Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 515 | 516 | (Page 517) | 518 | 519 | .... | 3278 | newer

  0 0

   BALOZI WA TANZANIA NCHINI ZAMBIA MHE. GRACE MUJUMA AKIWAKARIBISHA WADAU WALIOKUJA KUSHIRIKI MAONESHO HAYO KUTOKA NGORONGORO CONSERVATION AREA AUTHORITY. KUTOKEA KUSHOTO NI AFISA FEDHA WA UBALOZI HUDDY KIANGI, CAPT. MICHAEL MASOTA, MHE BALOZI GRACE MUJUMA, SALUMU MAYOMBO.
   MHE BALOZI GRACE MUJUMA AKIZUNGUMZA NA  WADAU WALIOKUJA KUSHIRIKI MAONESHO HAYO KUTOKA NGORONGORO CONSERVATION AREA AUTHORITY. KUTOKEA KUSHOTO NI CAPT. MICHAEL MASOTA, MHE BALOZI GRACE MUJUMA, SALUMU MAYOMBO NA AFISA UBALOZI RICHARD LUPEMBE.
  MHE GRACE MUJUMA NA MAAFISA WA NCAA

  0 0

  Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli amempa muda wa miezi miwili mkandarasi anayejenga barabara ya Ndundu-Somanga kufanya kazi usiku na mchana ili kumaliza kazi hiyo haraka bila kutoa visingizio vyovyote. 
  Waziri wa Ujenzi aliitoa kauli hiyo leo katika kijiji cha Manzese, Wilayani Kilwa mkoani Lindi wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika eneo hilo la ujenzi. Aidha, Dkt. Magufuli alisema kuwa mkandarasi huyo ameshalipwa fedha zote alizokuwa ana dai hivyo anachotakiwa ni kufanya kazi kila siku usiku na mchana ili amalize kazi hiyo haraka 
  “Tunataka mpaka mwezi wa tisa, tuone barabara ya lami na sio vinginevyo, wahandisi wote wa mkoa wa Pwani na Lindi wamsimamie kwelikweli na kwa muda wote ili aweze kukamilisha kazi hii kwa muda tuliompa” Alisema Waziri Magufuli 
  Pia  aliwaasa Wananchi kutomwibia Mkandarasi huyo Mafuta ili aweze kukamilisha kazi hiyo kwa wakati. “Msiibe mafuta kwa mkandarasi pia nayeye anatakiwa awalipe vizuri wafanyakazi wake kwasababu sisi pia tunamlipa vizuri, pia anatakiwa atunze vifaa vyake vizuri” alisema Waziri Magufuli Kuhusu barabara ya kutoka Lindi kuelekea Mtwara katika baadhi ya maeneo, Waziri Magufuli amewataka viongozi wa mkoa kusimamia malori yanayobeba gipsam na mawe makubwa kupita kiasi hali inayohatarisha usalama wa barabara hiyo. 
  “Nawataka msimamie hili pamoja na TANROADS ikiwezekana waweke mizani inayohamishika kupima malori hayo. Hii itasaidia kulinda barabara zetu ambazo tunatumia fedha nyingi kuzijenga” Alisema Dkt. Magufuli Kuhusu udongo unaodondoka katika eneo la Mchinga, Waziri Magufuli alisema katika mwaka huu wa fedha, wizara imetenga bajeti kwa kazi hiyo ya kutengeneza eneo hilo ili tatizo lisiendele.
   Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma mkoani Mtwara kabla ya Ufunguzi wa Barabara ya Masasi –Mangaka na uwekaji wa jiwe la msingi wa barabara ya Mangaka –Mtambaswala 71.5km

   Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli wakwanza kulia akipita juu ya daraja la Nangoo Wilayani Masasi wakati wa ukaguzi huku akifatiwa na  Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mhandis Mussa Iyombe pamoja na Mwakilishi kutoka  Benki ya Maendeleo ya Africa (ADB) Bi Tonia Kandiero.

   Sehemu ya barabara ya Ndundu Somanga kama inavyooneka baada ya mkandarasi kuanza kufanya kazi kwa kasi tofauti na hapo awali

   Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa kijiji cha Manzese kuhusu Mkandarasi anayejenga barabara katika eneo hilo la Ndundu Somanga kuwa anatakiwa ndani ya miezi miwili awe amekamilisha barabara ya lami bila visingizio vyovyote.

   Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mbele ya viongozi mbalimbali kutoka Mkoa wa Pwani na Wizara ya Ujenzi, ADB na wakandarasi kuhusu ujenzi wa barabara ya Ndundu Somanga baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kufanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa barabar hiyo

   Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi mara baada ya kuhutubia wakazi wa Manzese katika barabara ya Ndundu Somanga mkoani Lindi. 

  Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa mkandarasi anayejenga barabara ya Ndundu Somanga kuhusu kumalizia kipande cha kilometa kumi kilichobakia ndani ya muda wa miezi miwili…Picha zote kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano-GCU-UJENZI  0 0


  0 0

  Makamu mkuu wa shule ya sekondari Iwawa Fadhili Dononda akizungumza na mwandishi wetu ofisini kwake hii leo.

  Na Edwin Moshi, Makete
  Ikiwa zimepita siku chache tangu kutangazwa matokeo ya kidato cha sita mwaka huu, shule ya sekondari Iwawa iliyoko wilayani Makete mkoani Njombe imetoa siri ya mafanikio ya wanafunzi wake kufaulu na kushika nafasi ya nne kitaifa.  
  Akizungumza na mwandishi wetu ofisini kwake Makamu mkuu wa shule hiyo Mwl. Fadhili Dononda amesema miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na wanafunzi hao kuwa na utayari wa kusoma hivyo wanafunzi hao hawakuwa walevi wala watoro bali walikuwa wakizingatia masomo.  
  Amesema kutokana na wanafunzi hao kutopenda utoro wala ulevi na kuwasikiliza walimu wao na kufuata taratibu za shule kumepelekea wao kutumia muda mwingi katika masomo.  
  Mwalimu Dononda amesema pia nidhamu baina ya wanafunzi wenyewe kwa wenyewe pamoja na kwa walimu wao kumesababisha walimu kuwa na ari ya kuwafundisha na kutumia jitihada za hali ya juu kwa wanafunzi hao ili waweze kufaulu vizuri jambo ambalo limefanikiwa.  
  "Unajua kila mzazi anamleta mtoto wake shule ili afaulu, sasa ukiwakuta wanafunzi wana ari kwa kweli hata mwalimu unapata moyo wa kufundisha kwa bidii, wanafunzi hawa waliofaulu walikuwa wamechujwa ipasavyo toka wakiwa o'level (kidato cha i-iv) kutoka kwenye shule walizosoma, hivyo kila mmoja alikuwa na moyo wa kuhakikisha anafaulu, na pia wenyewe walikuwa na mshikamano pia" amesema mwalimu huyo.  
  Ameongeza kuwa katika mtihani wa utamirifu (mock) ambao ulifanywa na wanafunzi 39 pia ulionesha dalili njema za matokeo ya mwisho kuwa mazuri kwa sababu wanafunzi 29 walipata daraja la I, 9 wakapata daraja la II, na mmoja alipata daraja la III. 
  Kwa upande wake mwalimu Jitahidi Sanga ambaye alikuwa akifundisha masomo ya Jiografia na General Studies kwa wanafunzi hao na pia mwalimu wa darasa, amesema siri ya wanafunzi hao kufaulu vizuri ni pamoja na walimu kufundisha kwa muda wa ziada na wikiendi bila malipo yeyote.  
  Amesema utayari waliokuwa nao wanafunzi hao ulipelekea kufundishwa muda wa ziada bila kusukumwa.  
  "Kwa mfano likizo ya mwezi Juni mwaka jana wanafunzi hao wengi wao hawakwenda likizo, na mimi mwenyewe nilikuwa nikiwafundisha kwa muda wa ziada bila kudai malipo yeyote, na pia kwa kuwa nilikuwa mwalimu wa darasa nilikuwa nikiwasihi wazingatie masomo pamoja na yale waliyoaswa na wazazi wao" amesema mwalimu Sanga. 
  Bi Anita Sanga ni mzazi ambaye amezungumza na mwandishi wetu na kusema kuwa matokeo hayo wameyapokea kwa furaha na hawakutegemea kama shule hiyo ingefanya vizuri kwa kiasi hicho.  
  Amesema wanafunzi wote wazingatie masomo kama walivyofanya hao waliomaliza kidato cha sita ili shule hiyo iendelee kufanya vizuri na hatimaye iwe ya kwanza kitaifa kwa kidato cha nne na cha sita.  
  Shule ya sekondari Iwawa ni miongoni mwa shule tatu za serikali zenye kidato cha tano na sita wilayani hapo.

  0 0

  AMBASSADOR OMBENI Y. SEFUE, CHIEF SECRETARY

  0 0  0 0


  Mustafa Hassanali, Tanzania's  Pan African fashion designers, first statement piece was worn by Hoyce Temu who was crowned MISS TANZANIA 1999, in his signature EVENING GOWN.

  Stay tuned to MEREMETA NA HASSANALI, celebrating his 15th Anniversary in Dar es Salaam this August 2014

  0 0

   Wafanyakazi wa kampuni ya Majembe Auction Mart wakifungua mashine ya kutengenezea matofali katika eneo la Kwa Msuguri, Kimara jijini Dar es Salaam.Wizara ya Maji iliamrisha kukamatwa kwa vifaa na mali mbalimbali za Martin Kessy aliyekuwa amejiunganishia maji kinyume na sheria na kufanya biashara ya kufyatua matofali.  Zoezi hilo linaendelea. Zoezi hilo limefanyika jana katika eneo la Kwa Msuguri, Kimara jijini Dar es Salaam jana.  .

   Mwenyekiti wa kamati maalum ya Wizara ya Maji, Eng. Hamis Blangson (kulia) akisikiliza jambo wakati wa operesheni maalum ya kupambana na watu wanaojiunganishia maji kinyume na sheria na kusababisha hasara kwa serikali na matatizo ya huduma hiyo kwa wananchi. Wengine ni wajumbe wa kamati hiyo, Bw. Twaha Mohamed (kushoto) na Bw. Juma Maingu (katikati).  Zoezi hilo linaendelea

  Kifaa cha kubebea vifaa vizito cha DAWASA kikiondoka na moja ya mashine ya kutengenezea kutengenezea matofali katika eneo la Kwa Msuguri, Kimara jijini Dar es Salaam.


  0 0

   Wajumbe wa Mkutano wa 45 wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika (CPA Africa Region) wakiimba wimbo wa Taifa wa Tanzania kabla ya Ufunguzi wa Mkutano huo jana. Mkutano huo ulifunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhruri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mohammed Ghalib Bilal. 
   Makamu wa Rais wa Jamhruri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mohammed Ghalib Bilal akifungua Mkutano wa 45 wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika (CPA Africa Region) katika ukumbi wa Mikutano wa Arusha (AICC). Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe zaidi ya 500 ambao ni Maspika, Wabunge na Maafisa wa Mabunge kutoka bara la Afrika.
  Makamu wa Rais wa Jamhruri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mohammed Ghalib Bilal akiongea na Waandishi wa Habari mara baada ya Ufunguzi wa Mkutano wa 45 wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika (CPA Africa Region) katika ukumbi wa Mikutano wa Arusha (AICC). Kulia ni Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda ambaye pia ndiye rais wa chama hicho. Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe zaidi ya 500 ambao ni Maspika, Wabunge na Maafisa wa Mabunge kutoka bara la Afrika. 


  0 0

  Mr. Iddi Sandaly,
  Bachelors in Accounting, MBA, CPA, CGMA
  Controller at
  Property Management Company
  KUSHIRIKIANA NA KINA MAMA NA WATANZANIA WOTE HAPA DMV

  Kwa miaka mitatu mfululizo nimekuwa nikishiriki na kushirikiana na kikundi cha kina mama kwenye matembezi hiari ya Kansa. 
  Kikundi cha kina mama wa DMV ndani yake kukiwa na watanzania wenzetu walio pitia janga la Kansa wamekuwa mbele kuwaomba na kuwataka watanzania wachangie kwenye utafiti wa Kansa na pia kuwaomba watanzania wote wafanyiwe uchunguzi wa Kansa. 
  Na kwa miaka mitatu toka kikundi hichi cha wana DMV kilipoanza nimekuwa nikishirikiano nao kwa kutoa mchango wa kifedha kwenye utafiti wa Kansa na pia kwa kuwa nao kina mama wa hawa kwenye matembezi.
  Lengo na Mipango ni kushirikiana na kikundi hiki cha kinamama na kwa mwaka huu nitashirikiana nao na kuandaa na tutajaribu kuwaleta wataaalamu na huduma ya bure ya uchunguzi wa kansa kwa wana DMV kama nilivyoshirikiana na viongozi wenzangu na Nesiwangu kwenye kuleta huduma ya Bure ya Afya hapa DMV. 
  Pia tunafanya maandalizi ya mwakani lili tuweze kupata kina baba wengi kujumuika kwenye Matembezi haya ya Kansa,
  DMV KWANZA.

  0 0

  U.S. Embassy Public Affairs Officer Ms. Marissa Maurer (left)  presents a ticket to Clouds Media Presenter and Brand Manager Ms.  Louissa Babbie Kabae, who will participate in the U.S. Department of State sponsored U.S. Commitment to Africa Reporting Tour to be held from July 26 through August 8 in the United States.  
  Kabae will join more than 20 other African journalists in a working tour of Washington DC and the City of Atlanta to cover the U.S – African Leaders Summit and Young African Leadership Initiative (YALI) Forum hosted by President Obama.  
  These two initiatives build on, and seek to further strengthen partnership between United States and Sub-Saharan Africa  in strengthening democratic institutions, accelerating economic growth,  promoting trade and investments, advancing peace and security and investing in the next generation of African leaders. For more information about the events visit  https://youngafricanleaders.state.gov/http:/ and www.whitehouse.gov/us-africa-leaders-summit  (Photo courtesy of the American Embassy).


  0 0


  0 0

   Mbunge  wa Viti maalum(CCM) mkoa wa Arusha Namelok Sokoine akiangalia bweni la shule hiyo ya Irkisongo wilayani Monduli lililoteketezwa na moto 

   Mapacha wanaoishi Wakaazi wa New York Marekani Joy na Jane wakimkabidhi mkuu wa shule hiyo mama Nyange sehemu ya msaada wao wa kilo zaidi ya kumi za misumari

    
  Mjumbe wa kamati ya siasa(CCM) wilaya Monduli, Paulina Ngoyai(Mama Kalaine) akikabidhi msaada wake wa mifuko mitano ya sementi kwa shule hiyo


   Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Arusha(CCM) Namelok Sokoine akimkabidhi mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Irkisongo wilayani Monduli Happiness Nyange msaada wake wa shilingi millioni moja kufuatia kuungua kwa mabweni ya shule hiyo

  Mwakilishi wa kiwanda chaTanfoam cha jijini Arusha Sajid Ibrahim(kulia) akimkabidhi sehemu ya msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya shilingi millioni 3 kwa mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Irkisongo Wilayani Monduli Happness Nyange(kushoto), kufuatia mabweni ya shule hiyo kuteketea kwa moto hapo jana.Msaada huo unatokana na harambee ya papo kwa papo aliyoifanya mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akitumia simu yake ya kiganjani. Wadau kadhaa wa elimu wamejitokeza kusaidia ambapo mbunge wa Arusha Viti maalum Namelok Sokoine amechangia shilingi millioni moja.  0 0

  UNIVERSAL AUCTION CENTRE Kwa idhini waliyopewa na Ubalozi wa Switzerland, Finland & Sweden  watauza kwa mnada wa hadhara  Magari, Generators & Fanicha za Ofisi na nyumbani tarehe 26 July, 2014 Jumamosi saa 4.00 asubuhi. Mnada utafanyika Golden Resort Sinza,  Lion Street.

  MALI ZITAKAZOUZWA:Sofa sets, Dining Table & chairs, Coffee table, Book Shelves, Meza za ofisi/viti, File cabinets, Fridges, Cookers, TV set, Washer, Dryer, Camping Tents, Computer set, Photocopy m/c,  A/c split units Etc.

  MAGARI YATAKAYOUZWA:

  Idadi

  Aina

  Model

  Mwaka

  Ushuru

  1

  Nissan Patrol

               Diesel Engine  4x4    S/ Wagon

  2008

  Bado

  1

  Nissan Hard Body

               Diesel Engine   4x4   P/ UP D/ Cabin

  2008

  Bado

  1

  Nissan Ex Trail

                Diesel Engine   4x4  S/ Wagon

  2011

  Bado

  5

  Isuzu P/Up Double cabin

   4BJ1,  Diesel engine,  4x4    P/ Up D/ Cabin

  2006

  Bado

  1

  Generator  17 KVA

                Lister Diesel Engine 4 cylinder

  2005

  Bado

  Mali zote zinaweza kukaguliwa Golden Resort Sinza,Lion Street tarehe 24 na 25 July,  2014 kuanzia saa 4.00. asubuhi mpaka saa 10.00 jioni.


  MASHARTI YA MNADA:

  1. Mnunuzi  wa fanicha atatakiwa kulipa malipo yote pale pale. Na mnunuzi wa Generator/gari atatakiwa kulipa 25% pale pale na salio lilipwe ndani ya siku 7 ukishindwa kulipa kwa muda huu gari litauzwa tena na dhamana haitarudishwa.


  1. Mali zote zitauzwa kama zilivyo.


  1. Mnunuzi atawajibika kulipa ushuru.


  1. Mali yote iliyouzwa itatakiwa kuondolewa siku hiyo hiyo  baada ya kulipia malipo yote pamoja na ushuru

  Kwa maelezo zaidi waone:
  UNIVERSAL AUCTION CENTRE
  NKRUMAH STREET MKABALA NA CO-CABS

  SIMU NA:  0754-284 926, 0757 284 926               Email : universalauction@hotamail.com


  0 0
 • 07/25/14--03:17: UCHOKOZI WA KIJAST BIKOZZ


 • 0 0

   Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde akimkabidhi vifaa vya michezo Mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya soka ya vijana wa TFF Ayoub Nyenzi  kwa ajili ya mashindano ya Airtel Rising Stars yanayotariwa kuanza kutimua vumbi ngazi ya mkoa Jumapili ijyayo. Hafla ya makabidhiano ilifanyika jana jijini Dar-es-Salaam.
  ·          
  Saidi Meck Sadiki mgeni ramsi ufunguzi Jumapili.

  Airtel Tanzania Jana Alhamis Julai 24, 2014 imekabidhi vifaa vya michezo kwa timu 18 za wavulana zinazoshiriki michuano ya soka ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 maarufu kama Airtel Rising Stars ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi katika ngazi ya mkoa jijini Dar es Salaam Jumapili 27 Julai 2014.

  Dar es Salaam inajumuisha mikoa ya kisoka ya Ilala, Temeke na Kinondoni. Washiriki wengine wa mashindano hayo ya kubaini na kuendeleza vipaji watatoka katika mikoa ya Mwanza, Mbeya na Morogoro. Akizingumza katika hafla hiyo ya kukabidhi vifaa iliyofanyika kwenye uwanja cha Kumbu Kumbu ya Karume, Mwenyekiti wa kamati ya vijana ya TFF Ayoub Nyenzi amesema maandalizi yamekamilika.

   “Tunatajia kuwa na mashindano yenye ushindani mkali na ya kusisimua. Napenda kuchukua fursa hii kuwataka viongozi wa soka ngazi ya mkoa kuhakikisha wanakuwa makini ili kuchagua vijana wenye vipaji kuunda timu zao za mikoa zitakkazoshiriki fainali za taifa zitakazofanyika jijini Dar es Salaam mwezi ujao”, alisema Nyenzi.

  Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Saidi Meck Sadiki anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi rasmi wa Airtel Rising Stars katika mikoa ya kisoka ya Ilala, Temeke na Kinondoni utakofanyika kwenye uwanja wa Karume jijini Jumapili ijayo.

  Mkoa wa Mwanza utafungua rasmi michuano yake Agosti 3, ukifuatiwa na Mkoa wa Mbeya ambao umepangiwa kuanza mashindano yake Agosti 4 wakati mkoa wa Morogoro utaanza mechi zake Agosti 5. Wakuu wa mikoa husika wanatarajiwa kuwa wageni rasmi kwenye hafla za ufunguzi wa michuano hiyo.

  Mbali na timu za wavulana, mashindano hayo pia yatashirikisha timu za wasichana katika ngazi ya taifa na kufanya fainali hizo kuwa na jumla ya timu 12, sita za wasichana na sita za wavulana. Timu za wasichana zinatoka mikoa ya Ilala, Kinodoni, Temeke, Mbeya, Mwanza na Zanzibar. Huu ni mwaka wa tatu tangu mashindano ya Airtel Rising Stars yalipoanza kushirikisha timu za wasichana.        

  Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde amesisitiza nia thabiti ya kampuni ya Airtel ya kuendelea kudhamini programu hii ya vijana na kulipongeza Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, wizara inayosimamia michezo na wadau wengine wa soka kwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Airtel kusaidia maendeleo ya soka la vijana. 

  Michuano wa Airtel Rising Stars ni mpango kambambe kwa Afrika nzima ambao ni wa kutafuta na kukuza vipaji vya soka vinavyochipukia kwa wavulana na wasichana wenye umri chini ya miaka kumi na saba ambao watapata muda wa kuonyesha vipaji vyao na kukutana na wataalamu wa mpira wa miguu ambao watawapa mafunzo zaidi na kupata nafasi ya kukuza vipaji vyao.

  Airtel Rising Stars itahitimishwa kwa mashindano ya kimataifa ambayo yatashirikisha wachezaji nyota kutoka nchi 22 barani Afrika ambapo kampuni ya mawasiliano ya Airtel inafanya biashara.  Mashindano hayo ya kimataifa yamepangwa kufanyika nchini Gabon kuanzia Agosti 25 hadi 30.

  0 0
 • 07/25/14--06:17: KUMBUKUMBU
 • MAREHEMU MODEST SABINUS KWEKA.
  14-04-1968 - 25-07-1999 

  Ni miaka 15 leo,tokea ulipotuacha gafla baada ya kuitwa na Mungu Baba wa Mbinguni.Hatuna cha kusema ila ni kushukuru kwa kila jambo Mdogo wetu Modest, tokea hapo maisha ya Familia yetu hayajawa tena mazuri. machache Mungu alitukumbuka lakini kubwa kuliko yote, ni mama yako mzazi ambaye Kansa imemaliza sana, hana tena ziwa, Mguu mmoja na sasa tunakimbilia kukata wa pili. Tunaomba Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema atunusuru na janga hilo.

  Unakumbukwa sana na Mkeo Mpenzi Constancia, Mwanao wa pekee Kelvin,Mama yako mzazi Ursula, Ndugu zako

  Jane, Festo, Eugenia, Elizabeth, Cecilia, na Thadei;Mashemeji zako wote WaKweka wote wa Narumu, wa Wamallya na Manushi, Wafanyakazi wenzako wa Temeke Hospital wakazi wote wa Temeke Mikoroshini,Ndugu,Jamaa na Marafiki na wote waliokufahamu Misa ya Kumbukumbu Imesomwa mwanza leo Kanisa la Mt. Augustino – Mkolani Mwanza

  “Lakini mtu mwema hata akifa kijana atapata pumziko………………………….huyo alionekana amempendeza Mungu, akapendwa naye, hata pindi alipokaa katikati ya wakosaji akachukuliwa.Naye akahamishwa ili uovu usimgeuzie nia yake, wala hila isimdanganye roha yake” Hek 4:7-11

  “RAHA YA MILELE UMPE Ee BWANA”

  0 0


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete akimuapisha Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila leo jijini Dar es Salaam.
   Jaji Kiongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jaji Shaban Ally Lila (kulia) akitia saini hati ya Kiapo mbele ya Rais Jakaya Kikwete wakati wa hafla ya kuapishwa kwake  leo jijini Dar es Salaam. Katikati mwenye miwani Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akishuhudia tukio hilo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini hati ya Kiapo cha Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila wakati wa hafla ya kuapishwa kwa jaji huyo leo jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi  hati ya Kiapo  Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila wakati wa hafla ya kuapishwa kwa jaji huyo leo jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(kushoto) akimpongeza Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila mara baada ya kuapishwa rasmi kushika wadhifa huo katika hafla iliyofanyika Ikulu leo jijini Dar es Salaam.

  Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Majaji wa Mahaka Kuu Tanzania mara baada ya kuapishwa rasmi kushika wadhifa huo katika hafla iliyofanyika Ikulu leo jijini Dar es Salaam.Kushoto kwake ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman.Picha zote na Frank Shija- MAELEZO
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Afisa Uhusioano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (Wapili kulia), akimsalimia Mkurugenzi wa Kituo cha Kulea Watoto Yatima, (CHAKUWAMA), kilichoko Sinza jijini Dar es Salaam jana, baada ya wafanyakazi wa Mfuko huo kukab idhi misaadsa ya vyakula kwa ajili ya sikukuu ya Idd. Mfuko huo pia umekabidhi misaada kama hiyo kwa vituo vingine sita vya yatima jijini kwa ajili ya sikukuu ya Idd. Kulia ni Afisa wa fedha wa Mfuko huo, Mohammed Madenge, na kushoto ni A\fisa Masoko, Magire Werema
   Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Abdul Njaidi, (Kulia), akikabidhi msaada wa vyakula ikiwemo Mbuzi, kwa watoto wanaolelewa kwenye kituo cha kulea yatima cha Mwandaliwa kilichoko Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam jana. PSPF, imetoa misaada kama hiyo kwa vituo sita vya yatima jijini kwa ajili ya sikukuu ya Idd.
   Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Magira Werema, (Kulia), akikabidhi Mbuzi na vyakula kwa watoto wa kituo cha kulea watoto yatima cha Chakuwama, Sinza jijini Dar es Salaam jana. Mfuko huo umekabidhi misada kama hiyo kwa vituo vingine sita jijini kwa ajili ya sikukuu ya Idd inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki.
  Chakuwama_Said Hassan

  Afisa anayeshughulikia masuala ya fedha, wa Mfuko w aPensheni wa PSPF, Mohammed Madenge, (Wakwanza kjulia), akifuatana na Afisa Uhusiano Mwandamkizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi, (Katikati), na afdisa masoko, Magira Werema, wakikabidhi msaada wa vyakula ikkiwemo Mbuzi, kwa kituo cha kulea watoto hyatima cha Mwandaliwa kilichoko Bunju nje kidogo ya jiji jana. PSPF, imekabidhi misaada kama hiyo kwa vituo vinghine sita jijini kwa ajili ya khjusherehekea sikukuu ya Idd inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki au mwanzoni mwa wiki. 

older | 1 | .... | 515 | 516 | (Page 517) | 518 | 519 | .... | 3278 | newer