Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110010 articles
Browse latest View live

OFAB TANZANIA YATOA SEMINA KWA WAHARIRI WA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI NCHINI

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti cha Mikocheni (MARI), Dk. Andrew Ngereza akitoa historia fupi ya kituo hicho wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na Jukwaa la Bioteknoloji Tanzania (OFAB)
Mkurugenzi wa Sayansi Hai wa COSTECH, Dk.Flora Tibazarwa akitoa mada katika semina hiyo. 
Mtafiti Kiongozi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, (COSTECH), Dk.Nicholas Nyange (kulia), akielekeza jambo wakati wa semina hiyo.
Mtaalamu wa masuala ya Bioteknoloji, Dk. EmmaroldMneney akitoa mada kwa wahariri.
Mwakilishi wa UN-NEPAD, Profesa, Dirian Makinde (kulia), akitoa mada kuhusu matumizi sahihi ya Uhandisi Jeni.
Mtafiti Dk. Fred Tairo (kushoto), akiwaelekeza jambo wahariri hao, baada ya kutembelea Maabara ya Uhandisi Jeni iliyopo katika Kituo hicho.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO NCHINI MAREKANI

Ligi ya Wanawake Dar kuanza Agosti 28

$
0
0
LIGI ya Wanawake Mkoa wa Dar es Salaam inatarajiwa kaunza Agosti 28 mwaka huu katika viwanja vya  Benjamin Mkapa, Bandari na Makurumla.

Ofisa Habari wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Mohamed Mharizo alisema kuwa ligi hiyo ni moja ya mkakati wao wa kuimarisha mchezo ili uweze kuwa na hamasa kwa wanawake.

Alizitaja timu zitakazoshiriki ligi hiyo kuwa ni Mburahati Queens, Evergreen Queens, Sayari, Real Tanzanite, Uzuri Queens,  Simba Queens,  BYC Queens, JKT Queens,  Lulu Queens,  Mchangani Sisters, TMK Queens, Msimamo Queens na Mikocheni Queens.

“Kwa kweli ligi ya wanawake nayo ni muhimu kama ilivyo kwa wanaume, lengo letu ni kuona wanawake wanakuwa na ligi yao na sisi tunaona hili ni jambo zuri ambalo litasaidia kupata wachezaji wa timu ya taifa (Twiga Stars).

Mharizo aliyaomba makampuni na taasisi mbalimbali kujitokeza kudhamini ligi hiyo ili iweze kuleta ushindani kwa timu shiriki.

Naibu Spika wa Bunge na Ujumbe wake watembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Malaysia

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania,Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akiwa ameambatana na waheshimiwa   Wabunge Saleh Ahmed Pamba, (Pangani),Abdulkarim Esmail Hassan Shah (Mafia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Ponary Mlima (wa tatu kulia) pamoja na maafisa wa Ubalozi huo wakati walipotembelea Ubalozini hapo wakiwa kwenye ziara ya kikazi nchini Malaysia.

MKUU WA WILAYA YA NACHINGWEA ATEMBELEA BANDA LA JESHI LA MAGEREZA MAONESHO YA NANE NANE KITAIFA MKOANI LINDI

$
0
0
Afisa Mshiriki wa Maonesho ya Wakulima na Wafugaji katika Banda la Jeshi la Magereza, Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Yunge Saganda(kushoto) akitoa maelezo ya kitalaam kwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mhe. Regina Chonjo(kulia) namna viatu vya Ngozi vinavyotengenezwa na Jeshi hilo katika Kiwanda chake cha Gereza Karanga, Moshi Mkoani Kilimanjaro. Jeshi la Magereza ni Miongoni mwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vinavyoshiriki kikamilifu katika Maonesho hayo ya Kitaifa Mkoani Lindi.
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mhe. Regina Chonjo(wa pili kushoto) akiangalia Mbegu ya Ufuta inayozalishwa na Jeshi la Magereza kupitia miradi mbalimbali ya Kilimo katika Magereza ya Kilimo hapa Nchini(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Lindi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Tusekile Mwaisabila.
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mhe. Regina Chonjo akikagua Bustani ya Shamba Darasa iliyopo katika Banda la Jeshi la Magereza katika Viwanja vya Maonesho vya Ngongo, Mkoani Lindi. Bustani hiyo iliyostawishwa kwa kufuata Kanuni za Kilimo Bora na Biashara inatumika kutoa elimu kwa Wakulima wanapotembelea Banda hilo katika Maonesho haya ya Kimataifa.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Abdallah Ulega(kulia) akisalimiana na Mkuu wa Magereza Mkoani Lindi alipotembelea Banda la Jeshi la Magereza ili kujionea shughuli mbalimbali za Kilimo na Ufugaji zinazofanywa na Jeshi hilo katika Maonesho hayo ya Nane Nane.
Lango Kuu la kuingia katika Banda la Jeshi la Magereza katika Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika katika Viwanja vya Maonesho ya Ngongo, Mkoani Lindi. Jeshi la Magereza ni Miongoni mwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vinavyoshiriki kikamilifu katika Maonesho hayo(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

bosi wa azania bank anadi huduma yake mpya ya Diaspora banking kwa wanadiaspora Marekani

Mhe stephen masele aongelea mpango wa rais obama wa viongozi vijana wa afrika

ASKARI FEKI MWINGINE WA USALAMA BARABARANI ANASWA DAR

$
0
0
 Askari feki wa Usalama Barabarani ambae Jina lake halikufahamika haraka akiwa chini ya Ulinzi mkali wa Askari Polisi (hayupo pichani) mara baada ya kukamatwa kwa kujifanya ni askari wa usalama barabarani huku akifahamu kuwa ni kosa kisheria. Inasemekana Mtuhumiwa aliwahi kuwa askari wa Usalama barabarani ambapo kituo chake cha Kazi kilikuwa Mkoa wa Pwani na ni mmoja kati ya askari waliofukuzwa kazi kwa kuenda kinyume na taratibu na sheria za Jeshi la Polisi Tanzania
 Askari Polisi ambae jina lake halikufahamika mara moja (Mwenye sweta) akimkamata kwa makini mtuhumiwa aliyejifanya askari wa usalama barabarani leo katika eneo la Chamazi Jijini Dar Es Salaam
Askari feki akishangaa na kuduwaa mara baada ya jeshi la Polisi Kumtia nguvuni leo Katika Eneo la Chamazi Jijini Dar Es Salaam Mapema leo.Picha Kwa Hisani ya Mdau.

BAADA YA KIPIGO CHA SERENGETI BOYS, MALINZI AKIRI UBOVU WA MAANDALIZI NA KUKOSEKANA KWA MFUMO SAHIHI WA SOKA LA VIJANA

$
0
0
BAADA ya timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya miaka 17, Serengeti Boys kutolewa katika michezo ya kuwania kufuzu fainali za Afrika za vijana na Afrika kusini kwa wastani wa mabao 4-0, Rais wa shirikisho la soka Tanzania, TFF, Jamal Emil Malinzi amekiri kuwa bado timu haijaandaliwa vizuri.

Rais Malinzi amesema tatizo la timu ni maandalizi yasiyoridhisha yanayochangiwa na kukosa mfumo sahihi na mpango mzuri wa soka la vijana.

“Tatizo letu ni lile lile, kwenye maandalizi, lakini tunapozungumzia maandalizi tunazungumzia uwezo wa kiuchumi, kwamba timu yetu inaandaliwaje,” Alisema Malinzi.

“Tunaweza kusema timu imejitahidi, Lakini kiukweli hii ndio mechi yao ya pili ya kimataifa, mechi yao ya kwanza walicheza na Afrika kusini nyumbani.

“ Kwahiyo lazima sisi tukae kama nchi, kama shirikisho ili tuweze kuangalia programu zetu za soka la vijana ili watoto kama hawa kabla hawajaingia katika mechi kama hizi wawe wameshakaa kama timu kuanzia umri wa 12, 13, 14 na 15 , yaani wakae miaka minne kwenye timu ya taifa,” Aliongeza Malinzi.

Aidha, Rais Malinzi alisema shirikisho hilo limejipanga upya ili kuhakikisha nchi inakuwa na mfumo sahihi wa soka la vijana. “Kipo ambacho kinafanyika, tunaandaa mpango wa kitaifa wa maendeleo ya soka la vijana na tutazindua mwezi wa 10 mwaka huu, siku ambayo TFF itatimiza miaka 10 ya kujiunga na FIFA na tutaeleza haya tunayoyasema ili kama nchi tuwe na mpango endelevu wa soka la vijana,”

ALVIN NA SUSAN WAMEREMETA

$
0
0

 Alvin akivisha pete Susan kwenye harusi yao iliyofanyika siku ya Jumamosi Aug 2, 2014 kwenye ukumbi wa Noah's uliopo Fairview ma kuhudhuriwa ndugu, jamaa na marafiki kutoka kila kona ya Dunia.
 Susan akimvisha pete Alvin kwenye harusi yao iliyofanyika siku ya Jumamosi Aug 2, 2014 kwenye ukumbi wa Noah's uliopo Fairview ma kuhudhuriwa ndugu, jamaa na marafiki kutoka kila kona ya Dunia.
Maharusi wakichum baada kufunga ndoa yao.
Maharusi wakitoka nje baada ya ndoa yao kumalizika kuelekea kupata ukodak moment kwa ajili ya kumbukumbu yao ya siku hii maalum kwao na katika maisha yao.
Kwa picha zaidi bofya hapa

SIMBA WAFANYA MKUTANO, YAWAFUKUZA WANACHAMA 72 WALIOFUNGUA KESI MAHAKAMANI

$
0
0
Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva akifafanua jambo wakati wa mkutano maalum wa wananchama wa klabu hiyo uliofanyika kwenye Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Baadhi ya wanachama wa Simba wakiwa katika mkutano maalum wa klabu hiyo jijini Dar es Salaam 
Baadhi ya wanachama wa Simba wakihakiki kadi zao kabla ya kuingia katika ukumbi wa mkutano.
Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali akipitia nyaraka za klabu hiyo wakati akiingia katika ukumbi wa mkutano maalum wa Simba uliofanyika katika Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
 Wanachama wa Simba wakiwa katika mkutano huo.

Wanachama wa Simba wakipitia nyaraka mbalimbali wakati wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba, Damasi Ndumabaro akizungumza wakati wa mkutano huo.

WAZIRI MKUU ALIAGIZA JIJI LA MBEYA KUKUSANYA MAPATO ZAIDI

$
0
0
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameutaka uongozi wa Jiji la Mbeya uongeze mapato yake ya ndani kwa kuweka mifumo ya kisasa ya ukusanyaji mapato.

Ametoa agizo hilo jana (Jumamosi, Agosti 2, 2014) wakati akizindua stendi ya kisasa ya mabasi katika eneo la Nane Nane nje kidogo ya Jiji la Mbeya.

“Nikuombe Meya Kapunga, wewe na watu wako ongezeni mapato ya ndani ya Jiji la Mbeya. Wekeni mifumo ya kisasa ya makusanyo inayotumia teknolojia ya habari na mawasiliano, acheni kutumia risiti za kuandika wa mikono,” alisema.

Akizungumzia mradi wa stendi mpya ya mabasi, Waziri Mkuu alisema ujenzi wa stendi hiyo ni miongoni mwa kazi zilizo kwenye mradi mkubwa unaohusisha uboreshaji wa huduma na miundombinu kwenye miji na majiji saba hapa nchini (Tanzania Strategic Cities Programme).

Alisema mradi huo uliibuliwa na Serikali tangu mwaka 2006 kwa kushirikiana na Benki ya Dunia. Miji na majiji mengine yanayohusika na mradi huo ni Mwanza, Arusha, Tanga, Kigoma, Mtwara na Dodoma.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MTUKUFU AGAHKAN IKULU DAR ES SALAAM, LEO

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Mwanzilishi na Mwenyekiti   wa Taasisi ya Maendeleo ya Agakhan Duniani, His Higness Prince Karim Agakhan, wakati alipowasili Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Agosti 3, 2014 kwa mazungumzo. Mtukufu Agakhan yupo nchini kwa ziara binafsi ya siku nne, ambapo pia atatumia fursa hiyo kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo ya Taasisi hiyo, ikiwa ni pamoja na kukagua mradi wa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Agakhan ‘New Compass of Agakhan Univercity’ kinachojengwa jijini Arusha. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mwanzilishi na Mwenyekiti   wa Taasisi ya Maendeleo ya Agakhan Duniani, His Higness Prince Karim Agakhan, wakati alipowasili Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Agosti 3, 2014 kwa mazungumzo.  Kulia ni Mbunge Tabora Kaskazini, Shafin Sumari. Mtukufu Agakhan yupo nchini kwa ziara binafsi ya siku nne, ambapo pia atatumia fursa hiyo kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo ya Taasisi hiyo, ikiwa ni pamoja na kukagua mradi wa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Agakhan ‘New Compass of Agakhan Univercity’ kinachojengwa jijini Arusha.

President Kikwete visits INSTITUTE OF HEALTH IN USA (NATIONAL INSTITUTE OF HEALTH)

$
0
0
President Jakaya Mrisho Kikwete with Reasearch fellow and Senior Lecturer at the Muhimbili University of Health Sciences, Dr Julie Makani (left) and Prof. Mwaikambo during his familiarisation tour of the National Institutes of Health (NIH) in Washington DC July 2, 2014.
President Jakaya Mrisho Kikwete speaks with members of the National Institutes of Health (NIH) in Washington DC during a familiarisation tour of the NIH, reputedly the largest hospital and reasearch facility in the world July 2, 2014.
President Jakaya Mrisho Kikwete enjoys a light moment with President Dennis Sassou Nguesso of the Republic of Congo, during their familiarisation tour of the National Institutes of Health (NIH) in Washington DC July 2, 2014. 
President Jakaya Mrisho Kikwete and President Dennis Sassou Nguesso of the Republic of Congo, in a group photo with members of the National Institutes of Health (NIH) in Washington DC July 2, 2014.

WANANCHI WA MKOA WA LINDI WAASWA KUJIUNGA NA CHF-ZAMBI

$
0
0
SERIKALI imeutaka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuendesha huduma za elimu ya kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza katika mikoa yote hususani vijijini pamoja na upimaji wa afya bure ili wananchi watambue afya zao na hatimaye kuongeza uzalishaji katika sekta za kilimo na uvuvi na biashara kwa ujumla.

Agizo hilo lilitolewa na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Godfrey Zambi wakati wa maonesho ya Nane Nane Kitaifa yanayoendelea mkoani Lindi ambapo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeshiriki na unatoa huduma mbalimbali zikiwemo za elimu kwa Umma, usajili wa wanachama, upimaji afya bure ikiwemo saratani ya matiti.

Aidha alisisitiza kuwa mbali na huduma hizo nzuri zinazotolewa na Mfuko, ni vyema wananchi pia wakapata elimu juu ya umuhimu wa kujiunga na Mifuko ya Afya ya Jamii ili wanapougua wapate matibabu bila ya usumbufu wowote.

“NHIF mnafanya kazi nzuri sana nawapongeza, na hata huduma mliyoileta huku Lindi katika kipindi hiki cha siku nane naamini wananchi wa maeneo haya watanufaika na huduma hizi hususan ya upimaji wa afya bure, hivyo ninachowaomba sasa ongezeni kasi hasa kwa kwenda vijijini ambako ndiko kuna kundi kubwa la wananchi,” .

“Wakati mkifanya hizi huduma pia wahamasisheni wananchi kujiunga na Mifuko hii ya Afya ya Jamii ili wanapougua wapate huduma hata kama hawana fedha mfukoni,” alisema Naibu Waziri.

Aidha alitoa mwito kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi, Mtwara na wananchi wanaoishi jirani na mikoa hiyo kuhakikisha wanaitumia vyema fursa hii wakati wa maonesho haya kufika katika banda la NHIF ili kupata huduma ambazo zinatolewa bila malipo kwa wananchi lakini zimeghramiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

Naye Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Raphael Mwamoto, alisema kuwa NHIF kwa sasa inaendesha huduma hizi katika mikoa yote kwa lengo la kuwafanya wananchi kutambua umuhimu wa kujua afya zao lakini pia umuhimu wa kupata huduma za matibabu kupitia Mifuko ya Afya ya Jamii.

Alisema kuwa kwa upande wa elimu juu ya faida za kujiunga na Mifuko ya Jamii, NHIF inao mpango wa elimu ya Kata kwa Kata ambayo inafanyika zaidi katika maeneo ya vijijini ili kuwahamasisha wananchi kujiunga na kunufaika na Mifuko hii.

“Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa sasa una ofisi zake kila Mkoa Tanzania ikiwemo Ofisi ya Zanzibar, hivyo shughuli za elimu kwa umma na upimaji wa afya za wananchi hufanywa mara kwa mara na maofisa wa Mfuko walioko katika Ofisi zetu za mikoani” alisema.

Pia Ndugu Mwamoto aliendelea kusema kwamba matumizi sahihi ya fedha za tele kwa tele za CHF pamoja na fedha za matibabu zinazolipwa na NHIF katika vituo vinavyotoa huduma kwa wanufaika wa CHF na NHIF ni jambo muhimu sana. Alisema’’

Fedha zinazolipwa na Mfuko pamoja na CHF ni fedha nyingi ambazo zikitumika vizuri zinaweza kuboresha huduma za afya hasa upatikanaji wa dawa maeneo ya vijijini, kuna Halmashauri ambazo zimefanikiwa sana katika hili kwa mfano Nachingwea, Iramba, Igunga. Zingine ni Halamsahauri za Songea,Tanga ,Rombo,Singida na Mwanga. Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unaziomba Halmashaouri zingine nchini kote ziige mfano huu’’,
 Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti, Raphael Mwamoto akitoa maelezo ya huduma zinazotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi wakati alipotembea banda la Mfuko katika maonesho ya Nane Nane mkoani Lindi.
 Meneja wa Mkoa wa Lindi, Fortunata Raymond akielezea namna Mfuko wa Afya ya Jamii unavyofanya kazi Mkoani humo.
 Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi akisisitiza jambo baada ya kupata maelezo ya huduma za Mfuko huo ikiwa pamoja na kuupongeza kwa kazi nzuri.


NBC yatoa mkopo wa mabilioni ya shilingi kwa Mohamed Enterprises

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (wa tatu kushoto) akisaini hati za makubaliano ya mkopo wa shs bilioni 100 na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Mohamed Enterprises Ltd (METL), Mohamed Dewji kwa ajili ya kampuni dada ya METL ya Star Oils inayoshughulika na biashara ya uagizaji na usambazaji mafuta. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni baadhi ya watendaji wakuu wa NBC, METL na Star Oils.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (kushoto) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa METL, Mohamed Dewji wakionyesha mikataba muda mfupi baada ya kusaini hati za makubaliano ya mkopo wa shs bilioni 100 kwa ajili ya kampuni dada ya METL ya Star Oils inayoshughulika na biashara ya uagizaji na usambazaji mafuta. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Bi Mizinga Melu akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya kuipatia kampuni ya Star Oils mkopo wa takribani sh bilioni 100 ili kuongeza ufanisi katika kampuni hiyo ya uagizaji na usambazaji wa mafuta nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (wa nne kushoto), Ofisa Mtendaji Mkuu wa METL, Mohamed Dewji (wa nne kulia), watendaji wakuu wa NBC, METL na Star Oils wakipozi kwa picha ya kumbukumbu mara baada ya utiaji saini makubaliano hayo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa METL, Mohamed Dewji (kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya maofisa wa benki ya NBC katika hafla hiyo.

WASIWASI UMEIGHARIMU TAIFA STARS- KOCHA NOOIJ

$
0
0
Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij amesema moja ya sababu za kikosi chake kupoteza mechi dhidi ya Msumbiji (Mambas) ni wachezaji wake kucheza kwa wasiwasi katika kipindi cha kwanza.

Taifa Stars iliruhusu bao la kwanza sekunde chache kabla ya kumalizika kipindi cha kwanza katika mechi ya marudiano ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kutafuta tiketi ya kucheza hatua ya makundi iliyochezwa leo (Agosti 3 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa wa Zimpeto hapa Maputo.

Bao hilo katika mechi hiyo iliyomalizika kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, hivyo kusonga mbele kwa jumla ya mabao 4-3 lilifungwa kwa kichwa na mshambuliaji Josemar Machaisse.

Nooij alisema wasiwasi katika kipindi cha kwanza ndio ulioipa Msumbiji fursa ya kutawala mechi hiyo katika kipindi hicho na kukimalizia ikiwa mbele kwa bao hilo la mshambuliaji huyo wa klabu ya Bravos de Maquis ya Angola.

Alisema timu yake ilitulia kipindi cha pili baada ya kumuingiza Amri Kiemba badala ya Khamis Mcha. Pia alilalamikia bao ambalo Taifa Stars ilifunga dakika ya 16 kupitia kwa John Bocco lakini likakataliwa na mwamuzi Dennis Bate kutoka Uganda.

Aliongeza kuwa mchezaji Elias Pelembe aliyeifungia Msumbiji bao la pili dakika ya 83 kwa mpira wa adhabu nje ya eneo la hatari ndiye aliyemaliza mchezo huo. Pia ni mchezaji huyo aliyebadili matokeo ya mchezo wa kwanza jijini Dar es Salaam ambapo Msumbiji ilisawazisha dakika tatu kabla ya filimbi ya mwisho.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, na ambayo ilicheza vizuri kipindi cha pili ilipata bao lake dakika ya 78 na Mbwana Samata kwa shuti la pembeni akiwa nje ya eneo la hatari na kumshinda kipa Ricardo Campos.
Matokeo hayo yameipeleka Msumbiji katika kundi C lenye timu za Cape Verde, Niger na Zambia. Mechi za hatua ya makundi kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Morocco zitaanza kuchezwa mwezi ujao.

Mechi hiyo ndiyo itakayoamua ni timu ipi kati ya Tanzania na Msumbiji itakayoingia hatua ya makundi ya michuano ya Afrika kwa ajili ya kutafuta tiketi za Fainali itakayofanyika mwakani nchini Morocco.

Katika mechi ya kwanza iliyochezwa jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2. Timu itakayosonga mbele itaingia kwenye kundi lenye timu za Cape Verde, Niger na Zambia.

Taifa Stars inarejea Dar es Salaam kesho (Agosti 4 mwaka huu) saa 8 mchana kwa ndege ya Air Tanzania.

Kikosi cha Stars kilipangwa hivi; Deogratias Munishi, Said Moradi, Shomari Kapombe, Kelvin Yondani, Nadir Haroub, Erasto Nyoni, Mwinyi Kazimoto, Mcha Khamis/Amri Kiemba, John Bocco/Simon Msuva, Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu/Mrisho Ngasa.

Globu ya Jamii yajitosa kudhamini Miss Temeke 2014

$
0
0
Washiriki wa Shindano la Miss Temeke 2014,wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye kambi yao ya Mazoezi iliyoanza rasmi Agosti 3,katika viwanja vya Chang'ombe,Jijini Dar es Salaam.Globu ya Jamii kwa kushirikiama na Michuzi Media Group wamejitosa kudhamini Shindano hilo,ambapo watatoa zawadi nono kwa mrembo atakaeshita taji la Miss Photogenic.

SALAM ZA NANE NANE KUTOKA NGOMA AFRICA BAND AKA FFU

$
0
0
Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band yenye makao yake kule Ujerumani,inatoa salam maalumu za sikuu ya nane nane kwa wadau wote walio nyumbani Tanzania na nje. Sikuu kuu ya nane nane ambayo mwaka huu 2014 inafanyika kitaifa mkoani Lindi. Kikosi cha Ngoma Africa band aka FFU ughaibuni kinawatakia kila la heri na baraka katika Nane Nane oyeeee!!!! Usikose kupata burudani at http://www.ngoma-africa.com au www.ngoma-africa.com

PUBLIC LECTURE BY PROF. HOWARD FRENCH

Viewing all 110010 articles
Browse latest View live


Latest Images