potentially catastrophic result.”  Rather than just vent the 50-60 km3 of methane, Symbion will use the produced methane for power generation.  The methane gas production will be used to power reciprocating gas engine generator sets producing 50MW in a phased approach.
L to R - Rwanda's President Paul Kagame, USAID Administrator, Dr. Rajiv Shah, Symbion Power CEO, Paul Hinks at the White House Africa Heads of State Dinner.

FOR SALE

0
0
Building structure: Residencial (Sitting room, dinning, kitchen, 2 bedrooms, 2 master bedrooms, public toilet & bathroom, 2 verandas)

Location: Tegeta Mivumoni (Behind Wazo Hill)

Area of the plot: 802 square meters.

Price: 35,000,000/=

Contacts: +255766669271 / nachaliddy@gmail.com

NAPE AZUNGUMZIA MIDAHALO INAYOENDELEA

JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 28

DSTV KUKULETEA MOJA KWA MOJA MECHI YA UFUNGUZI WA LIGI KUU UINGEREZA

Katibu Mkuu kiongozi katika maonyesho ya Nane nane kanda ya kati Dodoma

0
0
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akisalimiana na wafanyakazi waliopo katika maonyesho ya Nane nane katika Jengo la maonyesho la Ofisi ya Rais maeneo ya Nzuguni Dodoma ambapo maonyesho haya yameadhimishwa kwa kushirikisha mikoa ya kanda ya kati.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiangalia baadhi ya Bidhaa zinazotengenezwa na badhi ya wajasiriamali wanaonufaika na mfuko wa maendeleo ya jamii-TASAF (Tanzania Social Action Fund) ndani ya Jengo lamaonyesho la Ofisi ya Rais Nzuguni Dodoma.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akisaini kitabu cha wageni katika Jengo la maonesho la ofisi ya Rais.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katikati akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi waliopo katika jingo la maonyesho nane nane 2014 Ofisi ya Rais Nzuguni Dodoma. Picha na Deusdedit Moshi wa Michuzi Blog Kanda ya kati.

Waziri wa Habari ziarani nchini China

0
0
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenela Mukangala yuko nchini China katika ziara ya kuangalia maendeleo ya Sekta ya Utangazaji na kuimarisha ushirikiano katika sekta ya Utangazaji kati ya Tanzania na China.

Katika ziara hiyo ameongozana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Sihaba Nkinga, Mkurugenzi Mkuu wa TBC Bw. Clement Mshana na Mkurugenzi wa Utangazaji TCRA Bwana Habbi Gunze.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenela Mukangala na ujumbe wake wakitembelea sehemu mbalimbali zikiwemo studio na vivutio mbalimbali vya Utangazaji katika kituo cha Tv cha Jimbo la Sichuan nchini China.

Tanzania and U.S. Sign “Power Africa” MOU Reaffirming Joint Commitments for the Energy Sector

0
0
On the eve of the U.S.-Africa Leaders’ Summit, Tanzanian Minister of Energy and Minerals Professor Sospeter M. Muhongo and the United States Ambassador to Tanzania Mark Childress signed a bilateral Memorandum of Understanding (MOU) for on-going and future U.S. Government support under Power Africa. The MOU signing took place on Sunday, August 3, 2014 at the Tanzanian Embassy to the United States in Washington, DC. Both Minister Muhongo and Ambassador Childress were in Washington, DC for the U.S.-Africa Leaders’ Summit.

The Power Africa MOU reaffirms joint commitments for the energy sector taken under the Partnership for Growth Initiative and expands them to include the full range of U.S. Government inter-agency support to Power Africa and the Government of Tanzania’s own Big Results Now (BRN) Initiative to increase generation capacity and expand access to electricity.

Power Africa in Tanzania is supporting the Tanzanian energy sector through transaction assistance for priority power generation projects, technical advice to release the constraints to private sector investment, and capacity building for key institutions. Transactions for power generation projects currently underway include: the Kinyerezi gas-fired plant in Dar es Salaam which will serve the main grid with a source of cheaper and cleaner energy; a small hydro project that will supply power to Mbeya, and a solar power plant that will provide power to Kigoma and the surrounding area.

The Power Africa Initiative, announced by President Barack Obama in June 2013, is designed to increase access to electricity in sub-Saharan Africa over the next five years beginning in six focus countries: Ethiopia, Kenya, Tanzania, Liberia, Ghana, and Nigeria. A key goal is to add cleaner, more efficient electric generation capacity.

ADMISSION TO VARIOUS PROGRAMMES OFFERED BY THE STATE UNIVERSITY OF ZANZIBAR FOR THE ACADEMIC YEAR 2014/2015

shule ya msingi kibamba yapata kitengo cha wenye ulemavu wa akili

0
0
Kitengo (madarasa) cha wanafunzi wenye ulemavu wa akili, shule ya msingi kibamba. Kitengo kimejengwa na Bw Rupin Rajani wa Rajani Group kupitia DSM Mentally Handicapped Children Support Group.
Kibao kinacho onesha wafadhili wa kitengo hiki.
Bw. Rupin Rajani na wanachama wa DSM Mentally Handicapped Children Support Group nje ya darasa moja wapo.
Bw. Rupin Rajani ndani ya darasa lenye wanafunzi wenye ulemavu wa akili katika shule ya msingi Kibamba, pamoja na waalimu wa elimu maalum na Mama Evelyne DSM Mentally Handicapped Children support Group.

WAKULIMA WATAKIWA KUONGEZA THAMANI YA MAZAO

0
0
Na Woinde Shizza,Arusha

Wakulima wametakiwa kutumia fursa ya kuongeza thamani mazao yao ili waweze kunufaika zaidi kiuchumi kuliko kuuza mazao yao yakiwa ghafi kwani watakuwa wanayonywa na kuzidi kuwa masikini.

Wito huo umetolewa jana na Ofisa masoko wa shirika la Farm Africa, Rahel Pazzia, wakati akizungumza na waandishi wa habari, kwenye maonyesho ya wakulima nane nane, kanda ya kanda ya kaskazini yanayoendelea jijini Arusha.  

Alisema kupitia Farm Africa wakulima wengi wa ufuta wa mkoa huo wamenufaika kiuchumi kutokana na kuongeza thamani mazao yao na kutouza yakiwa ghafi hivyo kujiongezea kipato zaidi kinachowaletea maendeleo.

“Farm Africa inawataka wakulima nchini waje wajifunze kupitia wakulima wetu wa ufuta, hivi sasa wananufaika zaidi kiuchumi kwani badala ya kuuza ufuta, wanaongeza thamani kwa kutengeneza mafuta, kashata, sabuni na kinywaji,” alisema Pazzia.   

Alisema wakulima sita wamefika kwa ajili ya kuonyeshaji mazao ya ufuta na misitu na wakulima 45 wamekuja kujifunza kwa ajili ya kuongeza elimu zaidi na pia kutoa elimu kwa wakulima wengine ili wajifunze kupitia wao.

Naye, Ofisa miradi wa misitu na masoko wa shirika hilo, Hakam Mohamed alisema wanavijiji 33 wa wilaya ya Mbulu na Babati mkoani Manyara, wananufaika kupitia msitu Nou na lengo lao ni kuijengea jamii uwezo zaidi wa kiuchumi.

Mohamed alisema ili kuhakikisha jamii haiharibu msitu huo kwa kuutumia kwa matumizi yasiyo ya mazuri wamebuni miradi ya kurina asali, miche ya miti, kulima uyoga na ususi wa vikapu, ambayo imewanufaisha wote wanayozunguka Nou.

“Tumewawezesha wawe na vicoba, wapate mikopo ili waweze kuibua miradi ambayo itawanyanyua kiuchumi na kutokuwa na wazo baya la kuharibu msitu wa Nou ikiwemo kukata miti kwa ajili ya kupata mbao,” alisema Mohamed.

Kwa upande wake, mkulima wa ufuta wa kijiji cha Ngolei, Costantine Martin alisema kupitia ufuta amenufaika kiuchumi kuliko kulima mahindi kwani gunia moja la kilo 85 anauza sh215,000 huku gunia moja la mahindi likiuzwa sh30,000.

Naye, mrina asali wa kijiji cha Boboa wilayani Mbulu, Philemon Lawrence alisema kupitia shirika la Farm Africa, wameweza kujinufaisha kiuchumi kwa kuwezeshwa kupitia miradi mbalimbali ikiwemo kupatiwa mizinga ya nyuki.
 Ofisa masoko wa shirika la Farm Africa, Rahel Pazzia (kulia) akiwa na baadhi ya wakulima wa ufuta wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara jana, katika banda la Farm Afrika kwenye maonyesho ya wakulima nane nane kanda ya kaskazini, yanayofanyika viwanja vya Themi jijijni Arusha.

Watanzania wenye asili ya bara Asia wakipewa maelezo ya ubora wa mafuta ya ufuta kwenye banda la shirika la Farm Africa, katika maonyesho ya wakulima nane nane kanda ya kaskazini, yanayoendelea kwenye viwanja vya Themi jijini Arusha.

WAZIRI WA UJENZI DK. MAGUFULI AIFAGILIA NSSF UJENZI WA DARAJA LA KIGAMBONI

0
0
WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, ameusifu Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa daraja la Kigamboni.

Ujenzi wa daraja hilo umekamilika kwa asilimia 60 ambapo mpaka sasa NSSF imetoa sh. bilioni 117 kati ya Bilioni 214 zitakazokamilisha ujenzi wa daraja hilo.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam, alipotembelea daraja kuona namna ujenzi unavyoendelea, Dk. Magufuli alisema kuwa ujenzi wa daraja hilo umekutana na changamoto nyingi ikiwemo kina kilichokuwa katikati ya bahari kupoteza malighafi ya ujenzi ambapo wahandisi waliamu kufanya utafiti.

Alisema kuwa juhudi za NSSF  katika kufadhili mradi huo umewezesha changamoto zilizokuwa zikiukabili maradi huo kufanyiwa kazi.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa NSSF, Ludovick Mrosso, alisema kuwa mradi huo unatarajiwa kukamilika Julai, 2015 ambapo katika daraja zitakuwa barabara sita za magari, mbili za wapita kwa miguu.
Maradi huo unajengwa kwa kushirikisha Wizara ya Ujenzi, NSSF na Tanroads. 
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (wa pili kulia) akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni kutoka kwa Meneja wa Mradi wa ujenzi wa daraja hilo, Mhandisi Kareem Mataka, wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja hilo.
 Mh. Magufuli akifafanua akitoa maelekezo kwa Mhandisi Kareem Mataka (kulia).
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (wa pili kulia) akikagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni linalojengwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii  (NSSF), kwa kushirikiana na Serikali. Kulia ni  Meneja Mradi ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Kareem Mataka.
 Waziri akiwa katika zira ya ukaguzi pamoja na maofisa kutoka Wizara ya Ujenzi, NSSF pamoja na waandishi wa habari.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ludovick Mrosso akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MGOGORO WA ZIWA NYASA: WAKATI WENZETU MALAWI WAKIPAMBANA KWA TEKNOHAMA SISI WATANZANIA BADO TUNAPAMBANA KWA MANENO.

0
0
Kaka michuzi naomba unichapishie makala yangu kwenye blog yako. Kama tunavyofahamu kwa wakati huu Tanzania ipo katika mgogoro wa ziwa nyasa kati yetu na Malawi wenzetu wameenda mbali zaidi kwa kutumia mtandao wa Google Map.

Google Map ni mtandao mkubwa ambo unaonyesha Ramani ya dunia nzima kwa kutumia picha ya satellite na watu wengi hususani watalii hutumia mtandao huu kabla ya kwenda mahali husika . Lakini mtandao huu huitaji watu kujaza taarifa zaidi kama kuonyesha mipaka ya mikoa nchi na maeneo mbalimbali. Kama ilivyo kwa nchi nyingine duniani ambao huchukulia jambo ili kwa manani na kulipa kipaumbele lakini hiyo imekua tofauti kwa Tanzania.

Ukiangalia kwenye mtandao huu kwa sasa utaona Ziwa Nyasa linaitwa Ziwa Malawi na pia mipaka inaonyesha mpaka wa nchi ya Malawi upo hadi pembezoni mwa ziwa nyasa kama madai yao yalivyo yaani eneo la Tanzania.

Hii inasikitisha sana kwa sababu serekali imeajiri wataalumu wengi wenye uwezo wa kuzijaza taarifa hizo kwenye mtandao huo na kwenye mitandao mingine duniani kwa ajili ya kulinda tunu za taifa letu lakini hali imekua ni tofauti.

Hii si mara ya kwanza Mali ya Tanzania kufanyiwa hivyo kwa mfano Mlima Kilimanjaro kuna wakati ulionyeshwa au kuta tangazwa kama upo Kenya na pia lugha ya Kiswahili kwa sasa inaandikwa kwenye vitu mbali mbali hususani kwenye programu mbalimbali za computer ambazo zina uchaguzi wa lugha mbalimbali hususani kampuni kubwa ya Microsoft. Hii inaonyesha ni jinsi gani taifa letu lilivyolala na kupigana vita vya maneno tu badala ya kupigana kwa vitendo.

Swala hili ni kubwa ambalo serekali inapaswa kulichukuli hatua kwa sababu kwa sisi tuliopo sasa tunajua kwamba ni upotoshaji lakini kwa vizazi vitakavyokuja miaka mingi ijayo vitaichukulia kama hiyo ni taarifa sahii na hivyo itakuja kuligharimu hata taifa letu la Tanzania

Kwa kupitia makala hii namwomba Rais wa jamuhuri ya Muungano Mh Kikwete kulichukulia swala hili kwa uzito unaohitajika na hata ikiwezekana kufuatilia kwenye kampuni ya Google ili taarifa hizi zibadilishwe maana ni upotoshaji mkubwa.

Pia napenda kuwakumbusha wataalamu wenzangu ambao mmeajiriwa kati wizara mbalimbali husika muwe pia makini na mitandao mbalimbali duniani kujaza taarifa muhimu za nchi yetu kwenye mifumo hiyo, nawaombeni tuwe wabunifu. Ni mimi Mtanzania Emmanuel Millinga Millinga_emmanuel@yahoo.com 0715 817788
Viewing all 109594 articles
Browse latest View live




Latest Images