Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 526 | 527 | (Page 528) | 529 | 530 | .... | 3272 | newer

  0 0


   Mkulima huyu akionyesha furaha wakati akihudumiwa na Mfanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonyesho ya wakulima 88 mkoni Lindi juzi.
   Maafisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, (Kulia), wakiwasikiliza wananchi hawa waliotembelea banda la Mfuko huo, kwenye maonyesho ya wakulima 88 mkoani Lindi juzi.
   Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, (Kushoto), akiwahudumia wananchi waliotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonyesho ya wakulima Nane Nane, mkoani Lindi juzi. Kilele cha maonyesho hayo yaliyoandaliwa kwa pamoja na mikoa ya Lindi na Mtwara, yatafanyika Agosti nane mkoani Lindi.
   Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, (Kuli), akiwahudumia wananchi waliotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonyesho ya wakulima Nane Nane, mkoani Lindi juzi. Kilele cha maonyesho hayo yaliyoandaliwa kwa pamoja na mikoa ya Lindi na Mtwara, yatafanyika Agosti nane mkoani Lindi


  0 0

  Taarifa ya kupotelewa kwa mtoto Faith Charles Ruhembe. Amepotea tangu 31.07.2014 saa saba mchana, eneo la makumbusho usalama. Ni binti wa miaka tisa (9) na anasoma shule ya msingi Martin Luther Dodoma.

  Usalama ni kwa shangazi yake Catherine Ruhembe, ambaye ni shemeji yangu na dada wa mke wangu Carolyne Ruhembe. Tumeshatoa taarifa vituo vya polisi na TV pia.

  Pamoja na ujumbe huu, naambatanisha picha yake  kwa ufafanusi zaidi. Kwenye picha ni huyo binti. Ikiwa ufafanuzi zaidi ya huu utahitajika, basi napatikana kwa number hii 0715 119893.
  Asanteni 

  0 0  Karibu kusikiliza hotuba ya Mhe. Dk Jakaya M Kikwete alipozungumza na waTanzania usiku wa Agosti 2, 2014 kwenye hotel ya Marriot, jijini Washington DC nchini Marekani.


  0 0

  SIMBA SC ambayo iko katika shughuli mbalimbali za kuadhimisha Simba Week imefanya ziara  ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza bia cha TBL kinachozalisha bia ya Kilimanjaro Premium Lager inayoidhamini timu hiyo.
  Akiongea katika ziara hiyo  Rais wa Simba, Evans Aveva alisema kuwa wao kama timu ya Simba wameamua kufanya ziara yao katika kiwanda hicho ikiwa ni sehemu ya utaratibu wao kutembelea wadhamini kila mwaka ili kuimarisha uhusiano na wadhamini na kuweza kujionea mambo mbalimbali ambayo yanafanywa na kampuni hiyo inayozalisha bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo ndio wadhamini wakuu wa timu yao.
  Wachezaji wa Simba SC wakiwa TBL jana
  Meneja wa Kilimanjaro, George Kavishe akifurahia jambo na kipa wa Simba SC, Ivo Mapunda kulia

  Alisema kuwa Kilimanjaro Premium Lager imekuwa ikiwapa ushirikiano mkubwa katika mambo mbalimbali ya kimichezo ikiwa ni pamoja na kuwapatia magari ya usafiri jezi pamoja na vifaa mbalimbali vya michezo hivyo wamefurahishwa sana na jinsi walivyopokelewa vizuri kiwandani hapo na aliwaomba waendelee na moyo huo huo wa kuthamini timu yao.
  Akiongea kwa niaba ya kampuni hiyo Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema kuwa wamefurahishwa sana na kitendo hiki cha timu hii ya Simba kuamua kuacha shughuli zao na kutembelea kiwanda chao na kuona kazi ambazo zinafanywa na kampuni hii.
  Alisema kuwa TBL inathamini mchango wa timu za Simba na Yanga kwa soka la Tanzania na ndio maana imekuwa ikizidhamini timu hizi kwa muda mrefu huku akibainisha kuwa wataendelea kudhamini timu hizi hadi mwisho.
  Alibainisha kuwa timu hizi mbili zimekuwa zikifanya mambo makubwa kwani zimekuwa zikiwapatia vijana mbalimbali ajira kwa kupitia timu zao.
  Aliwasihi wananchi kwa ujumla kuendelea kuisapoti timu hizi kwani ndio timu mbazo zina wachezaji wengi zaidi wanaochezea timu ya taifa.
  Kavishe alisema kuwa kupitia kudhamini timu hizi pia wamekuwa wakijitangaza sehemu mbalimbali kwani iwapo timu ikienda kucheza nje ya nchi wanaenda kukitangaza kinywaji chake cha Kilimanjaro Premium Lager hivyo wanafanya  kampuni hii pamoja na bia ya Kilimanjaro kuwa juu zaidi.

  0 0

  HAYATI JULIO GRONDORA
  Rais wa Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Shrikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa), Sepp Blatter kutokana na kifo cha makamu wake mwandamizi Julio Grondora.
  Amesema yeye binafsi na jamii ya mpira wa miguu Tanzania kwa ujumla wanaomboleza msiba wa Grondora ambaye pia alikuwa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Argentina (AFA).
  Ameongeza kuwa Grondora alikuwa mtumishi mwandamizi wa mpira wa miguu, kwani alijitoa katika kuutumikia mpira wa miguu, na mchango wake katika maendeleo ya mchezo huo utaendelea kukumbukwa wakati wote.
  Rais Malinzi amesema familia ya mpira wa miguu nchini Argentina imepata pigo, na ametoa pole kwa familia ya marehemu, AFA na familia nzima ya Fifa na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

  0 0

   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana na Mjumbe wa Bunge la Katiba, Frederick Msigallah kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo Agosti 5, 2014. 


  0 0

  Mhe. Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ( mwenye mkasi) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mtandao wa Kuunganisha Taasisi za Elimu ya Juu na Utafiti nchini. Anayeshuhudia ni Prof. Tolly Mbwete, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania na mwakilishi wa Benki ya Dunia, Tanzania.

  Mtandao huo umeunganisha Taasisi za Elimu ya Juu na Utafiti 22 nchini ambapo Vyuo Vikuu mbalimbali nchini vinaweza kuwasiliana, kutoa huduma ya elimu mtandao, maktaba mtandao, utunzaji wa taarifa na nyaraka, kufundishia, kuendesha mikutano kwa kutumia huduma ya audio na video, kuhifadhi, kutunza na kulinda taarifa.

  Mtandao huo Taasisi za Elimu ya Juu na Utafiti umeunganishwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ambapo unaziwezesha Taasisi hizo 22 kuwasiliana kwa haraka na kwa wakati. Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia imesimamia na kuratibu jukumu hilo la Uunganishaji wa Taasisi za Elimu ya Juu na Utafiti kwa kushirikiana na Benki ya Dunia. 

  Aidha, Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, Kampuni ya Simu Tanzania, Taasisi ya Serikali Mtandao na Chuo Kikuu Huria Tanzania kwa pamoja zitashirikiana kufanikisha matumizi Endelevu ya mtandao huo kwenye Taasisi za Elimu ya Juu na Utafiti nchini kwa manufaa ya Taifa letu na kuongeza kasi ya matumizi ya Tekonolojia ya Habari na Mawasiliano.

  Uzinduzi huo umefanyika Chuo Kikuu Huria Tanzania, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Wadau mbalimbali wa sekta ya TEHAMA nchini.

  Imetumwa na Prisca Ulomi, 
  Msemaji wa Wizara    

  0 0

  MTANDAO wa wanafunzi nchini (TSNP) Umetoa tamko dhidi ya mwenendo wa mchakato wa kupata Katiba mpya ya Tanzania.

  Mkurugenzi mtendaji wa mtandao wa wanafunzi Bwana Alphonce Lusako ametoa tamko hilo katika mkutano ulioudhuriwa na  waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

  Lusako ametoa ombi kwa vyama vyote vya siasa kurudi bungeni na kufanya maridhiano ili tuweze kupata katiba mpya ambayo itasaidia kuokoa mabilioni ya fedha za watanzania ambazo zimekwisha tumika katika mchakato wa kutafuta katiba mpya.

  “Tunawaomba CCM,UKAWA,TANZANIA ONE na wajumbe wa Bunge Maaalum la Katiba kujua kuwa kushindwa kwa mchakato huu siyo kushindwa kwa  kwa chama chochote ila ni kushindwa kwa Watanzania,”alisema Lusako.

  Viongozi wa mtandao wa wanafunzi nchini, umewaomba UKAWA, CCM na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wafikie muafaka na watambue kuwa sheria kuu ya wao ndani ya bunge ni kuboresha Katiba ya wananchi na siyo kupindua maamuzi ya wananchi.

  Wajumbe  wa Bunge Maalum la Katiba  wanatakiwa wajue kuwa hawapo kwa ajili ya kutafuta na kutambua mshindi na mshindwa, bali upo kwa ajili ya ushindi wa watanzania ambao pesa zao nyingi zimetumika.

  Aidha, ameongeza kwa kusema kuwa, mchakato haupo kwa ajili ya kutambua nani anamsimamo huu na msimamo ule,bali upo kwa ajili ya kutambua msimamo wa watanzania juu ya namna gani taifa lao litaongozwa na katiba iliyotokana na mawazo yao.

  Mtandao wa wanafunzi nchini uliitisha kongamano rasmi la wanafunzi wa Vyuo Vikuu na sekondari kwa ajili ya kujadili mchakato mzima wa kupata Katiba mpya ndani ya Taifa letu ambao uliwapa wanafunzi fursa ya kupaza sauti zao juu ya mchakato mzima wa katiba.

  0 0

  President Jakaya Mrisho Kikwete shakes hands with Virginia M. Ginni Rometty, the Chairman, President and Chief Executive Officer of IBM during a dinner hosted by Mayor of New York and Chairman of the Bloomberg Philanthropies, Mr Michael Bloomberg, in Washington DC on Monday July 4, 2014. Bloomberg Philanthropies are some of the major sponsors of the US-Africa Leadership Summit.
  President Jakaya Mrisho Kikwete with the Mayor of New York and Chairman of the Bloomberg Philanthropies, Mr Michael Bloomberg, during a dinner in Washington DC on Monday July 4, 2014. Bloomberg Philanthropies are part of the major sponsors of the US-Africa Leadership Summit. STATE HOUSE PHOTOS

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr. Rajab Lutengwe, ameusifia mtandao wa kijamii wa Mbeya Yetu Unaomilikiwa na Tone Multimedia Group kwa kuonesha mabadaliko ya kwenda na wakati katika  teknolojia ya  mawasiliano na habari teknolojia ya kisasa.

   Dr. Lutengwe ametoa pongezi hizo hivi wakati akitoa tathmini yake mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali kwenye maonesho ya wakulima  maarufu kama Nane nane yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

  Alisema kuwa mtandao huu umeonesha chachu ya mabadaliko katika sekta ya mawasiliano kwa kukuza na kutangaza uchumi wa ndani na nje ya nchi kwa kurusha matukio mbalimbali yanayoendelea katika maonesho hayo.

  “Nimewapenda sana wale vijana wa mtandao wa Mbeya Yetu  kwa kazi yao ya kurusha matukio yanayoendelea kwenye viwanja hivi, huko tunakoelekea hivi sasa katika kukuza biashara ya mazao yetu ni lazima tutangaze kupitia ‘Google’ Mbeya yetu imeonesha njia sahihihi ya kukabiliana na soko la uchumi na kama wataenedelea na kasi ile watafika mbali” alisema.

  Alisema kwa kutumia mitandao ya kijamii taarifa mbalimbali zinazohusu sekta ya kilimo zinawafikia wananchi wengi kwa mara moja na kuwa ni muhimu kwa halmshauri za wilaya kuanzisha Tovuti na Blogu ili kuendana na wakati.
  Banda la Mbeya yetu Blog
  Mtoa Maelezo kutoka Tone Multimedia Group kupitia Mtandao wao wa Mbeya yetu Blog Fredy Anthony Njeje wa kwanza kulia akitoa maelezo ya kina kwa   Mkuu wa Mkoa wa  katavi  Mh.Dr Rajab Lutengwe jinsi mtandao wa Mbeya yetu unavyofanya kazi pia unavyosaidia upatikanaji wa habari kwa urahisi kabisa. Pia kuekeza sababu za Kushiriki katika mashindano ya nane nane ikiwa ni pamoja na Kutoa elimu juu ya mitandao ya kijamii na faida zake hasa upande wa Blogs na matumizi sahihi.
   Fredy Anthony Njeje akijibu swali la Mkuu wa Mkoa wa Katavi  Mh.Dr Rajab Lutengwe kuwa si Mtandao wa Mbeya yetu pekeee lakini kupitia Blogs za Mikoa Tanzania ambazo zinajumuisha Blogs za mikoa yote Tanzania na hapa akimuonesha mtandao wa KATAVI YETU ambapo yeye ndipo anapotokea.
    Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Dr Rajab Lutengwe akiwapongeza Tone Multimedia Group kwa kuanzisha Mtandao wa Blogs za Mikoa na Mbeya yetu Blog ikiwemo ndani yake kwa ubunifu mkubwa na kazi kubwa wanayoifanya ili kufikisha taarifa kwa kila mkoa na Mtandao wake na kusisitiza kuwa ni vizuri kuendelea na moyo huo huo ili kuendelea kuhabarisha jamii kwa ujumla.
    Mkuu wa Mkoa wa Katavi  Mh.Dr Rajabu Lutengwe  wa tatu kutoka kushoto akitoa ushauri kwa Blog ya katavi yetu baada ya kuweka Mnyama Tembo awekwe mnyama Kiboko kwa sababu ndiye alama kubwa ya utalii katika Mbuga ya Wanyama ya Katavi.
   Fredy Anthony Njeje akiendelea kumpa maelezo Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr. Rajab Lutengwe juu ya kazi zengine ambazo kampuni ya Tone Multimedia Group inazifanya ikiwa ni pamoja na Radio ya Mtandaoni Tone Radio, Mtandao Maalum ambao unawahusu wanafunzi Matukio na wanavyuo, Huduma Mpya ya kupata habari kwa njia ya Simu kwa watu wenye Whatsapp Tone Mobile News, Mtandao wa watanzania waishio nje ya nchi pamoja na kazi zote za ambazo kampuni inazifanya. Wa kwanza kutoka kushoto ni Mwandishi wa Mbeya yetu Venance Matinya.
  Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu Blog Joseph Mwaisango wa kwanza upande wa kushoto akiendelea kutia maelezo kwa baadhi ya watu waliotembelea katika banda la Mbeya yetu blog.

  0 0

  Napenda kuwajulisha kwamba mtoto Faith amepatikana maeneo ya Msasani na ameshaungana na familia. Aliokotwa na Msamaria mwema ambaye nae alikuwa anafanya juhudi za kuitafuta familia yetu.

  Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru sana sana kwa msaada wenu wa kurusha habari ile ya kupotea kwake. Lakini zaidi sana nawashukuru  jinsi mlivyotenda kwa haraka (act promptly) nilipotuma tu ujumbe.

  Hii imeonyesha umuhimu wa mitandao hii na ni kweli ya wananchi na jamii. 

  Asanteni sana na kila la heri.

  0 0

  Bondia Khalid Chokoraa (kushoto), ambaye pia ni mwanamuziki wa bendi ya  Mapacha watatu  akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Rashidi Juma wakati wa mazoezi katika kambi yake iliyoko  Mwananyamala jijini Dar es salaam akijiandaa kupambana na  Said Memba katika mpambano wao utakaofanyika Agosti Nane wakati wa siku ya tamasha la matumaini Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
  Bondia Khalid Chokoraa akipiga begi wakati wa maandalizi ya kujiandaa na mchezo wake 
  Bondia Khalid Chokoraa  kushoto akielekezwa jinsi ya kupiga 'upper-cut' na Ramadhani Jifasto wakati wa mazoezi yake yanayoendelea katika kambi yake iliyoko  mwananyamala jijini Dar es salaam
  Bondia Khalid Chokoraa. Picha zote na Super D

  0 0

   KANISA la Waadventista wa Sabato la Pugu Chanika lililopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam sasa linaweza kuendeleza mradi wake wa ujenzi na upanuzi wa kanisa baada ya kupata msaada wa fedha wa shilingi milioni 5 kutoka kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL). Msaada huo uliotolewa wakati wa ibada Jumamosi, umefufua jitihada la kanisa za kutanua na kumalizia ukumbi wa kanisa uliopo sasa pamoja na kumalizia ujenzi wa majengo mengine.

  Mwakilishi kutoka IPTL ambayo ni kampuni tanzu ya Pan African Power Solutions Tanzania (PAP), Bw. Joseph Makandege, ambaye ni Katibu na Mwanasheria Mkuu wa kampuni hiyo, amesema msaada huo ni sehemu ya jitihada za kampuni yake kuunga mkono miradi mbali mbali yenye manufaa makubwa kwa kijamii.

  “Baada ya kupokea maombi toka katika kanisa hilo ya kututaka kusaidia mradi huo wa ujenzi, Bodi ya wakurugenzi ya IPTL/PAP ikiongozwa na Mwenyekiti Mtendaji Bw. Harbinder Singh Sethi mara moja ilipitisha kiasi cha shilingi milioni 5 kwa kuwa inaamini kuwa taasisi za kidini zinasaidia kulijenga taifa lenye watu wanaomuogopa Mungu na hivyo kuifanya nchi iwe na mazingira mazuri ya kufanya biashara ambayo inasaidia kuleta maendeleo ya kiuchumi.

  “Tunaamini kuwa katika makanisa, familia zilizotengana zinaunganishwa, waliuokosa matumaini wanapewa matumaini, na maisha ya watu yanabadilika. Inampendeza Mungu kusikia sauti za nyimbo zinazomtukuza, ujumbe madhubuti kutoka kwa wachungaji, ushuhuda wa kazi zitokanazo na Mungu, na sauti nzuri za watoto zisema Amina.

  “Kampuni yetu isingeweza kukataa ombi hilo la kusaidia kanisa katika mradi ambao utatukuza kazi ya Mungu na maisha ya walio wengi katika jamii yetu yatabadilishwa kwa ujumla,” alisema Makandege. Aliliasa kanisa kutumia fedha hizo vizuri ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa.

  Naye, Mchungaji wa Kanisa hilo, Gallus Gido aliishukuru IPTL/PAP kwa mchango wao ambao alisema umewagusa watu wengi na utalisaidia kanisa kuweza kuwahudumia waumini wengi wanaomtukuza na kumuomba Mungu.

  "Katika kitabu cha Matendo 10:1-4, kulikuwa na mtu aliyekuwa akitoa misaada/sadaka kwa jamii yake. Siku moja Mungu alimtokea na kumwambia kwamba sala na sadaka zake zimefika mbinguni. Nataka kuwaambia IPTL/PAP kwamba mchango wao wa kuendelea kusaidia taasisi mbalimbali ya kidini na jamii kwa ujumla, utawafungulia milango mbinguni kwa ajili ya baraka zaidi," alisema.


  Mchungaji aliongeza kuwa mchango wa IPTL/PAP unadhihirisha upendo wa kampuni hiyo kwa Mungu na watu, na kuhaidi kuwa atafanyakazi kwa ukaribu na kamati ya ujenzi kuhakikisha kuwa fedha hizo zinatumika vizuri kwa lengo lililokusudiwa.

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia(aliyevaa Kombati) akiangalia mazao ya chakula yanayolimwa  katika Magereza mbalimbali hapa nchini kama yanavyoonekana katika picha. Jeshi la Magereza katika kutekeleza jukumu lake la kuwalinda na kuwarekebisha Wafungwa huwapatia pia mbinu na Stadi za Kilimo bora ili waweze kuzitumia wanapomaliza vifungo vyao huko katika jamii zao.
   Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia akifurahia ubora wa bidhaa za ngozi zinazozalishwa na Jeshi la Magereza katika Kiwanda chake cha Viatu cha Gereza Karanga Moshi, Mkoani Kilimanjaro(kushoto) ni Afisa Masoko wa Shirika la Magereza, Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Yunge Saganda akionesha kiatu cha ngozi aina ya travota(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Banda la Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mlasani Kimaro.
   Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Mstaafu Simbakalia akitembelea Mabanda ya Mifugo ya Jeshi la Magereza mara tu baada ya kuwasili katika Banda la Jeshi la Magereza(kushoto t-sheti ya blu) ni Mtaalam wa Mkfugo(ndege) Sajini Taji Nesia Hozza toka Gereza la Wanawake, Kingolwira Mkoani Morogoro akitoa ufafanuzi wa Kitaalam namna Ufugaji wa kuku unavyopaswa kufanyika.
   Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia(aliyevaa Kombati) akipata elimu ya Shamba Darasa toka kwa Mtaalam wa Kilimo cha Mbogamboga wa Jeshi la Magereza, Sajini Taji Oliva William(mbele t-sheti ya blu) toka Gereza Nachingwea namna Bustani za Mbogamboga zinavyostawishwa kwa kuzingatia Kanuni za Kilimo cha Kisasa na Biashara(wa Nne kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Lindi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Tusekile Mwaisabila.
  Mkuu wa Banda la Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mlasani Kimaro(wa kwanza kulia) akikabidhi zawadi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia(aliyevaa Kombati) alipotembelea Banda hilo leo Agosti 04, 2014 katika Viwanja vya Maonesho ya Nane Nane vya Ngongo, Mkoani Lindi. Kanali Mstaafu Simbakalia amelipongeza Jeshi la Magereza kutokana na ubunifu mkubwa uliopo katika shughuli zake mbalimbali zilizopo katika Banda hilo.
   Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia(kushoto) akiwasili katika Banda la Jeshi la Magereza tayari kujionea shughuli mbalimbali zenye tija zinazofanywa na Jeshi la Magereza(kulia) ni Mkuu wa Banda la Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mlasani Kimaro akimuongoza Mkuu wa Mkoa wa Mtwara katika sehemu mbalimbali za Banda la Jeshi la Magereza alipotembelea leo Agosti 4, 2014 katika Viwanja vya Maonesho ya Nane Nane Kitaifa, Mkoani Lindi.
  .(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  0 0

   Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange pamoja na ujumbe wake, akiwa na Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe. Omar Mjenga, wakiwa katika picha ya pamoja na mtumishi wa Hoteli ya Continental ya Dubai, ambaye kwa sasa ndiye Mtu Mrefu Duniani.

  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akipokea maelezo ya kitaalam alipotembelea Makao Makuu ya Kampuni ya General Electric (GE)  ya nchini Marekani  inayojishughulisha na utengenezaji na uuzaji wa vifaa vya kufua umeme. Moja ya bidhaa zao ni mitambo ya kufua umeme itakayotumika katika mradi wa  kufua umeme wa Kinyerezi  I wa kiasi cha megawati 150.

  0 0

  Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Dodoma Mhe: Athuman Mwenda akipata maelezo ya kina jinsi ya uandaaji wa taarifa za hali ya hewa kwa wakulima ili kufanikisha kauli mbiu ya mwaka huu yenye ujumbe wa ‘Matokeo Makubwa Sasa’-Kilimo ni Biashara, vilevile Mamlaka inatekeleza mkakati wa Taifa wa KILIMO KWANZA.Maelezo hayo yalikuwa yakitolewa na kwa Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi Dkt. Ladislaus Chang’a katika banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa kwenye maonesho ya NaneNane 2014, viwanja vya Nzuguni-Dodoma.
  Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Dodoma Mhe: Athuman Mwenda akipata maelezo mafupi ya uangazi wa hali ya hewa ardhini kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi Dkt. Ladislaus Chang’a alipotembelea banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa, katika maonesho ya NaneNane 2014, viwanja vya Nzuguni-Dodoma.

  0 0

  Halmashauri zote nchini zinawajibika kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya vijana pamoja na kuwatengea vijana asilimia 5 ya mapato ya halmashauri husika kwa ajili ya kuwezesha shughuli hizo.

  Hayo yamesemwa jana ( leo) Mkoani Dodoma Wilaya ya Nchemba na Afisa Vijana wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bi. Amina Sanga katika mafunzo ya Vijana wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kuhusu mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.

  Bi. Amina alisema kuwa vijana ndiyo nguvu kazi ya taifa na kwa maana hiyo wanatakiwa waongozwe na wawezeshwe ili kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo kwa lengo la kujikwamua katika umaskini.

  “Vijana wanatakiwa kuhamasishwa kuunda na kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali na kuunda SACCOS za vijana ili waweze kupatiwa mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kwa ajili ya kuongeza mitaji na kupanua uzalishaji”. Alisema Bi Amina.

  Aidha aliwashauri kujituma na kuchangamkia fursa mbalimbali ikiwemo mikopo inayotolewa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.

  “Nchemba ni miongoni mwa Wilaya zenye fursa nyingi kwa vijana ikiwemo kilimo ambacho kimekuwa kikitoa ajira kwa Watanzania zaidi ya asilimia 70 waishio vijijini”.Alisema Bi. Amina Akiongea na vijana katika moja ya ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo alisema vijana wanayo nafasi kubwa ya kuleta maendeleo katika maeneo yao hivyo wanapaswa kuwa wabunifu wa miradi itakayowaingizia kipato.

  Pia aliwataka kuhakikisha kuwa wanasajili vikundi vyao ili viweze kutambulika kisheria na pia wajiunge katika SACCOS ya vijana ili iwe rahisi kupatiwa mikopo ya kuendeleza shughuli zao za uzalishaji mali.

  Katika mafunzo hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nchemba Bw. Boniface Mandi amewashauri vijana waachane na matumizi ya madawa ya kulevya na kutumia fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali.

  Kwa upande wa Vijana hao alishukuru Idara ya Maendeleo ya Vijana kupitia Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo kwa kuwapatia mafunzo hayo kwani wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali katika utendaji wao wa shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa.
  Afisa wa Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akitoa mada katika Mafunzo ya Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Nchemba mkoani Dodoma kuhusu Mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana. Picha na Benjamin Sawe

  0 0

  Nakumatt holdings MD Atul Shah (left) guides Tanzania's Deputy Minister Hon. Janet Mbene (centre) on a tour of the new Nakumatt Mlimani as the retailer's Regional Director Mr Thiagarajan Ramamurthy looks on.

  Regional retailer, Nakumatt Holdings, has officially opened its second, Dar Es Salaam, Tanzania, store as it inches closer to the opening of its 50thbranch in coming days.

  The opening of the 49thNakumatt store this morning, is a major milestone for the retailer which had earlier set a corporate target to open 50 branches by February 2015.

  Following its recent acquisition of three retail stores formerly owned by South African retailer Shoprite, Nakumatt, has now opened its 49th branch to be known as Nakumatt Pugu Road and is on course to open its 50thbranch in Arusha, Tanzania in the next two weeks.

  Speaking during the official opening ceremony, Nakumatt Holdings, Managing Director, Atul Shah, said the opening of the store, will further enhance the retailer’s footprint in Dar es Salaam.

  “The opening of Nakumatt Pugu Road Supermarket is a major milestone for us, particularly because we are essentially racing against time to complete the progressive launch of the three new Tanzania branches by mid-August,” Shah explained.

  And added: “The new Nakumatt Pugu Road will essentially enhance our footprint in Dar Es Salaam city where we are already enjoying overwhelming support following our recent opening of Nakumatt Mlimani also in Dar.”

  Located along the busy Nyerere road in Dar Es Salaam, Nakumatt Pugu Road, historically holds the pride of place as the first Shoprite store ever opened in Tanzania by the South African retailer way back in 2001. With the recent acquisition, the Nakumatt Pugu Road Complex will also host the retailer’s (Nakumatt) Tanzania’s Headquarters; acting as the hub for its Moshi, Arusha and Dar Es Salaam stores.

  As part of a phased out opening plan, the store has been outfitted to the signature Nakumatt corporate colours and layout.

  With the opening of Nakumatt Mlimani and Pugu road, Shah, pointed it out that Nakumatt now has three running stores in Tanzania. Nakumatt Pugu road and Mlimani are the latest additions to the existing Nakumatt Moshi store which opened its doors in 2011 in the bustling town at the foot of Mt Kilimanjaro.

  In Kenya, Nakumatt is also gearing up for the opening of three new stores in Kenya by the end of the year.

  0 0


older | 1 | .... | 526 | 527 | (Page 528) | 529 | 530 | .... | 3272 | newer