Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

RAIS KIKWETE AKUTANA NA RAIS WA MALAWI PROFESA PETER MUTHARIKA JIJINI WASHINGTON DC, MAREKANI

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika aliyemtembelea kumjulia hali kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani, ambapo wote walikuwa wamefikia. Rais Kikwete na Rais Mutrharika, ambao walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina ya nchi hizo mbili.
Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika akisalimiana na Mama Salma Kikwete alipomtembelea kumjulia hali Rais Kikwetev kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani, ambamo wote walikuwa wamefikia. Rais Kikwete na Rais Mutrharika, ambao walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina ya nchi hizo mbili.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika wakimsikiliza Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani, ambamo marais hao walikuwa wamefikia. Rais Kikwete na Rais Mutrharika, ambao walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina ya nchi hizo mbili.
Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika akiomngea na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani, alipomtembela kumjulia hali Rais Kikwete. Viongozi hao walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina ya nchi hizo mbili.
Mke wa rais Mama Salma Kikwete akisalimiana kwa furaha na mke wa Rais wa Malawi Mama Getrude Mutharika walipokutana kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani. Rais Kikwete na Rais Mutharika, ambao walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina ya nchi hizo mbili.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika na wake zao, Mama Salma Kikwete na Mama Getrude Mutharika, wakiongea kwa furaha walipokutana kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani. Rais Kikwete na Rais Mutharika, ambao walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina ya nchi hizo mbili. PICHA NA IKULU

PUB BUSINESS FOR SALE @ KINONDONI MANYANYA

$
0
0
Best located at the Busy-Business-Hub ‘Kinondoni’ along Kawawa (former Morocco) road, near NBC Bank Kinondoni Branch, Puma (the former famous ‘Mwanamboka’) Filling Station and Casablanca Bar; the Lounge is uniquely designed, walls well decorated with modern ‘crazy colours’.  Night Club lighting is well done to suite today’s market. It is fully air-conditioned, very well furnished with modern and durable local made furniture which will last many years to come. 

The indoor lounge is fully tiled; the counter is fitted with marble top, plus beautiful paintings on the walls. Three (3) 40’ (inch) flat plasma TV sets fitted on different walls of the indoor lounge. Indoor lounge also has an almost brand new Fully-Equipped-DJ-Music-System in its own DJ room, while the outdoor bar has its own music system. There is a small outdoor counter and a big kitchen fully tiled.

The business is on-going with a good customer base with good sales 7 days a week. The place is rented for Tshs. 550,000/= per month, now already paid up to 31st December, 2014. Existing contract is valid until 2017, renewable.


Phone: 0788 893364
Email: tinogobba2002@yahoo.com

Maonyesho ya Nane Nane jijini Arusha

$
0
0
Ofisa mahusiano wa shirika lisilo la kiserikali la Farm Africa, Goodness Mrema (kushoto) akiangalia uyoga uliohifadhiwa kitaalamu na mkulima wa uyoga wa kijiji cha Bashnet wilayani Babati, Rahabu Manase, kwenye maonyesho ya wakulima nane nane, viwanja vya Themi jijini Arusha jana (katikati) ni Ofisa miradi wa misitu na masoko wa shirika hilo, Hakam Mohamed.
Watanzania wenye asili ya bara la Asia wakinunua mafuta ya ufuta kwenye banda la shirika la Farm Africa, katika maonyesho ya wakulima nane nane kanda ya kaskazini, viwanja vya Themi jijini Arusha jana.
Mtoto wa jijini Arusha akipewa asali alipotembelea banda la shirika la Farm Africa jana kwenye maonyesho ya wakulima nane nane kanda ya kaskazini, yanayofanyika viwanja vya Themi jijini Arusha.

HITIMISHO LA SHINDANO LA ELIMU YA UWEKEZAJI KWA WANAZUONI (DSE SCHOLAR INVESTMENT CHALLENGE) KUFANYIKA AGOSTI 13 2014

$
0
0
Soko la Hisa Dar es Salaam (Dar es Salaam Stock Exchange), kwa udhamini wa benki ya NMB, Selcom na FSDT, linapenda kuwajulisha wanafunzi wa elimu ya juu nchini walioshiriki katika shindano la elimu ya uwekezaji kwa mwaka 2014 (DSE Scholar Investment Challenge 2014) kuwa maandalizi yote ya kuhitimisha shindano hili kwa sasa yamekamilika.


Mchakato wa kutambua nafasi ya kila mshiriki wa shindano umemalizika. Majina ya wanafunzi 50 wanaoongoza katika shindano hilo yamebandikwa katika mtandao wa DSE (www.dse.co.tz) kwenye kipengele cha Investment Challenge.



Sherehe za kuwatambua washindi na kuwapatia vyeti na zawadi zitafanyika tarehe 13 August 2014 jijini Dar es Salaam. Mialiko ya kuhudhuria sherehe hizo inaendelea kutumwa kwa njia ya simu.

 (sehemu ya umati wa wanafunzi walioshiriki katika elimu ya uwekezaji kwenye hisa na masoko ya mitaji nchini iliyoendeshwa na DSE kwa wanazuoni).

Shindano la elimu ya uwekezaji kwa wanazuoni (DSE Scholar Investment Challenge) lilianza tarehe 01/04/2014 na kumalizika tarehe 30/06/2014. Wanafunzi washiriki walipewa nafasi ya kutumia simu zao za mkononi ili kununua na kuuza hisa zinazouzwa katika soko la hisa (DSE) la Dar es Salaam. Kila mshiriki alipewa mtaji (virtual capital) wa shilingi milioni moja. Ushiriki kwa shindano hili ulikuwa ni bure na huru kwa yeyote aliyependa.


Nia kubwa ya shindano hili ni kuwapatia vijana walio katika vyuo vya elimu ya juu nchini fursa ya kuwekeza katika soko la hisa kwa majaribio na kuangalia mitaji yao ikikua. Elimu hii pia ni muhimu katika kujenga utamaduni wa utunzaji fedha na uwekezaji miongoni mwa vijana walio vyuoni (ambao ni viongozi, wawekezaji, wahasibu, wachumi, na washauri watarajiwa).


Washiriki walitegemewa kushindana kukuza mitaji waliyopewa kwa kipindi cha miezi mitatu. Mafanikio ya shindano na elimu hii ni makubwa sana. Mwanafunzi anayeongoza amekuza mtaji wake kutoka shilingi milioni moja aliyopewa na kufikisha shilingi milioni nne (kwa kipindi cha miezi mitatu tu).

DSE inawapongeza zaidi ya wanafunzi 5,000 walioshiriki katika shindano na elimu hii muhimu kwao na taifa kwa ujumla.



Shindano na elimu hii imepangwa kufanyika tena mwakani na kuwahusisha wanafunzi wengi zaidi ya elfu tano walioshiriki mwaka huu. DSE imepanga kuwawezesha wanafunzi na vijana nchini kutumia simu pamoja na intaneti mwakani ili kuwapa uwanja mpana zaidi wa kushiriki. Mipango ya baadaye ni kuwashirikisha wanafunzi walioko kwenye shule za sekondari pia.

President Obama Delivers Remarks at the U.S.-Africa Leaders Summit

TTCL YAZINDUA HUDUMA YAKE MPYA YA BWERERE.

$
0
0
 Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo TTCL,Bwa.Peter Ngota akionesha kipeperushi chenye taarifa mbalimbali kuhusiana na huduma yao mpya iliyojulikana kwa jina la Bwerere,Kwa waandishi wa habari,huduma hiyo imezinduliwa leo kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Ofisi za kampuni hiyo,zilizopo makao makuu mtaa wa Samora Jijini Dar. 
 Baadhi ya Wandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa huduma mpya ya TTCL iliyojulikana kwa jina la Bwerere ,kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Ofisi za kampuni hiyo,zilizopo makao makuu mtaa wa Samora Jijini Dar. 
Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo TTCL, Bwa.Peter Ngota akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa mkutano wa uzinduzi wa huduma yao mpya iliyojulikana kwa jina la Bwerere,kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Ofisi za kampuni hiyo,zilizopo makao makuu mtaa wa Samora Jijini Dar.

=======  ======= =======
Bwa.Peter alisema kuwa siku ya leo ,TTCL inazindua rasmi promosheni inayolenga kuwapa wananchi huduma bora na za bei nafuu. Promotion hii inajulikana kwa jina la  BWERERE   yaani pata huduma nyingi zaidi kwa bei nafuu zaidi.


''Promosheni hii inatoa fursa kwa wateja wa majumbani na maofisini ambao wanatumia  huduma ya malipo ya kabla(pre-paid) kufurahia gharama ya viwango vya chini kabisa vya kupiga simu TTCL kwenda kwenda mitandao mingine yote ikiwa ni pamoja na TTCL yenyewe,


Vilevile Promosheni hii inatoa fursa maalumu kwa watumiaji wa vifurushi vya intaneti(DATA)  kwa njia ya Broadband mtandao wa Nyaya na Mkongo waTTCL kitaalamu Fixed lines kuweza kupata intaneti bila kikomo''.Alisema Bwa.Peter Ngota.

DStV wazindua msimu wa soka leo

$
0
0
Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Ronald Baraka Shelukindo (kushoto) akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari (wahapo pichani) waliofika kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa Msimu wa Ligi kuu za Soka barani Ulaya unaotaraji kuanza mapeka wiki ijavyo katika viwanja mbali mbali,mechi hizo zote zitakuwa zikionyeshwa kupitia channel za michezo za Super Spotr zilizopo kwenye king'amuzi chao cha DStV.hafla hiyo imefanyika leo kwenye hoteli ya New Afrika,Jijini Dar es Salaam.Katikati ni Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Barbara Kambogi na kulia ni Meneja Mauzo wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Salum Salum.
Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Barbara Kambogi akifafanua jambo kwa baadhi ya waandishi wa habari (wahapo pichani) waliofika kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa Msimu wa Ligi kuu za Soka barani Ulaya unaotaraji kuanza mapeka wiki ijavyo katika viwanja mbali mbali,hafla hiyo imefanyika leo kwenye hoteli ya New Afrika,Jijini Dar es Salaam.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Salum Salum akielezea namna walivyojipanga kwenye swala zima la mauzo na hivyo wateja wao wasiwe na wasiwasi kwani mabo yako sawa kabisa.

TAMASHA LA MATUMAINI 2014 KESHO NDIYO KESHO TAIFA

$
0
0
SIKU iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa burudani mbalimbali imewadia ambapo kesho Agosti 8, katika Uwanja wa Taifa patakuwa hapatoshi wakati Tamasha la Usiku wa Matumaini litakapokuwa likichukua nafasi.
Mabondia Mada Maugo na Thomas Mashali wakitunishiana misuli.
Akizungumza na Centre Spread, mratibu wa tamasha hilo, Luqman Maloto alisema kuwa maandalizi yote yameshafanyika na tayari mkali wa muziki kutoka Nigeria anayetamba na ngoma ya Johnny, Yemi Alade ameshatua nchini, kinachosubiriwa ni burudani mwanzo mwisho.

“Kila kona ya burudani imeshakamilika hivyo kama wewe ni mpenzi wa ndondi kuna ngumi kati ya mabondia Mada Maugo dhidi ya Thomas Mashali, JB dhidi ya Cloud 112, Said Memba dhidi ya Khalid Chokoraa na wengineo.
Navy Kenzo.
“Wapenzi wa Bongo Fleva, kutakuwa na mfalme wao, Ali Kiba akiwa sambamba na mastaa kama Shilole, Madee, R.O.M.A, Meninah, Navy Kenzo, Scorpion Girls, Juma Nature na wengine kibao,” alisema Maloto na kuongeza:“Kwa wale wapenzi wa soka basi watakutana na mechi kabambe kati ya Wabunge Mashabiki wa Simba dhidi ya wenzao wa Yanga, Azam Fc dhidi ya Mtibwa, Bongo Fleva dhidi ya Bongo Movie na wengine wengi.”
Ally Kiba.
Maloto aliongeza kuwa jukwaa litashambuliwa pia na wanamuziki wa nyimbo za Injili kama Martha Mwaipaja, Upendo Nkone, Angel na wengine wengi. Tamasha la Usiku wa Matumaini linatarajiwa kuanza kesho saa 5 asubuhi hadi saa 6 usiku ambapo wapenzi wa burudani watainjoi mambo yote kwa kiingilio cha shilingi elfu 5 tu.


RAIS KIKWETE KATIKA MKUTNAO WA WAKUU WA NCHI ZA BARA LA AFRIKA,JIJINI WASHINGTON DC

$
0
0
o3
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Rais Barak Obama wa Marekani kwenye ukumbi wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani Agosti 6, 2014.o6 o7
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Rais Barak Obama wa Marekani kwenye ukumbi wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani Agosti 6, 2014o8
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU), Mhe. Dkt. Nkosazana Dlamini-Zum wakimsikiliza Rais Barak Obama wa Marekani wakati akiongoza Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC Agosti 6, 2014
o2
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa kimataifa Mhe Bernard Membe na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Librerata Mulamula kwenye Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani Agosti 6, 2014.

 BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Kongamano la mchakato wa Katiba lasogezwa mbele

$
0
0
Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania limesema kwamba kongamano la kujadili chakato wa kutunga Katiba mpya na changamoto zake lililopangwa kufanyika Agosti 9 na 10  mwaka huu limesogezwa mbele, hivyo litatangaza tarehe ya kufanyika.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa  baraza hilo, Peter Mziray katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari mjini Dodoma leo.

“Kutokana na uzito wa kongamano hilo na kazi kubwa ya maandaliziyake, inayotokana na uwingi  na uzito wa wageni waalikwa, kongamano hilo halitafanyika siku ya tarehe 9 na 10 Agosti, mwaka 2014 kama lilivyopangwa awali. Hivyo basi  tarehe ya kufayika kongamano hilo imepelekwa mbele na baraza litatangaza,” alisema Mziray.

 Aliongeza kuwa kongamano hilo litakuwa tukio kubwa na muhimu kwa nchini yetu, kwani litajadili kwa kina mchakato wa kutunga Katiba mpya unaoendelea  na changamoto zinazoendelea kukabiliana nazo.

“ Wadau wote wanaohusika na mchakato huu wataalikwa na watoa maoni yao,” alisisitiza.
 Aidha Mziray alisema kongamano hili litaibuka na maazimio ambayo, baraza hilo, linaamini yatakuwa na uzito na ushawishi  katika mchakato huo kwa kuwa yatazingatia maslahi mapana ya taifa, hali  halisi ya siasa, uchumi, utamaduni, jamii na haja ya kudumisha Muungano wetu na hatima ya nchi kwa miaka mingi inayokuja.

Awali akizungumza na waandishiwa habari hivi karibuni jijini Dares Salaam kufuatia kufanyika  Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa baraza hilo, Peter  Kuga  Mziray, wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao kati ya baraza hilo, na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa,akiwemo Msajili  wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mtungi kilichofanyika kwenye hoteli ya New Afrika jijini Dares Salaam.

Mwenyekiti huyo akizungumzia kuhusu kongamano hilo ,ambalo litamhusisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya  Kikwete,ambaye atakayelifungua, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe . Mohammed Gharib Bilal, Marais wastaafu,wabunge,majaji, maspika, viongozi wote waliowahi kushika madaraka, viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wa dini zote.

“Lengo la kongamano hili ni kujadili hali ya kisiasa na mchakato wa Katiba Mpya. Kongamano hili ndio njia ya kutafuta maridhiano  katika suala hili. Tunategemea busara za viongozi hawa zitatubadilkisha  na kutuweka pamoja  kwa maslahi ya taifa na kuachana na mambo ya kivyama,” alisisitiza.

Wakulima Dodoma wasifu Ufanisi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)

$
0
0
Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Dodoma na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Bw. Hamis Abdallah Mwenda (kushoto) akipata maelezo katika Banda la TPA lililopo viwanja vya nanenane Nzuguni, Dodoma kutoka kwa Afisa Mawasiliano, Bw. Focus Mauki (kulia). Katikati ni Afisa Mkuu wa TPA, Bi. Lydia Mallya.
Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Dodoma na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Bw. Hamis Abdallah Mwenda (kushoto) akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea Banda la TPA lililopo viwanja vya nanenane Nzuguni, Dodoma. Kushoto ni Afisa Mkuu wa TPA, Bi. Lydia Mallya na Afisa Mawasiliano, Bw. Focus Mauki (kulia).
Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Dodoma na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Bw. Hamis Abdallah Mwenda (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa TPA na Wageni wengine wakati alipotembelea Banda la TPA lililopo viwanja vya nanenane Nzuguni, Dodoma.
Afisa Mawasiliano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari TPA Focus Mauki (kulia) akiwaelezea kuhusu huduma zinazotolwa na TPA, baadhi ya wakazi wa mkoa wa Dodoma waliotembelea banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari TPA lilopo kwenye maonesho ya NaneNane ya Kanda ya Kati yanayoendela katika viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.
Baadhi ya wanafunzi waliotembelea banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari TPA wakimsikiliza kwa makini Afisa Mawasiliano wa Mamlaka hiyo Focus Mauki,wakati walipotembelea banda hilo lwa ajili ya kujifunza shughuli mbalimbali za bandari katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya kati yanayoendelea kwenye viwanja vya vya Nzuguni mjini Dodoma.

LHRC YATOA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MWENENDO WA MCHAKATO WA UTUNGAJI WA KATIBA MPYA TANZANIA UNAOENDELEA DODOMA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Helen Kijo-Bisimba (kulia), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu mwenendo wa mchakato wa utungaji wa Katiba Mpya ya Tanzania unaoendelea Dodoma. Kushoto ni Mtetezi wa Haki za Wanawake, Ananilea Nkya.
Mtetezi wa Haki za Wanawake, Ananilea Nkya (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Ofisa Mipango kutoka Taasisi ya Sikika, Patrick Kinemo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Helen Kijo-Bisimba
Mwanasheria wa LHRC, Harold Sungusia (katikati), akitoa ufafanuzi wa kisheria kuhusu mchakato huo wa Katiba Mpya. Kulia ni Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwajibikaji wa LHRC, Imelda Urrio na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Helen Kijo-Bisimba.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

President Kikwete joins other EAC leaders in a Presidential Breakfast session

$
0
0
EAC presidents at a Presidential Breakfast Discussion on trade and business potential in the region held at the US chamber of Commerce in Washington DC.

coca cola yaitangaza TANZANIA kwa aina yake

$
0
0
Kampuni ya CocaCola imetengeneza kopo la kinywaji cha coca cola maalumu kwa kuitangaza TANZANIA

Please vote for Richard Magumba

$
0
0
Please your vote is awaited for a beautiful short documentary titled "aka Shegena" done by Richard Magumba; a Tanzanian filmmaker based in Dar es salaam. It is an inspirational documentary to people with disabilities and a community at large.

Let us support this vibrant talented film-maker.

The voting closes on August 17th. See the link below.

THE CENTRE FOR FOREIGN RELATIONS (CFR) TO RUN SHORTCOURSES ON PROTOCOL AND PUBLIC RELATIONS AND DATA COLLECTION AND ANALYSIS, USING STATA AND SPSS SOFTWARES IN AUGUST 2014

$
0
0
Group photo of participants with their certificated held high.

President Mugabe satisfied with Sadc Summit preps

$
0
0
President Mugabe welcomes Sadc executive secretary Dr Stergomena Lawrence Tax and director of Policy Planning and Resource Mobilisation Dr Angelo Eduardo Mondlane at State House in Harare yesterday. — (Picture by Tawanda Mudimu)

Farirai Machivenyika Senior Reporter

ELEVEN Sadc Heads of State and Government have confirmed their attendance of the 34th Sadc Summit slated for August 17 to 18 in Victoria Falls. President Mugabe, who is set to assume the Sadc chair at the summit, opened a zanu-pf Central Committee meeting in Harare yesterday where he expressed satisfaction with preparations made to host the regional annual event.

“Already, out of the 14 Heads of State, 11 have indicated they are coming. The three are yet to indicate, they are in countries which are preparing for elections, but we know should they be held back by those preparations which they are doing they will send formidable members to represent their countries,” President Mugabe said.

Botswana and Mozambique are expected to go to elections in October, while Namibia is scheduled to hold its plebiscite in November.

The President told Central Committee members that he had met with Sadc Executive Secretary Dr Stergomena Lawrence Tax earlier in the day and she was satisfied with the country’s state of preparedness told the Sadc summit.

“It is also our fortune this year that we have been elected by Sadc as its host for this year and the chairmanship for the whole of the Sadc year which means up to next year, and just now the Minister of Foreign Affairs (Simbarashe Mumbengegwi) and I have been meeting with the Sadc Secretariat, the Executive Secretary and we have been working on the preparations as done to see whether the rhythm, the format of those preparations are in accordance with the Sadc tradition, what has become a tradition of holding our yearly conferences, and I am happy that the preparations have been well done,” President Mugabe said.

He urged the inter-ministerial committees tasked with ensuring the successful hosting of the summit to ensure they completed their work on time.

“As we look within ourselves as Sadc, we should also have an inward domestic look, are we fully prepared?” he said. “And our committees which have been set to undertake the task of working on those areas where preparations are necessary, those committees must complete their work where it has not been completed.

“We would have to ensure that transport facilities are ready, that we are not only providing cars that are apt and proper and befitting, but cars in good condition, that our accommodation is comfortable, accommodation and befitting to the status of people as we are used in Sadc.”

President Mugabe called on Zimbabweans to be hospitable to the visitors and guests who would be in the country during the Summit.

ALL IS SET FOR THE 8TH EDITION OF EAC MILITARY GAMES AND CULTURAL EVENT-2014 IN ZANZIBAR

$
0
0
Uganda’s Defense Liaison Officer at the EAC Headquarters in Arusha, Tanzania, Col. Sam Omara has today confirmed that all is set for the 8th Edition of the EAC Military Games and Cultural Event due to take place from 18 to 30 August 2014 at the Amaan Stadium in Zanzibar, the United Republic of Tanzania.

The EAC Military Games and Cultural Event are geared towards enhancing solidarity and promotion of cooperation through sports and culture among the EAC Partner States Armed Forces; undertaking mutual technical assistance towards the development of sports and culture in the Partner States Armed Forces; and contributing to regional effort for peace through sports and culture.

The Military Games and Cultural Event are also meant to encourage physical education, sports and interaction of the diverse and rich EAC culture and customs within the military; encourage and support all the measures designed to establish and strengthen the bonds of friendship and solidarity among the Partner States Armed forces; entrust the host Nation with the organization of the Event under its aegis, and offer equal opportunity to all participants in the spirit of friendship, solidarity and fair play.

The  8th EAC  Military Games and Cultural edition, which is running under the theme; One People One Destiny through EAC Military Games and Cultural Event 2014, will have its official opening ceremony on 20 August 2014 and the official closure  on 29 August 2014  at the 15,000 capacity Amaan Stadium in Zanzibar.

The sporting disciplines for the 8th EAC Military Games and Cultural edition will include; Football (Men), Basketball (Men), Netball (Women), Handball  (Men), Cross country (Women), and Cross country (Men).

A total of 430 troops will participate in the games and cultural event and entrance to the stadium is free of charge. The Corporate Communication and Public Affairs Department at the EAC Headquarters is calling upon the people of Zanzibar and friends to endevour to attend and follow the Games and Cultural event at the stadium.

The first EAC Military Games and Cultural Event was held in the Republic of Uganda in 2005, the second was in the Republic of Kenya in 2006, the third in the United Republic of Tanzania in 2007, Uganda hosted the fourth edition in 2008, the fifth was in the Republic of Rwanda in 2009, the Republic of Burundi hosted the sixth edition in 2011, and the 7th in the Republic of Kenya in 2013.

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YATOA TAARIFA YA MFUMUKO WA BEI NCHINI

$
0
0
Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu na Makazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akitoa taarifa ya mfumuko wa bei kwa mwezi Julai 2014 kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

Na. Aron Msigwa-MAELEZO.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu imeeleza kuwa ongezeko dogo la mfumuko wa bei nchini kutoka asilimia 6.4 za mwezi June hadi asilimia 6.5 za mwezi Julai 2014 linatokana na kupanda kwa bei za baadhi ya bidhaa na huduma katika maeneo mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na sensa ya Watu na Makazi Bw. Ephraim Kwesigabo amesema kuwa bidhaa zisizo za vyakula zikiwemo Bia, Sigara, mavazi kwa wanaume na yale ya watoto zimechangia ongezeko hilo.

Aidha, huduma na bidhaa nyingine zilizochangia ongezeko hilo ni gharama za udobi, kodi za pango, mazulia na mkaa wa kupikia Bw. Kwesigabo amefafanua kuwa hali ya mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na migahawa kwa mwezi Julai umepungua hadi 7.9 kutoka asilimia 8.5 kutoka asilimia 8.7 za mwezi Juni huku badiliko la fahirisi za bidhaa zisizo za vyakula likiongezeka hadi asilimia 4.9 kwa mwezi Julai 2014 kutoka asilimia 4.8 iliyokuwepo mwezi uliopita.

Kuhusu mfumuko wa bei unaopimwa kwa kipimo cha mwezi amesema kuwa umeongezeka kwa asilimia 0.1 ikilinganishwa na kupungua kwa asilimia 0.6 kama ilivyokuwa kwa mwezi Juni mwaka huu, huku fahirisi za bei za taifa zikiongezeka hadi kufikia 149.16 kutoka 148.98 za mwezi Juni 2014.

Kwa upande wa uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma za jamii kutoka mwezi Septemba 2010 hadi Julai 2014 umefikia shilingi 67 na senti 04 kutoka shilingi 67 na senti 12 za mwezi Juni mwaka huu.

“Kuongezeka kwa bei ya baadhi ya bidhaa na huduma kwa mwezi uliopita kunamaanisha kwamba, uwezo wa fedha yetu katika kununua huduma na bidhaa hizo unaupungua hii inamaanisha mfumuko wa bei unapopanda thamani ya shilingi nayo inashuka” Amebainisha.

Kuhusu ulinganifu mfumuko wa bei wa Tanzania na baadhi ya nchi za Afrika Mashariki amesema kuwa una mwelekeo unaofanana na kueleza kuwa mfumuko wa bei nchini Kenya umeongezeka na kufikia asilimia 7.67 kwa mwezi Julai 2014 ikilinganishwa na asilimia 7.39 za mwezi Juni huku Uganda ikiwa na mfumuko wa bei wa asilimia 4.3 mwezi huu ikilinganishwa na asilimia 5.0 za mwezi Juni.

WAKAZI WA JIJI LA ARUSHA WAMIMINIKA KWA WINGI NA KUJIUNGA NA MFUKO WA MAFAO YA KUSTAAFU WA GEPF

$
0
0
p2Bw Aloyce Ntukamazina Meneja Masoko kutoka katika Mfuko wa GEPF akifafanua jambo kuhusu  mafao yatolewayo na Mfuko wa GEPF katika maonesho ya wakulima ya nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Themi Njiro, Arusha.p1Mwanachama mpya akipata maelekezo ya namna ya kujiunga na Mfuko wa GEPF kutoka kwa Afisa wa GEPF Bi Jane Rutashobya katika maonesho ya wakulima ya nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Themi Njiro, Arushap4Afisa Masoko Clement Oningo akitoa maelezo kuhusu shughuli za Mfuko wa Mafao ya Kustaafu wa GEPF kwa wakazi wa jiji  la Arusha waliofika katika banda la GEPF.DSC_4775
DSC_4826Muonekano wa banda la GEPF katika viwanja vya nane nane jijini Arusha.Meneja Masoko Aloyce Ntukamazina ,   Alitoa wito kwa wakazi wa Arusha kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya nane nane ili kupata elimu na faida za kujiunga na mfuko huo. “Nawasihi wananchi wajitokeze kwa wingi katika maonyesho haya na kuja kutembelea katika banda letu na kuweza kupata elimu na faida za kujiunga na mfuko huu”alisema Ntukamazina.
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images