Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110150 articles
Browse latest View live

PSPF YASHIRIKI MAONYESHO YA WAKULIMA NANENANE MKOANI LINDI KWA MAFANIKIO

$
0
0
MKUU WA WILAYA YA LINDI MJINI DOKTA HAMID NASSORO (KATIKATI)  AKISAINI KITABU CHA WAGENI ALIPOTEMBELEA BANDA LA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF KWENYE MAONYESHO YA WAKULIMA NANENANE MKOANI LINDI, (WAPILI KULIA) NI AFISA MAKOSO WA PSPF RAHMA NGASSA. (KUSHOTO) NI OMARI KALILO AFISA MFAWIDHI WA PSPF MKOA WA LINDI.

BALOZI WA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF, MRISHO MPOTO “MJOMBA” AKIFURAHIA JAMBO NA MENEJA MASOKO WA PSPF, RAHMA NGASSA WAKATI AKITOA BURUDANI KWENYE MAONYESHO YA WAKULIMA NANENANE MKOANI LINDI.MENEJA MIRADI MFUKO WA PENSHENI WA PSPF, MASOUD AKITOA MAELEZO KWA WATU MBALIMBALI WALIOTEMBELEA BANDA LA PSPF KWENYE MAONYESHO YA WAKULIMA NANENANE MKOANI LINDI.
 AFISA UENDESHAJI WA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF DOLPHIN RICHARD AKIMWELEKEZA MARTHA HONGERA (KATIKATI) NAMNA YA KUJAZA FOMU YA UCHANGIAJI WA HIARI WALIOTEMBELEA BANDA LA PSPF KWENYE MAONYESHO YA WAKULIMA NANENANE MKOANI LINDI.

BANDA LA OFISI YA WAZIRI MKUU LAVUTIA NANE NANE DODOMA

$
0
0
Baadhi ya Wananchi wa Mjini Dodoma wakipata maelezo ya Uwekezaji na Uwezeshaji kutoka kwa Mchumi Mwandamizi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Vedasto Manumbu walipotembelelea Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea Mjini Dodoma, Viwanja vya Nzuguni.
Mratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Mollay akifafanua uratibu wa shughuli za serikali kwa Wanafunzi Shule ya Msingi Nzuguni “B” walipotembelea Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea Mjini Dodoma, Viwanja vya Nzuguni.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Nzuguni “B” wakisoma Picha zenye historia za Mawaziri Wakuu Wastaafu wa Tanzania, zilizopo katika Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea Mjini Dodoma, Viwanja vya Nzuguni.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Radio 5 yapongezwa kwa mchango wake wa kukuza sanaa za vichekesho vya majukwaani.

$
0
0
 Kituo cha Radio 5, kimepongezwa na wadau wa sanaa kwa mchango wake wa kukuza sanaa za vichekesho vya majukwaani hapa nchini.

Wadau hao wa sanaa za vichekesho vya majukwaani waliipongeza Radio 5, wakati wa burudani ya wachekeshaji wa majukwaani iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii katika ukumbi wa Golden Tulip. Burudani hiyo ambayo ilifana sana iliwajumuisha mchekeshaji kutoka Uganda, mwanadada Anne Kansiime, Fred Omondi kutoka Kenya na Pilipili wa Tanzania.

Akizungumzia onyesho hilo, mmoja ya mashabiki waliohudhuria onyesho hilo, amesema sanaa ya vichekesho vya majukwaani nchini haijapewa kipaumbele kama aina nyingine za sanaa. ‘Watu wengi bado wanaamini sanaa za kuchekesha majukwaani sio kazi rasmi kama kazi nyinginezo, lakini hii imeanza kubadilika hapa nchini, na tutarajie mabadiliko zaidi kama wadau wengine kama radio 5 wakijitokeza kusaidia’ alisema Farida Akida.

Akijibu swali aliloulizwa na waandishi wa habari kuhusiana na anavyoiona tasnia ya vichekesho vya majukwaani Afrika Mashariki, mchekeshaji Anne Kansiime anasema anaamini sanaa ya vichekesho vya majukwaani inaanza kujijengea heshima kubwa miongoni mwa wananchi.  ‘Mimi sio mbunge au mwanasiasa, lakini nimepata mapokezi makubwa, kwa kazi hii tu ya kuchekesha watu, hivyo naona hii tu pekee ni dalili ya kukua kwa tasnia hii hapa Afrika Mashariki’ alisema Anne.

Ikiwa ni mara ya kwanza kwa mwanadada Kansiime kuja Tanzania kutoa burudani, hasa baada ya kujijengea umaarufu mkubwa kupitia vipande vyake vya vichekesho vilivyo mtandaoni, tiketi za burudani yake ziliisha wiki moja kabla hajawasili.  Katika usiku huo wa burudani ulioitwa, Cheka Kwa Nguvu, mchekeshaji toka Tanzania, Pilipili aliwatoa kimasomaso mashabiki waliofurika kwa vichekesho vyake vilivyoonekana kuwagusa mashabiki moja kwa moja.

Huku mashabiki wengi wakiwa hawamfahamu vyema, Pilipili ambaye kitaaluma ni mwalimu, anasema aliacha kazi ya ualimu ili awe mchekeshaji, hivyo kwake yeye, kuchekesha ni kazi kama kazi nyingine. ‘Kwangu mimi hii ni kazi ambayo najivunia, na naamini nitaweza kuwawakilisha watanzania vyema kimataifa kupitia uchekeshaji, na naishukuru Radio 5 kwa kunipa fursa ya kuonyesha kwamba ninaweza’ alisema Pilipili.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Radio 5, Robert Francis amesema huu ni mwanzo tu wa kuwaandalia watanzania burudani za kipekee na watarajie mengi zaidi kutoka Radio 5. ‘Sanaa ya uchekeshaji jukwaani bado haijapewa nafasi kubwa hapa nchini, lakini kama mlivyoona, mashabiki wamejitokeza kwa wingi sana kwenye burudani yetu, hivyo watu watarajie burudani za aina hii nyingi zaidi kutoka kwetu’ alimaliza Francis.
 Sehemu ya washabiki na wapenzi wa fani hiyo wakivunjika mbavu kwa kucheka.
 mwanadada Anne Kansiime kutoka nchini Uganda akitoa burudani ya vichekesho kwa watazamaji (hawapo pichani),ndani ya moja ya ukumbi wa hotel ya Golden Tulip jijini Dar hivi karibuni

Wasanii wa fani ya Uchekeshaji mahiri kutoka nchini Uganda,Kenya na Tanzania wakitoa burudani kwa washabiki na wapenzi wa fani hiyo ,iliofanyika kwenye moja ya ukumbi wa hotel ya Golden Tulip Jijini Dar,pichani shoto ni Fred Omondi kutoka Kenya,mwanadada Anne Kansiime kutoka nchini Uganda na Mc Pilipili wa Tanzania.

Robo fainali ya Dance 100% yanukia

$
0
0
Kikundi cha Wakali Dance kutoka Bugurunii jijini Dar es salaam, wakionyesha umahiri wao wa kucheza wakati wa shindano la Dance miamia lililofanyika katika Viwanja vya Don Bosco Oysterbay chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania.Wakati wa shindano la kutafuta makundi 16 ya kuingia robo fainali itakayoanza Agosti 23 na kikundi kitakachoshinda katika shindano hilo kitajinyakulia kitita cha shilingi milioni 5.
Vijana wanaounda Kundi la Mob Squad wa Wilaya ya Temeke wakionyesha umahiri wao katika Viwanja vya Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam, wakati wa shindano la Dance miamia lililofanyika katika Viwanja vya Don Bosco Oysterbay,Wakati wa shindano hilo la kutafuta makundi 16 ya kuingia robo fainali itakayoanza Agosti 23 chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania kikundi kitakachoshinda kitajinyakulia kitita cha shilingi milioni 5.

ROBO fainali ya mashindano ya Dance 100% 2014 inatarajiwa kufanyika Agosti 23 ikishirikisha makundi 16 kutoka wilaya tatu za Kinondoni, Temeke na Ilala, jijini Dar es Salaam.

Hayo yalisemwa jana na mratibu wa mashindano hayo, Happy Shame alipokuwa akizungumza na mwandishi wa gazeti hili na kufafanua kuwa katika robo fainali hiyo watapata makundi kumi bora yatakayoingia kwenye nusu fainali hapo baadaye.

Aliyataja makundi ambayo yamefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali kuwa ni  Wazawa crew,Best boys crew,G.O.P,The-W-T,Best love,Tatanisha Dancers,Bustani,Qulity boys,Pambana Fasaha,wakali sisi,Tamtam,Mazabe,TWC,B2K na winners crew.

"Huu ni mwaka wa tatu East Africa Radio na East Africa Television wanaandaa mashindano haya kwa udhamini wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania na kinywaji cha Grand Malta na yamekuwa yakipata vijana wengi ambao hujitokeza kushiriki," alisema Shame.

Mratibu huyo alisema kuwa mashindano ya mwaka huu yalianza Julai 19 na kila yanapofanyika kwenye wilaya husika, yamekuwa yakirushwa East Africa Television kila Jumatano saa moja kamili usiku.

Alisema kuwa kundi ambalo litaibuka na ushindi litajinyakulia kitita cha Sh. milioni 5 na kwamba kila kundi limekuwa likijitahidi ili kuhakikisha kwamba litwaa kitita hicho.

Aidha, mratibu huyo alisema kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakikosea kuandika jina la shindano hilo na kuwataka wawe wanmauliza ili kupata uhakika wa jina la shindano hilo kuwa ni Dance 100% 2014.

Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wa shindano hilo, Matina Nkurlu alisema kuwa wao wana jukumu la kuendeza shindano hilo kwa kutambua kwamba muziki ni ajira.

Alisema kuwa Vodacom Tanzania inajua ni jinsi gani serikali ilivyokuwa na majukumu mengi moja wapo likiwepo la kuwapatia vijana ajira kwa kutambua kuwa suala la ajira siyo lazima kuajiriwa kwenye kampuni ama viwanda au ofisini.

"Kwa kutambua hilo ndiyo maana sisi Vodacom Tanzania tumedhamini mashindano hayo kwani tunaamini kwamba baada ya hapo vijana hao wanaweza kuchukuliwa kwenda kutoa burudani sehemu mbalimbali na wakalipwa,"alisema Nkurlu.

Meneja huyo aliwatia moyo vijana wanaoshiriki shindano hilo kwamba wasikate tamaa bali watambue wanachokifanya kinaweza kuwapa ajira hapo baadaye na kujikuta wakiendesha maisha yao bila wasiwasi.

NABAKI AFRIKA MABINGWA VIFAA VYA UJENZI

$
0
0
20140806_050949Meneja wa kampuni ya Nabaki Afrika tawi la Arusha Jesse S. Madauda akiongea na wateja waliotembelea katika  banda lao viwanja vya nane nane jijini Arusha.
20140806_051639
Hii ni Plumbing System ni kwaajili ya mfumo wa maji taka na safi na sifa yake kuu nikwamba huwezi kuona chemba zile za nje na haizibi
20140806_050615Vigae vya kuezeka (Decra Roofing Tiles )sifa yake kuu ni havipauki ,havipati kutu na havipukutiki na guarantee yake miaka 50

Kampuni ya Nabaki Afrika ni kampuni pekee isiyo na mshindani katika ubora wa vifaa mbalimbali vya ujenzi.Kampuni hiyo inahusika katika maeneo makuu matatu,yaani uezekaji,ujenzi (Construction) na maji.

Kwa mawasiliano  wasiliana nao kupitia info@nabaki.com au tembelea tovuti yao www.nabaki.com au piga simu namba 0766 827417 au 0786 966114.Nabaki Afrika imejaribiwa,Imepimwa na Imeaminiwa zaidi ya miaka 20 Tanzania.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Bendera atilia mkazo soka la vijana wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Airtel Rising Stars mkoani morogoro

$
0
0
Mkuu wa Morogoro Joel Bendera akipiga mpira kuashiria uzinduzi wa Airtel Rising Stars mkoani Morogoro.
  

 Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akikagua timu wakati wa uzinduzi wa Airtel Rising Stars mkoani Morogoro.


Bendera atilia mkazo soka la vijana.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera, atilia mkazo soka la vijana na kuwataka viongozi wa mpira wa miguu mkoa wa Morogoro na chama cha mpira wa miguu Tanzania kutilia mkazo program za vijana.

Kocha wa zamani wa timu ya Taifa – Taifa Stars atoa changamoto wakati akifungua mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mkoa wa Morogoro siku ya jumanne. Alisema kuwa hakuna njia ya mkato katika maendeleo ya mpira wa miguu zaidi ya kuwekeza katika shule za soka na programu za vijana kama Airtel Rising Stars. Awapongeza  Airtel kwa mchango wao.

Zaidi ya majuma mawili kumekua na maoni ya kutoka kwa wakuu wa mikoa na wadau wengine wakisisitiza viongozi wa mpira wa miguu nchini kutilia mkazo programu za vijana kuiwezesha Tanzania kufanya vizuri.

Wakifungua mashindano ya Airtel Rising Stars katika mikoa yao hivi karibuni, Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam Said Meck Sadiki na Mkuu wa mkoa Mbeya Abbas Kandoro nao walitilia mkazo kuwekeza katika mpira wa vijana. Wengine waliotoa maoni hayo ni meya wa Mwanza Stanslaus Mabula na Mbunge wa Ukonga Eugen Mwaiposa.

Mashindano ya Airtel Rising Stars yanaitimishwa leo (August 7) na timu zinatarajiwa kuwasili jijini Dar-es-Salaam siku ya jumamosi August 9 katika fainali za taifa ambazo zinaanza kutimua vumbi jumapili katika kiwanja cha kumbukumbu ya Karume. Fainali za Taifa zitamalizika tarehe 17 August na wachezaji wakiume na wa kike watakao chaguliwa wataweka kambi jijini Dar-es-Salaam wakijiandaa na mashindano ya kimataifa Airtel Rising Stars yatakayofanyika nchini Gabon.

Mwaka jana mashindano hayo yalifanyika nchini Nigeria na timu ya wasichana ya Tanzania walinyakua ubingwa na kuzawadiwa dollar za marekani 10,000.   

MKE NA MUME WAKUTWA NA MADAWA YA KULEVYA

$
0
0
 Pichani juu na chini ni Gari aina ya Toyota Corolla yenye namba za usajili T.589 AZS likiwa limebeba magunia ya madawa ya kulevya aina ya bhangi mara baada ya kukamatwa eneo la Sanawari jijini Arusha na askari wa kitengo cha kuzuia Madawa ya Kulevya mkoani humo. (Picha na woinde shizza,Arusha) 

Na Woinde Shizza,Arusha.

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limewakamata  watu watano wakiwa na magunia saba ya madawa ya kulevya aina ya bhangi wakiwemo mke na mume.

 Awali askari wa Kitengo cha Kuzuia Madawa ya Kulevya Mkoani hapa wakiwa doria walipata taarifa toka kwa raia wema iliyoeleza kuwepo kwa watu wanaosafirisha madawa hayo.

Mara baada ya kupata taarifa hiyo askari hao waliweka mtego maeneo ya Sanawari ambapo muda wa saa 3:30 usiku walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili ambao ni Hussein Rashid (35) mkazi wa Sakina, dereva pamoja na mwenzake Sebastian Wilbert (37) Fundi magari, mkazi wa Ilboru wakiwa wanasafirisha magunia matano ya madawa ya kulevya aina ya bhangi yenye uzito wa kilogramu 171 kuelekea nchi jirani ya Kenya kwa kutumia gari aina ya Toyota Corolla lenye namba za usajili T. 589 AZS.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas alisema kwamba, mara baada ya watuhumiwa hao kuhojiwa walikiri kosa hilo na kumtaja mwanamke aitwaye Flora John (38) Mkazi wa Ekenywa- Ngaramtoni kuwa ndio aliyewauzia.

Kamanda Sabas aliendelea kwa kusema kwamba, askari hao walianza kumfutilia mwanamke huyo ambapo jana Jumanne tarehe 05.08.2014 walikwenda nyumbani  kwake na kumkuta mtuhumiwa ambaye ni muuzaji akiwa na mume wake aitwaye John Meleji (45) Mkazi wa Ekenywa na mara baada ya kufanya upekuzi walikuta gunia moja la madawa ya kulevya aina bhangi ndani ya nyumba hiyo.

Mbali na kuwakamata watuhumiwa hao ambao ni mke na mume pia askari hao walimkamata jirani yao aitwaye Loseriani Metelami (21) Mkulima mkazi wa Ekenywa baada ya yeye pia kukutwa na gunia moja la madawa ya kulevya aina ya bhangi hivyo kufanya jumla ya magunia yaliyokamatwa kuwa saba.


Watuhumiwa hao watano wanatarajiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni mara baada ya upelelezi kukamilika.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO TAREHE 06.08.2014


Article 23

MH. PINDA AFUNGUA MASHINDANO YA MIFUGO DODOMA

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama mapishi ya pilau la kuku ya Mama Irene mamuya (kulia) wa Chako ni Chako Dodoma katika maonyesho ya wakulima Nanenane yaliyofanyika kwenye uwanja wa Nzuguni Dodoma August 6, 2014.
Ngombe mwenye kilo 1000 kutoka Mafinga Iringa akipita mbele ya mgeni rasmi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika mashindano ya mifugo yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu kwenye uwanja wa Nzuguni wa Nanenane mjini Dodoma August 6, 2014.
Ngombe wakiwa wamejipanga katika maonyesho ya mifugo yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye uwanja wa Nanenane wa Nzuguni uliopo Dodoma August 6, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dr. Titus Kamani kukagua banda la Wizarahiyo katika monyesho ya Wakulima Nanenane kwenye uwanja wa Nzuguni Dodoma August 6, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

RAIS KIKWETE AJIUNGA NA VIONGOZI WENGINE WA AFRIKA KATIKA MKUTANO WA VIONGOZI WA AFRIKA NA MAREKANI JIJINI WASHINGTON DC LEO

$
0
0
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili katika Ikulu ya Marekani (White House) jijini Washington DC kwa dhifa ya Kitaifa waliyoandaliwa viongozi wa Afrika na mwenyeji wao Rais Barak Obama Julai 5, 2014.
 Rais Jakaya Kikwete na viongozi wenzake wa Afrika katika mkutano wa Viongozi wa Afrika na Marekani  ambao umefunguliwa na Rais Barak Obama katika ukumbi wa State Department jijini Washington DC  leo Julai 6, 2014.
 Sehemu ya wajumbe wa Mkutano wa Viongozi wa Afrika na Marekani  ambao umefunguliwa na Rais Barak Obama katika ukumbi wa State Department jijini Washington DC  leo Julai 6,  2014.
 Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry anaelekeza namna ya kutumia kipaza sauti baada ya Rais Obama kufungua mkutano huo, wakati  mwenyekiti wa Umoja wa Afrika  Rais  Mohamed Ould Abdel Aziz alipoongea kwa niaba ya Viongozi wa Afrika.PICHA NA IKULU.

Captain Gardener G. Habash ndani ya Michuzi TV leo

SSRA YAZINDUA KANUNI MPYA ZA KUHUISHA MAFAO YA PENSHENI

$
0
0
Waziri wa Kazi na Ajira, Dk.Gaudensia Kabaka akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma juzi kuhusu mabadiliko ya Kanuni za Kuhuisha Mafao ya Pensheni kwa Mifuko ya  Hifadhi ya Jamii ya kuwa na aina moja kwa wastaafu.Katikati ni Mwenyekiti wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA),Juma Muhimbi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka hiyo, Irene Isaka.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa  Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Irene Isaka akifurahia jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Dodomajuzi.
 Wakurugenzi Wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wakimsikiliza Waziri wa Kazi na Ajira Dk Gaudensia Kabaka,kuhusumabadiliko ya Kanuni za Kuhuisha Mafao ya Pensheni kwa Mifuko ya  Hifadhi ya Jamii ya kuwa na aina moja kwa wastaafu kupitia Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA).
Wakurugenzi Wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wakiwa katika picha ya pamoja na  Waziri wa Kazi na Ajira Dk Gaudensia Kabaka na Naibu wake Makongoro Mahanga.

MAZISHI YA ANDREA DUMA BABA WA MWANDISHI WA HABARI WA MOblog SINGIDA

$
0
0
DSC00331
Jeneza lililobeba mwili wa mchungaji mstaafu wa kanisa la Free Pentekoste (FPCT) Ihanja wilaya ya Ikungi, Andrew Duma (92).
DSC00343
Katibu mkuu wa makanisa ya Free Pentekoste nchini,Elias Shija, akihubiri kwenye ibada ya mazishi ya mchungaji mstaafu wa Free Pentekoste Ihanja wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Andrea Duma.
DSC00357
Mjumbe wa halmashauri kuu CCM (NEC) Singida mjini, Hassan Mazala, akitoa nasaha zake kwenye ibada ya mazishi ya mchungaji mstaafu wa kanisa la Free Pentekoste Ihanja wilaya ya Ikungi, Andrea Duma.Mazishi hayo yamefanyika jumamosi katika kijiji cha Ihanja.
DSC00355
Baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini mbalimbali waliohudhuria mazishi ya mchungaji mstaafu wa kanisa la Free Pentekoste Ihanja wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida.Andrea Duma.Mazishi hayo yamefanyika katika kijiji cha Ihanja Jumamosi iliyopita.
DSC00337
Baadhi ya waombelezaji waliohudhuria mazishi ya mchungaji mstaafu kanisa la Free Pentekoste Ihanja Andrea Duma yaliyofanyika katika kijiji cha Ihanja.
DSC00347
DSC00363
Jeneza lillobeba mwili wa mchungaji mstaafu wa kanisa la Free Pentekoste (FPCT) Ihanja wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida Andrea Duma (92), likiingizwa kaburini, kuhitimisha safari yake hapa duniani.Mazishi hayo yamefanyika Jumamosi iliyopita katika kijiji cha Ihanja.(Picha zote na Nathaniel Limu).

Mahojiano na mgombea urais wa jumuia DMV, Liberatus Mwang'ombe

$
0
0
Karibu katika mahojiano kati ya Kwanza Production na Liberatus Mwang'ombe. Mgombea uRais wa Jumuiya ya waTanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia Uchaguzi unategemewa kufanyika Agosti 9, 2014

MO awashtaki CCM Singida kwa Kinana

$
0
0
kapambala
Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Naomi Kapambala akizungumza na waanndishi wa habari juu ya ufafanuzi wa maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo.

Na Hillary Shoo, Singida
Mbunge wa Jimbo la Singida mjini (CCM), Mohammed Dewji ameulalamikia uongozi wa Chama chake Mkoa wa Singida kwa kitendo cha kuchelewesha mchakato wa kumalizia ujenzi wa Uwanja wa michezo Namfua ikiwa ni moja ya ahadi zake alizotoa kwa wananchi wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.

Kuchelewa huko kuanza kwa mchakato wa ukarabati na uwekaji wa nyasi za bandia kwenye uwanja huo imeelezwa ni kutokana na urasimu na maslahi binafsi miongozi mwa viongozi wa CCM Mkoa wa Singida.

Katika barua yake ya Julai 31 mwaka huu kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Dewji amedai kuwa kwa kiasi kikubwa ameweza kutekeleza Ilani ya Uchaguzi kwa vipindi vyote viwili pamoja na ahadi zake binafsi, isipokuwa ahadi ya kumalizia ujenzi wa michezo Namfua.

Katika barua hiyo, ambayo pia ameinakili kwa Rais Jakaya Kikwete, Katibu Baraza la wadhamini CCM Taifa, Katibu wa Uchumi na Fedha na Katibu wa CCM mkoa wa Singida, Dewji amedai kuwa kila alipotaka kufanya hivyo alipata vikwazo kutoka kwa viongozi wa CCM mkoa wa Singida.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Hotuba ya Mhe Rais Uhuru Kenyatta kwa waKenya Washington DC. Aug 6, 2014

$
0
0
Mhe. Rais Uhuru Kenyatta akihutubia waKenya jijini Washington Aug 6, 2014
Karibu kusikiliza hotuba ya Mhe. Uhuru Kenyatta alipozungumza na waKenya usiku wa Agosti 6, 2014 kwenye hotel ya Marriott Wardman Park Hotel, jijini Washington DC nchini Marekani.

WEZI WA KAZI ZA WASANII KUKIONA,KAMATA KAMATA YAANZA RASMI

$
0
0


 Kampuni ya Msama Promotions Ltd,kwa kushirikiana na Wizara ya habari vijana,utamaduni na michezo  imetangaza neema kwa wasanii kuanza zoezi la kuwakamata watu wanaouza nakala feki  za wasanii hapa nchini.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo,Bwana  Alex Msama  amesema hayo jijini dar ,kuwa zoezi hilo limekwishaanza, na mpaka  sasa wamekamatwa vijana wane katika mkoa wa Dodoma na watatu jijini Mwanza.

‘’Kuna kazi mbalimbali ambazo zinaibiwa kila kukicha huku wamiliki wa kazi hizo wakiendelea  kushuka kiuchumi  na kutoona faida  yoyote ya kazi hizo,huu ni wakati kwa wasanii kuneemeka na kazi zao.Hivyo tutahakikisha tunafika kila mahali hata sehemu zisizofikika kirahisi na yote hii ni kuonyesha kuwa tunajali na tunathamini kazi za wasanii wetu’’,alisema Msama kwa msisitizo.

Alisema, nakala zote zitakuwa na stika za TRA  kuhakikisha hakuna wizi wowote unaofanyika  na unaotokea katika kazi mbalimbali za wasanii.Stika hizo zimewekwa ili kuwabaini wale wote wenye hulka hiyo ya kuiba kazi za wasanii .Operesheni  hiyo itafanyika  bila kujali wadhifa wake ama cheo chake,akaongeza kusema kuwa zoezi hilo ni salamu kwa wale wote wanoatumia kazi za wasanii bila kufuata  utaratibu wa sheria zilizopo.

Pia amelipongeza Jeshi la Polisi nchini kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha katika changamoto,na pia wamekuwa wakishirikiana  nao kuhakikisha  zoezi hilo linakuwa endelevu na kuzunguka kila mkoa kuhakikisha  kazi za wasanii zinaheshimiwa na zinalindwa kwa kila namna.

MBUNGE JOSHUA NASSARI AKUTANA NA VIONGOZI MBALIMBALI WAKIWEMO WA BARA LA AFRIKA

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akiwa katika picha ya pamoja na Mchungaji Jesse Jackson, Mwanaharakati wa siku nyingi wa Haki na Usawa.Kushoto ni Kiongozi wa Chama Kikuu cha Upinzani Afrika Kusini (Democratic Alliance) Mbali Ntuli.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari akiwa na rais wa Nigeria Goodluck Jonathan .
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari akiwa na Waziri mkuu wa Mauritius, Ramgoolam.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari akiwa na rais wa Uganda Yoweri Mseveni .
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akiteta jambo na Seneta Christopher Coons ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya Bunge la Marekani anayesimamia maswala ya Afrika.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari akiteta jambo na Balozi Suzan Rice ,mshauli wa Rais Obama maswala ya Usalama..
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari akiwa na rais wa Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo,Joseph Kabila.

Wizara ya Habari Vijana,Utamaduni na Michezo yakagua miradi ya vikundi vya Vijana vya Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma

$
0
0
Katibu wa Kikundi cha Muungano kilichopo kijiji cha Oloboloti kata ya Mrijo Halmashauri ya Chemba Mkoani Dodoma kinachojishughulisha na mradi wa kilimo cha nyanya aliyenyoosha mikono katikati Bw Juma Ally akitoa maelezo kwa Afisa wa Idara ya Maendeleo ya Vijana wa tatu kutoka kushoto Bi Amina Sanga katika ziara ya kukagua miradi ya Vijana, ziara hiyo ni sehemu ya mafunzo yanayotolewa na Wizara ya Habari Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Mfuko wa Vijana.
Katibu wa Kikundi cha Umoja kinachojishughulisha na mradi wa ufugaji wa mbuzi kilichopo katika kijiji cha Oloboloti katika Halmashauri ya Chemba Mkoani Dodoma Bw. Issa Mwinjo wa kwanza waliosimama mbele akitoa maelezo kwa Afisa wa Idara ya Maendeleo ya Vijana wa tatu kutoka kushoto Bi Amina Sanga katika ziara ya kukagua miradi yaVijana nchini.
Mkurugenzi Msaidizi kitengo cha Mafunzo na Maendeleo ya Ujuzi kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Venerose Mtenga akitoa mada katika Mafunzo ya Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma kuhusu Mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Viewing all 110150 articles
Browse latest View live




Latest Images